Sehemu Ya Tatu

Somo hili lilitolewa katika shule ya tatu ya Yusuf

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

وبه نستعين

Utangulizi

Sehemu ya pili imeandikwa kwa amri ya kimaanawy iliyotoka katika sura (Al-Fatiha) ambayo imo katika swala na kwa miminiko la nuru ya neno la shahada:

Ash hadu an la ilaha illa Allah.

Na kadhalika sehemu hii nimelazimika kuiandika kwa msukumo – unaotokana na sababu tatu sina idhini ya kuzibainisha kwa sasa – kwa tanbihi ya kimaanawy yenye kupatikana katika sentensi: Ash hadu anna Muhammada Rasulullah, na kwa kheri ya nuru ya aya tukufu ambayo imo mwishoni mwa surat Al-Fat’hi na ambayo imedhihirisha miujiza mitano ya ghaibu, nayo ni kauli yake Allah (s.w):

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا ۞ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُم

Mpaka mwisho wa aya…

Ama maelezo ya sehemu hii na ufafanuzi wake na hoja zake zenye kuegemezwa na dalili, basi nazielekeza katika Risala za (Al-Mu’jizaat Al-Ah’madiyyah) iliyochapishwa ikiwa katika jumla ya (Dhu al-Fiqar) na katika Al-Hizbul An-Nury ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Itaashiriwa kwa ishara tatu fupi sana. Katika ishara ya pili na ya tatu itaandikwa mfano wa tafsiri ya fungu la kwanza linalo husu shahada (Muhammad Rasulu Allah) katika Risala ndogo iliyoandikwa hapa, na iliyochotwa kutokana na ufupi wa ufupi wa Al-Hizbul An-Nury Al-Araby, na ambayo ni uradi wangu wa kudumu na kutafakari kwa Kiarabu pamoja na kalimatul tawhidi ambalo ninalikariri katika dhikiri.

Ishara ya kwanza

Muhammad (s.a.w) ambaye amepokea mionekano ya Rububiyya ya Bwana mlezi wa walimwengu wote, na umilele wa uungu wake, na neema zake zenye kuenea na ambazo hazihesabiki, amezipokea kwa uja wa jumla na kumtambulisha mola wake mlezi mtukufu. Nabii huyu mtukufu ni jambo la dharura kama dharura ya jua kwa ulimwengu huu, kwani yeye ni ustadhi mkuu wa wanadamu, na ni Nabii wao mkuu (s.a.w), na fahari ya ulimwengu, aliyekusudiwa kwa kuambiwa:

“لَوْلَاكَ لَوْلَاكَ لَمَا خَلَقْتُ الأَفْلَاكَ”

Wanazuoni wamelizungumzia hili kwa maana na kwa mjengo. Na huenda kauli ya Ali Al-Qaary ndio ya katikati kati ya wenye kuthibitisha na wenye kukanusha hilo. Ambapo anasema: Hakika hilo ni sahihi kwa maana japo ikiwa ni dhaifu ki mjengo (Sharhu Al-Shifaa 1/26).

Kama ilivyo hakika yake (Yaani hakika ya Muhammad (s.a.w)) ndiyo sababu ya kuumbwa kwa ulimwengu, matokeo yake na tunda lake lililo kamili zaidi, na vilevile hukamilika kwa hakika hiyo na kwa ujumbe wa Muhammad makamilifu ya kihakika ya viumbe wote, kwa kuwa huwa ni vioo vyenye kudumu kwa mzuri mtukufu wa milele zikiakisi midhihirisho ya sifa zake tukufu, na athari zake za thamani zenye kupewa majukumu mbele ya vitendo vyake vyenye hekima (s.w), na barua zake za fasaha zenye kutumwa kutoka hadhara tukufu kabisa na kuwa yenye kubeba ulimwengu wenye kubaki, wenye kuzalisha makao ya furaha ya milele na makazi ya akhera ya kudumu ambayo wenye utambuzi wote wanashauku nayo, na mfano wa hayo katika mifano ambayo inatimia kwa hakika ya Muhammad (s.w) na ujumbe wake. Kwa ajili hiyo kama unavyo shuhudia huu ulimwengu kwa ushahidi wa kukata shauri, na kwa nguvu na uthabiti mno juu ya utume wake (s.w), na kadhalika wanadamu wote bali wote wenye utambuzi na mbele yao ni ulimwengu wa Kiislamu, wote wanashuhudia juu ya ambayo ujumbe wa Muhammad umeyabashiria na hakika ya Muhammad ubashiri wenye nguvu wenye kukata shauri, hayo ndiyo maisha ya kudumu ambayo wanadamu wanayaomba kwa ashiki ya kudumu na shauku yenye kuambatana kila wakati, wanayaomba kwa nguvu zote za hakika yao jumuishi na kwa ndimi za maandalizi yao yote, na kwa ndimi za ibada zote, unyenyekevu na tawassuli zenye kupelekwa kwa mola mweza, huomba uhai wa kubakia milele, kuokoka na kukosekana, mchezo na kunyongwa kwa milele na kutoweka kabisa ambako ni kwenye kutisha zaidi na kuumiza zaidi kuliko Jahannam. Kama wanadamu wanavyo shuhudia hili kwamba yeye Muhammad (s.a.w) ndiye fahari ya wanadamu na bora wa viumbe wote, vivyo hivyo mfano wa mema yote na kheri zote ambazo wanavuna kila siku waumini mia tatu na hamsini milioni kila zama, kuingia katika daftari la mema yake (s.a.w) kwa mujibu wa kanuni ya (Sababu kama mtendaji), na haiba hiyo ya Muhammad ya kipekee kupata makamo ya juu yenye kupata uja wa jumla na kheri za kiungu kwa kiasi cha ibada ya mamia ya mamilioni bali mabilioni miongoni mwa wenye kuabudu wema, ni ushahidi wenye nguvu sana juu ya utume wake (s.a.w).

