MLANGO WA PILI

Hoja Za Tawhidi

Hakika yule msafiri aliyetumwa duniani kwa ajili ya imani, na ambaye amefanya utalii wa kifikira katika ulimwengu wa viumbe ili kutaka kujua kuhusu Muumba wake katika kila kitu, na kumtambua mola wake kila mahali, na kuimarika imani yake kwa daraja ya haki ya yakini kwa kupasa kwa uwepo wa mola wake anayemtafuta, mtalii huyu alizungumza na akili yake kwa kusema: 

Njoo tutoke pamoja katika utalii mwingine mpya ili kupitia utalii huo tuone hoja ambazo zitatuongoza katika upweke wa Muumba wetu mtukufu (s.w). Wakaanza kutafuta kwa pamoja kwa shauku kubwa kuhusu (Hoja za tawhidi) hizi, wakapata mwanzoni mwa ngazi kwamba kuna hakika nne takatifu zinazohodhi viumbe, na zinalazimisha tawhidi kwa daraja ya uwazi.

HAKIKA YA KWANZA: UUNGU WA MOJA KWA MOJA

Hakika kuzama kwa kila kundi miongoni mwa makundi ya wanadamu katika aina miongoni mwa aina za ibada, na kujishughulisha kwao kwayo kushughulika ambako ni kana kwamba ni kwa kimaumbile. Na wenye uhai wote kutimiza huduma zako na kazi zao za kimaumbile ambazo ni katika hukumu ya aina miongoni mwa aina za ibada na kuwa kila moja katika neema na takrima za kimada na kimaanawy ambazo zinawafunika viumbe ni kikurubisho cha ibada na shukurani kwa mwabudiwa, huwapa njia za ibada na kuhimidi. Na kutangaza wahyi na ilhamu iliyoteulika na kudhihirika kimaana kutoka katika ghaibu, kwa hali ya uabudiwa wa mola mmoja. Yote haya yanathibitisha waziwazi kuthibiti kwa uungu mmoja kabisa na kutamalaki kwake.

Kwa kuwa hakika ya uungu huu ni yenye kuwa na ipo, kwa hiyo haitakubali kushirikiana pamoja nao kwa kuwa wanao kabili uungu huo (yaani Uabudiwao) kwa shukurani na ibada ni matunda yenye hisia katika kilele cha mti wa viumbe. Kwa hiyo yumkini ya kuwepo kwa wengine wanaovuta mazingatio ya hao wenye kuhisi na kuwavutia kwao, na wanafanya kuona neema zao na kuwashukuru, wakijitahidi kuwasahaulisha mwabudiwa wao wa haki – ambaye anaweza kusahaulishwa kwa haraka kwa kuwa kwake mbali na kuonekana na kujificha kwake na kuonekana na macho – ni jambo lenye kupingana na hakika ya uungu na makusudio yake ya matakatifu wala haiyumkiniki kuikubali kamwe, na kwa ajili hii Qur’an tukufu imejaza maelezo katika kukataa katika kukataa vikali ushirikina na kuwahofisha washirikina kwa adhabu ya jahannam.

HAKIKA YA PILI: RUBUBIYYA ISIYO NA MIPAKA

Hakika usarifu wa jumla wenye kuenea kutoka kwa mkono wa ghaibu katika viumbe wote – na hasa walio hai kati yao – kwa hekima na rehema, katika malezi yao na kuwapa kwao maisha ambako kunatimia kwa pamoja kwa njia ile ile katika kila upande kati ya pande zote, na kwa sura isiyotumainiwa na kutazamiwa, pamoja na kuhifadhiana baadhi kwa baadhi nyingine, hakika ni vinyunyu na mwanga vinavyomaanisha hali ya Ubwana mlezi mmoja kabisa, bali ni hoja kali juu ya kuthibiti kwake.

Kwa kuwa kuna Rububiyya moja bila mipaka kwa hiyo haikubali ushirika, wala kushirikiana kabisa, hiyo ni kwa sababu malengo ya Rububiyya hiyo na makusudio yake ya mbali ni kudhihirisha uzuri wake na kutangaza ukamilifu wake na kuhudhurisha kazi za ufundi wake za thamani na kudhihirisha maajabu yake yenye thamani. Na makusudio haya yote yamekusanyika katika kila chenye roho bali hata katika vijisehemu vidogo, na kwa hiyo haiyumkiniki kukubali Rububiyya moja isiyo na mipaka ushirika wala washirika kabisa, kwani kuingilia kwa holela kwa ushirika katika chochote kilichopo katika vilivyopo – vyovyote kiwavyo ni kidogo – na katika kila kilichapo hai – vyovyote kitakavyokuwa ni kidogo – huharibu malengo hayo na kubatilisha makusudio hayo na kugeuza akili mbali na malengo hayo na mbali na yule aliyeyataka na kuyakusudia kuelekea katika sababu. Na hili ndilo linalotofautiana na Rububiyya isiyo na mipaka kikamilifu na kufanyia uadui. Hivyo hapana budi Rububiyya hii moja isiyo na mipaka izuie ushirikina na sura zake kwa namna yoyote iwayo. Maelekezo ya Qur’an tukufu mengi yenye kuendelea katika tawhidi na kutukuza na kutakasa na kusabihi katika aya zake tukufu na katika maneno yake  na hata katika herufi zake na maumbo yake vinachimbuka kutokana na siri hii tukufu.

HAKIKA YA TATU: UKAMILIFU

Naam, hakika vyote vilivyomo ulimwenguni miongoni mwa hekima za juu na uzuri wenye kufurutu ada na kanuni za uadilifu na malengo yenye hekima hakika si jambo lingine bali vinajulisha kwa uwazi juu ya uwepo wa hakika ya makamilifu, nayo ni ushahidi dhahiri juu ya ukamilifu wa Muumba (s.w) ambaye ameupatisha huu ulimwengu kutokana na kutokuwepo na kuendesha mambo yake katika kila upande uendeshaji wa kimuujiza wa kuvutia mzuri, zaidi ya kua ni dalili ya wazi juu ya ukamilifu wa mwanadamu ambaye ni kioo chenye kuhisi na kuakisi cha madhihirisho ya Muumba mtukufu (s.w).

Kwa kuwa kuna hakika ya ukamilifu, na kwa kuwa ukamilifu wa Muumba ambaye ameupatisha ulimwengu katika hali ya ukamilifu ni thabiti na upo kihakika, na kwa kuwa ukamilifu wa mwanadamu ambaye ni tunda kamili zaidi la ulimwengu na khalifa wa Allah (s.w) katika ardhi, na mtengenezwa bora zaidi na kiumbe mpendwa zaidi kwa Muumba (s.w) ni hakika yenye kuthibiti vile vile, hapana budi kwamba ushirikina unageuza sura ya ulimwengu – wenye ukamilifu na hekima iliyo dhahiri – kuwa ni mchezo mkononi mwa usadifu, upuuzi unaochezewa na Asili, machinjio dhalimu ya kutisha ya wenye uhai, na matanga ya giza ya kuogofya ya wenye hisia – ambapo kila kitu huangukia katika kutoweka, na kuporomoka  katika kuondoka, na kwenda kwa kasi bila shabaha wala lengo – na ni jambo linamuangusha mwanadamu ambaye makamilifu yake yako wazi katika athari zake, katika ngazi ya chini katika ngazi za mnyama kama kiumbe aliharibikiwa zaidi na dhalili zaidi, na ni jambo lenye kufunika pazia katika vioo vya madhihirisho ya ukamilifu wa Muumba (s.w) – navyo ni viumbe wote vyenye kushuhudia ukamilifu mtakatifu usio na mipaka wa Muumba mkarimu, hali ya kubatilisha kwa kufanya hivyo matokeo ya utendaji wake na uumbaji wake (s.w)! Haiyumkiniki shirki kuegemea katika ukweli wowote wala kuwepo katika ulimwengu kamwe. Na shirki kupinga makamilifu ya kiungu, kibinadamu na kiulimwengu na kuyafanyia uadui na kufanya uharibifu ndani yake imejadiliwa na kuthibitishwa kwa upambanuzi katika (Mwale wa pili) ambao unabainisha matunda matatu ya tawhidi na hasa katika kituo chake cha kwanza kwa dalili zenye nguvu kali hivyo tunahaulisha huko.

HAKIKA YA NNE: UTAWALA WA  MOJA KWA MOJA

Naam, hakika anaye tazama mtazamo mpana wenye kupekua kwenye ulimwengu, ataona ni mfano wa mamlaka ya kutisha sana, katika upeo wa utendaji na utukufu, na itaonekana kwake kana kwamba ni mji mkubwa uendeshaji wake unafanyika kwa busara, na wenye mamlaka na utawala katika ukomo wa nguvu na haiba, na ataona kila kitu na kila sampuli imezama na kutiishwa kwa jukumu maalum aya tukufu:

وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ Qur’an, 48: 7.

inaleta hisia za maana ya uaskari katika viumbe ambavyo huundwa kwanza na majeshi ya chembe ndogo kabisa na vikosi vya mimea na makundi ya wanyama hadi majeshi ya nyota. Yote hayo ni majeshi ya kiungu, yaliyo undwa kwa ajili ya Allah (s.w). Tunakuta katika hao watendao majukumu wote wadogo sana na katika majeshi hayo makubwa yote, kupita amri za kimaumbile zenye kutawala kote na kupita kwa hukumu zenye kutiisha na kanuni za mfalme mtakatifu katika yanayo julisha kwa kina na kwa uwazi juu ya uwepo wa hali ya kiutawala moja isiyo na mipaka, na hali ya kiamri moja ya jumla.

Kwa kuwa hali moja ya kiutawala isiyo na mpaka ni hakika yenye kuwa na ipo, hapana budi kwamba ushirikina kuwa hauna hakika yeyote, kwani hakika timilifu ambayo aya tukufu inaweka wazi:

 لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا Qur’an, 21: 22.

inamaanisha kuwa ikiwa mikono mingi itaingilia katika suala maalumu na ikawa na nguvu, suala lenyewe lingekuwa limejichanganya, lau ingekuwa katika ufalme fulani kuna watawala wawili au hata ingekuwa katika upande fulani kuna mas’uli wawili, nidhamu itaharibika na kuingia dosari, na utawala utageuka kuwa vurugu. Na hali ya kuwa kuna nidhamu nzuri sana inayoenea kuanzia katika bawa la mbu hadi katika kandili za mbinguni, na kutoka katika seli za mwili hadi katika  njia za nyota na sayari, jambo ambalo haiyumkiniki ushirikina ukawa na maingilio yoyote katika hili japo kwa kiasi cha chembe ndogo kabisa, na kadhalika hali ya kiutawala yenyewe hakika ni makamo ya utukufu, makamo haya hayakubali mshindani na hasimu kwa yaliomo miongoni mwa ukiukwaji wa haiba yake na kuvunja utukufu wake.

Naam, hakika ya uthubutu wa mwanadamu daima wa kwenda kwa yule atakayemsaidia – kwa ajili ya udhaifu wake na kushindwa kwake – kumuua ndugu yake au mwanawe – kwa dhuluma – kwa ajili ya Utawala wa nje wa muda mdogo tu, inajulisha kuwa Utawala haukubali mashindano kamwe. Ikiwa mwanadamu – naye ni mshindwa – anathubutu kufanya jambo kama hili kwa ajili ya utawala mdogo, haiyumkiniki kwa hali yoyote katika hali kwa yule ambaye ni Mweza wa yote ambaye anamiliki ulimwengu wote kuridhia kuingilia au ushirika kutoka kwa yeyote katika utawala wake wa dhati takatifu ambayo ni mhimili wa Rububiyya yake isiyo na mipaka na uungu wake wa kihakika wa jumla.

