Kituo cha pili

Katika Hoja Yenye Kung’aa

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

Hakika moja katika aya ya mwisho ya sura Al-Fatiha inaashiria milinganisho kati ya watu wa mwongozo na msimamo na watu wa upotevu na kuchupa mipaka. Na aya hiyo ndiyo chimbuko la vipimo na milinganisho yote iliyofungwa kwenye Risale-i Nur. Na vipimo hivi vinabainishwa kwa uwazi kwa ufasaha na kwa mtindo wa ajabu na vinaelezewa kimiujiza na aya ifuatayo katika Surat An-Nur:

اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ Qur’an, 24:35.

Na ambayo ipo baada yake 

أَوْ كَظُلُمَاتٍ فِي بَحْرٍ لُّجِّيٍّ يَغْشَاهُ مَوْجٌ مِّن فَوْقِهِ مَوْجٌ Qur’an, 24:40.

Aya ya kwanza, aya ya nuru inaelekea na ishara kumi kwenye Risale-i Nur na kuitazama, kama ilivyothibitishwa katika Mwale wa kwanza, ikitoa habari ya mustakabali ya muujiza kuhusu tafsiri hiyo ya Qur’an takatifu.

Na kwa kuwa aya hii tukufu ndiyo sababu kuu katika sababu za Risale-i Nur kupewa jina la (Nuru), na kwa msingi wa kubainisha muujiza wa kimaanawy wa aya hii tukufu, kama katika matembezi ya kimawazo ya kimfano ya kubainisha muujiza wa (Nun) ya Naabudu, katika sehemu ya Andiko la ishirini na tisa, hakika mtalii wa dunia katika Riasala ya (Al-Ayatul Al-Kubra) aliuliza viumbe vyote na aina zote za vilivyomo wakati wa kuuliza juu ya muumba wake na kumtambua, na akamtambulisha kwa njia thelathini na tatu na hoja za kukata shauri kwa elimu ya yakini na yakini yenyewe, mtalii mwenyewe alitembea kwa akili yake na moyo wake na mawazo yake katika anga za matabaka za enzi mbalimbali, ardhi na Mbingu, bila ya kupatwa na uchovu wowote, bali aliendelea kutembea ili kuweza kukidhi kiu yake hadi akatembea katika dunia pana yote, akatafiti pande zake zote kama anayetembea katika mji. Akiegemea katika akili yake wakati mwingine kwenye Qur’an na mara nyingine katika hekima ya falsafa akivumbua tabaka za mbali kwa miwani ya mawazo, hadi akaziona hakika kama zilivyo katika uhalisia, akaelezea sehemu ya hizo kwenye risala hiyo (Ishara kuu).

Sisi hapa tunabainisha kwa muhtasari namna tatu za ulimwengu tu kati ya aina hizo za ulimwengu na matabaka mengi, ambayo yule mtalii aliingia kwa matembezi ya kimawazo, na ambayo ndio hakika yenyewe, isipokuwa imedhihiri katika maana ya mithali na katika sura yake. Tunabainisha aina hizi za ulimwengu kama vielelezo na mifano kwa ajili ya milinganisho iliyokuja mwishoni mwa sura (Al-Fatiha), na kama mfano kwa upande wa nguvu ya kiakili pekee.

Ama mambo mengine aliyoyashuhudia na milinganisho yake tunaielekeza katika milinganisho iliyomo kwenye Risale-i Nur.

Kielezo cha kwanza:

Mtalii yule ambaye hakuja duniani ila apate kumkuta muumba wake na kumtambua, aliongea na akili yake kwa kusema:

Kila kitu tumekiuliza kuhusu muumba wetu, na tukachukua jibu lenye kuridhisha na kutosheleza, lakini kama inavyopokewa katika mithali: (Kuhusu jua inapasa kuliuliza jua lenyewe) sasa tunawajibika kufanya matembezi mengine, kwa ajili ya kumtambua muumba wetu kupitia midhihirisho ya sifa zake tukufu (kama elimu, utashi, na uweza) na kutokana na athari zake za ajabu na kutokana na kudhihiri kwa majina yake mazuri, akaingia duniani kwa shabaha hii, na haraka akapanda jahazi la ulimwengu kama watu wa upotevu ambao wanawakilisha mrengo mwingine, na akaiga miwani ya sayansi na falsafa isiyofungamanishwa na hekima ya Qur’an. Na akatazama kwa miwani ya mtazamo wa Jiografia isiyoongozwa na Qur’an akaona: Kwamba ardhi inaogelea katika anga lisilo na mipaka, ndani ya mwaka mmoja inamaliza mzunguko unaofikia miaka ishirini na nne elfu, ni zaidi ya kasi ya kurushwa kwa kombora kwa mara sabini. Na hali ya kuwa imebeba mabegani mwake mamia ya maelfu aina mbalimbali ya wenye uhai wasio na uwezo dhaifu. Kwa dakika moja tu kama itapotea na kukosea njia yake au kugongana na nyota inayoelea, itaparaganyika kwa kudondoka kwenye anga lisilo na mwisho, na kumwaga vilivyo juu yake wakiwemo viumbe hai dhaifu na kuwamimina kwenye kutokuwepo, mchezo na kupotea kabisa.

Akapata hisia ya giza la kimaanawy la kutisha lenye kukaba kama giza katika bahari yenye mawimbi inayotokana na ufahamu huu ambao uko katika mrengo wa

المَغضُوبِ عَلَيهِمْ

na

الضَّالِّينَ

Akasema kutoka kwenye kina cha moyo wake: Majuto yaliyoje! tumefanya nini? Kwa nini tumepanda jahazi hili lenye kutisha? Na tutaokoka vipi kutokana na hatari hii? akatupa miwani ya falsafa hiyo pofu na akaivunja, na akaingia mrengo wa

الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ   

muda huo hekima ya Qur’an inamuokoa ikiikabidhi akili yake miwani inayobainisha hakika kikamilifu, kwa kusema: Tazama sasa. akatazama na kuona:

Hakika jina la

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

limechomoza katika njia ya kauli yake (s.w):

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ Qur’an, 67:15.

na kufanya ardhi kuwa ni jahazi la amani na salama linakata mawimbi ya bahari ya ulimwengu mpana kwa mpangilio madhubuti ikizunguka jua kwa ajili ya hekima nyingi na manufaa mbalimbali, ikishehenishwa wenye uhai na riziki wanazohitajia, ikileta mazao ya misimu kwa wahitaji wa riziki, na Allah (s.w) ameweka malaika wawili wanaoitwa (Ng’ombe na Samaki) baharia wawili na viongozi wawili wa jahazi hilo. Wanaiendesha katika matembezi kupitia kwenye Ufalme wa kiungu ambao una haiba na kupendeza mno, wapate kutulia viumbe wa muumba mtukufu na wageni wake katika anga la ulimwengu huu mpana. Na kama hivyo utalii huu wa kutisha unabainisha hakika ya

اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

ambapo unamtambulisha muumba wake kwa udhihirisho wa jina hili.

Mtalii yule baada ya kutambua maana hii kutokana na kuishuhudia kwake ardhi akakariri kutoka katika kina cha moyo wake:

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

na akaingia katika kundi la wale walioneemeshwa.

Kielezo cha pili katika aina za ulimwengu alizoshuhudia yule mtalii:

Baada ya yule mtalii kuondoka kwenye jahazi la dunia, akaingia ulimwengu wa mwanadamu na wanyama, akatazama kwenye ulimwengu kwa miwani ya hekima ya kiasili isiyopokea ilhamu kwa maisha na roho kutoka katika dini, akaona kwamba haja zisizo na mipaka kwa ajili ya wenye uhai wasiohesabika, na maadui wengi mno wanaowazunguka wakiwapa udhia na kuwapa madhara makubwa katika matukio katili yasiyo na huruma, nao hawamiliki katika rasilimali isipokuwa moja katika elfu bali moja katika mia moja elfu mkabala na mahitajio hayo. Vitu hivyo vinavyowadhuru havimo katika uwezo wao isipokuwa moja ya milioni! Yule mtalii akapata maumivu mbele ya hali hii ambayo inachochea huruma, hofu, na maumivu – kwa kutokana na kuwa mwanadamu ana mahusiano ya huruma wa jinsi na huruma ya kisampuli na akili – akapata uchungu mkubwa kwa hali yao na kawahuzunikia huzuni inayompa maumivu ya hisia ya kukata tamaa, kama adhabu kali Jahannam, akajuta majuto elfu moja kwa kuingia kwake ulimwengu huu mbaya wa huzuni. Na wakati akiteseka na machungu haya na kupata tabu nayo kiasi cha kupata taabu tahamaki hekima ya Qur’an tukufu inamsaidia na kumpa huduma ya haraka, ikimkabidhi miwani ya

المَغضُوبِ عَلَيهِمْ

ikimwambia: Tazama, akatazama na kuona:

Kwamba kila jina katika majina ya Allah (s.w) mazuri mifano: Ar-Rahman, Ar-Rahiim, Ar-Razaaq, Al-Munim, Al-Kariim, Al-Hafiidh, yamechomoza mwanga kama jua lenye kuangaza, na hii kwa kudhihiri


اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

katika njia za aya tukufu:

ما مِنْ دَابَّةٍ إلاَّ هُوَ ءَاخِذٌ بِنَا صِيَتِهَا Qur’an, 11:59.

وَكَأَيِّن مِن دَابَّةٍ لَا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ Qur’an, 29:60.

وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ Qur’an, 17:70.

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ Qur’an, 82:13.

Ikafunika dunia ya mwanadamu na wanyama kwa rehema hiyo yenye kuenea na hisani ya jumla hata ikawa imegeuka kuwa ni pepo ya muda. Mtalii akatambua kwamba hii dunia na vyote vilivyomo vinamtambulisha vema mkaribishaji mwema katika nyumba hii ya wageni ambayo ni nzuri yenye kustahiki kushuhudiwa, iliyojaa mazingatio, akamshukuru Allah (s.w) mara elfu moja kwa kusema: Al-Hamdulillah Rabbi Al-Alamiin.

Kielelezo cha tatu katika matembezi ya mtalii ambacho kina mamia ya mambo aliyoyashuhudia.

Hakika ya yule mtalii wa dunia, ambaye anataka kumjua muumba wake, kupitia midhihirisho ya majina yake mazuri, na sifa zake tukufu akisemesha akili yake na mawazo yake kwa kusema: Haya na tupande katika mbingu za juu kama roho na malaika hali ya kuwa tumeacha miili yetu hapa ardhini, na tuwaulize wakazi wa mbinguni kuhusu muumba wetu. Akili ikapanda fikra na moyo ukapanda mawazo ya kufikirika vyote vikapanda juu mbinguni wakiongozwa na elimu ya falaki, na walitazama kwa miwani ya wale (Waliopotea… waliokasirikiwa) yaani kwa miwani ya falsafa ambayo haipi umuhimu wowote dini, mtalii yule akashuhudia: Kwamba maelfu ya sayari na nyota zenye kutoa moto na yenye kuizidi ukubwa ardhi mara elfu zinakwenda na kukimbia zikiingiliana kwa kasi zaidi kuliko makombora mara mia moja nazo zikiwa mfu hazina utambuzi, kana kwamba hazina udhibiti wowote, hata ikiwa itakosea moja wapo njia yake dakika moja kwa sadifu na kugongana na nyingine ambayo haina utambuzi wowote mambo yatavurugika na kuenea fujo na kutokea kinachofanana na kiama katika huo ulimwengu usio na mipaka.

Hakuna upande ambao yule mtalii aliangalia isipokuwa ulimsababishia upweke, mshangao, tahayari na hofu, akajuta mara elfu kwa kupanda kwake mbinguni, kwani akili ilivurugika na mawazo na kuchanganyikiwa kwa ujumla. Hata vikasema: Sisi hatutaki kujua maana haya mbaya yenye kuleta maumivu na mateso kama adhabu ya Jahannam, bali hatutaki nafsi zetu hata kushuhudia hayo, kwa sababu jukumu letu la msingi ni kuona na kuonesha hakika nzuri. Na wakati vikisema hivi tahamaki mdhihirisho kutoka

اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

ukaangaza majina mazuri ya kiungu: (Muumba wa mbingu na ardhi) na (Mtiishaji wa jua na mwezi) na (Bwana mlezi wa walimwengu) na mfano wa hizo, ziliangaza kama jua kupitia katika njia za aya tukufu:

وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاء الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ Qur’an, 67:5.

أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاء فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا Qur’an, 50:6.

ثُمَّ اسْتَوَى إِلَى السَّمَاء فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ Qur’an, 2:29.

Nuru za majina hayo zikajaza mbingu hizo zote kwa nuru na malaika. Na kuzigeuza kuwa msikiti mkubwa na kambi kubwa. Yule mtalii akaingia akiwa katika kundi la

الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ

na akaokoka kutokana na giza la


أَوْ كَظُلُمَاتٍ فِي بَحْرٍ لُّجِّيٍّ

na ghafla anaona milki ya ufalme nzuri ya kifahari yenye kupangiliwa kama pepo, thamani ya akili na mawazo ikapanda na majukumu yake yakawa juu kwa daraja elfu moja kwa yale waliyoyashuhudia kila upande ambaye anamtambulisha muumba mtukufu. Na hivi ndivyo tunavyomalizia somo letu pana tukitosheka na ishara hii fupi mno tukielekeza baki ya mambo aliyoyashuhudia mtalii ulimwenguni katika Risale-i Nur kwa kulinganisha juu ya vielelezo hivi vitatu vilivyotajwa kati ya mamia ya vielelezo katika utalii wake ili kumtambua ambaye ni wajibu kuwepo kupitia midhihirisho ya majina yake Allah (s.w). Na tunajaribu kwa kuashiria kwa muhtasari mno kumtambua muumba wa ulimwengu – kama ujuzi wa yule mtalii – na hii ni kupitia athari na kudhihiri kwa sifa za (Elimu), (Utashi) na (Uweza) tu kati ya sifa saba tukufu za muumba wetu na kutokana na hoja zinazothibitisha sifa hizo tatu tukufu, na tunaelekeza maelezo yake yakatazamwe kwenye Risale-i Nur.

