Kituo Cha Kwanza Kina Sehemu Tatu

Sehemu Ya Kwanza

Kutoka katika somo ambalo limetolewa katika shule ya Yusuf ya tatu. Nayo ni muhtasari wa muhtasari wa andiko la ishirini.

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

وَبِهِ نَسْتَعِيْن

Ambaye ametumia miaka thelathini na tano hali ya kujitenga na watu, na ameiaga dunia na kuisahau, na hasa katika nyakati za usiku, hata akawa mbali na watu, kwa wingi wa taabu alizopata kutokana na uangalizi wa kudumu na kulindwa daima kwa kazi zake ulinzi wenye chuki na tabia mbaya, muda wa miaka ishirini na tatu, hata akawa anaona dhiki kupitisha saa ya wakati wake pamoja na mtu na sehemu moja, isipokuwa mwenye shauku na Risale-i Nur na anayeisaidia. Nasema: Wamemuhamisha mnyonge huyu – mimi mnyonge – kwenda kwenye chumba cha tano cha gereza kwa lazima, ambapo kuna msongamano kwa kiasi kikubwa. Na wakawazuia ndugu zangu kunitembelea, kwa hoja ya kupeleka kwangu madai mahakama ya rufaa kuhusu hali yangu kwenye gereza la peke yangu miezi kumi na moja.

Nilipokuwa katika hali mbaya na hofu juu ya kutohimili maisha katika msongamano mkubwa, tahamaki hali ya hewa inakuwa baridi kali – kuwa ni alama ya hasira – kwa hali ambayo ningekuwa mahali pangu pa zamani nisingeihimili kamwe. Ugumu ukageuka kwangu kuwa wepesi, na shida ile ikashuka kwangu ikiwa ni rehema kutoka kwa Allah (s.w). Yakapita mawazo moyoni:

Pamoja na wanafunzi wa Risale-i Nur kutimiza majukumu yao – na kwa niaba yako – katika kufikisha hakika za Risale-i Nur kwa bidii na Ikhlasi, katika kila rad’ha katika rad’ha za gereza, hakika rad’ha hii ya tano yenye kufanana na mahali pa kujitenga kwa wenye kuipa nyongo dunia inakuwa mpya daima na kubadilika, kwa hiyo basi inahitaji mno masomo ya nuru.

Na vilevile vijana na wazee hapana shaka wana haja mno na masomo ya kiyakini ya kina katika kuthibitisha uwepo wake (s.w) na upweke wake. Ambapo wanasoma yanayoandikwa na magazeti katika hujuma ya Urusi kwa imani hujuma za ukafiri za kutisha, na kumkana Muumba mtukufu. Yaliyopita katika moyo nyakati za dhikiri baada ya swala ni haya. Na kwa upande wangu nikataja tahalili ambayo ninaitaja tangu zamani mara kumi baada ya swala ya alfajiri, nayo ni: (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w) hana mshirika na kila sifa njema zinamstahiki yeye anahuisha na kufisha naye ni hai hafi mikononi mwake mna kheri zote naye ni mweza kwa kila jambo na kwake tu ndio marejeo).

Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad, 4/227. Ibn Abi Shaiba, Al-Musnad 6/27, 7/171. Al-Bazar, Al-Musnad 3/260. Attabarany, Al-Muujam al-Kabir 20/65.

Tahalili hii tukufu na Tawhid tukufu ambayo inabeba jina kuu – kulingana na riwaya moja – imebainishwa na (Andiko la Ishirini) tukufu kwa namna ya uwazi wenye kuangaza kama jua, na hii ni katika maneno kumi na moja katika maneno yake katika hoja kumi na moja miongoni mwa hoja za wajibu wa uwepo wake (s.w) na upweke wa uungu wake, na limeleta bishara kumi na moja katika bishara za kufurahisha.

Naam, nilikuwa ninakariri sentensi hii takatifu kwa mazingatio ya kina pamoja na kutafakari katika muhtasari wa andiko la ishirini, ikapita moyoni ghafla: Toa muhtasari huu ukiwa ni somo kwa mwanazuoni mtukufu (Nadir) na wanao kaa hapa katika vijana. Nami kwa upande wangu nikasema: Bismillahi, nikaanza kutoa somo:

Hakika katika maneno haya ya kitawhidi kuna bishara kumi na moja, na hoja kumi na moja za kiimani, nitaashiria hoja peke yake kwa ishara fupi sana kwa kuhaulisha fafanuzi zake na bishara zake kwenda katika (Andiko la ishirini) na katika sehemu za Risale-i Nur.

Na nilipoandika somo hili, nimeona inafaa sana kuingiza maneno na nukta ambazo sikuzieleza kwa wafungwa.