Na kwa kuwa imethibitishwa hakika hii yenye kuangaza kwa dalili zenye nguvu katika (Kituo cha pili cha mwale wa pili) na katika maeneo mengi ya Risale-i Nur hivyo tunahaulisha huko.

Na kama hivi hakika ya swahiba wetu msafiri baada ya kuwa ameshuhudia hakika hizi nne imethibiti kwake Umoja wa Allah (s.w) kwa daraja la kushuhudia, hivyo imani yake ikakua na kupanda akaanza kuwa anarudiarudia kwa nguvu:

لاَ إلَهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَه

Kwa kuashiria somo alilojifunza katika ngazi hii imeelezwa katika kituo cha kwanza katika mlango wa pili.

[Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah (s.w), mmoja wa pekee ambaye imejulisha juu ya upweke waje na kupasa uwepo wake, kushuhudia kwa utukufu wa hakika ya udhihiri wa uungu usio na mipaka, na kadhalika kushuhudia kwa utukufu wa kuzunguka kwa udhihiri wa hali ya kiulezi usiyo na mipaka unaolazimu umoja, na kadhalika kushuhudia kwa kuzunguka hakika ya makamilifu kunakotokana na umoja, na kadhalika kushuhudia kwa utukufu wa kuzunguka hakika ya utawala isio na mipaka unaozuia na kukataa ushirika].

Kisha yule msafiri ambaye hatulii kabisa aliongea na nafsi yake akisema:

Hakika kukariri kwa watu wa imani

(لاَ إله إلاّهو)

kwa kuendelea na hasa masufi na kutangaza kwao wito wa tawhidi na kuikumbusha, inatubainishia kwamba kuna ngazi nyingi sana za tawhidi. Na kwamba tawhidi ndio jukumu muhimu zaidi takatifu na faradhi tamu zaidi ya kimaumbile na ibada ya juu zaidi ya kiimani. Kwa kuwa jambo liko hivi, basi moyo wangu njoo tufungue mlango wa kituo kingine katika vituo vya mji huu wa mazingatio na mtihani, ili tupate kujua kwa njia hiyo ngazi nyingine katika ngazi za tawhidi, kwa sababu tawhidi ya hakika ambayo tumekuwa tukiitafuta haiishii katika maarifa yatokanayo na kupata picha, bali  pia ni kile kilicho mkabala na kupata picha katika elimu ya mantiki miongoni mwa kusadikisha ambayo ni elimu nayo ni matokeo ya hoja, na hii ni ya juu sana kuliko maarifa ya kupata picha pekee.

Tawhidi ya kiuhakika ni hukumu, kusadikisha, kutii na kukubali, kwa kiasi mtu anaweza kumjua mola wake kupitia kila kitu, na kumuwezesha kuona katika kila kitu njia yenye nuru ambayo inamfikisha kwa Muumba wake mkarimu, halimzuii jambo katu kunako utulivu wa moyo wake na kuuhudhurisha katika kushikamana (kimoyo) na mola wake.

Ikiwa jambo sio kama hivi, mwanadamu angelazimika kuchana pazia ya viumbe na kuipasua – kila mara – ili aweze kumtambua mola wake. Kwa ajili hiyo msafiri alinadi kwa kusema: Haya twende ili tugonge mlango wa (Kibriyaa na Adhama) na tuingie nyumba ya (Athari na matendo) na ulimwengu wa (kupatisha na kutengeneza vema) hajaingia nyumba hii hadi akaona kwamba (kuna hakika tano zenye kuzunguka) zinatawala ulimwengu na kuthibitisha Tawhidi na kuilazimisha waziwazi.

HAKIKA YA KWANZA: HAKIKA YA ADHAMA NA KIBRIYAA

Kwa kuzingatia kufafanuliwa kwa hakika hii kwa hoja zilizopo katika (Kituo cha pili cha mwale wa pili) na katika sehemu mbalimbali katika Risale-i Nur hapa tutosheke na yafuatayo:

Hakika ambaye amezipatisha nyota ambazo ziko mbali kati yake kwa maelfu ya miaka, na ambaye anazisarifu katika wakati mmoja na kwa namna moja, na ambaye anaumba idadi isiyo hesabika ya sampuli moja kutokana na ua moja linaloota mashariki au magharibi au kaskazini au kusini katika ardhi, na kuzitia sura katika wakati mmoja na kwa umbo moja na sura moja na ambaye anatupa habari kuhusu tukio la ajabu mno lililopita na la kighaibu katika kauli yake (s.w):

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ Qur’an, 57: 4.

akithibitisha tukio hilo kana kwamba linatokea mbele yetu, kwa anavyoumba mifano yake midogo na wenza wake katika uso wa ardhi, na hasa wakati wa kuingia msimu wa machipuo ambapo tunaona ndani yake waziwazi zaidi ya mifano elfu moja ya ufufuo mkuu wa zaidi ya sampuli mia mbili elfu katika makundi ya mimea na mataifa ya wanyama ambayo yanaumbwa na kukuzwa ndani ya wiki chache tu, hapana shaka ambaye mkononi mwake kuna uendeshaji wa kundi hili kubwa kwa mkusanyiko, na kulilea na kulipa maisha na kupambanua baadhi yake na mengine, na kulipamba kwa ukamilifu wa mpangilio na mizani, bila kuchanganya au upungufu au kukosea na bila kuchelewa au kupuuza, na ambaye mzunguko wa ardhi upo mkononi mwake na kupatikana kwa tukio la usiku na mchana kwa mpangilio wa ajabu kama aya tukufu ilivyoweka wazi:

 يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ Qur’an, 31: 29.

hali ya kusajili na kufuta – kwa mzunguko huu – matukio ya kila siku na mabadiliko yake katika ukurasa wa usiku na mchana, naye ndiye ambaye anajua – katika wakati huo huo na punde hiyo hiyo, yaliyojificha vifuani na yanayopita nyoyoni, anayaendesha kwa matakwa yake, yatakikana awe – mtendaji wa matendo haya ambaye kila mojawapo ni kitendo kimoja pekee maalum – mmoja wa pekee mweza mwenye utukufu, ana utukufu na kibriyaa kwa uwazi kiasi kinachong’oa mashina ya ushirikina na kufuta athari zake zote na matazamio yake vyovyote iwavyo sampuli yake na kwa upande wowote uwao, na katika kitu chochote kiwacho, na mahali popote pawapo.

Kwa kuwa kibriyaa hii na uweza huu mkubwa vipo, na kwa kuwa sifa ya kibriyaa hii ni katika ukomo wa ukamilifu na kuzunguka timilifu, haiyumkiniki kuruhusu kabisa aina yeyote katika aina za ushirikina, kwa sababu ushirikina ni kuegemeza kushindwa na uhitaji katika uweza huo usio kuwa na mipaka, na ni kuambatanisha kasoro kwa kibriyaa hiyo, na kuupa upungufu ukamilifu huo, na kuuwekea mipaka uzungukaji huo kwa kifungo, na kukomesha kisicho na ukomo. haiyumkiniki kukubali hilo kila mwenye akili na utambuzi, na kila mwenye maumbile salama hayajaharibika.

Na kama hivyo, kwa vile ushirikina ni kukinzana na kibriyaa hiyo, na kudharau utukufu wa mwenye utukufu, na kushirikiana katika utukufu, ni kosa baya kabisa haliachi nafasi ya msamaha wa aina yoyote. Na kwamba Qur’an – yenye ufasaha wa kimuujiza – inalielezea hili na kulibainisha na kulitilia nguvu kwa mahofisho hayo makali na makamio ya kutisha kwa kauli yake (s.w)

 إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء Qur’an, 4: 48.

HAKIKA YA PILI: KUDHIHIRI KWA MATENDO YA KIUNGU KWA HALI ISIYO NA MIPAKA NA YENYE KUZUNGUKA

Nayo inashuhudiwa utendaji wake ulimwenguni kote na kudhihiri kwa namna isiyo na mipaka na hali ya kuwa yenye kuzunguka, vitendo hivyo havipangwi ila na hekima ya kiungu na utashi wa kiungu na ukubalifu wa matukio. Usadifu wa kiholela na Asili kiziwi na nguvu pofu na sababu mfu na chembe zenye kutapanyika, hazinyooshi mkono wake au kuingilia katika matendo hayo ambayo yapo katika ukomo wa umakini, mizani na hekima. Na ambayo hutimizwa kwa busara zote na uchangamfu na mpangilio na hekima, na sababu si lolote isipokuwa ni pazia za nje tu, uweza wenye kutenda huzitumia wa mwenye enzi na utukufu na kuzitiisha kulingana na amri zake na utashi wake na nguvu yake. Hapa tunapenda kubainisha mifano mitatu katika matendo ya kiungu – kati ya maelfu ya mifano hiyo – miongoni mwa ambayo aya tatu tukufu zinazoungana baadhi kwa baadhi yake nyingine zinaashiria katika surat An-Nahl. Na pamoja ya kuwa kila kitendo kati ya hivyo kinajumuisha nukta zisizohesabika isipokuwa sisi hapa tutaeleza tatu tu kati ya hizo.

Aya ya kwanza:

 وَأَوْحَى رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا Qur’an, 16: 68.

Naam, nyuki ni muujiza wa uweza wa kiungu kimaumbile na kwa jukumu, na muujiza uliyoje mkubwa hata ikaitwa kwa jina lake sura tukufu ndani ya Qur’an tukufu?! Hiyo ni kwa kuwa kusajili programu kamili ya jukumu lake kubwa katika kichwa kidogo sana cha mashine ya asali ndogo, na kuweka vyakula bora kabisa na vitamu zaidi katika tumbo lake dogo na kuipika humo. na kuchagua mahali munasibu kwa ajili ya kuweka sumu yenye kuuwa yenye kuvunjavunja viungo vilivyo hai katika mkuki wake mdogo bila ya kuathiri katika viungo vingine kwenye mwili, haiyumkiniki kufanyika – yote haya – isipokuwa kwa ukomo wa umakini, ujuzi na ukomo wa hekima na utashi na upeo wa mizani na mpangilio, kwa hiyo hakitaingilia kamwe kisicho na utambuzi wala nidhamu wala mizani mifano ya Asili ziwi au usadifu pofu katika vitendo kama hivi vya ajabu.

Na kama hivi tunaona miujiza mitatu katika ufundi huu wa kiungu na kushuhudia kudhihiri kwa kitendo hiki cha kiungu pia katika kiasi kisicho na mpaka cha nyuki katika pande zote za ulimwengu. Kudhihiri utendaji huu wa kiungu na kuzungukia kwake wote na kwa hekima ile ile na umakini uleule na mizani ile ile na katika wakati huo huo na kwa mtindo huo huo ni wazi kuwa inajulisha umoja na kuthibitisha upweke.

Aya ya pili:

وَإِنَّ لَكُمْ فِي الأَنْعَامِ لَعِبْرَةً نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَآئِغًا لِلشَّارِبِينَ Qur’an, 16: 66.

