Sehemu Ya Pili Muhtasari wa Surat (Al-Fatiha)

Kutoka katika somo moja tu lililotolewa katika shule ya Yusuf ya tatu katika kipindi kifupi sana wakati wa kuhamishwa kwangu katika kutengwa na jela ya pekee kwenda katika mahali pa jumla na kuchanganyika na wengine.

Kielelezo cha somo fupi sana lililotolewa kwa wanafunzi wa nuru jela

(Al-Fatiha) ambayo imo katika swala, imeamrisha moyo kubainisha tone katika bahari yake na mng`aro katika miminiko za rangi saba za jua lake. Na tumeandika nukta maridadi katika upeo wa uzuri wa hazina hii kuu ya Qur’an katika maandiko ya ishirini na tisa – sehemu yake – na hasa katika matembezi ya kufikirika katika (Nuun) ya neno (Naabud) na katika Risala ya (Al-Rumuuz al-Thamaniya), na katika tafsiri ya (Isharat al-I’jaz) na katika sehemu nyingine za Risale-i Nur. Isipokuwa nimelazimika – kwa upande mmoja – kuandika tafakuri yangu katika swala ya ishara ya muhtasari huo wa Qur’an mzuri katika nguzo za imani na hoja zake tu na muhtasari wake ambao ni mfupi mno kama sehemu ya kwanza.

Naanza kwa

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ۞ الرَّحْمـنِ الرَّحِيمِ ۞ مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ۞ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ۞ اهدِنَــــا الصِّرَاطَ المُستَقِيمَ ۞ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ

Neno la kwanza: nalo  ni (الْحَمْدُ للّهِ)

Hakika ishara kwa muhtasari mno katika hoja yake ya kiimani ni: Kwamba kichocheo cha himidi na shukurani ulimwenguni, ni neema ambazo zinaletwa kwa wingi kwa makusudi na hasa kuleta maziwa safi mazuri kwa wanywaji katikati ya kinyesi na damu kwa vichanga na watoto wasio weza lolote, na hisani na zawadi za hiari, na takrima na dhifa za rehema ambazo zimefunika uso wa ardhi yote, bali zimeenea ulimwengu wote, na kwamba thamani na kima kinachotolewa kwa ajili yake ni: (Bismillah) mwanzo kisha (Alhamdulillah) mwisho, na kati ya mawili hayo ni kuhisi kuneemeshwa ndani ya neema yenyewe, kisha kutokea hapo kufikia hadi katika kumtambua mola mlezi mtukufu. Basi jitazame nafsi yako hasa na tumbo lako na milango yako ya fahamu! Ni kiasi gani inahitajia mambo mengi na neema nyingi! na kiasi gani inahitaji riziki ladha na maonjo kwa thamani ya himidi na shukurani! Tazama hili na kipime kila chenye uhai kwa nafsi yako.

Na kama hivi hakika himidi isiyo na kikomo itokanayo katika ndimi za hali na kauli, kupitia neema hizi zenye kuenea, inabainisha kama jua liangazalo hali ya ulezi wa kiungu wa jumla na uwepo wa mwaabudiwa mhimidiwa na mneemeshaji mwingi wa rehema.

Neno la pili: nalo (رَبِّ الْعَالَمِينَ)

Hakika ishara fupi katika hoja iliyomo ni: Hakika tunashuhudia kwa macho yetu kwamba katika ulimwengu huu kuna maelfu ya ulimwengu na limwengu ndogondogo, bali mamilioni, na ghalibu yake zimeingiliana, pamoja na kuwa uendeshaji wa kila moja kati ya hizo na masharti ya kutawalia mambo yake ni tofauti, inaongozwa kwa ulezi uendeshaji utawala mkubwa mno. Ulimwengu wote ni ukurasa uliokunjuliwa mbele ya uoni wake (s.w) nyakati zote, na limwengu zote zinaandikwa kama msitari kwa kalamu ya uweza wake na kadari yake, na kufanywa upya na kugeuzwa. Basi shahidi za jumla na sehemu hujitokeza na kwa idadi ya atomu na vilivyomo vyenye kupatikana kutokana na muundo wake, kila punde kidogo na kila wakati, juu ya kupasa kwa uwepo wa mlezi wa walimwengu na upweke wake, ambaye anaendesha mamilioni haya ya limwengu na viumbe vyenye kumiminika kwa ulezi huria wenye elimu na hekima zisizo na mwisho na zenye uangalizi na rehema zenye upana kukifikia kila kitu.

Hakika asiyesadiki ulezi mtukufu unaolea na kuendesha mambo, kuanzia katika shamba la chembe ndogo mno hadi katika mfumo wa jua na katika duara la njia kubwa za sayari, na kutoka katika kijichumba katika mwili hadi katika bohari ya ardhi na katika ulimwengu wote, unalea na kuendesha mambo yake kwa kanuni hiyohiyo na kwa ulezi huohuo na kwa hekima hiyohiyo, wala hahisi wala hayatambui wala hayaoni, hakika anajaalia nafsi yake kuwa ni mstahiki wa adhabu ya kudumu na anainyang’anya kuhurumiwa.

