Barua ya tatu

(sehemu ya barua iliyoandikwa na Bediuzzaman kwenda kwa mmoja katika wanafunzi wake)

بِاسْمِهِ سُبْحَانَهُ وَاِنْ مِنْ شَيْءٍ اِلاَّ يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ

Hakuna chochote ila kinamtukuza! kwa sifa zake njema.

Uliandika katika moja ya barua zako ulizonitumia kwamba ulitaka nikusimulie hisia zangu, sasa sikiliza moja ya sehemu elfu ya hisia zangu.

Usiku mmoja, nikiwa juu ya jengo lenye duru mia moja kwenye nyumba yangu ya mti na kileleni mwa mti wa mwerezi nilitazama sura nzuri ya mbingu iliyojawa na nyota nikaona mwanga ulionyanyuliwa wa hali ya kimiujiza na siri ya kushangaza ya hekima katika kiapo cha Qur’an, yenye hekima zote.

فَلاَ اُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ* َالْجَوَارِ الْكُنَّسِ{Qur’an 81: 15-16}

Aya hii, inayohusiana na sayari na hali za kule kufichikana kwake na kutawanyika, inaonesha katika kutazama kwa watazamaji ufundi na sanaa tele zilizopo katika kitambaa kilicho pambwa kwa ufundi mkubwa pamoja na sayari zinazojitokeza kwenye mzunguko wa jua kama kamanda wake, na kuingia katika duara la nyota zilizothibiti mahali pake, na kuonesha mapambo mazuri na mifano ya sanaa mbinguni, wakati mwingine huja bega kwa bega na nyota nyengine na kuonesha mandhari ya kupendeza na mara nyingine huingia kati ya nyota ndogo na kushika nafasi ya kamanda hasa katika majira haya baada ya jioni.

Sayari ya zuhura ikiwa angani usawa wa mlalo na kabla ya mapema alfajiri moja ya wenza wake wanaong’ara huonesha mandhari ya kweli ya kuvutia na kupendeza, halafu, baada ya kutimiza majukumu yake kama wakaguzi na kutenda kama zana ya kupamba katika ufundi wa ufumaji zinarejea na kuingia katika duara linalong’ara mno la jua na kujificha, hapo zinadhihirisha ufalme mkuu katika mng’ao mfano wa jua unaoteremka kutoka kwa yule anayeizungusha hii dunia yetu na sayari ambazo zimeelezwa kwenye aya iliyopo hapo juu kwenye anga kwa mpangilio kamili angani, kila mmoja ni kama meli au ndege zake zenye kuzunguka mara elfu ilhali ni kubwa kuliko dunia, na zinazunguka katika mzunguko wa kasi mara elfu zaidi ya dunia.

Unaweza kuona kutokana na haya ni kiasi kipi cha furaha, na heshima kubwa ilioje, na kule kuunganishwa na ufalme uliomo ndani ya ibada na imani ya kweli na kuwa mgeni kwake, kisha nikatizama kwenye mwezi na kuona mwanga wake wenye kung’ara kimuujiza katika aya hii:

وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّى عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ {Qur’an, 36:39}

‘Na mwezi tumeukadiria vituo vyake mpaka ukarejea kama karara la mtende la zamani:’

Kwa kweli, maamuzi, mzunguko, na kuweka mizani na kung’ara kwa mwezi, na kuwaka kwake kwa kuzingatia dunia na jua, na muhtasari wa kumbukumbu ni ajabu sana, la kushangaza sana kwamba hakuna chochote ambacho kingekuwa kigumu kwa Al-Qadiir Muweza wa kila kitu ambaye anaamuru na kuamua hayo, hivyo, yanawaelekeza viumbe wote wenye akili wenye kuyafahamu hayo, na kuwasilisha fikra ya kwamba yule ambaye anayefanya hayo kwa namna hiyo, kwa hakika anaweza kufanya chochote kile.