Na kama hivi, maneno kumi na moja ya maneno hayo ya kitawhidi ni haya yafuatayo:

Neno la kwanza (لاَ إِلهَ إِلاَّ الله)

Hakika hoja ya kiimani katika neno hili ni risala ya (Al-Ayatul kubra), ni risala ya ajabu ambayo haina kifani.

Risala hiyo imepelekea wanafunzi wa Risale-i Nur wapate kuachiliwa huru mahakamani, na kudhihiri kwao katika Gereza la (Denizli) na kushinda katika mahakama zote za (Denizli na Ankara) na kuenea kwake kwa kificho kwa namna ya kuathiri. Kama ilivyokuwa kuchapwa kwake kwa siri sababu ya kuwekwa kizuizini wanafunzi wake kwa muda wa miezi tisa.

Naam, hakika Mwale wa (Al-Ayatul kubra) umedhihirisha ijmai thelathini na tatu kubwa na hoja za kijumla katika ulimwengu wote, pamoja na kuashiria kwake katika kila hoja ya kijumla hoja zisizo na mpaka zinathibitisha wajibu wa uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo, na upweke wake kwa uthibitisho angavu uliokuwa wazi kama mchana. Unatamkisha mbingu kwa maneno ya nyota katika utangulizi kisha ardhi kwa sentensi za wanyama na mimea na kama hivyo hadi anautamkisha ulimwengu wote kwa maneno ya hakika za kuzuka, yamkini na mabadiliko.

Basi ni juu ya wale wanaotafuta imani madhubuti isiyotetereka na wanaotafuta upanga mkali usiodugika mbele ya fujo la ukafiri kuipitia risala ya (Al-Ayatul kubraa).

Neno la pili: (وَحْدَه)

Na ishara fupi katika hoja iliyomo humo ni: Hakika katika kila upande wa huu ulimwengu na kila sehemu ina shuhudia umoja ulio wazi:

Kwa mfano: Ulimwengu wote ulivyo ni wenye kufanana sana na mji uliostawi, na kasri kubwa na kitabu fasaha chenye kuonekana, kwa kiasi kwamba kila aya ndani yake, bali kila herufi miongoni mwa herufi zake, bali kila nukta katika nukta zake ni katika hukumu ya muujiza na Qur’an iliyo kimwili.

Naam, kama ambavyo hili linabainisha umoja ulio kuwa wazi katika ulimwengu, basi taa ya kasri hii ni taa moja na kandili yake inayobainisha nyakati pia ni moja, na mpishi wake mmiliki wa moto ni mmoja, na mnyweshaji maji wake ni mmoja na kama hivyo mmoja, mmoja, mmoja, hadi inafikia elfu moja na moja katika moja na umoja.

Na kwa ulimwengu kudhihirisha umoja huu katika kila kitu, inathibitisha kwamba mwenye kasri hiyo na mji huo na kitabu hicho, hiyo Qur’an kubwa iliyo katika mwili, na mwandishi wake na msanifu wake yupo na mmoja wa pekee.

Neno la tatu: (لاَ شَرِيْكَ لَهُ)

Na ishara ya muhtasari sana kwa hoja iliyomo nayo ni: aya tukufu

قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لاَّبْتَغَوْاْ إِلَى ذِي الْعَرْشِ سَبِيلاً Qur’an, 17:42

ambayo ndio chimbuko la mwale wa (Al-Ayatul kubraa) na Ustadhi wake na msingi wake.

Naam, ingekuwa pamoja naye kuna miungu na wanaingilia katika uumbaji, kupatisha na uungu mpangilio wa ulimwengu wote ungeharibika. Wakati ambapo unashuhudiwa mpangilio mkubwa na madhubuti katika kila kitu kuanzia katika ubawa wa nzi mdogo, na kutokea katika kiini cha jicho lake na kutoka katika chumba chake kidogo na kukomelea katika ndege wa angani, ndege hao wasiohesabika na kumalizwa, hadi kwa mfumo wa jua. Basi katika kila kitu kwenye uwepo unaonekana mpangilio mkamilifu mno sawa iwe ni sehemu au yote, ndogo au kubwa. Jambo lenye kuthibitisha mpangilio huu mkamilifu mno uthibitisho usiokubali shaka kwamba ushirikina ni muhali kuwepo, na kwamba haupo kabisa. Na linathibitisha pia kuwepo kwa wajibu wa kuwepo na upweke wake.