Hakika ya amri hii ya kiungu inatona mazingatio na masomo. Naam, hakika kunywesha maziwa meupe safi, yenye lishe matamu, kutokea katika viwanda vya maziwa vilivyowekwa katika chuchu za wazazi, kuanzia ng’ombe, ngamia, mbuzi na kondoo, ambapo hububujika kwa ukarimu katikati ya damu na kinyesi bila kuchanganyika navyo au kutibuka. Na kupandikiza kilicho kitamu mno kuliko maziwa na kizuri zaidi na cha thamani zaidi katika nyoyo za wazazi hao navyo ni upole na huruma unaofika kiwango cha kujitolea fidia na kuwatanguliza watoto katika mema, kwa vyovyote jambo hilo linahitajia kiwango cha huruma, hekima, elimu, uweza, hiari na umakini, mambo ambayo kamwe hayawezi kuwa katika matendo ya kusadifu kwa holela na chembe potevu na nguvu pofu, na kwa hiyo utendaji wa ufundi huu wa kiungu, na kuzunguka kwa tendo hili la kiungu, na kudhihiri kwake katika hekima ileile, na umakini uleule, na muujiza uleule, na wakati mmoja na mtindo mmoja katika nyoyo za maelfu yaliyoundika kutokana na aina za kina mama wazazi na katika maziwa yao na katika uso wote wa ardhi. Inathibitisha umoja kwa waziwazi na kujulisha upweke.

Aya ya tatu:

 وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا إِنَّ فِي ذَلِكَ لآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ Qur’an, 16: 67.

Aya hii tukufu inageuza mitazamo na kutanabahisha kwenye mitende na mizabibu, inamtanabahisha mwanadamu kwamba katika matunda haya mawili kuna ishara kubwa kwa wenye akili, na hoja ya wazi juu ya Tawhidi. Naam, hakika ya matunda mawili yaliyotajwa yanazingatiwa kuwa ni lishe na chakula, na matunda wakati huohuo. Na mawili hayo ni chanzo cha maada nyingi za lishe tamu, pamoja na kuwa mti wa kila mmoja kati ya matunda mawili hayo hustawi katika udongo makavu, na kustawi katika ardhi kame. Kila moja kati ya miwili hiyo ni muujiza katika muujiza ya uweza wa kiungu, na ni jambo la kufurutu ada kati ya yanayo furutu ada ya hekima ya kiungu. Na kila moja kati yao ni viwanda vya sukari na halwa na maabara za vinywaji vyenye asali, na kazi za kiufundi zenye mizani makini yenye kuhisi mno na mpangilio kamili na umahiri wa hekima, na ufundi timamu, kwa kiasi kwamba anayemiliki kiasi cha Atomu ya akili na busara analazimika kusema: (Hakika ambaye ameumba vitu hivi kama hivi ndiye ambaye amepatisha viumbe vyote) kwa sababu tuyaonayo mbele ya macho yetu – mathalani – kuning’inia chini kwa yanayokaribia makonyo ishirini ya zabibu, kutokana na tawi hili dogo jembamba, kila konyo humo linabeba kiasi kinachokaribia punje mia moja katika punje laini na kokwa zenye asali, na kila punje katika punje hizo imefunikwa kwa kifuniko nyororo laini chenye rangi za kuvutia, na kukusanya ndani yake laini kokwa ngumu yenye kubeba historia ya maisha na mwendo wake. Naam, hakika kuumba yote haya katika zabibu na mifano yake – nayo haihesabiki – katika uso wa tandiko lote kwa umakini uleule, na hekima ileile, na kupatisha ufundi huo unaofurutu ada ambao ni muujiza kwa idadi yake kubwa wakati mmoja na kwa mtindo mmoja, hakika ni wazi inathibitisha kwamba anayetenda jambo hili si mwingine isipokuwa ni Muumba wa viumbe wote, na kwamba kitendo hiki ambacho kimelazimu uweza huo usio na mpaka na hekima ya hali ya juu, si vingine ila ni kutokana na utendaji wa Muumba huyo mtukufu.

Naam, nguvu pofu na Asili ziwi na sababu zenye kupotea na kutawanyika, haiwezekani kunyoosha mikono yake na kuingia katika mizani hiyo makini yenye kuhisi sana, kwa umahiri mkubwa, na mpangilio wa hekima wa ufundi huo, bali inatumika na kutiishwa kwa amri ya kiungu katika matendo ya kiungu, ni vyenye kutendwa na kukubali, bali si vinginevyo isipokuwa ni pazia zenye kutumiwa na mkono wake (s.w).

Na vilevile, kama zinavyo ashiria aya hizi tatu hakika tatu, na kila moja inajulisha Tawhidi kwa nukta tatu, kuna kiasi kisicho na mpaka cha matendo ya kiungu na kiasi kisicho na mpaka katika sarifu za kiungu, zenye kujulisha hali ya kuafikiana juu ya mmoja wa pekee na zinashuhudia ushahidi wa kweli juu ya dhati ya mmoja wa pekee mwenye utukufu na ukarimu.

HAKIKA YA TATU: HAKIKA YA KUPATISHA NA UUMBAJI WA AJABU

Yaani, kupatisha vilivyomo – na hasa mimea na wanyama – kwa wingi kabisa, kwa haraka kabisa, na kwa mpangilio bila mpaka, na kuumba viumbe kwa wepesi kabisa, katika upeo wa uzuri pamoja na umahiri mzuri na mpangilio kamili, na kutengeneza vema vitengenezwa katika upeo wa thamani, ubora na kupambanua kwa wazi pamoja na ukomo wa wingi na upeo wa mchanganyiko.

Naam, hakika kupatisha vitu katika ukomo wa wingi kwa ukomo wa kasi, na katika ukomo wa wepesi kwa ukomo wa ufundi na umahiri na kwa umakini na mpangilio, na katika ukomo wa ubora na ughali wa thamani na kupambanuka pamoja na ukomo wa wingi mno pasipo mchanganyiko au babaiko au dosari pamoja na wingi wa tofauti, kupatisha huku hakuwezi kufanyika – wala hakutofanyika –  isipokuwa kwa uweza wa mweza mmoja wa pekee hakimtopei kitu wala haiwi ugumu kwa uweza wake lolote.  

Naam, na ili tutambue tunachokiona na kukishuhudia kwa macho yetu yatakikana ziwe nyota na Atomu kwa namna moja mbele ya uweza huo, na vitu vikubwa ni kama vidogo, na idadi isiyo na mpaka ya sampuli ni kama moja yake, na jumla kubwa yenye kuzunguka kama sehemu ndogo maalum, na kuhuisha ardhi kubwa kama kuhuisha mti mmoja, na kuchipuza mti mrefu ni kama kupatisha mbegu ndogo sana.

Na kwa siri hii muhimu ambayo imo katika ngazi hii ya kitawhidi, na hakika hii ya tatu na neno la Tawhidi, yaani kuwa kikubwa (chote) kama kidogo cha (sehemu) mbele ya uweza wa kiungu bila ya kuwepo tofauti japo kidogo kati ya nyingi na chache, zinafichuka siri nyeti zilizojificha za Qur’an tukufu. Na ufafanuzi wa hekima hii yenye kuleta tahayari na fumbo kuu ambalo limetoka nje ya kiwango cha akili – pamoja na kuwa ni msingi wa Uislamu na uwanja wa kina zaidi wa imani na tofali kubwa la Tawhidi, hutambuliwa siri zilizojificha sana zisizojulikana za hakika ya kuumbwa kwa ulimwengu ambazo falsafa imeshindwa kuzitambua. Basi shukrani elfu moja na moja, na hamdi elfu moja na moja na sifa kwa Muumba wangu mwingi wa rehema nazinyanyua kwa idadi ya herufi za Risale-i Nur, kwa Risale-i Nur kuweza kufumbua siri hii ya ajabu, na kufunua hili ambalo mjinga analidhania kuwa ni fumbo la ajabu, bali imelithibitisha kwa hoja kali, na hasa katika kujadili (Naye juu ya kila jambo ni mweza) iliyopo mwishoni mwa (Andiko la ishirini) na katika kujadili (Mtendaji mweza) kwenye (Neno la ishirini na tisa) ikathibitisha ukunjufu wa uweza wa kiungu na ufasaha wake kwa hoja kali kwa daraja la jumla ya mbili zidisha mbili ni sawa na nne, na hiyo ni katika ngazi za (Allahu Akbar) katika (Mng’ao wa ishirini na tisa) ambayo imetungwa kwa lugha ya Kiarabu. Pamoja na kuhaulisha upambanuzi na ufafanuzi huko hapa nimetaka kubainisha kiujumla kama faharisi ya muhtasari wa misingi na dalili hizo ambazo zinashughulikia siri hii zinaifafanua na kuiweka wazi, kisha kuashiria katika siri kumi na tatu kwa ngazi kumi na tatu, na nikaanza kuandika siri ya kwanza na ya pili, lakini vizuizi viwili vya nguvu vya kimaada na kimaanawy vimenizuia –  kwa masikitiko – kati yangu na kati ya kuandika siri zilizobaki kwa wakati huu.     

Siri ya kwanza:

Ikiwa kitu ni cha kidhati, dhidi yake hakiwi chenye kuingia kwake kwa sababu huko ni kukutana kwa dhidi mbili na jambo hilo ni muhali. Basi kwa kujengea siri hii: Kwa kuwa uweza wa kiungu ni wa kidhati nayo ni dharura yenye kulazimu dhati takatifu, kushindwa ambako ni dhidi ya huo uweza hakuwezi kuingia katika dhati yenye uweza. Na kwa kuwa uwepo wa viwango katika kitu kimoja hutokea kwa kuingilia kwa dhidi yake – mfano vinavyofanyika viwango vya  nguvu na udhaifu wa mwanga kwa kuingilia kwa giza, na viwango vya kupanda kwa joto na kushuka kwake kwa kuingilia kwa ubaridi, na viwango vya nguvu na udhaifu wake kwa mkabala wa upinzani, – haiwezekani nguvu hiyo ya kidhati kuwa na viwango, nguvu hiyo inaumba vitu na kuvifanya viwepo kama kitu kimoja. kwa kuwa uweza huo wa kidhati hauna viwango, hauna udhaifu wala upungufu, hapana shaka hakisimami mbele yake kizuizi wala kuumba hakuwi kugumu kwake. Na kwa kuwa hakiwi kigumu kwake kitu chochote hivyo hapana budi kuwa haki yake kuleta ufufuo mkuu kama wepesi wa kuleta majira ya machipuo, na kuleta majira ya machipuo kama wepesi wa kuleta mti mmoja, na kuleta mti kama wepesi wa kuleta ua moja, na kwamba – uweza huo – unafanya uumbaji kwa wepesi na urahisi huu kama unavyofanya hilo kwa umakini mno ya uwavyo ufundi na utengenezaji mwema. Tunaona uweza huo unaumba ua kwa uzuri sawa na mti na kwa umuhimu na thamani yake, na unaumba mti kwa muujiza sawa na kutengeneza majira ya machipuo, na unaumba majira ya machipuo kwa ujumla wa ufufuo na hali yake ya mkusanyiko na muujiza wake, hivi ndivyo uumbavyo na kama hivi ndivyo tushuhudiavyo uumbaji wake mbele ya macho yetu.

Risale-i Nur imethibitisha kwa hoja nyingi kali zenye nguvu kwamba kama uumbaji haukuegemezwa kwa umoja na upekee, kuumba ua moja kuna kuwa ni vigumu kama ugumu wa kuumba mti bali ni vigumu zaidi, na kuumba mti inakuwa ni changamani zaidi kuliko kuumba majira ya machipuo. Na zaidi ya hivyo, vyote vitadondoka kiupande wa thamani na ufundi bora katika kutengenezwa, kiumbe ambaye anatengenezwa katika dakika moja atatengenezwa katika mwaka mmoja, bali ni muhali kumtengeneza kabisa.

Kwa msingi wa siri hii: Matunda, maua, na miti yote na vilivyo hai vidogo vinavyo ambatana navyo, hutokea katika uwepo kwa wingi mno pamoja na kuwa katika uzuri na upekee, hudhihiri kwa haraka na wepesi pamoja na kuwa katika upeo wa ufundi na kutengenezwa vyema, hutokea katika uwepo kwa nidhamu, hali ya kutekeleza majukumu yake na tasbihi zake na huku zikiwakilisha mbegu zake kuwa mbadala wake, zikienda zake.

