Jukumu La Risale-i Nur

Siku hizi nimesikiliza sehemu ya mazungumzo ya kimaanawy ya swali na jawabu nitawabainishieni muhtasari wake:

(Mmoja wao alisema: Hakika ya mikusanyo mingi na maandalizi yake ya kimapambano ya Risale-i Nur kwa maandalizi ya jumla, na jihadi yake kwa ajili ya imani na Tawhidi inaongezeka moja kwa moja, na pamoja na kwamba moja kati ya hizo yatosha kumlazimisha mkaidi mkubwa basi kwa nini inaendelea mfululizo kwa kiasi hiki cha joto na nguvu kufanyia hilo maandalizi mapya)?

Wamesema kujibu swali hili: (Hakika Risale-i Nur haifanyii matengenezo uharibifu mdogo wala kukarabati nyumba ndogo pekee iliyovunjika bali pia inajenga maharibifu yote kwa jumla. Na kukarabati ngome kuu yenye kuzunguka eneo – mawe yake kama majabali – inakumbatia Uislamu na kuuzunguka na haifanyi juhudi katika kutengeneza moyo mahususi na nafsi maalum pekee bali pia inajitahidi  – na hali yakuwa mkononi mwake kuna muujiza wa Qur’an – kwa kudumisha moyo wa jumla na kutibu fikra za jumla zilizojeruhiwa kwa nyenzo zenye kufisidi ambazo zimewekwa kwa ajili yake na kuandaliwa kwa mrundikano tangu miaka elfu moja na kuchangamkia kudumisha roho ya jumla ambayo inaelekezwa katika Ufisadi yakiwa ni matokeo ya kubomoka kwa misingi ya Kiislamu na mikondo yake na hisia zake ambazo ndio egemeo kubwa kwa wote na hasa waumini wa kawaida. Naam hakika inajitahidi kutibu majeraha hayo mapana yenye kushambulia kwa dawa za muujiza wa Qur’an na imani.

Basi mbele ya maharibifu haya ya jumla ya kutisha na mipasuko mikubwa na majeraha makubwa. Inatakiwa kuwepo kwa hoja kali na zana zilizoandaliwa kwa daraja ya haki ya yakini na kwa nguvu ya milima na Uimara wake na uwepo wa madawa mujarabu kwa ajili yake yenye sifa maalum zinazozidi tiba elfu moja na moja na ina sifa pekee inayofanana na tiba zisiyo na mipaka.

Hili ndio jukumu la Risale-i Nur linalotokana na muujiza wa Qur’an tukufu wa kimaanawy na katika wakati ambao unapo timiza hilo katika zama hizi kikamilifu inapata sifa ya kuwa ni mahali pa kufunuliwa kwa ngazi zisizo na mipaka za imani na chanzo cha kupanda katika ngazi zake za juu zisizo koma)

Na kwa namna hii yalipita mazungumzo marefu, nikayasikia yakiwa kamili na nikamshukuru Allah (s.w) sana nimekufupishieni kwenu.

Said Nursi

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.