Neno la nne: (لَهُ المُلْكُ)

Na ishara fupi sana kwa yaliyomo kutokana na hoja ndefu nayo: Hakika tunashuhudia kwa macho yetu kwamba nyuma ya pazia la ghaibu yupo ambaye anasarifu mambo mmiliki wa uweza huria hapingwi na mpaka wowote, na mmiliki wa elimu isiyopingwa na mipaka kwani amejaalia uso wa ardhi kuwa ni shamba kunjufu sawa na ukunjufu wa ardhi yote, kila majira ya machipuo anatawanya humo mbegu zaidi ya aina mia moja elfu za mimea, anazitawanya zote kwa pamoja na kwa hali ya kuwa zimechanganyika, kisha kuvuna mazao yake mavuno yenye kupambanuka bila kuchanganyika au kuvurugika pamoja na mpangilio kamili, na anagawa kwa mkono wa rehema na hekima kwa aina mia mbili elfu za wanyama kile kinachowiana nao katika riziki maalum kulingana na mahitajio yao. Kwa namna hii anasarifu mambo kwa ukunjufu wa ufalme wake mkunjufu na wenye nafasi, mkwasi mtoaji sana, na hasa shamba la ardhi.

Basi asiyemuamini msarifu huyu Mwingi wa hekima na Mfalme mwingi wa rehema analazimika kukanusha ardhi hii pamoja na mazao yake na anakuwa kama Wanasafsata wapumbavu.

Neno la tano nalo ni: (وَلَهُ الحَمْدُ)

Hakika ishara ya muhtasari sana katika hoja kunjufu sana iliyomo ndani yake ni:

Hakika sisi tunashuhudia kwa macho yetu na kutambua kwa akili zetu utambuzi kwa kiwango cha uwazi kabisa: Kwamba Mruzuku Mkarimu na Mhisani Mkarimu anasarifu na kuendesha mambo ya mji wa ulimwengu na anachunga mambo ya mtaa wa ardhi, na analea kambi ya mwanadamu na mnyama, hata kwamba yeye amegeuza Ardhi kuwa ni jahazi la kibiashara, na kuwa gari moshi la kuleta riziki, ili apate kushukuriwa na kuhimidiwa kwa neema tele anazomimina ambazo hazihesabiki akiwa amejaalia kutokana na majira ya machipuo yaliyokunjuliwa juu ya uso wa ardhi ambayo ni mfano wa gari moshi, lililoshehenezwa kwa aina mia moja elfu za vyakula, na kujaza chuchu ambazo ni shabihi ya mikebe ya maziwa mazuri kwa ajili ya kuwapa msaada wenye uhai wenye uhitaji ambao chakula chao kimekwisha mwishoni mwa majira ya baridi. Basi mwenye kuwa na chembe ya akili bila shaka ataamini kwamba jambo hili si vingine ila ni kutokana na matendo ya Mruzuku Mwingi wa rehema. Na asiyeamini haya na kupotea upotovu wa wazi kabisa analazimika kukana neema zote zilizotengwa na riziki maalum zenye kupelekea kushukuru, naye si mwingine isipokuwa ni mnyama mpumbavu mno mwenye kudhuru.

Neno la sita nalo ni: (يُحْيي)

Hakika ishara ya muhtasari sana kwa hoja iliyomo ndani yake nayo ni: Iliyothibitishwa katika (Neno la kumi) na katika sehemu za Risale-i Nur kwa hoja zenye nguvu kwamba: Huletwa katika uso wa ardhi kila majira ya machipuo jeshi kubwa la kiungu limeundwa kutokana na aina mia tatu elfu za wenye uhai na kiasi kisichokuwa na mpaka katika vitu kwenye maumbo mbalimbali. Basi hupewa uhai, na kuandaliwa kila kinacholazimu uhai kwa mpangilio kamili, jambo linalotubainishia vielelezo mia moja elfu katika vielelezo vya Ufufuo mkuu, bali katika alama zake.

Basi ambaye anahuisha viumbe hao anuwai bila mpaka kwa pamoja, na hali ya kuwa vimechanganyika na kuchukuana na kusukana baadhi yake kwa baadhi nyingine, bila ya kusahau wala kukosea wala kupungua, na bila ya kutahayari, na kuvipambanua pamoja na kuchanganyika kwake, na bila ya kusahau, na kuvipa uhai kwa ukamilifu wa mizani na mpangilio na kuvipa kutokana na manii zake ambazo ni matone ya maji yenye kufanana, na kutokana na kokwa zake zinazofanana, na kutokana na punje zake ndogo ndogo zisizotofautiana isipokuwa kidogo, na kutokana na vijiyai vya wadudu ambavyo ni sawa na vingine na kutokana na manii ya ndege, na kutokana na vijiyai vyake ambavyo ni sawa na vingine au kwa tofauti ndogo sana. Basi ambaye anahuisha mamia hayo katika maelfu katika wenye uhai ambao hujumuisha idadi isiyohesabika, yenye kutofautiana kwa sura, muundo na maisha, na kufufua mamia hayo katika maelfu miongoni na vilivyo hai, na kuandika vitabu mia moja elfu tofauti juu ya ukurasa wa ardhi na majira ya machipuo, anaiandika pamoja na hali ya kuwa imeingiliana na bila ya kukosea maandishi yalio katika hali nzuri kabisa, na anasarifu katika maandishi hayo kwa uangalizi usio na mpaka na kutenda kwa hekima isiyo na ukomo ndani yake. Naam, hakika ambaye anatenda haya ndiye muumbaji mjuzi wa kila kitu naye ndiye mhuishaji na aliye hai msimamizi wa kila kitu. Na asiyeitakidi hili hapana shaka analazimika kukanusha nafsi yake na kukanusha walio hai wote waliosambaa katika ardhi yote na waliotundikwa katika mkanda wa zama katika misimu yote ya machipuo iliyopita na waliopo juu ya ardhi hai na anga hai, na huyo si yeyote isipokuwa ni mpumbavu wa walio hai na mwovu wao wote.