Neno la tatu nalo ni: (الرَّحْمـنِ الرَّحِيمِ)

Ishara fupi mno katika hoja iliyomo nayo: Ni kwamba inashuhudiwa kwa uwazi sawa na mwanga wa jua uwepo wa rehema isiyokoma ulimwenguni na hakika yake. Basi rehema hii pana inashuhudia ushahidi wa kukata shauri kabisa – kama ushahidi wa mwanga juu ya jua – juu ya mwingi wa rehema mwenye kurehemu aliyejificha kwa sitara ya ghaibu.

Naam, sehemu muhimu ya rehema ni riziki, ambapo jina la Allah (s.w) (Ar-Rahman) hupewa maana ya Ar-Razzaq. Na riziki yenyewe inajulisha juu ya Al-Razzaq Ar-Rahiim kwa uwazi kwa kiasi kwamba humfanya mwenye utambuzi alazimike kusadiki na kuamini.

Kwa mfano:

Hakika (s.w) anatayarisha riziki za wenye uhai wote, na hasa wasiojiweza na hususan watoto, nao wameenea katika ardhi yote na katika anga lote, na anawaandalia kwa namna ya ajabu nayo ikiwa nje ya eneo la hiari yao na uwezo wao, kutokana na pasipo na chochote, kutokana na mbegu yenye kufanana, kutokana na matone ya maji, na kutokana na punje za mchanga. Hata kwamba anawadhalilishia vifaranga dhaifu visivyoweza kuruka na vilivyokaa kwenye viota vyake vileleni mwa miti, mama zao kama wanajeshi wenye kungojea amri, huzunguka kwenye mimea na kutafuta maji ili kuviletea riziki. Bali anamdhalilisha simba mwenye njaa kwa ajili ya mtoto wake, anamlisha nyama anayoipata bila ya kuila. Na anapeleka maziwa safi mazuri kwa wanywaji, kati ya kinyesi kichafu na damu nyekundu, kwenda kwa watoto wa wanyama na mwanadamu, na anapeleka kutokea kwenye chemchem za chuchu, pasipo kuchanganyika wala kuchafuka, akijaalia huruma za mama zao ni zenye kuwasaidia.

Na kama anavyotoa riziki munasibu kwa miti yote yenye kuhitajia kwa aina ya riziki kwa namna ya ajabu, ananeemesha hisia za mwanadamu ambazo zinahitajia aina fulani ya riziki za kimaada na kimaanawy, na kufanya vizuri kwa ajili ya akili yake moyo na roho yake hali ya kuwa ni meza ya chakula pana mno ya riziki mbalimbali. Hata kana kwamba viumbe ni mamia ya maelfu ya meza za vyakula za neema zenye kuingiliana na mamia ya maelfu ya vyungu vya vyakula tofauti, vikihifadhiana kama majani ya ua na kama vifuniko vya vikonyo, kifuniko ndani ya kifuniko. Inajulisha kwa asiyepofuka macho yake, juu ya mwingi wa rehema mtoa riziki na mwenye kurehemu mkarimu kwa ndimi kwa idadi ya vyungu hivyo vilivyotandazwa na kwa kiasi cha vyakula vilivyomo, ndimi mbalimbali kiujumla na kwa sehemu.

Na ikisemwa:

Kwamba yaliyo hapa duniani miongoni mwa misiba na mabaya na shari ni mambo ambayo yanapingana na rehema hiyo pana ambayo imekienea kila kitu, na kutibua usafi wake!

Jibu:

Sehemu za Risale-i Nur zimetosheleza jibu hili, na hasa Risala ya (Kadari). Tunaelekeza huko na huku tukiashiria ishara fupi:

Hakika kila kijisehemu na kila aina na kila kilichopo, kina kazi mbalimbali za jumla na za sehemu, na kila moja katika majukumu hayo kuna matokeo tele na matunda mengi. Na wingi kabisa kati yake ni matokeo mazuri na masilahi yenye manufaa, kheri na rehema nyingi. Na sehemu ndogo kati ya hizo huwa ni shari, ubaya kwa sehemu na kwa nje na dhuluma kwa yule ambaye amekosa hali ya ukubalifu, na wenye kukabiliana nayo kimakosa, au wenye kustahiki malipo na kutiwa adabu, au kwa yale yanayokuwa ni nyenzo ya uzalishaji mkubwa. Kama rehema ingezuilia kijisehemu hicho na hicho kilicho kwa ujumla kutimiza jukumu hilo ili kuzuia isije shari hiyo ndogo, hivyo basi yasingepatikana matokeo yake yote mengine mazuri yenye kheri. Na hapo zitatokea shari na mabaya kwa idadi ya matokeo hayo, kwani kukosekana kwa kheri ni shari, na kuharibu uzuri ni ubaya. Kwa maana kwamba mamia ya shari na dhuluma hutendwa kwa kuzuia isije kutokea shari moja, na jambo hili linapingana kabisa na hekima na masilahi na rehema ambayo ulezi wa kiungu unasifikana nayo.

