Utangulizi Wa Tafsiri Ya Kituruki Kutoka Tafsiri Ya Asili Ya Kiarabu Ya ‘Hutuba Ya Shamu’

Kwa jina lake mtukufu!

Hakuna chochote isipokuwa kinamtakasa kwa kumtukuza yeye

Assalaam alaykum warahamatullah wabarakatuhu milele na milele!

Ndugu zangu wapendwa wa dhati!

[Kwa hadhiri ya mustakabali, Saidi wa zamani amefahamu kweli zilizoandikwa katika hotuba hii ya Kiarabu, ambayo, kwa msisitizo wa mamlaka za kidini za Damascus, aliitoa miaka Arobaini iliyopita katika msikiti wa Umayya kwenye mkusanyiko wa takriban watu elfu kumi, uliojumuisha mamia ya wanazuoni wa kidini; alitoa habari za kweli hizo kwa uhakika kabisa kana kwamba zitatokea punde tu. Hata hivyo, vita vikuu viwili vya dunia na miaka ishirini na tano ya kuondoshwa kwenye nafasi kabisa ilichelewesha kutokea kwake; ni wakati huu ambapo ishara zilizobashiriwa wakati huo, zinaanza kuonekana katika ulimwengu wa Uislamu. Kwa hiyo kama unazingatia kuwa inafaa, mnaweza kuchapisha tafsiri ya sehemu hii yenye maelekezo muhimu na yenye kuelimisha mno, sio kama hotuba ya zamani iliyopitwa na wakati, lakini kama mpya maelekezo muwafaka kwa masuala ya kijamii na Kiislamu yakiyaelekea moja kwa moja katika mwaka 1371 badala ya 1327, mkusanyiko wa watu mia tatu na sabini (sasa ni zaidi ya milioni) katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu ukiachilia msikiti wa Umayya.]

Inafaa kuandika hapa jibu muhimu kabisa kwa swali muhimu kabisa. Kwa Saidi wa zamani aliandika kwa kutabiria katika somo hilo miaka arobaini iliyopita kana kwamba anayaona mafundisho ya kushangaza ya Risale-i Nur na athari zake. Ni kwa sababu hii ninaandika swali hilo na jibu hapa. Ni kama hivi:

Wengi wameniuliza mimi na wanafunzi wa Risale-i nur: “Ni kwa nini kwamba iko hivi Risale-i Nur haishindwi mbele ya upinzani mkubwa na wanafalsafa wakaidi na makafiri? Kwa kuzuia kuendelea kubomoka kwa mambo mengi ya thamani, vitabu sahihi kuhusu imani na Uislamu kwa kupitia matashi yao mbalimbali ya kidunia na dhambi zao, wamewazuia vijana wengi na wengine katika hakika za imani. Lakini mashambulizi yao makali zaidi, miamala mibaya, uongo na propaganda vimeelekezwa katika Risale-i Nur, kuiharibu na kuwaogofya watu wajiweke mbali nayo na kuwafanya watu kuachana nayo kabisa. Licha ya hivi, Risale-i Nur imeenea haijapatapo kuonekana katika kazi nyengine yeyote, nakala mia sita elfu za risala zake zimeandikwa kwa mkono kwa juhudi kubwa na kuchapishwa kwa siri. Ni vipi kwamba inasababisha kusomwa kwa hamasa kiasi hiki, kote ndani na nje ya nchi? Nini sababu ya hili? Kujibu maswali mengi sana ya aina hii, tunasema:     

Kuwa mfasiri wa kweli wa Qur’an tukufu kupitia siri ya muujiza wake Risale-i Nur inaashiria kwamba katika upotevu kuna aina ya jahanamu hapa duniani wakati katika imani kuna aina ya pepo. Inaashiria maumivu makali yaliopo katika dhambi, matendo mabaya na starehe zilizokatazwa na kuthibitisha kwamba katika matendo mazuri na maadili na ukweli wa sharia kuna furaha kama furaha ya pepo. Kwa namna hii inawaokoa wenye akili katika wale ambao wamedondokea katika maasi na upotevu. Kwa sasa kuna hali mbili za kutisha:

Ya kwanza:

Kwa kuwa mihemko ya mwanadamu, ambayo haioni matokeo ya vitu na kufadhilisha aunsi ya furaha ya sasa kuliko tani za furaha ya mustakabali, imekuja kutawalia akili na hoja, njia pekee ya kuwaokoa waliopotoka kutoka katika maasi yao ni kuwaonyesha maumivu ya sasa katika furaha zao na kuishinda mihemko yao. Japo kuwa wanajua mavuno ya mithili ya almasi na furaha za kama aya isemavyo:

الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا Qur’an, 14:3.

inaashiria, wakati wa kuwa waumini, watu wa upotevu wanachagua starehe za dunia ambazo ni kama vipande vya chupa punde vitavunjika. Njia pekee ya kuwaokoa kutoka katika mapenzi haya ya ulimwengu na kutokana na hatari ya kuangukia humo ni kwa kuwaonesha mateso ya kijahanamu na maumivu wanayoteseka nayo japo katika ulimwengu huu. Hii ndiyo njia ambayo Risale-i Nur inaichukua kwa kuwa wakati huu kutokana na uharibifu unaotokana na ukafiri wa kupindukia na ulevi unaofanywa na maasi na upotevu unaotokana na sayansi, huenda ni mmoja tu kati ya kumi anaweza kushawishiwa kuachana na tabia zake mbaya kwa kuthibitisha uwepo wa jahanamu na mateso yake baada ya kumwambia kuhusu Allah mtukufu. Kwa kusikia hili watu kama hao wanaweza kusema: “Allah (s.w) ni mwingi wa kusamehe na kurehemu na jahanamu ni safari ndefu hadi kuifikia” na kuendelea na makosa yao. Nyoyo na roho zao zimeelemewa na mihemko yao. Na kama hivi, kwa kuonesha kupitia mingi katika mifano yake matokeo mabaya na ya kutisha katika ulimwengu huu wa ukafiri na upotevu, Risale-i Nur huwafanya hata wale watu jeuri na wenye kiburi kuchukia starehe hizo za haramu, huwapelekea kutubu. Mifano mifupi katika neno la sita, saba na nane na ndefu katika kituo cha tatu katika neno la thelathini na mbili inamfanya mwanadamu kuhisi kujuta juu ya uovu juu ya upotevu wa njia aliyoichukua na kumsababishia kukubali mafunzo yanayotolewa nayo. Kwa mfano nitaeleza kwa ufupi hali niliyokuwa katika safari ya kimawazo ambayo kwa hakika ilikuwa ni kweli. Kwa wale wanaohitaji maelezo zaidi wanaweza kutazama mwishoni mwa (Muhuri wa kusadikisha ghaibu).

Nikiwa katika safari hiyo ya kimawazo nilitazama sampuli ya wanyama kupitia macho ya falsafa ya Wanamaada na watu wa upotevu na mghafala, mahitaji yasiyo na idadi ya wanyama na njaa yao kali pamoja na udhaifu wao na kutojiweza kwao, ilidhihiri kwangu kama ni jambo la kuhurumiwa na kusikitikiwa sana. Nililia kisha nikaangalia kupitia kikuza umbo cha busara ya Qur’an na imani kwamba jina tukufu la mwingi wa rehema limeinuka katika ishara ya mtoaji kama jua lenye kung’ara: likimulika kwa huruma zake ule ulimwengu wa wanyama wenye njaa ulioteketea.

Halafu nikaona ndani ya ulimwengu wa wanyama ulimwengu mwingine wa kuhuzunisha ambao ulikuwa umemezwa kwenye giza na kumfanya kila mtu kuwa na majonzi ambamo wadogo walikuwa wakihangaika katika mahitaji yao na kukosa nguvu kwao. Nilihuzunika niliangalia kupitia macho ya watu wenye upotevu. Tahamaki imani ikanipa miwani nyingine na nikaliona jina la mwenye kurehemu likiinuka katika ishara ya mneemeshaji; iligeuza na kuangazia ule ulimwengu wenye kusikitikiwa na kuwa katika hali ya furaha na uzuri; ikibadili machozi yangu ya malalamiko na huzuni kuwa machozi ya furaha na shukurani.