Amri yake inaliamrisha jua na wala halikengeuki njia yake hata kwa sekunde, au kubaki nyuma japo kidogo katika majukumu yake, inawafanya wale wanaotazama hayo watamke:

“Utukufu uwe kwa Yule ambaye ufundi wake unahemeza akili” hasa majira kama mwishoni mwa mwezi wa tano huja na muunganiko wa kilimia kwa umbo la hilali la kupendeza, ikijitokeza kama tawi la karara jeupe la mtende, na kilimia kikidhihiri kama kole la zabibu, inaleta sura katika mawazo kuwepo kwa mti mkubwa unaog’ara nyuma ya pazia ya mbingu ya kijani, kana kwamba ncha ya moja wapo ya matawi ya mti imetoboa pazia na kuungana kichwa chake na kole lake la zabibu na kwa kilimia na mwezi mchanga, na matawi mengine yamekuwa ni matunda ya mti uliojificha. Tazama werevu na ufasaha wa mfano.

كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ

‘kama karara la mtende la zamani’

Halafu aya hii ilinitokea:

سُبْحَانَ الَّذِى سَخَّرَ لَنَا هذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ{Qur’an 43:13}

Utukufu ni Wake aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya wenyewe.

Ambayo inamaanisha kuwa ardhi ni jahazi linalo endeshwa au kuabiriwa, kutokana na hili niliona nafsi yangu ikiwa juu ya meli kubwa iendayo kasi angani, nikasoma aya hii:

سُبْحَانَ اَلَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَاذَا

Utukufu ni Wake aliyemfanya huyu atutumikie.

Ambayo ni sunna kuisoma wakati wa kuabiri chombo cha usafiri kama farasi au meli.

Nimeona mwendo wa tufe la ardhi umechukua nafasi ya kikuza picha ambao unaonesha taswira kama kwenye sinema, unaleta mbingu zote kwenye mwendo na kuanza kukusanya nyota zote kama jeshi kubwa, unaonesha mandhari ya juu ambayo yanawalewesha wanayoyatafakari na kuwajaza mshangao: “Utukufu ni kwa Allah (sw)” nikapaza sauti “ni kazi nyingi, kubwa, za ajabu, utukufu kiasi gani, ambazo zinatendwa kwa gharama kidogo sana, nukta muhimu sana zinazohusu imani zilinitokezea baada ya hapa.

Kwanza:

Siku chache zilizopita niliulizwa swali na mgeni: Kiini cha swali hilo, ambalo lilimaanisha shaka lilikuwa hili: pepo na moto wa jahannam viko mbali sana kupitia rehema tukufu, watu wa peponi watapita katika sirat kama umeme au kwa kasi kama Buraq; na kuingia peponi lakini watu wa motoni, watakwendaje kwa miili yao mizito iliyotopewa na mizigo mizito ya dhambi zao watasafiri vipi?

Kilichonitokezea ni hiki: Kama kwa mfano mataifa yote yataalikwa kwenye baraza kuu marekani, na kila mmoja akapanda mashua kubwa na kwenda huko, kwa namna hiyo hiyo, dunia, ambayo hufanya safari kwa masafa ya miaka ishirini elfu, ndani ya mwaka mmoja katika bahari kuu ya ulimwengu, itachukua kwa watu wake kusafiri kuelekea katika uwanja wa kukusanyika siku ya kiama na kuwashusha huko, zaidi ya hapo moto ulio kati ya ardhi unaashiriwa na ukweli kwamba hali ya joto ya ardhi huongezeka nyuzi joto moja kwa kila mita thelathini na tatu kwamba moto wa Jahannam utamimina moto wake kwenye Jahannam kuu.

Joto hilo la nyuzi joto laki mbili ni sawa na lile lililoelezwa ndani ya hadithi na kwa mujibu wa hadithi itatimiza baadhi ya majukumu ya moto wa Jahannam kubwa hapa duniani na katika mamlaka ya mpito, halafu kwa amri tukufu ardhi itabadilishwa na kuwa katika muundo bora na wa kudumu, na itakuwa ni miji ya makao ya akhera.

