MAKALA YA ISHIRINI NA TATU

[Katika makala haya pana vipambanuzi viwili]

بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ

 لَقَدْ خَلَقْنَا اْلاِنْسَانَ فِى اَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ثُمَّ رَدَدْنَاهُ اَسْفَلَ سَافِلِينَ اِلاَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَ عَمِلُوا الصَّالِحَاتِ{Qur’an 95:4-6}

KIPAMBANUZI CHA KWANZA

Tutaeleza fadhila tano tu za imani miongoni mwa maelfu ya faida za imani.

NUKTA YA KWANZA

Kupitia nuru ya imani, mwanadamu hupanda hadi akafikia ngazi ya juu zaidi kuliko ngazi zote za juu, na hupata thamani inayostahili Pepo, na kupitia kiza cha kutokuwa na imani, hushuka hadi ngazi ya chini zaidi kuliko ngazi zote za chini, na huanguka hadi akafikia nafasi inayostahili Jahannam, kwani imani humuunganisha mwanadamu na Allah (sw) Al-Khaaliq (Muumbaji Mwenye wingi wote wa Utukufu), kwani imani humuunganisha kwa Mtengenezaji mkuu, haya ni mahusiano.

Kwa hiyo mwanadamu hupata thamani kwa kutokana na ubora wa fadhila wa sanaa ya Kiungu na michoro ya nakshi ya Asmaullahul-Husna (Majina ya Allah (sw) ambayo ni mazuri), ambayo huonekana kwake kupitia imani. Kutokuwa na imani (kufru), huvunja kujinasibu huko, na kwa ajili ya kuvunjika kwa huo uhusiano, sanaa ya Kiungu hufichika, na thamani hiyo ya mwanadamu hupungua hadi kuwa thamani ya kuweko kwake kimwili tu. Na kwa kuwa jambo hili hudumu muda mfupi tu, na ni la mpito tu, na la maisha ya kinyama ya muda tu, thamani yake huwa ni takribani sifuri. Tutaelezea siri hii kwa kubainisha kwa njia ya mifano.

Mathalan, miongoni mwa sanaa ya mwanadamu, thamani ya mali ghafi ambayo hutengenezea hiyo sanaa hutofautiana na thamani ya ile sanaa yenyewe inayotengenezwa. Wakati mwingine huwa sawa, pengine mali ghafi huwa na thamani kubwa zaidi, na mara nyingine

hutokezea kuwa mali ghafi kama chuma ambacho gharama yake ni Lira (pesa ya Kituruki) tano tu na ikitengenezwa huwa Lira tano; bali hutokezea wakati mwingine ile sanaa iliyotengenezwa ikawa ni kitu nadra na adimu sana na chenye thamani kubwa kiasi kwa mfano kufikia mamilioni ya shilingi ijapokuwa mali ghafi yake ni rahisi mno. Iwapo kazi hiyo ya sanaa itapelekwa katika soko la sanaa za kale, na ikahusishwa na msanii stadi na mweledi wa nyakati za zamani, na kutangazwa huku likitajwa jina la yule msanii, na ile sanaa yenyewe inaweza kuuzwa kwa gharama kubwa sana, ambapo ikipelekwa kwa wauzaji au wanunuzi wa mabaki ya metali, bei pekee itakayopatikana itakuwa haizidi shilingi tano tu.

Kwa hiyo, mwanadamu ni aina hiyo, ufundi wa kale wa Allah (sw). Yeye ni muujiza mahiri na mzuri wa uwezo Wake ambaye Alimuumba kudhihirisha Majina Yake yote na michoro yake katika umbo la sampuli la viumbe ulimwenguni.

Ikiwa nuru ya imani itamuingia mwilini mwake, michoro yote yenye maana juu yake yaweza kusomeka. Akiwa kama mtu anayeamini, huisoma kwa makini na kupitia uhusiano na nasaba hiyo, huwasababishia wengine kuzisoma. Hiyo ndiyo kusema kwamba sanaa ya Kiungu

kwa mwanadamu, huonekana kupitia maana kama: “Mimi ni sanaa ya Mtengenezaji Mwingi wa Huruma. Mimi ninadhihirisha huruma Yake na ukarimu mkubwa.” Yaani hiyo ni imani, ambayo huunganishwa na Al-Khaaliq (Muumbaji), hufanya zionekane kazi zote za sanaa kwa mwanadamu. Mwanadamu huyu ambaye hana umuhimu wowote huwa baada ya hapo hustahiki kupata maelezo ya kiungu, na kupata hadhi ya juu inayomfanya apate kuwa mgeni wa Allah (sw) peponi.

Lakini ikiwa ukafiri utaingia katika mwili wa mwanadamu kutokana na kukatika uhusiano huu, basi ile michoro yote ya Majina ya Kiungu yenye maana huzamishwa kwenye kiza na hufutika moja kwa moja, kwani iwapo Mtengenezaji atasahaulika, mambo ya kiroho ambayo humtizama Yeye hayataeleweka, yatakuwa kama vile yamegeuzwa nyuma.

Mengi ya sanaa zile zenye maana nzuri, na michoro iliyopandishwa juu, zitafichika, zilizobaki, zile zitakazoweza kuonwa kwa macho, zitahusishwa na shughuli duni, asili, na bahati, na yatakuwa hayana thamani kabisa. Wakati hizo ni almasi muruwa zenye kung’aa, zote zitakuwa vipande dhalili vya vioo tu.

Umuhimu wake hutazama kule kwenye unyama wake, hali ya mwili pekee. Na kama tulivyosema, nia na tunda la hali ya mwili wake, ni kupitisha sehemu tu ya maisha mafupi kwa mwanadamu ambaye ni kiumbe dhaifu mwenye uhitaji na mbaya zaidi ni kuwa baada ya hapo huondoka na huoza, na hivi ndivyo ukafiri unavyoharibu asili ya mtu, na huigeuza kutoka katika almasi kuwa makaa ya mawe.

NUKTA YA PILI

Kwa hakika imani, kama ambavyo ni nuru inayomuangaza mwanadamu na kuzifanya zionekane na zisomeke barua za Yule Mmoja anayetegemewa milele zilizochorwa juu yake. Pia inaangaza ulimwengu, na inawasilisha yaliyopita na yajayo baadaye kutoka gizani.

Tutabainisha siri hii, kwa ulinganisho niliyouona kwenye maono ambayo yanahusu maana moja ya aya ifuatayo ya Quran:

اَللّٰهُ وَلِىُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ اِلَى النُّورِ { Qur’an 2: 257}

Nayo ilikuwa hivi: Katika maono niliona milima miwili mirefu kabisa; iliyokuwa ikiangaliana; katikati yake kumejengwa daraja la kutisha;

mmoja ukiwa mkabala na mwenzie, chini ya daraja kulikuwa na bonde lenye kina kirefu, mimi nilikuwa juu ya daraja lile.

Giza zito liligubika kila sehemu ya dunia, nilitazama upande wangu wa kuume na nikaona kaburi kubwa sana katikati ya giza lisilo na ukomo, ndiyo kusema mimi niliifikiria hivyo, nilitazama upande wangu wa kushoto na kama vile niliona dhoruba kali na maafa inajikusanya katikati ya mawimbi ya kutisha ya weusi, nikatazama chini ya daraja na nikafikiri niliona lindi kubwa, nilikuwa na tochi yenye mwanga dhaifu katika giza lile la kutisha, niliitumia ile tochi na nikaona kidogo mwanga wake dhaifu, hali ya kutisha mno ikanitokea, kwa hakika majoka ya kutisha, simba, na madude; nikajisemeza: Laiti nisingekuwa na tochi ile iliyoniangazia wanyama wote hao wa kutisha, kwani kila nimulikapo ninaona hatari ile yenye kuogofya nikasema tena: “Oh! hii tochi inaniletea matatizo tu!” na kwa hasira nikaitupa tochi chini nikaivunja, kisha baada ya kuibwaga chini, ghafla mwanga ukasambaa, kama vile niliwasha swichi kwa taa kubwa ya umeme ambayo iliangaza dunia nzima, kila mahali pakajaa mwanga wa taa, ulionesha kila kitu kama kilivyo kiuhalisia.

Nikagundua  kwamba  daraja  nililoliona  lilikuwa barabara kuu iliyopita kwenye tambarare ipitayo juu ya ardhi sawia. Kaburi kubwa sana nililoliona kuumeni kwangu nilitambua kuwa toka juu mpaka chini yake lina mabustani mazuri ya kijani kibichi, na lina mikusanyiko kwa ajili ya ibada, utumishi, mazungumzo, na kumkumbuka Allah (sw) chini ya maelekezo ya watu wenye nuru, wenye kueneza furaha, na kuingiza katika nyoyo furaha, kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake.

Ama bonde lile kubwa, dhoruba kali na mawimbi niliyoyaona kushotoni mwangu, hayakuwa bali ni milima na nyuma yake kuna bustani nzuri kubwa yenye miti mizuri ya kijani kibichi yenye kumfurahisha mtazamaji.

Aidha viumbe nilivyofikiri kuwa ni madude na majoka makubwa, nilitambua kuwa ni wanyama wa kawaida wa kufugwa kama ngamia, ng’ombe, kondoo na mbuzi. Kisha nikasoma aya hii tukufu:

اَللّٰهُ وَلِىُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُمْ مِنَ الظُّلُمَاتِ اِلَى النُّورِ

Baada ya hapo nikasema: “Alhamdulillah kwa nuru ya imani” na nikazinduka kutoka kwenye maono yangu.

Kwa hiyo, ile milima miwili ilikuwa ni mwanzo na mwisho wa maisha, (yaani ulimwengu wa hapa duniani na maisha ya Barzakh (hayani maisha baada ya mtu kufa na kabla hajafufuliwa). Lile daraja lilikuwa ni barabara ya maisha. Upande wa kuume ni mambo yaliyopita na kushoto ni yajayo, ama kuhusu ile tochi ndogo ya mfukoni, ilikuwa ni nafsi ambayo ni ubinafsi, inayotegemea kile kinachojua, na hakijali ufunuo wa mbinguni, vitu vilivyodhaniwa kwamba ni madude ni matukio na viumbe vya ajabu vya duniani.