Kifungu cha Kiarabu kifuatacho ni uradu wangu wa kutafakari wa kudumu uliofupishwa kutokana na muhtasari wa Al-Hizbu An-Nur Al-Araby, ambacho kinabainisha ngazi tatu kati ya ngazi thelathini na tatu za maneno (Al-Lahu Akbar). Kwa hiyo tunaashiria sehemu ya maelezo yake na mfano wa tafsiri yake kwa ishara fupi yale yaliyoshughulisha sana wanazuoni wa elimu ya Al-Kalaam na wanazuoni wa itikadi kujua sifa hizo kwa midhihirisho yake ulimwenguni na kusadikisha kwa imani yenye kina kwa dhati ya yakini. Fungu hili la Kiarabu linafungua njia kwenda kwenye imani kamili kwa hizo sifa tatu – kwa elimu ya yakini – juu ya uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo kwa daraja ya uwazi:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلّهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَم يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ
 الذُّلَّ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا Qur’an, 17:111.

Allah (s.w) ni mkuu kuliko chochote kwa uwezo na ujuzi kwani yeye ni mjuzi wa kila kitu kwa elimu yenye kufunika kila kitu yenye kuambatana na dhati yake, inaambatana na vitu haiyumkiniki chochote kutengana nayo kwa siri ya kuhudhuria, ushahidi na kuzungukia kinuru, na kwa siri ya kuambatana kwa uwepo kwa ujuzi na kuzunguka nuru ya elimu kwa ulimwengu wa kuwepo.

Naam, mipangilio iliyowekwa kwenye vipimo, kuwiana vipimo kulikopangiliwa, hekima za makusudio ya jumla, na uangalizi mahususi wa jumla, hukumu zilizonadhimika, kadiri zenye kuleta matunda, nyakati maalum, riziki zilizopangwa, uzuri uliopendezesha, kupewa umuhimu kulikopambwa, upeo wa ukamilifu wa mpangilio, uratibu na kusawazika, kuwekwa vema, kupangiliwa vipimo na kupambanuka kwa ukamilifu wa wepesi kabisa, vinajulisha juu ya kufunika kwa ujuzi wa kila kitu wa mjuzi wa mambo ya ghaibu.

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ Qur’an, 67:14.

uwiano wa kujulisha ufundi wa kumtengeneza mwanadamu vizuri juu ya utambuzi wa mwanadamu kwa uwiano wa kujulisha uzuri wa umbo la mwanadamu juu ya ujuzi wa muumbaji wa mwanadamu ni kama mng’aro mdogo wa nyota ya kilimia katika usiku wenye giza kwa myale angavu ya jua katikati ya mchana. Tunaashiria kwa ishara fupi katika (Ujuzi wa kiungu). Hakika hii ya kiimani iliyo wazi, ndani ya tafsiri fupi mno ya kifungu hiki cha Kiarabu, tukielekeza maelekezo yake ya kina kwenye Risale-i Nur, tunasema:

Sehemu ya pili imeandikwa wakati wa kutaabika na maradhi ya kutisha sikupata kuyaona uhai wangu wote kutokana na kutiliwa sumu. Hivyo basi nataraji kutazamwa kasoro zangu kwa mtazamo wa msamaha. Na (Khosrouv) anaweza kutengeneza, kubadili, na kurekebisha analoliona haliko sawa. (Mtunzi)

Naam, kama ilivyo rehema inajibainisha yenyewe kama jua kwa riziki zake za ajabu na kuthibitisha kwa dalili yenye kukata shauri kwamba nyuma ya pazia ya ghaibu kuna Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, kadhalika (Ujuzi) ambao umechukua nafasi kati ya mamia ya aya za Qur’an, na ambao ni – kwa upande mmoja – ni bora ya sifa saba tukufu inajibainisha kama mwanga wa jua kwa matunda na hekima za nidhamu na mizani, na inajulisha juu ya uwepo wa mjuzi wa kila kitu kwa namna iliyo wazi kabisa.

Naam, uwiano wa dalili ya kutengenezwa mwanadamu kwa mpangilio kuliko kadiriwa utambuzi wake na ujuzi wake, na dalili ya uzuri wa kuumbwa mwanadamu katika umbo bora kabisa kwa ujuzi wa muumba wa mwanadamu na hekima yake (s.w) kama uwiano wa mwanga mdogo wa kimulimuli katika usiku wenye giza kulinganisha na mionzi miangavu ya jua katikati ya mchana.

Na sasa kabla ya kuingia katika kubainisha dalili za ujuzi wa kiungu, hakika dalili ya midhihirisho ya sifa hiyo takatifu katika aina ya viumbe juu ya dhati takatifu, ni dalili ya wazi mno mazungumzo ambayo yamepita usiku wa Miiraji ya mtume (s.a.w), kuhusu hadhi ya mtume (s.a.w) kuhudhuria na kuongea na Allah (s.w) yameshuhudia na kujumuisha hilo pale aliposema:

(At-Tahiyyaatu Al-Mubarakatu As-Swalawatu At-Twayyibatu ) kwa jina la wenye uhai na viumbe wote, kwa kuwa yeye ni mjumbe na mtume wake, akapeleka kwa muumba wake mtukufu zawadi za viumbe wote wenye uhai, kwa namna ya ujuzi wa viumbe wote hao kwa mola wao kwa midhihirisho ya ujuzi, hayo ameyasema katika mahali pa salamu na kwa niaba ya wenye utambazi wote. Yaani, makundi manne ya wenye uhai wote hupeleka zawadi kwa maneno manne:

(At-Tahiyyaatu Al-Mubarakatu As-Swalawatu At-Twayyibatu ) na kwa midhihirisho ya jina la azali ya milele, maamkizi yake na pongezi zake na uja wake na utambuzi wake mzuri mbele ya mjuzi wa mambo ya ghaibu, kwa hiyo kusoma mazungumzo haya ya Miiraji takatifu imekuwa ni faradhi kwa Waislamu wote katika tashahudi.

na kwa midhihirisho ya jina la azali ya milele, maamkizi yake na pongezi zake na uja wake na utambuzi wake mzuri mbele ya mjuzi wa mambo ya ghaibu, kwa hiyo kusoma mazungumzo haya ya Miiraji takatifu imekuwa ni faradhi kwa Waislamu wote katika tashahudi.

Tutabainisha maana kati ya maana za mazungumzo hayo matukufu kwa ishara nne za muhtasari mno, tukielekeza ufafanuzi wake kwenye Risale-i Nur.

Neno la kwanza ni: (التّحِيَّاتُ لِلّه)

Na maana yake kwa muhtasari:

Ikiwa fundi fulani atatengeneza mashine ya ajabu, kwa kutumia ujuzi mpana alionao na busara ya ajabu, basi kwa kila atakayeiona mashine hiyo ya ajabu atampongeza fundi huyo kwa heshima na kupendezwa. Na atampa zawadi na maamkizi ya kimaada na kimaanawy pamoja na sifa iliyojazwa maelezo ya kupendeza. Na kwa zamu yake mashine nayo inapongeza na kubariki mafundi wake kwa ulimi wa hali na kumpa fundi wake zawadi na maamkizi ya kimaanawy, na hii ni kwa kubainisha matakwa ya fundi huyo kikamilifu, na kuonesha maajabu ya umakini ya ufundi wake na uhodari wake wa kielimu.

Vivyo hivyo makundi yote ya walio hai katika viumbe wote, bali kila kundi kati yao, na kila mmoja kati yao, ni mashine ya muujiza kwa pande zake zote, inampongeza fundi wake mtukufu ambaye anajitambulisha kwa midhihirisho ya ujuzi wake mpana ambao unaona uhusiano wa kila kitu na kitu kingine chochote kiwacho, na kukifikishia kila mahitaji ya lazima katika maisha yake katika wakati wake, kinampongeza na kumpa maamkizi na kumbariki kwa maneno (At-Tahiyaat Lillahi) kwa ndimi za hali ya maisha yao, kama zilivyo ndimi za wenye utambuzi kama wanadamu majini na malaika wanavyompongeza. Vyote vyenye uhai hupeleka maamkizi yao moja kwa moja kwa maana ya ibada kwa muumba wao ambaye anajua hali za viumbe wote. Basi mtume Muhammad (s.a.w) akaeleza wakati alipohudhuria mbele ya mwenye kupasa kuwepo usiku wa Miiraji kwa jina la vyenye uhai vyote kwa kusema: (At-Tahiyyatu Lillah) badala ya kutoa salamu, kwa kukabidhi maamkizi ya makundi yote ya vyenye uhai na zawadi zao na salamu zao za kimaanawy.

Naam, ikiwa mashine iliyopangika katika hali ya kawaida inajulisha juu ya kuwepo fundi mahiri hodari kwa utengenezaji wake wa mpangilio na wenye vipimo sawa, basi kila mashine katika mashine hai ambazo zinajaza ulimwengu na ambazo ni nyingi mno hazihesabiki, kwa hiyo zinadhihirisha miujiza elfu moja na moja ya kielimu, bila shaka wenye uhai wanajulisha juu ya kupasa kuwepo kwa mtengenezaji wao wa milele na kuwa mstahiki wa kuabudiwa kwa midhihirisho ya ujuzi ambayo ni kama mwanga wa jua kulingana na kujulisha kwa mashine hiyo ambayo kama mwanga wa kimulimuli.

Neno la pili tukufu katika maneno ya Miiraji ni: (المٌبَارَكَاتُ)

Kwa kuwa swala ni Miiraji ya muumini kama lilivyothibiti hilo katika hadithi tukufu, na ndani yake kuna midhihirisho ya Miiraji tukufu, na kwamba mtalii wa dunia amempata muumba wake mjuzi wa mambo yote yasiyoonekana katika kila ulimwengu kwa sifa ya ujuzi. Na sisi vilevile tunaingia pamoja na yule mtalii ulimwengu mpana wa Al-Mubaarakatu na ambao unawatamkisha wengine kwa kubariki na kutoa pongezi, na tujaribu kumjua muumba wetu kwa elimu ya yakini – kama yule mtalii – kupitia midhihirisho ya muujiza makini kwa sifa tukufu ya kiungu, sifa ya ujuzi. Na hii wakati wa kushuhudia ulimwengu huo, ulimwengu wa Al-Mubaarakatu na kuukagua, na hasa wadogo wa wenye roho nyororo wenye kubarikiwa wasio na makosa yoyote, na kokwa na mbegu ambazo ni mikebe midogo inakusanya makadirio na programu ya wenye uhai.

Naam, hakika tunashuhudia kwa macho yetu, hakika ya watoto wote hao wapole na wasio kuwa na hatia na sehemu hizo za kuhifadhia na mikebe midogo yenye kubarikiwa, vyote vinatoka na kila mojawapo kati yao kwa mkupuo mmoja kwa ujuzi wa mjuzi wa kila kitu mwingi wa hekima ili kwenda katika kile ambacho kimeumbiwa kwa ajili yake hadi michakato hiyo inamtamkisha kila anayevitazama kwa mtazamo wa hakika kwa kusema: Baarakallahah, Maa shaallah mara elfu elfu.

Naam, manii kwa mfano mayai, mbegu na kokwa, kila kimoja kati ya hivyo ni ndani ya mpangilio makini unaokuja kutokana na elimu. Na kwamba mpangilio huo ni ndani ya kipimo kinachotokana na umahiri kamili, na kipimo hicho ni ndani ya mpangilio mpya, na hii ni ndani ya upimaji na uzani mpya. Na hii nayo kwa nafasi yake ni ndani ya malezi, na upambanuzi, na alama zenye kutenganisha zilizokusudiwa mbali na zenye kushabihiana mfano wake. Na hii ni ndani ya upambaji na urembaji uliofanywa vizuri kabisa, na hii pia ni ndani ya zana kamili na uwekaji sura mnasaba makini wenye hekima tele. Na hii ni ndani ya kutofutiana kwa nyama za viumbe hao, matunda na vinavyoliwa kati ya hivyo, ili kuwashibisha wahitaji wa riziki kushibisha kwa takirima kwa hali inayoendana na maonjo yao. Na hii nayo ndani ya nakshi na maumbo ya mapambo yenye kutofautiana yamepambwa kwa ujuzi na muujiza, na hii ni ndani ya harufu nzuri anuwai na ladha tamu mbalimbali, kiasi kudhihiri kwa sura za viumbe wote na kupambanuka kwa viumbe vyote hivyo na kujipembua baina yake na vingine kwa nidhamu kamili, bila kukosea wala kusahau katika kasi isiyo na mipaka, na upana usio kuwa na mipaka, na pamoja na kuwa vimo kwenye wingi usio na mipaka, na kudumu kwa hali hiyo ya ajabu kwa kila msimu, kunafanya kila mmoja kati ya wote wanadhihirisha ujuzi wa kiungu kwa ndimi hizi kumi na tano, na macho kuyageuzia kwenye umahiri wa ajabu wa Bwana wao mlezi, na kwayo vinajulisha juu ya ujuzi wake wa kimuujiza, basi kwa uwazi humtambulisha kama jua fundi wao ambaye ni wajibu kuwepo, mjuzi wa yote yasioonekana.

Basi huu ushahidi wao mpana angavu sana na pongezi zao na kumheshimu kwao muumba wao, ndiyo ambayo mtume (s.a.w) ameielezea ambaye ameongea kwa jina la viumbe wote katika usiku wa Miiraji na akasema: (Al-Mubaarakaatu) badala ya kutoa salamu.