Ishara ya pili

Kifungu kifuatacho ambacho ninakizingatia sana ni katika nyiradi zangu, ni kinaashiria zaidi ya shahidi ishirini juu ya utume wa Muhammad (s.a.w), tunafupisha yaliomo kwa muhtasari. Nacho ni:

(Muhammad mtume wa Allah mkweli wa ahadi mwaminifu kwa ushahidi wa kudhihiri kwake kwa mkupuo mmoja pamoja nakutokujua kwake kusoma, amekuja na dini kamilifu mno ya Kiislamu na sharia, na imani yenye nguvu mno, itikadi na ibada, na ulinganio wa juu mno na munaajati na maombi, na ufikishaji muhimu mno na umadhubuti timamu mno wa ajabu wenye kuleta matunda yasiyo namfano].

Vifungu hivi vilivyotengwa kati ya mabano yamepatikana katika Matamko kwa lugha ya Kiarabu.

Moja ya shahidi hizo ni:

Hoja ya utume unaochimbuka kutokana na hali kumi na moja katika hali zake (s.a.w).

Naam, yeye pamoja na kuwa hajui kusoma hakujifunza kusoma na kuandika, amekuja na dini iliyowaingiza wenye akili wa karne kumi na nne na wanafalsafa wake katika tahayari, kupendezwa na mshangao, na amezivuka dini za mbinguni na amedhihirisha kwa mkupuo mmoja bila ya kuwa na majaribio yaliyotangulia, na hii ni hali isiyo na mfano wake.

Na vilevile Uislamu uliochimbuka kutokana na kauli zake, matendo yake na hali zake, na kuongoza kwake wanadamu mia tatu na hamsini milioni wakati wote, hali ya kulea roho zao, kutakasa nafsi zao, kunawirisha akili zao na kuwapeleka katika kupanda kimaanawy, na hii ni hali haina mfano wake.

Na vilevile ameleta sheria angavu kubwa kiasi ambacho ametawala kwa kanuni zake za uadilifu humsi ya wanadamu kipindi chote cha karne kumi na nne utawala ambao umeuhakikishia kunyanyuka kimaada na kimaanawy na hii ni hali isiyokua na mfano wake.

Na vilevile kudhihiri kwake kwa imani yenye kujikita madhubuti na itikadi isiyotetereka kwa kiasi kwamba watu wa hakika wanapata ilhamu kutoka kwake kila wakati na kusadikisha kwa maafikiano kwamba yeye yupo katika daraja ya juu mno na ngazi tukufu zaidi, ukiachia mbali kutoleta walio dhidi yake na maadui wake na wapinzani wake wakati huo – utata wowote – wala wasiwasi wala shaka katu, jambo lenye kubanisha kwa uwazi kwamba hana mfano wake katika nguvu ya imani pia hakuna mwenza wa imani yake ya juu ya kiujumla.

Na vivyo hivyo amedhihirisha uja na ibada kubwa kiasi ameunganisha pamoja msingi na ukomo, bila ya kumwiga yeyote hali ya kuzingatia siri madhubuti za ibada, na kuzichunga hata katika nyakati za misukosuko mikubwa na amezitekeleza katika sura kamilifu mno na nzuri zaidi. Na hii ni hali isiyo na mfano wake.

Na vivyo hivyo amenyenyekea kwa mola wake mkarimu na kuomba maombi ya upole laini kiasi hakufikia yeyote ngazi ya maombi hayo na munajaati hadi zama hizi pamoja na kukutana kwa fikira mbali mbali.

Kwa mfano:

Amejaalia majina elfu na moja katika majina ya mwenyezi mungu kuwa yenye kuombea dua yake katika munajaati ya (Al-Jawashan al- Kabiir) akamsifu muumba wake mtukufu wasifu wa kupendeza unaofaa kwa makamo yake, na akamtambulisha utambulisho usiokuwa na mfano kabisa.

Na kama hivi kutofikia yeyote alipofikia katika kumjua Allah (s.w), ni hali isiyo na mfano wake katu.

Na vilevile yeye amewalingania watu katika dini ulinganifu ulio jaa uaminifu na amefikisha ujumbe wake kwa ushujaa na uthubutu kwa namna ambayo upinzani wa watu wake na ami yake na madola makubwa ulimwenguni na wafuasi wa dini zilizotangulia na uadui wao, haikumpa hofu wala kurudi nyuma kabisa, bali aliwapa changamoto walimwengu na kuwashinda wote, na hii ni hali isiyo na mithili yake.

Na kama hivi hakika jumla ya hali hizi nane za ajabu ambazo hazina mfano wake ni ushahidi katika ukomo wa nguvu juu ya ukweli wake mtume (s.a.w) na kuthibiti kwa malinganio yake. Na hizo ni hali ambazo zinadhihirisha kiasi cha kutulia kwake na ukomo wa bidii yake, kisi kikubwa cha uhakika wake, ukamilifu wa ukweli wake na uadilifu wake.

Kwa hiyo ulimwengu wa Kiislamu unampongeza na kumbariki Nabii huyu mtukufu s.a.w kwa kusema katika kila kikao cha tashahudi katika swala kila siku na kwa mamilioni ya ndimi: “As-Salaamu alayka ayyuha An-Nabiyyu warahmatullahi wabarakatuhu” kwa kuwasilisha utii wake kwa jukumu la unabii, na kumsadikisha katika ubashiri wake wa furaha ya milele aliyokuja nao, unampokea kwa utambuzi wa wema mkubwa na shukurani yenye kuenea mkabala na kufungua njia iliyonyooka kuelekea katika maisha ya kudumu ambayo wanadamu wanaitafuta kwa ashiki iliyojificha, yenye kina, na shauku ya kimaumbile kubwa na kwa maandalizi yenye nguvu mno, kwa kusema: “As-Salaamu alayka ay-Yuuha An-Nabiyyu” ukielezea kwa tamko hilo juu ya ziara ya kimaanawy kwake (s.a.w) na kukutana naye, na kumkaribisha na kumpongeza yeye kwa jina la mia tatu na hamsini milioni bali mabilioni ya waumini.

