[Wasifu Ambao Unajibu Maswali: Risale-i Nur Ni Nini? Hali Yake Halisi Ni Nini? Na Nini Hali Halisi Ya Mfasiri Wake?]

Watumishi wa juu wa dini wanaoelezewa katika hadithi ya kuja mwanzoni mwa kila karne si wenye kuleta upya, wao ni wafuasi. Hiyo ni kusema, wao hawabuni chochote kipya wao wenyewe hawaleti sheria zozote mpya; wao wanaweka sawa na kuimarisha dini kwa njia ya kufuata kikamilifu maandiko, misingi na sheria ya dini na sunna za Nabii Muhammad (s.a.w); wanatangaza ukweli na maana asilia ya dini; Wanaondoa na kuzingatia kuwa ni batili mambo yasiyo ya msingi ambayo yamechanganywa nayo; wanakataa na kuteketeza mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya dini; wanaweka amri, wanatangaza na kutambulisha utukufu na adhama ya sheria tukufu. Ila tu bila ya kuvuruga hali ya msingi au kuharibu roho asilia, wanatekeleza majukumu yao kupitia njia mpya ya ushawishi unaoliangana na ufahamu wa wakati uliopo na kwa mtindo na maelezo mapya.

Maafisa hao wa kiutawala wanathibitisha nafasi zao kutokana na matendo na kazi zao. Wanatimiza jukumu lao la kuakisi uimara wa Imani yao na ikhlasi yao. Wanadhihirisha katika matendo yao kiwango chao cha imani. Wanaonesha kwamba wanafuata kama yalivyoandikwa matendo ya Muhammad (s.a.w) na kwamba ni kweli wamevikwa taji la utume. Kwa ufupi: Kwa jamii ya Muhammad (s.a.w) wanaunda ruwaza kamilifu katika kuheshimu matendo na maadili na kufuata na kuendana na sunna ya mtume (s.a.w); wao ni mifano inayofaa kufuatwa. Kazi wanazoandika zinafafanua kitabu cha Allah na kuweka wazi maelekezo ya dini, wanawasilisha haya kwa mujibu wa ufahamu wa sasa na kiwango chake cha kujifunza, sio matunda ya akili yao ya juu yenye rutuba; wao si matokeo ya werevu na ujuzi wao. Ni moja kwa moja hayo ni wahyi na maelekezo ya msingi safi wa utume, ambaye ni chanzo cha wahyi. Jaljalutiyya, Mathnawi-i Sharif, na futuh al-Ghayb na kazi kama hizo zote ni za aina hii. Watu hao watukufu wana sehemu katika kupangilia zile kazi za hiari, na katika namna ya kuwa wazi; hiyo ni kuwa; wao ni mahali ambapo maana yake yanadhihirishwa na kuakisiwa.

Kuja katika Risale-i Nur na mfasiri wake: Kwa kuwa katika kazi hii ya fahari iko katika mwangaza wa hali ya juu na ukamili usiyo na mwisho haijapata kuonekana kabla katika kazi yoyote kama hiyo; na kwa kuwa inashuhudiwa kwamba ni urithi wa mwangaza wa Qur’an ambayo ni taa takatifu na jua la mwongozo na mwezi wa furaha; ni hakika iliyo wazi kama jua inabeba mwangaza wa nuru ya Muhammad (s.a.w) kwa kiasi kikubwa kuliko kuwa ni kazi ya mawalii, kwamba kushiriki ndani yake, na kuhusika nayo, na katika idhini takatifu ya msingi safi wa utume (s.a.w) ni kubwa zaidi kuliko katika mawalii, na ufikiaji na ukamilifu wa ambaye ni mfasiri na mahali pa udhihirisho ni wa hali ya juu na isiyo na kifani kwa kiwango hichohicho.