Neno la saba: nalo ni (وَيُمِيْتُ)

Hakika ishara iliyo katika ukomo wa muhtasari katika hoja zake nayo ni:

Hakika tunashuhudia wakati sampuli mia tatu elfu za walio hai zinaachiliwa huru kutokana na majukumu yao kwa jina la umauti wakati wa mapukutiko, hakika kila sampuli na kila mmoja huweka mbegu zake katika mkono wa hekima kwa mhifadhi mtukufu, zile mbegu ambazo ni mikebe ya kurasa za matendo yake na faharisi za matendo yake, na orodha ya atakayoyafanya katika majira ya machipuo yajayo, nayo inafanana na roho yake yenye kubaki kwa upande mmoja – kama mbegu za tini ndogo ndogo mno ambazo zinabeba kanuni zote za uhai za mti wake, hiyo ni sawa na roho yake yenye kubakia – muumbaji mwingi wa hekima anaandika humo, aliye hai ambaye hafi, kwa kalamu ya kadari – kama kuandika katika nguvu yenye kuhifadhi – historia ya maisha ya mti kana kwamba ni kitabu kikubwa. Basi asiyemwamini muumba huyu mwingi wa hekima aliye hai ambaye hafi sio tu ni mtu mpumbavu na mnyama asiye na hisia, bali vilevile mtu huyo ni mbaya zaidi kuliko Shetani unawashwa kwake moto wa Jahannam na amehukumiwa umauti wa milele.

Naam, hakika matendo haya yaliyotajwa na ambayo yanaashiria hoja za maneno haya, nayo ni matendo yenye hekima ya jumla na kufunika na katika ukomo wa muujiza na yanajumuisha miujiza na mambo chungu nzima yenye kufurutu ada. Matendo haya haiyumkiniki kuwa bila ya mtendaji kabisa, bali hilo ni muhali kwa muhali mia moja, na ni batili kabisa, kuyaegemeza kwa sababu pofu kiziwi zenye kushindwa zisizokuwa na utambuzi, mfu zenye kuchanganyika na zisizo tawalia zisizo pangika, ni jambo lisilowezekana kwa mara elfu na moja na halina msingi kabisa.

Kama yatakabidhiwa matendo hayo yenye hekima kwa asiye mtendaji mwingi wa hekima ingelazimu kuwepo kwa uweza huria na hekima huria na ufundi mzuri wa jumla unahusu kuundika mimea yote na maua katika kila atomu moja katika atomu za udongo, na inapasa kuwepo kwa ukubalifu wa kufahamu na kufahamisha kauli na mazungumzo na maneno ya sauti zote na redio katika kila atomu miongoni mwa atomu za hewa kama ilivyoelezwa katika nukta ya kitawhidi katika neno (Huwa) katika (Mwongozo kwa vijana).

Na mtazamo huu wa ajabu haumfalii Shetani yeyote yule awaye kumkinaisha yeyote katu, ukafiri na kukanusha ambako kuko nje ya eneo la akili kwa kiwango hiki, nao uko mbali sana na uhakika na ni udhalilishaji kwa viumbe wote na kudhuru haki zao, hauna malipo isipokuwa moto, na huo ndio uadilifu hasa. Basi yatakikana kusema kuwa: (Na iishi jahannam kwa ajili ya watu mfano wa hawa wakanushao).

Neno la nane: (وَهُوَ حَيٌّ لاَ يَمُوْتُ)

Hakika ishara ya muhtasari mno katika hoja iliyomo nayo: Hakika ya majua madogo yenye kushuhudiwa kwa mfano nyakati za mchana juu ya mapovu ya uso wa bahari na juu ya uso wa mto unaotembea, hufichikana kwa kuondoka kwa mapovu hayo, hapo hudhihiri majua madogo ambayo huyafuatia kama yale yaliyotangulia, hili linaashiria jua ambalo lipo mbinguni na kulishuhudia. Na kwa kutoweka na kufa kwake yanajulisha uwepo wa jua la kudumu na la kubakia.