Ushahidi wa pili katika shahidi ishirini za jumla na ambazo zinakusanya shahidi nyingi zaidi nao ni:

[Na kwa ushahidi wa hakika za imani zote katika kumsadikisha]

Yaani hakika za nguzo sita za imani na kuthibiti kwake na ukweli wake na kusibu kwake vinashuhudia ushahidi wa kukata shauri juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) na juu ya ukweli wake na kusibu kwake, kwa sababu haiba ya kimaanawy ya maisha ya utume wake, na msingi wa malinganio yake yote, na hakika ya unabii wake, hakika ni hizo nguzo sita, na kwa hiyo dalili zote zenye kujulisha juu ya kuthibiti kwa nguzo hizo zinajulisha kwamba utume wa Muhammad (s.a.w) ni kweli na yeye ni mkweli mwenye kusadikishwa, kama risala ya matunda ilivyobainisha (Matunda ya imani) na nyongeza za (Neno la kumi) nguzo nyingine za imani kujulisha juu ya kuthibiti kwa Akhera, hali kadhalika kila nguzo kati ya hizo pamoja na hoja zake zote zinathibitisha Utume wake (s.a.w).

Ushahidi wa jumla wa tatu ambao unakusanya maelfu ya shahidi

(Na kwa kushuhudia kwa dhati yake (a.s) kwa maelfu ya miujiza yake na makamilifu yake na tabia zake njema)

Yaani yeye ni kama jua ni dalili kwa nafsi yake. Kama risala ya ajabu ilivyo thibitisha, risala ya (Miujiza ya Muhammad) rehema na amani zimwendee mwenye miujiza hiyo, katika zaidi ya miujiza mia tatu kwa mapokezi sahihi, vilevile kupasuka kwa mwezi pande mbili kwa kidole katika kiganja chake chenye baraka (s.a.w) kama aya inavyoweka wazi:

وَانشَقَّ الْقَمَرُ Qur’an, 54:1.

Vilevile kutiririka maji kutoka katika vidole vyake vyenye baraka na kufoka kama yanavyofoka kutoka katika chemchemu tano, na kunywa jeshi kamili na kushuhudia kwao hilo, kulikonakiliwa kwetu kwa mapokezi sahihi ya tawatur, ukiachilia mbali kukariri kwa tukio hili la ajabu mara mbili katika maeneo mengine. Na vilevile kurusha kwake gao la mchanga kwa kiganja hichohicho kwa jeshi la adui linaloshambulia na kuingia kwa mchanga kwenye jicho la kila mmoja wao na kushindwa kwao wakati wa kushambulia kama uwazi wa aya tukufu:

وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ Qur’an, 8:17.

vilevile jiwe kusoma tasbihi kwenye kiganja hichohicho, tasbihi wazi ya bayana ambayo imepokelewa kwa mapokezi sahihi, na mfano wa hiyo miongoni mwa miujiza ambayo imedhihiri kutoka katika mkono wake uliobarikiwa na sehemu yake imesimuliwa katika vitabu vya sira na historia kwa mapokeo yaliyokuja kwa tawatur ya kukata shauri na ambayo inazidi mamia bali inafika elfu kwa wanazuoni wahakiki. Vilevile maafikiano ya mawalii na maadui kuwa yeye yuko katika kilele cha tabia njema

Hata Sayyidina Ali (r.a) anasema, akiimarishwa kwa ushujaa wa hali ya juu: tukihemewa na jambo – kwenye vita – tulikuwa tukitafuta himaya kwa mtume wa Allah (s.w) na kujilinda kwake. Na historia zimenakili kwamba maadui wake vilevile wameshuhudia kwamba yeye (s.a.w) alikuwa katika kilele katika kila jambo tukufu kama ilivyo katika Ushujaa. (Mtunzi)

na kuafikiana watu wote wa tahakiki wenye kupita njia yake kwa kufuatilia nyayo zake wenye kufikia makamilifu na wenye kutambua hakika kwa dhati ya yakini, na kusadikisha kwao wote kwa haki ya yakini, kwamba makamilifu ya Muhammad ni katika kilele cha daraja, kama zinavyojulisha hilo kheri za ulimwengu wa Kiislamu, zenye kutokana na dini yake (s.a.w), na hakika za dini tukufu ya uislamu. Hapana shaka kwamba mtume huyo mtukufu anashuhudia ushahidi mpana wa jumla wenye kuangazia juu ya utume wake yeye mwenyewe.

Ushahidi wa nne ambao unabeba shahidi nyingi zenye nguvu:

[Na kwa ushahidi wa Qur’an kwa hakika na hoja zisizo na mpaka]

Yaani Qur’an yenye muujiza wa bayana inashuhudia kwa hakika zake na hoja zake, ambazo hazihesabiki juu ya Utume na ukweli wake (s.a.w).

Naam, Qur’an ambayo ni muujiza mkubwa kwa pande arubaini (Kama ilivyothibitisha Risala ya Muujiza wa Qur’an iliyochapishwa katika jumla ya machapisho ya Dhu al-Fiqar), na ambayo imetia nuru karne kumi na nne, na ambayo imeongoza nusu ya kanuni zake zilizonyooka ambazo hazibadiliki, na ambayo imetoa changamoto na bado inaendelea kutoa changamoto kwa wapinzani wote hata hakuthubutu kuipinga yeyote hadi sasa japo kwa sura moja. Bali pande zake sita ni za nuru haziingii shaka kabisa, na makamo sita makubwa yanasadikisha juu ya ukweli na uadilifu wake, na inaegemea hakika sita zisizotetereka, kama ilivyothibitishwa katika risala ya (Al-Ayatu al-Kubra), na ambacho kinasomwa wakati wote kwa ndimi za mamia ya mamilioni na kwa kila shauku na heshima, na ambayo inaandikwa katika nyoyo za mamilioni ya mahafidhi kila dakika uandishi mtukufu, na ambacho kinatona kutokana na shahidi zake shahidi zote na imani ya ulimwengu wa Kiislamu, na inanasibiana kutoka katika chimbuko lake elimu zote za kimani na Kiislamu.