Mfano wa hilo:

Hakika barafu na baridi na moto na mvua na aina mbalimbali mfano wa hayo hubeba kila moja kati yake mamia ya hekima na masilahi, kama mmoja kati ya wazembe akitenda shari kwa uchaguzi wake mbaya katika haki ya nafsi yake kama kuwa ameingiza mkono wake kwenye moto kisha akasema: Katika kuumbwa kwa moto hakuna rehema, hakika faida za moto wenye kheri na huruma – wenye manufaa nazo hazihesabiki – zinakadhibisha kauli yake na kumpiga kofi katika kinywa chake.

Kisha matashi ya mwanadamu na hisia zake duni ambazo hazioni mwisho, haziwi – moja kwa moja – kuwa ni kipimo na mizani sahihi kwa kanuni za wingi wa rehema na wingi wa hekima na ulezi wa kiungu unaopita katika ulimwengu, kwani anaona uwepo kupitia hisia hizo kulingana na rangi za kioo chake. Basi moyo wenye giza usiokuwa na rehema huona viumbe vinalia vibaya vinachanika kati ya kucha za dhuluma na kugeuka katika msongo wa giza. Wakati ambapo akivitazama kwa jicho la imani angeviona katika sura ya mwanadamu mkubwa mwenye kuvaa mpambao sabini elfu yenye kupendeza mno yenye kushonwa kwa rehema, kheri na hekima, zikipandiana hizi juu ya hizi kana kwamba ni huri kutoka peponi amevaa mapambo yake sabini elfu, na kumwona daima mwenye kutabasamu kucheka na mwenye furaha. Na kuona sampuli ya mwanadamu ambaye ndani yake ni ulimwengu uliofanywa mdogo, na kila mwanadamu ni ulimwengu mdogo, basi atasema kutokea katika kina cha moyo na roho yake.

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ۞ الرَّحْمـنِ الرَّحِيمِ ۞ مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ

Neno la nne: nalo ni (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ)

Ishara kwa muhtasari sana katika hoja iliyomo ndani yake ni:

Kwanza:

Hakika dalili zote zenye kuashiria ufufuo na akhera na zenye kushuhudia hoja ya (Wailayhil Al-Maswiir) mwishoni mwa sehemu ya kwanza ya somo hili, zinashuhudia vilevile juu ya hakika ya kiimani pana ambayo inaziashiria.

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ

Pili:

kama ilivyo ulezi wa kiungu wa mtengenezaji wa ulimwengu huu na rehema yake pana na hekima yake ya milele, na kadhalika uzuri wake, utukufu wake na ukamilifu wake wa Azali na milele, na vilevile sifa zake tukufu zisizo na mipaka na mamia ya majina yake mazuri, yote yanahitajia kabisa Akhera –kama ilivyosemwa mwishoni mwa neno la kumi – basi kadhalika Qur’an tukufu kwa maelfu ya aya zake na hoja zake. Na vivyo hivyo mjumbe mtukufu Muhammad (s.a.w) kwa mamia ya miujiza na hoja zake. Pia na mitume wote Anbiyaa na Mursalina (a.s). Na vilevile vitabu vya mbinguni na sahifa takatifu kwa dalili zake zisizo na mipaka, zote zinashuhudia akhera.

Na baada ya hayo, ambaye haamini maisha ya kudumu katika makao ya akhera hakika anaitupa nafsi yake kwenye Jahannam ya kimaanawy inayoletwa na ukafiri, hivyo atateseka na adhabu daima, na hali ya kuwa bado yungali duniani, ambapo nyakati zote zilizopita na zijazo na viumbe na vilivyomo kwa kutoweka kwake na utengano wao vitanyesha mvua mbaya juu ya roho yake na moyo wake na kumuonjesha machungu yasiyo kuwa na ukomo na dhambi kama adhabu za Jahannam kabla hajaingia huko akhera kama hilo lilivyowekwa wazi katika risala ya Mwongozo kwa vijana.

Tatu:

Tunaashiria kwa alama

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ

katika hoja tukufu na yenye nguvu ya ufufuo. Lakini hali maalum iliyotokea kwa ghafla imesababisha kuahirisha hoja hiyo hadi muda mwingine. Na pengine hoja hiyo haihitajiki tena, kwa kuwa Risale-i Nur imethibitisha kwa mamia ya hoja zenye nguvu za kukata shauri kwamba kuchomoza kwa Asubuhi ya Ufufuo na kuingia majira ya machipuo ya kiama ni yakini kama ujio wa mchana baada ya usiku na ujio wa machipuo kufuatia majira ya baridi.