Kwa hivyo yule anayetegemea nafsi yake ambaye huangukia kwenye giza la kutojali, na kuathirika kwa giza la kupotoshwa basi mtu huyo atafanana na hali yangu ya mwanzo katika maono yale niliyoyaona, ambaye huona yaliyopita kwa mwanga wa tochi ile dhaifu, ambapo ni kufahamu kwa hali ya kupotoshwa kama vile kaburi kubwa katikati ya giza lililochanganyika na kule kutokuwepo, ilionesha kuwa mambo yajayo ni dhoruba na ardhi iliyoachwa iliyotawaliwa na upatanifu kama ilivyosawirisha matukio na yaliyomo (yakiwa na watumishi kutoka kwa Mola Karimu), kama vile madude yenye kutisha, mtu kama huyo ni haki juu yake hukumu ya aya hii tukufu:

وَالَّذِينَ كَفَرُوا اَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُمْ مِنَ النُّورِ اِلَى الظُّلُمَاتِ{Qur’an 2:257}

Lakini iwapo mtu kama huyo anaafiki mwongozo wa Kiungu, na imani imwiingie moyoni mwake, na akavunja ufirauni katika nafsi yake; na anakijali na kukisikia Kitabu cha Allah (sw), atafanana na hali yangu ya pili katika maono (tukio lile nililoliota), wakati huo ulimwengu na viumbe ghafla utachukua rangi ya mchana na atajazwa na mwanga wa Kiungu, dunia itaisoma aya hii:

اَللّٰهُ نُورُ السَّمٰوَاتِ وَاْلاَرْضِ {Qur’an 24:35}

Kisha ataona kwa jicho la moyoni kwamba mambo yaliyopita siyo kaburi kubwa; ambako vikundi vya roho zilizotakaswa ambazo kila karne baada ya kutakasa shughuli zao za kuabudu chini ya uongozi wa Nabii au waja wake wema huongoza wadhifa ule mtukufu na huisambaza na kuthibitisha nguzo zake kwa raia katika hali ya ukamilifu, baada ya kundi hili kubwa la watu hawa wenye roho safi katika kutekeleza majukumu yao ya kimaisha na kimaumbile hupaa katika mastakimu yaliyonyanyuliwa na kurejea kutamka

اَللَّهُ اَكْبَرُ

(Allah (sw) ni mkuu kuliko chochote) zikipasua pazia za mustakbali. Na pindi anapogeuka kushotoni mwake, kwa mbali anaona (kwa miwani ya nuru ya imani) kuwa kule kwenye mastakimu yaliyonyanyuliwa, wakiendelea kwenye yaliyopita wakiendelea kwenye ya zamani.

Atatazama upande wa kushoto, na kwa kutumia nuru ya imani abainishe kule mbali mahali pa kufanyia karamu pa Mwenye Huruma zaidi kuliko wote iliyopangwa mahali pa upeo wa furaha kwenye mabustani ya peponi, mbele zaidi ya mageuko kutoka maisha ya Barzakh na yale ya akhera. Na atatambua kwamba dhoruba na matetemeko ya ardhi na matukio ya tufani yote ni maafisa watii; na ataelewa kuwa mifano ya mvua, vimbunga, katika matukio, ni njia ya mfano ya hekima ambayo ingawa yaonekana ni kali lakini ni ya upole kabisa.

Na hata ataona kifo kuwa ni utangulizi wa maisha ya milele, na kaburi, mlango wa furaha ya milele. Wewe unaweza kufikia uhitimisho wa mengineyo zaidi kwa ajili yako mwenyewe. Utumie kipimo hicho! kwenye ulinganisho.

NUKTA YA TATU

Imani ni vyote, nuru na nguvu. Naam, yeyote anayeipata imani ya kweli huweza kuukabili ulimwengu mzima, na kuepushwa dhidi mashinikizo ya matukio, kwa mujibu wa nguvu ya imani yake. Huku akisema

تَوَكَّلْتُ عَلَى اَللَّهِ

“Namtegemea Allah (sw)”, husafiri katika meli ya maisha kwa usalama kamili, kati ya mawimbi makali kama vile milima. Hukabidhi mizigo yake yote kwenye mkono wenye Uwezo wa Yule Mmoja Mwenye Nguvu kabisa, husafiri humo duniani kwa raha mustarehe, kisha hupumzikia katika Barzakh na hustarehe. Baadaye aweza kuruka kwenda Peponi kuingia kwenye furaha ya milele.

Vinginevyo, ikiwa hamtegemei Allah (sw), badala ya kuruka, mizigo ya duniani itamburuza chini mpaka chini kabisa kuliko walio chini. Hivyo ni kusema kuwa imani inalazimu ridhaa ya Tawhidi (Kumpwekesha Allah (sw), inalazimu kujisalimisha kwa Allah (sw), na kujisalimisha kwa Allah (sw) hulazimu kumtegemea Allah (sw), na kumtegemea Allah (sw) inaweza kupelekea furaha katika dunia hii na ijayo. Lakini usielewe vibaya hii kumtegemea Allah (sw) siyo kukataa sababu moja kwa moja, bali ni kujua kwamba sababu ni pazia kwenye mkono wa uweza wa Kiungu. Kujua kuwa kujaribu sababu ni aina ya swala kiutendaji, ni kutafuta athari kutoka kwa Allah (sw). (Mweza wa kila kitu), kutambua kuwa matokeo hutoka Kwake Peke Yake tu, na kumshukuru Yeye.

Wale wanaomtegemea Allah (sw) na wale wasiomtegemea, wanafanana na watu wawili katika hadithi hii: “Wakati mmoja watu wawili walibebesha mizigo mizito migongoni na vichwani mwao, wakanunua tikiti na wakapanda meli kubwa, mara walipokwishaipanda, mmoja wao aliiacha mizigo yake juu ya meli na akaikalia juu yake ili kuilinda, yule mwingine, kwa kuwa alikuwa mpumbavu na mwenye kujivuna, hakuweka chini mizigo yake, alipoambiwa, “Iweke hiyo mizigo yako juu ya meli ili ustarehe.” Alijibu, “Hapana, sitoiweka mizigo yangu chini, kwani yaweza kupotea, mie nina nguvu, nitailinda mizigo yangu kwa kuibeba kichwani na mgongoni kwangu, akaambiwa tena, “meli hii ya mfalme inayokuchukua wewe na sisi ina nguvu zaidi, na yaweza kuilinda mizigo yako vizuri zaidi kuliko wewe, unaweza kupata kizunguzungu na ukaangukia baharini pamoja na mizigo yako, kwa vyovyote vile wewe baadaye utapoteza nguvu zako, na polepole hiyo mizigo yako itakuwa mizito zaidi, na mgongo wako uliokunjana na kichwa chako kisicho na akili hakitakuwa na uwezo wa kuihimili.

Na kama Nahodha akikuona hivyo, ama atasema wewe ni mwehu na akufukuze kutoka kwenye meli yake, au atafikiri huna shukrani kwa kuishutumu meli yake na kutuzomea sisi, na ataamuru utiwe jela, pia unajionesha kuwa wewe ni mwehu mbele ya watu, watambuzi wanaoelewa kuwa unaonesha uzembe kupitia majivuno yako, kutokujiweza kwa lolote kupitia kujisingizia usivyokuwa, na umejifanya mwenyewe mbele za watu kuwa kichekesho na kuonekana dhalili, kila mtu anakucheka. Maneno haya yalimfanya huyu mtu asiye na bahati arejeshe akili zake timamu.

Akaweka mizigo yake chini juu ya meli na akaikalia. Akawaambia wenziwe, “Ah! Allah (sw) awe radhi nanyi’’ nimeokolewa kutokana na adha ile, na kifungo kile, na kudharaulika.”

Ewe mtu uliye mbali na Allah (sw)! Wewe pia rejea kwenye akili zako timamu utawakkali kwake (kumtegemea) Allah (sw) kama mtu yule na umuamini yeye, ili uepuke kuombaomba mbele ya viumbe vyote, kuwa na hofu mbele ya kila tukio, iokoe nafsi na ria na istihzai na tabu ya milele na minyororo ya dhiki duniani.

NUKTA YA NNE

Imani humfanya mtu kuwa mtu, na hakika humfanya mtu kuwa mfalme. Kwa kuwa hivi ndivyo ilivyo, wajibu wa mtu wa msingi ni “kumuamini Allah (sw) na kumuomba yeye”. Utovu wa imani humfanya awe mnyama wa porini.

Kati ya maelfu ya thibitisho za jambo hili, tofauti kwa jinsi wanyama na mwanadamu huja humu duniani ni dalili za wazi na uthibitisho kamili.

Naam, hakika tofauti kati ya mwanadamu na mnyama katika kuja kwao duniani, zinadhihirisha kwamba ubinadamu huja ukawa ubinadamu kupitia imani. Kwani pale wanyama hawa wanapoingia duniani huja kamili kwa mujibu wa uwezo wake, kama vile kwa kawaida ameshakamilika katika dunia nyingine, kwa hivyo hujifunza hulka zote za maisha yao, mahusiano yao na ulimwengu, na sheria za maisha ndani ya saa mbili, au siku mbili, au miezi miwili, na hivyo hupata kipawa hicho; kidege kidogo au nyuki kwa mfano; hupata uwezo katika maisha yake na tabia katika matendo yake kwa njia ya ilhamu kutoka kwa Allah (sw) na uongofu wake, hayo huyapata kwa siku ishirini tu, ambapo mwanadamu huyapata kwa miaka ishirini.

Yaani wao hutiwa ilhamu na Mwenyezi Allah (sw), hii maana yake ni kwamba kazi ya msingi ya wanyama siyo kukamilishwa kwa kupitia mafunzo na maendeleo kwa kupata elimu, wala kutafuta msaada na kutoa maombi kwa kudhihirisha kwao wao wenyewe, bali kwa uwezo wao wa kufanya kazi na kutenda, kazi yao ni kufanya kazi ya kuabudu kiutendaji.

Ama kwa mwanadamu, anahitaji kujifunza kila kitu anapoingia duniani, yeye huwa hajui chochote na hawezi hata kujifunza kikamilifu masharti na kanuni za maisha ndani ya miaka ishirini, hakika anahitaji kuendelea kujifunza mpaka mwisho wa maisha yake, tena yeye huletwa duniani akiwa katika hali ya lolote, naye hawezi kusimama kwa miguu yake mwenyewe isipokuwa baada ya miaka miwili, ni pale afikishapo miaka kumi na tano tu ndipo anaweza kubainisha kati ya madhara na faida, wala hawezi kufanikisha kwa nafsi yake manufaa wala maslahi katika maisha yake au kujizuia na madhara ila kwa kushirikiana na wengine kwa kuingiliana nao katika maisha ya kijamii.