Siri ya pili:

Kama lilivyo jua moja linachoma mionzi yake katika kioo kimoja, kwa kudhihiri kutokana na uwezo wa kidhati na kwa kuegeme katika siri ya hali ya kinuru na kuangaza na utii, hakika linajiakisi kwa wepesi kwa sura hiyohiyo – yenye mwanga na joto – kwa utendaji mpana kwa uwezo wake usio na mpaka kwa amri ya kiungu, kwenda katika kiasi kisicho na mpaka cha vioo vyenye kung’ara na matone.

Na likitamkwa neno moja hakika ya neno hili huingia kwa wepesi timamu kwenye sikio la mtu, – kwa kuegemea ukunjufu mpana wa hali ya kiuumbaji – na huingia katika masikio ya mamilioni ya watu kwa wepesi na urahisi kwa amri ya kiungu, na mbele yake maelfu ya wasikilizaji na msikilizaji mmoja ni sawa na hakuna tofauti kati yao.

Na kama jicho linavyoangalia mahali pamoja na maelfu ya mahali kwa wepesi timilifu, hakika ya nuru kama Jibril (a.s) wakati anashuhudiwa anakwenda na kuhudhuria sehemu moja kwa wepesi – kwa kuegemea ukamilifu wa upana wa utendaji wa kiungu katika kudhihiri kwa rehema – basi pia anashuhudiwa na anakwenda na kuhudhuria – kwa uweza wa kiungu – kwa wepesi huo huo katika maelfu ya mahali hapa hakuna tofauti kati ya uchache na wingi.

Na kama hivyo, uweza wa kidhati wa kiazali,

(ولله المثل الأعلي)

kwa kuwa kwake ni nuru pole zaidi na mahususi zaidi bali hiyo ni nuru ya nuru zote, na kwa kuwa kiini cha vitu na hakika yake na sura za ufalme timilifu ndani yake ni angavu zenye kung’ara kama vioo, na kwa kuwa kila kitu – kuanzia atomu, mimea, aina za walio hai wote, nyota, majua mpaka miezi – ni wafuasi na watiifu kwa namna timilifu wa hukumu ya uweza huo wa kiungu, na ni wenye kutiishwa na kuamuriwa kama askari na wanyenyekevu kabisa kwa amri za uweza huu wa kiazali. Hapana shaka kuwa unaanzisha vitu chungu nzima na kuviumba kama kitu kimoja, unahudhuria katika kila kitu kwa kila wakati na katika kila mahali, kitu hakizuilii kingine kikubwa na kidogo, kingi na kichache, na sehemu na jumla yote, ni sawa kwake haushindwi na kitu wala hakiwi chochote kigumu kwake.

Na kwa kuegemea siri za kupangika, mizani, kutekeleza amri na kutii hukumu – kama ilivyoelezwa katika (Neno la  kumi) na la (Ishirini na tisa), hakika ya jahazi kubwa sana yawezekana kuongozwa na kuendeshwa kwa wepesi sawa na uendeshaji wa mtoto kwa mwanasesere wake kwa kidole. Na hakika kiongozi kama anavyoongoza askari mmoja kwa amri yake: (shambulia), kwani kwa amri hiyohiyo anaongoza jeshi lililopangika tiifu kwenye vita. Na kukiwa na milima miwili katika hali ya uwiano wa mizani katika ncha mbili ya mizani kubwa yenye kuhisi sana, kisha ikaletwa mizani nyingine ikawekwa katika kila kitanga chake yai moja katika ulinganifu timamu, kama inavyoyumkinika kwa joza moja kunyanyua moja ya vitanga viwili kwenda juu na kingine kwenda chini, kadhalika joza hiyohiyo inaweza – kwa kanuni ya hekima – kunyanyua moja ya vitanga viwili vya mizani kuu yenye kunyanyua mlima katika kilele cha mlima na kukiteremsha kingine katika kilindi cha konde. 

Mambo kama hivyo, na ndivyo yalivyo katika uweza wa kiungu kwa kuwa hauna mipaka na sio wenye ukomo, na wa kinuru wa kidhati na wakudumu milele na upo pamoja na hekima isiyo na mipaka na uadilifu timamu ambazo ni chimbuko la nidhamu na mifumo na uwiano wa mizani na chanzo chake na uwanja wake, cha sehemu na cha jumla yote kikubwa na kidogo, chochote kile na katika kila kitu ni chenye kutiishwa kwa hukumu ya uweza huo kinafuata utendaji wake. kwa hiyo uweza huo huendesha nyote na sayari kwa wepesi sawa na kuendesha Atomu na kuzipa harakati na hii kwa siri ya mfumo wa hekima, na kama inavyohuisha nzi katika majira ya machipuo kwa wepesi, huendesha makundi yote ya wadudu na mimea na wanyama katika medani ya uhai na kuvihuisha kwa wepesi uleule na kwa amri ileile na kwa hekima iliyomo ndani yake na kwa siri ya mizani kama inavyootesha mti katika majira ya machipuo kwa wepesi wa hali ya juu na kupuliza uhai katika mashina yake ambayo kama mifupa inahuisha kwa uweza huo usio na mpaka wenye hekima adilifu na kwa amri hiyohiyo Ardhi hii kubwa ambayo ni kama jeneza kubwa, kama ilivyohuisha ule mti kaatika majira ya machipuo kwa wepesi, hali ya kuwa inaleta katika uwepo mamia ya maelfu ya aina za mifano na vielelezo ambayo inajulisha juu ya ufufuo. Na kama (s.w) anavyo huisha ardhi kwa amri ya kufanya hakika ni katika madhumuni ya aya tukufu zijazo:

 إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ Qur’an, 36: 53.

 وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلاَّ كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ Qur’an, 16: 77

 مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Qur’an, 31: 28

Ataleta wote wanadamu na majini na kilicho cha kinyama na kiroho na kimalaika, wote atawaleta kwa amri hiyohiyo kwa wepesi uleule katika uwanja wa mkusanyiko mkuu wa ufufuo na mbele ya mizani kuu, basi kitendo  hakizuii kitendo kingine katu.

Hakika ni kwamba, imeahirishwa kuandika baki ya siri nyingine kutoka katika siri ya tatu kinyume na matakwa yangu hadi wakati mwingine Inshaallah (s.w).

HAKIKA YA NNE: UJUMLA WA VILIVYOMO NA KUTOKEA KWAKE KWA PAMOJA

Hakika uwepo wa vilivyomo na kudhihiri kwa pamoja kwa kuingiliana na kufana baadhi na vingine, na vingine kuwa ni mfano mdogo kwa vingine na kielelezo chake kikubwa na sehemu yake kuwa ni jumla yote na baadhi kuwa ni sehemu na idadi moja pamoja na kufanana katika muhuri wa uumbaji na uhusiano madhubuti katika nakshi ya ufundi na kufanya vyema na kusaidiana kati yake na kila mmoja kukamilisha jukumu la mwingine la kimaumbile, na mifano mingi kama hii katika nukta nyingi yaupande wa umoja mwingi katika vilivyomo. Inatangaza Tawhidi kwa uwazi na kuthibitisha kuwa mtengenezaji wake ni mmoja wa pekee, inaonesha kwa upande wa Rububiyya yenye kutawala –  hakika ya viumbe vyote havikubali kugawanyika  kwa hukumu ya yote  jumla na jumla.

Mfano wa hilo:

Hakika ya kuleta vitu bila idadi vya aina mia nne elfu ya aina za mimea na wanyama katika majira ya machipuo na kuviongoza kwa pamoja wakati mmoja, na kwa mtindo mmoja, pamoja na kuingiliana baadhi yake kwa ingine, pasipo kosa au dosari, na kuipa maisha kwa ukamilifu wa hekima na uundaji mzuri na kutenda vyema na vilevile kuumba vitu visivyo na mipaka vya sampuli ya ndege kuanzia na mfano mdogo, (na vijidudu) hadi mifano yake mikubwa (vipanga) na kuvipa uweza kutembea angani, na kuvianna misaada inafanyika ndani daa kwa zana zinazowasaidia kwa maisha kuhangaika nakutembea nakueneza furaha angani, na kuweka muhuri wa ufundi wa muujiza na kuhitimisha usoni mwake  na kuweka muhuri wa hekima katika miili yao kwa uangalizi mkubwa na kuweka alama za umoja katika utambulisho wake kwa uangalizi  na malezi yote. Na vilevile kuzipa seli atomu za chakula na kuwapa wanyama mimea na mwanadamu kuwapa wanyama na watoto wadogo wenye kushindwa kuwapa huruma za wazazi na matunzo yao na kufanya jitihada hizi na utoaji na msaada hufanyika katika hekima timilifu na katika rehema kamili na kufanya jitihada hizi zinafanyika ndani ya hekima na huruma kamili vilevile utendaji kwa nidhamu yenyewe hiyohiyo na upendezeshaji huohuo na kwa kitendo kilekile na kwa hekima hiyohiyo kuanzia katika mfumo wa sayari – katika mizunguko ya mikubwa ya kiulimwengu – hadi katika mfumo wa majua na katika chembe za ardhi bali hata katika kiini cha jicho na majani ya vikonyo vya maua na mbegu za mahindi na tikiti – kwa mfano –  kana kwamba ni duru zenye kuingiliana na kwa hukumu ya kilicho sehemu na  cha jumla. yote hayo ilikuthibitisha kuwa ambaye nafanya matendo haya hakika si mwingine bali ni mmoja wa pekee ameweka muhuri wake katika utosi wakila kitu katika uwepo.

Na kama ilivyo kuwa hana mpaka na mahali basi yeye yupo kila mahali, na yeye yu karibu na kila kitu pamoja na kuwa kila kitu kiko mbali naye kama jua. Na kama yanavyokuwa mepesi kwake mambo magumu sana ya duru za kiulimwengu kubwa na mfumo wa jua hakifichikani kwake pia mambo madogo kabisa za chembe za damu na mawazo nyeti ya kimoyo hakuna kitu kinachobakia nje ya utawala wake na duara la utendaji wake. na vyovyote kitakavyokuwa kitu kiwe kikubwa au vingi ni rahisi na chepesi kwake kama kitu kidogo mno na kichache na anaumba mdudu mdogo katika mpangilio wa kipanga na uzuri wake. Na anaumba ua katika hali ya mti  mpangilio wake. Na anaumba ua akatika sura ya bustani na kupendeza kwake na anaumba majira ya machipuo katika urembo wa majira ya machipuo na maua yake, na aumba majira ya machipuo katika ukuu wa ufufuo na haiba yake. Na anatuletea wingi wa vitu kwa kuvifanya vizuri na ghali mno kwa thamani kwa thamani rahisi duni bali naitengeneza kwa kutufanyia hisani kisha hataki kutoka kwetu isipokuwa (Bismillah) na (Alhamdulillah) yaani thamani iliyokadiriwa kwa neema hizo ni bismillah Ar-rahmani ar-rahiim kwa kuanzia na Alhamdulillah kwa kuhitimisha.

Tutosheke na kiasi hiki kwa kuangalia kuwa Risale-i Nur imefafanua hakika hii ya nne na kuithibitisha kwa upambanuzi zaidi.

