Mambo aliyoshuhudia mtalii anayeuuliza ulimwengu kuhusu Muumba wake.

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

 تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ يُسَبِّحُ بِحَمْدَهِ وَلَـكِن لاَّ تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا Qur’an, 17: 44.

Kituo hiki cha pili katika wakati ambapo kinafasiri hii (Al-Ayatul kubra), kinabainisha vilevile hoja za kituo cha kwanza ambacho imo ndani yake na ambayo ipo katika lugha ya Kiarabu na kufafanua hoja zake.

          Hakika aya nyingi za Qur’an tukufu – mfano wa aya hii tukufu – zinataja (Mbingu) mwanzoni mwa kutambulisha kwake Muumba wa ulimwengu huu ambazo ni ukurasa unaong’ara zaidi wa tawhidi, kwa kiasi ambacho mchunguzaji yeyote hazichunguzi hizo ila itamfunika tahayari na kugubikwa na mshangao, na hivyo anastarehe kuziangalia kwa kila kionjo na ladha; kwa hiyo kilicho bora ni kuanza nazo.

          Naam, kila anayekuja akiwa ni mgeni katika mamlaka ya dunia hii na kukaa katika nyumba ya dhifa yake, kila anapofungua macho yake na kutazama ataona makaribisho katika upeo wa ukarimu, na maonesho katika upeo wa kupendeza, na kambi ya mazoezi katika upeo wa haiba, na maeneo ya utalii katika upeo wa kuvutia, na mahali pa matangazo katika upeo wa kusisimua na furaha, na kitabu kilichofunguliwa chenye maana yaliyo katika upeo wa ufasaha na hekima.

          Na wakati anahima mgeni huyu mtalii ajue na kumtabua mwenye dhifa hii tukufu, na mtunzi wa kitabu hiki kikubwa, na mfalme wa mamlaka haya yenye haiba kubwa, tahamaki uso mzuri wa mbingu unaomemetuka kwa nyota angavu unamkabili kwa kumwita: “Niangalie mimi, nitakutambulisha unacho kitafuta”.          

Mtalii anaangalia na kuona kwamba rububiyya iliyo dhahiri inaonekana katika kunyanyua mamia ya maelfu ya sayari za mbinguni pasi na nguzo wala maegemeo, kati yake zipo zilizo kubwa kuliko dunia yetu mara elfu, na zipo zilizo na kasi ya mwendo kuliko bomu kwa mara sabini, na katika mwendo wake na kukimbia kwake sayari hizo kwa pamoja kwa kasi ya juu bila kusongamana wala kugongana, na katika kuwasha kwake taa hizo zinazoning’inia chini zisizo hesabika, bila mafuta wala kuzimika, na katika kuyaongoza maumbo hayo makubwa mno yasiyo na mpaka bila kelele wala mayowe wala kutetereka.

          Na anaona kudhihirika kwake pia: Katika kutiisha kwake viumbe hivyo vikubwa katika majukumu maalum, kama kusalimu amri kwa jua na mwezi ili kutekeleza majukumu yao bila kugoma au kusitasita, na katika kugeuza idadi hii kubwa isiyodhibitika kwa nambari ndani ya umbali huo mpana sana usio na kikomo eneo lililopo kati ya vipenyo viwili mageuzo yanayofanyika wakati huohuo, na kwa nguvu hiyohiyo na kwa aina hiyohiyo, na katika njia ya maumbile ileile, na kwa sura hiyohiyo, na katika hali ya kukusanyika bila ya kusibiwa na uchache wa upungufu au dosari yoyote.

          Na imemshangaza anachokiona katika kudhihiri kwa rububiyya: Katika kutiisha kwake sayari hizo kubwa ambazo zinamiliki nguvu kubwa na kuvuka mipaka yake, zenye kufuata na kutii kanuni zake bila kuvuka au kwenda upogo.

          Na kule kuufanya uso wa mbingu safi uliotakata unatakasika kabisa na uchafu unaoletwa na maumbo hayo makubwa bila ya kuonekana juu yake taka wala udhia, na katika kuziendesha sayari hizo kana kwamba ni mazoezi yaliyopangika ya askari, na kuonesha kwake mbele ya viumbe wenye kutazama kana kwamba kutazama picha ya senema, kwa kuzungusha ardhi usiku na mchana, na kufanya upya mitindo ya mionekano ya kihakika yenye kuvutia yenye kuamsha taswira akilini ya mazoezi hayo mazuri na kuyadhihirisha kila usiku na kila mchana.

          Basi rububiyya hii tukufu dhahiri na yanayo dhihiri ndani ya nguvu yake ya utendaji katika ukweli ulio wazi uliyoundwa katokana na (Kutiisha, Kuongoza, Kuendesha, Kunadhimu, Kusafisha, na Kukabidhi majukumu), vinashuhudia wajibu wa uwepo wa Muumba wa mbingu hizo na umoja wake, kwa ukubwa wake huu wa kutisha, na kuzungukia kwake kwa ujumla huku, na vinashuhudia – kama inavyoshuhudiwa – kwamba uwepo wake (s.w) ni dhahiri zaidi kuliko uwepo wa mbingu hizo.

          Na maana hii imeelezwa katika ngazi ya kwanza katika kituo cha kwanza kama ifuatavyo:

          [Hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah (s.w) aliyewajibu kuwepo ambaye katika umoja wake zimejulisha kupasa kwa uwepo wake: Mbingu na vyote vilivyomo, kwa ushahidi wa ukuu wenye kuzunguka kote kiuhakika: Kutiisha, kuongoza, kuendesha, kunadhimu, kusafisha, kupanga majukumu kupana kunakokamilishwa kwa kushuhudia]

          Kisha hakika anga ambalo ni mkusanyiko wa maajabu na maonesho ya mambo yenye kufurutu ada na linaloitwa (Anga) limenadi kwa sauti ya juu yenye kushuka kwa yule anayekuja duniani yule mgeni mtembezi: “Nitazame ili nikuongoze kwa unayemtafuta kwa shauku na hamu, na nikutambulishe aliye kutuma hapa”.

          Na anaangalia uso wa anga mpana na hali unavuja rehema! na kusikiliza kishindo cha sauti cha kutisha mno na hali inabeba kinywaji cha bishara! anaona kuwa: (Mawingu) ambayo yametundikwa baina ya mbingu na ardhi yanamwagilia bustani ya ardhi umwagiliaji unaobubujika hekima na rehema, na kuwapa wakazi wake maji yanayoleta uhai, yakipoozea ukali wa joto – yaani ukali wa joto la maisha – na kutambua mara moja popote inapokuwa haja. Na pamoja mawingu hayo makubwa yanatekeleza majukumu mengi kama haya, hujificha na kupotea haraka baada ya kuwa yamejaa maeneo ya anga, basi sehemu zake zote zinajiondoa ili zikatulie katika mapumziko na kujificha mbali na macho pasipo kuacha athari yoyote kwa mfano wa kudhihiri na kujificha kwa jeshi lenye kupangwa kulingana na amri za papo kwa papo, lakini hayapokei amri ya (Haya teremsha mvua), isipokuwa yanakusanyika na kujaza anga ndani ya saa moja bali kuligubika ndani ya dakika kadhaa, na kujiandaa tayari kama askari anayesubiria amri ya kiongozi.

          Kisha mtalii huyo anaangalia (Upepo) ambao unasafiri angani, na kuona kwamba hewa hutumika katika kazi nyingi, katika ukomo wa hekima na ukarimu, matumizi ambayo kana kwamba kila chembe katika chembe ndogo kabisa za hewa isiyo hai – isiyo na hisia – inasikia na kufahamu kinachotolewa kwake katika amri zitokazo kwa mfalme wa ulimwengu huu, hivyo hutekeleza huduma zake kwa nguvu ya huyo mwamrishaji na utawala wake na kuzitekeleza kwa mpangilio wote na umakini, pasi na kuchelewesha chochote kati ya hizo basi chembe chembe hizo ndogo huingia katika pumzi ya hewa wavutayo viumbe wote walio hai, au kusafirisha sauti, au maada za lazima kwa ajili ya wenye uhai kama vile joto, mwanga na umeme, au kuwa kiungo cha kuhamilisha mimea au mfano wa hayo katika majukumu mengi, basi hutumiwa kwa huduma zote hizi kutokana na mkono usioonekana matumizi ambayo yako katika ukomo wa hisia, ujuzi, na hali ya uhai.

          Kisha anaangalia (Mvua) anaona kwamba matone hayo laini angavu matamu yaliyotumwa na kumiminiwa kutoka katika hazina ya rehema ya hali ya ughaibu, yamesheheni zawadi za kiungu mwingi wa rehema na majukumu kedekede hata kana kwamba rehema iliyotunukiwa imejiunda umbo hali ya kuwa imewekwa kutoka katika macho ya hazina za kiungu kwa sura ya matone hayo yenye kunyesha, na kwa ajili hii mvua imepewa jina (Msaada) na (Rehema).

          Kisha anatazama (Umeta) na kusikiliza (Radi), anaona kuwa viwili hivyo hutumika katika mambo yenye upeo wa kustaajabisha.

Anainua uoni wake kwenda katika akili yake na kuongea na akili yake kwa kusema: Hakika ya mawingu haya yasiyo na uhai yasiyo na hisia, na yenye kutawanyika kama sufi, hapana shaka hayatujui sisi na hayawezi kujikusuru nafsi yake kwa ajili ya kutuhurumia na kutufanyia upole kwa hali yetu, na hayawezi kudhihiri hali ya kuonekana mbinguni, na kujificha kwa kujitawanya pasi na amri yeyote, bali hapana budi kuwa yanajitahidi kutimiza jukumu lake kulingana na amri itokayo kutoka kwa Mwamrishaji, Mweza, Mwenye uweza usiyo na mpaka. na Mwingi wa rehema isiyo na mipaka. Ambapo hujificha bila ya kutazama nyuma, kisha yanadhihiri ghafla, yakipokea majukumu ya kazi yake, hujaza ulimwengu wa anga na kupakua baina ya wakati na wakati kwa kutekeleza amri ya Mfalme mtukufu mwenye cheo mtendaji bila kizuizi, daima anachora kwenye ubao wa mbingu kwa hekima yake na kufuta kwa kusamehe, hali ya kuufanya kuwa ni (Ubao wa kufuta na kuthibitisha), na kuwa sura iliyodogeshwa ya ufufuo na kiama. Kwani mawingu yanakwea ndani mwa upepo kwa amri kutoka kwa mtawala mwongozaji mwenye mema na hisani, ukarimu na utunzaji, hali ya kubeba hazina za mvua pana upana sawa na milima na ukubwa wake, hali ya kutoa huduma kwa mawingu hayo maeneo ya ardhi yanako yahitajia, kana kwamba yanaisikitikia hali yake na kuyalilia kwa machozi yake na kuiacha ikicheka kwa maua na mirehani, na kupoza ukali wa joto la ardhi na kuzinywesheleza bustani za ardhi na machunga yake na kuosha uso wake na ngozi yake na kuitakasa kutokana na takataka ili ing’ae kwa usafi na kupata maji.

Kisha msafiri yule mwenye shauku anazungumza na akili yake kwa kusema: Hakika hewa hii isiyo na uhai wala hisia wala uthabiti wala lengo, na iko katika kubabaika daima na kuhangaika bila ya kutulia, yenye dharuba na vimbunga visivyotulia, huja katika uwepo na kudhihiri kwa sababu yake tu – na kwa sura yake yenye kudhihiri –  mamia ya kazi, majukumu, neema na misaada yenye kusheheni hekima na rehema na usitadi, jambo lithibitishalo wazi kwamba: Pepo hizi zinazokwenda hazina harakati za dhati yake zenyewe, hazichakatiki zenyewe kamwe bali hufanya kuwa katika mchakato amri itokayo kutoka kwa Mwamrishaji, Mweza mjuzi wa kila kitu bila mpaka na mwingi wa hekima, mkarimu bila mpaka, kana kwamba kila chembe ndogo kabisa katika chembe zake, inafahamu na kusikia – kama askari mtiifu –  kila amri itokayo kwa huyo Mwamrishaji na inaitambua na kuifuata, na kuwafanya walio hai wote wanaivuta hewa hiyo kwa kupumua ili ichangie katika kudumisha uhai wao, na kushiriki katika kuzalisha mimea, kukua na kusaidia katika kupeleka maada muhimu kwa ajili ya uhai wake, na kupeleka mawingu na kuyaendesha, na kuendesha jahazi zisizokuwa na mafuta na kujaalia na kuzifanya zikate bahari na kutembea humo, na kuwa kiunganishi katika kufikisha sauti, mazungumzo na mawasiliano kupitia mawimbi yasiyo ya waya, na umeme na redio, na mifano kama hiyo ya hudumu za viumbe wote za jumla, ukiachilia mbali kwamba chembe chembe za hewa  zimeundika kutokana na maada rahisi kama al-Azout na  mzalishaji wa acid (Oksijeni). Na pamoja na kufanana kwao sizioni isipokuwa zinatumika kwa mkono wa mwingi wa hekima na kwa mpangilio kamili katika mamia ya maelfu ya aina za kazi za ufundi wa kiungu.

Kwa ajili hiyo, yule mtalii alihukumu akisema: Kweli kama ambavyo aya tukufu ilivyosema wazi:

 وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخِّرِ بَيْنَ السَّمَاء وَالأَرْضِ لآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ Qur’an, 2: 164.

hakika ambaye anapitisha amri yake kwenye hewa na kuitumia katika huduma na majukumu ya kiungu yasiyo na mipaka, kwa kugeuza pepo, na katika kazi za wingi wa rehema zisizo na mipaka, kwa kutiisha mawingu, na kuifanya hewa iwepo kwa namna hiyo, si mwingine isipokuwa ni Mola mlezi aliye wajibu kuwepo, Mweza juu ya kila jambo na mjuzi wa kila kitu mwenye utukufu na ukarimu.

Kisha anarejesha macho yake kwenye (Mvua) anaiona kuwa imejazwa manufaa yenye mifereji mingi na inabeba madhihirisho ya wingi wa rehema kwa idadi ya michururiko yake, na inadhihirisha hekima kwa kiasi cha tone zake, na anaona kwamba matone hayo matamu laini yenye kubarikiwa yako katika upeo wa mpangilio na katika ukomo wa uzuri na kuvutia na hasa umande ambalo linapelekwa – na kuteremshwa hadi wakati wa kiangazi – kwa mpangilio na vipimo, kiasi kwamba vimbunga havisababishi vitu vikubwa kugongana havipotoshi vipimo vya baridi wala mpangilio wake, wala haivifanyi kuwa ni vitu vyenye kudhuru hali ya kuwa vinakusanya punje zake, maji haya ambayo ni kiumbe kisichokuwa hai rahisi hakina hisia hutumika katika mifano ya kazi hizi za hekima, hasa kutumika kwake katika kuhuisha na kunywesha, nayo inaundika kutokana na mada mbili rahisi zisizokuwa na hisia; nazo ni chanzo cha maji na chanzo cha tindi kali – hidrojeni na oksijeni – isipokuwa inatumika katika mamia ya maelfu ya huduma na kazi za ufundi mbalimbali zilizosheheni hekima na hisia.

Kwa hiyo mvua hii si chochote isipokuwa ni rehema iliyokuwa katika muundo wa mwili hasa, wala utengenezaji wake hautimii isipokuwa katika hazina za ghaibu ya rehema ya (Ar-Rahmani na Ar-Rahiim), nayo kwa kuteremka na kumiminika kwake ardhini inafasiri kimatendo na kwa uwazi aya tukufu:

 وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِن بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُ Qur’an, 42: 28.

Kisha anasikiliza kwa mshangao (Radi) na kutazama (Umeme) kwa kustaajabu, anaona haya matukio mawili ya ajabu ya angani yanafasiri kikamilifu aya mbili tukufu:

وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ Qur’an, 13: 13.

 يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ يَذْهَبُ بِالْأَبْصَارِ Qur’an, 24: 43.

hizo pia zinaelezea kuhusu kuja kwa mvua hivyo zinawabashiria wahitaji. Naam, hakika kutamkisha anga lenye kiza ghafla kwa ukelele mkubwa unaonguruma na kurindima, na kujaza kiza totoro kwa nuru inayokaribia kupofua macho, na kwa moto unaohofisha kila kiumbe, na kuwasha mawingu makubwa kama, yaliyotawanywa kama sufi, yenye kubebeshwa umande, barafu  na maji, na mifano kama hii ya hali hizi zenye hekima za ajabu humzindua mwanadamu aliyeghafilika na kumuamsha, na kupungia fimbo juu ya kichwa chake kilichoteremshwa kwa kusema: Ewe fulani! Nyanyua kichwa chako na tazama maajabu ya ufundi na ya kushangaza katika uumbaji ya Mtendaji mkuu Mweza ambaye anataka kujitambulisha kwa waja wake. Basi kama ulivyokuwa si huru mwenye kuachiliwa bila kufungwa na hatamu katika ulimwengu huu, matukio haya hayatokuwa ya bure bure tu au ya mchezo bali kila mojawapo kati ya hayo linapelekwa katika majukumu yenye hekima kwa unyenyekevu na kusalimu amri na yote hayo yanatumiwa kutokea kwa Mola mlezi mwendeshaji mwingi wa hekima.

Na namna hii msafiri huyu mwenye hamu kubwa anasikia ushahidi mkubwa wa dhahiri wa ukweli uliyoundwa kutokana na kutiishwa kwa mawingu, kugeuza upepo, kuteremsha mvua na kuendesha matukio ya anga, hivyo anasema: Nimemwamini Allah. Ngazi ya pili ya kituo cha kwanza imefaidisha

Tanbihi: Nilikuwa ninataka kuweka wazi ngazi thelathini na tatu miongoni mwa ngazi za tawhidi zilizoelezwa katika (Makamo ya kwanza), isipokuwa kutoruhusu kwa hali yangu wakati uliopo kumenifanya nilazimike kutosheka na hoja zake za muhtasari mno na kutafsiri maana zake tu. Na kwa kuwa Risala thelathini katika Risale-i Nur bali Risala mia moja kati yake zimebainisha – kila moja kati ya hizo – sehemu katika hizo ngazi thelathini na tatu, pamoja na dalili zake kwa njia tofauti, kwa ajili hiyo maelezo yameelekezwa huko. (Mtunzi).

mambo aliyoyaona msafiri huyu angani kama ifuatavyo:

[Hapana Mola wa haki isipokuwa Allah ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye kupasa kwa uwepo wake kumejuulishwa na anga na vyote vilivyomo ndani yake, kwa ushahidi wa utukufu wa kuzungukia kila sehemu kwa uhakika wa: Kutiisha, kugeuza, kuteremsha, kupanga, kupana na kwenye kukamilisha kwa kushuhudia].

Kisha msafiri yule mwenye kutafakari, mzoefu wa utalii wa kifikra (Tufe la ardhi) lilimnong’oneza kwa lugha ya hali yake kwa kusema: “Kwa sababu gani unatembea hewani na kuzunguka pande za mbingu na anga? Njoo kwangu ili nikujulishe unayemtafuta. Chunguza majukumu ninayoyatekeleza na usome yaliyoandikwa katika kurasa zangu”. Yule mtalii akaanza kutazama na kuona kuwa: Ardhi ni kama – mawlawiyu mwenye mapenzi – inaandika kwa mizunguko yake miwili katika maeneo ya uwanja wa mkusanyiko mkuu, kwa mzunguko huo hupatikana siku, miaka na majira, nayo ni kama jahazi ya kiungu kubwa iliyobeba zaidi ya aina elfu mia moja za wenye uhai pamoja na riziki zao zote na mahitaji yao ya kimaisha, na kapasua njia za anga na kuzunguka katika safari ya kitalii na kuzunguka jua kwa ukamilifu wa mizania na mpangilio ulio timamu kabisa.