Kama inavyosadikisha vitabu vya mbinguni vilivyotangulia, inapata usadikishaji wa kimaanawy vilevile kutoka katika vitabu vyote na suhuf za mbinguni. Basi Qur’an hii tukufu pamoja na hakika zake zote, na hoja zake zinazothibitisha ukweli wake na uadilifu wake, inashuhudia juu ya ukweli wake na utume wake.

Ushahidi wa jumla wa tano, sita, saba na nane:

[Na kwa kushuhudia Al-Jawshanu kwa utakatifu wa ishara yake, na Risale-i Nur kwa nguvu ya dalili zake, na zenye kupita kwa tawatur ya Irhasat (miujiza yake kabla ya utume), na kupokelewa kwa kusadikishwa na maelfu ya matukio yake].

Yaani kama ilivyo (Al-Jawshan al-Kabiir) ambayo inajumuisha majina elfu moja na moja katika majina ya kiungu kwa uwazi na kwa kuashiria, na inatokana – upande mmoja – kutoka katika Qur’an tukufu, huu munajati wa mtume wa ajabu ambao unapita munaajati wa wajuzi wote wa Allah ambao wamepanda katika ngazi za kumjua Allah (s.w), na kushika nafasi za juu, ameileta Jibril (a.s) ikiwa ni wahay katika vita akisema: (Vua nguo ya vita (Al-Jawshan) na soma Jawshan hii). Hakika ambazo zimebebwa katika munajati huu na sifa zenye kuelekezwa ndani yake kwa mola wake mtukufu kwa dhati yake inashuhudia ushahidi wa kweli juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na juu ya Utume wake.

Vilevile Risale-i Nur inayotona kutoka katika Qur’an tukufu na yenye kuchotwa – kwa upande mwingine – kutokana na (Al-Jawashan al-Kabiir) ni hoja moja juu ya utume wa Muhammad kwa sehemu zake zenye kufikia risala mia moja na thelathini na hii kwa uthibitisho wake wa kiakili na kimantiki hakika zote za utume wake (s.a.w), bali kuzifundisha na kuzifahamisha kwa wepesi jambo ambalo falsafa inashindwa na kuyaelezea mambo ambayo yapo mbali sana na akili na kuyaonesha kuwa ni maswala yenye kukubalika na kuingia akilini kana kwamba yanaonekana. Risala hizi zinazofikia mia moja na thelathini zinashuhudia ushahidi wa ujumla juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na juu ya utume wake.

Halikadhalika muda uliopita ni ushahidi wa kiujumla juu ya utume wake, kwani Irhasat ambazo ni mambo yaliyo furutu ada yametangulia kipindi cha utume na zinahesabiwa ni katika miujiza ya mtume (s.a.w) ambaye atakuja, matukio mengi yameelezwa katika vitabu vya sira na historia maelezo ya tawatur kabisa. Basi irhasat hizi zinashuhudia ushahidi wa kweli juu ya utume wake. Na hizi irhasat ni aina nyingi sehemu yake itabainishwa katika ushahidi ujao, sehemu yake nyingine imeelezwa katika mkusanyiko wa (Dhu al-Fiqar) na vitabu vya historia vimenakili kwa usahihi.

Kwa mfano:

Kutuma ndege ili kulirushia vijiwe jeshi la Abraha ambalo limekuja kwa ajili ya kuvunja Al-Kaaba vijiwe vya moto kabla ya kuzaliwa kwake (s.a.w), na kudondoka masanamu kwenye Al-Kaaba usiku wa mazazi yenye baraka, na kuvunjika vibaraza vya kisra, na kuzimika kwa moto wa majusi ambao ulikuwa unawaka tangu miaka elfu, na mtume (s.a.w) kufunikwa na kiwingu kama alivyosimulia Bahira padri na Halima As-Saadiyya. Na mfano wa hayo katika matukio mengi ambayo yameelezea utume wake (s.a.w) kabla ya kupewa kwake utume.

Na vivyo hivyo mustakabali, yaani matukio ambayo yametokea baada ya kutawafu kwake (s.a.w), aliyoyaelezea nayo ni mengi sana na aina nyingi mno, kati ya hayo: Kuelezea kwake kwa ghaibu kunakohusu jamaa na masahaba wema, na ushindi wa Kiislamu, na imeshathibitishwa katika Risala ya Al-Muujizaat Al-Ahmadiyya (Iliyochapishwa ikiwa ni sehemu ya mkusanyiko wa Dhu al-Fiqar) kwa mapokezi sahihi matukio manane yametokea kama alivyoelezea. Mfano: Kufa shahidi Sayyidina Uthumani (r.a) wakati akisoma msahafu mtukufu, na kufa shahidi Sayyidina Husein ra. huko karbala, na kufungua nchi za Shamu, Uajemi na Istanbul, na kusimama kwa dola la Al-abbasiyya na kuanguka kwake na kuteketea kwake kwa mkono wa Jenkiz Khan na Holako, na mfano wa hayo katika miujiza yake katika kuelezea kwake ghaibu ambako kumedhihiri katika matukio manane, katika yaliyo nakiliwa kwetu kwa usahihi kwa kuegemea vitabu vya sira na historia ambavyo nimevieleza kwa ufafanuzi. Basi maelezo haya ya ghaibu na baki ya aina yake ambayo yanajulisha ukweli wake (s.a.w) na matukio ya mustakabali mengi sana yanajulisha ukweli wake (s.a.w), yaani mustakabali unashuhudia ushahidi wenye nguvu wa kijumla juu ya Utume wa Muhammad (s.a.w).