Na swahiba yetu mtalii aliona katika ngazi ya pili:

HAKIKA YA TANO: NIDHAMU KAMILI NA UMOJA WA MAADA

Yaani umoja wa mpangilio ulio kamili mno katika mkusanyiko wa ulimwengu na nguzo zake na sehemu zake bali katika kila kilichomo ndani yake na umoja wa watendaji kazi na maada ya ulimwengu kunjufu ambayo ni mhimili wa uongozaji wake na wenye kuambatana na hali yake ya jumla na kuwa kwa majina na matendo yenye kutenda katika mji huo mkubwa na mkusanyiko wa ajabu ni yenye kuzunguka na kukusanya kila kitu, jina ni hilohilo na kitendo ni hichohicho na hakika ni hiyohiyo katika kila mahali pamoja na kuingiliana baadhi yake kwa baadhi nyingine, na kuwa kwa chembe na sampuli ambazo ndio msingi katika kujenga kasri hiyo kubwa na kuiendesha na kuweka furaha juu yake, hali ya kuzunguka katika uso wa Ardhi kwa kauenea kwake katika nyingi ya maeneo ya Ardhi, pamoja na kubakia kipengele hichohicho na sampuli yenyewe moja na yenye utambulisho mmoja katika kila mahali pamoja nakuingiliana baadhi kwa baadhi nyingine. Yote hayo yanalazimu waziwazi, na kujulisha kwa udharura na inashuhudiwa na kuonekana kwamba fundi wa ulimwengu huu na mwendeshaji wake na mfalme wa ufalme haya n mlezi wake na mwenye nyumba hii na mjenzi wake ni mmoja wa pekee hakuna kama mfano wake chochote hana waziri wala msaidizi hana mshirika wala mwenza ametakasika na kushindwa amepukana na  kasoro zote.

Naam, hakika mpangilio timamu hakika yenyewe ni dalili ya umoja kwani yanahitaji mpangiliaji mmoja  ushirikina hauufai ambao ni mhimili wa mjadala na ushindani.

Na kwa kuwa kuna mpangilio na umakini katika ulimwengu mzima –kiujumla au kitu kiwe ni sehemu – kuanzia katika mzunguko wa Ardhi wa kila siku na kila mwaka, hadi katika alama ndogo za mwanadamu, na katika mfumo wa hisia zake, katika kuzunguka kwa chembe za damu nyekundu na nyeupe na kutembea kwake kwenye damu haiyumkiniki kitu kunyoosha mkono wake na kuingilia kwa kukusudia na kupatisha isipokuwa mweza na mwenye hekima zote zisizo na mipaka bali kila kitu kisichokuwa yeye ni mtendewa na mpokezi na kudhihirisha kwa kukubali na sio vinginevyo.

Na kwa kuwa kufanya mpangilio na kutunuku mpangilio na hasa kufuatilia malengo na kuyaratibu kwa kudhihirisha masilahi haiwi isipokuwa kwa elimu na hekima isipokuwa kwa utashi wenye kutimia na hiari hapana budi kwamba mpangilio huu ambao unakwenda pamoja na hekima na aina hizi mbalimbali za mpangilio katika viumbe visivyo na mipaka ambako kunaonekana mbele ya macho yetu na wenye kwenda kulingana na masilahi inajulisha wazi na inashuhudia kwa kila hali kwamba Muumba wa viumbe hivi na mwendeshaji wake ni mmoja naye ni mtendaji naye ndiye ambaye anamiliki hiari kila kitu kinachotokea katika uwepo hakika kinatokea kwa uweza wake yeye, na kuchukua hali maalum kwa utashi wake yeye na kuchukua sura iliyopangika kwa hiari yake yeye.

Kwa kuwa taa iwakayo ya hii dunia mahali pa wageni ni moja, na kandili yake iliyoteremka chini kwa hesabu ya siku ni moja, na kwamba mawingu yake yenye rehema ni mamoja, na kwamba jiko lake lenye kuwaka ni moja, na kwamba kinywaji chake ambacho kinaleta ni kimoja nakwamba shamba lake lenye himaya ni moja ni moja moja moja moja hadi elfu moja na moja. hapana budi kwamba haya mamoja moja kwa dhahiri yanashuhudia kwamba fundi wa mahali hapa pa ugeni na mwenyewe ni mmoja naye ni mkarimu kwa wageni wake katika ukomo wa ukarimu, hata ya kwamba yeye anawatiisha wakubwa wa wafanya kazi wake hawa na kwafanya wahudumu watiifu ili kudhamini raha ya wageni wake walio hai.

Na kwa kuwa hayo majina mazuri ni mamoja na mambo ya kiungu na matendo ya kiungu Bwana mlezi ambayo yanasarifu mambo ya ulimwengu na ambayo yanadhihirisha madhihirisho yake na nakshi zake na athari zake pande zote za ulimwengu basi majina mazuri: (Al-Hakiim, Al-Muswawwir, Al-Mudabbiru, Al-Muhyi na Al-Murabby) na mifano kama hiyo yenyewe hiyohiyo kila mahali. Na mambo ya hekima na Rehema na uangalizi) na mifano yake ni hiyo hiyo kila mahali na matendo ya (kutia sura) kuendesha, na malezi) na mfano wa hayo kila mahali. Na yote hayo yameingiliana kila moja kati ya hayo ni katika ngazi ya juu sana na mzunguko wa mpana zaidi na kutamalaki, kama ili vyo kila moja kati hayo hukamilisha nakshi ya mingine hata inakuwa kana kwamba majina hayo na matendo hayo yanaungana na mengine kwa pamoja, Uweza ni ndio hiyo hekima na Rehema na hekima inakuwa ndio hiyohiyo uangalizi na uhai, inapojitokeza – kwa mfano – utendaji wa jina (Al-Muhyi) katika kitu fulani, unajitokeza utendaji wa jina (Muumba na mtengeneza sura na mtoa riziki) na majina mengine mengi vilevile wakati huo huo, kila mahali na kwa mpangilio huohuo, hapana budi na hakuna kizuizi kwamba hilo kwa uwazi linashuhudia kwamba mwenye kuitwa majina hayo yenye kuzunguka mna mtendaji wa matendo hayo yenye kukusanya na kuonekana kila mahali kwa namna hiyohiyo hakika huyo ni mtendaji mmoja wa pekee tumeamini na tumesadiki!

Na kwa kuwa vipengele ambavyo ndio nyenzo za kazi zilizotengenezwa na johari zake na misingi yake, inazunguka uso wa Ardhi na kugawanyika juu yake na kila sampuli kati ya sampuli za viumbe – zenye kubeba mihuri mbalimbali ya upweke – imesambaa katika uso wa Ardhi na kuenea kote, pamoja na kuwa kwake ni sampuli moja tu, hapana budi kuwa vipengele hivyo na vikusanywavyo vyake vyote na sampuli hizo na sehemu zake moja moja hakika ni mali ya mmoja na kazi zilizotengenezwa zenye kuamrisha na huyo mmoja mweza ambaye anaye tumia kwa uweza wake mkunjufu vipengele hivyo vikubwa vyenye kutawala kana kwamba ni wahudumu watiifu na kutiisha sampuli hizo zilizotawanyika kila upande wa Ardhi kana kwamba ni Askari wa kinidhamu.

Na kwa kuwa Risale-i Nur imethibitisha na kuweka wazi hakika hii, tunafupisha kwa ishara hii fupi.

Swahiba yetu mtalii msafiri alihisi uchangamfu wa kiimani baada ya kuwa amechuma ujazo wa kiimani na maonjo ya kitawhidi kutokana na kufahamu kwake hakika hizi tano. Akatunga hali ya kufasiri hisia zake na mambo aliyo yashuhudia  kwa kuusemesha moyo wake.

Tazama ukurasa wenye rangi wenye kupendeza wa kitabu cha ulimwengu mpana.

Namna ilivyopita kalamu ya uweza na namna Muumba alivyotia sura.

Haikubaki nukta yenye giza kwa wenye utambuzi.

Kana kwamba hasa Bwana mlezi ameandika aya zake kwa nuru.

Na ujue vilevile: Vitambo hivi visivyo na mipaka ni kurasa za kitabu cha ulimwengu.

Na zama hizi zisizohesabika ni misitari ya matukio ya dahari

Imepigwa katika ubao wa hakika iliyohifadhiwa

Kila kilichomo ulimwenguni ni lafudhi yenye mwili yenye hekima

Na kadhalika sikiliza:(lugha nyingine)

Yaani: Kila kitu kwenye uwepo kinatamka na kukariri kwa pamoja: Lailaha illa Allah, na dama kinanena kila wakati: Ewe Haki: Wote wanatamka na wote wanaongea kwa sauti: Ewe hai.

Naam,

Na katika kila kitu ni ishara kwake inajulisha kuwa yeye ni mmoja

Shairi la Abu Al-Atahiya katika Diwani yake. Na linanasibishwa kwa Ali karramallah wajhah. Na Ibn Kathir katika Tafsiri yake amelinasibisha kwa Ibn Al-Muutazz.

Na kama hivyo, moyo wa mtalii ulisadiki nafsi yake na vikasema vyote kwa pamoja: Naam, naam.

Hivi imekuja katika nyumba ya pili katika mlango wa pili katika cha kwanza ishara fupi katika aliyoyashuhudia mtalii wa ulimwengu na mgeni katika huo ulimwengu katika hakika tano za kitawhidi nazo:

[Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w) mmoja wa pekee ambaye juu ya upweke wake katika kupasa kuwepo kwake hakika ya kibriyaa na utukufu katika ukamilifu na kuzunguka na kadhalika kushuhudia hakika ya kuonekana kwa vitu kwa mawanda huru na bila ukomo hayafungwi na chochote isipokuwa utashi na hekima na kadhalika kushuhudia kwa hakika ya kupatisha vilivyopo kwa wingi wenye mawanda huru kwa na kwa kasi kabisa na kuumba viumbe kwa wepesi kabisa kwa uzuri kabisa na kutengeneza vilivyoundwa vyema kwa utoaji ulio wazi katika upeo wa utengenezaji mwema na ughali wa thamani na vilevile kushuhudia kwa hakika ya uwepo wa viliyokuwepo katika sura ya yote na ujumla na upamoja na ujumuishi na mwingiliano na kunasibiana. Na vilevile kushuhudia kwa hakika ya mipangilio ya jumla inayokana ushirika na kadhalika kushuhudia kwa umoja wa mizunguko ya uendeshaji wa viumbe yenye kujulisha umoja wa fundi wake kwa uwazi na kadhalika umoja wa majina na matendo vyenye kusarifu vyenye kuzunguka, na vilevile umoja wa vipengele na sampuli tofauti zenye kuenea na kutawala katika uso wa ardhi].

Wakati yule mtalii alipokuwa anatembea ulimwenguni katika zama alisadifu kukutana na shule ya mujaddid wa elfu ya pili imamu Ar-Rabbany Ahmad Al-Faruqi akaiingia na kaanza kuwa anasikiliza imamu alikuwa akisema ndani ya somo lake kuwa: “Hakika ya matokeo muhimu sana ya Tarika za kisufi zote ni kufunuka kwa hakika za kiimani kudhihirika kwake na hakika kuwa wazi kwa suala moja na kufunuka kwake ni bora zaidi kuliko karama elfu moja”.

Tazama: Imam ar-Rabbany, Al-Maktoubat. Al-maktoub 210.