Kisha anatazama kurasa zake anona kila ukurasa miongoni mwa kurasa hizo unamtambulisha Mola wake kwa maelfu ya dalili zake, lakini kwa kuwa hakupata wasaa wa kutosha kuweza kupitia kurasa zote, amefupisha kwa kutazama ukurasa mmoja tu, na huo ni ule unao weka wazi kuumba kwa wenye uhai na kuviongoza wakati wa majira ya machipuo. Akashuhudia kwamba idadi isiyo na mpaka ya elfu mia moja ya aina mbalimbali sura zake zinafunguka na kuchanua kutokana na maada rahisi kwa ukomo wa mpangilio, na kulelewa kwa ukomo wa rehema, na huenezwa katika maeneo mbalimbali kwa ukomo wa wasaa, na kutunukiwa mbegu za sehemu kati yake vijibawa laini kwa ajili ya kuruka katika upeo wa muujiza, na kwamba vinaendeshwa kwa ukomo wa kiutawala, na hupewa uhai na kulishwa kwa ukomo wa huruma na upole, na huaminishwa riziki zao tele anuwai nzuri kwa ukomo wa huruma na kuruzuku, zinatimizwa pasi na chochote, na kutokana na mchanga mkavu, na kutokana na mashina magumu kama mifupa, na kutokana na mbegu zenye kufanana, na kutokana na matone ya maji yenye kufanana, na hupelekwa kutoka katika hazina ya ghaibu kwendea kwa wenye uhai kila machipuo – kama behewa la treni lililosheheni – mia moja elfu na moja aina za vyakula na mahitaji kwa ukamilifu wa kupangilia na kuratibika na hasa kutuma maziwa safi matamu yenye kutoka kwa kasi kutoka katika mifereji ya maziwa ya wazazi waliojawa na upole na mahaba waliozingirwa na huruma, rehema, hekima zikiwa ni zawadi kwa watoto na vichanga, yote hayo kwa uwazi kabisa yanathibitisha kuwa ni udhihirisho kwa ukomo wa malezi na huruma katika dhihirisho za rehema za mwingi wa rehema mwenye kurehemu na hisani yake enevu.

Muhtasari:

Msafiri amefahamu kwa kuangalia ukurasa huu wa kimaisha wa majira mazuri ya machipuo, kuwa ni sura katika sura za mkusanyiko na ufufuo kwa mamia ya maelfu ya vielelezo na vifani, na hii inafasiri kimatendo tafsiri inayotambulika yenye kupendeza ya aya tukufu:

فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ Qur’an, 30: 50.

na aya hiyohiyo inamaanisha kwa namna ya kimiujiza nzuri maana yaliyomo katika ukurasa huu, na amefahamu ambayo tufe la ardhi inayakariri kwa kurasa zake zote na kwa kulingana na ukubwa wake na nguvu zake, kutoka katika.

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

Na kama hivi kwa ajili ya kubainisha ushahidi wa muhutasari wa upande mmoja tu katikapande ishirini za ukurasa mmoja katika kurasa pana za tufe la ardhi, ambazo zinavuka kurasa ishirini na kwa ajili ya kubainisha yale yaliyomaanishwa na aliyoshuhudia msafiri yule katika pande nakurasa nyingine imetajwa katika ngazi ya tatu katika kituo cha kwanza:

[Hapana apasaye kuabudiwa ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye imejulisha kupasa kwa uwepo wake katika upekee wake: Ardhi kwa vyote vilivyomo ndani na juu yake, kwa ushahidi wa ukuu wa kuzungukia kila kitu kwa uhakika wa: Kutiisha, kutawala, kulea, uchanuzi, kugawanya mbegu, kuhifadhi, kuongoza, kuwapa maisha wenye uhai wote, na hali ya wingi wa rehema na urehemevu wenye kuenea unaokamilishwa kwa kushuhudia].     

Kisha akawa yule msafiri mwenye kutafakari kila aliposoma ukurasa imani yake ilipata nguvu, ambayo ndio ufunguo wa furaha, na maarifa yake ya Allah (s.w) yaliongezeka ambayo ni ufunguo wa ngazi za kimaanawy, na katika busara yake ilifunuka ngazi nyengine katika hakika za kuamini Allah (s.w) ambao ndio msingi uliyonyooka kwa makamilifu yote na chemchem ya ujazo mtamu. Pamoja na kuwa amefahamu masomo bayana na timamu kutoka mbinguni, angani na ardhini, akawa anatafuta ziada, kila kurasa hizo zilivyompa vionjo vitamu na vizuri vya kimaanawy, na ladha nyingi za kiroho zikichochea shauku yake na kuzindua hamu yake vikali kwa kusema: Je, kuna ziada? tahamaki anasikia mwangwi wa dhikiri za (Bahari, na Mito mikubwa) ambayo inabubujika unyenyekevu na shauku, anasikiliza minong’ono yenye huzuni yenye ladha, ikisema kwa lugha ya kauli na hali: “Hututizami sisi? Hutupitii?” hapo anatazama kwa mtazamo wa kutahayari na kuona: Bahari ambazo zinapiga mawimbi kwa uhai na kupigapiga vikali daima, ambapo hali yake ni kutawanyika na kujimwaga na kugharikisha, imezunguka tufe la ardhi, viwili hivyo vinatembea pamoja katika ukomo wa kasi na kwenda ndani ya mwaka mmoja mnamo duara kadiri yake ni miaka ishirini na tano elfu, na pamoja na yote haya, haitengani kamwe wala haimwagiki kabisa wala haimezi jirani yake nchi kavu, hapana budi kuwa inatulizwa na kuendeshwa na kuhifadhiwa kwa amri ya ambaye ana uweza usio na mipaka, na ukuu usio na mipaka.

Kisha anatazama ndani ya tumbo la bahari na kuona – zaidi ya lulu zake zenye kung’ara ambazo ziko kwenye upeo wa uzuri na mapambo na mpangilio – kwamba kuwapa maisha maelfu ya wanyama anuwai na kuwatawala na kuainisha mazazi yao na vifo vyao vinakwenda katika ukomo wa mpangilio na ustadi, na kwamba kuja kwa riziki zao na kuanzishwa kwa vyakula vyao kutokana na mchanga rahisi na kutokana na maji chumvi, ni kwepesi na kamili kiasi kwamba inathibitisha wazi kuwa hayawi hayo ila kwa uendeshaji wa Mweza mtukufu, na kutunuku maisha kwa mwingi wa rehema mwenye uzuri. Kisha msafiri yule anatazama mito, na kuona kuna manufaa na masilahi, huduma na kazi na matokeo ya masurufu na mapato yanayotoa yaliyohesabiwa kwa hekima pana, na kwa rehema kubwa kwa kiasi kwamba inathibitisha kwa uwazi kuwa vidimbwi vyote na mifereji na chemchem na mito mikubwa inachimbuka na kutembea kutoka katika hazina ya mwingi wa rehema mwenye utukufu na ukarimu, bali inahifadhiwa na kuwekezwa kwa namna inayofurutu ada iliyozoeleka, hubadili na kwenda mwendo wa juu kuliko uliyozoeleka, hata imepokelewa katika hadithi sharifu ambayo maana yake ni: (Hakika mito minne inatembea kutokea peponi).

Uk 42.  Kutoka kwa Abu Huraira amesema: Amesema mjumbe wa Allah (s.a.w): “Sayhan na Jayhan na Furati na Nili yote ni miongoni mwa mito ya peponi”. Tazama: Al-Bukhary, kuanza kwa uumbaji 6. Manaqib al-Answary 42. Al-Ashribat 12. Muslim, Al Iman 264, al-Jannah 26. Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad 2/260, 289, 440, 3/164, 4/208, 209.

Kwa maana kutembea kwa mito hii, ni juu ya hisabati za sababu za dhahiri kwa namna nyingi tu, kwa hiyo haitembei ila kutoka katika hazina ya pepo ya kimaanawy isiyokatika na kutoka katika chanzo cha ghaibu kisichotindikia. Kwa mfano: Huu mto wa Naili ambao umebadili majangwa ya Misri kame kuwa bustani ya dunia, unatembea kama bahari ndogo bila ya kuisha na unachimbuka kutokea katika mlima uliopo kusini unaitwa (Jabali al-Qamar), lau maji yake yangekusanywa kwa miezi sita na kukaushwa, ingepatikana kilicho kikubwa kuliko mlima huo! hali ya kuwa mahali palipowekwa mahsusi kwa ajili ya kuhifadhi hapafikii sudusi ya mlima huo, ama maingizo yake ni machache sana, kiasi ubahili wa mvua, ukali wa joto la eneo hilo na ukame wa ardhi, vyote hivyo kwa pamoja haviweki nafasi yeyote ya kuhifadhi isipokuwa chache, wala haviruhusu katika uhifadhi katika mizani ya maingizo yake na matoleo yake, kwa ajili hiyo, imepokewa kuwa huo mto unatembea kutokea (Pepo) ya namna isiyoonekana ambayo iko juu ya kanuni za kiardhini za kawaida. Mapokeo hayo yamemaanisha hakika muhimu yenye faida ya kina sana.

Kama hivyo, msafiri ameona ushahidi mmoja na hakika moja katika maelfu ya shahidi na hakika ambazo ni pana sawa na upana wa bahari zenyewe, na amefahamu kwamba zote hizo zinakariri kwa pamoja na kwa nguvu ya ukubwa wa bahari:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

na wamedhihiri mbele yake mashahidi kwa idadi ya viumbe wa bahari kusadikisha ushahidi huu.

Na kwa ajili ya kubainisha ushahidi wa bahari na mito kwa pamoja, ngazi ya nne imemaanisha katika kituo cha kwanza yafuatayo:

[Hapana Mola wa kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye vimejulisha juu ya kupasa kuwepo kwake katika umoja wake: Bahari zote na mito yote na vilivyomo vyote kwa ushahidi wa utukufu wa kuzungukia kwa hakika ya: Utiishaji, uhifadhi, na uendeshaji mpana wenye kupangika kwa kushuhudia].                            

Kisha milima na majangwa vinamwita msafiri yule aliyezama katika utalii wa kifikra kwa kusema: “Husomi vilevile ukurasa wetu?”, naye kwa upande wake anatazama kwa makini na kuona kwamba kazi za jumla za milima na faida zake za jumla zina ukubwa na hekima inayohemeza akili.

Kwa mfano:

Kudhihiri kwa milima na kujisukuma kwake kutoka ardhini kutokana na amri ya kiungu inatuliza ukali wa ardhi na kupunguza hasira yake na ukali wake unaotokana na migeuko yake ya ndani, na kuiacha ipumue kwa kupumzika kwa kufoka kwa milima hiyo kupitia tundu zake, na kwa hiyo hujikomboa kutokana na mitetemeko ya kuangamiza na mipasuko yenye kuteketeza, na hairudi tena kunyang’anya raha ya wenye kubaki kwa amani katika wakazi wake. Kama inavyosimikwa nguzo na vigingi kwa ajili ya majahazi ili kuhifadhi mizania yake na kuyakinga na misukosuko na kuzama, hivyohivyo milima ni vigingi vyenye hazina kwa ajili ya jahazi la ardhi, inailinda isipate mitetemekona kuithibitisha na kuhifadhi urari wake. Na Qur’an tukufu imebainisha maana hizi katika aya nyingi:

 وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا Qur’an, 78: 7.

 وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ Qur’an, 15: 19.

 وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا Qur’an, 79: 32.

Kwa mfano:

Hakika yaliyomo ndani ya milima miongoni mwa aina za mifereji, maji, madini, mada na madawa, yote hayo yanahitajiwa na viumbe hai, vimewekezwa kwa hekima na kuhudhurishwa kwa ukarimu na kuhifadhiwa kwa utawala kwa kiasi ambacho inathibitisha kwa uwazi kabisa kwamba milima hii ni hazina na ghala za kuhifadhia chini ya amri ya Mweza ambaye uweza wake hauna ukomo, na mwingi wa hekima ambaye hekima zake hazina ukomo. Msafiri anatambua hili, na anapima kwa johari hizi mbili yanayozifuatia katika kazi za milima na majangwa na hekima zake – ambayo ni kwa ukubwa wa milima na upana wa majangwa – anaona kwamba milima na majangwa vinashuhudia na kupwekesha kwa:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

kwa ulimi wa hekima zake zote na kwa lugha ya nyadhifa zake zote na kwa hasa uhifadhi wake wa akiba katika maada na kwamba shahada hiyo na Tawhidi vina nguvu kujikita kiasi cha tambo za juu, na vina uenevu na upana kiasi cha mawanda makavu na majangwa ulimi unakariri kwa unyenyekevu: Nimemwamini Allah (s.w).

Na kama hivyo yametajwa katika ngazi ya tano katika kituo cha kwanza katika kubainisha maana hii yafuatayo:

[Hapana Mola wa kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye wajibu wa uwepo wake umejuulishwa na: Milima na majangwa yote, kwa vyote vilivyomo ndani yake na juu yake, kwa ushahidi wa utukufu wa kuzungukia kwa hakika ya: Kuwekeza, kuendesha, kutawanya mbegu, uhifadhi, uongozi na kuzungukia kwa namna ya kiungu kuliko kupana enevu kuliko pangika kwenye kukamilishwa kwa kushuhudia].

Na wakati msafiri huyu alipokuwa anazunguka kifikra milimani na majangwani, ulifunguka mbele ya fikira yake mlango wa ulimwengu wa (Miti na Mimea) ukimwita kwa kusema: “Njoo kwetu na utembee katika bustani zetu na usome mistari yetu”, akaingia na kuona kuwa miti na mimea imefanya kikao kikubwa chenye kupendeza cha tahalili na Tawhidi, na kutengeneza halaka yenye heshima ya dhikiri na shukurani. Akajua kutokana na ndimi za hali zao kana kwamba zinatamka pamoja, na kukariri kwa umoja:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

kutokana na alichoona miongoni mwa hakika tatu kubwa za jumla zinajulisha kuwa miti yote yenye kuzaa matunda na mimea yote yenye kuchanua maua inatimiza shahada yake kwa kuleta tasbihi na kusema kwa pamoja, kwa ndimi fasaha za majani yake yaliyolinganishwa vipimo, na maneno mazuri ya maua yake mazuri na kwa maneno bayana ya matunda yake yaliyonadhimika:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ) 

Kwanza:

Hakika ya kuneemesha na kukirimu yenye kukusudiwa, na hisani na kutunuku kwa kutaka, ambako kunatambulika maana yake kwa utambuzi wa kidhahiri katika kila mmea na mti, kama ilivyo ni hakika ya dhahiri ya wazi uwazi wa jua katika vyote.

Pili:

Hakika ya kupambanua na kutenganisha kulikokusudiwa kwa hekima, na kupamba na kutia sura kulikokusudiwa kwa rehema, nayo iko wazi uwazi wa mchana – hakika na maana – kupambanua baina ya aina hizo na vitu hivyo visivyokuwa na mpaka ni shabaha iliyokusudiwa, hitilafu na kutofautiana kati yake ni hekima inayotakiwa, na miguso ya kutia uzuri na kupendezesha ni rehema yenye kutakiwa, na hakika hii iko wazi uwazi ambao katu hauachi uwanja wa sadfa, jambo linalodhihirisha bayana kuwa ni athari za fundi mwenye hekima na nakshi zake zenye kupendeza.

Tatu:

Hakika ya kufungua sura za vitu vilivyotengenezwa visivyokua na mipaka, kwa mamia ya maelfu ya sampuli tofauti na maumbo anuwai kutokana na punje nyingi zenye kurandana, na kutokana na kokwa maalum zenye kufanana, na kuziotesha katika ukomo wa mpangilio na urari na ukomo wa mapambo na urembo, pamoja na kuwa ni rahisi zisizo na uhai na zenye kuchanganyika. Basi kufungua sura ya kila mojawapo katika idadi ya aina hizo tofauti – ambazo zinavuka aina mia mbili elfu – kila moja kipekee kwa mapangilio kamili na kwa vipimo timilifu na hali ya uhai na hekima na pasi na makosa, ni hakika yenye kung’ara iliyo wazi zaidi kuliko jua.

Mtalii akafahamu kuwa wapo mashahidi na dalili za kuthibitisha juu ya hakika hiyo kwa idadi ya maua ya majira ya machipuo, na kwa idadi ya matunda yake na kwa idadi ya majani yake na vilivyomo, akaelezea kuhusu yaliyopita moyoni mwake kuhusu maana njema akasema:

(Alhamdulillahi kwa neema ya imani).

Na kwa kubainisha hakika hizi na shahidi hizi yametajwa katika ngazi ya sita ya kituo cha kwanza yafuatayo:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye kupasa kwa uwepo wake kumejulishwa katika upweke wake na: Makubaliano ya pamoja ya aina zote za miti na mimea, yenye kusoma tasbihi na kutamka kwa maneno ya majani yake yaliyopimika na ya fasaha, na maua yake yenye kupambika yaliyo tele, na matunda yake yaliyopangika yenye bayana, kwa kushuhudia utukufu wa kuzungukia kila jambo wa hakika ya uneemeshaji, ukarimu na hisani kwa makusudi na rehema, na hakika ya upambanuzi na upambaji na kuweka sura kwa kutaka na kwa hekima, pamoja na hali isiyopingika ya umaanishaji wa kufungua sura zake zote zilizowekwa katika vipimo zilizopambwa zilizo mbalimbali anuwai zisizo na mpaka kutoka katika kokwa na punje zenye kufanana na kushabihiana, zenye kudhibitika, kiasi chenye idadi maalum].

Wakati msafiri mwenye hamu ya kujua – ambaye alizidi kupanda kwa maonjo na shauku – alipokuwa akirudi kutoka katika safari ile ya kiutalii wa kifikra hali ya kufurahia kwa utamu wa kusimama kwenye hakika na kupata kwake bustani za imani, na kurejea kutoka katika bustani ya majira ya machipuo, hali ya kubeba shada kubwa pana, – kutoka katika maua ya maarifa na imani – upana wa majira ya machipuo yenyewe, tahamaki mlango wa ulimwengu wa ndege na wanyama unafunguka upande wa akili yake inayotafuta hakika na fikra yenye shauku ya maarifa, wale ndege na wanyama wakimwita kwa mamia ya maelfu ya sauti zilizo tofauti na lugha mbalimbali, kwa ajili ya kuingia katika ulimwengu huo mpana na kukaribisha ujio wake katika ulimwengu wake, akaingia ulimwengu ule na kuona kuwa ndege wote na wanyama wote kwa sampuli zake na mataifa yake na makundi yake yote yanataja kwa hali ya kuafikiana (لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ) kwa lugha ya hali yake na kauli yake, hata kana kwamba sura ya ardhi ni baraza la dhikiri la kutisha na mkusanyiko mkubwa wa tahalili, na akaona kila moja kati ya hizo yenyewe kwa dhati yake ni mfano wa kasida ya kiungu inaziimba neema za kiungu, na ni neno la kisubhana lenye kutamka kwa kutukuza Muumba wake, na herufi ya kirahmani yenye maana inayotokana na rehema ya kiungu mwingi wa rehema, wote wanamsifia Muumba wao na wanamsifu kwa himidi na kumnata, kana kwamba milango ya fahamu ya ndege hao na wanyama na hisia zao na viungo vyao na ala na vyombo vyao na nguvu zao, maneno yaliyopimwa na kupangiliwa, na maneno fasaha ya kufahamika, katika hilo yule mtalii akaona hakika tatu kuu zenye kuzungukia pande zote zenye kujulisha kwa ukweli kwamba ndege wale na wanyama wanatekeleza shukurani yao kwa Muumba wao na Mruzuku wao kwa maneno hayo na kushuhudia upweke wake (s.w) kwa maneno hayo.

Ya kwanza:

Hakika ya kupatisha, kutengeneza na ufundi, yaani hakika ya kuhuisha na kutunuku roho, na ambayo haiwezekani kuinasibisha kabisa na usadifu wa holela na nguvu pofu na asili ziwi, kwani ni kupatisha kutokana na  pasipo kuwepo kunakotokea kwa hekima, na ufundi ulioambatana na utengenezaji mzuri, na uumbaji unaosuhubiana na kutaka, na uanzishaji utokanao na elimu, inadhihirisha kwa uwazi wa kudhihirisha (Elimu, Hekima na Utashi) kwa namna ishirini, nayo ni hoja dhahiri juu ya kupasa uwepo wa (Al-Hayyu Al-Qayyum) na shahidi wa haki juu ya sifa zake saba zilizo tukufu na aya ya kweli juu ya ukweli wa upweke wake (s.w). Yaani hakika ya kuhuisha inasukuma katika uwepo ushahidi wa kuthibitisha kwa idadi ya wenye roho wote.