Hii maana yake ni kuwa wajibu wa mwanadamu ni kukamilishwa kwa njia ya kujifunza, na kutangaza kumuabudu Allah (sw) na kumtumikia Yeye kupitia dua, hii ni kusema kwamba, ni kujua majibu na njia ya maswali: “Kupitia kwa huruma ya nani maisha yangu yanasimamiwa kwa machungo haya yenye hekima namna hii?” Kupitia kwa ukarimu wa nani unaonilea kwa wema namna hii? Kupitia uhisani wa nani unaonifunza kitaratibu na kulelewa kipole namna hii?” Na uwepo wa nani ninalishwa kwa sura hii ya riziki? Hivyo basi huona kwa wadhifa wake ni kuomba na kujidhalilisha na kutegemea na kutaraji kwa ndimi ya ufukara na unyonge kwa mwenye kukidhi haja zake, na hili lina maana kuwa wadhifa wake ni kupaa juu kwa mbawa zake ‘Unyonge na ufukara’ katika mastakimu ya uja wa juu.

Hii inamaanisha kwamba mwanadamu alikuja huku duniani kukamilishwa elimu na maombi, kuhusu asili na uwezo kila kitu kimefungiwa kwenye elimu, na msingi, chanzo, nuru, na roho ya elimu ya kweli yote ni elimu ya kumjua Allah (sw) kama ambavyo msingi wa hili ni imani ya Allah (sw).

Isitoshe, kwa kuwa mwanadamu hukabiliwa na matatizo yasiyo na mwisho, na hudhuriwa na maadui wengi mno juu ya kwake kusipokuwa na mipaka, na anataabika kwa mahitaji yasiyokuwa na mwisho, na ana matamanio mengi mno juu ya ufukara usiyo mipaka, baada ya imani, kazi yake ya asili ni dua, ama kuhusu maombi, huo ndiyo msingi wa kumwabudu Allah (sw) na kumtumikia Yeye, ili kupata tamanio au mahitaji asiyoweza kuyapata, ama mtoto atayalilia au atayaomba, yaani ataomba kwa ulimi kupitia ulimi wa kutokujiweza kwake, ama kwa vitendo au kwa maneno, na atafaulu katika kuyapata, kwa njia hiyo hiyo, mwanadamu ni kama mtoto laini na mdekaji katika dunia ya viumbe hai, ama atalia na kuegemea kwa Ar-Rahiim (Mwenye huruma kuliko wote) kupitia udhaifu na kutokujiweza mwenyewe, au afanye maombi kupitia ufukara wake na mahitaji yake, ili vitu anavyovihitaji avipate kwa ajili yake, na hapo basi atakuwa ametekeleza maombi na dua yake. Vinginevyo, kama mtoto mjinga anayefanya ghasia akisema kwa majivuno, “kwa nguvu zangu mwenyewe huvishinda vitu ambavyo haiwezekani kuvishinda na vitu ambavyo vina nguvu zaidi ya mara elfu, nami huvifanya vinitii mimi kupitia fikra na vipimo vyangu.”, huonesha kutokushukuru kwa zawadi, na kama hii ilivyo kinyume cha asili ya kuzaliwa, kwa hiyo hujifanya yeye mwenyewe astahili adhabu kali.

NUKTA YA TANO

Kama ambavyo imani hupelekea katika ‘dua’ na huichukulia kama ni nyenzo yenye kukata; na wasita baina ya muumini na Mola wake na kama ambavyo fitra ya mwanadamu hutweta kwa shida na shauku, vivyo hivyo Allah (sw) vile vile humtaka mwanadamu katika jambo lenyewe kwa kauli ya:

قُلْ مَا يَعْبَؤُا بِكُمْ رَبِّى لَوْلاَ دُعَاؤُكُمْ{Qur’an 25: 77}

Ambayo ina maana ya: “Umuhimu gani utakaokuwa nao wewe ikiwa hukuniomba Mimi?”

Pia Anaamuru:

اُدْعُونِى اَسْتَجِبْ لَكُمْ{Qur’an 40: 60}

Utakaposema: “Mara nyingi sisi huomba dua, lakini hatukubaliwi, lakini aya ni ya kijumla, inasema kuwa kila ombi, huitikiwa”.

Jibu: Kujibu ni kitu kimoja, kukubali ni kitu tofauti kabisa. Kila dua hujibiwa, lakini kule kujibiwa kwake, na kitu kilichoombwa kupewa hutegemea hekima ya Allah (sw) Mwenye Nguvu zote, kwa mfano, endapo mtoto mdogo atapiga kelele kwa daktari na kusema: “daktari! daktari!

Niangalie mimi na unichunguze” naye hujibu: “niko hapa, unataka nini? Na mtoto aseme, “nipatie dawa ile”, daktari ama atampa dawa ile ile aliyoiomba au dawa bora zaidi na yenye faida kubwa zaidi kwake, au akijua kwamba dawa ile ina madhara kwa ugonjwa wake, hatompa chochote nayo ni kulingana na muktadha wa hekima na maslahi ya mtoto.

Kwa hiyo Mwenyezi Allah (sw) Mtukuka ni mwenye hekima wa jumla na mchunguzi mwenye kuhesabu na kutosheleza wakati wote, hujibu dua za mja Wake, kupitia uwepo wake na itiko lake, hugeuza kuachwa kwa upweke wake na upweke kuwa mazowea, lakini hufanya hivi siyo kwa mujibu wa kigeugeu na matakwa ya king’ang’anizi cha kibinadamu, lakini kwa mujibu wa matarajio ya hekima ya Kiungu. Yeye hutoa kile kilichoombwa au kilicho bora zaidi kuliko kile, au hatoi chochote kabisa.

Pia maombi ni aina ya ibada na utambuzi wa utumishi wa mwanadamu kwa Allah (sw) na matunda yake ni akhera, ama makusudio ya kidunia yana nyakati zake na aina makhususi za maombi na ibada na sio ukomo wa malengo yenyewe, kwa mfano swala na dua kwa ajili ya kuomba mvua ni aina ya ibada na hali ya ukame ndio hupelekea watu kufanya ibada kama hii. Ibada na dua za aina hii siyo kwa ajili ya kuleta mvua, iwapo zinafanywa kwa nia hiyo pekee, hazistahili kukubaliwa, kwani siyo ibada halisi kwa ajili ya Allah (sw), machweo ni wakati wa swala za jioni. Na kupatwa kwa jua na mwezi ni nyakati za aina mbili za swala ziitwazo swalat al-kusuf na swalat al-khusuf, hiyo ndiyo kusema kwamba, kwa kuzitia pazia hizo ishara mbili zinazong’aa za usiku na mchana ukubwa mno wa Allah (sw) hutangazwa, kwa hiyo Al-Qaadir (Allah (sw) ni Muweza wa kila kitu) huwaita waja wake kwa aina ya ibada nyakati hizo.

Swala hizo siyo kwa ajili jua na mwezi zitadhihirishwa ambazo kuonekana kwake na kupatwa kwake kwa njia yoyote kutaendelea kuhesabiwa na wanafalaki. Kwa njia hiyo hiyo ni wakati wa swala za mvua, na kuenea na watu kupatwa na maafa na madhara ni nyakati za dua maalum ambapo mwanadamu hutambua kwake, na kupitia maombi yake na kubembeleza anaomba makimbilio kwenye mahakama ya Yule Mmoja Anayemiliki Uwezo mkubwa kabisa.

Hata kama maafa hayajaondoshwa juu ya maombi mengi, haiwezi kusemwa kwamba hayajapokelewa. Bali na isemwe kwamba wakati wa maombi haujamalizika. Iwapo kupitia madaha yanayovutia na ukarimu mkubwa, Al-Qaadir Allah (sw) Mwenye uweza wote huondosha balaa, nuru juu ya nuru, basi wakati kwa yale maombi umekwisha, hiyo ndiyo kusema kwamba, maombi huwa na maana ya ibada na mwanadamu kukiri utumishi wake kwa Allah (sw) na kwa dua hii ni siri miongoni mwa siri za uja.

Ama kwa ibada na utumishi wake kwa Allah (sw) ni sharti iwe kwa ajili ya Allah (sw) kidhati na kiaminifu, mwanadamu sharti atangaze kwake na aombe makimbilio Kwake kupitia dua, asiingilie kati kwenye Uungu Wake, lazima awache uchukuaji wa hatua Kwake na ategemee Hekima Yake, kamwe asishutumu Huruma Yake.

Naam, kwa hakika vimethibiti kupitia dalili mbali mbali zilizo wazi kuwa vilivyomo humtakasa Allah (sw) kila kimoja hutakasa kivyake, katika ibada maalum, katika kusujudu kwake kwa aina yake, aina za ibada hizi makhususi zisizo na hesabu hadi kupanda kwa Mahakama ya Kiungu kutoka katika ulimwengu wote ni maombi.

Ama kupitia na uwezo wake, kama vile dua ya mimea na wanyama wote, ambapo kila kimojawapo kinataka kutoka katika utoaji usio na mipaka ambayo ni sura fulani yenye maana katika majina yake matukufu.

Ama kupitia ndimi ya mahitaji yao ya kimaumbile kama vile dua za viumbe vyote hai kupata mahitaji yao ya msingi ambayo yapo nje ya uwezo wao, hivyo kila kiumbe hai kinaomba kutoka kwa Al-Wahaab Mwingi wa kheri na kutoa, kwa ndimi ya haja zake za kimaumbile vitu vitakavyomuwezesha kuwepo kwake ambayo ndio riziki yake.

Au ni maombi kupitia kwa ulimi wa kidharura, ambayo kupitia viumbe vyote vyenye roho ambao hujikuta wamo katika hali ngumu au tatizo husoma dua na huomba makimbilio ya haraka kwa mlinzi asiyejulikana, na kwa yakini humgeukia Mlezi wenye upendo wote. Ikiwa hakuna kitu cha kukataza hilo, aina hizi za maombi hukubaliwa kila mara.

Aina ya nne ya maombi inafahamika sana; ni maombi yetu, hii pia ina aina mbili, moja ni kiutendaji na kwa silika, na nyingine, kwa maneno pamoja na moyo.

Kwa mfano kuchagua sababu ni swala ya kiutendaji, kukusanya pamoja na sababu siyo kwa ajili ya kutengeneza athari, bali kupitia ulimi wa silika kuchukua nafasi inayokubalika ili kuomba athari kutoka kwa Al-Qaadir (Allah (sw) ni Muweza wa kila kitu), hata kulilima shamba ni njia ya kupiga hodi katika mlango wa hazina ya huruma. Kwa kuwa aina hii ya maombi ya kivitendo yanapelekwa kwa jina na cheo cha Al-Jawad (Yule Mmoja Mkarimu Kabisa), hukubaliwa kwa takribani kesi zote.