Vivyo hivyo, viumbe katika uso wa bahari ya ulimwengu wenye kubadilika daima na katika anga lake lenye kufanyika upya lisilo na mpaka, na katika shamba la atomu zake, viumbe hivi huchuruzika haraka na kwa mwendelezo katika mto wa zama ambao hupiga mawimbi kwa kukumbatia matukio yote ya vilivyomo vyenye kutoweka, na kufa pamoja na sababu zake za kiudhahiri. Ulimwengu fulani huonja umauti kila mwaka, na kila siku, na kushika nafasi yake ulimwengu mwingine mpya, na hufa dunia zenye kutembea kwa mfululizo na limwengu zenye kumiminika katika shamba la atomu baada ya kuchukua mavuno katika mashamba hayo.

Kama mapovu na majua madogo kwa kutoweka kwake hubainisha jua la kudumu, basi kifo cha viumbe hao wasio kuwa na mpaka na kuondoka kwa mavuno hayo, na kuviachia pamoja na sababu zake za kidhahiri kuachilia huru kwa mpangilio kamili, hujulisha kabisa kama mchana angavu na jua katika mwanga wa mchana juu ya kupasa kuwepo kwa aliye hai asiye kufa, juu ya jua la milele, juu ya muumbaji mwenye kubakia, juu ya mwamrishaji mtakatifu, na juu ya upweke wake (s.w), na juu ya uwepo wake, kujulisha kuliko dhahiri mno kuliko uwepo wa viumbe vyenyewe kwa mara elfu, na chenye kushuhudia hili ni kila kilichopo kwa dhati yake na vilivyopo vyote kwa pamoja.

Hapana shaka kuwa mmetambua kiwango cha upumbavu, uziwi na jinai ya yule asiyesikia sauti hizi za juu ambazo zinajaza anga lote la ulimwengu na shahidi hizi zenye nguvu na za kweli.

Neno la tisa: ni (بِيَدِهِ الخَيْرُ)

Ishara katika ukomo wa muhtasari katika hoja iliyomo humo ni: Hakika tunashuhudia katika kila duara katika maduara ya ulimwengu huu na katika kila aina miongoni mwa aina zake na katika kila tabaka katika tabaka zake hata katika kila mmoja mmoja miongoni mwa vilivyomo ndani yake, bali katika kila kiungo miongoni mwa viungo vyake, bali katika kila kijichumba miongoni mwa vyumba vya mwili wake, kuna hazina ya akiba na ghala la kuhifadhi riziki, na shamba na hazina inayotayarisha mahitaji yake na kinga yake, na mkono wa ghaibu hukabidhi kwa mkono wa kiumbe huyo – vilivyomo humo – katika wakati mnasibu sana na kwa namna asiyotarajia, bali kwa namna ilio nje ya uwezo wake na utashi wake, ndani ya mpangilio timamu kulingana na kipimo madhubuti, na yote hayo hufanyika katika ukomo wa hekima na upeo wa uangalizi. Milima kwa mfano huweka akiba mahitaji ya viumbe hai na mwanadamu miongoni mwa madini, madawa na mahitaji yote muhimu ya maisha. Ni hazina zilizojazwa kwa ukamilifu kabisa kwa amri ya mmoja wa pekee na kwa uendeshaji wake. Kama ilivyo ardhi kuwa ni shamba, kiwanda na jiko linalotayarisha vyakula vya viumbe hai wote na kwa mpangilio na kipimo kamili, na hii ni kwa nguvu ya Mtoa riziki Mwingi wa hekima, bali katika kila mwanadamu na katika kila kiungo miongoni mwa viungo vyake kuna hazina na ghala la kuhifadhia akiba, bali hata katika kila kijichumba miongoni mwa vyumba vya mwili vilevile ni hazina ndogo inayowiana nao kwa ajili ya kuhifadhi chakula cha akiba, na vivyo hivyo katika kila kilichomo kuna hazina, hata kwamba hazina ya akhera ni makazi ya dunia, na shamba la pepo na ghala lake ni ulimwengu wa Uislamu na ulimwengu wa utu wa kweli, ambao huchimbuka humo mazuri, uzuri na nuru. Na hazina katika hazina za jahannam ni maada mbovu na makundi yenye kuchafuka ambayo hutoa mimea ya shari, ubaya na ukafiri, shari hizo zinazotokana na kutokuwepo na zenye kuchafua limwengu za uwepo ambazo ni kheri. Na hazina ya joto la nyota na mapito yake ni jahannam, na hazina ya nuru zake na chanzo chake ni pepo.

Kama hivi hakika neno (Biyadihil khairu) kwa kuashiria kwake hazina zote hizo zisizo na mpaka linabainisha hoja ya wazi sana.