Nukta ya pili:

Inayokuja akilini, ni kaida ya mtengenezaji Al-Qadiir Muweza wa kila kitu, Muumba ambaye ni Al-Hakiim Mwingi wa hekima ni Mmoja wa pekee, ili kuonesha ukamilifu katika uweza wake na uzuri wa hekima zake na uthibitisho wa upweke wake ni kutenda matendo mengi kwa kiasi kidogo sana na kuwa na majukumu makubwa yanayotimizwa kwa vitu vidogo kabisa kama nilivyosema katika baadhi ya maneno, kama mambo yote yangehusishwa kwa mmoja pekee, basi mambo huwa ni mepesi kama kuwa kama ya lazima, wakati ambapo kama yatahusishwa kwa wafanyaji wengi na kwa yale wanayofanyia kazi, basi ugumu mwingi utajitokeza na kuyafanya hayo kuwa ni muhali, kwa mtu mmoja pekee kama afisa au mjenzi mkuu na nafasi za askari wengi kwa kitendo kimoja pekee, mchakato mmoja, hupatikana tija ya jambo, lakini kama kwa ajili ya kupata nafasi na matokeo hayo, yanayohusishwa na askari katika jeshi au mawe katika kuba, ambayo bila msaada yanaweza kutimizwa kwa matendo mengi ya kweli, ugumu mwingi na kuchanganyikiwa kukubwa.

Na kwa hiyo, kama matendo hayo katika mfano wa misokoto na mizunguko ya mahala pake na kuzunguka kitu kingine, na utukuzo wa matembezi na mtawanyiko na kuleta majira manne, mchana na usiku duniani, haya yanahusishwa na umoja na kuamuru dunia moja na kwa amri moja, mmoja anaweza kupata hali hizo tukufu na matokeo makuu, anaweza kudhihirisha maajabu katika kubadilishana misimu na maajabu ya hekima katika mizunguko ya mchana na usiku, na matukio ya neema ya kuvutia na mienendo dhahiri ya nyota, jua na mwezi. Kwani majeshi yote ya viumbe ni yake.

Kama anataka anaweza kuagiza askari kama ardhi kuwa ni kamanda wa nyota zote, na kulifanya jua lenye nguvu kuwa ni taa inayotoa joto na mwanga kwa watu wake, na misimu minne ambayo ni meza ya maandishi ya uweza wake kama urembo, na usiku na mchana ni kurasa za maandiko yake ya hekima, na anaweza kuweka katika mapindo kwa kuonesha mwezi kila siku kwa umbo tofauti huufanya kuwa ni kalenda kwa ajili ya kukumbuka wakati, kama anavyozifanya nyota kuwa ni taa za kupamba, za usanifu na kung’ara mikononi mwa malaika, zikicheza kwa furaha kwa hiyo pia anaonesha mifano mingi ya hekima inayoonekana kwenye ardhi, kama hali hii haikutazamiwa kwa mmoja aliyopo, ambaye amri, sharia na kanuni zake zinawalenga viumbe wote, basi jua na nyota zote zingelazimika kwenda masafa yasiyo na ukomo kila siku kwa mwendo halisi na kasi isiyo na kikomo.

Kwa sababu ya wepesi wa uso na upeo kwenye umoja na ugumu usio na upeo katika wingi, hadi wafanya biashara na wanaviwanda huweka umoja kwenye wingi na kwa hiyo kufanya vitu kuwa rahisi hii ndio maana wanaunda mashirika.

Kifupi: Kuna ugumu usio na tamati katika njia ya wapotevu, na wepesi usio na tamati katika njia ya Umoja (Tauhid) Wa milele Yeye ni wa milele!

(Said Nursi)

Qur’an inakutaka kukamilisha imani yako na sio kuiacha.

Wito kwa Ahlil-kitab:

وَالَّذ۪ينَ يُؤْمِنُونَ بِمَٓا اُنْزِلَ اِلَيْكَ وَمَٓا اُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ

Na wale wanao amini yaliyoteremshwa juu yako. Quran 2:4.

Kwa kuzingatia kipande “na yale yaliyoteremshwa kabla yako” namna kinavyorejea katika kipande kilichotangulia ni mjadala ambao unatokana na kinachowekewa ushahidi, iko kama hivi:

Enyi wanadamu! Kama mnaamini Qur’an, aminini pia na vitabu vilivyotangulia, kwa kuwa Qur’an inathibitisha ukweli wake.

Au vinginevyo ni mjadala unaotokana na hoja inayowekwa kama hivi.

Nyie Ahlil-kitab! Kama mnaamini Mitume na vitabu vilivyotangulia mnalazimika pia kuamini Qur’an na Muhammad (saw), kwa sababu vitabu vilieleza habari njema juu ya kuja kwake zaidi ya hayo, uthibitisho wao, na ufunuo waliofunuliwa na ushahidi wa utume wa Mtume (saw) huonekana kwa uhakika na ukamilifu wa kiroho zaidi katika Qur’an na kwa ufasaha zaidi kwa Muhammad (saw) kwa hiyo kwa mujibu wa hoja hii madhubuti, Qur’an ni neno la Allah (sw). Na Muhammad (saw) ni mjumbe wake.