Aina ya pili: Ni kutoa ombi kwa ulimi na moyo, na kuomba matakwa ambayo mkono hauwezi kuyafikia, kipengele muhimu kuliko vyote, nia nzuri kuliko zote, tunda tamu kuliko yote la hii ni hii: “Yule anayetoa maombi, anafahamu kwamba Yupo Mmoja Ambaye Anasikia matakwa ya moyo wake, Ambaye Mkono Wake unaweza kufikia vitu vyote, Ambaye Anaweza kuleta kila moja la matakwa yake, Ambaye Hukuonea huruma kwake, na Hujibu ufukara wake.”

Ewe mtu muhitaji usiyejiweza wewe mwenyewe! Usipuuze njia kama maombi, ambayo ndiyo ufunguo wa hazina ya huruma na wa nguvu zisizomalizika. Ing’ang’anie hiyo! Panda mpaka katika kilele kirefu zaidi kuliko vyote vya kibinadamu! Weka katika maombi yako pamoja na ya ulimwengu wote, kama mfalme! Sema:

Kama mtumishi na msaidizi anayewakilisha ulimwengu wote! uwe katika sampuli nzuri zaidi kuliko zote za maumbile.

KIPAMBANUZI CHA PILI

Kinajumuisha kauli tano zinazoelezea furaha na mateso ya mwanadamu.

Kwa hakika mwanadamu ameletwa kwenye dunia hii, akiwa hajimudu na hana uwezo, lakini kwa matokeo ya maumbile yake na maajabu ya sanaa ya uumbaji; njia mbili zikafunguliwa mbele yake ambazo akizifuata ima zitamnyanyua au kumuangusha pasipo na mwisho; amewekwa katika uwanda wa majaribio na mtihani ambamo anaweza kupanda au kuanguka hadi kwenye vituo, vyeo, na madaraja ya chini sana kuliko yaliyo chini, mpaka kwenda juu sana kuliko yaliyo juu, kutoka kitandani mpaka kwenye kiti cha enzi cha Kiungu, na kutoka kwenye punje ndogo sana mpaka kwenye jua, dunia hii imepanuliwa kwake katika kufuata moja ya njia mbili isiyo na ukomo katika kupanda na kushuka, na kwa sababu ameumbwa kwa umbile lililo bora kabisa; na akapewa matayarisho yaliyokusanya mengi.

Kwa hili tutabainisha siri ya maendeleo ya mwanadamu, na kurudi kwake kuwa chini, katika ‘Kauli’ tano:

KAULI YA KWANZA

Mwanadamu ni mwenye kuhitajia aina nyingi za mahitaji ya viumbe ulimwenguni na ameunganishwa nazo. Mahitaji yake yanasambaa kupitia kila sehemu ya dunia, na matamanio yake huenea daima dawama, kama anavyotaka huwa, ndivyo hutaka majira ya kuchipua kama anavyotamani bustani, ndivyo pia hutamani pepo ya milele, kama anavyopendelea kumwona rafiki, ndivyo anavyotamani kumwona Mwingi wa uzuri wa utukufu peponi, kama anavyopenda kumzuru mmoja anayempenda anayeishi mahali kwingine, basi hutarajia mlango wa mpenzi wake ufunguliwe kwa ajili yake yeye, ili pia apate kuwazuru tisini na tisa (99) ya mia ya rafiki zake ambao wameshasafiri kwenda katika ulimwengu wa Barzakh ili aepuke na kutenganishwa milele, anatarajia kuomba makimbilio kule katika Ikulu ya Yule Mmoja Mwenye Nguvu sana kabisa, kwani ni Yeye Ndiye Atakayeufunga mlango wa dunia hii kubwa na Aufungue mlango wa akhera, ambao ni maonesho ya maajabu, aondoshe dunia hii na aweke akhera mahali pake ili amuokoe mwanadamu huyu maskini kutokana na maumivu ya kutenganishwa milele.

Kwa hiyo, hapana anayefaa kuwa ni mwenye kuabudiwa kwa mwanadamu katika hali yake hii, isipokuwa ni Yule Mmoja ambaye mkononi mwake ndimo hatamu za vitu vyote, ambaye kwake Yeye ziko hazina za vitu vyote, anayeona vitu vyote, na aliyeko kila mahali, ameepukana na kutokujiweza, hana makosa, na yuko mbali sana na kasoro zote ni Mmoja Mwenye Nguvu zote za Utukufu, Mmoja Mwenye Huruma zote wa Uzuri wote, Al-Hakiim Mmoja Mwenye Busara na Ukamilifu.

Na hilo ni kwa sababu hakuna anayeweza kutekeleza haja za watu na matarajio yao yasiyo na ukomo isipokuwa ni kwa Yule mwenye uwezo usio na ukomo na mwenye elimu enevu isiyo na mpaka kwani hastahiki kuabudiwa isipokuwa yeye.

Ewe mtu! kama wewe ni mtumishi wa Yeye peke Yake, utastahili mahali palipo bora kuliko viumbe vyote, lakini ikiwa unajizuia kuwa katika utumishi huu Kwake Yeye, utakuwa mtumwa uliyedunishwa kwa wale viumbe wasiojiweza wenyewe, iwapo utategemea nafsi yako na nguvu zako mwenyewe na uwache kumtegemea Allah (sw) na kutawakkali kwake na kuomba dua, kisha ufuate njia ya kujiona na kujivuna, basi utaangukia chini kuliko chungu au nyuki kuhusiana na wema na uumbwaji, na uwe dhaifu kuliko buibui au nzi. Utakuwa mzito kuliko mlima kuhusu uovu na uharibifu, na mwenye madhara zaidi kuliko tauni.

Ndiyo, ewe mwanadamu! Una vipengele au sura mbili: Mosi ni ile ya uumbaji, vyema, na matendo chanya, ya pili ni uharibifu, uovu, ukanaji na maono, katika hali hizo wewe uko chini kuliko nyuki au jurawa, na dhaifu kuliko buibui au nzi kwa upande wa kwanza.

Ama upande wa pili wa uharibifu ni kwa uwezo wako, unaipita milima, ardhi, na anga, unachukua mzigo ambao uliwashinda wengine ambao walikiri kutouweza, na wewe unajichukulia eneo pana na kubwa zaidi kuliko wao, kwani wewe unapofanya kwa jitihada na uwezo wako, unaweza kufanya vizuri kadiri za nguvu, uwezo na mkono wako unapoweza kufikia, lakini unapotenda maovu na maangamizi, basi maovu yako hushinda kabisa na maangamizi husambaa sehemu zote.

Kwa mfano, kufuru ni uovu, uharibifu, kukosekana kwa uthibitisho, lakini uovu huu mmoja unatukana ulimwengu mzima, kudharau majina yote ya Kiungu, na kuutukana utu na ubinadamu wote, kwani hivi viumbe vina hadhi ya juu na kazi za maana, wao ni barua za Kiungu, vioo vya Kiungu, na maafisa wa Kiungu, lakini kufuru huwafukuza kutoka katika vyeo vyao vya kuwa vioo, maafisa waliyopewa kazi, na vinachukua maana, na huwapunguza wao hadi kwenye daraja la asiyefanya lolote la maana na huwa vitu vinavyochezewa kwa bahati, na kupitia maangamizi ya kifo na utenganisho, huwashusha wao hadi kwenye daraja la kuwa vitu vinavyooza haraka vinavyokosa kuwa vya maana na thamani, hadi kuwa si kitu.

Na wakati huo huo, hukana majina yote matukufu na huyapuuzia, majina yale ambayo nakshi zake zinaonekana na uzuri wake katika kioo cha viumbe vyote, hata kile kinachoitwa ‘utu’ ambao ni utenzi wa busara uliotungwa vizuri, unaotangaza utukufu wa majina matukufu nao ni muujiza mkubwa kama vile mbegu za mti wa milele.

‘Utu’ huu hutupwa na ukafiri katika sura yake iliyo hai ambayo ipo juu ya ardhi, milima, anga, kwa kilichokuwa katika mabega yake amana kubwa kiasi cha kufadhilishwa juu ya malaika na akapata ukuu na kuwa mwenye hadhi ya ukhalifa ardhini na hutupwa kutoka katika kilele hiki cha hadhi na cheo cha juu hadi kwenye udhalili wa chini katika sura yenye kuchukiza, mbaya zaidi yenye kupotea haraka na kubadilika.

Matokeo yake kwa kifupi: Ni kuwa Nafsi inayoamuru maovu inaweza kutenda makosa Ya jinai yasiyo kikomo, lakini kuhusu uundaji na wema, uwezo wake ni mdogo mno na wa sehemu moja, katika kupata na katika mambo ya kheri, naam, mwanadamu anaweza kuvunja nyumba kwa siku moja tu, ingawaje anaweza asikamilishe kwa kujenga kwa miaka mia moja.

Ama mwanadamu atakapoacha ubinafsi, na akaomba na kutafuta kheri na uwepo kwa tawfiki ya Allah (sw), na akamtegemea yeye na akawa mbali na shari na uharibifu na akaacha kufuata matamanio ya nafsi yake, akaukamilisha uja wake kwa Allah (sw) akiwa ni mwenye kutubia na kufanya istighfaar huku akimdhukuru Allah (sw), atakuwa ni mwenye kudhihirisha aya hii tukufu ifuatayo:

يُبَدِّلُ اللّٰهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ{Qur’an 25: 70}

Uwezo wake usiyo kikomo wa maovu, utabadilishwa kuwa uwezo usiyo na kikomo cha mema, itapata thamani ya ‘umbo lililo bora kabisa’ na ipande mpaka kufika juu kabisa kuliko juu zote.

Ewe mtu uliyeghafilika! Tazama upaji mkubwa na ukarimu wa Allah (sw) Mwenye Nguvu zote, ingawa itakuwa ni haki kwa uadilifu ovu moja kuandikwa maovu mia moja, na jema moja kuandikwa jema moja, au lisiandikwe kabisa kwani kheri yake na maslahi yake hurejea kwake yeye mwanadamu, hata hivyo kwa utukufu na uwezo wake anaandika ovu moja kwa ovu moja na jema moja analipa kwa kumi mfano wake au sabini au mia saba au mara elfu saba mfano wake.

Ninafahamu kwa kauli hii kuwa kuingia jahannam ni malipo ya matendo na ni uadilifu na haki kabisa, ama kuingia peponi ni fadhila za kiungu na ukarimu halisi na rehema haswa.