Ndiyo wakati akiwa bado ni mdogo na bado kamwe hajawa amesoma katika kitambo cha miezi mitatu ili kuweza kuokoka na wageni, mfasiri wa Risale-i Nur alifanywa kuwa mrithi wa elimu za zamani na sasa, elimu ya kiimani, hakika za mambo, siri za ulimwengu na hekima ya kiungu ambayo hakuna yeyote aliyetunukiwa kabla. Mafunzo na maadili yake ikiwemo na kuwa amepewa wasifu wa mbele na ujasiri usio wa kawaida na kujitegemea kikamilifu, alikuwa ni muujiza wa maumbile ni kuundika kwa fadhila za kiungu, uwezo wake ulikuwa ni tunuku za kiungu.

Akiwa ni mwanazuoni asiyelinganishwa na yeyote, mjuzi wa ajabu akiwapa changamoto ulimwengu wote wa kujifunza kabla ya kufikia umri wa kubaleghe, aliwanyamazisha wanazuoni wote aliofanya nao mdahalo, alijibu kwa usahihi hasa na pasi na kubabaika karibu maswali yote aliyoulizwa, alibeba nafasi ya muhimili ya Ukuu kuanzia umri wa miaka kumi na nne, na kwa mfululizo aliangaza nuru ya elimu na mwanga wa hekima. Kwa umakini kwa kina cha ufafanuzi, ufahamu na ufasaha wa maelezo yake na uoni wake wa werevu na mwanga wa hekima, aliwashangaza wanazuoni na wasomi kwa ustahiki kabisa alipata cheo cha utambulisho kuwa (Bediuzzaman) (maajabu ya zama). Kama mtu ambaye kwa wasifu wake wa juu na thamani za kiusomi aliitangaza na kuithibitisha kikamilifu sana Dini ya Muhammad (s.a.w), alipata kwa hakika fadhila kubwa za mola wa mitume na alikuwa katika ulinzi wake imara na himaya yake. Bila ya shaka yeye alikuwa mmoja wa thamani tukufu ambaye alipanda hadi katika daraja la utume mtukufu, na alitenda chini ya amri yake na alikuwa ni mrithi wa kweli zake na kuakisi nuru yake.

Kama ilivyoashiriwa katika kufanya kwake nuru na elimu ya Muhammad (s.a.w) na mwangaza wa mshumaa wa kiungu (Qur’an) kung’ara kwa uwazi mno, na umuhimu wa kimahesabu wa Qur’an na hadithi kukamilishwa kwake na udhihirisho wa kimahesabu wa aya zinazoelezea matamshi ya mtume (s.a.w) zinazopatikana kwake mwenyewe, hakuna shaka kwamba alikuwa ni kioo kilichoangazwa cha utume mtukufu katika kuhudumia maudhui ya imani na tunda la mwisho lenye kung’ara la mti wa utume, na kinywa cha mwisho cha hakika kuhusiana na ulimi wa haiba ya utume, na mbeba furaha wa mwisho wa mshumaa mtukufu kuhusiana na kuhudumia imani.

Kwa niaba ya wanafunzi wa Risale-i Nur ambao wamehudhuria somo moja la madrasa ya tatu ya Yusuf, ikiwa imejumuisha ushahidi angavu na Zuhreti’n-nur,

Ahmed feyzi, Ahmed Nazif, Salahaddin, Zubeyir, Ceylan, Sungur, Tabancali, wamenipa fungu kubwa kuliko ninavyostahiki. Lakini kukosa ujasiri wa kuwaudhi watia saini hawa nimebaki kimya na nimekubali wasifu wao kwa niaba ya haiba ya pamoja ya wanafunzi wa Risale-i Nur.

Said Nursi

Kwa jina lake mtukufu!

Na hakuna chochote isipokuwa kinamtakasa kwa kumsifu.

Assalam alaykum wa Rahamatullah wabarakatuh daima abadan!

Bwana wetu mpendwa sana, mheshimiwa mwema!