Neno la tatu nalo ni (وَالصَّلَوَاتُ)

Hakika watu milioni mia moja miongoni mwa wenye Imani hulitangaza neno hilo tukufu ambalo limesemwa katika Miiraji kuu ya Muhammad (s.a.w), na husemwa katika Miiraji maalum ya muumini, yaani katika tashahud ya swala, kila siku kwa uchache mara kumi, kwa kumfuata kwao mtume mtukufu (s.a.w) wanalitangaza pande zote za ulimwengu wakiliwasilisha neno hilo mbele ya hadhara ya kiungu.

Na kwa msingi wa ufafanuzi ulio wazi na uthibitisho wenye nguvu wa kukata shauri, katika Risala ya Miiraji (Neno la thelathini na moja) na kufafanua kwake hakika zote za Miiraji, hata wakati wa kuongea na mpingaji mwenye ukaidi, tunaelekeza katika risala hiyo kupata maelezo ya somo hili na hoja zake, isipokuwa tunaashiria kwa muhtasari sana wa maana pana wa neno hili la tatu la Miiraji na ambalo aina za limwengu za ajabu za makundi ya wenye roho na utambuzi zinalibainisha, tunapojaribu kumtambua muumba wetu, uwepo wake, ukamilifu wa wasifu wake wa Rahmaniya na Rahiimiya, ukubwa wa uweza wake na kuenea kwa utashi wake tunashuhudia aina hizo za ulimwengu, na hiyo ni kupitia midhihirisho ya ujuzi wa kiazali.

Naam, hakika tunashuhudia katika ulimwengu huu kila chenye roho hupata utambuzi kwa hisia na kwa maumbile – hata kama haikuwa kwa utambuzi na kwa akili – kwamba anataabika na hali ya kushindwa na udhaifu bila mipaka, pamoja na kuwa maadui zake na vinavyomuumiza ni vingi mno havihesabiki, na kila mmoja kati yao anageuka geuka kwenye ufakiri na uhitaji bila mipaka pamoja na mahitaji yake na ayatafutayo ni mengi bila mipaka. Na kwa kuwa uwezo wake na rasilimali yake havitoshelezi moja ya elfu katika mahitaji hayo, utamuona anaomba msaada na kulia kwa nguvu zote anazomiliki, na anayenyekea kwa kimaumbile na hali iliyomo ndani yake. Ambapo anaelekea kwenye mamlaka ya mjuzi wa kila kitu mweza wa kila kitu kwa sauti yake maalum na ulimi wake maalum na kwa dua swala na maombi na manyenyekevu na aina ya swala inayomhusu yeye tu, hapo tunashuhudia kwamba mweza mwingi wa hekima mjuzi wa kila kitu ujuzi bila kizuizi, anajua kila haja miongoni mwa haja za hao wenye uhai na kuwatimizia na anaona kila ugonjwa katika magonjwa yao na kuwasaidia, na anasikia kila wito na maombi wanayomuomba kimaumbile na kumtaka msaada na anawaitikia, Allah (s.w) anageuza vilio vyao kuwa ni tabasamu tamu na maombi yao ya msaada anayabadili kuwa aina za sifa njema na shukurani.

Hakika ya msaada huu wenye alama ya hekima ujuzi na rehema unajulisha kwa uwazi midhihirisho ya ujuzi na rehema kwa mwenye kujibu maombi yote mtoa msaada Mwenye kurehemu Mkarimu sana. Basi swala zote na ibada zinatoka katika aina hizi za limwengu, limwengu za wenye roho, zinazopanda kwa huyo Mwenye kujibu maombi yote Mwenye kutoa msaada Muhammad (s.a.w) ameyaelezea – kwa maana hii – na ameyawasilisha na kuyahusisha katika Miiraji kuu, na kila muumini anayakariri katika Miiraji ndogo katika kila swala. kwamba (As-Swalawaatu at-Twayyibbatu lillah).

Neno la nne tukufu nalo: (وَالطَّيِّبَاتُ لله)

Kwa kuwa hakika nyingi za Risale-i Nur zinapita moyoni mwangu kwenye dhikiri za swala, nimejiona kama ninapelekwa – kwa msingi wa hekima hii – kubainisha hakika za maneno ya sura Al-fatiha na Tashahud kwa ishara fupi bila ya hiari yangu.

Na kama hivi, neno takatifu: (At-Twayyibaatu) ambalo limesemwa katika Miiraji ya Muhammad (s.a.w) ambalo linabeba maana ya mambo mazuri yote ambayo hayana mpaka, na yatokanayo na wanadamu, majini, malaika na maruhani ambao ni watu wa ujuzi na Imani na utambuzi wa jumla. Na ambao wanaupendezesha ulimwengu wote kwa mazuri na mema yao na ibada zao nzuri, zote zinazoelekea kwenye ulimwengu wa vizuri, na ambao wanatambua kikamilifu mazuri na mema yasiyokuwa na mpaka ya mzuri kabisa wa milele, na uzuri wa kudumu wa majina yake mazuri ambayo yanatia uzuri ulimwengu hivyo wanaukabili kwa ibada za jumla zilizojazwa ashiki na shauku, na harufu nzuri zenye uturi za Imani yenye kuangaza, na maarifa mapana na sifa zote njema na hata wanazoziwasilisha kwa Muumba wao Mtukufu.

Na kwa mujibu wa maana hii pana ya mazuri hayo yasiyo na mipaka na kwa madhumuni ya yaliyosemwa kwenye Miiraji, umma wote hukariri neno hilo takatifu kwenye Tashahudi kila siku bila uchovu wala uvivu.

Naam, hakika huu ulimwengu ni kioo kinachoakisi uzuri wa milele, na wema usio na mipaka, bali midhihirisho yake (s.w). Na uzuri uliomo kwenye ulimwengu na wema unatokana na wema huo wa milele, na kuchukua uzuri kwa kujinasibisha nao hivyo hupanda na kuwa juu, wakati bila ya kujinasibisha huko ulimwengu ungegeuka kuwa ni matanga yenye kutisha na mivurugiko na kuteketea na fujo kubwa mno.

Na kujinasibisha hutambulika kwa maarifa ya Wanadamu, majini, Malaika, Maruhani na kwa kusadiki kwao, na hao ni waliganiaji wenye kujulisha ufalme wa kiungu, hata sifa njema wanazozitangaza walinganiaji hao na kueneza sifa zao kwenda kila upande kwenye ulimwengu na kwenye Arsh tukufu kwa hili hewa husimama katika hali ya kujiandaa kutimiza jukumu hili, kana kwamba ni ndimi zinazoongea zimefanywa kuwa ndogo, kuwasilisha maamkizi hayo mazuri mbele ya hadhara ya kiungu. Ikapita kwenye moyo wangu kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kutunuku jukumu hilo muhimu la ajabu sana kwa hewa.

Na kama hivi kama alivyo mwanadamu na malaika wanamtambulisha mwabudiwa Mtukufu kwa imani yao na ibada zao, ndivyo hivyo pia Mwingi wa hekima mwenye utukufu anajitambulisha utambulisho wa dhahiri wa wazi kwa maandalizi mengi jumuishi aliyoyaweka kwa walinganiaji na zana za ajabu alizowapa na mambo makini ya kielimu yaliyomo ndani yao, na akamjaalia kila mmoja kati yao kuwa na mafungamano na ulimwengu wote kana kwamba kila mmoja kati yao ni ulimwengu mdogo.

Mathalani:

Kuumba nguvu yenye kuhifadhi ya kimawazo na ya kutafakari, na mashine za ajabu kama hizi, mahali padogo kwenye ubongo wa mwanadamu hauvuki ukubwa wa jauzi moja (ni aina ya mbegu kama karanga hivi), na akajaalia nguvu yenye kuhifadhi ni sawa na maktaba kubwa, inabainisha kwamba Allah (s.w) anajidhihirisha kwa midhihirisho ya ujuzi wa kiazali waziwazi kama jua katikati ya mchana. Hakika maradhi yangu makali mno hayaruhusu kufafanua na niliyoyaandika hakika ni chimbuko na msaada wa jukumu la (khosrouv) katika kutafsiri na sio vingine. (Mtunzi)

Na sasa tunaashiria kwa muhtasari mno, maana ya kifungu cha maneno cha Kiarabu, kilichoelezwa kwenye utangulizi wa somo hili, wenye kuonesha hoja za jumla za ujuzi wenye kufunika kila kitu, na hiyo ni hoja kubwa inakusanya dalili kupita kiasi na kubainisha ujuzi wa kiazali kwa dalili kumi na tano.

Dalili ya kwanza kati ya dalili kumi na tano:

Ni: [Mipangilio iliyowekwa kwenye vipimo]

Yaani kupangika kuliko kadiriwa kiasi chake na kunako onekana kwenye viumbe vyote, na kadhalika kuwa katika nidhamu kulikowekwa kwenye vipimo kwenye viumbe hivyo, vinashuhudia juu ya ujuzi wenye kuingia kwenye kila kitu. Naam, kuanzia ulimwengu wote ambao kama kasri ya kupendeza yenye kupangiliwa sehemu zake, na kutoka katika mfumo wa jua, na kutoka katika kipengele cha hewa ambayo atomu zake zinaeneza maneno na sauti uenezaji unaoleta tahayari na kustaajabu, unabainisha mpangilio wa kupendeza, na kutoka katika uso wa ardhi ambayo huandaa aina mia tatu elfu katika aina mbalimbali kila majira ya machipuo katika nidhamu na mpangilio kamili, katika kila zana miongoni mwa zana za kila kiumbe hai bali katika kila kiungo ndani yake bali katika kila chumba kidogo katika mwili wake, bali katika kila atomu katika atomu za mwili wake, yote hayo hakika ni athari ya ujuzi maridadi unaozungukia kila kitu haupotei wala kusahau.

aani kupangika kuliko kadiriwa kiasi chake na kunako onekana kwenye viumbe vyote, na kadhalika kuwa katika nidhamu kulikowekwa kwenye vipimo kwenye viumbe hivyo, vinashuhudia juu ya ujuzi wenye kuingia kwenye kila kitu. Naam, kuanzia ulimwengu wote ambao kama kasri ya kupendeza yenye kupangiliwa sehemu zake, na kutoka katika mfumo wa jua, na kutoka katika kipengele cha hewa ambayo atomu zake zinaeneza maneno na sauti uenezaji unaoleta tahayari na kustaajabu, unabainisha mpangilio wa kupendeza, na kutoka katika uso wa ardhi ambayo huandaa aina mia tatu elfu katika aina mbalimbali kila majira ya machipuo katika nidhamu na mpangilio kamili, katika kila zana miongoni mwa zana za kila kiumbe hai bali katika kila kiungo ndani yake bali katika kila chumba kidogo katika mwili wake, bali katika kila atomu katika atomu za mwili wake, yote hayo hakika ni athari ya ujuzi maridadi unaozungukia kila kitu haupotei wala kusahau.

Naam, hakika kuwepo kwa mpangilio huu wenye kuwekwa kwenye vipimo na nidhamu timilifu katika yote yaliyoelezwa yanajulisha kwa dalili yenye nguvu na kubainisha na kuutilia ushahidi kwa ufasaha kamili ujuzi wenye kuzungukia kila kitu.

Dalili ya pili ni [Uwiano wa vipimo uliofumwa]

Kuwepo kwa mizani katika ukomo wa mpangilio na kipimo katika ukomo wa uwiano katika vitu vyote vilivyotengenezwa vilivyomo ulimwenguni sehemu zake na jumla yake, kuanzia sayari zinazopita mbinguni hadi katika chembe nyekundu na nyeupe kwenye damu, kwa hakika kwa uwazi kabisa inajulisha kuwepo kwa ujuzi unaozungukia kila kitu na inalishuhudia hilo ushahidi wa kukata shauri kabisa.

Naam, tunashuhudia kwa mfano viungo vya mwanadamu au nzi na zana zake, bali hata vyumba vidogo vya mwili wake na chembe zake ndogo za damu nyekundu na nyeupe vimewekwa mahali pake panapofaa mnasaba na panapowiana, kwa kipimo cha hisia kali mno makini mno vinawiana uwiano timamu baadhi yake na baadhi nyingine pamoja na baki ya viungo vingine. Kwa kiasi inajulisha kwa kukata shauri kabisa kwamba asiyekuwa na ujuzi wenye kuzungukia kila kitu hawezi kuviweka vitu hivyo katika hali hiyo na haiwezekani hilo kwa hali yoyote iwayo.

Na kama hivyo, kwa hakika vyenye uhai vyote na viumbe kuanzia kwenye atomu hadi sayari za mfumo wa jua, vimo kwenye uwiano wa vipimo timamu haviendi kombo japo chanda kimoja, na vyote vinatawaliwa na kipimo kilichopangiliwa vyema, katika yanayojulisha kwa kukata shauri kabisa juu ya ujuzi unaozungukia kila kitu na inashuhudia ushahidi wa kweli. Kwa maana kwamba kila dalili katika dalili za ujuzi ni dalili pia juu ya uwepo wa mjuzi mwenye habari ya kila kitu. Kwani ni muhali kuwepo ufundi bila ya mwenye kusifika nao. Kwa hiyo hoja zote za ujuzi wa azali ni hoja zenye nguvu pia juu ya wajibu wa kuwepo kwake (s.w).

Dalili ya tatu: nayo [Hekima za jumla za makusudi]

Yaani hekima zilizokusudiwa kwa ujuzi, zinawekewa kwa kila chenye kutengezwa, na kwa kila kundi katika ulimwengu ambalo hupitiwa na uumbaji wa kudumu, utendaji endelevu na kubadilika kwa kudumu na uhuishaji endelevu na kukabidhi majukumu na kupumzisha vyenye kudumu, hayo ambayo yana faida na majukumu kwa kiasi ambacho haiwezekeni kuyaegemeza kwenye sadfa kamwe. Basi tunashuhudia kwamba ambaye hana ujuzi wenye kuzungukia kila kitu hawezi kuwa mmiliki wa chochote kati ya hivyo na kwa namna yeyote iwayo kwa upande wa kupatisha.