Neno la tano nalo ni: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Kabla ya kuashiria hoja iliyomo umepita kwenye moyo ufafanuzi wa matembezi ya kifikira yenye hakika, ufafanuzi mfupi kwa msingi wa kuweka wazi (Andiko la ishirini na tisa) nayo ni kama ifuatavyo:

Nilipokuwa ninatafuta miujiza ya Qur’an, kama ilivyobainishwa katika Risale-i nur, katika tafsiri ya (Isharaat al-I’jaz) na katika Risala ya (Ar-Rumuuz al-Thamaniya). Na nilipoona miujiza kadhaa kuhusu maelezo ya ghaibu katika aya ya mwisho kwenye sura Al-Fathi, na muujiza wa kihistoria katika:

فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ Qur’an, 10:92

bali nimeona ming’aro ya miujiza mbalimbali sehemu nyingi katika maneno ya Qur’an na nukta za kimiujiza makini katika baadhi ya herufi zake. Na wakati huu nikiwa ninasoma surat Al-Fatiha ndani ya swala limejitokeza swali moyoni mwangu, ili linifundishe muujiza kati ya miujiza ya (Nun) ambayo imo katika (Na’budu wanastaiin).

Na swali ni kwamba:

Kwa nini amesema (Na’budu..nastaiin) kwa nuun ya mzungumzaji na mwingine na hakusema (A’bud … astaiin)?

Na ghafla ilifunguliwa mbele ya mawazo yangu uwanja mpana wa matembezi kutokana na mlango wa (Nun) hiyo. Nikajua kwa kiwango cha kushuhudia siri kubwa iliyomo kwenye sala ya jamaa, na nikashuhudia manufaa yake matukufu na nikajua kwa yakini kwamba herufi hii moja yenyewe kwa dhati yake ni muujiza, nao ni:

Nilipokuwa nikiswali wakati huo katika msikiti wa (Bayazid) na wakati wa kusema kwangu:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

nikaona kwamba jamaa ya msikiti huo wanaunga mkono madai yangu haya kwa kusema kwao kama nisemavyo mimi, na wanashirikiana nami ushirikiano kamili katika madai yangu haya na katika dua langu ambalo limo katika

إِهْدِنَا

wakinisadikisha mimi. Katika wakati huu hasa ilifunuliwa pazia mbele ya mawazo yangu nikaona kana kwamba misikiti ya Istanbul yote imegeuka kuwa ni (Msikiti wa Bayazid) mkubwa na wenye kuswali humo wote wanasema kama mimi:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

wakisadikisha na kuitikia amina katika dua yangu. Na katika kuchukua kwao sura ya waombezi wangu, ikafunguliwa pazia nyengine mbele ya mawazo yangu, nikaona kwamba ulimwengu wa Kiislamu umechukua sura ya msikiti mkubwa sana na kuchukua Makka tukufu na Al-Ka’ba ni mihirabu ya msikiti huo mkuu na wenye kuswali wote waliojipanga safu wameelekeza nyuso zao kwa mzunguko kuelekea mihirabu hiyo takatifu nao wakisema mfano wangu:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ۞ اهدِنَــــا

na kila mmoja anasadikisha wote na kuomba kwa jina lao, na kuwafanya wanaosali wote ni waombezi wake.

Na nilipokuwa nikifikiria kwamba njia wanayopita jamaa kubwa kwa kiasi hiki haiwi njia ya upogo hata kidogo na maombi yake hayawi isipokuwa ni yenye kusibu, na wala maombi yao hayarudishwi bali hufukuzwa shubuhati za shetani, wakati nikisadikisha manufaa makubwa ya swala katika jamaa usadikishaji wa kiushuhuda, ikaondoshwa pazia nyingine, nikaona:

Kana kwamba ulimwengu ni msikiti mkubwa na mataifa yote ya viumbe wamezama katika swala kubwa ya jamaa,

كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُ وَتَسْبِيحَهُ Qur’an, 24: 41.

wanatekeleza aina ya swala yao maalum kwa ulimi wa hali, kwa kutimiza utumishi mpana mkubwa sana mbele ya ulezi wenye kuzunguka kila kitu wa mwaabudiwa mtukufu, wote kati yao wanasadikisha ushaihidi wa wote juu ya tawhidi kwa kiasi kila mmoja kati yao hupata ithibati ya matokeo hayohayo, nilipokuwa nikishuhudia mambo haya, pazia nyingine ilinyanyuliwa, na nikaona:

Kama ulivyo ulimwengu ambao ni mwanadamu mkubwa unasema kwa ulimi wa hali na ulimi wa maandalizi na haja ya kimaumbile ya sehemu zake nyingi, na kwa ulimi wa kauli kwa wenye utambuzi kati ya vilivyomo:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

wakidhihirisha utumishi wao kwa muumba wao mbele ya ulezi wake wa kiungu wenye rehema, vivyo hivyo mwili wangu, huu ulimwengu mdogo, kama mwili wa kila mwenye kuswali na mimi katika jamaa ile kubwa unasema kwa Atomu zake na nguvu zake na hisia zake pia:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

kwa ulimi wa utii na uhitaji mbele ya ulezi wa muumba wake, akifuata amri ya mola wake hali ya kusalimu amri kwa utashi wake (s.w), na nikaona kwamba jamaa ile miongoni mwa chembe vumbi na nguvu na hisia kila wakati inaonesha uhitaji wake kwa uangalizi wa muumba wake mtukufu na kukunjua mbele ya rehema zake na msaada wake. Na nikashuhudia kwa kuvutiwa kwa siri ya hali ya juu ya jamaa katika swala, na nimeona muujiza mzuri wa (Nuun) ya naabudu. Na nikaaga matembezi hayo ya kimawazo mbele ya mlango wa (Nun) nilioingia kupitia hapo. Na nikamhimidi Allah (s.w) kwa kusema: Alhamdulillah na nikatembea niseme:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

kwa ulimi wa jamaa zile tatu, wale marafiki wakubwa na wadogo.

Na sasa utangulizi umekwisha, na turudi katika mazungumzo yetu. Nayo ni ishara fupi katika hoja ambayo inaashiria

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Kwanza:

Hakika tunashuhudia kwa macho yetu utendaji na uumbaji mkubwa wenye kudumu katika mpangilio na uwiano unaotokea ulimwengu mzima na hasa katika uso wa ardhi. Na tunashuhudia ulezi bila mpaka wenye rehema wenye kuendesha ndani ya huu utendaji na uumbaji unaitikia maombi ya

msaada yanayotokea kwa wenye uhai wasio na ukomo na dua zao za kimatendo na kihali na kikauli mwitikio wenye sifa ya ukamilifu wa hekima na ukomo wa uangalizi. Na tunaona midhihirisho ya uungu usio na mipaka na sifa ya kuabudiwa ya jumla ndani ya ulezi huu na ndani ya matukio ya kumwitikia kila kiumbe mmojammoja uitikiaji wa kimatendo kukabiliana na maelfu ya aina ya ibada za kimaumbile na kihiari ambazo viumbe wote wanazitekeleza na hasa wenye uhai na hasa mataifa ya mwanadamu, akili iliyosalimika inaona na imani pia inaona hilo. Kama vitabu vyote vya mbinguni vinavyoelezea hilo na manabii watukufu (a.s).

Pili:

Hakika kujishughulisha kwa kila jamaa katika jamaa hizo tatu zilizotajwa hapo mwanzo, na ishara inayo ashiriwa na (Nuun) ya Na’budu, kujishughulisha wote kwa pamoja na ibada za kimaumbile na za hiari na kwa namna mbalimbali kunajulisha waziwazi kwamba ni mkabala wa shukurani mbele ya uungu wenye kuabudiwa na ni ushahidi wenye nguvu kabisa juu ya uwepo wa mwaabudiwa mtakatifu.

Na kwamba kila jamaa kati ya jamaa tatu zilizotajwa na katika kila kundi kati ya makundi yake, na kila mmoja kati yao kuanzia katika mkusanyiko wa ulimwengu wote hadi katika jamaa ya atomu za kiwiliwili kimoja, ina msaada wa kimatendo na kihali, na kila moja kati yao kuwa na dua maalum kwake kama inavyo ashiria hilo (Nuun) ya Nastaiin. Utendaji wa kusaidia kila mmoja kati ya hao, kuwaokoa na kujibu dua zao, ni ushahidi wa kweli haukubali shaka kabisa juu ya mwendeshaji Mpole Mwingi wa rehema.

Mathalani:

Kama (Neno la ishirini na tatu) lilivyotaja: Hakika kuitikia maombi ya aina tatu yanayoombwa na viumbe wote ardhini kote, mwitikio wa ajabu mno na kwa namna isiyodhaniwa, kunashuhudia bila shaka yoyote kuwepo kwa Mola mlezi Rahimu Mujibu.

Naam, kama tunavyoshuhudia kwa macho yetu, kuitikiwa kwa dua ya kila kokwa na kila mbegu inayomuomba muumba wake kwa maandalizi ili iwe mti na shuke. Vivyo hivyo tunashuhudia kupelekwa kwa riziki kwa wanyama wote ambao mikono yao ni mifupi kuweza kuzifikia, na kuwapa yanayolazimu katika maisha yao, na kuitikia maombi yao ambayo yapo nje ya uwezo wao, na ambayo wanayaomba kutoka kwa mmoja wa pekee kwa ulimi wa uhitaji wa kimaumbile.

Basi uitikiaji huu na misaada inashuhudia ushahidi wa kweli juu ya muumba mkarimu ambaye anaitikia maombi yote hayo yatokanayo na ulimi wa uhitaji wa kimaumbile, kama tunavyoshuhudia kwa macho yetu wazi kabisa, na kulazimisha viumbe wa ajabu wasio na hisia kuwasaidia wanyama hao katika wakati munasibu na katika hekima timamu kabisa.