Ushahidi wa tisa, kumi, kumi na moja, na kumi na mbili ambao unaashiria:

[Na kwa ushahidi wa ali zake kwa nguvu ya yakini yao, katika kumsadikisha kwa daraja ya haki ya yakini, na masahaba kwa ukamilifu wa imani yao katika kumsadikisha kwa daraja ya dhati ya yakini, na wateule kwa nguvu ya uhakiki wao katika kusadikisha kwao kwa daraja ya elimu ya yakini, na maqutubu kwa kulingana sawa kwao juu ya Utume wake kwa kufunuliwa na maono kwa yakini]

Basi kutokea katika ushahidi ya kiujumla ambao unashuhudia kwa ukweli juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na uadilifu wake:

Ushahidi wa tisa:

Nao ni ushahidi wa jamaa zake Muhammad (s.a.w) ambao wamepata ngazi ya (wanazuoni wa Umma wangu ni kama manabii wa wana wa Izraili) na mabao wanalingana na jamaa wa Ibrahimu a.s, katika swala za tashahudi, nao ni mawalii wakubwa na maimamu kumi na mbili (r.a), na anawatangulia wote hao imamu Ali, Hasan na Husein Mungu awaridhie, na sheikh Al-Kaylany, Ahmad Al-Rifaiy, Ahmad Al-Badawy, Ibrahim Ad-Dusuqy, Abu Al-Hasan Al-Shadhily (Q.S) na mfano wa hao katika maaqtabu na maimamu, wote wanashuhudia na kwa kuafikiana kwa itikadi yao ya yakini na kwa kufunuliwa, maono, karama na mwongozo waliyoidhihirisha katika umma, hivyo wanasadikisha kwa imani yao madhubuti Utume wa Muhammad (s.a.w) na ukweli wa mtume mtukufu.

Ushahidi wa kumi:

Ni ushahidi wa maswahaba watukufu ambao ni bora wa watu wenye daraja ya juu zaidi baada ya manabii (a.s), na ambao wameuongoza ulimwengu kutokea mashariki hadi magharibi kwa uadilifu na usawa baada ya kunawirika na nuru ya Muhammad (s.a.w) katika kipindi kifupi licha ya kuwa kwao ni mabedui wasiojua kusoma na kuandika. Na kushinda madola makubwa na kuwa ni maustadhi wa mataifa yalioendelea yenye ustaarabu na elimu na siasa, na walimu wao na wanasiasa wenye kuhukumu kwa uadilifu, wakaigeuza karne hiyo kuwa karne bora kabisa na enzi za furaha. Masahaba hawa wema baada ya kuchunguza sana kila hali katika hali za Muhammad (s.a.w) na kushuhudia kwao kwa macho yao nguvu ya miujiza yake mingi, waliacha uadui wao uliotangulia, na wakaikataa njia ya mababu zao wakajitolea kwa nafsi na kilicho ghali kujitolea kwa heshima na hadhi na kujiunga chini ya bendera ya Uislamu, kama Khalid bin Waliid, Ikrima bin Abi Jahali na mfano wa hao katika walioacha wazazi wao na kabila lao. Hakika imani ya masahaba hawa watukufu inayofikia daraja ya dhati ya yakini, ni ushahidi wa kweli wa jumla juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na kuwa utume wake ni wa haki.

Ushahidi wa kumi na moja:

Nao ni ushahidi wa maelfu wa watu wa uhakiki, yaani ushahidi wa mujtahidina na maimamu wanazuoni wakubwa na wanazuoni wahakiki ambao wote hao wanaitwa: Wateule na masiddikina, na wanafalsafa hodari mfano wa Ibn sina na Ibn Rushd ambao wameamini imani ya kimantiki na kiakili, pamoja na kutofautiana maslaki ya kila mmoja na mwingine kati yao, wakiegemea maelfu ya hoja zenye nguvu na dalili madhubuti, mpaka walifika daraja ya elimu ya yakini, hakika imani ya watu wote hawa kumwamini Muhammad (s.a.w) na utume wake na ukweli wake na kusibu kwake ni ushahidi wa jumla kwa kiasi ambacho haiwezekani kuupinga ila mtu ambaye mwenye busara inayolingana sawa na busara zao.

Na Risale-i Nur ni mojawapo kati ya mashahidi hao wa kweli katika zama hizi, ambao hawahesabiki, lakini hoja ilipoanguka katika mikono ya wakanushaji na hawakuwa na pakugeukia, walijaribu kuituliza kwa mahakama kwa kuwadanganya watu wa usalama na vyombo vya sheria.

Ushahidi wa kumi na mbili:

Ni ushahidi wa al-Aqtabu ambao kila mmoja kati yao anajumuisha sehemu muhimu katika umma wa Kiislamu ndani ya duara la somo lake na maelekezo yake, na kwa maelekezo ya ajabu na mwongozo wenye kusibu na karama za wazi wamewapeleka katika kupanda kimaanawy wakiegemea katika maeneo ya hoja mambo waliyoshuhudia na kufunuliwa. Hawa ni watu wa kipekee wa uhakiki na hakika, kwa kufunuliwa kwenye kupanda kwao kiruhani wameshuhudia ukweli wa Muhammad (s.a.w) na ukweli wa utume wake na kwamba yuko kwenye kilele cha ngazi za ukweli, uadilifu na haki. Basi ushahidi wa watu hawa kwa kuafikiana na kuchukuana sawa, juu ya utume wake (s.a.w) ni uthibitisho wenye nguvu kwa kiasi ambacho haiwezekani kuukosoa ila kutoka kwa aliyepata ukamilifu na fadhila sawa na waliyopata watu hawa.

Ushahidi wa kumi na tatu: Ni hoja nne zenye nguvu pana za kiujumla:

[Na kwa ushahidi wa zama zilizopita kwa tawatur ya bishara za makuhani na sauti na watambuzi katika duru za waliopita na kwa kushuhudia kwa bishara za mitume mursalina na Anbiya na kwa ushahidi wao na bishara zao (a.s) kwa utume wa Muhammad (s.a.w) ndani ya vitabu vitakatifu].