Pili:

Hakika ya kupambanua, kupamba na kusawiri ambako kunajiweka wazi kupitia hivyo vilivyotengenezwa visivyo na mipaka ambavyo vinatofautiana kati yao kwa alama zenye kutenganisha zenye kupambanuka katika sura mbalimbali, na kwa maumbo yenye kupambika mazuri yaliyo tofauti, na kwa vipimo madhubuti mbalimbali, na kwa sura zenye kupangika na kuratibika, ni hakika yenye nguvu kuu kwa namna ambayo haiyumkiniki kumiliki kitendo hiki chenye kuzunguka ambacho kina dhihirisha – waziwazi – maelfu ya hekima na vifurutu ada isipokuwa Mweza juu ya kila kitu na mjuzi wa kila kitu, na hakuna uwezekano mwingine kabisa.

Tatu:

Hakika ya kufungua picha za wanyama hao zisizokuwa na mipaka kwa mamia ya maumbo na sampuli kutokana na mayai na vijiyai vyenye kufanana, na kutokana na matone maalum yenye kushabihiana au kutofautiana kwa tofauti ndogo sana. Basi kufungua sura hizo – ambazo zenyewe ni muujiza wa hekima – kwa mpangilio kamili na uwiano wa vipimo uliyo timamu pasi na kuwepo kosa lolote wala kasoro, ni hakika ya wazi inayochota nuru yake kutokana na dalili na maegemeo kwa idadi ya wanyama wote.

Na kama hivi mtalii ameshuhudia ulimwengu wa ndege na wanyama na amepokea somo kamili kutokana na dalili za hizi (Hakika tatu) zenye kuafikiana, dalili ya wazi ya kwamba aina zote za wanyama zinashuhudia hali ya kusema kwa pamoja:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

mpaka ikawa ardhi kana kwamba ni mwanadamu mkubwa kabisa inataja

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

kwa kulingana na ukubwa wake inajaza – kutokana na nguvu yake – kuba la mbingu hadi watu wa mbinguni wanasikia.

Na hakika yametajwa katika ngazi ya saba ya kituo cha kwanza kubainisha hakika hizi maneno yafuatayo:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo ambaye juu ya kupasa kuwepo kwake katika umoja wake kumejulishwa na: Kuafikiana kwa wanyama wa aina zote na ndege wenye kuhimidia na kushuhudia kwa maneno ya hawasi zake na nguvu zake na vyenye kuhisi na vilivyo laini vyake vilivyopimwa kupangika na fasaha, na kwa maneno ya zana zake, viungo vyake, na ala zake zenye kukamilisha zenye kufikisha ujumbe fasaha, kwa kushuhudia utukufu wa kuzungukia uhakika wa kupatisha kutengeneza na kurembesha kwa ajabu kwa utashi, na hakika ya kupambanua na kupamba kwa makusudio. Na hakika ya kukadiria na kutia sura kwa hekima, pamoja na dalili ya kukata ya hakika ya kufungua sura zake zote zenye kupambika zenye kutofautiana za aina mbalimbali zisizohesabika kuanzia kwenye vijiyai na matone yenye kufanana yenye kudhibitika].

Kisha mtalii huyu mchunguzi akataka kuingia ulimwengu na dunia ya mwanadamu ili aendelee zaidi katika ngazi zisizo na mpaka za maarifa ya kiungu, na apande daraja ya juu zaidi ya vionjo vyake, na nafasi yenye hadhi zaidi katika nuru zake zisizo na ukomo, na hapo wakamuita apate kuingia wateule wa wanadamu wa kwanza ambao ni (Manabii (a.s)) na akapita akitembea ndani ya zama kabla ya kila kitu akaona kwamba (Manabii wote (a.s)) – nao ni kundi bora zaidi la wanadamu wote na kamilifu zaidi kuliko wao wote – wanataja kwa ulimi mmoja na wanakariri pamoja kwa makubaliano ya ujumla:

(لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ)

nao wote wanalingania katika Tawhidi safi kwa nguvu ya miujiza yao ya wazi yenye kuwasadikisha wao na malinganio yao, na kaona kuwa wote hao wanawalingania wanadamu katika kumwamini Allah (s.w), ili kuwatoa katika daraja la unyama na kuwainua hadi daraja la malaika, kwa ajili hiyo yule mtalii alipiga magoti kwa adabu kubwa na heshima kubwa katika kumbi za shule hiyo ya kinuru na kaona kuwa mbele ya kila mmoja kati ya hao maimamu waongofu wenye hadhi ya juu katika wanadamu kuna miujiza na yenye kufurutu ada, ikiwa ni alama za kuwasadikisha kutoka kwa Mola mlezi wa walimwengu (s.w). Na kwamba limeundika kundi kubwa na taifa kubwa lenye kusadikisha miongoni mwa wanadamu, walioingia katika ngome ya imani kwa ufikishaji wa kila mmoja kati yao, na kwa ajili hii yule mtalii aliweza kulinganisha kiwango cha nguvu ya Tawhidi na umadhubuti wake. Hakika ambayo hao wa kweli wameafikiana ambao wanavuka zaidi ya mia moja elfu na akafahamu vilevile kiwango cha kosa kubwa na jinai kuu ambayo hufanywa na watu wa upotevu wenye kukanusha hakika hiyo madhubuti yenye nguvu hii na ambayo wameisadiki na kuiunga mkono idadi hii ya wapasha habari wa kweli na kuthibitisha kwa miujiza yao ambayo haina mpaka. Halikadhalika akatambua kiasi wanachostahiki cha adhabu iumizayo ya milele, na akajua vilevile kiwango cha kusibu na haki ya wale waliowasadiki na kuwaamini wakaingia katika ngome ya imani. Kwa hiyo mbele yake ikadhihiri nafasi kuu ya utakatifu wa imani na cheo cha Tawhidi.

Ndiyo, hakika miujiza isiyo na hesabu ni usadikishaji wa kimatendo kutoka kwa Mola wa haki (s.w), kwa manabii (a.s). Na mapigo ya kimbinguni yaliyoshuka kwa wakanushaji wapingaji yamedhihirisha manabii kuwa wenye haki na Allah (s.w) kuwaunga mkono. Na makamilifu yao ya kihaiba na maelekezo yao ya sawasawa yanajulisha kuwa wao wako kwenye haki yenye kung’ara mno. Na nguvu ya imani yao na upeo wa jitihada zao za kweli na ukomo wa kujitakasa kwao vyote hivyo vinashuhudia juu ya ukweli wao na kusibu kwa malinganio yao, na vilivyomo mikononi mwao ikiwemo vitabu na nyaraka takatifu, na wanafunzi wao wasiokuwa na idadi na ambao wamefikia hakika na kupanda katika ukamilifu na kuongoka katika nuru kwa ajili ya kuwafuata kwao wao, vyote hivyo vinashuhudia haki na kusibu kwa njia yao. Na juu ya yote haya hakika makubaliano ya hao wenye kufikisha, wa kweli katika masuala yenye kuthibitika kwao hakika ni hoja ya kukata shauri kabisa juu ya ukweli wa imani na ni nguvu kubwa inayoimarisha hakika yake kwa namna ambayo kamwe nguvu yoyote ile ulimwenguni haiwezi kupambana nayo. Ni hakika yenye kuvunja hoja, mbele yake huondoka kila utata na shaka.

Mtalii akajua hekima ya kuwa kuwasadiki mitume wote ni nguzo katika nguzo za imani, na kwa vipi hiyo ni chemchem yenye kusukuma kwa kasi na chanzo kikubwa cha nguvu cha imani yake, basi haraka akachota kutoka katika chemchem hii iliyojaa.

Imeshatajwa katika ngazi ya nane katika kituo cha kwanza yenye kuleta maana ya yaliyomo kwenye somo lililoelezwa kwa huyu mtalii.

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki, ambaye kupasa uwepo wake katika upekee wake kumejulishwa na makubaliano ya manabii wote kwa nguvu ya miujiza yao yenye kudhihiri wazi yenye kusadikisha na kusadikishwa].

Na wakati mtalii yule mwenye kutafuta ambaye ameonja maonjo matukufu kutokana na nguvu ya imani na kavuta hewa ya maisha safi kabisa anarejea kutoka baraza la (Manabii (a.s)) wakamwita wale ambao wamethibitisha kwa elimu ya yakini na wakasimamisha hoja zenye kuvunja ubishi juu ya ukweli wake miongoni mwa Maulamaa wenye kuhakikisha na Mujitahidina waliozama ambao wote huitwa Asfiyaa na Masiddikina (wateule na wafuasi wa ukweli), hao walimwita katika madrasa zao akaingia na kuona mkusanyiko mkubwa uliosheheni maelfu ya mabingwa wasio na kifani na mamia ya maelfu ya wachunguzi makini katika watu wenye elimu na uhakiki wakisimamisha dalili na kunyoosha hoja na kuthibitisha – kwa uchunguzi wao wa kina ambao hauachi shaka japo kidogo – masuala ya kiimani yenye kuthibiti na mwanzoni mwao kupasa kwa uwepo wa Muumba (s.w), na upweke wake.

Ndiyo, hakika kuafikiana kwa wanazuoni hao wakubwa – pamoja na kutofautiana maandalizi yao na kupishana kwa vipawa vyao vya kimaumbile na kutofautiana kwa maslaki zao – juu ya misingi ya imani na nguzo zake, kila mmoja akiegemea juu ya nguvu ya hoja zake na yakini yake, ni hoja ya kiumaliza ubishi, haiwezekani yeyote kuipinga au kuivunja au kubishana nayo, isipokuwa kama ana busara kali zaidi na ya juu zaidi kuliko ya wakuu hao, na hoja yake ikiwa ni yenye nguvu zaidi kuliko hoja za hao wote! na hili ni muhali, na kwa hiyo haiyumkiniki kukabiliana nazo isipokuwa kwa ujinga na kujifanya kutokujua na kukanusha katika yasiyowezekana kuyathibitisha katika masuala yenye kukanushwa, au kwa ukaidi na kufumba jicho upande wa nuru hiyo, na hali ya kuwa yule afumbaye macho yake ameufanya mchana wake kuwa ni usiku.

Yule mtalii akafahamu kuwa nuru ambazo hawa Maustadhi wamezieneza waliobobea katika shule hii tukufu yenye kuangaza hakika zimeangazia nusu ya tufe la ardhi ndani ya  kiasi cha miaka elfu moja, na kutokana na hili akapata nguvu ya kimaanawy kubwa ikijikita katika haiba yake, na kujaza pambizo zake kwa kiasi ambacho lau kama wakanushaji watajikusanya na wakaidi wote kwa ujumla hawataweza kumteteresha japo chembe ya unywele mmoja. Na kama hivi imetajwa ishara ya muhtasari katika ngazi ya tisa ya kituo cha kwanza kwa yale aliyoyachota mtalii katika shule hii miongoni mwa masomo na mazingatio kama ifuatavyo:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w) ambaye kupasa uwepo wake kumejulishwa na kuafikiana kwa wateule wote kwa nguvu ya hoja zao zenye kung’ara zenye kuhakikisha na kuafikiana].

Na huyo msafiri mchunguzi alipokuwa anarejea kutoka katika shule ya wanazuoni ilimsonga shauku ya kuzidi kwa imani na kufunuka kwake, na kumtawalia raghba kubwa ya kuona nuru na maonjo ambayo yapo katika njia ya kupanda cheo kutoka katika ngazi ya ujuzi wa yakini kwenda ngazi ya kuona kwa dhati ya yakini. Wakamwita maelfu na mamilioni ya (Mawalii wema) viongozi wenye hadhi ambao walijitahidi kutafuta hakika na wameifikia haki na kufika ngazi ya kuona kwa jicho la dhati ya yakini kwa utukufu wao na kupanda kwao chini ya kivuli cha ngazi ya mtume Muhammad (s.w), na kwa kufuata nyayo ya mtume (s.a.w) katika njia kuu ya Muhammad. Hawa walimuita kwenda katika mahali pakuu pa dhikiri penye bashasha, na mahali pa mwongozo ulionyooka mtukufu, panachomoza baraka na nuru yenye kujaa pande zote, na kububujika chemchem kwa kukutana kiasi kisicho kuwa na mpaka cha vituo vyao. Akaingia na kuona watu wa Al-Kashfu na karama hawa wana kariri kwa kuafikiana na kukubaliana kwa pamoja: (lailaha illaa huwa) wakitangaza kwa kusema hivyo, kupasa kwa uwepo wa Mola mlezi (s.w) na upekee wake, wakiegemea katika kufunuliwa kwao na karama zao na mambo waliyoyashuhudia.

Naam, kama ilivyo jua linatolewa dalili ya uwepo wake kwa rangi saba za mwanga wake, hakika ya Tawhidi vivyo hivyo wanazisadikisha hawa watambuzi wakipekee na mahodari wenye nuru kwa ijmai na kuafikiana, nao wanawakilisha watu wa tarika anuwai za kweli na watu wa maslaki mbalimbali zenye kusibu na wenye mashirabu mengi ya haki ambao wamejiremba kwa rangi sabini, bali kwa idadi ya majina mazuri ya Allah (s.w), miongoni mwa rangi zenye nuru yenye kudhihiri katika nyoyo na anga kutokana na nuru ya azali na milele. Yule mtalii alishuhudia kudhihiri kwa hakika hiyo ya wazi, kwa jicho la yakini. Kwa hiyo aliona kwamba hakika inayokubaliwa kwa pamoja na (Manabii a.s), na wanayowafikiana juu ya ukweli wake (Wanazuoni wateule) na wanayowafikiana pamoja nayo (Mawalii wema) ni hakika ya wazi kuliko mwanga wa mchana unaotoa dalili ya kuwepo kwa jua.

Na kama hivyo imeelezwa katika ngazi ya kumi katika kituo cha kwanza ishara ya muhtasari ya alichochukua msafiri huyu miongoni mwa baraka katika rabita za kisufi na zawiya zake:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ambaye juu ya kupasa uwepo wake katika upweke wake kumejulishwa na ijmai ya mawalii kwa funuo zao na karama zao za dhahiri zenye kuhakikisha na kusadikisha].

Kisha yule mtalii akataka kwa kila upole wake na nguvu zake aongezeke kupanda na kuwa juu katika nguvu ya imani na kufunuka maarifa yake kwa Allah (s.w) kwa kujua kwake kuwa mahaba ya Allah (s.w) yatokanayo na imani ya Allah (s.w) na yanayochimbuka kutokana na kumjua ni ukamilifu mkubwa zaidi na muhimu na mkunjufu zaidi wa kibinaadamu, bali ni chimbuko la kamilifu zote na msingi wake, kwa ajili hiyo akanyanyua kichwa chake hali akiangalia mbinguni na kuisemesha akili yake:

Maadamu uhai ni kitu ghali mno katika ulimwengu, na vilivyomo vyote vimetiishwa kwa ajili ya uhai, na kwamba vya thamani mno katika vyenye uhai ni vyenye roho na vyenye hadhi zaidi kati ya vyenye roho ni vile vyenye hisia. Na maadamu tufe la ardhi – kwa ajili ya cheo hiki cha juu – huachwa tupu kila zama na kila mwaka, na kujazwa kwa mfululizo ili kuvifanya vyenye uhai kuwa vingi, hapana budi – na hakuna namna –  mbingu hizi za juu zilizopambwa, ziwe na wakazi na watu wake wenye kuwiana nazo miongoni mwa wenye uhai na wenye roho na wenye hisia. Hadi zimenakiliwa riwaya zenye tawaturi zenye kutilia mkazo kuonekana kwa (Malaika) na kuongea nao tangu zamani, kama kujitokeza kwa Jibril (a.s) katika sura ya mwanadamu na kudhihiri kwake mbele ya masahaba katika baraza la mtume (s.a.w). Yule mtalii akasema: Laiti ningefikia katika utukufu wa kuona wakazi wa mbinguni, na laiti ningejua waliyonayo kuhusu hakika ya imani na Tawhidi. Kwa sababu ushahidi muhimu sana katika haki ya Muumba wa ulimwengu ni ushahidi wao, na hakuwa anakaribia kukamilisha maneno yake hata akasikia ghafla kana kwamba sauti ya mbinguni ikisema: (Kwa kuwa unataka kukutana nasi na kusikiliza somo letu, jua kwamba masuala ya kiimani ambayo yameteremshwa kupitia sisi kwenda kwa manabii wote, na katika utangulizi wao ni Muhammad (s.a.w) aliyeteremshiwa Qur’an tukufu, tumeyaamini sisi kwanza. Na elewa vilevile kuwa roho zote njema kutokana na sisi na zenye kuonekana kwa mwanadamu zote zimeshuhudia pasi na kubagua na kwa kuafikiana juu ya kupasa uwepo wa Muumba wa ulimwengu na upweke wake na sifa zake takatifu. Na kwamba habari nyingi zilizoelezwa zinaafikiana pamoja na kushikana kikamilifu, basi kuafikiana kwa habari hizi kusiko na mpaka na kushikana kwake ni dalili kwako kama jua). Mtalii akayafahamu wanayoyakusudia, na nuru ya imani yake ikang’ara hadi akapanda juu kwenda mbinguni.

Na kama hivi ishara fupi imeeleza somo la malaika alilopata mtalii huyu katika ngazi ya kumi na moja ya kituo cha kwanza:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ambaye ni wajibu kuwepo ambaye uwepo wake katika upekee wake umejulishwa na kuafikiana kwa malaika ambao wanaonekana machoni mwa watu na wenye kuongea na wanadamu mahsusi, kwa habari zao zenye kushikana na kuafikiana].

Halafu msafiri yule mwenye shauku kubwa ya somo ambalo amelipokea kutoka kwa ndimi za makundi maalum na kutokana na hai zao, katika ulimwengu wa kushuhudia na upande wake wa kiwiliwili na kimaada, amepata shauku ya ziada ya safari na utalii na kutafiti na kutafuta hakika hivyo akaendelea mbele kutalii katika ulimwengu wa ghaibu na pia ulimwengu wa barzakh. Mbele yake ukafunguka mlango wa (Akili zilizonyooka sawa zenye nuru na nyoyo salama zenye nuru) ambazo haziwezi kukosa kuwepo katika maumbile ya wanadamu, kwani akili na moyo ni viwili vyenye hukumu ya kiini cha ubinadamu na kwa fadhila ya hivyo viwili ameweza kuwa tunda la ulimwengu, na vinamiliki uwezo wa kukunjuka kiasi cha kuweza kuufunika ulimwengu wote pamoja na udogo wake.

Mtalii akaona kuwa nyoyo na akili ni barzakhi za kibinadamu, kati ya limwengu mbili za ghaibu na wa kushuhudiwa, mahusiano na alama kati ya limwengu hizo mbili – kulingana na mwanadamu – huenda katika nukta hizo, kwa hiyo aliisemesha akili yake na moyo wake kwa kusema: (Njooni, hakika njia fupi mno katika njia zenye kufikisha kuelekea kwenye hakika ni kupitia milango yenu nyinyi wawili, haya tupate faida kwa kutalii kwetu akili na nyoyo zenye kusifikana na imani na kudurusu kwetu namna zake na aina zake, hili ni somo ambalo halichukuliwi kutoka katika ndimi kama ilivyo hali kwenye njia nyingine). Akawa anageuza nyaraka za akili na kukunjua kurasa za nyoyo akiwa anafanya umakini wa kuangalia na kurefusha fikira, kwa hiyo akaona akili zote zilizonyooka zenye nuru zinaafikiana katika itikadi madhubuti zilizo wazi katika imani na Tawhidi, na kuendana katika yakini ya kukata azimia na kujiridhisha kuliko tulivu, pamoja na kupishana kukubwa katika utayari wake na umbali na kuhitilafiana kati ya madhehebu yake. Yaani zimejiegemeza na kufungamana kwa itikadi isiyobadilika na kuingia katika hakika ya tangu isiyokatika, hivyo makubaliano ya akili hizi katika imani na kupasa na Tawhidi hakika ni mnyororo wa kinuru usiyokatika na dirisha pana lenye mwanga mkali uliopo kwenye hakika.