Na kama hivi basi kwa kupimia sehemu hizi mbili, hakika kuitikiwa kwa aina zote za dua ambazo zinaombwa kwa ulimi wa kauli, na hasa dua za Manabii (a.s) na viumbe mahususi, kuitikiwa kwa ajabu, kunashuhudia juu ya hoja ya upekee ambao umo katika

وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Neno la sita اهدِنَــــا الصِّرَاطَ المُستَقِيمَ

Hakika ishara fupi mno katika hoja yake ni:

Kama ilivyo njia fupi kabisa kati ya njia zinazoelekea kutoka mahali hadi mahali pengine ni njia iliyonyooka sawasawa, na kwamba misitari mifupi kabisa iliyonyooka kati ya nukta moja na nyingine iliyo mbali nayo ni msitari ulionyooka, kadhalika hakika njia yenye kusibu zaidi katika mambo ya kimaanawy na katika njia za kimaanawy na katika masilaki (Mwelekeo wa kisufi) ya kimoyo na yenye kunyooka zaidi ni ile fupi na nyepesi. Mathalani: Hakika vipimo vyote katika Risale-i Nur kati ya njia ya imani na ukafiri vinabainisha kwa kukata shauri kwamba njia ya imani na tawhidi ni fupi yenye kusibu, nyepesi na yenye msimamo zaidi. Ama njia za ukafiri na kukanusha ni ndefu mno na zenye matatizo na hatari. Hapana shaka ulimwengu huu ambao unaendeshwa katika njia yenye kunyooka na hekima – nayo ni njia fupi na nyepesi zaidi katika kila kitu – haiwezekani ndani yake kuwemo hakika ya ushirikina na ukafiri. Wakati hakika za imani na tawhidi ni wajibu na lazima katika ulimwengu huu kama ulazima wa kuwemo jua.

Vilevile hakika njia nyepesi mno katika tabia za kibinadamu, zenye kufaa, fupi, na salama zaidi ni katika njia iliyo nyooka na katika msimamo.

Mathalani:

Kama nguvu ya akili ikikosa mpaka wa katikati, nayo ni hekima na msimamo, ambayo ni mwepesi na wenye manufaa, huanguka katika mapungufu na kupitiliza viwango katika mvurugiko wenye kudhuru na upumbavu wenye balaa, na kuteseka na maangamivu katika njia zake ndefu. Kama nguvu ya ghadhabu haikupita katika njia ya ushujaa ambayo ndio mpaka wa msimamo ulio nyooka, huporomoka katika kupitiliza viwango katika jeuri yenye madhara makubwa na dhulma mbaya mno, na katika kupunguza viwango kuangukia katika kiasi kingi cha kujiweka kwenye hofu yenye kudhalilisha na kuumiza, basi kupata mateso ya kimoyo daima hayo yakiwa ni malipo kutokana na makosa waliyoyafanya yaliyowakosesha mpaka wa msimamo ulio nyooka. Na nguvu ya matamanio aliyonayo mwanadamu, ikipoteza njia ya unyofu salama na kujihifadhi, itadondokea kwa kuvuka kiwango katika maovu ambayo yana misiba, na katika kupunguza kiwango hupelekea katika kuzimika, yaani kuzuilika na maonjo na ladha za neema, na hapo kuteseka na machungu ya maradhi hayo ya kimaanawy.

Na kama hivi kwa kupimia yaliyoelezwa, unyofu ndio njia yenye kufaa zaidi nyepesi na fupi zaidi kati ya njia zote zenye kupitwa katika maisha ya mwanadamu ya kibinafsi na kijamii. Mwanadamu anapokosa njia iliyo nyooka basi njia hizo huwa ndefu sana na zenye mabalaa na misiba na madhara mengi.

Kwa maana kwamba

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

ni dua yenye kujumuisha na uja mpana, na pia hiyo ni ishara katika hoja ya tawhidi na somo katika hekima na kufundisha tabia.

Neno la saba: nalo ni صِرَاطَ الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ

Ishara fupi ya hoja iliyomo ni:

Kwanza:

Nani mkusudiwa katika ?

 عَلَيْهِمْ

Aya tukufu inaifasiri:

﴿وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَـئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ Qur’an, 4:69.

kwani inabainisha makundi manne katika sampuli ya mwanadamu waliopata neema ya kupita njia ya unyofu, kwa kuashiria (An-Nabiyyiin) kwa Bwana wao Muhammad (a.s), na kwa (As-Swiddiqin) kwa Abu bakar As-Swiddiq) (r.a), na (As-Shuhdaa) kwa Omar, Othman na Ali. Aya tukufu inaelezea ghaibu na kubainisha mng’aro wa kimuujiza kwamba wanaokuja baada ya mtume (s.a.w), ni As-Swiddiq kisha Omar kisha Othmani kisha Ali. Mungu awaridhie wote, watakuwa makhalifa na kufa mashahidi.