Yaliyomo katika fungu hilo kwa ufupi yatafafanuliwa hapa, ama ufafanuzi wake kamili na hoja zake umo mwishoni mwa Risala ya (Al-Muujizat Al-Ahmadiyya) sehemu ya mkusanyo ya Dhu Al-Fiqar)

Na fungu hili lina maana kuwa watu mashuhuri katika zama zilizopita, wakitanguliwa na manabii watukufu (a.s) na watambuzi na makuhani na sauti, wameeleza kwa kuafikiana kuja kwa Muhammad (s.a.w), na kuhusu utume wake, habari ambazo zinaitwa (Irhasat) maelezo hayo yako wazi na yamekaririwa na kutajwa katika vitabu vya historia na sira na hadithi tukufu, kwa mapokeo sahihi na sehemu kati yake ni mutawatir. Risala ya (Al-Muujizatul Al-Ahmadiyyah) imeelezea na kubainisha Irhasat ambazo zina nguvu na zilizothibiti zaidi kati ya maelfu ya hizo, basi tunaelekeza huko kwa ishara ya muhtasari mno.

Ama kuelezea kwa manabii kumetajwa katika (Andiko la kumi na tisa) ishara ishirini zinazohusu utume wa Muhammad (s.a.w) kwa kiasi kinachokaribia kwa uwazi na mamia ya aya zilizomo katika vitabu vya mbinguni kama Taurati, Injili na Zaburi, Husein Al-Jisr kwenye kitabu chake amekusanya ishara mia moja kati hizo zinazobashiri utume wa Muhammad (s.a.w) pamoja na upotoshaji mwingi uliotokea kwenye vitabu hivyo kwa upande wa Wakristo na Mayahudi.

Ama makuhani mbele yao kuna makuhani wawili mashuhuri (Shaq na Satiih) wanaelezea ghaibu kupitia maruhani na majini. Wakaelezea Riwaya sahihi zilizopokelewa kwa tawatur na za wazi hakuna shaka yoyote katika habari hizo kuhusu ujio wa mtume (s.a.w) na kuondosha kwake Dola la Uajemi. Na kudhihiri kwa nabii karibuni huko Hijazi.

Na Kaab bin Luayy ameeleza – ni katika mababu wa Mtume (s.a.w) – na Seif bin dhi Yazin miongoni mwa wafalme wa Yemen na Tubbai miongoni mwa wafalme wa Uhabeshi na mfano wao kati ya watambuzi, mawalii wa zama hizo, wameeleza waziwazi kuhusu utume wa Muhammad (s.a.w) na kuutangaza kwa mashairi. Hata mmoja wa wafalme hao alisema: “Mimi nachagua kumhudumia Muhammad kuliko huu ufalme”. Na mwingine alisema: “Ningemkuta ningekuwa ni bin ami yake” yaani ningekuwa kama Ali (r.a) mwenye kujitole na waziri wake. Imetajwa katika (Andiko la kumi na tisa) habari muhimu na thabiti katika habari hizi. Kwa hali yoyote hawa watambuzi wanashuhudia ushahidi wa kweli wa kiujumla wenye nguvu juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) na juu ya ukweli wake, kama vitabu vya historia na sira vilivyoeleza habari hizi kwa ukunjufu kamili.

Vilevile maruhani, hawaonekani lakini husikika kauli zao na wanaitwa: Hawatifu na wanashuhudia ushahidi wa kweli kama watambuzi na makuhani, juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) kwa uwazi sana.

Na vilevile wengi kati ya waelezaji, bali hata wanyama dhabihu zinazo chinjwa kwenye madhabahu yao kwa ajili a masanamu, na masanamu yenyewe na ushahidi wa makaburi wote hao wameelezea kuhusu unabii wake (s.a.w). Wanashuhudia ushahidi wa kweli juu ya utume wake na haki yake kwa ulimi wa historia.

Ushahidi wa kumi na nne: ushahidi wenye nguvu wa ulimwengu unaashiriwa na kifungu hiki cha Kiarabu:

[Na kwa ushahidi wa viumbe kwa malengo yake na makusudio ya kiungu kwao juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) ambao ni jumuishi, kwa sababu ya uhitaji wa kupatikana kwa malengo ya viumbe na makusudio ya kiungu kutegemea hilo na kuthibiti thamani yake na majukumu yake na kudhihiri kwa uzuri wake na ukamilifu wake na kutimia kwa hukumu ya hakika zake juu ya utume wa Ubinadamu hasa kwa utume wa Muhammad (s.a.w), kwani ndiyo wenye kudhihirisha na uwanja ulio kamili, bila utume huo, viumbe hivi vyenye kukamilisha na kitabu kikubwa chenye maana ya milele ingekuwa ni vumbi lenye kupeperushwa, maana yale yenye kuruka mbali na ukamilifu wake ungedondoka na jambo hilo ni muhali kwa namna mbalimbali]

Risala ya (Ishara kuu) imeeleza yanayohusu fungu hili la Kiarabu yafuatayo:

Ulimwengu huu kama unavyojulisha juu ya fundi wake na mwandishi wake na mtia sura wake ambaye ameupatisha na anayeuendesha na kupangilia na anausarifu kwa kuupa sura kukadiria na kuendesha kana kwamba ni kasri kubwa na kana kwamba ni kitabu kikubwa au kama ni maonesho ya ajabu au kama ni makusanyo makubwa, basi vilevile hakuna namna unahitajia kuwepo kwa atakayeelezea yaliyomo katika kitabu hiki kikubwa maana yake mbalimbali, na anayejua na kujulisha makusudio ya kiungu nyuma ya uumbaji wa ulimwengu, na kubainisha hekima za kiungu, katika mabadiliko yake, na kusomesha matokeo ya michakato yake ya kimajukumu, na kutangaza thamani ya hakika yake na ukamilifu wa viumbe vilivyomo, kufafanua na kujibu maswali ya kutisha na yanayosababisha kutahayari, vilivyomo vinatokea wapi hivi, na hatima ni wapi, na kwa nini havikai hapa bali vinapita na kuondoka haraka? Na kufafanua maana ya kitabu hicho kikubwa na kufasiri hekima za aya zake za kimaumbile. Yaani unahitajia mlinganiaji mkubwa, mwitaji wa kweli, ustadhi wa hakika na mwalimu hodari. Ulimwengu kwa muktadha huu unajulisha na kushuhudia ushahidi wenye nguvu na wa kiujumla juu ya ukweli wa nabii mtukufu (s.a.w), na kusibu kwake, ambaye ndiye mtu bora zaidi aliyetimiza majukumu haya. Na kwa kuwa yeye ni mtume bora na mkweli zaidi aliyetumwa na Bwana mlezi. Basi ulimwengu unashuhudia kwa kusema: Ash hadu ann Muhammadan Rasuulu Al-Lah.