Naam, hakika neno hilo na pia ibara ya (Biyadihi makaaliidu kulli shayin) ni hoja mbili za uungu na upweke zisizo na ukomo wa ukunjufu wake, nazo ni zenye maajabu na miujiza bila mipaka, zinabainishwa na sentensi hizi mbili kwa asiyepofuliwa macho yake. Tazama kwa mfano katika hazina hizo funguo hizo tele bila ukomo katika haya tu basi:

Hakika Mwendeshaji Mwingi wa hekima mmiliki wa funguo za mbegu na kokwa, hizo hazina ndogo ambazo kila moja kati ya hizo inajumuisha zana za njia ya vikadiriwa vya mti mkuu au ua lenye harufu nzuri, kama anavyoamsha mlango wa mbegu kwa amri yake (Amka) kwa ufunguo wa utashi, na kwa mizani ya mpangilio kamili, vivyo hivyo anafungua hazina ya ardhi kubwa kwa ufunguo wa mvua, basi anafungua hazina zote ndogo yaani punje ndogo ambazo ni mbegu za uhai za mimea na vyanzo vya wanyama, na matone ambayo ni mbegu za uhai za ndege na vijidudu vyenye kuundika kutokana na hewa na maji, anazifungua zote na kwa pamoja na bila kosa kwa kupokea kwake amri ya kufunguka na kufunukana. Na Allah (s.w) anafungua katika muda huohuo hazina zote za ulimwengu za jumla na za sehemu, za kimaada na kimaana, kwa ufunguo maalum kwa kila moja kati ya hizo kwa mkono wa hekima, utashi, rehema na kutaka.

Ikiwa unataka kujua hili na kuliona basi tazama katika hazina zako ndogo ambazo ni moyo wako ubongo wako mwili wako na tumbo lako (mfuko wa chakula). Na tazama bustani yako majira yako ya machipuo ambayo ni pambo la ardhi na maua yake na matunda yake, hakika yake (s.w) anazifungua kwa funguo zake kwa mikono ya mkono wa ghaibu kwa funguo mbalimbali anuwai zinazotokana na kiwanda cha ﴿كُنْ فَيَكُوْن﴾. Anazifungua kwa ukamilifu wa mpangilio, vipimo, rehema na hekima, basi hutoa ratili moja au mia moja ratili za vyakula wakati mwingine kutokana na aunsi moja kutokana na mikebe midogo, anazitoa kwa mpangilio kamili na vipimo kwa kutumia vyakula hivyo hali ya kuweka karamu ya fahari kwa wenye uhai.

Je, ni katika yumkini kwa nguvu pofu na asili kiziwi na sadifu ya kiholela na sababu zisizo na hisia jinga zenye kushindwa kuingilia katika kutenda yasiyo na ukomo yenye kupelekea katika daraja hii ya mpangilio, elimu na busara, na katika ufundi makini wenye hekima timamu sadifu haiikaribii kabisa, na katika usarifu wenye kupimwa hakuna kosa ndani yake kabisa, na katika ulezi mtukufu wa kiungu adilifu uadilifu uliotimia hakuna dhuluma ndani yake asilani?

Na je, inayumkinika kwa asiyeona vitu vyote katika wakati mmoja na hawezi kuviendesha vyote kwa mkupuo mmoja, na wala hajaalii atomu na nyota za angani kuwa chini ya amri yake kwa pamoja, kuingilia katika uendeshaji huu na kusarifu mambo ambayo pande zake zote ni zenye hekima, muujiza na mizani?

Na kama hivi basi asiyemwamini mfano wa huyu Msarifu wa mambo, Mwendeshaji mwingi wa rehema, na Bwana Mlezi Mwingi wa hekima, na ambaye mikononi mwake kuna kheri zote, naye ana funguo za kila kitu, na anapotea upotevu wa mbali, hana isipokuwa moto ambao unawaka na kughadhibika hata

َكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ Qur’an, 67:8

kama alivyosema Allah (s.w). Jahanamu inasema kwa ulimi wa hali yake: Hakika anastahiki adhabu yangu ya kudumu, yeye si mwenye kustahiki rehema.

Neno la kumi: nalo (وَهُوَ عَلَي كُلِّ شَيْئٍ قَدِيْرُ)

Hakika ishara ya muhtasari sana katika hoja iliyomo ni: Hakika kila chenye utambuzi huja katika dunia hii ya ugeni, na kufungua jicho lake na kuona: Uweza unaoshika ulimwengu wote katika fumbato lake, na kukusanya elimu ya kiazali kabisa hapotei wala kusahau na hekima ya milele haina mchezo ndani yake kabisa na inajumuisha uangalizi wa hali ya juu, kiasi hufanya kila moja kati ya walio katika jeshi la atomu yenye kuvutika kwa mvuto wa kimawlawy, hivyo kuvitumia katika majukumu mbalimbali, na kuendesha tufe la ardhi katika punde hiyohiyo katika duara pana masafa yake yanafika miaka ishirini na nne elfu ndani ya mwaka mmoja na kuizungusha kama Muashiki wa kimawlawy kwa kanuni hiyohiyo.