Pili:

Makundi haya manne ambayo wao ni wa kweli kuwazidi wote katika sampuli ya wanadamu na wenye tabia iliyo nyooka zaidi na wenye hadhi ya juu zaidi, wamelingania kwa nguvu zote walizopewa na kwa kiasi kisichohesabika katika hoja, miujiza, karama, dalili na mafunuo; wamelingania hakika ya tawhidi, na habari zao wamezisadikisha aghalabu ya wanadamu tangu Bwana wetu Adamu (a.s). Hapana shaka kwamba hakika hiyo ni hakika ya kukata shauri kama kuthibiti kwa jua, kwa hiyo kuafikiana kwa kundi hili kubwa katika wabora wa wanadamu wote katika waliodhihirisha ukweli wao na uadilifu wao kwa mamia ya maelfu ya miujiza na hoja ambazo zisizo na mipaka, na kukubaliana kwao wote katika maswala ya kiwajibu kama tawhidi na kupasa kwa uwepo wa muumba, ni hoja ya nguvu inaondosha kila shaka. Naam, hakika tukufu ambayo yameamini makundi hayo manne yaliyoelezwa ambayo yanawakilisha sampuli ya watu wanyoofu zaidi ya mwanadamu ambaye ndiye matokeo muhimu ya kuumbwa kwa ulimwengu na khalifa wa ardhi, na ndiye mwenye sifa jumuishi zaidi ya viumbe hai kwa maandalizi na mwenye hadhi ya juu zaidi, bali ni viongozi wao wa kweli zaidi wenye kusadikisha, na viongozi wao katika makamilifu. Hawa wameeleza kwa pamoja na kuafikiana kuhusu hakika hiyo ambayo wameiamini na kuitakidi itikadi ya kuamua kwa haki ya yakini na kwa elimu ya yakini na kwa dhati ya yakini, na wametulia nayo utulivu usiotetereka wakiudhihirishia ulimwengu na vilivyomo vyote kwa dalili. Je hawi yule anayekanusha na wala hatambui hakika hii tukufu kuwa anatenda jinai, na kustahiki adhabu ya kudumu.?!

Neno la nane: Nalo ni غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ

Hii ni ishara fupi ya hoja iliyomo humo:

Hakika historia ya mwanadamu na vitabu vitakatifu, vinaeleza kwa kuafikiana maelezo ya kukata shauri na kwa uwazi kamili, kwa kuegemea katika tawaturi na matukio ya jumla yaliyothibiti na maarifa ya mwanadamu na mambo yenye kushuhudiwa na mwanadamu, kwamba kujibiwa maombi ya Manabii (a.s) nao ni watu wa njia iliyo nyooka kwa maombi ya ghaibu zaidi ya kawaida katika maelfu ya matukio, na kutimizwa maombi yao hasa, na kuteremka ghadhabu na misiba ya mbinguni kwa maadui wao makafiri katika mamia ya matukio, inajulisha bila shaka yoyote kwamba ulimwengu huu na kwa sampuli ya mwanadamu ambaye yumo ndani yake, vina mola mwenye kuhukumu mwadilifu mwema mkarimu mshindi asiyeshindwa mwendeshaji wa mambo mtiishaji, amewapa ushindi wenye kuungwa mkono na uokovu wa ajabu manabii wema wengi mfano wa Nuhu, Ibrahim, Musa, Hud na Swaleh (a.s) katika matukio mapana ya kihistoria, na wakati huohuo akateremsha duniani misiba ya mbinguni yenye kutisha juu ya watu madhalimu makafiri mfano wa Thamud, Ad, na Firauni mkabala na kuasi kwao mitume.

Naam, hakika mirengo miwili mikubwa imepita kwa mwanadamu ikipingana tangu zama za Adamu (a.s).

Kwanza:

Ni watu wa utume na wema na imani ambao wamepata neema na furaha ya makao mawili kwa kupita kwao njia iliyonyooka, kwa mwenendo wao mwema matendo yao na shughuli zao vikawiana pamoja na uzuri wa hakika wa ulimwengu nidhamu yake kupangika kwake na ukamilifu wake, kwa ajili hiyo wakapata huruma za bwana mlezi wa walimwengu, na furaha za makao mawili, na wakawa ni sababu ya kumwinua mwanadamu kwenda katika ngazi za malaika bali hata za juu kuliko hizo, wakavuna na kuwavunisha wengine pepo ya kimaanawy hata katika dunia, pamoja na furaha ya kudumu huko akhera, yote hayo kwa siri ya hakika za imani.