Mathalani:

Ulimi ni zana moja katika zana mia moja katika zana za mwanadamu ambaye ni kati ya kiasi kisicho na mpaka cha walio hai, ulimi huu ni kipande cha nyama na si vinginevyo. Lakini unakuwa ni nyenzo ya mamia ya hekima, matokeo, matunda na faida kwa kutimiza kwake majukumu mawili:

Kutimiza kwake jukumu la kuonja vyakula: Ni kufikishia mwili na tumbo la chakula habari za ladha zote za aina kwa aina katika aina za vyakula, na kuwa ni mkaguzi mahiri katika majiko ya rehema ya kiungu.

Na kutimiza kwake jukumu la maneno: Ni kuwa mkalimani mwaminifu na mwenye kujikita katika kueleza mambo yanayopita kwenye moyo na yanayopatikana katika roho na ubongo. Yote hayo yanajulisha kwa namna ya ukomo wa kuangaza, na kukata shauri juu ya kuwepo ujuzi wenye kuzungukia kila kitu hakuna shaka katika hilo.

Ikiwa basi ulimi mmoja tu unajulisha kwa kiasi hiki hekima na matunda yaliyomo, hakika ndimi nyingi bila ukomo na wenye uhai wasiohesabika na vilivyotengenezwa visivyo na ukomo, bila shaka vinajulisha kwa uwazi kuliko jua na vinashuhudia ushahidi bayana kuliko mchana juu ya uwepo wa ujuzi usio na ukomo. Na vyote vina tangaza kwamba hakuna kitu nje ya duara la ujuzi wa ghaibu wala nje ya utashi wake (s.w).

Dalili ya nne: Ni: [Uangalizi maalum wenye kuenea]

Yaani aina za uangalizi na huruma na utunzaji maalum wenye kuwiana kwa kila aina bali kwa kila mmoja na wenye kuenea kwa wote waliopo katika ulimwengu wa walio hai na wenye utambuzi zinajulisha kwa uwazi juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu. Zinashuhudia ushahidi usio kuwa na mpaka juu ya kupasa kuwepo kwa mjuzi wa kila kitu mwenye uangalizi anawajua hao ambao wamepata uangalizi huo na anajua mahitaji yao.

Tanbihi:

Ufafanuzi wa maneno ya Kiarabu ambayo ni krimu ya muhtasari wa muhtasari wa Risale-i Nur unatona kutoka katika Qur’an tukufu, nayo ni ishara ya yale ambayo yaliyochukua Risale-i Nur kutokana na hakika zinazotokana na aya za Qur’an tukufu hasa dalili na hoja ambazo zinahusu (Ujuzi), (Utashi) na (Uweza) kwa namna ambayo inafasiri kwa kutilia umuhimu kikamilifu yale ambayo maneno haya ya Kiarabu yana ashiria katika dalili za kielimu. Kwa maana kwamba kila moja kati ya hayo ni ufafanuzi wa nukta na ishara ya Qur’an tukufu, na kama siyo hivyo basi sio tafsiri, ufafanuzi wake na wala tarjumi (katika lugha nyingine) ya maneno hayo ya Kiarabu.

Turejee katika maudhui yetu:

Naam, hakika tunashuhudia kwa macho yetu kwamba mjuzi wa kila kitu mwenye kurehemu, anatutambua na anajua hali yetu na hali ya wenye roho wote, kwa hiyo wote hao anawaenezea rehema yake na himaya yake na anawachukua kwenye hifadhi ya rehema yake kwa utambuzi na busara, na anatimiza mahitaji ya kila mmoja kati yao hivyo huwapa msaada kwa uangalizi na upole wake.

Tunatoa mfano mmoja kati ya mifano chungu tele: Uangalizi maalum na wa jumla na unaopatikana kwa upande wa riziki ya mwanadamu na anayoyahitaji katika madawa na madini yanabainisha waziwazi ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na kushuhudia juu ya mwingi wa rehema mwenye kurehemu kwa idadi ya riziki na madawa na madini.

Naam, kumpa maisha mwanadamu hasa wasiojiweza na watoto wanyonge, na hasa kufikisha riziki katika viungo vya mwili vyenye kuihitajia kutokea kwenye jiko la tumbo la chakula, hata katika vyumba vyake vidogo, kila moja kwa namna inayonasibiana nayo, na vivyo hivyo kufanya milima mikubwa kuwa ni hazina za madini na bohari ya madawa anayo yahitajia mwanadamu na matendo mengine ya hekima kama haya, haiwezekani kutokea isipokuwa kwa ujuzi unaozungukia kila kitu. Basi sadfa isiyo na malengo na nguvu pofu na Asili kiziwi na sababu mfu zisizokuwa na utambuzi na vipengele rahisi vyenye kutawalia, haviwezi kuingilia kabisa katika mambo kama haya ya upaji wa maisha, uongozi, himaya na uendeshaji wenye sifa ya ujuzi, uoni, hekima, rehema na uangalizi. Hizo sababu za kidhahiri sio lolote isipokuwa ni pazia za utukufu wa uweza wa kiungu kwa amri ya mjuzi wa kila kitu na kwa idhini yake na ndani ya duara la ujuzi wake na hekima yake.

Dalili ya tano na ya sita

Nazo ni: [Hukumu zilizopangika na kadari zenye kuzaa matunda]

Hakika maumbo ya kila kitu na hasa maumbo ya mimea, miti, wanyama, binadamu na kadiri zake yamepambanuliwa vema kabisa kwa kanuni za aina mbili za ujuzi wa azali nazo ni Qadhaa na Kadari, yameshonwa kwa namna inayowiana kimo cha kila mmoja kati yao uwiano kamili, na kueneza kwa kila mmoja kati yao likapewa umbo lililopangika katika upeo wa hekima. Kila kitu kati ya vitu hivi na vyote kwa pamoja vinajulisha juu ya ujuzi usio na ukomo na kwa idadi yake inashuhudia juu ya fundi mjuzi wa kila kitu.

Kutoka katika mifano yake mingi isiyo na mipaka tuchukue mfano mmoja: Mti mmoja, au mtu mmoja, tunashuhudia kwamba huu mti wenye kuzaa matunda na huyu mwanadamu aliyebeba zana nyingi mipaka ya nje na ndani yake imechorwa kwa bikari ya ghaibu na kalamu ya ujuzi makini, kwani kila kiungo chake kimepewa sura inayolingana nayo ili kiweze kuzaa matunda yake na kutoa matokeo yake na kutimiza majukumu ya kuumbwa kwake. Na kwa kuwa haya hayatokei isipokuwa kwa ujuzi usio na ukomo, inahitajia ujuzi usio na mipaka wa fundi mtia sura na mjuzi wa kila kitu mkadiriaji anajua uhusiano kati ya vitu vyote na anahesabu mafungamano ya kila kitu kwa vitu vyote na anajua mifano yote ya mti huu na huyu mtu, na aina zake zote na anakadiria kwa bikari na kalamu ya hukumu yake na kadari ya ujuzi wake wa azali makadirio ya ndani yake na nje yake na anaweka sura yake kwa makadirio ya hekima, na kwa uoni na ujuzi. Yaani kwa yakini dalili na shahidi juu ya kupasa uwepo wake (s.w) na juu ya ujuzi wake wa kila kitu ni kwa idadi ya mimea na wanyama.

Dalili ya saba na nane:

[Na nyakati zilizopangwa maalum na riziki zilizowekewa kanuni]

Hakika ya nyakati maalum na riziki ambazo kwa nje zinaonekana kana kwamba zisizojulikana na zisizokuwa maalum, isipokuwa katika uhalisia ni kuwa hayo ni mambo yaliyokadiriwa chini ya pazia la kutojulikana katika daftari la Qadhaa na Kadari la azali, na katika ukurasa wa makadirio ya kiuhai. Muda wa umri uliyopangwa lazima kutimia kwa kila mwenye uhai umekadiriwa na kuwekwa maalum hautangulii saa wala kuchelewa, na riziki ya kila chenye roho imeainishwa na kuhusishwa, na vyote hivyo vimeandikwa katika ubao wa Qadhaa na Kadari,

Zipo kiasi kisichokua na mpaka cha dalili juu ya hukumu hii, miongoni mwa hizo:

Hakika kufa kwa mti mkubwa na kurithisha mbegu zake ambazo ni sawa na aina ya roho yake, ili zitimize majukumu iliyokuwa unayatekeleza, hakutimii isipokuwa kwa kanuni ya mwenye hekima ya mjuzi wa kila kitu Mwenye kuhifadhi kila kitu. Hakika yanayobubujika kutoka katika chuchu ambayo ni maziwa safi na riziki kwa mtoto, na kutoka kwake kati ya kinyesi na damu bila kuchanganyika, yakiwa safi twahara, na kutiririka kwake kwenda kwenye kinywa chake, inajibu jibu lenye nguvu dhidi ya uwezekano wa kutokea hayo kwa kusadifiana, na inabainisha kutokea kwake wazi kabisa kuwa ni kupitia katika kanuni yenye huruma iliyowekwa kutoka kwa Mtoaji riziki mjuzi wa kila kitu mwenye kurehemu. Na pimia baki ya wenye uhai na roho kwa vielezo hivi viwili ambavyo ni sehemu ndogo.

Hakika ya mambo ni kuwa umri ni maalum na umekadiriwa, na riziki hivyohivyo, vimewekwa katika daftari la vikadiriwa na kila moja kati yao imejaaliwa kuwa ni maalum. Lakini viwili hivyo vinaonekana – katika hali ya nje – vimeambatana katika nyuzi za kutojulikana, visivyoonekana kudhihiri kana kwamba sio maalum hasa, na kana kwamba zimefungwa kwenye kusadifiana, yote hayo ni kwa ajili ya hekima makini na upeo wa umuhimu!

Ingekuwa muda wa kifo ni maalum kama kuzama kwa jua mwanadamu angekuwa anatumia nusu aya umri wake katika tabaka la ghafla na kuupoteza, hali ya kuwa mbali na jitihada ya akhera kisha anaingia katika nusu nyingine ndani ya hofu za kutisha, atakuwa kama mtu ambaye kila siku anapiga hatua moja kuelekea katika milingoti ya mahali pa kunyongea, na msiba ambao ungekuwa umeingia katika siku ya kifo unaongezeka kwa mamia! Na kwa ajili ya siri hii makini – misiba ambayo humrejea mwanadamu kwa kawaida – imebakishwa chini ya pazia la ghaibu. Bali hata siku ya mwisho wa dunia yenyewe ambayo ni kiama ameificha (s.w) – kwa rehema na huruma zake – chini ya pazia la ghaibu kwa sababu hiyohiyo.

Ama riziki, kwa sababu ni hazina kubwa inaleta neema baada ya neema ya uhai, na chimbuko tajiri mno huelekewa kwa shukrani na sifa njema, na hazina jumuishi mno ya uja na dua na mahali na njia za matarajio, imeoneshwa katika sura yake ya dhahiri kana kwamba haijulikani na imefungwa na kusadifiana, na hii ni kwa sababu mlango wa kutafuta riziki usifungwe kwa dua kutoka kwa mwenye kuruzuku Mkarimu kila wakati, na ili mlango wa kukimbilia na maombi yenye kutumiwa shufaa kwa sifa njema na shukurani kwa Allah (s.w) usifungwe, kwani kama riziki ingekuwa ni maalum (inajulikana) kama kuchomoza kwa jua na kuzama kwake, hakika yake ingekuwa imegeuka kabisa, na ingekuwa milango ya matarajio na madirisha ya unyenyekevu na ngazi za dua ambazo zote zimejazwa shukurani nzuri na ridhaa njema ingefungwa hadi mwisho wake, bali ingekuwa milango ya uja wenye khushui, nyenyekevu imefungwa moja kwa moja.

Dalili ya tisa na kumi:

Nazo ni: [Ufundi fani kwa fani na umuhimu uliowekewa mapambo]

Yaani kila kilichotengenezwa katika viumbe vyote vizuri vilivyotawanywa ardhini kote, na hasa katika majira ya machipuo kinabainisha midhihirisho ya uzuri wa kudumu milele. Kwa mfano chukua: Maua na matunda na ndege wadogo na vijidudu na hasa wenye rangi ya dhahabu ya kung’ara, katika kuumbwa kwao na katika sura zao na katika zana zao kuna umahiri na muujiza na ufundi makini wa ajabu na ukamilifu wenye muujiza wa fundi wake mtukufu, katika maumbo anuwai na namna tofauti na mashine makini kuna kinachojulisha waziwazi juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na uwezo wa kielimu wenye stadi na fani mbalimbali – ikifaa maelezo hayo –, na kinashuhudia kwa ukweli kwamba kuingilia sadifu na sababu zenye kusongana zisizokuwa na utambuzi, ni muhali katika muhali.

Na kwamba maelezo: (Na umuhimu uliwekewa mapambo) yanamaanisha: Kwamba katika hivyo vilivyotengenezwa vizuri kuna upambaji maridadi mtamu na mapambo ya fahari yenye kupendeza sana na urembo wa ufundi unaovutia anafanya uyafanyayo kwa ujuzi usio na ukomo, na anajua hali nzuri zaidi na hali maridadi zaidi ya kila kitu, na anataka kuonesha uzuri wa ukamilifu wa upendezeshaji na ukamilifu wa uzuri wake kwa wenye utambuzi kwa kiasi anaumba ua dogo sana la kisehemu na mdudu mdogo sana na kumtia sura kwa kumtilia umuhimu wa kiwango kikubwa na kwa umahiri wa hali ya juu na kwa ufundi wa ajabu.

Huku kupamba na kurembesha ambako kuna sifa ya kutilia umuhimu na utunzaji, kunajulisha wazi juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na kunashuhudia juu ya kupasa uwepo wa fundi mjuzi mwenye uzuri kwa idadi ya viumbe wazuri.