Kisha ulimwengu wa wanadamu ukaonekana kwangu kana kwamba katika kioo cha sinema niliangalia kupitia darubini ya watu wa upotevu na kuuona ulimwengu huo kuwa wenye giza sana na kutisha hadi nikalia kutokea kwenye kina cha moyo wangu “Eeh!” nikalia kwa sababu wao wana matamanio na matumaini ambayo yanakunjuka hadi milele, fikira na mawazo yanayouenea ulimwengu, matamanio ya kumiliki furaha ya milele na pepo, na uwezo wa kimaumbile na nguvu ambazo hazikuwekewa kikomo na ambazo zilikuwa ni huru, bado licha ya mahitaji yao yasiyo na idadi na udhaifu wao na kutojiweza kwao wana hatari ya kushambuliwa na maadui wasio na idadi na dhoruba za majanga yasiyo na idadi. Chini ya kitisho cha kudumu cha umauti wameishi katika maisha yao mafupi na yenye dhiki katika mazingira ya kuharibika. Wakiangalia kwenye kaburi ambalo kwa wapotevu ni mlango wa kuelekea kwenye giza la milele, waliteseka na mapigo ya mfululizo ya kifo na utengano, hali ya kuumiza kabisa kwa moyo na ufahamu. Niliona hivyo kwa mmoja-mmoja na kwa makundi yakiwa yanatupiwa kwenye kisima hicho cheusi.

Katika kuangalia ulimwengu wa mwanadamu katika giza hili nilikaribia kulia kwa moyo, roho na akili, na vipawa vyote nyororo vya ndani, kwa kweli sehemu zote za uwepo wangu, ilipotangulia nuru na nguvu kutoka katika Qur’an na kuvunja miwani hizo za upotevu na kunipa maono. Nikaliona jina tukufu la mwadilifu likichomoza kama jua katika ishara ya mwingi wa hekima, jina la mwingi wa rehema likichomoza katika ishara ya mwenye kurehemu, jina la mkarimu lilichomoza katika ishara, ni kusema, kwa maana ya mwingi wa msamaha, jina la mwenye kufufua limechomoza katika ishara ya mrithi wa kila kitu, jina la Al-Muhyi (Mtia uhai) likichomoza kwa ishara ya mneemeshaji, na jina la Ar-Razzaq (Mtoa riziki) likichomoza katika ishara ya mmiliki. Yameangaza ulimwengu mzima wa binadamu na ulimwengu wote ndani yake. Yametokomeza hali zote za jahanamu, yamefungua limwengu zenye kung’ara za akhera, na kutawanya nuru kwenye ulimwengu wa binadamu. Nikasema: “Alhamdulillah kwa namba za chembe zote katika uwepo!” Nilifahamu kwa uhakika kamili kuwa katika imani kuna aina ya pepo katika ulimwengu huu, pia katika upotevu kuna aina ya jahanamu.

Kisha ulimwengu wa ardhi ulidhihiri, katika safari hiyo ya kimawazo kanuni za kinadharia zenye giza za falsafa zisizotii dini zimeonesha ulimwengu wa kutisha. Anga lenye kusafiri katika jahazi la ardhi yenye miaka mingi – ambayo inasafiri mara sabini zaidi kuliko risasi ya bomu masafa miaka ishirini na tano ndani ya mwaka mmoja, muda wote ikiwa katika hatari ya kuvunjika, ndani yake kuna hali ya vurugiko – hali ya mwanadamu mwenye hali mbaya ilidhihiri kwangu katika giza lenye kutenganisha. Macho yangu yaliingia giza. Nilitupa chini miwani ya falsafa nikizivunja. Na halafu nikaangalia kwa matazamo ulionawirishwa kwa hekima ya Qur’an na imani na nimeona majina ya Muumba wa mbingu na Ardhi, Mweza, Mjuzu wa kila kitu, Mtoa riziki, Allah Mruzuku wa mbingu na Ardhi, Mteza nguvu wa jua na mwezi,  yamechomoza kama majua katika ishara ya rehema, mpaji na utawala. Vimeangaza giza lile la ulimwengu wa kutengwa na kutisha na kwa hiyo tufe la ulimwengu lilidhihiri katika macho yangu ya imani likiwa ni jahazi lililopangika vema, kutezwa nguvu, lenye kupendeza, na salama, au ndege au gari moshi. Ilikusanya riziki ya kila mmoja, na imerembeshwa kwa ajili ya biashara na furaha na kuchukua viumbe wenye roho ndani ya ulimwengu wa kiutawala kuzunguka jua. Niliguta: “Alhamdulillah kwa idadi ya chembe za neema ya imani.”