KAULI YA PILI

Mtu ana nyuso mbili:

Mosi: Ubinafsi katika maisha yake duniani.

Pili: Unyenyekevu unaoendelea hadi maisha ya milele.

Kuhusu uso wa kwanza ni kiumbe masikini mwenye utashi mdogo kama vile unywele na mwenye kuwa chini ya kudura mwenye udhaifu, na katika maisha yake hapa duniani ana mwenge ambao hauishi kuzimika na umri wake ni mdogo wenye kupita kama pepeso la jicho, na uwepo wake ni kiwiliwili chenye haraka na kupotea. Pamoja na haya yote mwanadamu ni mtu mwema, mnyonge miongoni mwa viumbe anuwai wasio na hesabu.

Ama Kuhusu uso wa pili na hususani kutokujiweza kwake na ufukara wake ambao umegeuziwa kwenye upande wa kuabudu, hakika mtu anayo mapana makubwa sana na umuhimu mkubwa, kwani Aliye na Busara zote Muumba amejumuisha katika asili ya mtu kutokujiweza kwa hali ya juu mno na ufukara mwingi mno usio na mipaka, ili awe ni kioo kilichokuwa na ishara zisizohesabika za huyo Mmoja Mwenye nguvu na huruma ambaye nguvu zake hazina mwisho, na Mwingi wa ukarimu na utajiri wote zisizokuwa na mipaka.

Naam, mtu hufanana na mbegu, mbegu hii imepewa uwezo mkubwa na nguvu za Kiungu na programu yenye thamani, ngumu kutambulika na zimepewa kwa Kadari ya Kiungu, ili iweze kufanya kazi chini ya ardhi, na iibuke kutoka kwenye dunia ile nyembamba yenye kiza, iingie kwenye dunia pana ya hewa, na mwishowe atawassali na kunyenyekea kwa Muumba wake kwa ulimi wa matayarisho ya utayari kwa kuwa mti, ipate ukamilifu inayostahili.

Iwapo, kwa sababu ya silika mbaya, mbegu inatumia mada yenye madhara isiyokuwa na ubora wavivutie vitu fulani vyenye madhara chini ya ardhi, baada ya muda mfupi hudhoofika na kuoza katika pale mahali pembamba bila faida, lakini ikiwa mbegu itafuata amri ya uumbaji ya mpasuaji mbegu na kokwa na ikatumia programu ile ya matayarisho kwa matumizi mazuri, basi utaibuka kutoka kule kwenye dunia nyembamba, na kupitia kuwa mti mkubwa unaozaa matunda, na ukweli wake mdogo mahususi, na roho yake itachukua umbile kubwa la ukweli wa kilimwengu.

Ikiwa mbegu hali yake ni hii, kadhalika mwanadamu, kwani amewekewa nyenzo muhimu kutoka kwenye nguvu za kiungu na programu zenye thamani zimewekwa katika asili ya mtu na nguvu za Kiungu na kadari, endapo mtu atatumia vibaya na kwa makosa uchaguzi na hiari yake na akapelekea kuacha kutumia vipawa vyake na hivyo kuwa chini ya starehe ya maisha ya dunia na ulimwengu wa dhiki wa ardhini ataoza na atageuza hali yake ya asili katikati ya matatizo katika maisha mafupi mnamo mahali palipobinywa kama mbegu iliyooza, na aibebeshe uwajibikaji roho yake isiyo na bahati, kisha ajiondokee kutoka kwenye dunia hii.

Lakini hata hivyo akitunza mbegu kwa uwezo wake na kuimwagia kwa maji ya Kiislamu na nuru ya imani yake chini ya ardhi ya kuabudu na utumishi kwa Allah (sw), aifuate amri ya Qur’an, na ageuze ustadi wake kwenye lengo lake halisi, watazalisha matawi na chipukizi katika ulimwengu wa Barzakh na akhera na peponi neema na ukamilifu usio na ukomo.

Naam, maendeleo ya kweli ni maelekezo ya moyo, siri, roho na akili na hata fikra na nguvu zingine alizopewa mwanadamu, katika maisha ya milele yenye kudumu, na kushughulishwa na kila kimoja kwa kile chenye kuhusu na kuinasibu miongoni mwa wadhifa wa uja, ama yale wanayodhania waliopotoka katika kuzama katika starehe ya maisha ya dunia na ladha zake duni zenye kupita bila kuelekea kwenye uzuri wa yote na starehe zenye kudumu milele wakitumia moyo, akili na mambo mazuri ya mwanadamu chini ya maamrisho ya nafsi yenye kuamrisha maovu na kuyatumia zote kuihudumia hali hii haina maana ya maendeleo yoyote, bali huku ni kushuka na kudondoka.

Niliuona ukweli huu katika maono ambayo yanaelezwa katika ulinganisho ufuatao: Nilikuwa naingia katika jiji kubwa, nilipotazama nikaona lilikuwa limejaa kasri nyingi kubwa zenye ghorofa kubwa, katika milango ya baadhi ya hizi kasri, kulifanywa sherehe za furaha kama nyumba zinazong’ara za maonesho ya tamthilia iliyowavuta na kushikilia usikivu wa kila mtu na walikuwa wanastareheshwa.

Nilitazama kwa makini nikaona kuwa bwana wa kasri kama hiyo alikuja mlangoni alikuwa anacheza na mbwa. Wasichana walikuwa wakicheza na wavulana wasio maharimu wao, ama wanawake watu wazima walikuwa wanasimamia michezo ya watoto, na mlinda mlango (bawabu) alikuwa akiwaongoza watu, nikatambua kuwa ndani ya hilo kasri kulikuwa tupu, kazi zilizorembeshwa zote zilibakia hazifanywi. Maadili ya watu wale yalikuwa mabaya na dhamira zao zilikufa, akili na nyoyo zao zilikuwa tupu wakawa ni kama wanyama wakicheza kwenye kasri.

Kisha nilikwenda mbele na ghafla nikaliona kasri lingine, nilimuona mbwa mwaminifu amelala mlangoni akiwa ni mpole mwenye heshima, kasri hili halikuwa na mvuto wowote, nilishangazwa na utulivu huu na ukimya huu! Nikaulizia sababu na nikaingia ndani ya kasri nikakuta watu wengi, wenye nyadhifa mbali mbali na majukumu yanayofanywa na watu wa kasri ile, kila mmoja yupo kwenye ghorofa lake wakiwa na furaha na kazi zao kiasi cha kuleta katika nyoyo furaha.

Chumba cha juu kilikuwa na watu wenye shughuli nyingi zinazohusu kazi zao tofauti zilizoboreshwa. Wanaume walioko katika chumba cha kwanza walikuwa wakisimamia utawala na uendeshaji wa kasri, katika chumba juu ya hiki, wasichana walikuwa wakiwafunza watoto, juu ya hicho chumba wanawake walishughulika na sanaa za kupendeza na tarizo nzuri sana, na kwenye ghorofa ya juu bwana alikuwa anaongea kwa simu na mfalme, na akishughulika sana na kazi yake mwenyewe ili kudhibiti ushwari wa watu na upatikanaji wa maendeleo kwa watu wa kasri ile na kila mmoja akifanya kazi kulingana na ujuzi wake kwa ukamilifu unaotakiwa.

Hawakunizuwia mimi kwa kuwa sikuwa naonekana, na niliweza kuzunguka mle, baadaye nilikwenda nje nikaendelea kutazama: Kila mahali mjini kulikuweko hizi aina mbili za kasri, niliuliza juu ya hizi kasri na wakaniambia:

“Mahala ambako kulikuweko na starehe milangoni, na ambamo ndani yake ni tupu, zilimilikiwa na viongozi wa kufuru na upotofu, ama aina ya pili ya kasri ni za viongozi wa waumini wenye wivu na utu.

Halafu katika kona moja, niliikuta kasri lililoandikwa jina langu juu yake (Said), nikashangazwa na hilo, nilipoangalia kwa kina zaidi nikaona kama vile sura yangu inaniangalia, nikapiga yowe kwa mshangao ule nikarejesha akili yangu na kuzindukana. Na sasa nitakutafsirieni.

Mji ulikuwa maisha ya kijamii ya kibinadamu, na jiji lilikuwa la ustaarabu wa kibinadamu, kila kasri lilikuwa ni binadamu. Watu wa kasri zile walikuwa ni kama viwiliwili vya mwanadamu na milango yake ya fahamu kama vile macho, masikio, moyo, moyo wa ndani, roho, akili, na vitu kama roho, na mawazo ya ghafla, na nguvu za matamanio na ghadhabu ya mwili.

Kila kipawa cha mwanadamu kina kazi tofauti za kuabudu, na raha na maumivu tofauti. Ama nafsi na matamanio na nguvu ya matamanio na ghadhabu ni mfano wa mlinzi mlangoni na Yule mbwa wake. Hivyo basi kuwa chini ya maadili yale mema chini ya maamrisho ya Nafsi yenye matamanio bila shaka hupelekea kuanguka na kuparaganyika na sio kupaa, pima hali kama hiyo sehemu zingine.

KAULI YA TATU

Kwa hakika mwanadamu kulingana na matendo na amali na kuwa msingi wa utafutaji ni hayawani dhaifu, na kiumbe asiyeweza. Kuhusu matendo yake na amali yake na ajira ni mnyama mdhoofu, kiumbe kisichojiweza chenyewe, kiasi cha nguvu yake ya kutumia na umilikaji katika kadhia hii ni nyembamba mno kiasi kwamba siyo kubwa kuliko umbali wa mkono wake utakofikia. Wanyama wanaofugwa, hata usimamiaji (hata hatamu) ambao kapewa mwanadamu, kila moja imechukua hisa ya udhaifu wake, kutokujiweza, na uvivu, kiasi kwamba iwapo watalinganishwa na wenzao wanyama pori tofauti kubwa huonekana. (Kama mbuzi na ng’ombe wanaofugwa, na wale wa porini).