Dalili ya kumi na moja yenye kukusanya dalili tano na hoja tano:

[Na upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingana vipimo, kupambanuka, bila mipaka na kwa wepesi usio na mipaka.

Na uumbaji vitu kwa wingi usio na mipaka pamoja na uzuri usio na mipaka.

Na katika kasi isio na mipaka pamoja na kulingana vipimo bila mipaka.

Na katika upana usio na mipaka pamoja na ukamilifu wa ufundi mzuri.

Na katika umbali usio na mipaka pamoja na kuafikiana kusiko na mipaka.

Na katika mchanganyiko usio na mipaka pamoja na kupambanuka kusiko na mipaka]

Dalili hii ni tamko lingine la dalili iliyoelezwa mwishoni mwa kifungu cha Kiarabu kilichopita na ni kizuri zaidi kuliko hicho, nao ni ufafanuzi wa dalili tano na sita ambazo ni pana, tunaiashiria kwa upeo wa kufupisha kwa sababu ya maradhi makali.

Kwanza:

Tunashuhudia ardhini kote kwamba ufundi wa mashine za ajabu, kwa wepesi wote na urahisi kwa mkupuo, kunatokana na ujuzi kamili na umahiri uliotimia, bali baadhi yake kutengenezwa kwenye dakika moja, kwa namna iliyopangika yenye kupimwa, pamoja na tofauti na viumbe wengine mfano wake, kunajulisha kikamilifu juu ya ujuzi usio na kikomo, na juu ya ukamilifu wa ujuzi huo, kwa kiwango cha wepesi na urahisi unaotokana na umahiri wa kiujuzi katika utengenezaji.

Pili:

Hakika kuumba viumbe katika wingi wa kupindukia usio na ukomo na idadi kubwa isiyokuwa na mipaka kwa ufundi na bila kukosea wala kubabaika kunajulisha juu ya ujuzi usio na mipaka ndani ya uweza usio na ukomo, na unashuhudia shahidi zisizo na mpaka juu ya mjuzi asiye na mipaka na mweza asiye na mipaka.

Tatu:

Hakika kuumba viumbe ambavyo viko katika upeo wa mizani na kipimo katika ukomo wa kasi, kunajulisha juu ya ujuzi usio na mipaka, kunashuhudia kwa idadi ya viumbe hivyo juu ya mjuzi wa kila kitu bila mipaka na mweza wa kila kitu bila mipaka.

Nne:

Hakika kuumba vyenye uhai visivyodhibitika na hesabu katika ukunjufu usio na mipaka unaotosha ardhi yote, katika ufundi ulio timamu mno katika kutengeneza na katika kupamba, na ukamilifu wa uzuri wa kutengeneza, kunajulisha juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu, usio potea wala kusahau na unaona vitu vyote mkupuo mmoja wala hakimzuii kitu chochote na chochote, kila kilichopo kinashuhudia na vyote kwa pamoja ya kwamba ni kazi iliyotengenezwa na mjuzi wa kila kitu na mweza juu ya kila kitu.

Tano:

Hakika kuumba kila kimoja ya aina ambazo zinatenganishwa kati yake na masafa makubwa, mojawapo iko mashariki na nyingine iko magharibi na nyingine iko kaskazini na nyingine iko kusini, katika wakati mmoja, na kwa namna moja ikiwa inashabihiana na kufanana pamoja na kupambanuka kila moja kati yao na nyingine katika mwonekano, haiwezekani kuwa isipokuwa kwa uweza wa mweza wa kila kitu mwenye uweza usio na mipaka anatawalia ulimwengu wote kwa uweza wake na ujuzi wake anavizungukia vilivyomo pamoja na hali zake. Kwa hiyo viumbe hivi vinashuhudia ushahidi usio na mipaka juu ya ujuzi yenye kuzungukia kila kitu na juu ya mjuzi wa mambo yote ya ghaibu.

Sita:

Hakika kuumba mashine mengi yenye uhai katika mpambanuko maalum timamu na alama zenye kutenganisha na nyingine kama hizo, pamoja na kuwa katika msongamano mkali na katika mahali mwa giza – kama kokwa ambayo ipo chini ya udongo – na bila kuchanganyika wala kukosea wala kubabaika pamoja na kuwa imo katika mchanganyiko usio na mipaka, na kuumba zana za kila moja kati yao bila kasoro uumbaji wa muujiza, unajulisha kwa uwazi kama jua juu ya ujuzi wa azali na unashuhudia kwa bayana kama mchana juu ya Rububiyya na uumbaji wa mweza asiye na mipaka na mjuzi wa kila kitu asiye na mipaka.

Tunalifupisha somo hili refu sana tukielekeza maelezo yake kwenye Risale-i Nur. Na sasa tunaanza suala la (Utashi) ambalo limo katika muhtasari wa muhtasari.

[Allah ni mkubwa kuliko kila kitu kwa uweza na ujuzi, kwani yeye ni mwenye utashi wa kila kitu, anachotaka Allah huwa na asichokitaka hakiwi, kwa sababu mpangilio wa kupatisha vilivyotengenezwa kwa dhati, sifa, haiba na wasifu ni kati ya yamkini zisizo kuwa na mipaka na njia zisizo na tija na uwezekano wenye kubabaisha na mifano yenye kushabihiana, na ni katikati ya mifereji ya vipengele vyenye kusongana, kwa mpangilio huu makini nyororo, na kupimwa kwake kwa mizani hii nyeti sana, na kuipambanua kwa mifano hii yenye kushabihiana na ainisho zilizopambwa na kupangika, na kuumbwa viumbe vyenye kunadhimika hai kutoka katika rahisi na uhai mfu, kama mwanadamu na zana zake zote kuanzia kwenye manii na ndege na viungo vyake vyote kutokana na yai na mti na viungo vyake kutokana na kokwa na punje inajulisha kuwa kila kitu ni kwa utashi wake (s.w), uchaguzi wake, makusudio yake na majaaliwa yake, kama ilivyo kuafikiana kwa vitu katika misingi ya viungo ya kiaina na jinsia inajulisha kuwa mtengenezaji wa vitu hivyo ni mmoja wa pekee, vilevile kupambanuka kwake kwa aina zilizopambika na maumbo yenye kupambanuka inajulisha kuwa fundi huyo mmoja wa pekee ni mtendaji mwenye hiari anafanya anachokitaka na anahukumu anachokitaka].

Kifungu hiki ni dalili moja ndefu na ya jumla katika dalili za (Utashi wa kiungu) inajumuisha hoja za jumla nyingi sana, tunabainisha pamoja na kutafsiri yaliomo kwa muhtasari, dalili inayothibitisha utashi wa kiungu, hiari na kutaka kwake kwa namna ya kukinaisha, ukiachilia mbali kwamba dalili zote za (Ujuzi wa kiungu) zilizotajwa hapo kabla ni dalili za Utashi wa kiungu vilevile, kwa kuwa midhihirisho ya (Ujuzi na utashi wa kiungu) na athari zake zinashuhudia kwa pamoja katika kila kilichotengenezwa.

Muhtasari wa yaliyomo katika kifungu hiki cha Kiarabu ni: Kwamba kila kitu hupatikana kwa Utashi wake (s.w), basi akitakacho hua na asichokitaka hakiwi, hufanya atakacho, na hakiwi chochote asichokitaka.

Na hoja moja katika hoja zake ni: Hakika tunashuhudia kila kilichotengenezwa kati ya hivi vilivyotengenezwa kimepambanuka kwa dhati maalum na sifa mahsusi na haiba yake maalum, na sura yenye alama zenye kutenganisha na kupambanua. Na wakati ambapo inayumkinika hali zote hizi ndani ya yamkini na ya yawezekanayo yenye kubabaisha bila mipaka, na kupita katika njia nyingi zisizo na tija wakati wa maingiliano ya mifereji ya vipengele na ndani ya mifano yenye kushabihiana yenye kusababisha kusahau na kuchanganya, kwani kuumba kwake – sambamba na hali hizi zenye kugongana na kuchanganyika – ndani ya mpangilio makini uliopimwa na kuratibiwa, na kila moja kati ya viungo vyake na zana zake kuchukua mizani nyeti yenye hisia sana, na kila moja kati yake kuituliza mahali pake panapofaa, kuikabidhi nyadhifa, na kutunuku uso wake alama za haiba maalum nzuri zenye kupambwa, na kuumba viungo vyake vyenye kuhitilafiana kuwa mbalimbali kutokana na maada rahisi mfu, ikiwa na uhai imewekwa vizuri kiufundi, kama kumuumba mwanadamu ambaye anabeba mamia ya zana anuwai katika sura ya muujiza kutokana na tone la maji. Na kumuumba ndege kwa zana na viungo tofauti anuwai kutokana na yai jepesi, na kuanzisha mti pamoja na matawi yake yenye kusongana na kupachana na sehemu tofauti, kutokana na mbegu ndogo sana yenye kuundwa kutokana na vitu rahisi mfu ambazo ni kaboni na azuweti na kizalishi cha tindi kali na kizalishi cha maji (Oksijeni na Haidrojeni), na kuwekea umbo lililopangika na lenye tija, inathibitisha bila shaka na uwazi na ukinaishi usio na shaka bali kwa kiwango cha wajibu na dharura na ulazima kwamba kila kilichotengenezwa kati ya hivi vilivyotengenezwa hupewa hali hiyo maalum kamili kwa atomu zake zote na zana zake na sura yake na haiba yake, kwa utashi wa mweza mwenye uwezo usio na mipaka, kwa kutaka kwake, hiari yake na makusudio yake (s.w). Na kwamba hicho kilichotengenezwa kinatii maamuzi na utashi wenye kuenea kila kitu.

Ni hivi hakika ya kujulisha kwa hiki kilichotengenezwa kimoja kwa hali isiyo na shaka ndani yake juu ya (Utashi wa kiungu) kunabainisha kwamba vyote vilivyotengenezwa vinashuhudia ushahidi wa ukweli fasaha usio na ukomo na kwa idadi ya kila kimoja kwa ukinaishi dhahiri kama jua na mchana juu ya (Utashi wa kiungu) wenye kuenea katika kila kitu. Na kwamba hizo ni hoja za kukinaisha hazina mpaka juu ya kupasa kuwepo mweza mwenye utashi.

Kisha dalili zote za (Ujuzi) zilizoelezwa huko nyuma ndiyo dalili za (Utashi wa kungu) vilevile, kwani zote hizo mbili zinafanya pamoja na (Uweza wa kungu) haiachani moja wapo na nyingine. Kama ilivyo kwamba kuafikiana kwa viungo vya kiaina na kijinsia kwa watu wa kila jinsia na kila aina kunajulisha kwamba mtengenezaji wake ni mmoja pekee, vilevile tofauti katika alama za nyuso zao tofauti yenye hekima, kunajulisha kwa kukinaisha kabisa kwamba huyo fundi mmoja wa pekee, ni mtendaji mwenye uchaguzi, anaumba kila kitu kwa kutaka, kuchagua, kupenda na makusudio.

Na kama hivi ufafanuzi wa tafsiri ya muhtasari imekwisha ya kifungu cha Kiarabu kilichoelezwa, kinachojulisha kwa ujumla wa kipekee juu ya (Utashi wa kiungu).

Nilikuwa nimeazimia kuandika nukta muhimu sana zinazohusu (Utashi wa kiungu) kama ilivyo kwenye suala la (Ujuzi wa kungu), isipokuwa maradhi yanayotokana na kutiliwa sumu yametia uchovu katika ubongo wangu, hivyo ninayaahirisha hadi wakati mwingine kwa kupenda kwake Allah (s.w).

Ama fungu ambalo linahusu Uweza wa kiungu ni:

[Hakika Allah (s.w) ni mkubwa kuliko kila kitu kwa uweza na ujuzi kwani yeye ni mweza juu ya kila kitu kwa uweza usio na mipaka wenye kuzungukia kila kitu wa dharura wenye kuanzisha wenye kulazimu wa kidhati takatifu, basi ni muhali kuingilia dhidi yake, na hakuna ngazi katika huo, kwa mnasaba wake vinakuwa sawa atomu, nyota, sehemu, kitu kizima, cha sehemu, cha kitu kizima, kokwa, mti, ulimwengu na mwanadamu, kwa siri ya kushuhudia upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingana vipimo, kupambanuka na kutengeneza uzuri kusiko na mipaka. Pamoja na wepesi katika wingi, kasi na mchanganyiko usio na mpaka. Na kwa siri ya hali ya nuru, uangavu, kukabiliana, kuendana vipimo, kupangika na utekelezaji. Na kwa siri ya msaada wa Umoja, wepesi wa Umoja na kudhihiri kwa upekee. Na kwa siri ya kupasa, kutakasa na kutofautiana kwa hakika. Na kwa siri ya kutofungika,  kutokushika upande maalum na kutokugawanyika katika sehemu mbalimbali. Na kwa siri ya kupinduka kwa vikwazo na vizuizi kwenda katika nafasi ya nyenzo na virahisishi. Na kwa siri ya kuwa atomu, kijisehemu, kokwa na mwanadamu sio kitu kichache kwa kutengenezwa na wepesi kuliko nyota, kitu kizima, cha jumla, mti na ulimwengu, basi muumba wake ndiyo muumba wa hii kwa mawazo ya kiushahidi. Na kwa siri kwamba kilichozungukwa na vijisehemu ni kama mifano iliyoandikwa iliyowekwa katika umbo dogo au kama nukta zilizokamuliwa sana. Basi hapana budi mzunguko na vitu vizima kuwa katika udhibiti wa muumba wa vyenye kuzungukwa na vijisehemu ili kuingiza mifano yake humo kwa vipimo vya ujuzi wake au kuvikamua kutokea humo kwa kanuni za hekima yake. Na kwa siri ya kama ilivyo Qur’an ya utukufu iliyoandikwa kwenye atomu inayoitwa kwa jina la johari pekee kwa atomu za Athiir sio yenye ujazo wa uchache na ajabu wa ufundi kuliko Qur’an ya U-adhama iliyoandikwa kwenye ukurasa wa mbingu kwa wino wa nyota na majua, vilevile ua sio la uchache kwa ujazo na ufundi kuliko nyota ya zuhura yenye kumetameta wala mdudu chungu kuliko tembo, wala kimelea kulinganisha na genosera, wala nyuki kuliko mtende, kwa mnasaba wa uweza wa muumba wa viumbe. Kama ilivyo kwamba upeo wa ukamilifu wa wepesi na urahisi katika kupatisha vitu kumewaingiza watu wa upotevu katika mgogoro unaolazimiana wa muhali zisizokuwa na mpaka zinazomiminwa na dhana, vivyo hivyo imewathibitishia watu wa hidaya kusawazika kwa nyota pamoja na atomu mbele ya uweza wa muumba wa viumbe (s.w) lailaha illa Huwa Allahu Akbar].