Mrengo wa pili:

Ni wale ambao wamepotea njia ya sawa kwa kupitiliza na kupunguza, wameifanya akilia ni nyenzo ya adhabu na zana ya kukusanyia maumivu, hivyo wakauporomosha ubinadamu katika ngazi za chini za upotevu zaidi kuliko wanyama, wakastahiki ghadhabu za kiungu yakawashukia mapigo ya masaibu ikiwa ni malipo ya dhulma yao waliyoitenda duniani. Zaidi ya hayo, kwa upotevu waliokuwa nao na kwa akili inayofungamana na vilivyomo, wamejaalia ulimwengu kuwa ni mahali pa huzuni, machungu na matanga ya jumla, na machinjio ya wenye uhai, wanageuka geuka katika shida za kutoweka na utengano, na machuno machafu na fujo zimekwenda mbali katika anga. Kwa hiyo, roho ya mpotevu imejifunga na moyo wake kwa jahannam ya kimaanawy duniani, na kuwa mwenye kustahiki adhabu iumizayo huko akhera.

Vilevile hakika aya tukufu ambayo imo mwishoni mwa sura Al-Fatiha:

الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ

inabainisha mirengo hii mikubwa miwili.

Chimbuko la vipimo vyote vilivyoelezwa katika Risale-i Nur na msingi wake na mwongozo wake ni aya hii tukufu. Na kwa kuwa Risale-i Nur imeifasiri aya hii tukufu kwa mamia ya vipimo vyake. Hivyo basi tunaelekeza katika hizo Risala hali ya kuwa tunatosheka na ishara hii.

Neno latisa : nalo ni آمين

Ishara fupi sana ni:

Kwa kuwa (Nuun) ambayo imo katika

نَعْبُدُ  

na

نَسْتَعِينُ  

inatubainishia makundi makubwa matatu, na hasa kundi lenye kupwekesha katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu na hasa mamilioni ya wenye kuswali ambao wakati huo wanatekeleza swala, na kutufanya tuwe sehemu ya safu zao, ikitufungulia njia iliyonyooka mbele yetu ili tuvune sehemu ya maombi yao, na ili tupate kusadikisha kwao kwetu kwa kutamka kwao mithili ya tunavyotamka sisi, na ili tupate aina katika shufaa yao, basi nasi vilevile kwa kusema kwetu: (Amin) tunatia nguvu maombi ya hao wapwekeshaji wenye kuswali, na tunasadikisha dua zao, na tunataraji kwa Neno (Amin) Allah (s.w) aitikie maombi yao, hali ya kugeuza uja wetu mdogo na maombi yetu madogo kwenda katika uja wa jumla, dua ya jumla na madai ya jumla mbele ya Rububiyya ya jumla yenye kuenea. Kwa maana kwamba neno (Amin) hufanya kuvuna ujumla mpana bali yaweza kuwa sawa na mamilioni ya (Amin) kwa siri ya udugu wa kiimani na umoja wa Kiislamu na kwa kupitia kwenye Radio za kimaanawy na muungano wa umoja wa kundi linalovuka mamilioni ya wenye kuswali, waliojipanga katika swala katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu.

Na kama hivi mtu wa kawaida anapochukua kitu kwa kiasi cha kokwa. basi mtu kamili ambaye kiroho amepanda juu anachukua fungu kama Mtende. Kila mmoja kulingana na ngazi yake. Lini ambaye bado hajapanda. Haitakikani kwake kukumbuka maana haya kwa makusudi wakati wa kusoma kwake Surat Al-Fatiha ili asipoteze utulivu wake na umakini wake, pindi anapopanda katika makamo hayo hakika maana hayo yatadhihiri yenyewe. (Mtunzi)

الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

﴿سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَاۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

Hakika tumemuuliza Ustadhi wetu ufafanuzi wa neno (kwa makusudi) lililopo katika maelezo haya ya pembeni na tumeandika chini yake aliyoyaeleza kama  alivyosema:

Kwa jina la wanafunzi wa Nur

Katika shule  ya Yusuf ya Tatu / Jaylan

Naona ni kuwa inayumkinika kutafakari kwa maana mapana ya juu ya tashahudi na Surat Al-Fatiha, lakini hayakusudiwi maana hayo kwa kukusudiwa, bali ni kwa sura ya kufuatia, kwani yanayosababisha uhadhiri wa moyo kupata kughafilika ni yale maelezo yake. Wakati ambapo maana yake ya ujumla hutokomeza mghafala na kunawirisha ibada na Munajati na kuung’arisha. Basi hudhihirisha kikamilifu thamani za hali ya juu za swala Al-Fatiha na Tashahhudi.

Ama lenye kutakiwa kutokana na (kutokushughulika kwa makusudi) kulikopatikana katika sehemu ya pili ni kuwa kushughulika na maelezo ya maana hayo hasa wakati mwingine huweza kusahaulisha swala na wakati mwingine huharibu umakini wa moyo na kuwa hadhiri. Na kama si hivyo hakika mimi ninahisi faida zake kubwa ikiwa kutafakari ni kwa hali ya kufuatia na kwa namna ya ufupi. (Mtunzi)

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.