Na kadhalika aliona nyoyo zote salama na zenye nuru zikiafikiana kati yake katika funuo zake na mashuhudio yake – ambayo ni dhati ya kuafikiana, utulivu na kuvutika – katika nguzo za imani, na kuambatana katika Tawhidi pamoja na kuwa mbalimbali maslaki zao na kupishana kwa mashirabu yao. Yaani kila moyo kati ya nyoyo hizi zenye nuru, ni kiti cha enzi kidogo sana kinachotandaa juu yake maarifa ya kiungu, na ni kioo chenye kukusanya nuru za madhihirisho ya kiungu Mtegemewa kwa haja zote, kwa hali inayokabiliana na hakika na kufikisha na kujidhihirisha kwayo, kwa hiyo ni madirisha yaliyo wazi kwa upande wa jua la hakika. Yaani mjumuiko wa nyoyo hizi kunaunda kwa pamoja kioo kikubwa kipana kama bahari mbele ya jua hilo.

Na kuafikiana kwa nyoyo hizi na akili hizi na kakubaliana kwa pamoja katika kupasa uwepo wake (s.w) na katika upweke wake ni dalili kamilifu mno na kiongozi kikubwa hakina shaka yoyote, kwani hakuna uwezekano kabisa wala kutazamiwa katu – katika upande wowote uwao – dhana yeyote isiyo na hakika kuleta udanganyifu na fikira isiyohusu hakika kwa uhusiano na sifa isiyo na asili, kuyadanganya macho yote haya yenye kuona yenye kupenya yaliyo makali ya wingi huu, katika wenye nyoyo safi na akili za sawasawa, na kudumu udanganyifu huu kupitia karne nyingi na kwa kujikita kikamilifu, au wote kuwaingiza katika nyavu ya hadaa na kughafilika. Je! yupo anayeona matazamio kama haya asiyekuwa anayebeba akili mbovu ya uvundo? bali hata Wanasafsata wapumbavu ambao wanakanusha ulimwengu wanaikataa na wala hawairidhii! Kama hivi mtalii alifahamu akasema akienda sawa na akili yake na moyo wake (Nimeamini Allah).

Na kwa kuashiria maarifa ya kiimani katika aliyojifunza mtalii huyu kutokana na akili zilizonyooka na akili zenye nuru pametajwa katika ngazi ya kumi na tatu katika kituo cha kwanza yafuatayo:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ambaye ni wajibu kuwepo kwake ambaye uwepo wake katika umoja wake umejulishwa na mkusanyiko wa akili zilizonyooka zenye nuru kwa itikadi zake zenye kuafikiana na kwa kukinai kwake na yakini zake zenye kuendana pamoja na kutofautiana na maandalizi na madhehebu na kadhalika imejulisha juu wajibu wa uwepo wake katika umoja wake kuafikiana kwa nyoyo salama zenye nuru kwa funuo zake za kuendana na mashuhudio yake yenye kuafikiana pamoja na kupishana kwa masaliki na masharibu].

Kisha mtalii yule ambaye alitazama ulimwengu wa ghaibu kwa karibu na kutembea katika limwengu mbili za akili na moyo, akawa anagonga mlango wa ulimwengu huo kwa mtindo huu wa kutafakari: (Je, nini unasema ulimwengu wa ghaibu?). Ikiwa tunaona katika ulimwengu huu wa kushuhudia wa kimwili haya, kwamba aliyejificha nyuma ya pazia ya ghaibu (s.w) Anaitambulisha dhati yake kwetu kwa kiasi hiki kikubwa katika vitengenezwa vyake vilivyopambwa na kutengenezwa vema, na kutupelekea katika kumpenda yeye kwa kiwango hiki kisichodhibitiwa cha neema zake tamu nzuri, na kutupa habari kuhusu makamilifu yake yaliyojificha  kwa kiwango hiki chenye kupendeza kilichojaa athari zake zenye kufurutu ada za ajabu, naam, ambaye anajitambulisha nafsi yake na kuipendezesha kiutendaji na kwa ulimi wa hali ambao ni fasaha zaidi kuliko maneno na kuongea, hapana budi kwamba ataongea kwa kauli na kuzungumza kama anavyo ongea kwa kutenda na kwa hali akiitambulisha na kuipendekeza nafsi yake.

Kwa hiyo mtalii aliiambia nafsi yake kwa kusema: (Ni juu yetu kumtambua (s.w) katika maonekano ya uungu wake na ubwana mlezi wake katika ulimwengu wa ghaibu). Moyo wake ukazama katika kina kirefu na akaona kwa jicho la akili yake kwamba hakika ya (wahyi wa kiungu) ni yenye kutamalaki kila wakati – kwa mambo yenye kudhihiri katika upeo wa nguvu na uwazi – katika pande zote za ulimwengu wa ghibu. Ushahidi wa kuwepo kwake na upweke wake (s.w)  unakuja kutoka kwa mjuzi wa ghaibu yote. Nao ni ushahidi wa wahyi na ilhamu ambao ni wenye nguvu zaidi kuliko ushahidi wa viumbe, kwa kuwa Allah (s.w) haachi kuitambulisha dhati yake wala dalili za uwepo wake na upweke wake kuishia katika ushahidi wa viumbe vyake pekee, bali anaongea maneno ya kiazali yanayowiana na dhati yake, basi hakuna mpaka wala ukomo wa maneno ya ambaye ni mwenye kuhudhuria na kutazama kila mahali kwa uweza wake na elimu yake. Na kama yanavyomtambulisha kimaana maneno yake hakika kuongea kwake pia kunamtambulisha kwa sifa yake.

Naam, hakika kuja kwa tawaturi laki moja ya manabii (a.s) na kuafikiana kwao katika upashaji wao habari wote, utokanao na wahyi wa kungu, na dalili na miujiza ya vitabu vitakatifu na nyaraka za mbinguni ambazo ni wahyi ulioshuhudiwa na matunda yake, na ambao wameusadikisha walio wengi kabisa katika binadamu na kuufuata na kushika mwongozo wake, kumemfanya mtalii afahamu kwa uwazi kwamba wahyi ni hakika iliyothibiti hakuna ubishi katika hilo.

Na amefahamu vilevile kwamba hakika ya wahyi ina maana ya hakika tano takatifu kuitilia mkazo na kuipa nuru.

Kwanza:

Kuongea kulingana na fahamu za wanadamu na kwa kiwango cha akili zao ndio kunakoitwa kuwa ni (Kujishusha kiungu kuzielekea akili za wanadamu) naam, ambaye amewasemesha wenye roho wote katika viumbe wake na anajua wanayoongea, uungu wake unalazimisha kuweka maana ya maneno yake ya kiazali katika maneno yatakayokuwa mepesi kwa wanadamu kuyasoma kati ya maneno yao.

Pili:

Hakika yule aliyeumba uwepo katika hali ya miujiza na kujaza miujiza yake ya kushangaza ili kuubainisha, na kuifanya kuwa ndio ndimi zenye kuzungumzia makamilifu yake, hapana budi kuwa atatambulisha dhati yake pia kwa maneno yake.

Tatu:

Hakika ambaye anajibu kwa matendo maombi ya watu wa kihakika na shukrani zao, nao ni muhtasari wa vilivyomo na taji lake na wenye haja zaidi na shauku zaidi na wenye upole zaidi, hakika kujibu maombi hayo na shukurani hizo kwa maneno yake (s.w), ni katika jambo la sifa ya uumbaji.

Nne:

Hakika sifa ya kuongea ambayo ni ya dharura ya lazima na jambo lenye kuangazia sifa mbili: (elimu) na (uhai) hapana budi kuwa inapatikana kwa sura ya kuzungukia na ya umilele kwa mwenye elimu yenye kuzungukia kila kitu na uhai wa milele.

Tano:

Ambaye ameumba viumbe wake juu ya kushindwa na shauku, ufukara na uhitaji, na hofu ya hatima, na kuwatunuku mahaba na uja, hata wakawa wanahisi mahaba makali na shauku kubwa kwa kutaka kumjua Mola wao wa haki na mwenye kumiliki mambo yao, na wanahisi uhitaji wao mkubwa katika nguvu ya kuegemea – hali wakiwa wanageuka geuka katika ufakiri, kushindwa, na hofu ya hatima – basi ni kutokana na hali ya uungu wake huwajulisha uwepo wake kwa kuongea kwake (s.w).

Na namna hii mtalii yule amefahamu kwamba dalili zinazojulisha kwa makubaliano juu ya uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo, na upweke wake (s.w), katika wahyi wa mbinguni wa jumla ambao ndani yake kuna (kujishusha kwa kiungu) na (utambulisho wa kiungu) na (majibu ya kiungu mwingi wa rehema) na (mazungumzo matakatifu) na (ujulisho wa kiungu mtegemewa kwa haja zote) ni hoja kubwa, bali zina nguvu kuliko ushahidi wa jua kwa lenyewe katikati ya mchana.

Halafu alitazama katika (ilhamu) akaona kuwa ilhamu za kweli pamoja na kuwa zinafanana – kwa upande  mmoja – na wahyi kutokana na kuwa kwake aina ya maongezi ya kiungu, ila kuna tofauti mbili:

Ya kwanza:

Ni kwamba wahyi ambao ni wa juu kuliko ilhamu kwa mengi hakika hufanyika kwa njia ya malaika, wakati ambapo ilhamu kwa kiwango kikubwa mno hufanyika pasipo mkaa kati, na ili kufafanua hilo tunaleta mfano ufuatao:

Katika yajulikanayo ni kuwa kuna namna mbili za sura za kuwasiliana na kutoa amri kwa mfalme:

Kwanza:

Kwa jina la dola na utukufu wake na utawala wake na mamlaka yake kwa wote, basi humtuma mmoja ya washenga wake kwa mmoja ya maliwali wake, – na mara nyingine – hukutana naye, na hapo hufikisha hiyo amri, na hii huwa kwa ajili ya kuonesha utukufu wa utawala ule na umuhimu wa amri hiyo.

Pili:

Kwa jina lake binafsi na sio kwa jina la ufalme wala siyo kwa anuani ya mfalme huongea maneno maalumu, kwa simu yake binafsi katika jambo maalum na katika muamala mdogo pamoja na mtumishi wake maalum au pamoja na mmojawapo mwa raia wake katika watu wa kawaida.

Hali kadhalika mfalme wa azali anayo maneno ya wahyi na ilhamu ya jumla – ambayo hutenda majukumu ya wahyi – anazungumza kwa jina la Bwana Mlezi wa walimwengu wote, na kwa anuani ya Muumba wa ulimwengu, naye ana mtindo mwingine wa maneno, na kwa namna maalum na kutokea nyuma ya vizuizi na pazia pamoja na kila mmoja, na pamoja na kila mwenye uhai, kulingana na ukubalifu wao, na hii ni kwa kuwa kwake yeye ni Mola wao mlezi na Muumba wao.

Tofauti ya pili:

Hakika ya wahyi ni safi na pasipo kivuli chochote, ni maalum kwa walio maalum, ama ilhamu, kuna kivuli na kuchanganyika kwa rangi, nayo ni ya jumla, na ina namna anuwai, na zenye kutofautiana sana, kama ilhamu za malaika, ilhamu za mwanadamu, na ilhamu za wanyama. Nazo kwa aina zake mbalimbali na maumbo yake yenye kupishana sana hubainisha kiasi cha upana wa maneno ya kuungu na wingi wake ambayo yanazidi idadi ya matone ya bahari. Mtalii kutokana na haya akafahamu upande fulani wa tafsiri ya aya tukufu:

 قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي Qur’an, 18: 109.

Halafu alitazama hakika ya ilhamu akichimbua siri yake na kutaka kujua hekima yake na ushahidi wake, akaona kuwa hakika yake, hekima yake na matokeo yake ni jumla ya nuru nne:

Nuru ya kwanza:

Ni kuwa mfano wa ambavyo Allah (s.w) anajipendezesha kwa viumbe wake kupitia matendo yake kwao kunakojulikana kuwa ni (kujipendezesha kwa kiungu) katika yenye kulazimu sifa ya upendo na wingi wa rehema (yaani kuwa yeye ni mwenye wingi wa upendo na mwenye kurehemu) kujipendezesha kwao kwa kauli na kuhudhuria na usuhuba pia.

Nuru ya pili:

Mfano wa anavyojibu (s.w) dua za waja wake kwa matendo yake, katika hali ya wingi wa rehema ni kuwajibu kwa manene vilevile kutokea nyuma ya pazia.

Nuru ya tatu:

Kama anavyojibu Mola (s.w) kwa matendo kuwasaidia viumbe wake wenye kusibiwa na mabalaa magumu na majanga makali na maombi yao na manyenyekeo yao, hakika katika yenye kulazimu na rububiyya kuwaliwaza na kuondosha hofu ya upweke wao hivyo huwasaidia kwa maneno ya kiilhamu ambayo ni katika hukumu ya aina ya maneno yake.

Nuru ya nne:

Kwamba mfano wa namna anavyojulisha (s.w) kimatendo uwepo wake na himaya yake kwa wenye ufahamu katika viumbe wake – ambao wako kwenye kushindwa na udhaifu mkubwa na katika ufakiri na kusongeka kukubwa, na katika uhitaji mkubwa na shauku ya kumjua Muumba wao na muhami wao mwendeshaji wao na muhifadhi wao – basi ni katika yanayolazimu upole wa kiungu na huruma ya kiulezi wa kiungu na jambo muhimu mno kwa sifa hizo, ajulishe vilevile uhadhiri wake na upamoja wake na uwepo wake kwa kiumbe maalum, kwa namna maalum kulingana na ukubalifu wake, kupitia sehemu ya ilhamu za kweli, kwa kauli kuelekea kwenye sauti ya moyo wake, katika yanayohesabiwa katika hukumu ya mazungumzo ya kiungu. Kisha alitazama ushahidi wa ilhamu akaona kuwa kama jua lingekuwa na uhai na hisia – kwa makadirio – na zikawa rangi saba ambao zimo kwenye mwanga wake – kwa makadirio – sifa zake saba kwa hiyo lingekuwa lina mtindo wa mazungumzo kwa mionzi yake na madhihirisho yake yaliyomo kwenye mwanga wake, basi katika hali hii: Uwepo wa sura yake na kuakisi kwake katika vitu vyenye kupokea mwanga; yaani kuongea kwake na kila kioo chenye kuakisi na kila kitu chenye kung’ara, na vipande vya vioo na mapovu ya bahari na matone yake, hata pamoja na atomu zenye kupokea mwanga kulingana na ukubalifu wa kila moja kati ya hivyo na kujibu kwake haja ya kila moja kati ya hivyo, vyote hivyo vitakuwa shahidi wa kweli wa uwepo wa jua, na kukosekana kuzuilia tendo kwa tendo wala kusongamana kwa maneno kutokana na maneno yake mengine.

Basi kama yashuhudiavyo haya kwa uwazi kabisa hivyo ndivyo mambo yalivyo katika mazungumzo ya mfalme wa azali na wa milele mwenye utukufu, na Muumba wa vyote mwenye uzuri, nuru ya azali, ni mazungumzo ya u-wote na kuzungukia kila kitu, kama ujuzi wake (s.w) na uweza wake, kwa hiyo ni dhahiri kabisa inatambulika madhihirisho yake mapana ni kulingana na ukubalifu wa kila kitu, bila ya kuwa swali moja kusongamana na swali lingine, wala tendo moja kulizuia tendo lingine, wala mazungumzo kuchanganyika na mazungumzo mengine.

Mtalii akajua kwa elimu ya yakini kwa karibu namna iwavyo kwenda katika kuona kwa yakini kwamba madhihirisho yote na mazungumzo yote na ilhamu zote hizo kila moja kati ya hizo na kwa ujumla wake, zinajulisha na kushuhudia kwa kuafikiana juu ya kupasa kwa uwepo wa yule mnawirishaji wa azali (s.w) na juu ya umoja wake na upweke wake.

Na kama hivi ishara ya muhtasari imeelezwa kuhusu yale aliyoyapokea huyu mtalii, mwenye hamu kubwa ya somo la ujuzi kutoka katika ulimwengu wa ghaibu katika ngazi ya kumi na nne na kumi na tano ya kituo cha kwanza:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ambaye ni wajibu kuwepo, mmoja, mpweke ambaye juu ya kupasa uwepo wake katika umoja wake kumejulishwa na makubaliano ya wahyi zote za haki zenye kujumuisha teremsho za kiungu, mazungumzo ya kiutukufu, matambulisho ya Bwana mlezi, makabiliano ya mwingi wa rehema wakati wa kuongea na waja wake, na majulisho ya mtegemewa katika haja zote kwa uwepo wake kwa viumbe vyake. Na vilevile kumejulisha juu ya kupasa uwepo wake katika umoja wake kuafikiana kwa ilhamu za kweli zenye kujumuisha mapendezesho ya kiungu na majibu ya kiungu mwingi wa rehema kwa maombi ya viumbe vyake, misaada ya kiungu Bwana mlezi kwa maombi ya unyenyekevu ya waja wake, na matendo ya kufanya hisia ya kiutukufu kwa uwepo wake kwa vitengenezwa vyake].

Kisha yule mtalii alizungumza na akili yake duniani kwa kusema: Kwa kuwa ninamtafuta mmiliki wangu kwa kuvitamkisha vilivyomo kwenye ulimwengu huu ni katika jambo la ukamilifu zaidi kwangu nimtembelee yule ambaye ni mwanadamu mkamilifu zaidi katika uwepo, na mkamilifu zaidi anayeongoza katika kheri – hata kwa kusadikisha kwa maadui zake – na mwenye sauti ya juu zaidi na mkweli wao zaidi kwa mazungumzo na mtukufu wao zaidi kwa daraja na mbora wao zaidi kwa nuru ya akili, ehe naye ni Muhammad (s.a.w) ambaye kwa fadhila zake ameangaza na kwa Qur’an yake muda wa karne kumi na nne, na ili nipate bahati ya zira yake tukufu na kumuuliza kwa ninayoyatafuta kwake yatakikana twende pamoja katika karne bora katika enzi za furaha, enzi za utume. Akaingia na akili yake katika zama hizo akaona kwamba zama hizo zimekuwa zama za furaha ya wanadamu kweli, kwa sababu yeye (s.a.w) amebadili katika muda mfupi kwa nuru aliyowaletea watu walio zama katika ujinga mkubwa na ubedui wa kitambo amewabailisha na kuwa maustadhi na mabwana wa ulimwengu.

Na vilevile aliisemesha akili yake kwa kusema: (Ni juu yetu kabla ya chochote tuelewe jambo kuhusu utukufu wa dhati hii ya miujiza, na hii ni kupitia ukweli wa mazungumzo yake na ukweli wa habari zake, kisha tumuulize kuhusu Muumba wetu (s.w)) akaanza kutafuta na kukuta juu ya ukweli wa unabii wake dalili za kukata shauri zenye kuthibiti kiasi kisichohesabika wala kudhibitika lakini aliishia katika dalili tisa

Ya Kwanza:

Ni kule kusifika kwake mtume (s.a.w) kwa tabia zote njema na mambo ya kusifika hata hayo waliyashuhudia maadui wake na kutokea kwake mamia ya miujiza kama kupasuka mwezi katika vipande viwili kwa ishara ya kidole chake kama Qur’an ilivyoeleza hilo:

 وَانشَقَّ الْقَمَرُ Qur’an, 54: 1.

Na kushindwa kwa jeshi la maadui kwa kuingia machoni mwao wote mchanga mchache aliowamwagia kwa gao lake kama aya ilivyo elezea hilo:

 وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـكِنَّ اللّهَ رَمَى Qur’an, 8: 17.

Na kunywa sahaba zake kutokana na maji yaliyotoka kama mto wa Kauthar kati ya vidole vyake vitano vyenye kubarikiwa walipozidiwa na kiu, na mingine katika mamia ya miujiza iliyotokea kwake na ambayo imenakiliwa kwetu kwa unakili sahihi wa kukata ubishi au mutawatir, basi mtalii akaipekua katika (Andiko la kumi na tisa) yaani (Risala ya miujiza ya Muhammad) risala ile ya ajabu yenye karama inayojumuisha miujiza mia tatu kati ya miujiza yake (s.a.w) kwa dalili zake madhubuti na isinadi zake za kutegemewa.

Kisha akaiambia nafsi yake kwa kusema: (Hakika aliye na tabia njema kwa kadiri hii na fadhila kwa kiasi hiki na miujiza ya kushangaza kwa wingi huu hapana shaka kwamba yeye ni mwenye maneno ya kweli zaidi na kwa mintarafu hiyo haiyumkiniki kamwe – na hasha – kuwa ateremke katika hila, uwongo na ghushi ambao ni mwendo wa mafisadi).