Kabla ya kuingia katika kubainisha yaliyomo katika kifungu hiki kitukufu ambacho kinahusu (Uweza wa kiungu) na ambayo ni sawa na tafsiri na madhumuni yake, tunabainisha hakika iliyopitishwa moyoni nayo:

Hakika kuwepo kwa uweza wa kiungu ni kwenye kukinaisha zaidi kuliko kuwepo kwa ulimwengu, bali viumbe wote na kila kiumbe kwa dhati yake, ni maneno yalio kwenye mwili ya uweza huo, yanaibainisha na kuidhihirisha kwa dhati ya yakini, nazo ni shahidi kwa idadi yake juu ya mwenye kusifika wake mweza asiye na mipaka, kwa hiyo hapana haja ya kuthibitisha uweza huo kwa hoja na dalili. Bali inalazimu kuthibitisha hakika tukufu inahusu uweza na mbayo ni msingi muhimu katika imani na jiwe la msingi madhubuti la ufufuo na kukusanywa na eneo la lazima la masuala mengi ya kiimani na hakika tukufu za Qur’an na madai yanayotolewa na Aya tukufu:

مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Qur’an, 31:28.

na ambayo yamefanya akili kuhemewa kuhusiana nayo na kubakia katika tahayuri na kutojiweza, bali baadhi yake zimepotea.

Basi msingi huo na hilo jiwe la nguzo ya pembeni na nyanja hiyo na madai hayo na hakika hiyo ndiyo maana ya aya tukufu iliyotajwa.

Yaani enyi majini na wanadamu hakika kuwaumbeni na kuwafufua siku ya kiama ni jambo jepesi kwa uweza wangu sawa na wepesi wa kupatisha nafsi moja, yeye ndiye ambaye anaumba majira ya machipuo mfano wa kuumba kwake ua moja kwa wepesi na urahisi, hakuna tofauti kulingana na uweza huo kati ya sehemu, kitu kizima, kidogo, kikubwa,  kichache na kingi, uweza huo unaendesha sayari kwa wepesi ule wa kuendesha atomu.

Basi kifungu hicho cha Kiarabu kilichoelezwa kinabainisha suala hili tukufu kwa hoja yenye nguvu ya kukinaisha katika ngazi tisa.

Hakika ya kifungu kifuatacho kinaashiria katika msingi wa ngazi na kufupisha kifungu cha Kiarabu kwa muhtasari sana:

[Kwa kuwa yeye ni Mweza juu ya kila kitu kwa uweza usio na mipaka wenye kuzungukia kila kitu wa dharura wenye kuanzisha wenye kulazimu kidhati, kwa dhati takatifu. Basi ni muhali kuingilia dhidi yake, hakuna ngazi katika uweza huo, hivyo vinakuwa sawa kwa mujibu wake atomu, nyota, sehemu, kitu kizima, cha sehemu, cha kitu kizima, kokwa, mti, ulimwengu na mwanadamu].

Yaani ni mweza juu ya kila kitu kwa uweza wenye kuzungukia kila kitu, na wenye kulazimu kwa ulazima wa kidhati na ni wa wajibu wa kidharura wenye kuanzisha – kama katika elimu ya mantiki – kwa ambaye ni wajibu kuwepo, ni muhali kuachana kwake na haiyumkiniki hivyo kabisa.

Kwa kuwa mfano wa uweza huu ni wenye kuambatana kama hivi na dhati takatifu, hapana shaka kutojiweza ambako ni dhidi ya uweza hakuingii kwa upande wowote uwao, hakiwi kipingamizi cha dhati tukufu. Kwani kuwepo kwa ngazi katika kitu, ni kwa kuingilia dhidi yake ndani yake – kwa mfano: Ngazi za joto na viwango vyake ni kwa kuingia ubaridi, na viwango vya urembo ni kwa kuingilia ubaya – basi ni muhali kukaribia kwa kutojiweza ambako ni dhidi ya uweza, katika uweza huu usio na mipaka, na kwa kuwa hakuna ngazi ndani yake, nyota na atomu mbele yake huwa sawasawa, na hakuna tofauti kati ya sehemu moja na sampuli yake yote na mwanadamu na ulimwengu kwa mnasaba na uweza huo. Na kuhuisha kokwa moja na mti uliostawi na nafsi moja na wote wenye roho katika ufufuo ni sawa kwa upande wa uweza huo na ni rahisi kwake. Basi kwake hakuna tofauti kati ya mkubwa na mdogo na chache na nyingi. Chenye kushuhudia kwa ukweli wa kukinaisha juu ya hakika hii ni kile tunachokishuhudia katika uumbaji wa vitu kutokana na ukamilifu wa ufundi mpangilio na vipimo na kupambanuka na wingi katika kasi kubwa bila ukomo pamoja na wepesi usio na ukomo na urahisi uliotimia.

Hakika hii iliyoelezwa ni madhumuni ya ngazi ya kwanza ambayo:

[Na kwa siri ya kushuhudia upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingamana vipimo, kupambanuka na kutengenezwa vema kusiko na mipaka, pamoja na wepesi usio na mipaka katika wingi na kasi na mchanganyiko].

Ngazi ya pili: Nayo ni: [Na kwa siri ya Nuru, uangavu, kukabiliana, kuendana vipimo, kupangika na utekelezaji].

Ufafanuzi wa ngazi hii na maelezo yake tunaelekeza mwishoni mwa (Neno la kumi) na katika (Neno la ishirini na tisa) na kwenye (Andiko la Ishirini) na hapa tunaashiria kwa ufupi:

Naam, kama kuingia kwa mwanga wa jua na sura yake – kwa upande wa kinuru – kwa uweza wa kiungu katika uso wa bahari na vipovu vyake vyote ni jambo jepesi, kama kuingia kwake vyote sawasawa katika kipande cha chupa. Na vivyo hivyo uweza wa kinuru wa ambaye yeye ni nuru ya nuru, kuumba kwake mbingu na nyota na kuviendesha ni rahisi juu yake kama kuumba nzi na atomu na kuviendesha, hakuna kigumu kwake.

Na kama inavyopatikana – kwa sifa ya uangavu – sura ya jua ya kimfano katika kioo kidogo na katika kiini cha jicho kwa uweza wa kiungu, basi kwa wepesi huohuo hutoa mwanga huo na sura hiyo kwa amri ya kiungu kwenda kwenye vitu vyote vyenye kung’ara na kwenye matone yote na atomu zote angavu na katika uso wa bahari. Vivyo hivyo hakika ya kudhihiri kwa uweza wa kiungu kusiko na mipaka na kuathiri kwake katika kupatisha nafsi moja nayo ni kwa wepesi huohuo katika kuwaumba wanyama wote kwa kuwa upande wa Kiufalme na hakika ya vyenye kutengenezwa na angavu na ng’avu. Hakuna tofauti kwa mnasaba wa uweza huo kati ya kichache na kingi kidogo na kikubwa.

Kama ikiwa zitawekwa jauzi (punje kama karanga) mbili katika vitanga viwili vya mizani nyeti iliyotengenezwa vizuri sana inayopima milima, kisha ikawekwa kokwa ndogo kumojawapo kati ya vitanga viwili mizani hiyo itainyanyua kwa wepesi hadi kilele cha mlima na kushusha kingine hadi chini ya bonde, na ikiwa itawekwa milima miwili iliyo sawasawa badala ya jauzi mbili, hakika moja ya milima miwili utanyanyuka hadi mbinguni na mwingine utashuka hadi kwenye vina vya mabonde kwa urahisi uleule kama ingewekwa kokwa ndogo katika kitanga kimojawapo, vilevile (uwezekano ni wa sawasawa pande mbili) kwa mujibu wa maelezo ya elimu ya al-Kalaam, yaani uwepo wa vitu vya yamkini – yaani visivyokuwa vya lazima wala kuzuilika – na kukosekana kwake ni sawasawa, hakuna tofauti kati ya kuwepo kwake na kukosekana kwake kama haikuwepo sababu.

Katika yamkini hii na kuwa sawasawa kati ya uwepo na kukosekana, huwa sawa chache na nyingi, ndogo na kubwa, na kama hivyo viumbe ni yamkini, na kwa kuwa uwepo wake na kukosekana kwake ni sawasawa ndani ya duara la kuyumkinika. Hakika uweza wa aliye wajibu kuwepo wa azali bila mipaka kama unavyotunuka uwepo kwa yamkini moja kwa wepesi sana, hukivika kila kitu uwepo unaoafikiana nao ukinyongesha mizania kati ya uwepo na kukosekana. Na kuiondoshea vazi la uwepo wa nje ikiwa jukumu lake limekwisha, na kuipeleka katika kukosekana kwa sura na dhahiri, bali katika uwepo wa kimaanawy kwenye uwanja wa ujuzi.

Kwa maana ikiwa vitategemezwa vitu kwa mweza wa kila kitu na kukabidhi mambo yake kwake (s.w) hakika kuhuisha majira ya machipuo inakuwa rahisi kama kuhuisha ua moja, na kuhuisha watu wote kwenye ufufuo kunakuwa rahisi kama kuhuisha nafsi moja. Wakati ambao ikiwa itategemezwa uumbaji wa vitu kwenye sababu inakuwa kuumba ua moja ni ngumu kama ugumu wa kuumba majira kamili ya machipuo, na kuumba nzi mmoja kama kuumba walio hai wote.

Na vivyo hivyo hakika ya jahazi moja kubwa na ndege kubwa hutembea kwa kiasi tu cha kugusisha ufunguo kwenye vyombo hivyo, kwa siri ya mpangilio, kwa wepesi wa kufungua saa na kufanyisha kazi. Vivyo hivyo hakika kukipa kila kitu kiwe kizima au sehemu, kidogo au kikubwa, kichache au kingi, wasifu wa kimaanawy, na kiwango maalum na mipaka maalum, kwa taratibu za ujuzi wa kiazali, na kwa kanuni za hekima ya milele, na kwa misingi maalum, na midhihirisho ya kiujumla ya utashi wa kiungu, hufanya vitu vyote kuwa ndani ya mipangilio ya kielimu kamili na kanuni ya Utashi. Hapana shaka kuendesha mfumo wa jua kwa uweza wa Mweza wa hali zote na kuendesha jahazi la ardhi katika mzunguko wake wa kila mwaka ni kwa wepesi sawa na uendeshaji wa damu na vilivyomo miongoni mwa chembe nyekundu na nyeupe na kuendesha atomu zake, mwendo na mzunguko ndani ya mpangilio na hekima hadi kwamba unaumba mwanadamu pamoja na zana zake za ajabu kutokana na tone la maji ndani ya mpangilio wa ulimwengu bila taabu wala uchovu.

Kwa maana ikiwa kupatisha ulimwengu kutaegemezwa kwa uwezo huo wa azali wa hali zote mambo yanakuwa mepesi kama kupatisha mwanadamu mmoja, na kama hakukuegemezwa kwake basi kumuumba mwanadamu mmoja pamoja na zana zake za ajabu na hisia zake nyeti, itakuwa ni tatizo na jambo gumu kama kuumba ulimwengu wote.

Na vivyo hivyo kama ilivyo kiongozi mmoja kwa kumwamrisha askari mmoja kushambulia itampelekea katika kushambulia, kwa siri ya utiifu na kutekeleza na kupokea amri, mtu huyo kwa amri hiyohiyo na kwa wepesi huohuo, vilevile atalipeleka jeshi kubwa tiifu kwenda kushambulia.

Halikadhalika vilivyotengenezwa vipo katika ukamilifu wa utiifu wa kanuni za utashi wa kiungu kupokea ishara za amri za bwana mlezi za kimaumbile, nazo ni kama askari aliyekuwa tayari na kama mtumishi mwenye kuamuriwa katika mwelekeo wa kimaumbile na shauku ya kimaumbile ndani ya duara la taratibu za mstari wa kupita ambao ujuzi wa azali na hekima ya azali zimeuainisha, nao ni wenye utiifu zaidi na kufuata amri kwa mara elfu kuliko utiifu wa askari jeshi, hivi vilivyotengenezwa na hasa vilivyo na uhai kati yao kila mmoja anapopokea amri ya kungu Bwana mlezi: (Toka kwenye kutokuwepo nenda kwenye uwepo na shika jukumu) huivika uweza wa kiungu kwa wepesi wa hali zote uwepo maalum kwa namna ambayo ujuzi umeiainisha na kwa sura ambayo utashi umeihusisha na kuishika mkono wake hadi kwenye medani ya uwepo.

Na kama hivyo, kwa wepesi huohuo na kwa nguvu na uweza huohuo Allah (s.w) huumba jeshi la walio hai katika majira ya machipuo na hulikabidhi majukumu.