Na vilevile alikuwa anasema: “Baadhi ya wakubwa walisema zamani: hakika atakuja mmoja ya wanafalsafa na katika wanazuoni wa falsafa na atathibitisha kwa dalili za kiakili uthibitisho wa wazi hakika zote za kiimani na za Kiislamu na laiti huyo mtu ningekuwa mimi na pengine ndiye mimi;

Wakati umethibitisha kwamba mtu huyo sio mtu wala mwanamume bali ni Risale-i Nur. Na huenda watu wa Kashfu wameshuhudia katika funuo zao Risale-i Nur katika haiba ya Mfasiri wake na mfikishaji wake ambaye hana thamani wala umuhimu wowote, wakasema: Hakika huyo ni Mtu (Mtunzi).

ambapo imani na Tawhidi ndio misingi ya makamilifu yote ya ubinadamu na johari yake na nuru yake na uhai wake, na kwamba kanuni (kufikiri saa moja ni heri kuliko ibada ya mwaka mmoja”

Tazama: Al-ghazzaly, Ihyau Uloum ad-Diin 4/423, Al-Qurtouby, Al-Jaamiu al-Ahkam al-Qur’an 4/314. Ali Al-Qaary , Al-Masnuu. Uk 82.

inahusu kufikiri kwa imani na dhikiri ya kificho si kingine katika Tarika ya Nakshabandi na umuhimu wake isipokuwa ni aina katika aina za kufikiri huku kutukufu)

Hivi ndivyo alivyokuwa imamu anafundisha na mtalii anasikiliza na kwa umakini wote kisha aliirejea nafsi yake na kuisemesha: alipokuwa imamu huyu akisema hivi na kwamba kuzidi kwa nguvu ya imani japo kwa kiasi cha Atomu ni kwa thamani sana kuliko tani za kuchuma elimu na makamilifu bali ni tamu na nzuri zaidi mara mia moja kuliko utamu wa vionjo na wijdi na kwa sababu mapingamizi na utata uliorundikana kuhusu imani na Qur’an – ambao wanafalsafa wa ulaya wanauibua tangu miaka elfu moja – imeingia katika nyoyo za waumini na wanawashambulia nazo watu waimani na wanajitahidi kwa kufanya hivyo kuteteresha nguzo za imani ambazo ni msingi wa furaha ya milele na mahali pa uhai wa kubakia milele na ufunguo wa pepo ya kudumu hivyo hapana budi –na kabla ya kila kitu – tuzidishe nguvu imani yetu na tuigeuze kutoka imani ya kuiga na kuwa imani ya kuhakikisha.

Ewe nafsi haya twende mbele pamoja na ngazi hizi za kiimani ishirini na tisa ambazo tumezikuta ambayo kila mojawapo ni imara kama mlima mkubwa tukikusudia kufikisha idadi ya dhikiri tasbihi zilizobarikiwa za swala nazo ni thelathini na tatu na tugonge mlango wa uongozi na kutunuku maisha wa kiungu katika ulimwengu wa walio hai ambao unabubujika mazingatio na mawaidha na tuufungue kwa ufunguo wa Bismillah Rahmanir Rahiim, ili tuone nyumba ya tatu na tushuhudie yaliomo ndani yake.

Mtalii akagonga mlango wa nyumba ya tatu ambao ni mkusanyiko wa maajabu na mageni aliugonga kwa huruma zote na upole na hapo akaufungua kwa (Bismillahi al fattah) ikadhihiri kwake nyumba ya pili na kaingia ndani na kakuta kuwa huko kuna hakika nne kuu zenye kuzunguka zinaangazia na zinafunua Tawhidi na n kuibainisha kama jua lenye kuchomoza

Hakika ya kwanza nayo ni hakika ya (Alfattaahiyya)

Yaani hakika ya kufunguka kisicho na mipaka katika sura zenye kupangika aina tofauti kwa kudhihiri kwa jina la (Al-Fattah) kutokana na mada rahisi sana na kufunuka kwake pamoja linadhihiri jina la (Al-Fattah) katika kila upande wa ulimwengu na katika wakati mmoja na kwa kitendo kimoja.

Naam, kama ilivyo uweza wenye kuumba umefungua viumbe mbalimbali visivyo na mipaka na katika mawanda ya vyenye kuwepo, kama kufunguka kwa maua ikatunuku (kwa jina la Al-Fattah) kila kimoja kati yao aina yenye mpangilio unao nasibiana na haiba ya pekee inayoitambulisha imetoa vilevile – kwa namna yenye muujiza zaidi – sura iliyopimwa, kupambwa na yenye kupambanuka, kwa kila chenye uhai katika mia nne elfu sampuli katika sampuli za bustani ya Ardhi na yo ikiwa katika upeo wa ufundi na hekima.

Naam hakika huku kufungua kwa sura ni dalili yenye nguvu sana ya Tawhidi, na muujiza wa ajabu sana wa uweza wa kiungu, kulingana na maana ipatikanayo katika Aya tukufu:

يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ذَلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّى تُصْرَفُونَ Qur’an, 39: 6.

إِنَّ اللّهَ لاَ يَخْفَىَ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الأَرْضِ وَلاَ فِي السَّمَاء هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاء لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ Qur’an, 3: 5-6.

Kwa msingi wa hekima hii, na kwa kuangalia kwa ujazo wa Risale-i Nur katika kubainisha hakika ya kufungua sura mbalimbali (na hasa katika ngazi ya sita na saba kutoka mlango wa kwanza wa Risala hii) tunahaulisha huko na hapa tunatosheka kwa kusema:

Imedhihiri matokeo ya tafiti mfululizo za kina kwa elimu mbili za mimea na wanyama na kwa ushahidi wake, kwamba huku kufungua sura katika kuzunguka na kuenea na ufundi kiasi kisichoyumkinika kumiliki kitendo hiki jumuishi chenye kuzunguka isipokuwa mmoja wa pekee mweza kabisa ambaye anaona kila kitu, na kukitengeneza, hii ni kwa kuwa hili  tendo la kufungua sura linahitajia ukomo wa hekima na ukomo wa umakini na komo wa kuzungukia ndani ya uweza kabisa unaotamalaki kila mahali na kila wakati, basi uweza kama huu haumiliki ila mmoja mpweke ambaye mikononi mwake kuna hatamu za Ardhi na mbingu.

Naam, kama ilivyokuja katika aya tukufu iliyotajwa

(فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ)

hakika kuumba mwanadamu na kufungua sura zake moja moja katika matumbo ya kinamama kwa mizani na mapambo na kwa mpangilio na upambanuzi bila kuchanganya au kuchanganyika au kosa au upungufu, kutokana na mada Rahisi ni dalili tosha ya Upweke. Na kwa hivyo kuzunguka kwa hakika hii – kufungua kwa sura na kuenea kwake kwa uweza huo huo, na hekima hiyo hiyo na ufundi huo huo kwa watu wote, na kwa wanyama wote na mimea yote katika pande zote za Ardhi hakika ni hoja yenye nguvu sana juu ya upweke na hii ni kwa sababu tendo la kuzunguka hilo kwa dhati yake ni umoja mmoja hauachi nafasi ya ushirikina.

Na kama ilivyo hakika kumi na tisa katika mlango wa kwanza imeshuhudia (kwa uwepo wake) juu ya kupasa kwa uwepo wa Muumba (s.w) pia inashuhudia (kwa kuzunguka kwake) juu ya umoja na upweke.

Na hakika ambayo swahiba yetu mtalii ameona  katika nyumba ya tatu ni:

HAKIKA YA PILI: NAYO NI HAKIKA YA (RAHMAANIYYA)

Nayo ina maanisha kuwa kuna mmoja ambaye ametujaalia Ardhi – kama ilivyo dhahiri mbele ya macho yetu – kuwa ni mahali pa zuri pa kufikia wageni na kujaza uso wake maelfu ya zawadi za rehema na kututandikia kwa rehema hizo karamu inayo kusanya mamia ya maelfu ya vyakula mbalimbali vitamu vilivyoandaliwa katika meza hiyo ametufanyia ndani ya Ardhi  – kwa rehema zake na hekima yake – ni hazina kubwa ya maelfu ya hisani zake na neema zake za thamani na anatulea kwa malezi ya ukomo wa huruma kwa kuibebesha Ardhi kutoka katika ulimwengu wa ghaibu katika mzunguko wake wa kila mwaka –kana kwamba ni meli ya Biashara – kwa mamia ya maelfu katika na nzuri mno ya aina za mahitaji muhimu ya kimaisha ya mwanadamu na kuzipeleka kila mwaka kana kwamba ni jahazi lililosheheni au gari moshi lililojazwa basi kila majira ya machipuo katika hiyo Ardhi ni mfano wa gari moshi linalobeba  Riziki zetu na mavazi yetu Na ili tunufaike kwa zawadi hizi na neema hizi zote ametupa mamia bali maelfu ya riziki na mahitaji na matakwa na hisia.

Naam, imekuwa wazi katika (Mwale wa nne) unaosherehesha aya tukufu:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ Qur’an, 3: 173.

na imethibitishwa huko ya kwamba yeye (s.w) ametupa tumbo la chakula kiasi kwamba tunaweza kwa tumbo hilo kusaga chakula vingi mno na kupata ladha yake. Na (s.w) ametufanyia vyema uhai kwa namna ambayo tunafaidika kwa milango yake ya fahamu neema nyingi bila mipaka imeenezwa pande za huu ulimwengu unaoshuhudiwa mkubwa kama vyombo vya neema vilivyo tandikwa na (s.w) ametukirimu kwa utu ambapo tunapata maonjo kwa zana zake nyingi – kama akili na moyo – katika zawadi zisizo na ukomo za ulimwengu wa maada na ulimwengu wa maana ambazo tunapata maonjo na ametufundisha uislamu kwa namna  ambayo unachukua nuru kutoka katika hazina zisizo na ukomo za ulimwengu wa ghaibu na ulimwengu wa kushuhudia na ametuongoza latika imani kwa namna tunafaidika nayo na kupata nuru kwa nuru zisizokadirika katika nuru za walimwengu wa dunia na Akhera na zawadi zake. kana kwamba hivi vyenye kuwa ni kasri kubwa imara limepambwa kutokea kwa rehema kunjufu kwa vitu vyenye thamani mno na kukabidhi mkono wa mwanadamu funguo za hazina zake na nyumba zake zisizohesabika na kumalizwa hesabu na kuweka amana katika maumbile yake mahitaji yote na hisia za lazima za kufaidika na kila kilichomo ndani ya Kasri.

Basi Rehema kama hii inazunguka Dunia na Akhera kwa pamoja na kwa kila kitu hapana budi kuwa ni udhihirisho katika midhihirisho (ya upweke) katika huo (Umoja) yaani kama ilivyo uzungukiaji wa mwanga wa jua na kuenea kwake vitu vyote vinavyolielekea ni mfano wa wazi juu ya (umoja) hakika kuchukua kila kitu angavu na king’aavu kulingana na uelekeo wake kwa mwanga wa jua na joto lake na rangi saba ambazo ndani yake kuna akisi zake ni mfano juu ya (Umoja) kwa hiyo ambaye anona mwanga wa jua unaofunika ulimwengu anahukumu kwamba jua la Ardhi ni moja, na kwamba kwa kushuhudia kwake kuakisi kwa mwanga wa jua lenye joto kutoka katika kila kitu chenye kutoa mwanga, hata katika matone anaweza kusema umoja wajua, yaani kuwa liko karibu na kila kitu kwa sifa zake lipo katika kioo cha moyo wakila kitu.

Sawa kabisa mambo yalivyo kama katika mfano huu (Aya) – hakika kufunika kwa Rehema za Mwingi wa Rehema mwenye uzuri kufunika kwa jumla kama mwanga kunadhihirisha upekee wa huyo Mwingi wa Rehema na kutokuwepo kwa mshirika wake kwa namna yoyote iwayo na kwamba kuwepo kwa midhihirisho ya nuru ya majina mengi zaidi ya huyo Mwingi wa Rehema, na aina ya udhihirisho wa dhati yake takatifu katika kila kitu.