Ya Pili:

Kuwa kwa Qur’an aliyonayo (s.a.w) muujiza katika pande saba, hiyo amri itokayo kwa mmiliki wa ulimwengu ambayo wanaikubali na kuisadiki zaidi ya milioni mia tatu ya wanadamu katika kila zama. Na kwa kuwa (Neno la ishirini na tano) yaani risala ya (Miujiza ya Qur’an) nalo ni jua la Risale-i Nur, imethibitisha kwa dalili zenye nguvu, kwamba Qur’an hii tukufu ni muujiza kwa namna arubaini na kwamba ni maneno ya Mola mlezi wa walimwengu wote, kwa ajili hiyo alilipeleka mtalii yule jambo hilo kwenye risala hiyo mashuhuri kwa ubainisho wake wa upambanuzi wa muujiza. Kisha akasema: Hakika mwaminiwa juu ya maneno ya Allah (s.w) na mkalimani wake wa kimatendo na mfikishaji wa habari hii kubwa kwa watu wote naye ni haki yenyewe hasa na hakika kwa dhati yake haiwezekani kutokea urongo katu na kamwe hatakuwa ni mahali pa kutia shaka.

Ya Tatu:

Hakika mtume (s.a.w) ametumwa kwa sharia safi na kwa dini ya kimaumbile na kwa uja uliyo takata na kwa dua ya unyenyekevu na kwa malinganio yenye kukusanya na kwa imani iliyojikita, hakuna mfano kwa kile alichotumwa nacho na hautakuwepo – na haukupatikana – mkamilifu zaidi kuliko huo, na wala hautapatikana.

Kwa sababu sharia ambayo imedhihiri kutokana na Ummiyyu (s.a.w) na kuongoza humsu ya wanadamu pamoja na tofauti zao tangu karne kumi na nne, mwongozo unaosimamia haki na uadilifu kwa kanuni zake madhubuti zilizosheheni, haikubali mithili kamwe.

Na vivyo hivyo (Uislamu) ambao umetokana na matendo ya ambaye ni Ummiyyu (s.a.w) na kutokana na maneno yake na hali zake, ni kiongozi na chimbuko la milioni mia tatu ya watu na rejea yao kila zama, na mwalimu wa akili zao na mwelekezi wake na mnawirishaji wa nyoyo zao na mwadibishaji wao na mlezi wa nafasi zao na mzunguko wa kufunuka kwa roho zao na madini ya kupanda kwao hakuja wala hatokuja mithili yake.

Na kadhalika kuwa kwake juu (s.a.w) katika aina zote za ibada zinazokusanywa na dini yake na uchaji wake mkubwa zaidi kuliko yeyote awaye, na hofu yake kubwa kwa Allah (s.w) na juhudi zake zenye kuendelea na uchungaji wake wa hali ya juu kwa siri madhubuti za uja hata katika hali na mazingira magumu, na kutimiza kwake mtume (s.a.w) uja huo ulio takata pasi na kumuiga yeyote na kwa maana yake yote hali ya kuanza na kwa ukamilifu mkubwa wa sura hali ya kupwekesha kwa kuanzia na kukomea, hapana shaka haikuonekana na hatoonekana mithili yake.

Na vivyo hivyo anasifia katika (Jawshan al-Kabiir) ambayo ni mojawapo katika maelfu ya dua zake, na maongezi yake na Allah (s.w) anamsifu Mola wake kwa maarifa ya kiungu yaliyo matukufu, wajuzi na mawalii hawajafikia kiwango hicho cha maarifa wala daraja la wasifu huo tokea tangu pamoja na kukutana kwa fikara, katika yanayoonesha kuwa hana mithili yake katika dua, na kwa mwenye kutazama katika ufafanuzi wa muhtasari wa kifungu kimoja kati ya vifungu tisini na tisa vya Jawshan al-Kabiir – na hii ni mwanzoni mwa risala ya (Munaajah) hatoweza isipokuwa kusema kuwa hakuna mithili ya dua hii yenye kupendeza (Al-Jawshan) ambayo inawakilisha kilele cha maarifa ya kiungu.

Na kama hivyo hakika kudhihirisha kwake katika (kufikisha ujumbe) na katika kulingania kwake watu katika haki kiasi cha uimara uthabiti na ujasiri namna asiyoikaribia yeyote, haikumuingia – japo chembe – athari yoyote ya kusita wala kumvaa wasiwasi katu, na hofu haikumpata yeye hata kidogo, pamoja na kufanyiwa uadui na madola makubwa, na dini kuu – na hata watu wake na kabila na ami yake walimfanyia uadui mkubwa – akaichagiza peke yake dunia yote na Allah (s.w)  alimnusuru na kumpa ushindi akavika uongozi wa dunia kwa taji la Uislamu basi ni nani mfano wa Muhammad (s.a.w) katika kufikisha jumbe za Allah (s.w)?

Na vivyo hivyo kubeba kwake imani yenye nguvu iliyojikita na yakini ya kukinaisha iliyofurutu ada na kufunuliwa kwa maumbile yakiwa ni muujiza, na itikadi ya hali ya juu iliyojaza nuru ulimwengu, hazikuweza kuathiri kwake fikra zote na itikadi zote na hekima ya wenye hekima na elimu za wakuu wa kiruhani zilizoenea katika enzi hizo, japo kwa shubuha, au kusita au kwa udhaifu au kwa wasiwasi. Ndiyo, hazikuweza kuathiri si katika yakini yake wala katika itikadi yake wala katika kumtegemea kwake Allah, wala katika utulivu wake kwake, pamoja na kupinga kwake na kuhitilafiana nayo, na kukanusha juu yake. Ongeza juu ya hili kupata ilhamu ya wale wote waliokuwa juu katika mambo ya kimaanawy na ngazi za kiimani miongoni mwa watu wa uwalii na wema, na mbele yao ni masahaba watukufu, na kupokea kwao daima kutoka katika ngazi yake ya kiimani, na uoni wao kwake kwamba yeye yuko katika daraja na vyeo vya juu. Yote hayo yanaonesha – kwa uwazi – hakika ya imani yake mtume (s.a.w) haina mfano vilevile.

Mtalii akafahamu na akasadikisha akili yake kwamba ambaye mwenye sheria hii njema isiyokuwa na mfano, na Uislamu uliyonyooka sawa usiyo na mfano wake, na utumishi uliyo safi usiyo na kifani, na dua ya ajabu yenye kupendeza, na ulingano wa ulimwengu wa jumla, na imani ya miujiza, hatakuwa na uongo katu, na hatakuwa mwenye kuhadaa kamwe.

Dalili ya nne:

Ijimai ya Manabii (a.s) na kuafikiana kwao juu ya hakika za kiimani zenyewe, ni dalili yenye kukata juu ya uwepo wa Allah (s.w) na juu ya upekee wake, nao ni ushahidi wa kweli vilevile juu ya ukweli wa nabii huyu (s.a.w) na juu ya ujumbe wake, hiyo ni kwa sababu kila linalojuulisha juu ya ukweli wa unabii wa hao Manabii (a.s) na kila ambalo ni eneo la unabii wao katika sifa takatifu, na miujiza na majukumu waliyoyabeba yapo mfano wake na kwa ukamilifu zaidi kuliko hayo kwake mtume, kama hilo lilivyosadikishwa kihistoria. Basi hao manabii wameelezea kwa ulimi wa maneno – Yaani kwa Taurati, Injili na Zaburi na suhufi zilizokuwepo baina yao – kwa kuja kwa dhati hii yenye baraka na wakawabashiria watu kwa kuja kwake (s.a.w) (hata kwamba zaidi ya ishara ishirini za wazi kabisa katika ishara zenye kubashiria vitabu hivyo vitakatifu hakika imebainishwa kwa namna ya dhahiri na imethibitishwa katika risala ya Muujizat al-Ahmadiya).  

Kama ilivyo kwamba wamebashiri ujio wake (s.a.w), hivyo wao wanamsadiki (s.a.w) kwa ulimi wa hali yao – yaani kwa utume wao na miujiza yao – na wanatia muhuri kwa kuunga mkono juu ya ukweli wa malinganio yake kwani yeye ndiye mtangulizi aliye mkamilifu katika jukumu la utume na ulinganiaji kwa Allah (s.w). Mtalii akatambua kwamba kama wanavyojulisha – yaani hao manabii – kwa ulimi wa kauli na makubaliano juu ya upweke, basi hakika wao wanashuhudiwa – kwa ulimi wa hali na kwa kuafikiana juu ya hilo – juu ya ukweli wa nabii huyu (s.a.w).

Dalili ya tano:

Hakika maelfu ya mawalii kuifika haki na hakika na waliyo yapata miongoni mwa makamilifu na karama na mambo waliyofuzu katika mafunuo na ya kushuhudiwa sio vingine ila kwa kufuata mwongozo wa  kanuni za nabii huyu na kwa malezi yake na kumfuata yeye na kufuatilia nyayo zake, kama ambavyo wote wanajulisha juu ya upweke basi wao kwa makubaliano pamoja wanashuhudia na kwa kuafikiana juu ya ukweli wa nabii huyu mtukufu (s.a.w) – ustadhi wao na imamu wao – na juu ya kuwa ujumbe wake ni wa haki. Mtalii akaona kuwa kuona kwa hawa sehemu katika aliyoelezea nabii (s.a.w) katika ulimwengu wa ghaibu kwa nuru ya uwalii na itikadi yao kwake na kusadiki kwao yote aliyoyaeleza kwa nuru ya kumuamini yeye, – ima kwa elimu ya yakini, au kwa yakini yenyewe au kwa haki ya yakini – hakika inadhihirisha kama jua: Ukweli uliyoje wa kiongozi wao mkuu na haki iliyoje kwake.

Dalili ya sita:

Hakika mamilioni ya wanazuoni wachunguzi makini wateule na wahakiki wa kweli, na werevu wenye hekima waumini katika ambao waliofika daraja za juu kwa fadhili ya waliyoyasoma na kujifunza katika yale aliyokuja nayo mtume huyu mtukufu (s.a.w)  – pamoja na kuwa kwake ummiyyu – miongoni mwa hakika takatifu na yaliyochimbuka kwake katika elimu za juu na yaliyofunuka kwake katika maarifa ya kiungu, hakika ya wote hawa kama wanavyothibitisha upweke ambao ndio msingi wa ulinganiaji yake na kuisadiki wakiafikiana kwa hoja zao za kukata, basi wao wanaafikiana vilevile na wanashuhudia juu ya ukweli wa mwalimu huyu mkuu na kusibu kwa ustadhi huyu mkuu juu ya uhaki wa maneno yake (s.a.w) basi ushahidi wao huu ni hoja ya wazi kama mchana juu ya ukweli wake na kusibu kwa ujumbe wake. Na Risale-i Nur  na sehemu zake zote ambazo zinavuka mia moja mathalan si kingine isipokuwa ni hoja moja tu juu ya ukweli na kusibu kwa nabii huyu kipenzi.

Dalili ya saba:

Hakika kundi kubwa la ambao wanaoitwa (Jamaa na masahaba) ambao ni mashuhuri zaidi katika wanadamu baada ya manabii kwa firasa (Uwezo wa kujua jambo haraka kimoyo kwa kutazama mara ya kwanza tu) na wingi wa ujuzi na wenye makamilifu ya juu na bora wao kidaraja na wenye sauti zaidi na wenye kushikamana zaidi na dini na wakali zaidi kwa kuona, hakika ya kupekua kwa hawa na umakini wao kwa yote yaliyojificha na yaliyodhihiri  katika hali za nabii huyu (s.a.w), fikira zake na matendo yake kwa kutafiti kwa shauku kubwa na kwa upeo wa umakini na kwa ukomo wa bidii, kisha kusadiki kwao kwa kuafikiana na kukubaliana kwa umoja kwamba mtume (s.a.w) ni mkweli zaidi wa maneno kuliko wote waliomo duniani na mwenye hadhi ya juu, na mwenye kushikamana zaidi na haki na hakika, kusadiki kwao huku kusiko tetereka pamoja na imani ya kina sana waliyonayo hakika ni dalili ya wazi kama mwanga kujulisha jua.

Dalili ya nane:

Hakika ya ulimwengu huu kama unavyo julisha muundaji wake, mtia sura wake aliyeupatisha, anayeuendesha na kuuratibu na kufanya hali mbalimbali ndani yake kwa kutia sura kukadiria na kuendesha kana kwamba ni kasri imara au kama kitabu kikubwa au kama maonesho ya ajabu, au mahala pakubwa pa kutangaza, kadhalika unahitaji pasi na namna nyingine uwepo wa mwenye kuelezea maana yaliyomo katika kitabu hiki kikubwa, na ajue na kujulisha makusudio ya kiungu nyuma ya kuumba huu ulimwengu, na kujulisha hekima za kimola mlezi katika mabadiliko yake, na kufundisha matokeo ya michakato yake ya kimajukumu na kutangaza thamani ya hakika yake na makamilifu ya vilivyomo ndani yake. Yaani inahitajia mlinganiaji mkuu, na mnadi wa kweli na ustadhi mhakiki, na mwalimu fundi. Mtalii yule akatambua kwamba ulimwengu – kwa upande wa kulazimu huku –  unajulisha na kushuhudia juu ya ukweli wa nabii huyu na kusibu kwake (s.a.w) ambaye yeye ni mbora aliyetimiza majukumu haya, na kwamba yeye ni mbora na mkweli mno aliyeagizwa na Mola mlezi wa walimwengu wote.

Dalili ya tisa:

Maadamu huko nyuma ya pazia yupo atangazaye ukamilifu wa kuwa ni fundi muundaji vema, kwa vitengenezwa vyake hivi, mwenye kufanya vema na hekima, na anaitambulisha nafasi yake na anaipendezesha kwa viumbe vyake visivyokuwa na mpaka vyenye urembo na uzuri na kuwajibisha kushukuru na kuhimidi kwa neema zake zisizodhibitika kwa idadi vyenye ladha na tunu, na kuwatia shauku viumbe katika kuabudu kuelekea rububiya yake kwa uja wenye kusifika kwa mahaba na wema na shukurani mkabala na malezi haya, na kutunuku maisha kwa jumla kwenye huruma na himaya (hata kwamba anaandaa vyakula na dhifa za kimola mlezi zenye kutuliza maonjo ya vinywa makini mno na sampuli zote za hamu za kula), na kuwatiisha viumbe katika imani, kusalimu amri, kufuata. na utii kwa uungu wake ambao anaudhihirisha kwa kubadili misimu, na kuzungusha usiku na mchana na kutofautiana kwao viwili hivyo, na mfano wa hayo katika matendo makuu na shughuli tukufu, na utendaji wa kushangaza na uumbaji wa hekima, na kudhihirisha uadilifu wake na insafu yake kwa kuhami kwake daima wema na watu wema, na kuondosha kwake ubaya na watu wabaya, na kufuta kwake madhalimu na wakadhibishao na kuwaangamiza kwa mabalaa ya kimbinguni.

Hapana shaka kwamba kiumbe mpendwa kabisa mbele ya huyo aliyejificha kwa ghaibu, na mja mkweli mno kwake ni yule aliye kuwa ni mtendaji mwenye ikhlasi kwa makusudio yake yaliyotajwa hapo nyuma, na ambaye anafumbua siri kuu ya kuumbwa ulimwengu na kutegua fumbo lake, anayejitahidi daima kwa jina la Muumba wake na kutaka nguvu kwake na kumuomba msaada yeye peke yake katika kila kitu na anapata misaada na taufiki kutoka kwake (s.w). Na ni nani huyu awaye hivi asiyekuwa Muhammad mkuraishi (s.a.w).

Kisha mtalii aliisemesha akili yake: (kwa kuwa hizi hakika tisa ni zenye kushuhudia kwa ithibati juu ya ukweli wa nabii huyu mtukufu (s.a.w), hapana shaka kwa hiyo: Yeye ni mhimili wa utukufu wa wanadamu, na mahala pa kuzungukia kujifaharisha kwa ulimwengu, na kwamba anastahiki na yawiana kumwita ni usharifu wa wanadamu, na kumpa jina fahari ya walimwengu. Na kwamba alicho nacho mkononi katika amri ya Allah (s.w) Mwingi wa rehema, nayo ni Qur’an tukufu yenye kujumuisha utukufu wa mamlaka ya kimaanawy juu ya nusu ya ardhi pamoja na anayoyamiliki katika makamilifu ya haiba yake binafsi na tabia zake njema yanadhihirisha kuwa mtu mkuu kabisa katika uwepo wote ni huyu nabii mtukufu, kauli pambanuzi kwa hiyo kwa haki ya Muumba wetu (s.w) ni kauli yake (s.a.w). 

Ewe akili yangu njoo na uzingatie. Hakika ya msingi wa malinganio yake yote huyu nabii mtukufu (s.a.w) na upeo wa uhai wake wote hakika si lingine bali ni kushuhudia juu ya uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo, na kujulisha juu ya upweke wake, na kubainisha sifa zake tukufu, na kudhihirisha majina yake matukufu na kuthibitisha yote hayo, na kuyatangaza na kuyajulisha; kwa kuegemea yaliyomo kwenye dini yake miongoni mwa maelfu ya hakika zenye msingi imara, na nguvu ya yale aliyoyadhihirisha Allah (s.w) mkononi mwake miongoni mwa mamia ya miujiza yake ya wazi ya kukata ubishi kabisa.

Yaani hakika ya jua la kimaanawy ambalo linaangaza huu ulimwengu na hoja yenye nuru juu ya kuwepo kwa Muumba wetu (s.w) na upweke wake, hakika si mwingine bali ni huyu nabii mtukufu aliyepewa jina kuwa (kipenzi cha Allah (s.w)). Kuna aina tatu za ijmai (makubaliano ya pamoja) kuu hazihadai wala kuhadaika zina unga mkono ushahidi wake na kuusadikisha:

Ijmai ya kwanza:

Ni ya wale ambao wamekuwa mashuhuri na kujipambanua ulimwenguni kwa jina la: (Jamaa Wa Muhammad (s.a.w) kundi hilo la kinuru ambalo analitangulia imamu Ali (r.a) ambaye amesema: (Lau ingenyanyuliwa hijabu nisingezidi yakini) na nyuma yake wamemfuata maelfu ya mawalii wakubwa miongoni mwa wenye mitazamo mikali, na kuangalia ghaibu kwa usuhuba, mfano wa hao ni Sheikh Al-Kaylani (Siri yake itakaswe) ambaye alikuwa anaangalia kwa uoni wake mkali kwenye Arshi tukufu na Israfiil kwa utukufu wake na hali ya kuwa bado alikuwa angali ardhini.

Ijmaa yapili:

Ni ijmai ya kundi lijulikanalo kama Masahaba wema walio mashuhuri ulimwenguni (r.a.a) na kusadikisha kwao kwa kuafikiana na kwa imani madhubuti yenye nguvu kwa nabii huyu, hata hilo lika wapelekea katika kujitoa muhanga na fidia kwa roho zao na mali zao na baba zao na jamaa zao, nao ni ambao walikuwa watu mabedui wakiishi katika mazingira ya ujinga yasiyokuwa na hali za maisha ya kijamii na fikira za kisiasa, hawana mwongozo wala kitabu chenye nuru. Na walikuwa wamegubikwa katika giza la zama za al-Fatra (kukatika kwa mafundisho ya manabii), katika muda mfupi wakawa ni maustadhi waongozi na wanasiasa na watawala waadilifu kwa mataifa yaliyoendelea sana kwa ustaarabu na elimu na jamii na siasa, wakautawala ulimwengu mashariki na magharibi na bendera za uadilifu wao zikapepea bara na baharini.

Ijmai ya tatu:

Ni kusadikisha kwa kundi kubwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wasiohesabika wala kujulikana idadi waliobobea katika elimu zao na wahakiki wachunguzi waliokulia katika taifa lake na kushika njia tofauti, nao katika kila enzi wana maelfu ya wanaofuzu nafasi ya mbele – kwa umahiri wao – katika kila elimu. Basi wote hawa kumsadiki yeye kwa maafikiano na kwa daraja ya elimu ya yakini ni ijmai, ijmai iliyoje!