Wakati inaleta mavuno ya misimu kwa wanyama na mwanadamu, wakati huohuo kwa kanuni hiyohiyo inafanya jua ni chombo cha anga na kukiendesha katika mhimili wake mzunguko wa kuvutika kwa Mwashiki vilevile hali ya kuzitiisha nyota za angani ambazo ni sehemu ya jeshi za mfumo wa jua katika huduma na majukumu matukufu kwa ukamilifu wa mizani na mpangilio.

Na hakika ya uweza huohuo huandika kwa kanuni ya hekima ileile, katika wakati huohuo mamia ya maelfu ya sampuli juu ya ukurasa wa ardhi yote, na ambazo kila moja kati ya hizo ni katika nafasi ya mamia ya maelfu ya vitabu, inaziandika kwa pamoja na hali ya kuingiliana, bila kuchanganya wala kusahau, huku ikidhihirisha kwayo vielelezo vya Ufufuo mtukufu.

Na kwamba uweza huohuo, katika wakati huohuo hugeuza ukurasa wa hewa kuwa ni ubao wa kufuta na kuthibitisha, ukiwa unajaalia kutokana na atomu zake zote kana kwamba ni ncha za kalamu za kitabu hicho na nukta zake, ukizitumia katika nyadhifa nyingi katika yanayohusishwa na mambo, amri na utashi wa kiungu. Hata hakika yake imetoa ukubalifu kwa kila moja miongoni mwa hizo atomu ili zipokee maneno na mazungumzo yote kana kwamba zinajua kwa maneno hayo na kuyaeneza bila ya kosa wala kubabaika kana kwamba hizo atomu ni vijisikio vidogo na vilimi vidogodogo sana. Katika ambayo yanathibitisha kwamba chembe ya hewa ni kiti cha enzi cha amri na utashi wa kiungu.

Na kama hivi basi kwa kulinganishia ishara hii ya muhtasari: Basi yule ambaye ameujaalia huu ulimwengu katika hukumu ya mji uliopangika na kasri yenye kuimarika, karamu ya fahari, kitabu cha muujiza, na Qur’an yenye fasaha, na kushika katika fumbato la uweza wake kwa mizani ya elimu na mpangilio wa hekima tabaka zote za viumbe na duru zake na mataifa yake kwa kuanzia katika atomu moja kati ya atomu zake na kumalizia katika mkusanyiko wa ulimwengu wote, na kuendesha mambo yake na kuyasarifu, na kudhihirisha hekima yake ya hali ya juu jumla ya uweza wake mtukufu na rehema zake kunjufu, na hujulisha kupitia uungu wake mkunjufu, na kutambulisha uwepo wake na upweke wake, utambulisho wa dhahiri kama jua katikati ya mchana. Kupitia kujitambulisha kwake anataka atambulike kwa imani, na kupitia kujipendekeza kwake anataka apendwe kwa ibada, na kupitia neema zake anataka ashukuriwe na kuhimidiwa.

Basi wale ambao hawamjui huyu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu wala hawajibidiishi kwa uja kwa ajili ya kumpenda, bali wanapotelea katika kukanusha na kudhamiria aina fulani ya uadui upande wake. Hawa sio ila ni mashetani katika sura za watu na katika hukumu ya kina Namrudi wadogo na kina Firauni wadogo. Na hapana shaka kwamba wao wanastahiki adhabu ya kudumu isiyo na ukomo.

Neno la kumi na moja nalo: (وَإِلَيْهِ المَصِيْرُ)

Yaani mafikio ni katika eneo la hadhara yake, na katika ulimwengu wake wa kubaki, na katika maisha ya akhera yake, na katika nyumba ya furaha yake ya kudumu, kama alivyo kuwa yeye ni marejeo ya viumbe vyote vya ulimwengu vinaegemea kwake na kurejea katika uweza wake nyororo zote za sababu, ikijulikana kwamba sababu ni pazia zimewekwa mbele ya utendaji wa hiyo kudura, kwa ajili ya kuhifadhi haiba yake na utukufu wake mtakatifu. Basi sababu zote za kiudhahiri ni pazia hazina taathira kabisa katika upatishaji. Na kama sio amri yake (s.w) na utashi wake kisingeweza chochote – hata atomu – kutikisika.