Mheshimiwa bwana wetu, ambaye ameachana na matakwa yake na kuacha mambo yote kwa matakwa ya utawala wa Allah, ambaye anaona huruma na hekima ya Kadari katika kila janga la dhahiri na shida na kwa kutegemea kikamilifu na kusalimu amri akingojea kwa subira matokeo ya dhihirisho ya kiutawala wa kiungu! Katika karne hii yenye balaa wakati katika mahali pengine katika mambo ambayo wanayoyategemea waumini yameanza kuporomoka, na bayana wakipinga nguzo za imani wakanushaji wa Allah wanajitanua wazi na kwa kiburi na kutenda kwa kupinga amri za Qur’an na kutoamini nguvu za kiroho, na kunasibisha haki ya kuumba kwa Asili isiyokuwa na utambuzi, pofu na bubu, vinazingatiwa kuwa alama za ustaarabu na kuwa na mila adhimu na kuwa na busara, katika wakati ambao mkuu wetu ameandika Risale-i Nur muujiza wa Qur’an ikitoa ponya yake kwa nyoyo zilizoharibikiwa zenye haja ya maji ya Uhai wa imani, amewapa habari njema ya furaha ya milele. Katika barabara yake kuu ya uhakika ambayo inathibitisha mafundisho yake kwa dalili na hoja za kukinaisha na zilizopangika, kupitia siri ya kiongozi wetu wa wazi (s.a.w), kwake inarejewa (sababu ni sawa na mfanyaji) sawasawa ya matendo yote yaliyotekelezwa na mamia ya maelfu ya wanafunzi wa Risale-i Nur ambao wameokoa imani yao kupitia Risale-i Nur imepita kwenye daftari la matendo yake!

Kama ilivyokuwa katika jela ya Denizli Allah (s.w) amefadhili matunda ya imani, ambayo ponya zake zilikuwa zinatosha kwa hakika kabisa kumaliza kabisa majonzi ya kuzuiliwa, na manukato mazuri ya waridi yaliyo ondosha maumivu yote ya miba na kutokomeza maumivu yetu yote ya muda mfupi; kwa hiyo vilevile hapa katika jela ya Afyuni hali ya kudhikika kimwili kwa siku moja ambako ni sawa na dhiki ya mwezi mzima katika jela ya Denizli, mwingi wa Rehema mwenye ukarimu wa uzuri ametunuku kupitia mikono ya mkuu wenu hoja zenye nguvu zinathibitisha umoja wa kiungu na utume wa Muhammad (s.a.w), ambazo ni tiba na ponya. Sisi wanafunzi wako wakosaji mno, ambao kupitia mwanga wa Risale-i Nur tumejifunza kusoma na kuandika, tunazingatia risala zote hizi tatu kuwa ni shahidi za kukinaisha za ukweli wa Risale-i Nur, na ni namna ya muhtasari wake, katika hali hiyohiyo kwamba programu na faharisi ya mti maridadi wa msonobari umejumuishwa katika mbegu zake.

Hatuna uwezo wa kuelezea thamani ya maandiko haya matatu lakini katika kuyasoma roho zetu zinahisi faraja kubwa, maumivu yetu ya kimwili yamegeuzwa kuwa ni furaha na yanatuletea matunda yasiyohesabika kutoka katika bustani ya imani. Na dalili zake kumi na moja za umoja wa kiungu, ya kwanza kati ya hizo inatokomeza giza la ukafiri, upotevu na hali ya sasa. Ya pili inachambua kwa dalili tukufu za imani surat Al-fatiha, chanzo, misingi na mfano mkuu kuliko yote katika Risale-i Nur. Na ya tatu inafafanua kwa ufasaha katika namna kwamba inayohakikisha uhakika kamili wa sehemu ya pili ya utume wa Muhammad (s.a.w) iliyoletwa kwako bwana wetu, hapa katika jela ya Afyuni.

Japo kwa vyovyote hatuna ubora wa chochote, tutajitahidi kwa nguvu zetu zote kutangaza kazi hizi tulizozipokea. Tukitoa shukurani zetu zisizokuwa na mwisho kwa mola wetu mtukufu, Tunamwomba kwa kusema: “Mwingi wa rehema wa warehemevu! Tunakuomba umridhie mkuu wetu daima milele na milele!”

Mwenye kubaki, ndiye mwenye kubaki!

Kwa jina la wanafunzi wa Risale-i nur,

Zubeyir, Ceylan, Sungur, Ibrahim

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.