Mtalii akaamua kuwa ushahidi wa nabii huyu Ummiyyu (s.a.w), juu ya upweke si ushahidi wa mtu binafsi na uliyo mdogo, bali ni ushahidi wa jumla na wenye sifa ya wote, madhubuti hautetereki. Na mashetani wote hawataweza kuukabili katika upande wowote hata kama watakusanyika kwa hilo.

Na kama hivyo imeelezwa ishara ya muhtasari kwa yale aliyopokea mtalii yule ambaye alitembea kwa akili yake katika enzi za wema pande za maisha katika shule hiyo ya nuru katika ngazi ya kumi na sita ya kituo cha kwanza kama ifuatavyo:

[Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo, mmoja, wa pekee ambaye kupasa kuwepo kwake katika upweke wake kumejulishwa na: Fahari ya ulimwengu na sharafu ya sampuli ya wanadamu, kwa utukufu wa mamlaka ya Qur’an yake, na heshima na ukunjufu wa dini yake, na wingi wa makamilifu yake, na hadhi ya tabia zake, hata kwa kusadikisha maadui zake. Na kama hivyo ameshuhudia na kuthibitisha kwa nguvu ya mamia ya miujiza ya wazi yenye kusadikisha na kwa nguvu ya maelfu ya hakika za dini yake yenye kuangaza na kubainisha, kwa ijmai ya ali zake wenye nuru, na kwa kuafikiana Masahaba zake wenye maono ya mbali, na kwa kuafikiana kwa wahakiki wa umma wake wenye hoja  na busara zenye nuru].

Kishamtalii yule asiyepatwa na uchovu wala kushiba na ambaye amejua kwamba lengo la uhai katika dunia hii bali uhai wa uhai si mwingine bali ni imani, amejibizana mtalii huyu na moyo wake kwa kusema:

Hakika maneno ya huyo tunaye mtafuta ni maneno mashuhuri mno katika uwepo, ya kweli mno na yenye hekima zaidi, hakika yamewapa changa moto kila zama wale wasiyoyafuata, hiyo ni Qur’an tukufu yenye ufasaha wa miujiza basi na tukirejee kitabu hicho kitukufu na tufahamu kinasema nini, lakini ebu tusimame punde kidogo kabla ya kuingia kwetu kwenye ulimwengu huu mzuri, ili tutafute yale yatakayotufanya tuwe na yakini kwamba hicho ni kitabu cha Muumba wetu sisi, na kama hivi alianza kuchunguza na kutafiti.

Na kwa kuwa mtalii huyu ni katika watu wanaoishi zama hizihizi kwanza aliangalia kwenye Risale-i Nur ambazo ni minga’aro ya miujiza wa kimaanawy wa Qur’an tukufu, akaona kwamba hizi risala zinazofika mia na thelathini zenyewe ni tafsiri ya thamani ya aya za Qur’an kwani zinafunua nukta zake madhubuti na nuru zake zenye kumemetuka.

Na pamoja na kuwa Risale-i Nur imeeneza hakika za kiimani  kwa juhudi mfululizo katika anga zote katika zama hizi kaidi za kikafiri, hakuweza yeyote kuipinga wala kuikosoa, jambo linalo thibitisha kuwa Qur’an tukufu ambayo ndio kiongozi chake na chanzo chake na rejea yake na jua lake si vingine bali hiyo ni ya kimbinguni katika maneno ya bwana mlezi wa walimwengu wote, na wala siyo maneno ya wanadamu. Hata (Neno la ishirini na tano) na hitimisho la (Andiko la kumi na tisa) nazo ni hoja moja kati ya mamia ya hoja, inazozisimamisha Risale-i Nur ili kubainisha muujiza wa Qur’an, inauthibitisha kwa pande arobaini, uthibitisho uliomshangaza kila aliyeutazama, akauheshimu na kupendezwa nao – achilia mbali ya kuwa kwamba hawakuukosoa na hawakuupinga katu – bali waliusifia sana.

Hakika yule mtalii alihaulisha uthibitisho wa namna ya miujiza wa Qur’an tukufu kwamba ni maneno ya Allah (s.w) ya haki kwa Risale-i Nur, isipokuwa aliangalia kwa makini katika nukta chache zinazobainisha kwa ishara ya muhtasari utukufu wa Qur’an tukufu:

Nukta ya kwanza:

Kama ilivyokuwa Qur’an tukufu pamoja na miujiza yake yote na hakika zake zenye kujulisha juu ya kuwa ni ya haki ni muujiza wa Muhammad (s.a.w), hakika Muhammad (s.a.w) na miujiza yake yote na dalili za unabii wake na makamilifu yake ya kielimu ni muujiza vilevile wa Qur’an tukufu na ni hoja kali kwamba Qur’an tukufu ni maneno ya Allah Mola mlezi wa walimwengu.

Nukta ya pili:

Hakika Qur’an tukufu imebadilisha maisha ya kijamii mabadiliko makubwa imenawirisha anga ikazijaza kwa furaha na hakika, na imezua mapinduzi makubwa sawa katika nafsi za watu na nyoyo zao, au katika roho zao na akili zao, au katika maisha yao ya kibinafsi, kijamii na kisiasa, na ikadumisha mapinduzi haya na kuyaongoza kiasi kwamba aya zake zilizofikia elfu sita mia sita na sitini na sita

Elfu moja ni aya za amri, kama kauli yake (s.w) {وَأَقِيمُواْ الصَّلاَة} (2:43 ) na aya elfu moja za makatazo, kama kauli yake (s.w) { وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى } (Al-Israa :32) na aya elfu moja ni za ahadi kama kauli yake (s.w) { وَمَن يُطِعْ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا } (Al-Ahzab, 71) na elfu moja za makamio, kama kauli yake (s.w) { وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآؤُهُ جَهَنَّمُ } (An-Nisaa, 93) aya. Na elfu moja ni habari. Kama kauli yake (s.w): { وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـذَا الْبَلَدَ آمِنًا} (Ibarahim: 35) aya. Na visa elfu moja kama kisa cha Yusuf (a.s). pamoja na ndugu zake. Na aya mia sita ndani yake mna hukumu za halali na haramu. Na sitini na sita ni Nasikh na Mansukhu. [Kutoka katika tafsiri ya Abdau al-bayan lijamiii ayi al-Qur’an cha Sheikh Muhammad Badrul Diin Al-tolwy uk.3, Dar an-Nil, Izmir 1992. Na ameipokea Ibn Khuzaymah katika kitabu chake: (An-Nasikhu wal mansukhu)].

zinasomwa tangu karne kumi na nne, kila wakati kwa ndimi za zaidi ya watu mia moja milioni kwa uchache kwa utukuzo na heshima zote, inawalea watu na kutakasa nafsi zao na kusafisha nyoyo zao na kuzipa roho ufunuo na kupanda cheo, na akili hupewa msimamo wa sawa sawa na nuru, na uhai kupewa uhai na furaha. Hapana shaka kuwa hapana mwenza wa kitabu kama hiki wala hakuna kinachoshabihiana nacho wala mithili. Ni yenye kufurutu ada na ni muujiza.

Nukta ya tatu:

Qur’an tukufu imedhihirisha balagha ya hali ya juu iliyoje, tangu zama hizo hadi zama zetu hizi, hata imeshusha thamani ya (Muallaqati saba) zilizo mashuhuri nazo ni kasida za washairi wenye fasaha zaidi zilizoandikwa kwa dhahabu na kutundikwa juu ya kuta za Al-Kaaba hata binti wa (Labiid) aliiteremsha kasida ya baba yake kutoka kwenye ukuta wa Al-Kaaba, huku akisema: (Kwa kuwa zimeshakuja aya hivyo hakuna mahali pa mfano wako tena hapa).

Kadhalika fanani bedui aliposikia aya tukufu:

فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ Qur’an, 15: 94.

aliporomoka hali ya kusujudu, akaambiwa: Je umesilimu? akasema: Hapana bali nimesujudu kwa fasaha ya aya hii.

Na kadhalika hakika maelfu ya viongozi wa balagha na mabingwa wa fasihi mfano wa Abdulqadir Al-Jurjani na As-Sakkaki na Az-Zamakhshary wote wamekiri kwa pamoja na kuafikiana kwamba fasaha ya Qur’an ni juu ya uwezo wa wanadamu na haiyumkiniki kufikiwa.

Na vilevile, hakika Qur’an tukufu tangu kuteremka kwake – na haijaacha kuwa – inampa changa moto kila mwenye kughurika na mkaidi katika wanafasihi na wenye fasaha, na kuwashinda kutokana na ukaidi wao na kujikweza kwao, imewapa changa moto ya kuleta sura moja mfano wake au waridhie kuangamia na udhalili duniani na akhera.

Na wakati Qur’an inatangaza changamoto yake hii, tahamaki wanafasihi wakaidi wa zama hizo wameacha njia fupi nayo ni kuleta usawazisho na kupinga na kuleta sura katika mfano wake, hali ya kuwa wanapita njia ndefu, njia ya vita ambayo huleta balaa na kuteketeza roho na mali, jambo linalothibitisha uchaguzi wao huu kwamba haiwezekani kutembea katika njia hiyo fupi. Na kadhalika vipo mikononi mwa watu mamilioni ya vitabu vya Kiarabu ambavyo wameviandika watu wa Qur’an kwa shauku ya kuchota mtindo wake na kuiiga, au wameviandika  maadui wake kwa ajili ya kuipinga na kuikosoa, basi yote yaliyo na yatakayoandikwa pamoja na kuendelea na kuinukia katika mtindo utokanao na kukutana kwa fikira – tangu wakati huo na hata sasa – haiwezekani kuwa sawa au kuukaribia wowote kati ya hiyo mtindo wa Qur’an tukufu, hata kama mtu wa kawaida angesikiliza kinachosomwa katika Qur’an tukufu angelazimika kusema: Hakika ya hii Qur’an haifanani na chochote katika vitabu hivi na hataweza mwanadamu yeyote awaye si kafiri na wala mpumbavu kusema: Kwamba hiyo iko chini ya vyote, hivyo basi, inalazimu fasaha yake kuwa juu ya vyote. Hata mmojawao alisoma aya tukufu:

 سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ Qur’an, 57: 1.

kisha akasema: (Hakika mimi sioni upande wa muujiza ambao muuonao nyinyi katika fasihi ya aya hii tukufu) akaambiwa: (Rejea na fikira zako – kama mtalii huyu – katika zama hizo na ukaisikilize huko). Wakati akijifikiria kifikra kuwa yuko huko katika muda kabla ya kuteremka kwa Qur’an tukufu, tahamaki anaona kwamba viliyomo ulimwenguni vimetupwa katika anga tupu pana bila mipaka, katika dunia ya kutoweka na kuondoka, na hali vikiwa katika hali ya kukata tamaa, ya kubabaika inajigongagonga katika giza totoro, na vikiwa pasi na uhai wala hisia na pasi na kazi wala jukumu lolote. Lakini punde aliposikiliza aya hii tukufu tahamaki anaona aya hii imefunua pazia iliyokuwa imeshushwa mbele ya uso wa dunia na ulimwengu wote hadi ukawa huo uso ni wenye kuangaza, basi maneno haya ya azali na amri ya milele yakatoa somo kwa watu wote wenye hisia wateule kulingana na zama zote, na hali ya kuonesha kwamba huu ulimwengu ni sawa na msikiti mkubwa, na kwamba viumbe wote – na hasa mbingu na ardhi – vimezama katika dhikiri na tahalili na tasbihi inayotweta kwa uhai. Na wamenyanyua wote majukumu yao kwa shauku na furaha, wakiwa wanayatimiza kwa furaha na shukurani zote.

Kama hivi huyu mtalii alishuhudia utendaji kazi wa aya hii tukufu ulimwenguni akaonja kiasi cha ukuu wa fasaha yake. Akapimia kwa aya hiyo aya tukufu nyingine. Akatambua siri iliopo katika kutawala kwa fasaha ya Qur’an tukufu kwa pekee kwa nusu ya ardhi na humsu ya wanadamu wote, na akajua hekima moja katika maelfu ya hekima ya kudumu utukufu wa mamlaka ya Qur’an tukufu kwa heshima na taadhima zote kwa kitambo cha karne kumi na nne cha muda bila kukatika.

Nukta ya nne:

Hakika Qur’an tukufu imeonesha utamu na ladha wenye uhalisi na hakika kiasi kwamba kukariri kwingi – kunakosababisha kuchoka hata kutokana na vitu vizuri mno – hakuleti unyong’onyo kwa mtu ambaye moyo wake haujafisidika na kupumbaza uonjaji wake, bali kukariri kuisoma huzidisha utamu na ladha yake, na jambo hili ni lenye kukubaliwa na wote tangu zama hizo, mpaka ikawa ni jambo la kupigiwa mifano.

Vivyo hivyo Qur’an tukufu imedhihirisha katika kupendeza na uimara, kung’ara na umadhubuti kiasi inazihifadhi sifa hizo kana kwamba imeshuka hivi sasa. Pamoja na kupita muda wa karne kumi na nne. Na pamoja na wepesi wa kuipata kwa watu wote. Kila zama wameipokea ikiwa ni kijana mng’avu kana kwamba inaisemesha zama hiyo. Na kila kundi la kielimu pamoja na kuwa wanaikuta iko mikononi mwao na kuchota kutokana nayo kwa kila wakati na wanafuata nyayo za mtindo wa ufasaha wake, wanaiona daima ni yenye kuhifadhi ukweli uleule katika mtindo wake na uimara uleule katika kuchora fasaha yake.

Nukta ya tano:

Hakika Qur’an tukufu imefungua moja ya mbawa zake mbili upande wa muda uliopita na mwingine upande wa mustakabali, basi hakika ambayo manabii waliotangulia wameafikiana ni shina la Qur’an na moja ya mbawa zake mbili. Inawasadikisha na kuwaunga mkono na kwa upande wao wanaiunga mkono na kusadikisha kwa ulimi wa hali ya tawafuq.

Na kama hivyo mawalii wema na wanazuoni wateule wao ni matunda wamechukua maisha kutokana na mti wa Qur’an tukufu. Basi ukamilifu wao wa kiuhai ni dalili kuwa mti wao wenye baraka ni wenye uhai na tunuku na bubujiko la kudumu na hakika na kina. Ambao waliojiweka chini ya himaya ya ubawa wake wa pili na kuishi katika vivuli vyake miongoni mwa watu wa tarika za haki za uwalii na watu wa elimu zote za haki za Uislamu, wanashuhudia kwamba Qur’an ni haki yenyewe na mkusanyiko wa hakika, na hakuna mfano wake katika ujumuishi wake na mkusanyo wake, ni muujiza wa wazi.

Nukta ya sita:

Hakika pande sita za Qur’an tukufu, ni zenye kunawiri na kuangaza jambo ambalo linabainisha ukweli na uadilifu wake.

Naam, kutoka chini yake kuna nguzo za hoja na dalili, na juu yake kunang’ara muhuri wa muujiza, na mbele yake (lengo lake) kuna zawadi za furaha ya maisha ya makazi mawili, nyuma yake (yaani nukta yake ya kuegemea) kuna hakika za wahyi wa kimbinguni, na kuliani kwake kuna usadikishaji wa kiasi kisicho na mpaka miongoni mwa dalili za akili nyoofu, na kushotoni kwake kuna utulivu wa bidii na kuvutika halisi na kusalimu amri kikamilifu kwa nyoyo zilizosalimika na dhamira zilizo tohara.

wakati – hizo pande sita – zinathibitisha kuwa Qur’an ni ngome madhubuti ya kimbingu ardhini hawi na nguvu ya kuipasua mpasuaji yeyote wala hapenyi katika ukuta wake mpenyaji yeyote, pia kuna (vituo sita) zinasisitiza kuwa hiyo ni ukweli kwa dhati yake na haki kwa nafsi yake yenyewe na kwamba si maneno ya wanadamu katu, na kwamba batili haiji kutokea mbele yake wala nyuma yake.

Cha kwanza katika vituo hivyo, uungaji mkono wa msarifu wa ulimwengu huu na mwendeshaji wake, ambaye amejifanyia kudhihirisha zuri na kuuhami wema na ukweli na kufuta wahadaaji na kuwaondosha wazushi kuwa ni kawaida yenye kuendelea kwa utendaji wake (s.w). Basi kaunga mkono na kusadikisha (s.w), Qur’an hii kwa nafasi ya heshima aliyoitunuku na taadhima na kutawalisha cheo cha taufiki na kufuzu nayo ni yenye kukubaliwa zaidi na cheo cha juu zaidi na kitawalicho zaidi katika ulimwengu.

Na kadhalika hakika itikadi ya kina na heshima inayowiana kutoka katika dhati yenye baraka (s.a.w) upande wa Qur’an tukufu inazidi wote naye ni chemchem ya Uislamu na mkalimani wa Qur’an, na kuwa kwake kati ya hali yu macho na kulala wakati wahyi ukiwa unateremka hivyo inateremka kwake pasi na kutaka kwake, na kutofikia maneno yake mengine kilele cha hiyo Qur’an bali kutoshabihiana nayo pamoja na kuwa yeye ni mfasaha zaidi kuliko watu wote, na kubainisha kwake – kwa hii Qur’an – ubainishaji wa kighaibu kwa yaliyopita miongoni mwa matukio ya kiulimwengu yenye kutokea, na yatakayokuja kati ya hayo pamoja na kuwa yeye ni ummiyyu (si msomaji wa maandishi) bila ya kusita sita na kwa utulivu wote, na kutokuonekana hila yoyote au kosa au yaliyo mfano wa hayo japo kidogo pamoja na kuwa yeye alikuwa katikati ya watu wanaomchunguza sana matendo yake, basi imani ya huyu mkalimani mwema na mfikishaji mkuu (s.a.w) na kusadiki kwake kwa nguvu zake zote kwa kila hukumu miongoni mwa hukumu za Qur’an tukufu na kutomteteresha chochote kwa vyovyote iwavyo kwa ukubwa inaunga mkono na kutilia mkazo kuwa Qur’an ni ya ki mbingu na yote ni ukweli na uadilifu na maneno ya baraka ya Bwana mlezi wa walimwengu.

Na vilevile kufungamana kwa humsu ya wanadamu bali sehemu kubwa yao na Qur’an tukufu inayoonekana mbele yao mafungamano ya kuvutika na kushika dini, na kuisikiliza kwao kwa bidii na shauku na hamu na kuja jumbe za majini na malaika na maruhani kwake na kumzunguka wakati wa kuisoma mfano wa mzunguko wa vipepeo kwenye nuru kwa ushahidi wa alama na matukio na mafunuo mengi ya kweli. Yote hayo ni kusadikisha kuwa hii Qur’an na kitu cha kuridhiwa na kupendwa na ulimwengu na kwamba Qur’an ina nafasi ya juu humo (ulimwenguni).

Vilevile kuchukua kila tabaka katika matabaka ya wanadamu – kuanzia kwa mpumbavu mwenye upumbavu mkali na mtu wa kawaida hadi kwa mwerevu mkali wa werevu na mwanazuoni – fungu lake kamili katika masomo ambayo Qur’an tukufu inayatoa, na kufahamu kwao kutokana nayo hakika za kina sana, na kuzalisha kwa makundi yote ya wanazuoni wa mamia ya elimu na fani za Kiislamu na hasa mujitahidina wa sharia pole na wahakiki wa Usulu Ad-diin na mabingwa wa elimu yaAl-Kalaam na mfano wa hao, na kutoa kwao majibu ya kutosheleza kwa yale wanayo yahitajia katika masuala yanayohusu elimu zao kutoka katika Qur’an tukufu, hakika sio lingine bali ni kusadikisha kuwa Qur’an tukufu ni chimbuko na chanzo cha haki.

Na vilevile kutopinga kwa wanafasihi Waarabu ambao wako mbele katika fasihi hasa wale ambao hawakuingia katika Uislamu – pamoja na kutaka sana kupinga – na kushindwa kwao kabisa mbele ya upande mmoja – nao ni upande wa kibalagha – kati ya pande saba kuu za muujiza wa Qur’an, na kushindwa kwao kuleta sura moja tu, katika sura za Qur’an tukufu na kuzuilika kwao na hilo, na kutokuipinga katika waliokuja miongoni wa wanafasihi mashuhuri na mabingwa wa wanazuoni hadi sasa upande wowote katika pande za muujiza – pamoja na kutaka kwao kutangazika sauti yao kwa upingaji – na kunyamaza kwao huku wakiwa wameshindwa hilo, ni hoja kali kwamba Qur’an tukufu ni muujiza na iko juu ya uwezo wa wanadamu.