Uislamu ambao ni matokeo ya Qur’an na umeibuka kutokana na hayo katika enzi za furaha tele, ni kama mti, ambapo asili yake imefungwa katika kina cha muda uliopita mizizi yake iliyosambaa inapewa lishe kutoka katika vyanzo vya maji wakati huo vikileta maisha na nguvu, na vilevile matawi yake yamechanua katika anga la mustakabali na kuzaa matunda ya kimwili na kiroho kwa ajili ya ulimwengu wa watu, kwa kweli Uislamu chini ya mbawa zake wakati uliopita na wa baadaye, na kuzishika nyakati hizo katika kivuli, kinachohakikisha utulivu wa jumla.

Tunapojadili Ahlil-kitab kuamini Uislamu, Qur’an inafanya hilo kuwa ni jambo la kawaida kwao, na jepesi, ndio inamaanisha kwamba; Enyi Ahlil-kitab! hamtaona ugumu wowote katika kuukubali Uislamu; isonekane kuwa ni ngumu kwenu. Kwani Qur’an haiwataki nyinyi muache dini yenu yote kabisa, bali inashauri mukamilishe imani yenu tu, na mujenge juu ya misingi ya dini ambayo tayari mnayo. Kwa sababu Qur’an inakusanya ndani yake thamani za vitabu vyote vilivyotangulia na misingi ya dini zote zilizotangulia; inarekebisha na kukamilisha misingi, iliyokuwapo.

Inaweka tu taratibu mpya katika mambo ya daraja la pili, ambayo yanakubali kubadilika kulingana na tofauti za muda na wakati; na jambo hili kwa vyovyote haliendi kinyume na sababu za maana na kimantiki, kwa mabadiliko ya majira ya mwaka, chakula na mavazi na mambo mengi mengine pia hubadilika; kwa hiyo vile vile ngazi za maisha ya mwanadamu zinaruhusu mabadiliko kwa namna ya elimu zao na malezi yao. hali kadhalika inavyolazimu hali kutokana na hekima na mahitajio taratibu za dini zinazohusu mambo ya daraja la pili, hubadilika kwa mujibu wa mabadiliko ya hatua za maendeleo ya mwanadamu, kwa sababu nyingi kati ya hizo zinaweza kwa wakati fulani kuwa za manufaa na kwa wakati mwengine kuwa na madhara, dawa nyingi zilikuwa na manufaa sana kwa mwanadamu katika hali ya uchanga wake na bado baadaye zikakomaa kuwa ni ponyo kwake wakati wa ujana wake. Hii ndio sababu kwamba Qur’an imetengua baadhi ya kanuni za daraja la pili. Hivyo ikatangaza kwamba hizo muda wake umekwisha, na imekuwa zamu ya maagizo mengine.

Mwanadamu anahitajia aina nyingi mno za viumbe ulimwenguni na ana umuhimu navyo, mahitaji yake yamesambaa kila sehemu ya ulimwengu, na raghba zake zinatanuka hadi katika umilele, kwa kuwa anahitajia ua , kwa hiyo anahitajia majira ya machipuo, kwa kuwa anahitajia bustani kwa hiyo anahitaji pepo ya kudumu milele. Kama anavyotazamia kumuona rafiki, ndivyo anavyotazamia kumuona Mzuri kuliko wote Mwenye utukufu. Kama ilivyo ili kumzuru mtu ampende anayeishi kwengine, anahitajia kufunguliwa kwake milango na huyo mpendwa wake, kwa hiyo ili kumtembelea rafiki ambaye amesafiri katika ulimwengu wa Barzakh na kuokolewa na utengano wa milele, anahitaji kutafuta kimbilio katika mamlaka ya Muweza bila ukomo. Kwa sababu ni yeye ambaye atafunga mlango wa ulimwengu huu na kufungua mlango wa maisha ya akhera, ambayo ni maonesho ya maajabu, na kuuondosha ulimwengu huu na badala ya kusimamisha akhera.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.