Lakini kuhusu ukimya, kuafiki, dua’, na maombi kwa Al-Kariim Mola karimu katika nyumba ya duniani ambayo amekaribishwa na Yule Mmoja Aliye Mkarimu mno kiasi kwamba hazina nyingi mno za huruma amefunguliwa Yeye, na viumbe vya kipekee vingi sana na watumishi wengi wako chini Yake. Na uwanja wa mviringo mkubwa mno umeandaliwa kwa ajili ya mapumziko, burudani, na faida ya huyo mgeni kiasi kwamba nusu ya kipenyo chake ni kirefu na kipana kadiri ya dhana itakavyoweza kujinyoosha

Kwa hivyo, iwapo mtu atategemea nafsi yake na kufanya ubinafsi, na kuyafanya maisha yake ya kidunia ndiyo lengo lake na matarajio yake na juhudi yao na mbio zake ni kupata anasa za muda wakati anajitahidi sana kutengeneza maisha yake, hudidimiza ndani yake kwenye duara finyu na kutafuta kwake kutakuwa patupu, na vipawa vyake alivyopewa na Mola wake vitashuhudia dhidi yake wakati wa ufufuo na vitalipa kisasi dhidi yake, ambapo iwapo atajua yeye mwenyewe kuwa ni mtu mgeni dhaifu; na atumie mtaji wa maisha yake ndani ya mipaka ya ruhusa na kumridhisha Yule Mmoja Mwenye Ukarimu ambaye ndiye mgeni wake, atakazana kupata maisha marefu milele katika mipaka ile mipana, kisha apumzike na atulie katika maisha ya milele, na huko ataishi kwa salama na amani na atapumua kwa pumzi za watu waliokuwa juu na kufurahi na wakati huo ndipo atakapoweza kupanda juu kuliko walio juu na hapo ndipo vipawa vyake vitamshuhudia huko akhera kwa neema aliyopewa na Allah (sw), vitakuwa radhi naye.

Naam: Bila shaka uwezo wote wapewao watu haukuwa kwa haya maisha ya kidunia yasiyo maana, lakini kwa maisha ya milele yenye umuhimu mkubwa. Kwani tukimlinganisha mwanadamu na wanyama, tunaona kuwa mwanadamu yu tajiri sana kuhusu vipawa na kipaji chake mara mia zaidi kuliko wanyama.

Lakini katika starehe za maisha ya kidunia na katika maisha ya wanyama yeye anashuka mara mia moja chini zaidi, kwani kwa kila starehe anayoipata mwanadamu imo athari nyingi ya maelfu ya machungu, machungu yaliyopita na woga wa yajayo, na machungu kwa kila starehe inayopita, yote hayo yanaharibu maono na ladha na maonyo na huchosha uchangamfu wake, ambapo kila starehe na ladha huacha athari ya maumivu.

Lakini wanyama hawako hivyo, kwani wao hupata starehe bila ya machungu. Huchukua hiyo raha bila ya masikitiko, hata masikitiko ya yaliyopita hayawapi mateso, wala woga wala hayawapi dhiki. Wao huishi kwa amani na hutoa shukurani kwa Muumba wao.

Hii inamaanisha kwamba: Iwapo mwanadamu aliyeumbwa kwa ‘umbo lililo bora kabisa’ anawekea mipaka fikra zake kwa maisha ya dunia hii, hushuka mara mia moja chini kuliko kiumbe kama jaruwa, ingawa yeye yuko juu zaidi kuliko wanyama kulingana na rasilimali zake mara mia moja.

Nilielezea ukweli huu mahali pengine kwa njia ya ulinganisho, na nitaurejea tena kwa mnasaba huu.

Na hivyo basi, mtu mmoja alimpa mtumishi wake dinari kumi; na hivyo kuamuru kutengeneza kivazi kwenye kitambaa maalum, kisha kwa wa pili akampa vipande elfu moja vya dhahabu, na akaweka katika mfuko wa mtumishi karatasi ambayo iliandikwa maneno yenye mahitaji na orodha ya vitu vichache na akaviweka katika mfuko wa mtumishi na akamtuma sokoni, mtumishi wa kwanza alinunua suti nzuri kabisa ya kitambaa kizuri sana kwa vipande kumi vya dhahabu, wakati mtumishi wa pili hakutumia kichwa chake vizuri, na akamuiga yule mtumishi wa kwanza na bila ya kuisoma ile karatasi aliyopewa yenye orodha ya mahitaji, na bila ya kurejea orodha ile aliamua kumpa muuza duka vipande elfu moja vya dhahabu na akamtaka ampe suti kamili ya mwanamume. Muuza duka asiyekuwa mwaminifu akampa suti ya mavazi yenye kiwango cha chini.

Kisha yule mtumishi bazazi alirejea kwa bwana wake na akapewa kemeo kali na adhabu ya kutisha.

Kwa hivyo hata mtu asiye na akili kabisa ataelewa kwamba vipande elfu moja vya dhahabu alizopewa mtumishi wa pili hazikuwa za kununulia suti ya mavazi bali zilikuwa ni za kufanyia biashara muhimu.

Kwa njia hiyo hiyo, kila mtu aliyepewa vipawa hivi utakapolinganisha na kila kimoja alichonacho mnyama itadhihiri kuwa ni chenye uwezo mkubwa zaidi ya mara mia moja zaidi kuliko walivyo wanyama.

Kwa mfano, fikiria uwezo kama macho ya mwanadamu ambayo yanaweza kutambua daraja zote za uzuri, na hisia yake ya ladha, ambayo inaweza kutofautisha mabadiliko yote ya ladha mahususi za vyakula, na akili yake, ambayo yaweza kupenya kufikia viwango vyote vya ukweli, na moyo wake ambao unatamania kila aina ya ukamilifu, na kisha fikiria vipawa vidogo mno walivyonavyo wanyama ambao wameendelea kwa daraja moja au mawili tu? Ipo tofauti hii tu, kuwa katika wanyama vipawa mahususi kwa kazi fulani na maalumu kwa aina mahususi huendeleza zaidi. Lakini haya maendeleo ni mahususi.

Na siri ya wingi wa vipawa vya mwanadamu (alivyopewa) ni: Kuwa milango ya fahamu, hisia zake huendelea kukua, kwa kilichomiliki miongoni mwa fikra na akili, namna ya kupokea kwa hisia zake kumekuwa kingi mno nayo hutokana na mahitaji yake kuwa ni mengi, hilo limepelekea hisia zake kuwa anuai, na kwa sababu anamiliki umbile lililokusanya mengi hivyo imekuwa ni mzunguko wa matarajio yake na matamanio mengi na kutokana na wingi wa nyadhifa zake za fitra (maumbile yake ya asili) imefarijika vipawa vyake na kutanuka zaidi na kuwa ya umbile zuri zaidi lililotayarishwa juu ya aina nyingi za ibada basi amepewa matayarisho mengi ya kufikia ukamilifu.

Kwa hivyo, huu utajiri mkubwa katika vipawa na mtaji mwingi alionao mwanadamu, bila ya shaka haukutolewa kwa ajili ya kununua haya maisha ya kidunia ya muda mfupi yenye kupita na kuondoka, bali kazi za msingi za mwanadamu ni kutekeleza kazi zake, ambazo zinazingatia malengo mengi sana yasiyo na ukomo, na hutangaza kutokujiweza kwake, ufukara karibu na Mwenyezi Allah (sw) katika uja (unyenyekevu) wake, na kasoro katika hali ya kuabudu; na kuangalia kwa makini kutukuzwa kwa viumbe kwa jicho la kilimwengu, kupata ushahidi kwao, na kuona mifano ya msaada wa Yule Mmoja Mwenye huruma kuliko wote, kutoa shukrani, na kukazia macho miujiza ya uwezo wa Kiungu katika viumbe na katika sanaa zake anuwai, hivyo hupata kufikiri ndani yake na kuiangalia kwa mtazamo wa mazingatio na kustaajabishwa.

Ewe mwanadamu mtafuta dunia na ashiki wa maisha haya, mwenye kughafilika na siri ya ‘Umbo lililo bora zaidi! kwa hakika ‘Said wa zamani’ alishuhudia ukweli wa dunia hii, katika maono yake akasikiliza ukweli huu wa kufikirika ambao unamathilisha hakika ya maisha ya dunia, ukweli ule wa tamthilia aliyeuona ‘Said wa zamani’ na ukambadilisha na kuwa ‘Said mpya’.

“Niliona kuwa nilikuwa msafiri na nilikuwa ninakwenda safari ndefu, hivyo ni kusema kwamba, nilikuwa napelekwa. Yule aliyekuwa bwana wangu hatimaye alinipa baadhi ya pesa kutoka katika vipande sitini vya dhahabu alizonipangia.

Niliitumia, na nikaja kwenye hoteli kulikokuweko burudani za kila aina pamoja na Casino, katika usiku mmoja ndani ya hoteli ile nilitumia vipande vya dhahabu kumi kwa kamari, burudani na starehe ya kujionesha na kupata umaarufu, kufika asubuhi sikubakiwa na pesa. Isitoshe sikufanya biashara wala sikununua bidhaa kwa mahali nilikokuwa nakwenda. Kitu pekee kilichobakia kwangu kutoka katika pesa, zilikuwa dhambi na machungu, na kutoka katika burudani, majeraha na masikitiko yaliyotokana na starehe na ladha zisizo za halali, yaliyobakia yalikuwa ni majeraha na majonzi kutokana na ujinga ule.’’

Wakati nikiwa katika hali ile ya majonzi, akanitokea mtu mmoja ghafla, akaniambia:

‘‘Umepoteza mtaji wako wote hivi hivi, bure bure na unastahili adhabu. Unakwenda unakoishia safari yako ukiwa mikono mitupu, lakini ukiwa ni mwenye akili na uoni, mlango wa toba bado uko wazi. Kuna uwezekano wa kudunduliza nusu unachopata, katika kilichobakia katika vipande kumi na tano vya dhahabu ili ununue baadhi ya mahitaji yako huko unapokwenda.” Niliishauri nafsi yangu lakini haikuwa radhi kwa hilo, Yule bwana akasema: “Basi dunduliza theluthi.” Hata hivyo nafsi yangu bado ikakataa na haitaki kuachana na mazoea yake maishani. Yule bwana akageuza uso wake kwa hasira na kuondoka.

Ghafla, mandhari ikabadilika, nilijiona katika gari la moshi ndani ya njia ya reli ya chini ambayo ilikuwa ikisafiri haraka sana kama vile inasafiri chini wima. Nikashtuka, lakini ningefanya nini! hakukuwepo na pa kuepuka popote.

Kwa ajabu maua ya kupendeza na matunda ya kuvutia yakatokea sehemu zote mbili za treni. Na mie, kama mjinga na nisiye na uzoefu, nikayatazama na nikanyoosha mkono wangu, nikajaribu kuyachuma, lakini yalikuwa yamefunikwa na miba na ikanichana mikono yangu nilipoyagusa yakanifanya nitoke damu.

Kwa sababu treni ilikuwa inakwenda mbio sana, mikono yangu ikachanwa chanwa kwa matunda yale kutenganishwa na mimi, yalinigharimu sana, ghafla! muhudumu ndani ya treni akasema.