Naam, hakika thamani ya maneno na kuwa kwake juu hujiweka wazi katika kubainisha: (Nani aliyeyasema? na nani amemwambia? na kwa nini ameyasema?).

Na kwa msingi huu, hakika Qur’an tukufu haikuja – na haitakuja – mfano wake na wala hakitaikaribia kitu chochote  katu – hiyo ni kwa sababu Qur’an tukufu si kitu kingine bali ni mazungumzo, kutoka kwa Bwana mlezi wa limwengu zote na ni maneno kutoka kwa Muumba wake nayo ni mazungumzo haiyumkiniki kuyaiga, – kwa upande wowote uwao – na hakuna ndani yake alama inayoashiria kwa kujifanyisha. Kisha msemeshwa ni mwenye kuletwa kwa jina la wanadamu wote. bali kwa jina la viumbe wote, naye ni mbora ya aliyekuwa msemeshwa na mwenye utajo wa juu zaidi kuliko wote, naye ndiye ambaye Uislamu mtukufu umemteua kutokana na nguvu ya imani yake, hata akapazwa mpaka mkabala wa pinde mbili au karibu zaidi akashuka huku amevikwa taji la mazungumzo ya kiungu mkusudiwa kwa haja zote.

Kisha Qur’an tukufu ambayo ni yenye ufasaha wa kimuujiza imeelezea njia ya furaha ya makazi mawili, na kuweka malengo ya kuumbwa kwa ulimwengu na yaliyomo miongoni mwa makusudio ya kiungu hali ya kuweka wazi yale ambayo msemeshwa huyu mtukufu anayabeba katika imani ya hali ya juu kunjufu ambayo inakusanya hakika za Kiislamu zote kwa kuhudhurisha kila upande katika pande za huu ulimwengu mkubwa mno na kuupindua kama anayepindua ramani au saa iliyopo mbele yake. Hali ya kumjulisha mwanadamu mtengenezaji wake Muumba (s.w) Kupitia hatua za ulimwengu na mabadiliko yake, basi hapana shaka na hapana budi kwamba haiyumkiniki kuleta mfano wa Qur’an kamwe, haiwezekani kabisa kufikiwa kiwango cha muujiza wake.

Na vilevile maelfu ya wanazuoni mabingwa ambao kila mmoja aliandika tafsiri ya Qur’an tukufu katika mijalladati baadhi yake imefikia mijalladati thelathini au arubaini bali hata mijalladati sabini, na kubainisha kwa isinadi zao na dalili zao katika yaliyomo kwenye Qur’an tukufu katika sifa za kipekee za hali ya juu kiasi kisichokuwa na mpaka na nukta zenye balagha na sifa mahususi makini na siri zilizojificha na maana ya juu na utoaji habari wa ghaibu nyingi kwa aina zake mbalimbali, na wote hawa kudhihirisha sifa hizo za kipekee na kuzithibitisha ni dalili ya wazi kwamba Qur’an tukufu ni muujiza wa kiungu wenye kufurutu ada na hasa kuthibitisha kila kitabu katika vitabu vya Risale-i Nur vipatavyo vitabu mia moja na thelathini sifa pekee katika sifa za Qur’an tukufu na nukta katika nukta zake za ajabu kwa uthibitisho wa wazi kwa hoja zenye nguvu, na hasa Risala ya (Miujiza ya Qur’an) na (Kituo cha pili katika neno la ishirini) ambayo inatoa mengi katika maajabu ya ustaarabu kutoka katika Qur’an tukufu mifano ya gari moshi na ndege. Na (Mwale wa kwanza) unaoitwa (Al-Ishaarati al-Qur’aniyyah) ambao unabainisha ishara za aya katika Risale-i Nur na katika umeme, na risala ndogo nane ziitwazo (Ar-Rumuzu al-Thamaniyah) ambazo zinazobainisha kiasi cha kupangika kuliko makini kwa herufi za Qur’an tukufu na kiasi gani zilivyo na siri na maana tele, na risala ndogo ambayo inabainisha mwishoni mwa sura Alfat’hi na inathibitisha muujiza wake kwa namna tano kwa upande wa kutoa habari ya kighaibu, na mifano yake katika risala mbali mbali. Hakika kuonesha kila sehemu katika sehemu za Risale-i Nur hakika moja wapo katika hakika za Qur’an tukufu na nuru katika nuru zake yote hayo ni kusadikisha na kutilia mkazo kwamba Qur’an tukufu haina mithili yake, na kwamba ni muujiza na kifurutu ada na kwamba ni lugha ya ghaibu katika ulimwengu huu wa kushuhudiwa na kwamba ni maneno ya mjuzi wa mambo yote ya ghaibu.

Na kama hivyo kwa ajili ya sifa hizi za pekee na mahsusi za Qur’an tukufu ambazo zimeashiriwa katika nukta sita na katika pande sita, na katika vituo sita, umedumu utawala wake wa kinuru mtukufu na mamlaka yake matakatifu yenye kuadhimishwa, kwa ukamilifu wa matukuzo na heshima huku  ikiangazia nyuso za zama na kutia nuru nyuso za ardhi pia,  muda wote wa miaka elfu moja na mia tatu. Na kwa ajili ya sifa hizo mahususi pia Qur’an tukufu imepata sifa pambanuzi takatifu kiasi kila herufi katika herufi zake kuna thawabu kumi na mema kumi kwa uchache, na matunda kumi ya kudumu, bali kila herufi katika herufi za fungu la aya na sura hutoa matunda mia na elfu au zaidi katika matunda ya Akhera, inapanda juu nuru ya kila herufi na thawabu zake katika nyakati za baraka kutokea kumi hadi mamia na mfano wa hivyo katika sifa za pekee takatifu amezifahamu mtalii wa ulimwengu akausemesha moyo wake kwa kusema:

Kweli, hakika hii Qur’an tukufu ambayo ni muujiza kwa kila upande katika pande zake imeshuhudia kwa makubaliano ya sura zake na kuafikiana kwa ya zake na tawafuq za siri zake na nuru zake na kuambatana kwa matunda na athari zake, ushahidi thabiti kwa dalili juu ya uwepo wa aliye wajibu kuwepo, na juu ya upweke wake (s.w), na juu ya sifa zake tukufu, na juu ya majina yake mazuri hata zikateulika shahidi zisizo na mpaka za watu wote wa imani kutokana na ushahidi huo.

Na kama hivi imeelezwa katika ngazi ya kumi na saba ya kituo cha kwanza ishara fupi kwa aliyoyapokea mtalii katika somo la Tawhidi na imani kutoka katika Qur’an tukufu.

[Hapana Mola ila Allah (s.w), ambaye ni wajibu kuwepo  mmoja wa pekee ambaye imejulisha juu ya wajibu wa uwepo wake katika upweke wake Qur’an yenye ufasaha wa muujiza, yenye kukubalika yenye kutakiwa kwa jinsi za malaika, watu na majini, isomwayo aya zake zote kila dakika kwa heshima kamili kwa ndimi za mamia ya mamilioni ya sampuli ya mwanadamu, yenye kudumu utawala wake mtakatifu katika maeneo ya ardhi na vyenye kuwepo, na katika nyuso za enzi na zama mbali mbali, na yenye kuenea utawala wake wa kimaanawy wa kinuru juu ya nusu ya ardhi na humsu ya wanadamu katika karne kumi na nne katika heshima kamili, Na pia imeshuhudia na kuthibitisha kwa ijmai ya sura zake takatifu za ki mbinguni, na kuafikiana kwa aya zake zenye nuru za kiungu, na tawafuq ya siri zake na nuru zake na kuambatana kwa hakika zake na matunda yake na athari zake kwa kushuhudia na kuona kwa macho].

Kisha yule mtalii na msafiri aliyetajwa amekwishajua kwa yakini kwamba imani ambayo ameifikia ni rasilimali kuu kabisa ya mwanadamu; kwa sababu haimpi – naye ni fakiri – shamba lenye kutoweka na makazi ya muda, bali inampa umiliki wa ulimwengu mkubwa na kumfanya astahiki kupata ufalme mpana wa kubakia milele mpana kuliko dunia, na inampatia – naye ni mwanadamu mwenye kutoweka – mahitaji ya uhai wa kudumu milele, hivyo inamuokoa – naye ni masikini anayengojea kinyongo cha muda maalum – kutokana na mwisho wa kutisha, na kutolewa katika uwepo milele, hali ya kumfungulia hazina za furaha za milele, kwa hiyo mtalii aliiambia nafsi kwa kusema: Haya tangulia tupate kufuzu daraja lingine katika madaraja ya imani ambayo hayadhibitiwi na mpaka wowote, na tuchungulie mkusanyiko wa ulimwengu na tuusikilize tuone unasema nini tena ili tuongeze nuru juu ya masomo yale ambayo tumeyapata kutokana na nguzo za ulimwengu na sehemu zake. 

Yule mtalii aliangalia mkusanyiko wa ulimwengu kwa darubini pana yenye kuzungukia sehemu zote ambayo ameiazima kutoka katika Qur’an tukufu, akaona kwamba ulimwengu huu umepangiliwa mpangilio wa ajabu, na wenye kuhifadhi maana chungu tele, kiasi kwamba unadhihiri katika sura ya kitabu cha kiungu kulichotakasika chenye mwili, au Qur’an ya kiungu Bwana mlezi ya kimwili, au kasri ya kiungu iliyopambwa ya Mola mkusudiwa kwa haja zote, au ni mji ulipangika wa kiungu mwingi wa rehema, kwa sababu sura zote za kitabu hicho, aya zake, maneno yake, bali herufi zake  milango yake, fasili zake, kurasa zake na misitari yake, na yanayopita kwa wote ikiwemo (Kufuta na kuthibitisha) kwenye maana pole, na kuhaulisha na kugeuza kwenye hekima na kustaajabisha, yote hayo kwa makubaliano ya pamoja yanamaanisha kwa uwazi uwepo wa mjuzi wa kila kitu, Mweza wa kila kitu, na yanaelezea uwepo wa Muumba mwenye utukufu na mtia sura mwenye ukamilifu anaona kila kitu katika kila kitu, na anajua uhusiano wa kila kitu na kila kitu, hivyo anakichunga.

Na kama hivyo, hakika yote yaliyomo ulimwenguni pamoja na nguzo zake zote na sampuli zake zote na sehemu zake zote na wakazi wake wote na jumuisho zake zote na maduhuli yake yote na usarifu wake wote na mabadilisho yake yote yenye masilahi na ufanyaji upya wenye hekima, yanamaanisha na kufahamisha kwa maafikiano uwepo wa upweke wa Muumba mwenye daraja za juu na fundi hakuna kama mfano wake chochote, anafanya kwa uweza usio na mpaka na kwa hekima isiyo na ukomo.

Ushahidi wa huu ulimwengu mkubwa juu ya uwepo wa Muumba na upweke wake unathibitishwa na hakika mbili kuu zenye kunasibiana pamoja na wasaa wa ulimwengu na ukubwa wake nazo ni:

Hakika ya kwanza:

Nayo ni (Hakika ya kuzuka na uyumkini) ambayo wenye hekima wa Kiislamu na maulamaa mahodari wa Usuli Ad-diin na Elimu ya al-Kalaam wameiona na kuithibitisha  kwa hoja yenye nguvu. Wamesema: (kwa kuwa ulimwenguni na katika kila kitu, kuna kugeuka na kubadilika, basi huo (ulimwengu) ni wenye kutoweka na kuzuka na hauwi wa tangu, na kwa kuwa ni wenye kuzuka hapana budi kuwepo kwa mtengenezaji wake mwenye kuuzusha na kwa kuwa kila kitu kipo sawasawa, endapo haikuwa katika dhati yake sababu ya uwepo na kukosekana hakitokuwa ni wajibu wala cha azali) na vilevile imethibitishwa kwa hoja zenye nguvu kwamba haiyumkiniki kupatisha vitu baadhi kwa baadhi nyengine kwa zamu na kwa mfuatano (sawa na mnyororo wa matukio) ambao ni batili na muhali. Kwa hiyo inalazimu  kuwepo aliye wajibu kuwepo na inazuilika (haiwezekani kuwepo) mwenza wake, na ni muhali kuwepo mithili yake, na kila asiyekuwa yeye ni yamkini na kila asiyekuwa yeye ni mwenye kuumbwa.

Naam, kwa yakini (Hakika ya kuzuka) imetawala ulimwenguni, jicho linaona wingi wake, na akili inaona sehemu nyingine katika hiyo; hii ni kwa kuwa sisi tunashuhudia kwamba kwa kuingia kwa majira ya mapukutiko kila mwaka hufa ulimwengu mkubwa sana, hufa visivyo na idadi aina mia moja elfu ya mimea na wanyama wadogo, kila aina katika hiyo ni sawa na ulimwengu wenye uhai. Lakini umauti huo unatokea katika upeo wa mpangilio, kiasi kwamba vitu hivyo huacha mbegu zake, kokwa zake na mayai yake – ambavyo vinakuwa ndio mahali pa kuzunguka kwa kufufuliwa na kukusanywa kwake, na ambayo yenyewe ni miujiza ya rehema na hekima na maajabu ya uweza na ujuzi – huziweka hali ya kuwa ni amana katika ya hekima ya mhifadhi wa kila kitu mwenye utukufu, na chini ya uangalizi wake na himaya yake, ikisalimisha mikononi mwake nyaraka za amali zake, na programu za majukumu waliyoyatanguliza, na baada ya hapo hufa. Na kwa kuingia msimu wa machipuo, hufufuliwa kwa dhati zake, vile ambavyo vilifishwa miongoni mwa miti, mashina na wanyama wadogo. Na huhuishwa na kumbwa mifano na mashabihiano ya sehemu nyingine kutokana nayo katika mahali pake. Na kwa hiyo hutoa mifano ya mia moja elfu na vielelezo vya ufufuo mkuu na dalili mia moja elfu. Basi viumbe vilivyomo katika msimu wa machipuo uliyopita, kwa kufungua kwake kurasa za amali iliyoyafanya na kutangaza kwake kurasa hizo katika machipuo haya,  huonesha kwa uwazi mfano wa aya tukufu:

 وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ Qur’an, 81: 10.

Na kama hivyo kwa upande wa ulimwengu kama kitu chote, basi katika kila mapukutiko na katika kila machipuo hufa ulimwengu mkubwa, na kuja ulimwenguni ulimwengu mpya, na vifo vilivyomo na vizazi na aina zisiodhibitika miongoni mwa vilivyo hai hufanyika katika upeo wa mpangilio na mizani, hadi kana kwamba dunia ni kituo na mafikio, hukaribishwa hapo viumbe hai, huja katika dunia limwengu zenye kutalii na dunia zenye kutembea hutimiza humo majukumu yake kisha huondoka hapo na kuiacha dunia.

Na kama hivyo, hakika kuzusha limwengu zenye uhai, na kupatisha viumbe vyenye majukumu hapa duniani, kuzusha na kupatisha kwa elimu yote na hekima, na mizani na kuendana mizani, kupangika na nidhamu, na kuitumia kwa uweza, na kuitumia kwa rehema katika makusudi ya kiungu, na katika malengo ya kiungu, na katika huduma za mwingi wa rehema, inajulisha kwa uwazi juu ya kupasa kuwepo kwa dhati takatifu tukufu haina mpaka kwa uweza wake na haina ukomo wa hekima yake na kuidhihirisha kwa ajili ya akili hali ya kuwa wazi kama jua.

Tunafunga mlango wa (Masuala ya kuzuka) na tunauhaulisha kwenye Risale-i Nur na vitabu vya wanazuoni wa Al-kalaam

Ama upande wa (yamkini) nao pia umetawalia ulimwengu na kuuzunguka, kwani tunashuhudia kila kitu sawa kiwe kizima au ni sehemu, kikubwa au kidogo, na kila kilichopo – kutokea katika Arshi hadi katika tandiko na kutoka katika chembe za atomu hadi katika sayari – hakika hutumwa duniani kwa udhati maalum na kwa sura maalum na kwa haiba yenye kupambanuka na kwa sifa mahsusi na kwa namna zenye hekima na kwa zana zenye masilahi na faida, na hali ya kuwa kutoa hali hiyo mahsusi kwa dhati hiyo mahsusi na kwa hakika hiyo kati ya yamkini zisizo na mipaka, na kadhalika kuivika sura hiyo maalum yenye nakshi na alama zenye kutenganisha na zenye kuwiana kati ya yamkini na matazamio mengi kwa idadi ya sura zenyewe, na kadhalika kuhusisha haiba hiyo yenye kuwiana kwa uchaguzi wa kipekee kwa hicho kilichopo chenye kubabaika kati ya yamkini nyingi kwa kiasi cha watu wa jinsi yake, na kadhalika kuwezesha sifa maalum zenye kuwiana zenye masilahi katika hicho kilichotengenezwa ambacho hakina umbo na chenye kusitasita ndani ya yamkini na matazamio mbalimbali kwa idadi ya aina za sifa na ngazi zake, na vilevile kuandaa kiumbe yule kwa namna zile zenye hekima na kumpachika zana hizo zenye uangalizi ambazo inayumkinika kuwa katika njia mbalimbali na aina zisizo na mpaka, na yeye ni mwenye kutahayari aendaye pasi na na lengo ndani ya yasiyo na mpaka kati ya yanayo yumkinika na matazamio, hakika ishara na dalili na ushahidi wote huu unaotokana na hakika ya (kuyumkinika) zinaunda bila shaka moja wapo ya mbawa mbili za ushahidi huu mkubwa wa ulimwengu; kwa sababu huo ulimwengu kwa idadi ya vyote vilivyo yumkinika vya ujumla na sehemu, na kwa idadi ya kuwezekana kwa kila yamkini – katika vilivyoelezwa – miongoni mwa hakika na sifa, na vilivyo navyo katika umbo na sura, na sifa na hali inayovipambanua, kuna ishara na dalili na ushahidi juu ya uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo sw, na ambaye anahusisha na kuchagua na kuainisha na kuzusha, na hakuna mpaka wa uweza wake wala hakuna ukomo wa hekima yake wala hakifichikani kwake chochote wala lolote wala hakimshindi chochote wala hakimpotei chochote, basi kitu kikubwa kwake ni chepesi kama kidogo, naye ni mweza wa kupatisha majira ya machipuo kwa wepesi wa kupatisha mti na kupatisha mti kwa wepesi wa kupatisha mbegu.

Na kwa kuwa sehemu za Risale-i Nur – na hasa neno la ishirini na mbili na thelathini na mbili na andiko la ishirini na la thelathini na tatu – yamethibitisha kikamilifu na yameweka wazi kitimilifu ushahidi wa ulimwengu kwa mbawa zake zote mbili na kwa hakika zake zote mbili, kwa hiyo tunahitimisha swala hili refu sana kwa kulihaulisha katika risala hizo.

Ama ubawa wa pili wa ushahidi mkubwa wa jumla unaotoka katika mjumuisho wa ulimwengu ni:

Hakika ya pili: Hakika ya (kusaidiana)

Kwa hakika, hakika ya kusaidiana inaonekana katika vilivyomo nje ya uwezo wa viumbe vinavyojikusuru katika kuhifadhi uwepo wake na majukumu yake na kulinda uhai wake – ikiwa ni vyenye uhai – na kutekeleza wadhifa wake ndani ya mageuzi haya yenye kubabaika ya kudumu na mabadiliko yenye kugongana ya kudumu. Mathalani: Hakika kujikusuru kwa vijiasili kwa ajili ya kusaidia vyenye uhai, na hasa mawingu kuipa mimea, na kwa upande wake mimea kusaidia wanyama, na wanyama kumsaidia mwanadamu na maziwa mazuri yaliyomo kwenye chuchu na yenye kububujika ili kulisha watoto wadogo, na kusalimisha haja ya vilivyo hai na riziki zake nyingi sana na zilizo nje ya uwezo wake mikononi mwake kwa namna isivyotegemea, na kupita kwa chembe ndogo za vyakula ili kujenga seli za mwili na mfano wa hayo katika mifano mingi ya hakika ya kusaidiana inayokwenda kwa utiishaji wa kiungu Bwana Mlezi na uhudumishaji wa kiungu Mwingi wa rehema, hudhihirisha kwa uwazi hali ya Ulezi wa Bwana Mlezi wa walimwengu wa jumla wenye kuzunguka, na hali ya wingi wa rehema iliyo pana yenye kukusanya na ambayo inaendesha ulimwengu wote mpana kwa wepesi sawa na kuendesha kasri ndogo.