Kwa maana kwamba kila kitu kikiegemezwa kwenye uweza huo, hakika kupatisha majeshi ya atomu zote na makundi ya nyota zote ni rahisi kama urahisi wa kupatisha atomu moja na nyota moja, wakati ambapo ikiwa itaegemezwa kwenye sababu kuumba atomu katika kiini cha jicho la kiumbe hai na katika ubongo wake – hali ya ukubalifu ili iweze kutekeleza majukumu ya ajabu – inakuwa ni jambo lenye mishkeli na ugumu kama kuumba wanyama wote.

Ngazi ya tatu: [Na kwa siri ya msaada wa Umoja na wepesi wa umoja na kudhihiri upekee]

Tutaangalia madhumuni yake kwa ishara fupi sana:

Kama kiongozi mkuu na mfalme mwenye haiba kwake huwa rahisi kuendesha mambo ya nchi pana na taifa kubwa kama wepesi wa kuendesha wakazi wa kijiji kimoja, na hiyo ni kwa umoja wa utawala wake na raia wake kufanya kulingana na amri zake peke yake. Kwa sababu kwa upande wa umoja katika utawala wake watu wa taifa hilo wanakuwa kama askari mmoja mmoja katika jeshi ni nyenzo za kurahisisha, hivyo amri na kanuni hutekelezwa kwa wepesi. Wakati ambapo mambo yakikabidhiwa kwa watawala tofauti, licha ya kuanguka katika lindi la mivutano na migongano kwa hakika kuendesha kijiji kimoja bali nyumba moja inakuwa na mishkeli kama kuendesha nchi pana.

Kisha kila mtu katika watu wa taifa hilo tiifu lenye kufungamana na kiongozi mmoja tu, kama askari anaegemea kwenye nguvu ya kiongozi huyo na anategemea ghala la zana zake katika jeshi lake kubwa, na kwa ajili hiyo anaweza kumteka mfalme katika wafalme, na kutimiza kazi ambazo zaidi ya anazozifanya katika kazi zake binafsi. Kunasibiana na huyo mfalme kunakuwa ni nguvu kuu isiyo na ukomo na uwezo usio na mipaka kwa hiyo hutekelezea matendo makubwa matukufu, wakati ambapo kujinasibu huko kukikatika, hiyo nguvu kuu inaondoka na kupeperushwa na upepo, hawezi kutimiza kazi isipokuwa kiasi kilichomo kwenye mkono wake cha nguvu ya sehemu ndogo, na zana chache anazozibeba mgongoni mwake na mirusho michache. Kama askari huyu atatakiwa kutekeleza kazi anazotekeleza yule askari aliyeelezwa ingelazimu kuwepo nguvu ya jeshi kamili mkononi mwake na hazina za zana za mfalme ziwe mgongoni mwake!

Jambo liko vivyo hivyo, hakika mfalme wa azali na milele, fundi mweza, kutokana na umoja wa ufalme wake na umoja wa utawala wake wa hali zote huendesha ulimwengu kwa wepesi sawa na kuendesha mji mmoja, na anaumba majira ya machipuo kwa wepesi wa kuumba bustani moja, na kuhuisha wafu wote katika ufufuo kwa wepesi wa kuumba majani ya miti ya bustani hiyo na maua yake na matunda yake kwenye majira ya machipuo yajayo, na anaumba nzi kwa mfumo wa kipanga mkubwa kwa wepesi na urahisi, na anajaalia mtu kuwa katika hali ya ulimwengu mkuu kwa wepesi na urahisi pia.

Wakati ambapo jambo likiegemezwa kwenye sababu hakika kuumba kidudu kimoja inakuwa ni ngumu ugumu wa kuumba kifaru mkubwa, na kuumba tunda katika matunda ni kwa ugumu wa kuumba mti kamili wenye mishkeli. Bali inapasa kila Atomu katika Atomu zenye kufanya kazi ilizopewa katika majukumu ya ajabu katika vyumba vidogo vya mwili wa kiumbe hai kuwa na macho ya kuonea kila kitu na elimu ya kutambua kila kitu, ili iweze kutekeleza majukumu hayo ya kiuhai yaliyo madhubuti yaliyowekwa vyema.

Kisha wepesi na urahisi yanafikia katika umoja kwa kiwango, kiasi inakuwa rahisi kupatikana maandalizi ya jeshi kamili kutoka katika mkono mmoja kutoka kiwanda kimoja, kama wepesi wa kuandaa askari mmoja kwa zana za kiaskari, na pindi itakapoingilia mikono mbalimbali mingine na kuchukuliwa kila kifaa katika vifaa hivyo anuwai kutoka katika viwanda mbalimbali, hakika kumwandaa askari mmoja – kwa upande wa kiasi – haiwezekani isipokuwa kwa mishkeli elfu moja na mmoja, kwani mambo huwa ni magumu ugumu ule wa kuandaa askari elfu ambapo wakuu wengi wanaingilia na makamanda wengi.

Hakika kuongoza askari elfu moja na kuwa mkuu juu yao kukiegemezwa kwa kamanda mmoja, inakuwa rahisi urahisi wa kumwongoza askari mmoja, kwa upande mmoja, wakati ambapo uongozi ukiachwa kwa makamanda kumi au kwa askari wenyewe. Hapo kutatokea mchanganyiko mwingi na fujo na mishkeli. Na mambo yanakuwa hivyo hivyo kila kitu kinapoegemezwa kwa mmoja wa pekee hakika kinakuwa rahisi kama wepesi wa kitu kimoja. Wakati ambapo yakiegemezwa kwa sababu, hakika jambo la kiumbe hai mmoja linakuwa gumu na zito kama ardhi yote, bali linakuwa haliyumkiniki kabisa.

Kwa maana katika Umoja kuna urahisi kwa kiwango cha kuwa wajibu na ulazima na katika wingi na mwingiliano wa mikono hufikia ugumu kwa kiwango cha kutoyumkinika.

Basi kama ilivyoelezwa katika (Al-Maktubati) kutoka katika mkusanyiko wa Risale-i Nur ikiwa kuhitilafiana kwa usiku na mchana, harakati za nyota na kugeuka majira ya mwaka kama mapukutiko, baridi, machipuo na majira ya joto ikiwa yatakabidhiwa kwa mwendeshaji mmoja na mtoa amri mmoja, hakika mwamrishaji huyo mkuu anaiamrisha ardhi ambayo ni askari katika askari wake kuwa: simama, zunguka, tembea, nayo kwa nafasi yake inasimama ikiwa imevutika kwa uchangamfu wa amri na inachakatika kama Ashiki wa kimaulawy michakato miwili ya siku na mwaka, na kuwa ni nyenzo rahisi mno ya mabadiliko ya majira na michakato ya nyota ya dhahiri na kufikirika, ikidhihirisha urahisi kamili na wepesi wa ukomo katika umoja.

Lakini kama jambo litaachwa – sio kwa yule mwamrishaji mmoja – bali kwa sababu na katika matashi ya nyota na matakwa yake, na ikaambiwa ardhi: Simama usitembee. Huenda katika hali ya ardhi ikatokea katika kupata majira na usiku na mchana kwa kukata maelfu ya nyota na majua ambayo ni makubwa kuliko ardhi kwa mara elfu nyingi ya masafa yanayofikia mamilioni ya miaka bali mabilioni ya miaka katika kila usiku na katika kila mwaka!

Yaani jambo linakuwa gumu na ni mushkeli kwa kiwango cha muhali na lisiloyumkinika.

Kilichomo kwenye ngazi ya tatu: Katika neno la (kudhihiri kwa upekee). Linaashiria hakika yenye ukomo wa upana, kina, umadhubuti na adhama. Tunaelekeza ufafanuzi wake na uthibitishaji wake kwa Risale-i Nur tukibainisha nukta moja katika nukta zake kwa kutoa mfano mfupi mno.

Naam, kama lilivyo jua linatia nuru ardhi yote kwa mwanga wake. Na linakuwa ni Mfano wa umoja, kwa kuwepo kwa sura yake na mfano wake kwa rangi zake saba na sura yake ya dhati katika kila kinachokabiliana nalo katika vitu angavu kama kioo ndani yake linakuwa ni mfano wa upekee.

Ingekuwa jua lina ujuzi, uweza na hiari na vikawa vipande vya kioo, matone ya maji na mapovu ambavyo majua madogo yanaakisi humo upokeaji. Lingekuwa linapatikana jua kamili kwa kanuni ya utashi wa kiungu katika kila mojawapo na pembeni mwa kila moja kati yake, vinapatikana kwa sifa yake na sura yake, bila ya kuzuia au kupunguza uwepo wake katika maeneo mengine katika utendaji wake hata kidogo. Inakuwa sababu ya mionekano mingi mno, kwa amri ya uweza wa kiungu na kuathiri kwake na hukumu yake. Basi inabainisha yaliyomo katika upekee miongoni mwa urahisi juu ya kawaida.

Kadhalika mtengenezaji mtukufu hakika kwa kuzingatia umoja anaona vitu vyote naye ni mwangalizi wake kwa ujuzi wake, utashi wake na kwa uweza wake wenye kuzungukia kila kitu, kama kwamba yeye kwa upande wa upekee na kwa udhihiri wake yupo kando ya kila kitu na hasa vyenye uhai, kwa majina yake na sifa zake tukufu, kwa kiasi anaumba kwa urahisi uliotimia katika muda mmoja anaumba nzi katika mpangilio wa kipanga, na mwanadamu katika nidhamu ya ulimwengu mkubwa. Anaumba wenye uhai kwa miujiza mingi mingi kwa kiasi kwamba lau zingekusanyika sababu zote ili kumuumba kasuku mmoja au nzi mmoja zingeshindwa. Basi anayeumba kasuku ni muumba wa ndege na sio mwingine na ambaye anaumba mwanadamu ndiye muumba wa ulimwengu na sio mwingine.

Ngazi ya Nne na tano: Nazo

[Na kwa siri ya kupasa, kutakasika na kutofautiana kwa ainisho, na kwa siri ya kutokufungika, kutokuchukua mahali na kutogawika katika sehemu].

Hakika kunakili faida inayotokana na ngazi hizi mbili katika fahamu za watu wa kawaida ni kugumu sana. Kwa hiyo tunabainisha yaliyomo katika ngazi hizo kwa muhtasari pamoja na kutaja nukta chache fupi kutoka katika ngazi hizo.

Yaani hakika Mweza wa hali zote anamiliki uwepo ambao ni wa nguvu na madhubuti mno wa ngazi za uwepo nayo ni ngazi ya kupasa ambao ni wa azali na wa milele na mwenye kutakasika na hali za kimaada na mwenye kuepukana nazo, na anabeba ainisho takatifu lenye kuwa mbali na ainisho zote, huyu mweza wa hali zote ni rahisi kwa uweza wake uendeshaji wa nyota kama kuendesha Atomu, na ufufuo mkuu ni rahisi kwake kama Majira ya machipuo, na kuhuisha watu wote katika ufufuo ni kwepesi kwake kama kuhuisha nafsi moja.

Kwa sababu kiasi cha chanda katika aina ya nguvu katika tabaka za uwepo hushika mlima mkubwa kwa tabaka hafifu za tabaka za uwepo na kuuendesha. Basi mathalani kioo, na utunzaji kumbukumbu, na hivyo ni uwepo wa nje – nao ni uwepo wenye nguvu – yamkini viwili hivyo kuunganisha na kuendesha milima mia moja na vitabu elfu moja kutoka katika uwepo wa kimfano na wa kimaanawy ambao ni dhaifu na hafifu, na kama hivyo, ni kiasi duni kiasi gani kwa upande wa nguvu uwepo wa kimfano kulinganisha uwepo wa nje. Hakika aina za uwepo wenye kuzuka na kupita wa vya yamkini, vilevile ni duni mno kwa maelfu ya ngazi na hafifu mno kuliko uwepo wa wajibu wa milele wa azali, kwa kiasi kwamba hakika ya udhihirisho katika uwepo huo mtakatifu kwa kadiri ya Atomu unaendesha Ulimwengu wa vya yamkini.

Nasikitika hakika sababu tatu zinafanana na maradhi yatokanayo na kupata sumu wakati huu. Haziruhusu kubainisha hakika hii kuu kwa nukta zake. Hivyo ninazielekeza kwenye Risale-i Nur na kwa wakati mwingine kwa kutaka kwa Allah (s.w).

Ngazi ya sita: Nayo ni [Na kwa siri ya kupinduka kwa vikwazo na vizuizi kuwa sawa na nyenzo zenye kurahisisha].

Yaani  kama ilivyo kwa kanuni katika midhihirisho ya utashi wa kiungu na amri ya kiuumbaji – ambayo elimu za kisasa wanizingatia kuwa ni fundo la kimaisha – inapeleka maada za lazima na riziki kwa kuelekea kwa utashi huo na amri kutoka katika hilo fundo la kimaisha ambalo ni kama msukumaji na mapigo yake kuelekea katika matunda ya mti mkubwa usio na utambuzi na kwenye majani yake na matunda yake. Na hayawi matawi yake yenye kutanzuka wala mashina yake yenye nguvu makakamavu hayawi vikwazo na vizuizi dhidi yake, bali yanakuwa ni nyenzo za kurahisisha na vikaao kati vya kurahisisha. Vivyo hivyo katika kuumba ulimwengu na kupatisha viumbe vyote vinaacha vikwazo vyote na vizuizi vigome na kujizuia mbele ya udhihirisho wa utashi wa kiungu na kwa kuelekea kwa amri ya kungu na kuwa ni nyenzo ya kurahisisha. Basi uweza wa milele unaumba ulimwengu na viumbe vya ulimwengu vyote kwa wepesi wa kuumba huo mti, haiwi ugumu kwake kitu chochote. Viumbe visingeegemezwa kwenye uweza huo hakika kuanzisha mti huo mmoja na kuuendesha inakuwa ni ngumu sawa na ugumu wa kuendesha miti yote, bali litakuwa ugumu sawa na kuumba ardhi na kuiendesha. Kwa sababu kila kitu wakati huo, kinakuwa ni kizuizi na kipingamizi. Na lau zingekusanyika sababu zote katika hali hii haziwezi kutuma riziki za lazima kutoka katika tumbo la fundo lake la kiuhai na mienendo yake ya amri na utashi, na kuifikisha kwa mpangilio hadi katika matunda yake, majani yake na matawi yake. Isipokuwa ikiegemezwa katika sehemu katika sehemu za mti bali hata katika kila Atomu katika Atomu zake jicho linaloona mti wote na kila sehemu yake na kila Atomu katika Atomu zake, na ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na uweza uwezao kila kitu.