Na hasa katika kila chenye uhai, na hasa katika mwanadamu – kwa kile ambacho Ar-Rahman amemtunuku chini ya sitara ya rehema zake kunjufu jumuishi kwa kila mmoja, kwa kiasi kinachomwezesha kuelekea nazo kwa viumbe vyote na nafuma mahusiano na mafungamano navyo – inathibitisha upweke wa huyo Ar-Rahman (s.w) na kuhudhuria kwake mbele ya kila kitu na kwamba yeye ndiye ambaye anafanya kila kitu kwa kitu chochote kiwacho.

Naam, kama ilivyo kuwa huyo Mwingi wa Rehema kwa umoja wa Rehema hiyo na kwa kufunika kwake inadhihiri haiba ya utukufu wake na kudhihiri kwake juu ya ulimwengu wote juu ya Ardhi yote hakika kwa kudhihiri kwa upweke wake katika kila chenye uhai na hasa kwa mwanadamu na kwa kusanya kwake vielelezo vyote vya neema hizo na kuvipandikiza katika viungo vya huyo kiumbe hai na katika zana zake na kupangilia kwake na kumfanya huyo mmoja kuchukua – kwa upande mmoja – viumbe wote  pasi na kutapanyika maskani yake kana kwamba anatangaza upole wa uzuri wake na kutambulisha kujikita sampuli za hisani yake kwa mwanadamu.

Mathalani tungechukua tikiti katika kila mbegu moja miongoni mwa nguzo zake kunapatikana tikiti lenyewe basi Muumba wa hiyo mbegu moja hapana budi kuwa yeye ndiye Muumba wa hilo tikiti kwani hunyonya kiini hicho kutokana na hilo tikiti na kuzikusanya na kuzifanya zipate umbo kwa vipimo vya ujuzi wake maalum na kanuni za hekima yake inayomhusu hakuna kitu katu, kinachoweza kutengeneza mbegu hiyo isipokuwa mtengenezaji mmoja wa tikiti hilo, bali hakika mwingine kuliumba tikiti hilo ni muhali na kwa msingi huu ulimwengu umekuwa – kwa udhirihirisho wa Rahmaniyya – ni mfano wa mti na Bustani na Ardhi imekuwa kama tunda na kama tikiti na wenye uhai na mwanadamu amekuwa kama mbegu kwa hiyo yatakikana Muumba wa kiumbe hai mdogo sana awe ndiye Muumba wa ardhi yote, na Bwana mlezi wa viumbe wa ulimwengu wote.

Muhtasari:

hakika kupatisha sura zote zilizopangika za vyote vilivyomo na kuzifungua kutokana na maada rahisi – kwa hakika ya Al-Fattahiyya ambayo ni yenye kufunika  inathibitisha umoja kwa uwazi na kwamba ulezi wa vyote vilivyo hai kama hivyo ambavyo vilivyokuja katika uwepo na kuingia uhai wa Dunia na hasa walio kuja ambao wageni – kwa hakika ya Rahmaniyya ambayo inafunika kila kitu – maelezo yaliyo katika ukomo wa mpangilio na kufikisha mahitaji muhimu ya maisha yake na kutosheleza pasipo kumsahau hata mmoja na kuenea kwa neema yenyewe na kufika kwake kwa kila mmoja kila mahali na kila wakati inadhihirisha umoja kwa uwazi na inaonesha upweke katika umoja huo vilevile.

Na kwa kuwa Risale-i Nur ni katika madhihirisho ya majina mawili ya (Al-Hakim) na (Ar-Rahmat) katika majina mazuri na kufafanua mazuri ya (Hakika ya rehema) na midhihirisho yake pamoja na uthibitisho wake imepatikana katika sehemu nyingi za Risale-i Nur. Kwa ajili hiyo hapa tumefupisha kwa kuiashiria kwa tone hili kutoka katika bahari hiyo pana.

Na alichokiona swahiba yetu mtalii katika nyumba ya tatu ni: 

HAKIKA YA TATU: NAYO NI HAKIKA YA (TADBIRI NA UONGOZI)

Yaani hakika ya kuendesha madude ya mbinguni nayo yana kasi sana na makubwa sana na kuendesha vipengele na hali vikiwa katika mchanganyiko na mwingiliano sana na kuendesha viumbe vya Ardhini na hali yakuwa viko katika ukomo wa uhitaji na udhaifu uendeshaji wenye sifa ya ukamilifu wa mpangilio na mizani na baadhi yake inafanya jitihada kusaidia nyingine pamoja na kuchanganyika sana yaani ni hakika ya kuangalia katika uendeshaji wa mambo yake yote na kuufanya ulimwengu huu mkubwa kana kwamba ni ufalme kamili na mji wa kupendeza mkubwa na kasri ndefu yenye kupambwa. 

Hapa tutachukua sura moja yenye kukusanya mwenendo wa uendeshaji huo katika ukurasa mmoja wa uso wa Ardhi na katika waraka mmoja katika majira ya machipuo hali ya kuacha duru zile kubwa za kijabari na kurasa pana ambazo zinatona Rehema kwa kuangalia kwamba zimefafanuliwa na kuthibitishwa katika Risala muhimu za Risale-i Nur kama (Neno la kumi) na tutalibainisha kwa mifano kama ifuatavyo:

Ikiwa mtu mkubwa mwenye kufurutu ada ataunda jeshi kutokana na mataifa mia nne elfu na makundi mbalimbali na kutimiza yanayomhusu kila askari katika mataifa na makundi hayo mbalimbali ikiwemo mavazi silaha chakula mafunzo misamaha  na huduma mbalimbali kwa sampuli tofauti sana, na kuwaandaa kwa zana mbalimbali pasipo kuwa na uchache wa nakisi au kasoro au kosa na kuwapa vitu hivyo kwa wakati wake bila ya kuwepo japo kwa uchache ucheleweshaji au kuchanganya na kwa ukamilifu wa mpangilio hapana budi kwamba uongozi uendeshaji huo – na hali ya kuwa uko katika upana sana na kuchanganyika sana umakini na mizani wingi na uadilifu – sio vingine isipokuwa ni kutokana na uweza wenye kufurutu ada wa mweza mwenye kufurutu ada, haiyumkiniki kwa sababu yoyote kunyooshea mkono wake hayo kwani angenyoosha basi angeharibu mizani hiyo na mambo yangechanganyika.

Kama yalivyo mambo katika mfano, huu kama hivi, hakika tunashuhudia kwa macho yetu vilevile kwamba mkono wa ghaibu unaanzisha kila majira ya machipuo na inaendesha jeshi la kuogofya lenye kuundwa kutokana na mia nne elfu kutokana na aina mbalimbali ya vilivyo hai kisha katika majira ya mapukutiko ambayo ni kielelezo cha kiama – husamehewa mia tatu elfu katika jumla ya mia nne elfu kutokana na majukumu yao kwa sura ya kutoweka na kwa jina la umauti. Na katika majira ya machipuo – ambayo ni mfano wa ufufuo –huanzisha vielelezo mia tatu elfu vya ufufuo mkuu katika wiki chache kwa ukamilifu wa mpangilio. hata kwamba (s.w) baada ya kutuonesha katia mti mmoja aina nne ya ufufuo mdogo kwa kuufufua mti huo huo na majani yake na  maua yake na matunda yake – kama ilivyokuwa katika majira ya machipuo yaliyopita inatudhihirishia na kututhibitishia umoja na upekee wake na uweza wake mpana na Rehema yake kunjufu ndani ya ukamilifu wa Rububiyya na utawala na hekima (s.w) analiandika jambo hili la tawhidi kwa kalamu ya Kadari katika waraka wa kila majira ya machipuo juu ya uso wa Ardhi, na hii ni kwa kule kutunuku kwake kila aina nakila kundi katika jeshi hilo la kiungu subhana ambalo sampuli zake zinafikia mia nne elfu yanayolihusu katika riziki mbalimbali na silaha mbalimbali za kiulinzi linazozihitaji mavazi yanayonasibiana nalo na mafunzo yanayowiana nalo na misamaha yake mbalimbali na yanayoafikiana nalo katika zana zake na mahitaji yake yote (s.w) anatoa yote hayo kwa ukamilifu wa mpangilio bila hata kidogo kusahau au kukosea na bila kuchanganya na kuitunuku kwa wakati wake maalum uliopangwa kuokana na vyanzo havifikiriki na akili yeyote.

Swahiba yetu mtali baada ya kupitia ukurasa waraka mmoja tu katika majira ya machipuo moja na kuona jambo la tawhidi humo kwa uwazi alisemesha nafsi yake na kusema

Hakika ambaye aliyeanzisha aina hizi za ufufuo katika kila majira ya machipuo, ambazo zinavuka maelfu na kuzidi ajabu ya ufufuo mkuu ndiye ambaye amewaahidi manabii wake wote kwa maelfu ya ahadi kuwa ataleta ufufuo na kiama kwa ajili ya thawabu na adhabu na hilo ni rahisi zaidi kwa uweza wake kuliko machipuo yenyewe na ameingiza maelfu ya ishara katika Qur’an tukufu kuhusu ufufuo ambayo inathibitisha kwa uwazi katika aya elfu moja miongoni mwa aya zake tukufu, juu ya ahadi zake na makamio yake (s.w) hapana shaka kwamba adhabu ya Jahannam ndio hasa uadilifu wenyewe kwa haki ya yule anayetenda kosa la kupinga ufufuo mbele ya huyo mweza jabari mteza nguvu mwenye utukufu.

Na kama hivi swahiba yetu mtalii alihukumu na nafsi yake ikatulia ikarudia tena kusema: tumeamini alichokishuhudia mtalii katika nyumba ya tatu ni:

HAKIKA YA NNE : NAYO NI NGAZI YA THELATHINI NA TATU AMBAYO NI HAKIKA YA (AL RAHIIMIYYA NA  AL RAZZAQIYYA)

Yaani hakika ya kutoa riziki kwa wote wenye uhai na hasa wenye roho na hasa wenye kushindwa na walio dhaifu na hasa watoto wadogo katika uso wote wa Ardhi na ndani yake na kwenye anga lake na baharini mwake na kwapa riziki zao wote – sawa iwe ni za kimaada za kitumbo katika hizo auza kimaanawy za kimoyo na kwa huruma na upole wote na hii ni kutokana na vyakula vinavyofanywa kutoka katika udongo rahisi mkavu na kutokana na vipande vikavu vya vigogo vigumu kama mifupa na hasa kwa kutoa vyakula laini kabisa ya hivyo kutoka katikati ya kinyesi na dau na kutoa viwango vikubwa vya vyakula kutokana na mbegu moja ngumu kama mfupa na hali yakuwa haina uzani hata wa dirhamu moja, basi kutoa hayo yote katika wakati wake munasibu na mbele ya macho yetu utoaji wa kiufundi  bila kusahau hata kimoja kuchanganya au kukosea hasa ni hakika ya kuwa riziki ni kutoka katika mkono wa ghaibu. Naam hakika aya tukufu:

إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ Qur’an, 51: 58.

ambayo inahusisha kutoa maisha na chakula na kufunga kwa Mwenyezi mungu (s.w) na pia aya tukufu:

وَمَا مِن دَآبَةٍ فِي الأَرْضِ إِلَّا عَلَي للهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلّ فِي كِتَابٍ مُبِيْنٍ Qur’an, 11: 6.

ambayo inajumuisha riziki za watu na wanyama wote chini ya ahadi na dhamana ya Mola Mlezi (s.w) na pia ya tukufu:

 وَكَأَيِّن مِن دَابَّةٍ لَا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ Qur’an, 29: 60.

ambayo inathibitisha na kutangaza kwamba Allah (s.w) ndiye ambaye anadhamini – na kama inavyo shuhudiwa – riziki za masikini na wanyonge, na wenye kushindwa na mifano ya hao katika wasioweza kuifikia, anawapelekea kwao kwa namna wasiyoitegemea, na kutokana na vyanzo visivyopita katika mawazo yao kabisa, bali ni kutokea ghaibu, bali kutokana na pasipo na kitu chochote, kama mfano wa wadudu waliomo vina virefu vya bahari ambavyo hula kutokana na pasipo na kitu na watoto wote wachanga ambao riziki zao huwajia kutoka upande usiotegemewa na wanyama wote ambao Allah (s.w) amedhamini riziki zao anawaruzuku hasa kimatendo kutokea ghaibu moja kwa moja kama inavyoshuhudiwa kila majira ya machipuo – hata kwamba yeye ndiye ambaye anatuma riziki za hao wenye kufitinishwa na sababu chini ya pazia ya sababu, hawaruzuku hao asiyekuwa yeye. Na kama zilivyo hizo aya tukufu na matukio yanayoshuhudiwa inaonekana hali ya uruzuku na inaithibitisha na kuitangaza kama hivi, pia zinabainisha aya nyingi za Qur’an na shuhuda za kilimwengu nyingi mno zikiafikiana kwamba kila chenye uhai kinalelewa ndani ya uangalizi wa hali ya urehemevu wa mruzuku mmoja mpweke mtukufu.