Naam, hakika kudhihirisha vitu vyenye kusaidiana – navyo vikiwa vigumu visivyo na hisia wala huruma – hali zenye kuonesha huruma na hisia kati yake ni dalili na dalili iliyoje juu ya kwamba hivyo vina sukumwa msukumo wa kutoa msaada na kusaidia na kupita kwa nguvu ya mwenye utukufu na kwa rehema ya Mwingi wa rehema ya moja kwa moja na kwa amri ya Mwingi wa hekima.

Na kama hivi, hakika ya (kusaidiana) kwa ujumla kunakutokea kwenye ulimwengu na (Kuwiana kwa vipimo) kwa ujumla kunakotokea kwa ukamilifu wa mpangilio, na (kuhifadhiana) kwa jumla, kuanzia katika maumbo makubwa ya mbinguni na sayari hadi katika zana za kiumbe hai na viungo vyake nyeti bali hadi katika chembe ndogo za mwili wake, na (kupamba) ambako kalamu yake inapita kutokea katika uso wa mbingu zenye kumeremeta hadi kwenye ardhi yenye kupendeza, bali hadi katika sura za maua mazuri, (na mpangilio) unaotawala kuanzia njia ya Darb At-tabana (Aina ya njia ya angani ya mkusanyiko wa nyota kubwa nyingi mno) hadi katika mfumo wa jua na katika matunda ya mahindi, koma manga na mfano wake, na (kupanga majukumu) kunakotokea kuanzia kwenye jua na mwezi na viasili na mawingu hadi kwenye nyuki na nyenyere na mfano wake katika hakika kubwa sana na zenye kushuhudia ushahidi wenye kunasibiana pamoja na ukubwa wake, kunaunda ubawa wa pili wa ushahidi wa ulimwengu juu ya uwepo wa wake (s.w) na upweke wake na zinathibitisha hilo.

Kwa kuwa Risale-i Nur imethibitisha ushahidi huu mkubwa na kuubainisha hivyo tunatosheka kwa ishara hii fupi sana.

Na kama hivi imeelezwa katika ngazi ya kumi na nane katika kituo cha kwanza ishara fupi kwa yale aliyoyapata mtalii wa dunia katika somo la imani kutoka katika ulimwengu:

[Hapana mla apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w) Ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye haiwezekani kuwapo mwenza wake, na kila kisichokuwa yeye ni yumkini, ni mmoja wa pekee ambaye kimejulisha juu ya kupasa uwepo wake katika upweke wake kitabu kikubwa kilichoundika umbo, na Qur’an ya kimwili yenye kuadhimishwa, na kasri lenye kupambwa lenye kupangika, na mji ulioheshimika uliopangika kwa makubaliano ya pamoja ya sura zake, aya zake, maneno yake, herufi zake, na milango yake, fasili zake, kurasa zake na misitari yake, na kuafikiana kwa nguzo zake, aina zake, sehemu zake na vijisehemu vyake na wakazi wake na makusanyo yake na maduhuli yake na usarifu wake kwa ushahidi wa utukufu wa kuzungukia kwa hakika ya kuzuka na kugeuka na kuyumkinika, kwa makubaliano ya pamoja ya wanazuoni wa elimu ya Al-Kalaam wote, na kwa ushahidi wa hakika ya kubadilisha sura yake na yaliyoyakusanya kwa hekima na kwa mpangilio, na kufanya upya herufi zake na maneno yake kwa mpangilio na uzani.

Na kwa ushahidi wa utukufu wa kuzungukia hakika ya: kusaidiana, kupokeana, kusaidiana, kuingiliana, na kuendana sawa mizani, na kuhifadhiana, katika viumbe vyake vilivyomo kwa kushuhudia na kuona waziwazi].

Kisha mtalii ambaye amekuja duniani na kumtafuta Muumba wake na kupanda katika ngazi kumi na nane na kufika kiti cha enzi cha hakika kwa miraji ya kiimani, alipanda kutoka katika kituo cha maarifa ya kighaibu na kwenda katika kituo cha mahudhurio na mazungumzo. Huyu mtakaji mno mwenye shauku akaongea na roho yake kwa kusema:

Hakika himidi na sifa zote za kighaibu tangu mwanzoni mwa surat Al-Fatiha hadi katika neno (wewe tu) yanaleta utulivu humpaza mwanadamu na kumuinua hadi katika ngazi ya maongezi kwa (wewe tu), kwa hiyo basi ni juu yetu kumuuliza yule tunayemtafuta kutokana na yeye moja kwa moja na tuache kumtafuta kighaibu, kwani yapasa kuuliza juu ya jua – ambalo linaangaza kila kitu – kutokana na jua lenyewe kwa sababu ambaye anadhihirisha kila kitu na kukiweka wazi hapana shaka kwamba anadhihirisha zaidi nafsi yake kuliko vitu vyote, kwa hiyo kama inavyoyumkinika kwetu kuliona jua na kulitambua kutokana na mionzi yake na mwanga wake, inayumkinika kwetu pia kujitahidi – kulingana na ukubalifu wetu – katika kumtambua (s.w) kutokana na madhihirisho ya majina yake mazuri na kutokana na nuru za sifa zake tukufu.

Na katika Risala hii tutabainisha kwa ujumla na muhtasari hakika mbili tu kati ya hakika nyingi na pambanuzi kunjufu za ngazi mbili katika ngazi zisizokuwa na mpaka za njia mbili kati ya njia nyingi za makusudi haya:

Hakika ya kwanza:

Hakika ya kiutendaji yenye kutawala, hali hiyo ya kiutendaji yenye kutamalaki ulimwengu na yenye kushuhudiwa mbele ya macho yetu, na ambayo inaendesha, inabadilisha, na kuweka upya vyote vilivyomo ambavyo vinazunguka na vya kudumu, vyenye kupangika na vikubwa sana na vya mbinguni na ardhini, na ambayo inapelekea katika kuhisi hakika ya kudhihiri kwa hali ya kiulezi ya Bwana mlezi wa kila kitu kwa uwazi ndani ya hakika ya huo utendaji wenye hekima kwa pande zake zote, na hisia hii inapelekea kutambua kudhihiri uungu kwa kiudharura ndani ya kudhihiri kwa hali ya ulezi wa Bwana mlezi yenye kuangaza kwa rehema kwa pande zake zote.

Yaani yanahisiwa – kama vile yanaonekana – matendo ya mtendaji mweza mjuzi wa kila kitu, kutokana na hali hii ya kiutendaji wenye hekima wenye kutamalaki wa kudumu na kutokea nyuma ya pazia yake. Na hujulikana kwa uwazi – kwa daraja ya kuhisi – majina ya mwenyezi mungu mazuri yenye kudhihiri katika kila kitu, kutokana na matendo haya ya kiungu yenye uendeshaji, malezi, na kutokana na nyuma ya pazia yake, na inajulikana kwa ujuzi wa yakini, bali kwa yakini ya kuona, bali kwa haki ya yakini, uwepo wa sifa saba takatifu na kuthibiti kwake kutokana na majina haya mazuri yenye kudhihiri kwa utukufu na uzuri na kutokea nyuma ya pazia. Na inajulikana vilevile kwa elimu isiyo na shaka na kwa wazi na dharura na kwa elimu ya yakini na kwa ushahidi wa vyote vilivyotengenezwa, katika madhihirisho yasiyokoma ya sifa hizi saba takatifu, zenye uhai, uweza, ujuzi, usikivu, kuona, utashi na maneno, uwepo wa msifiwa aliye wajibu kuwepo, na mwenye kuitwa mmoja wa pekee, na mtendaji wa pekee mtegemewa kwa haja zote. Hivyo inakuwa uwepo wake Allah (s.w) ni dhahiri mno kwa uoni wa akili kuliko jua kwa uoni wa macho na mkali zaidi, na kuitambua hata kama vile unaiona, na hii kwa sababu kitabu kizuri chenye maana njema na jengo lenye kupangika vema, kwa uwazi vinalazimisha matendo mawili ya kuandika na kujenga na matendo ya kuandika vizuri na kujenga kulikopangika vilevile vinalazimisha kwa uwazi majina mawili; mwandishi na mjenzi na majina mawili ya mwandishi na majenzi vilevile yanalazimisha kwa uwazi ufundi wa uandishi na ujenzi na sifa zake, na ufundi huu na sifa vinalazimisha kwa uwazi dhati ambayo itakayokuwa ni yenye kusifiwa na yenye kutengeneza, kiitwa na mtenda, kama isivyowezekana kuwepo na kitendo pasipo kuwapo na mtendaji wala jina bila kiitwa, vivyo hivyo haiyumkiniki kuwepo kwa sifa bila msifiwa wala ufundi bila fundi.

Na kama hivyo, inathibiti kwa kujengea hakika hii na kanuni hii kwamba ulimwengu huu – kwa vyote vilivyomo – umeandikwa kwa kalamu ya Kadari, na kujengwa kwa nyundo ya uweza, ikaandikwa ndani yake yasiyo na mpaka katika yaliyo kaika hukumu ya vitabu na barua zenye maana njema na kujengwa ndani yake ambayo ni mfano wa majengo na kasri, basi kila moja kati ya hizo inaashiria ishara zisizo na mpaka kwa maelfu ya sura na vinashuhudia pamoja kwa sura zisizo na mipaka shahidi zisizo na ukomo – juu ya wajibu wa kuwepo na upweke wa dhati tukufu ya azali ya milele, ndio msifiwa wa sifa hizo saba zenye kuzunguka zilizo takatifu na madini yake, kwa matendo ya kiungu Bwana mlezi mwingi wa rehema yasiyo na ukomo, na kwa madhihirisho yasiyo na mpaka ya majina elfu moja na moja katika majina mazuri ambayo ndio chimbuko la matendo hayo, na kwa kujidhihirisha kusiko na ukomo kwa sifa saba za kisubhana ambazo ni ndio chimbuko la hayo majina mazuri, na kadhalika hakika yaliyomo katika vilivyomo vyote katika sura zote za uzuri na aina za thamani na ukamilifu na katika uzuri mtakatifu unaowiana na matendo hayo ya kiungu Bwana mlezi na majina ya kiungu na sifa za kiungu mtegemewa kwa kila haja na mambo ya kisubhana na kuafikiana nazo, kila kati ya hiyo  – kwa dhati yake hasa – inashuhudia na kwa ujumla wake inashuhudia kwa uwazi juu ya uzuri mtakatifu na ukamilifu mtakatifu wa dhati yake (s.w).

Na kama hivyo, hakika ya Ubwana mlezi wenye kudhihiri ndani ya hakika ya kiutendaji yenye kutawalia inaitambulisha nafsi yake na kuibainisha kwa mambo yake na utendaji wake katika kuumba, kupatisha kutengeneza, na kuunda vema ambako kunafanyika kwa elimu na hekima, na kuidhihirisha katika kukadiria kuti sura, kuendesha, na kuongoza ambako kuna sifa ya mpangilio na mizani, na kudhihiri katika kuhaulisha, kubadilisha, kuteremsha na kukamilisha ambako kunatimizwa kwa makusudio na utashi, na inaiweka wazi katika kulisha, kuneemesha, kukirimu, na kutenda hisani ambako hutelewa kwa wema na huruma.

Na hakika ya kudhihiri kwa uluhiyya pia ambayo ina hisiwa na ipo kwa waziwazi ndani ya hakika ya kudhihiri kwa rububiyya inaitambulisha na kuifahamisha nafsi yake kwa madhihirisho ya majina mazuri yenye huruma na ukarimu, na kwa madhihirisho ya kiutukufu na kiuzuri ya sifa saba za kiuthibiti ambazo ni: Uhai, elimu, uweza, utashi, usikivu, uoni, na kuongea.

Naam, kama ilivyo sifa ya (Kuongea) inaitambulisha dhati tukufu (s.w) kwa wahyi na ilhamu, basi sifa ya (Uweza) kadhalika inaitambulisha dhati yake (s.w) kwa athari zake za kupendeza ambazo ni sawa na maneno yake yenye kubeba umbo ambayo yanasifu mweza mwenye utukufu na kuitambulisha kwa kudhihirisha kwake ulimwengu kutokea sehemu yake moja ya mbali  hadi sehemu nyengine ya mbali zaidi kwa hakika ya upambanuzi wa kimwili, na kwamba sifa ya (Elimu) pia inaitambulisha dhati ya mmoja wa pekee mwenye kusifiwa kwa kiasi cha vilivyotengenezwa vyote kwa hekima vyenye mpangilio na kupimwa, na kwa idadi ya viumbe vyote ambavyo vinaendeshwa, kusimamiwa, kupambwa na kupambanuliwa kwa elimu.

Ama sifa ya (Uhai) hakika athari zote zinazojulisha juu ya (Uweza) na sura na hali zenye mpangilio na hekima na mizani na mapambo ambavyo vinahabarisha kuhusu uwepo wa (Elimu) na dalili zote ambazo zinatoa habari kuhusu sifa nyingine tukufu, pamoja na dalili za sifa za (Uhai) zenyewe zinajulisha juu ya uwepo wa sifa ya (Uhai). Na uhai wenyewe vilevile pamoja na dalili zake zote hizo zinadhihirisha vyenye uhai vyote ambavyo vina hukumu ya vioo vyake, na kubadilisha ulimwengu wote kuwa katika sura ya kioo kikubwa kinachoundika kutokana na vioo visivyokuwa na mpaka vyenye kubadilika daima na kufanyika upya kwa mfululizo kwa ajili ya kudhihirisha madhihirisho yenye kupendeza na nakshi maridadi za aina kwa aina mpya chipukizi kila wakati.

Na kwa kupimia hili, hakika sifa za (Uoni) na (Usikivu) na (Utashi) na (Kuongea) zote hizo zinaitambulisha dhati tukufu kwa namna pana sana na kuifahamisha kwa upana wa ulimwengu. Na kwamba sifa hizo kama zinavyojulisha juu ya uwepo wa dhati yake (s.w), basi kwa uwazi pia zinajulisha juu ya uwepo wa uhai na kuthibiti kwake, na kwamba (s.w) ni (Hai) na hiyo ni kwa sababu elimu ni alama ya uhai na usikivu ni alama ya hali ya uhai, na uoni unawahusu walio hai na utashi unakuwa pamoja na uhai na uweza wa kihiari  hupatikana kwa wenye uhai, ama kuongea ni jambo la walio hai wenye utambuzi.

Na kama hivyo, inafahamika katika nukta hizi: Kwamba sifa ya (uhai) ina dalili na hoja zinazofikia mara saba ya upana wa ulimwengu, zinajulisha uwepo wake na uwepo wa msifiwa wake, (Al-Hayyu) hata uhai umekuwa ni msingi wa sifa zote na chimbuko lake, na chanzo cha Al-Ism Al-A’adham na uwanja wake. Na kwa kuwa Risale-i Nur imefafanua kitu fulani katika hakika hii ya kwanza na kuithibitisha kwa hoja zenye nguvu, kwa sasa tunatosheka kwa hili tone lililoelezwa katika bahari hii.

Hakika ya pili:

Ni kuongea kwa kiungu kunakotokana na sifa ya maneno. Hakika maneno ya kiungu (s.w), hayana ukomo, na hiyo ni kwa siri ya aya tukufu:

قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا Qur’an, 18: 109.

Maneno ni dalili ya dhahiri mno ya kujua uwepo wa mzungumzaji yaani hakika hii (kuongea kwa kiungu) inashuhudia shahidi zisizokoma juu ya uwepo wa mzungumzaji wa kiazali (s.w) na juu ya upweke wake. Na kwa hakika shahidi mbili zenye nguvu juu ya hakika hii zimekuja kwa kile kilichobainishwa katika ngazi mbili ya kumi na nne na kumi na tano katika risala hii kwa upande wa wahyi na ilham. Na ukaja ushahidi mwingine mkunjufu katika ngazi ya kumi katika Risala hiyo ambapo vimeashiriwa vitabu vitakatifu vya mbinguni, na kuna ushahidi mwingine wa wazi na wenye kukusanya katika ngazi ya kumi na saba ambapo kuna Qur’an tukufu ambayo ni muujiza. Basi tunahaulisha ufafanuzi wa hakika hii na ushahidi wake kwa ngazi hizo.

Na vivyo hivyo nuru na siri za aya tukufu:

 شَهِدَ اللّهُ أَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ وَالْمَلاَئِكَةُ وَأُوْلُواْ الْعِلْمِ قَآئِمَاً بِالْقِسْطِ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ Qur’an, 3: 18.

zilizotangaza hakika hii kwa namna ya kimuujiza na ikamaanisha ushahidi wake pamoja na ushahidi wa hakika nyinginezo, zimekuwa ni za kutosheleza na kutimiza kwa swahiba yetu mtalii hata hakuweza kuzivuka.

Imeelezwa katika ngazi ya kumi na tisa ya kituo cha kwanza ishara za maana fupi ya aliyoyapata msafiri huyu katika masomo katika kituo hiki kitakatifu:

[Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ambaye ni wajibu kuwepo mmoja wa pekee, mwenye majina mazuri, ana sifa tukufu, na ana mfano wa juu ambaye imejulisha juu ya kupasa kuwepo kwake katika umoja wake dhati ya wajibu kuwepo, kwa ijmai ya sifa zake tukufu zenye kuzunguka, na majina yake yote mazuri yenye kudhihiri, na kwa kuafikiana kwa mambo yake yote na matendo yake yenye kusarifu, kwa ushahidi wa utukufu wa hakika ya kudhihiri kwa uungu katika kudhihiri kwa hali ya kiungu ya Bwana mlezi, na katika kudumu utendaji wenye kutawala kwa kupatisha, kuumba, kutengeneza, kuanzisha kwa utashi na uweza, na kwa tendo la kukadiria, kuendesha, na kuongoza kwa hiari na hekima, na kwa tendo la usarifu, mpangilio, uhifadhi, uongozi na kutoa maisha kwa makusudi na huruma, na kwa ukamilifu wa mpangilio na mizani. Na kwa ushahidi wa utukufu wa kuzunguka kwa hakika ya siri za:

شَهِدَ اللّهُ أَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ وَالْمَلاَئِكَةُ وَأُوْلُواْ الْعِلْمِ قَآئِمَاً بِالْقِسْطِ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

Tanbihi

Kila hakika katika hakika zenye kushuhudia ngazi kumi na tisa katika ngazi za mlango wa kwanza wa kituo cha pili kilichotajwa muda uliyopita, kama inavyojulisha juu ya wajibu wa kuwepo kwa kuthibiti kwake na kuwepo kwake, vivyo hivyo inajulisha kwa kuzunguka kwake juu ya umoja na upekee, isipokuwa zimehesabiwa kuwa ni (dalili za kupasa kuwepo) kwa kuwa zimethibitisha kwanza – kwa uwazi – uwepo.

Ama mlango wa pili wa kituo cha pili kwa kuthibitisha kwake Tawhidi – kwa uwazi – kwanza, na kuthibitisha uwepo ndani yake, umeitwa (Hoja za Tawhidi). Na kama si hivyo – zote mbili hizo – yaani mlango wa kwanza na wa pili – inathibitisha uwepo na Tawhidi kwa pamoja lakini kwa ajili ya kupambanua kati ya milango hiyo inakaririwa katika mlango wa kwanza kifungu (Kwa ushahidi wa utukufu wa kuzunguka hakika) na katika mlango wa pili kifungu (Kwa ushahidi wa utukufu wa kuzunguka hakika) hali ya kuashiria Tawhidi iliyo wazi dhahiri, na kana kwamba ni kuona.

Niliazimia kufafanua ngazi za mlango wa pili ujao, kama ilivyo katika mlango wa kwanza, lakini vizuizi vya baadhi ya hali vimenilazimisha kufupisha, kwa hiyo tunahaulisha kwenye Risale-i Nur ili kutimiza haki yake ya kuweka wazi.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.