Hili limethibitishwa kwa mifano mingi katika Risale-i Nur kwamba wale ambao wanafuata uasi na upotovu wanateseka na maumivu ya kijahanamu katika ulimwengu huu pia, wakati kupitia midhihirisho ya kiimani, waumini na watu wema wanaweza kuonja raha za peponi kupitia matumbo ya imani na ubinadamu. Wanaweza kunufaika kulingana na kiwango cha imani yao. Lakini katika nyakati hizi za dhoruba, mawimbi yanayotia ganzi hisia na kutawanya mkazo wa binadamu katika masuala ya ziada, yakimtosa humo, yameua fahamu zake na kumchanganya. Kama matokeo ya hili watu wa upotevu kwa muda mfupi wanashindwa kuhisi mateso yake, wakati watu wa uongofu wamekumbwa na kughafilika hawawezi kiukweli kufaidi furaha zake.

Hali ya pili ya kutisha ya enzi hizi: Katika nyakati zilizopita kulinganisha na sasa kulikuwa na kiasi kidogo sana cha kutoamini kabisa, au upotevu unaotokana na sayansi, au kutoamini kunakotokana na kiburi cha kupindukia. Mafunzo ya wanazuoni wa Kiislamu wa nyakati hizo na hoja zao kwa hiyo zilikuwa zinatosha kwa haraka kutokomeza ukafiri wowote unaotokana na shaka. Kuamini Allah kulikuwa kwa jumla na waliweza kuwashawishi watu zaidi kuachana na upotevu wao na matendo mabaya kupitia kuwafundisha kuhusu Allah (s.w) na kuwakumbusha na moto wa jahanamu. Lakini kwa sasa kuna makafiri mia moja katika mji mdogo mmoja badala ya pengine mmoja katika nchi nzima. Wale ambao wanapotea njia yao kwa sababu ya sayansi na elimu na kwa ukaidi wanapinga kweli za imani wameongezeka mara kumi zaidi kulinganisha na zamani. Kwa majigambo kama yale ya firauni na upotevu wao mbaya kabisa hawa Wazandiki wanapinga kweli za imani. Ukweli mtakatifu kwa hiyo unahitajika sana ambao utaharibu kabisa misingi yao ya ukafiri katika dunia hii kama bomu la atomu, na kukomesha mashambulizi yao na baadhi yao kuwaleta katika imani.

Alhamdulillah kwa kuwa kwa mifano yake mingi kama tiba kamili ya majeraha ya wakati huu, Risale-i Nur muujiza wa Qur’an yenye ufasaha wa kimuujiza ikiendelea katika Mwanga wake imeng’oa hadi wazandiki wakaidi kabisa kwa upanga wa almasi wa Qur’an. Dalili na hoja zake kwa idadi ya atomu za ulimwengu zikiashiria umoja wa kiungu na kweli za imani zinaonyesha kwamba katika miaka ishirini na tano haikushindwa usoni mwa mashambulizi makali bali imeweza kuenea na yenyewe na kuibuka mshindi. Naam, kwa mifano yake ya imani na ukafiri na uongofu na upotevu, Risale-i Nur imethibitisha hoja hizo kwa kujieleza wenyewe. Mazingatio yakichukuliwa kwa mfano wa hoja na ming’ao ya kituo cha pili cha neno la ishirini na mbili, makamo ya awali ya kisimamo cha kwanza cha neno la thelathini na mbili, ‘Madirisha’ ya andiko la thelathini na tatu, na dalili kumi na moja za (Fimbo ya Musa), itaeleweka kwamba ni kweli za Qur’an zilizodhihirishwa kwenye Risale-i Nur ambazo zitavunja na kuharibu ukafiri na kukabiliana na upotevu wakati huu.

Kwa namna hiyohiyo kwamba sehemu za Risale-i Nur ambazo zinafumbua siri kubwa ya dini na fumbo la kuumbwa kwa ulimwengu zimekusanywa pamoja katika mkusanyiko wa ‘Mafumbo’ (Tılsımlar Mecmuası), sehemu zinazoelezea jahanamu katika ulimwengu huu wa watu wa upotevu na furaha za mfano wa pepo kwa watu wa uongofu na kuonesha kwamba imani ni kama mbegu ya pepo wakati ukafiri ni mbegu ya mti wa zakkum wa jahanamu, zitawekwa pamoja katika mkusanyiko mdogo inshaAllah na kuchapishwa.

Said Nursi

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.