“Wewe nipe mimi shilingi tano, nami nitakuchagulia kiasi unachotaka cha maua yale na matunda, kwani kwa hivyo ufanyavyo utapata majeraha mara nyingi kuliko yale utakayopata kwa shilingi tano mbali ya kuwa kuna adhabu utakayopata ya tendo lako hili, kwani unachuma bila ya idhini.”

Huku nikiwa na mateso nilinyoosha mkono wangu nje ya dirisha na nikatazama mbele nione ile njia ya reli ya chini inakoishia, nikaona kuwa mahali pa mlango wa njia ya reli ya chini kulikuwa na mashimo mengi sana, wasafiri wa treni ile pamoja nami tulikuwa tukitupiwa humo kutoka kwenye treni ndefu, nikaona shimo mkabala na mimi, kutoka kwenye sehemu zote mbili za treni kulikuwa na tofali la jina la kaburi. Nilitazama kwa mshangao.

Nikaona kuwa upande mmoja wa tofali la kaburi liliandikwa jina la Said. Katika mshangao wangu na utatanishi nikasema ghafla kwa mshangao: “Ole wangu!” Kisha ghafla nikasikia sauti ya yule mtu aliyenipa nasaha pale penye mlango wa hoteli. Akaniuliza: “Je! umezindukana?” Nikajibu: “Ndiyo, lakini nimekwishachelewa sasa baada ya kuondoka kwa nguvu zangu na kwa sasa hivi sina ujanja wala nguvu.”

Kwa hiyo akasema: “tubia na Mtegemee Allah (sw).” Nikajibu kuwa nimeshatekeleza. Kisha nikaamka na nikajiona kama “Said Mpya”; “Said wa zamani” kapotea.

Kwa hiyo, yale ndiyo yalikuwa maono. Allah (sw) na Asababishe mema kuja kwayo. Nitatafsiri sehemu moja au mbili zake kisha nanyi mtatafsiri yaliyobaki wenyewe, safari ilikuwa ni safari inayopita kutoka Dunia ya Roho kupitia kwenye tumbo la mama, ujana, uzee, kaburi, Maisha ya Barzakh, ufufuo, na Daraja la Sirati mpaka milele.

Vipande sitini vya dhahabu ni miaka sitini ya maisha, ninafikiri niliyaona maono nilipokuwa na umri wa miaka arubaini na tano, sikuwa na chochote cha dhamana ya kuishi hadi miaka sitini ya umri wangu, lakini mwanafunzi mwaminifu wa Qur’an yenye busara zote alininasihi nitumie nusu ya miaka kumi na tano umri wangu kwa njia ya kupata akhera, hoteli kwa ajili yangu ilikuwa ni mji wa Istanbul. Treni ilikuwa ni zama (wakati), na kila mwaka ni behewa lake moja.

Ama kuhusu njia ya reli ya chini ilikuwa maisha ya dunia hii. Maua na matunda yenye miiba vilikuwa starehe haramu na burudani iliyokatazwa ambazo husababisha machungu wakati wa kuendekeza matakwa ya mtu kwa kufikiri kupita kwake, na katika kutenganishwa huchana chana moyo na kuufanya utoke damu. Pia husababisha kupata adhabu. Mhudumu kwenye treni aliniambia nipe shilingi tano ili anipe kiasi nikitakacho.

Maana ya haya ni kama ifuatavyo: Starehe na raha ambayo mtu hufaidi kupitia kujitahidi kihalali ndani ya tufe lililo halali yanamtosha yeye huyo, hakuna haja ya yanayobakia kuingia katika haramu, unaweza kutafsiri mengine yaliyobaki wewe mwenyewe.

KAULI YA NNE

Mwanadamu hufanana na mtoto dhaifu mwenye kupendwa, mtoto huyu anabeba nguvu kubwa kwenye udhaifu wake, kwani kupitia nguvu ya udhaifu wake na uwezo wa kutokujiweza kwake ndiyo haya yaliyomo vimewekwa chini yake na kuongozwa kwake, ikiwa mtu haelewi udhaifu wake na anatamka maombi yake kwa mdomo na kwa hali na kwa mwenendo, na hutambua kutokujiweza kwake na huomba msaada, na akatoa shukrani kwa kulainishwa basi atafanikiwa matakwa yake na yatadhalilika kuwa makusudio yake na kufanikisha malengo yake yakimjia hali ya kuwa yamemtii pamoja na udhaifu wake wa uwezo wa kuyapata mwenyewe kwa nguvu zake binafsi yenye mpaka bali hawezi mwenyewe.

Mara nyingine yeye huhusisha kimakosa uwezo wake mwenyewe upatikanaji wa mahitaji ambayo amesababishiwa yapatikane kupitia dua’ yaliyotolewa kwa ulimi wa silika yake, kwa mfano nguvu katika udhaifu wa kitoto cha kuku husababisha mama-kuku kumshambulia simba, na kitoto cha simba aliyetoka kuzaliwa humuweka chini yake mama-simba mwenye njaa, ikimwacha mama simba katika hali hiyo huku kitoto cha simba kimeshiba, itazame hii nguvu katika udhaifu na uoneshaji wa huruma ya Allah (sw), ambayo yanastahili kutambuliwa!

Kama ambavyo kupitia kulia au kuomba au kuonekana kukosa furaha, mtoto kwa udhaifu wake hupata huruma ya wengine, na hufaulu sana katika kupata anachotaka kiasi kwamba asingeweza kupata moja ya elfu ya hicho akitakacho kwa kutumia mara elfu moja ya nguvu zake mwenyewe.

Yaani, kwa kuwa udhaifu na kutokujiweza husisimua huruma na hisia ya kulindwa kwake, mtoto anaweza kuwaweka chini yake mashujaa kwa kidole chake kidogo. Sasa, mtoto mdogo mwenye maringo ya kipumbavu akanushe huruma na ashutumu ulinzi (aliopewa) kwa kusema: “Ninawaweka hawa mashujaa chini yangu kwa nguvu zangu mwenyewe.” Bila ya shaka atapigwa kofi.

Vivyo hivyo ikiwa mwanadamu huyo atakana rehema ya Mola wake na akatuhumu hekima yake na akasema kama ilivyosema Quran, alikana neema:

اِنَّمَا اُوتِيتُهُ عَلَى عِلْمٍ{ Qur’an 28: 78}

Yaani, ‘Nilipata hivi kupitia elimu yangu na uwezo wangu’ kwa njia ambayo inaashiria utovu wa shukrani na inakanusha huruma ya Muumba, na anashutumu hekima yake, bila shaka anastahili adhabu, hii inamaanisha nafasi na hadhi hii anayoipata mwanadamu ni maendeleo ya upatikanaji wa ustaarabu hautokani na kuwa kwake juu na uwezo wa kujadili na utawala wake, bali mwanadamu amepewa kutokana na udhaifu wake na kusaidiwa kwa unyonge wake, na ufukara wake na amekirimiwa hayo kwa uhitaji wake na ya kuwa ni mwenye nguvu au kinachokadiriwa na elimu bali ni huruma ya Mola na wema wake na hekima yake ambayo amedhalilishiwa vitu na vimejisalimisha kwake.

Naam, mwanadamu ni mwenye kushindwa na vidudu kama nge wasiyokuwa na macho na nyoka wasiyo na miguu, na sio uwezo wake uliyomvisha Hariri kutokana na vijidudu na kumlisha asali kutoka kwenye mdudu mwenye sumu, bali haya ni matokeo ya matunda ya udhaifu wake unaotokana na kudhalilishiwa na Mola, mwenye kukirimu, mwenye huruma.

Ewe mtu! Kwa kuwa ukweli wa mambo ni hivyo, wacha ubinafsi na majivuno. Kwa ulimi wa kuomba msaada, tangaza kutokujiweza kwako na udhaifu katika Mahakama ya Kiungu na kwa ulimi wa kusihi na dua’ na maombi mengine, ufukara wako na mahitaji yako. Onesha kuwa wewe ni mtumwa Wake. Sema: ‘Allah (sw) Anatutosha kwani Yeye ni Mkataji mashauri kabisa ya mambo.’

حَسْبُنَا اللّٰهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ{Qur’an 3: 173}

Panda katika hatua za juu, pia usiseme: “Mimi si chochote. Umuhimu gani ninao ambao ulimwengu sharti uwekwe chini yangu kwa Yule Mmoja Mwenye busara zote kabisa, na mjuzi wa yote kwa kukusudia na kuchunga na hadi anitake mimi kushukuru yote”.

Na kwa hilo unaweza kuihesabu nafsi yako na kujiona kuwa ni kama haupo vile, japokuwa kwa wadhifa wako na hadhi yako ni mtu mwenye kushuhudiwa mwenye akili, na mtazamaji mwenye akili kwa viumbe wakubwa. Bali wewe ndiye msemaji mwenye ufasaha mwenye kuzungumza kwa niaba ya viumbe hivi vyenye hekima.

Na kuwa wewe ni msomaji mwerevu wa kitabu hiki cha ulimwengu huu na wewe ni msimamizi mwenye kufikiri katika viumbe hivi vyenye kuogelea, na wewe upo kama ni profesa mzoefu na msanii mkarimu wa sanaa hii yenye kuabudu na kusujudu.

Ndiyo, Ewe mwanadamu! Kuhusu kiwiliwili chako, wewe ni sehemu ndogo na kiumbe dhalili na mnyama mnyonge na dhaifu, mwenye mahitaji, ambaye alijitupa juu ya mawimbi ya mafuriko katikati ya viumbe hivi vyenye kutisha vinavyoondoka.

Lakini kwa upande wa utu wako uliokamilika kwa malezi ya kiislamu yaliyoingizwa nuru ya imani yenye mwanga wa mapenzi ya kiungu katika utawala wa uja huu, nawe pamoja na kuwa ni sehemu bali ni mkamilifu na pamoja na udhaifu ulionao wewe ni mwenye kuelea kwenye ulimwengu mpana na ni mwenye hadhi za juu na uoni katika mzunguko huu mpana pamoja na udhalili uliokuwa nao, kiasi unaweza kusema:

“Hakika Mola wangu Rahimu ameifanya dunia kuwa ndio makazi yangu na jua na mwezi kuwa ndio nuru na mwanga wangu, msimu wa kuchipua kuwa ni ‘ua’, na kiangazi kuwa ni meza yenye neema na akajaalia wanyama kuwa ni wahudumu dhalili, na mwishowe ameijaalia mimea kuwa ni pambo na samani na furaha katika makazi na nyumba yangu.”