Naam, hakika ya ulimwengu, thamani yake na sifa zake pambanuzi hutimia kwa nuru ambayo amekuja nayo Muhammad (s.a.w) na kwa nuru hiyo hujulikana kazi za vilivyomo na matokeo yake na majukumu yake na thamani yake, na kwa nuru hiyo ulimwengu unazingatiwa kuwa ni maandishi fasaha ya kiungu na Qur’an ya kiungu yenye umbo na maonesho ya athari za kiungu za kutisha. Kwani bila ya nuru yake (s.a.w) ulimwengu ungekuwa ni matanga wenye kutisha na uharibifu wa kuogofya wenye michanganyiko yenye kushabihiana na misukosuko yenye kufuatana unaoangukia kwenye giza la kukosekana, mchezo, na kutoweka.

Kwa msingi wa hakika hii hakika sifa za ulimwengu na makamilifu yake na mabadiliko yake yenye hekima na maana yake ya kudumu milele yanasema kwa nguvu: Nash hadu anna Muhammdan Rasulu Allah.

Ushahidi wa kumi na tano ambao unakusanya ushahidi mwingi: Nayo ni:

Hakika mabadiliko yote, michakato, utulivu, uhai, umauti, na mfano wa hayo miongoni mwa matendo yanayoendelea ulimwenguni hutimia kwa amri itokanayo na nguvu ya dhati takatifu ambayo ni wajibu kuwepo ambayo inasarifu katika ulimwengu huu kuanzia atomu (chembe vumbi ndogo kabisa) hadi katika sayari, basi vinashuhudia matendo ya Rububiyya yake na matendo ya rehema zake juu ya utume wa Muhammad (s.a.w). Fungu lijalo la Kiarabu linaelezea ushahidi huu mtukufu wa hali ya juu:

[Na kwa kushuhudia mwenye viumbe na muumba wake na msarifu wake juu ya utume wa Muhammad (s.a.w), kwa matendo ya rehema zake na matendo ya Rububiyya yake, kama utendaji wa hali ya rehema kwa kumteremsha Qur’an ya muujiza ya ubainifu, na kwa kudhihirisha aina ya miujiza kupitia yeye, na kumwafikisha na kumhami katika hali zake zote, na kwa kudumisha dini yake kwa hakika zake zote, na kuinua makamo ya utukufu wake juu ya viumbe wote kwa kuonekana waziwazi, na kama utendaji wa Rububiyya yake kwa kufanya ujumbe wake ni jua la kimaanawy kwa viumbe, na kwa kufanya dini yake ni faharisi ya makamilifu ya ibada zake, na kwa kufanya hakika yake ni kioo chenye kukusanya midhihirisho ya Uungu wake, na kwa kumpa nyadhifa za dharura za lazima kwa uwepo wa viumbe katika viumbe hivi kama ulazima wa rehema, hekima, na uadilifu na kama dharura ya ulazima wa chakula, maji, hewa na mwanga.]

Maelezo ya ushahidi huu mkubwa wenye kukata shauri ambayo ni mapana sana tunaelekeza kwenye Risale-i Nur, na tunatazama maana yake ya jumla kwa ishara fupi mno:

Hakika tunashuhudia kwenye ulimwengu kwa macho yetu kwamba katika ada ya Rububiyya inayoendelea kila wakati kwa uadilifu, hekima na uangalizi, kuwahami wema na kuwatia adabu waongo na waharibifu, tunashuhudia hayo ndani ya matendo yake (s.w) yaliyopangika. Kwa mujibu wa matendo yake ya rehema kuteremsha Qur’an ambayo ni muujiza wa bayana juu ya Muhammad (s.a.w), na kudhihirisha aina ya miujiza mingi yenye kufikia kiasi cha miujiza elfu moja mikononi mwake, na kumhami chini ya ubawa wa upole wake wenye huruma katika hali zake zote bali katika mazingira yake magumu hatari mno, hata kumlinda kwake kwa njiwa na buibui! Na kumwafikisha kwa taufiki yenye kutia nguvu katika majukumu yake, na kuidumisha dini yake na hakika zake zote, na kuvika taji ardhi na wanadamu kwa Uislamu wake. Na kunyanyua makamo na utukufu wake kwenda katika makamo matukufu zaidi, na kumfanya kuwa bora juu ya viumbe wote kwa kumtunuku makamo ya kuridhiwa na kukubaliwa na daima yanayovuka bora wa wanadamu, na kumpa haiba inayobeba tabia nzuri mno kwa maafikiano ya wanaompenda na maadui hata ikafanywa humsi (moja ya tano) ya watu ni katika umma wake, yote hayo yanashuhudia kwa ukweli bila shaka yoyote juu ya ukweli wake (s.a.w) na utume wake. Na kadhalika tunashuhudia kwa upande wa matendo ya Rububiyya yake (s.w): Kwamba msarifu wa ulimwengu huu na mwendeshaji wa mambo yake amejaalia utume wa Muhammad (s.a.w) ni jua la kimaanawy la ulimwengu. Hakika imethibitishwa katika Risale-i Nur: kwamba ametokomeza giza lote kwa utume huo, hali ya kudhihirishia hakika za kinuru za kiulimwengu, na amefurahisha wote wenye utambuzi bali ulimwengu wote, kwa bishara ya maisha ya kudumu. Na kufanya dini yake vilevile ni faharisi ya makamilifu ya waja wake wote wenye kukubaliwa, na mwongozo ulionyooka wa matendo ya uja. Na kufanya hakika ya Muhammad (s.a.w) nayo ni haiba yake ya kimaanawy ni kioo chenye kujumuisha midhihirisho ya uungu wake, kwa dalili ya Qur’an tukufu na Al-Jawshan al-Kabir, bali amemjaalia kuwa anapata – zaidi ya hakika tulizoashiria – mfano wa mema ya uma wake wote kwa kila siku kwa muda wa karne kumi na nne, na kumleta kwa wanadamu wote na kumkabidhi majukumu matukufu, na kumfanya kigezo chema na kiongozi bora na Bwana mtukufu zaidi kwa wanadamu wote, kwa dalili ya athari zake katika maisha ya kijamii, ya kimaanawy na kiutu, na kufanya wanadamu wote wanahitajia dini yake na sharia yake na hakika zake ambazo amezileta katika Uislamu,