Tunaashiria kwa muhtasari hoja iliyomo katika neno hili kwa hiyo tunasema:

Kwanza:

Hakika ya ufufuo na akhera na uhai wa kubaki ambao neno hili takatifu linauelezea tunahaulisha uthibitisho wake katika (Neno la kumi) na nyongeza zake na katika (Neno la ishirini na tisa) ambalo linathibitisha kutokea kwake kwa hakika ya moja kwa moja kama kutokea kwa majira ya machipuo, na katika (Suala la saba katika Risala ya matunda), na katika Mwale wa (Al-Munajat), na katika juzu za kiimani za Risale-i Nur.

Ni kweli kwamba Risala hizo zimethibitisha nguzo hii ya kiimani kwa hoja zisizo na ukomo, kwamba kutokea kwa akhera ni thabiti kwa daraja ya kutokea uwepo wa dunia ambayo wanasadiki hata wakanushaji wakaidi mno.

Pili:

Hakika theluthi ya Qur’an inajadili akhera na ufufuo, na kujengea madai yote katika hakika hiyo, kwa ajili hii kama ilivyo miujiza yote ya Qur’an na hoja zake, ambazo zinathibitisha haki yake zinajulisha juu ya uwepo wa akhera, hali kadhalika miujiza yote ya Mtume (s.a.w) yenye kushuhudia juu ya ukweli wa utume wake na hoja zote za ukweli wake zinashuhudia juu ya akhera na ufufuo, kwa sababu kitu kikubwa alicholingania Mtume huyu mtukufu (s.a.w) muda wote wa uhai wake ni akhera, kama walivyo mitume watukufu laki moja na ishirini na nne elfu wote walilingania juu ya uhai wa kubakia na furaha ya milele na wamewabashiria hilo wanadamu na wamethibitisha ukweli wa madai yao hayo kwa chungu tele ya miujiza na dalili zenye nguvu. Hapana shaka miujiza yao yote na hoja zao zenye kujulisha juu ya utume wao na juu ya ukweli wao katika madai yao inashuhudia pia juu ya akhera na uhai wenye kubakia ambayo ndio malinganio yao makubwa na ya kudumu zaidi.

Kwa kulinganisha juu ya hili kwamba dalili zote ambazo zinathibitisha nguzo nyingine za imani zinashuhudia kwa nafasi yake juu ya kutokea kwa akhera na juu ya kufunguka kwa milango ya furaha ya kudumu.

Tatu:

Hakika ya muumba wa ulimwengu huu ambaye ameuumba kwa atomu zake zote na sayari zake na sehemu zake na tabaka zake hali ya kuweka katika kila kimoja jukumu bali majukumu mengi kwa ukamilifu wa hekima na huku akitiishia kwa mfululizo kwa kudhihirisha ukamilifu wake uweza wake na uungu wake, na ambaye anatuma makundi ya viumbe msafara baada ya msafara bali anatuma dunia zinazofuatana kufanyika upya zikimiminika katika mahali hapa pa karamu ya wageni pa ulimwengu huu na katika medani ya mtihani ya maisha haya ya kidunia, ili kuonesha midhihirisho isiyo na kikomo ya majina yake mazuri ya milele na ili kuchukua picha za viumbe hao na amali zao na sifa zao kwa kamera za kibarzakh na sinema za kiakhera zimewekwa katika ulimwengu wa kimithali. Na baada ya kuwaruhusu hutuma makundi mengine msafara baada ya msafara, bali anatuma aina katika dunia zenye kwenda na kumiminika katika medani hiyo, ili kuweza kushika nafasi ya kilele ya nyadhifa tukufu na kuwa ni vioo vya midhihirisho ya majina yake mazuri.

Je ni katika yanayo yumkinika kwa huyu muumba mzuri, fundi mtukufu, Allah (s.w) mwenye ukamilifu, asifanye makao ya thawabu na malipo? Na kwamba asisimamishe ufufuo kwa sampuli ya mwanadamu ambaye anayekabiliana kwa utambuzi na akili katika dunia hii ya kwisha na makusudio yote ya muumba huyu mtukufu, na ambaye anampenda huyo muumba na anampendezesha kwa maandalizi yake yote, na ambaye anamjua na kumjulisha, na kuomba kwa unyenyekevu kwake kwa dua zisizo na mpaka ili kufikia mafanikio ya milele na kubaki kiakhera, na ambaye anaomba maisha ya kudumu ambayo yenyewe ni ladha kabisa, anayaomba kwa maumbile yake yote na roho yake na maandalizi yake kwa maumivu yasiyo na mpaka anayoumia kwa akili aliyonayo. Basi je inayumkinika mwanadamu huyu asiwe na thawabu wala adhabu? hasha kwa Allah na hapana mara elfu.

Hakika maelezo na ufafanuzi wa ishara hii fupi yapo kwa sura zake angavu na hoja zake zenye nguvu sana katika Risale-i Nur, kwa hiyo tunaelekeza huko na suala hili refu sana tunalifupisha.

سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَاإِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.