HITIMISHO

Endapo utamsikiliza Shaitani na roho yako, utashuka mpaka chini zaidi kuliko vyote vilivyoko chini.

Lakini kama utaisikiliza Qur’an na haki basi itapanda juu, juu zaidi na kuwa ‘Katika umbo lililo bora kabisa’ katika ulimwengu huu.

KAULI YA TANO

Mwanadamu amepelekwa katika dunia hii kama mfanyakazi na mgeni, na amepewa vipaji vingi na matayarisho ya kutosha kabisa, na amekabidhiwa kazi muhimu kwa mujibu wa uwezo huo ili kumtumia mtu kutekeleza malengo hayo na kazi hizo, ushawishi wa nguvu na vitisho vikali vimefanywa.

Hapa tutafanya muhtasari wa misingi ya ibada na kazi za mwanadamu, ambao tumeueleza kwa kirefu mahali pengine ili tuweze kudiriki siri ya ‘umbo lililo bora kabisa’ hivyo tunasema: Katika kuja ulimwenguni mwanadamu ana sura mbili za kuabudu na kuwa mtumwa wa Allah (sw). Moja ni kuabudu na kutafakari bila kuweko Lengo la Kuabudu. Nyingine ni kuabudu na kuomba katika sura ya anayekusudiwa akiwepo.

Sura ya Kwanza: Ni kusadikisha kwa dhati na unyenyekevu mamlaka ya Uungu unaoonekana ulimwenguni na kuchunguza ukamilifu wake na ubora na uzuri kwa mshangao wa kutukuza.

Kisha ni kuchukua mazingatio na masomo kutoka katika sanaa za nakshi ya majina yake matukufu na kuyatangaza na kuyasambaza.

Kisha ni kupima kwa johari za majina matukufu ya kiungu na duru zake. Kila kimoja katika hizo ni hazina zilizojificha kwa kipimo cha ufahamu na uoni na kuthamini kwa mwanga wa makadirio na utukufu na rehema zenye kutoka katika nyoyo, kisha ni kuchunguza na kutafakari kwa mshangao kurasa za viumbe na majani ya ardhi na anga, ambayo ni kama maandiko.

Kisha kupitia kutazama kwa makini kwa kupenda mapambo na sanaa za kistadi katika viumbe, ni kuhisi upendo wa elimu ya Muumba wao Mwenye Uzuri Wote na kutamani kupanda kwenye uwepo wa Mtengenezaji Mwenye Ukamilifu Wote na kupokea upendeleo Wake.

Sura Ya Pili: Hiki ni kituo cha uwepo na anwani ambako mtu hupita kutoka kwenye kazi mpaka kwenye mzalishaji na huona kwamba Mtengenezaji Mwenye Uzuri Wote Anataka kujitambulisha Mwenyewe Ajulikane na afahamike kupitia miujiza ya sanaa Yake, na anajibu kwa elimu na imani.

Kisha huona kwamba Mola Mtoaji Mwenye Ukarimu wote anamlea yeye na kumpa furaha kwa zawadi za maana na anataka kumpendezesha kwa matunda mazuri matamu kwa rehema zake, hilo ni kwa mkabala wa yeye kuifanya nafsi yake kupendwa kwake kwa mapenzi halisi na unyenyekevu halisi kwake.

Kisha huona kwa Mwenye kuneemesha na mkarimu humzamisha kwa ladha ya neema zake mbali mbali za kifedha, na za vitu na zisizokuwa hizo, kwa mkabala wa matendo, maneno yake kwa fahamu na vipawa vyake vyote (kadiri awezavyo) kwa kumshukuru na kumuomba yeye.

Kisha huona kuwa mtukufu mzuri anadhihiri kwenye kioo katika vilivyomo kwa utukufu na ukamilifu wake na hudhihiri utukufu wake na uzuri wake ndani yake kiasi cha kuvuta nadhari na yote haya mkabala wake ni: Kurudia rudia

اَللّٰهُ اَكْبَرُ سُبْحَانَ اللّٰهِ

na husujudu kwa sijida ya wasiochoka kwa babaiko ni mshangao na mahaba yenye kuondoka au kuyeyuka.

Kisha huona kuwa Yule Mwenye Utajiri Mkubwa Sana anaonesha utajiri Wake na hazina katikati ya wingi wa ukarimu mkubwa sana. Kwa hiyo katika kujibu humpandisha cheo na kumsifu Yeye, husihi na anauliza kwa ajili yao, akidhihirisha mahitaji yake kabisa.

Kisha huona kwamba Muumba Mwenye Utukufu Wote Ameifanya sura ya ardhi kama maonesho na kaonesha juu yake kazi zake zote za sanaa za kale, kwa hiyo kwa kujibu hutamka kwa kufurahia:

مَاشَاءَ اَللَّهُ

“maajabu yaliyoje haya Allah (sw) kayapenda” na katika kutamani:

بَارَكَ اللَّهُ

“Baraka gani Allah (sw) Amezileta! na katika mshangao:

سُبْحَانَ اللّٰهِ

‘Utukufu uwe kwa Allah (sw)’ na katika mshango: rudia

اَللّٰهُ اَكْبَرُ

Allah (sw) ni mkuu zaidi kuliko Wote!

Kisha huona kuwa katika kasri Yake ya ulimwenguni Huyo Mmoja wa Umoja Amepiga lakiri juu ya viumbe wote kwa tawhidi, saini isiyowezekana kuigwa, na hiyo mihuri Yake imenakishiwa kwa aya za tawhidi na kujazwa mabango ya tawhidi katika kila sehemu duniani, ikitangaza uungu wake, naye hujibu hayo kwa kusadikisha kwa imani na tawhidi na kufuata kwa shahada na unyenyekevu.

Kwa hivyo, kupitia kuabudu na kutafakari, kwa aina hii mtu huwa mtu kweli. hudhihiri kwa ‘umbo lililo bora kabisa’ na anakuwa ni Khalifa wa ardhi mwenye kustahiki amana.

Ewe mwanadamu usiyejali uliyeumbwa juu ya ‘Umbo lililo bora kabisa’ ambaye kwa kutumia vibaya matakwa yake anashuka mpaka chini zaidi kuliko za chini zote! Hebu nisikilize mimi! Na angalia mabango mawili yaliyoandikwa katika sehemu ya kwanza katika ‘Neno la kumi na saba (17)’ na wewe unaona kama mimi nilifikiri kuwa katika kutojali kulikoshawishiwa na kulewa kwa ujana, Mimi, kama wewe, nifikiri dunia ni nzuri na inapendeza. Kisha asubuhi nilipozindukana na ulevi wa ujana na kuwa mzee sasa, niliona jinsi sura ya dunia ilivyokuwa mbaya ambayo haikugeuzwa kwenye akhera, ambayo huko nyuma nilifikiri kuwa ni nzuri. Lakini kwa sasa niliona kuwa ni mbaya na kuwa uso wa dunia unaoelekea akhera ni nzuri. Sasa unaweza kuyarejea mabango yale mawili, katika Kituo cha Pili cha Neno la Kumi na saba, ili ujionee wewe mwenyewe.

Bango la Kwanza:

Taswira ya dunia ya walioghafilika, Niliona bila ya kupumbazwa nayo, ni mfano wa dunia ya watu waliopotea ambao wamezibwa na pazia ya kughafilika.

Bango la Pili:

Linaashiria ukweli wa watu walioongoka na wenye nyoyo zilizotulia. Sikubadilisha chochote katika mabango hayo mawili, bali niliyaacha kama yalivyokuwa, na hata kama zilikuwa zikifanana na mashairi lakini hayakuwa mashairi.

سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا اِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَا اِنَّكَ اَنْتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ{ Qur’an 2: 32}

رَبِّ اشْرَحْ لِى صَدْرِى وَيَسِّرْ لِى اَمْرِى وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِنْ لِسَانِى يَفْقَهُوا قَوْلِى

اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّمْ عَلَى الذَّاتِ الْمُحَمَّدِيَّةِ اللَّطِيفَةِ اْلاَحَدِيَّةِ شَمْسِ سَمَاءِ اْلاَسْرَارِ وَ مَظْهَرِ اْلاَنْوَارِ وَ مَرْكَزِ مَدَارِ الْجَلاَلِ وَ قُطْبِ فَلَكِ الْجَمَالِ اَللّٰهُمَّ بِسِرِّهِ لَدَيْكَ وَ بِسَيْرِهِ اِلَيْكَ آمِنْ خَوْفِى وَ اَقِلْ عُثْرَتِى وَ اَذْهِبْ حُزْنِى وَ حِرْصِى وَ كُنْ لِى وَ خُذْنِى اِلَيْكَ مِنِّى وَ ارْزُقْنِى الْفَنَاءَ عَنِّى وَ لاَ تَجْعَلْنِى مَفْتُونًا بِنَفْسِى مَحْجُوبًا بِحِسِّى وَاكْشِفْ لِى عَنْ كُلِّ سِرٍّ مَكْتُومٍ يَا حَىُّ يَا قَيُّومُ يَا حَىُّ يَا قَيُّومُ يَا حَىُّ يَا قَيُّومُ وَ ارْحَمْنِى وَارْحَمْ رُفَقَائِى وَ ارْحَمْ اَهْلِ اْلاِيمَانِ وَ الْقُرْآنِ آمِينَ يَا اَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ وَ يَا اَكْرَمَ اْلاَكْرَمِينَ

وَ آخِرُ دَعْوَيهُمْ اَنِ الْحَمْدُ لِلّٰهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ {Qur’an 20:25-28}

Ewe Mola shusha rehema katika dhati njema pekee ya Muhammad (saw), jua la mbingu ya siri na mandhari ya nuru, na kituo cha utukufu na kigingi cha falaki ya uzuri, ewe Mola kwa siri yake iliyo kwako na kwa mwenendo wake kuja kwako Wewe, nisalimishe na khofu yangu, na yapunguze makosa yangu, na ondosha huzuni na pupa yangu, na kuwa kwa ajili yangu, na nichukue mimi kwako, na niruzuku kukinai na usinifitinishe kwa nafsi yangu, Mwenye kukingwa na hisia zangu, nifungulie siri zilizojificha ewe uliye hai Mwenye kudumu, na warehemu marafiki zangu, na warehemu watu wa imani na wa Qur’an, ewe Mrehemevu wa kurehemu na ewe Mkarimu zaidi.

Na mwisho wa dua zao ni Alhamdulillah Rabil ‘Alamiyn.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.