Na kama hivyo panda ngazi hizi tano na uangalie ni kiasi gani katika ushirikina na ukafiri kuna mishkeli na muhali. Na ujue kiasi cha kuzuilika kwake na umbali wake na vipimo vya akili na mantiki, na kiasi cha urahisi katika njia ya Imani na Qur’an bali kiasi cha haki na hakika zilizomo zenye kukubalika kwa kiwango cha kupasa. Na kiasi cha kuingia kwake akilini na ukinaifu wake na urahisi wake kwa kiwango cha ulazima. Shuhudia hakika hii na useme: Alhamdulillah juu ya neema ya Imani.

(Mikandamizo na kero zimesababisha kuahirisha sehemu iliyobakia katika ngazi hii kuu katika wakati mwingine apendapo Allah).

Ngazi ya saba: [Na kwa siri ya kwamba Atomu, sehemu, kipande cha sehemu, kokwa na Mwanadamu sio ya uchache kwa ufundi na ukuu kuliko nyota, jumla, sehemu ya jumla, mti na ulimwengu].

Tanbihi:

Hakika misingi ya hakika ya ngazi hizi tisa na hazina zake na jua lake ni katika Aya mbili za Surat Al-Ikhlasi :

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ ۞ اللَّهُ الصَّمَدُ

Hiyo ni Ishara fupi ya ming’ao ya midhihirisho ya siri ya upekee na kutegemewa kwa haja zote.

Tutatupa jicho katika yaliyomo kwenye ngazi hii ya saba kwa nukta moja au mbili tukielekeza maelezo yake kwenye Risale-i Nur.

Na hiyo inamaanisha hakika ya Atomu ambayo inatekeleza majukumu ya ajabu kwenye jicho na ubongo sio ya uchache wa kiufundi na kupendezesha kuliko nyota, na sehemu sio ya uchache kwa ukuu kuliko jumla yake yote. Basi mathalani: Ubongo na jicho sio ya uchache kutengenezwa vema na kupendezeshwa kuliko mwanadamu. Wala kiungo cha sehemu ni cha uchache wa kupendezeshwa kuliko sampuli ya jumla, kwa upande wa uzuri wa kutengenezwa vema na ajabu katika kuumba. Wala mwanadamu sio wa uchache kiufundi kuliko jinsi ya wanyama kwa ujumla, kwa upande wa viungo vyake vya ajabu. Wala mbegu ambayo ni sawa na faharisi na programu na kumbukumbu sio ya uchache wa kutengenezwa vyema kuliko mti wake ulio stawi, kwa upande wa ukamilifu wa ufundi na kuhazini. Wala mwanadamu ambaye ni ulimwengu mdogo sio mchache kwa kutengenezwa kwa kupendeza kuliko ulimwengu mkubwa, kwa kiasi kwamba yupo katika umbo lililo bora kabisa na anamiliki viungo vyenye kufurutu ada vyenye kujumuisha vimeandaliwa kutimiza maelfu ya majukumu ya ajabu.

Basi ambaye anaumba Atomu kwa hiyo hashindwi kuumba nyota, na ambaye anaumba Ulimi – nacho ni kiungo katika Mwanadamu – anaumba mwanadamu kwa urahisi na wepesi bila shaka. Na ambaye anamuumba mwanadamu katika umbo bora mno hapana shaka kwamba yeye ni mweza kuumba wanyama wote kwa wepesi kamili, mfano wa anavyowaumba mbele ya macho yetu. Na ambaye anaumba kokwa kwa ainisho la Faharisi na orodha ya misamiati, na daftari la kanuni za amri, na fundo la kiuhai, hapana shaka ndiye ambaye atakuwa Muumba wa miti yote. Na ambaye amemjaalia mwanadamu kuwa anafanana sana na mbegu ya kimaanawy ya ulimwengu na tunda lake lenye kukusanya na mahali pa kuonekana kwa majina yake yote ya kiungu na kioo chake na mwenye kufungamana na viumbe vyote na khalifa wa Ardhi, hapana shaka kwamba anamiliki uweza wenye kuweza kuumba ulimwengu wote na kuuratibu kwa urahisi wa kumuumba mwanadamu. Na kwa ajili hii basi mwenye kuwa ni muumba, mtengenezaji na Bwana Mlezi wa Atomu, sehemu, kinachohusiana na sehemu, kokwa na mwanadamu, basi kwa uwazi na hapana shaka kuwa yeye ndiye muumba wa nyota, sampuli, vyote, mikusanyiko ya jumla, miti, viumbe vyote na mtengenezaji wake, na mola wake mlezi hasa, basi ni muhali kuwa mwingine na ni jambo lisilowezekana kabisa.

Ngazi ya Nane: [Kwa siri ya kwamba kilichozungukwa na vijisehemu ni kama mifano iliyoandikwa midogo au kama matone yaliyokamuliwa, basi hapana budi kuwa mzungukaji na mikusanyiko ya jumla katika mshiko wa muumba wa chenye kuzungukwa na vinavyohusiana na sehemu ndogo ili aingize mfano wake ndani yake kwa mizani ya ujuzi wake au kukamua kutokea humo kwa taratibu za hekima yake].

Yaani, hakika ya uwiano wa vijisehemu vyenye kuzungukwa, kila moja, kokwa, na mbegu ambazo zinabebwa na vyote, mjumuiko wa hadi kwenye mikusanyiko mikubwa na yenye kuzunguka, ni vyenye kurandana na vielelezo vilivyowekwa katika umbo dogo na mifano iliyoandikwa ndani yake kama yaliyoandikwa timamu katika yote na mikusanyiko uandishi madhubuti unaowiana na vipande hivyo vidogo. Na kwa ajili hii basi mikusanyiko ya jumla yenye kuzunguka iko katika mshiko wa Muumba wa hivyo visehemu na bila shaka chini ya usarifu wake na hiyo ili aingize kitabu cha mzunguko huo mkubwa kwa vipimo vya ujuzi wake na kwa kalamu zake madhubuti katika mamia ya vipande na madaftari madogo.

Kisha uwiano wa sehemu na vijisehemu vilivyozungukwa kwa majumuisho yenye kuzunguka na mifano yake, vinashabihiana na matone yanayokamuliwa au kutoka kwenye mijumuiko yenye kuzunguka. Basi kwa mfano kokwa ya tikiti ni kama tone lililokamuliwa kutoka pande zote za aina ya tikiti au ni nukta iliyoandikwa ndani yake kitabu kamili cha tikiti hata kwamba hiyo kokwa inabeba faharisi yake, orodha yake ya yaliyomo na programu yake.

Basi kwa kuwa jambo liko hivi, hivyo vijisehemu na matone na nukta na kila moja vinalazimu kuwa kwa mkono wa Mtengenezaji wa jumla hiyo yenye kuzunguka na mikusanyiko hiyo yenye kuzunguka, ili akamue kila moja, matone, na nukta kutokana nazo kwa taratibu za hekima yake nyeti. Kwa maana kwamba Muumba wa kokwa moja na kitu kimoja ndiye muumba wa jumla hiyo kubwa na mikusanyiko, na muumba wa mikusanyiko na jinsi ambazo zinazizidi ukubwa na kuzizungukia vilevile na sio mwingine. Na kwa ajili hii basi muumba wa nafsi moja anaumba watu wote, na ambaye anafufua maiti mmoja anafufua majini na wanadamu na wafu wote siku ya ufufuo, na atawafufua. Na kama hivi shuhudia kiasi cha ukweli wa madai

مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Qur’an, 31:28.

na kiasi cha kuthibiti kwake na ukinaishi wake, shuhudia kwa sura yake angavu na dhahiri mno.

Ngazi ya Tisa: [Na kwa siri kama ilivyo Qur’an ya utukufu iliyoandikwa kwenye Atomu inayoitwa kuwa ni Johari ya pekee kwa Atomu za Ether (Athiir) sio ya uchache kiukuu na ufurutu wa kiufundi kuliko Qur’an ya Adhama iliyoandikwa juu ya ukurasa wa Mbingu kwa wino wa nyota na majua, vivyo hivyo hakika ua la mti wa maua sio la uchache wa ukuu na ufundi kuliko nyota ya aina ya zuhura, wala nyenyere kuliko tembo, wala kirusi kuliko kiboko, wala nyuki kuliko mtende, kwa mujibu wa uweza wa muumba wa viumbe. Na kama ilivyo upeo wa ukamilifu wa kasi na urahisi katika kupatisha vitu kumewaingiza watu wa upotevu katika kuchanganya kuunda na kuundika kunakolazimu mihali isiyo na mipaka inayotolewa na dhana, vilevile imethibitisha kwa watu wa uongofu kuwa sawa kwa nyota pamoja na Atomu kwa mujibu wa uweza wa Muumba wa viumbe (s.w) na lailaha illa huwa Allah Akbar].

Nilikuwa nataka kubainisha maana ya ngazi hii ya mwisho kwa urefu lakini kwa masikitiko taabu na dhiki itokanayo na udhibiti wa kiusumbufu vimezuilia jambo hili. Na udhaifu ambao uliokuwa mwilini mwangu kutokana na kuingiwa na sumu ukiachilia mbali maradhi yenye kuumiza. Kwa hivyo nimelazimika kutosheka na ishara fupi kwenye maana yake. Nayo ina maana: Kama ingeandikwa Qur’an kubwa kwenye Atomu – ambayo inayoitwa katika Elimu ya Al-Kalaam na Falsafa kuwa ni Johari ya pekee ambayo haikubali kugawanyika – kwa Atomu za Ether ambazo ni ndogo kuliko hizo, na vilevile ingeandikwa Qur’an kubwa nyingine kwenye kurasa za mbingu kwa nyota na majua, kisha zikalinganishwa baina yake, hapana shaka kwamba Qur’an iliyoandikwa kwa johari ya pekee sio ya uchache kwa ukuu, muujiza na kupendezeshwa kuliko Qur’an adhimu kubwa ambayo imetia uzuri uso wa mbingu, na huenda hiyo ni yenye ukuu zaidi kuliko hiyo kwa upande mmoja. Vivyo hivyo ua sio la uchache wa ukuu na ufundi kuliko nyota ya aina ya Zuhura wala nyenyere sio duni mno kuliko tembo bali kidudu kidogo ni cha ajabu zaidi kuliko kifaru kwa umbo na nyuki kwa maumbile yake ya ajabu ni ajabu zaidi kuliko mtende kwa kulingana na uweza wa muumba wa viumbe. Kwa maana kwamba muumba wa nyuki anaumba wanyama wote, na ambaye anaifufua nafsi moja anawakusanya watu kwenye eneo la ufufuo na kuwafufua wote, na kuwakusanya kwa vyovyote. Hakiwi kigumu kwa uweza huo kitu chochote. Kama mamia ya vielelezo vya ufufuo vinavyoshuhudiwa mbele ya macho yetu kila majira ya machipuo.

Maana ya kifungu cha Kiarabu cha mwisho na yaliyomo kwa muhtasari ni: Hakika watu wa upotevu kwa ujinga wao wa hakika zilizothibiti na imara za ngazi zilizotangulia, na kwa kudhihiri kwa vilivyomo kwenye uwepo katika ukomo wa wepesi na urahisi, imechanganyika kwao kuundwa kwake na kupatishwa kwake kwa uweza wa mtengenezaji mweza uweza wa hali zote, pamoja na kuundika kwake na kupatikana kwake kwa nafsi yake, wakijifungulia wenyewe milango ya upotofu na mihali isiyo na mipaka inayokataliwa na dhana na akili. Kwani katika hali hiyo – mathalan – inalazimu kuipa kila Atomu miongoni mwa Atomu za kiumbe hai uweza uwezao kutengeneza kila kitu na ujuzi na macho yanayoona kila kitu. Yaani kwa kutokubali kwao Mungu mmoja wa pekee wamelazimika kukubali Miungu mingi kwa idadi ya Atomu kwa mujibu wa mrengo wao wa kifikra. Wakistahiki kuingia chini ya chini ya jahanamu.

Ama watu wa uongofu hakika zenye nguvu kwa ngazi zilizopita na hoja zilizopangika imara zimetunuku katika nyoyo zao salama na akili zao zenye kusibu ukinaifu wa kukata shauri na imani yenye nguvu na kusadiki kwa dhati ya yakini, hata wakaitakidi pasipo na shaka wala utata na kwa kila utulivu wa moyo kwamba hakuna tofauti kati ya nyota na Atomu na kitu kidogo mno na kikubwa zaidi mbele ya uweza wa kiungu, ambapo tunashuhudia mbele yetu viumbe hivi vya ajabu. Kila ufundi wa ajabu kati yake unasadiki madai ya aya tukufu

مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ

na kushuhudia kwamba hukumu yake ndio dhati ya haki na hakika tupu. Na unasema kwa ulimi wa hali Allah Akbar. Nasi kwa nafasi yetu tunasema Allah akbar kwa idadi ya viumbe tukisadiki hukumu ya Aya hii tukufu kwa nguvu yetu yote na kukinai kwetu na tunashuhudia kwamba hukumu yake kuwa ndiyo haki  na hakika yenyewe kwa hoja zisizo na ukomo.

سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَاۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

اللَّهُمَّ صَلّ وَسَلّمْ عَلَي مَنْ أَرْسَلْتَهُ رَحْمَةً لِلْعَالمَيْنَ وَالْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.