Hakika nilihisi nikiwa katika hali ya kusumbuliwa na uzee wangu na kudhoofu kwangu moja katika mamilioni ya riziki za kimaanawy ambazo amekuja nazo huyu mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w). Ingekuwa ni katika uwezo wangu ningemshukuru kwa mamilioni ya ndimi na swala.

Nazo:

Hakika mimi ninaumia upeo wa kuumia kutokana na utengano na kutoweka, pamoja na kuwa dunia ambayo ninaipenda na wanadunia ambao wananiacha kwa kuondoka kwao na kutengana kwao nami. Na mimi nikiwa najua safari yangu pia. Kunanichukua kukata tamaa kwenye machungu na giza. Lakini ninaliwazika na ninaokoka kwa ujumla kutokana na huku kukata tamaa kwa kusikiliza bishara ya Milele na Uhai wa kubakia kutoka kwa Nabii Mtukufu (s.a.w) hata mimi ninaposema: “Amani juu yako ewe Mtukufu wa daraja na Rehema za Allah na Baraka zake” katika Tashahudi, ninamkabidhi ahadi yangu na utiifu wangu na kusalimu kwangu amri kwa jukumu lake. Na ninambariki katika jukumu lake hali ya kukabidhi kwake aina fulani ya shukurani ikiwa ni badala ya bishara hiyo ya furaha ya milele, na kama hivi wanatamka Waislamu salamu hii mara tano kila siku. (Mtunzi)

haja yake ya rehema, hekima, uadilifu, chakula, hewa, maji na mwanga, hoja zote hizi za kiujumla zenye kukata shauri zinazofikia hoja kumi na mbili, ni ushahidi wenye nguvu wa hali ya juu wa utume wa Muhammad (s.a.w).

Je inayumkinika kwamba utume wa Muhammad usiwe jua la kimaanawy la ulimwengu hai ya kuwa umepata idadi hii ya ushahidi wa kiujumla mpana kutoka kwa bwana mlezi wa walimwengu wote ambaye hapuuzii kuchunga na kupangilia chochote vyovyote kiwavyo hata ubawa wa nzi na ua dogo sana. Kila ushahidi katika shahidi hizi kumi na tano zinajumuisha shahidi nyingi mno, hata ushahidi wa tatu umethibitisha madai: Ash hadu anna Muhammadan Rasuulullah kwa kukata shauri kabisa na nguvu iliyojikita kwa kuingia chini yake shahidi elfu moja kwa ulimi wa miujiza, na zimetangaza kutimia kwake na thamani yake na umuhimu wake mkuu kiasi mamia ya mamilioni ya ndimi urefu wa ulimwengu wa Kiislamu na upana wake zinatangaza madai hayo kwa ulimwengu kila siku mara tano. Kama ilivyo mabilioni ya watu wa imani wameridhia na kusadikisha bila shaka kwamba msingi wa madai hayo – nayo ni hakika ya Muhammad (s.a.w) – ni mbegu ya asili ya ulimwengu na sababu ya kuumbwa kwake na ukamilifu wa tunda lake, na kwamba Bwana mlezi wa walimwengu wote (s.w) amejaalia hiyo haiba ya Muhammad (s.a.w) ni mlinganiaji wa hali ya juu kwa ufalme wa Rububiyya yake, ufumbuzi wa kweli wa fumbo la viumbe na funiko la viumbe, na ni mfano wenye kuangaza wa upole wa rehema zake, na ulimi wenye ufasaha wa huruma yake na mapenzi yake, na mbashiri mkuu wa furaha ya kudumu katika ulimwengu wa milele, na aliyeletwa mwisho na mkuu kati ya mitume wake (s.a.w).

Basi hasara iliyoje kwa mtu ambaye haamini ukweli wenye hakika hii, au hauthamini! Ubaya uliyoje na ukubwa wa kutenda kwake upumbavu na jinai kubwa.

Kama ilivyo sura (Al-Fatiha) ambayo imo kwenye swala kwa ishara zake kwenye sehemu ya pili inabainisha hoja za kukata shauri juu ya madai ya hakika ya Tawhidi katika (Ash hadu an laa ilaha illa Llah) na kuweka kiasi kisicho na mipaka cha alama ya kusadikisha, vivyo hivyo inaleta katika sehemu hii ya tatu vilevile mashahidi wenye nguvu wanasadikisha yaliyomo katika Tashahudi (Ashahadu anna Muhammadan Rasuulullah) na wanaweka alama nyingi za kusadikisha zisizo na hesabu.

فيا ارحم الراحمين

بحرمة هذا الرسول الأكرم ﷺ، وفِّقنا لنيل شفاعته واتباع سنته السنية، واجعلنا بجوار آله وأصحا به الكرام في دار السعادة الأبدية.

آمين آمين آمين.

اللهم صل وسلم عليه والي آله وصحبه بعدد حروف القرآن المقروءة والمكتوبة آمين

سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَاۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.