Naam, hakika kuharakisha kwa riziki za mimea kuziendea – na hali yakuwa ni yenye kuhitajia  riziki  – bila ya kuwa na uwezo wowote wala hiari wala utashi na hali imetulia mahali pake ni yenye kumtegemea Allah (s.w) pia kumiminika kwa maziwa safi katika mabomba hayo ya ajabu kwenda katika vinywa vya watoto wachanga wanyonge na kukatika kwa ulishaji huo mara tu baada ya kupata uwezo kiasi na kiasi cha hiari na utashi pamoja nakuendelea huruma ile iliyotolewa kwa kina mama yote hayo yanathibitisha kwa uwazi kwamba riziki ya halali haiji kwa kulinga na uwezo na utashi bali inakuja kwa kulingana na udhaifu na kushindwa ambazo huleta kutegemea.

Uwepo wa nguvu ya uwezo hiari na busara vimeleta  – vyenye kuchochea pupa inayopelekea aghlabu katika kuzuiliwa, hao wanafasihi ambao wamepata hisia kwayo, kuelekea katika kujidhalilisha bali katika ombaomba wakati ambapo kutokuwa na uwezo kulikopambwa kwa kutegemea aghlabu ya watu wa kawaida wapumbavu katika utajiri hata ikapita methali:

Wanazuoni wangapi wanazuoni nyendo zimewachosha nyendo zao na mjinga unamkuta mwenye kuruzukiwa.

Na katika Tabaqatul shuaraa.1/131 Cha Ibn al Mu’tazz: ananasibisha kwa Yaaquti El Himawy na Abi Hiyyan Tawhidiy na kiasi kidogo cha hitilafu:

Basi mwenye akili mtambuzi nyendo zake zimechoka

Na mjinga aliyeharibikiwa unamkuta ameruzukiwa.

Katika yanayothibitisha kuwa riziki ya halali kiumbe haipati kwa nguvu ya uwezo na hiari bali hupewa kutokana na Rehema iliyokubali jitihada zake, na anapewa hisani kutokana na huruma na upole imehurumia uhitaji wake isipokuwa riziki ni aina mbili:

Kwanza:

Riziki ya hakika ya kimaumbile ya maisha, ambayo ipo chini ya uangalizi wa mola mlezi nayo imekadiriwa kwa namna ambayo iliyohifadhiwa mwilini kwa sura ya mafuta au kwa sura nyingine inaweza kumpa maisha mwanadamu na kudumisha uhai wake zaidi ya siku ishirini bila ya kuonja chakula. Basi wale wanaokufa njaa kwa dhahiri kabla ya siku ishirini au thelathini bila yakumalizika riziki yao ya kimaumbile kifo chao hakitokani na kukosekana kwa riziki bali ni kutokana na maradhi yanayo sababishwa na mazowea mabaya na kutokana na kuacha kawaida.

Sehemu ya pili ya riziki:

Ni riziki ya kimajazi na kufanyisha ambayo inakuwa kwa hukumu ya dharura baada ya kuwa mwanadamu ameibobea kwa mazowea na ubadhirifu na matumizi mabaya na sehemu hizi sio ndani ya udhamini wa kiungu bali inafuatia hisani yake (s.w) ima aitoe au aizuie.

Mwenye kufaulu – katika riziki hii ya pili – na mwenye bahati katika hiyo ni yule mwenye kujua kwamba jitihada za halali kwa kufanya uchumi na ukinaifu – na hizo ni nyanja za furaha na ladha – hiyo ni aina ya ibada nayo ni dua ya kimatendo ya kuchuma riziki kwa hiyo huyu mwenye kufaulu natumia maisha yake kwa furaha na nakubali hisani hiyo kwa shukurani na furaha.

Na mwenye kuharibikiwa katika riziki hii ni yule mwenye kuacha jitihada za halali kwa ubadhirifu na pupa – na mawili hayo ni sababu ya ubaya hasara na maumivu – hutumia uhai wake bali kuteketeza kwa kugonga kila mlango kwa uvivu kuhisi kudhulumiwa na malalamiko. Kama ambavyo tumbo hutafuta riziki, moyo roho akili jicho sikio kinywa na viungo kama hivyo katika vipole vya mwanadamu na hisia zake nyingine hutafuta riziki zake kutoka kwa Mtoa riziki Mwingi wa Rehema na huzichukua kwake kwa shukurani zote Allah (s.w) huzipa kila moja kati ya hizo kutoka katika hazina za Rehema zake riziki zake ambazo zina nasibiana nazo kuziridhia na kupata ladha mbali hakika ya Mtoa riziki Mwingi wa Rehema ameumba kila moja katika hivyo vipawa kama jicho sikio moyo hayali akili na mifano yake ni sawa na ufunguo wa hazina za johari za thamani za uzuri zinazokunjuka katika uso wa viumbe viungo vingine ni kama hivyo kila moja kati yake ni ufunguo wa ulimwengu maalum hufaidika kwa imani kwa kila hali basi na turejee katika asili ya maudhui.

Kama ilivyo kwamba Muumba Mweza Mwingi wa hekima ameumba uhai ni muhtasari jumuishi uliofupishwa kutokana na viumbe hukusanywa ndani yake makusudio yake ya jumla na midhihirisho ya majina yake, vilevile amejaalia riziki katika ulimwengu wa uhai ni kituo jumuishi ya kiungu hali ya kuwa ameumba kwa wenye uhai maumbile ya kutamani na kuonja riziki kwa ajili hiyo ifungue nafasi kwa ajili ya lengo muhimu kabisa la kumbwa viumbe na hekima yake nalo ni kujaalia bei ni katika shukurani na ridhaa za kudumu na za jumla zinazotimia kwa nyenyekevu na utumishi wote mbele ya Ulezi wake na upendo wake (s.w).

Mathalani:

Hakika (s.w) ameimarisha kila upande katika pande za ufalme wa kiungu mpana sana, akajaza mbingu kwa malaika na vyenye roho na kujaza ulimwengu wa ghaibu kwa roho kama alivyojaza ulimwengu wa kimaada – kwa hekima ya kueneza roho na kuingiza furaha ndani yake na hasa ulimwengu wa hewa na Ardhi bali katika kila upande na katika kila wakati kwa kuwepo kwa walio hai – na hasa ndege na virukavyo na vidudu akapandikiza mahitaji ya riziki na kuionja kwa wanyama na mwanadamu, na kuwafanya wanajitahidi daima kufuatia riziki zao kana kwamba uhitaji huo ni kichocheo cha kutia shauku kwao kinawaongoza na kuwapa mchakato na kuwaendesha kuifuatia riziki hali ya kuwaondoa kutoka katika uvivu na kubweteka na hilo si lolote isipokuwa ni hekima katika hekima za mambo ya kiungu Bwana Mlezi Na kama zingekuwa mfano hekima kama hizi katika hekima muhimu Allah (s.w) angekuwa ainisho zilizowekewa kanuni kwa wanyama zinaziendea bila bidii na tabu na kwa uhitaji wa kimaumbile kama alivyojaalia riziki za mimea zinaiendea kama hivi.

Lau lingekuwepo jicho linaloweza kuona aina za uzuri za jina (Ar-Rahiim) na pande uzuri za jina la (Ar-Razzaq) na ushahidi wa majina hayo kwa umoja uoni timamu kiasi inayumkinika kufunika kwa ujumla uso wa Ardhi na kuushuhudia kwa wakati mmoja, lingekuwa linaona kiasi cha starehe ya uzuri na kiasi cha utamu wa uzuri katika kudhihiri kwa huruma ya (Ar-Razzaq Ar-Rahiim) na upole wake ambao unatoa msaada kwa ghaibu na kufanya uzuri kwa hisani ya kirahmani misafara ya wanyama ambayo imekaribia kwisha riziki zake mwishoni mwa majira ya baridi kwa vyakula na neema katika ukomo wa ladha na ukomao wa wingi na ukomo wa aina mbalimbali kwa kuzikabidhi katika mikono ya mimea na kuwekwa kwenye miti na kuning’inizwa kwenye chuchu za kina mama na kupelekewa kutoka kwenye hazina za rehema ya ghaibu tupu na hapo utajua kuwa yule ambaye anatengeneza tufaha moja mathalani –na kuitoa ikiwa ni riziki ya hakika hali ya kumneemeshea mtu, haiyumkiniki isipokuwa yule ambaye anayeendesha misimu yote usiku na mchana na kujaalia tufe la Dunia kama jahazi la kibiashara inazisafirisha na kuipeleka hali ya kukusanya mazao ya misimu na kuleta kwa wageni wake wahitaji Ardhi hini. Kwa sababu muhuri wa maumbile na hekima na alama ya kiungu Mtegemewa na kila kitu na muhuri wa Rehema iliyopo katika paji la hilo tufaha la Ardhi yote na juu ya baki ya matunda na mimea na wanyama wote kwa hiyo mmiliki wa tufaha hilo moja na mtengenezaji wake wa hakika ndiye mmiliki na mtengenezaji wa mifano yake na yanayorandana na jinsi yake ya wakazi wa Ardhi, naye ndiye mmiliki na Mtengenezaji wa Ardhi kubwa ambayo ni bustani yake, naye ndiye Muumba wa mti wa viumbe ambao ndio kiwanda chake na ambaye ni mwenye kupatisha msimu wake ambao ndio maabara yake Naye ni mpelekaji wa majira ya machipuo na majira ya joto ambayo ni medani ya malezi yake na makuzi yake, huyo basi ni mmiliki Mwenye utukufu na Muumba Mwenye uzuri, hana mshirika na hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye.

Kila tunda kwa hiyo ni muhuri mzuri sana uliokuwa wazi wa umoja, kwa kiasi unamjulisha mwandishi na fundi wa mti wake nayo ni Ardhi, na unamjulisha mwandishi na muumba wa bustani yake nacho ni kitabu cha ulimwengu na kudhihirisha umoja wake (s.w) na kuashiria kwamba jambo la upweke limepigwa muhuri kwa muhuri wa uthibitisho mwingi kwa idadi ya matunda.

Na kwa kuwa Risale-i Nur ni mdhihirisho wa majina mawili ya (Ar-Rahiim na Al-Hakiim) katika majina mazuri na kwa ajili ya kuthibitisha ming’aro mingi ya hakika ya Rahiimiyya na siri zake nyingi katika sehemu kadhaa miongoni mwa sehemu za Risale-i Nur tunahaulisha kwenda huko naweza kutosheka kwa ishara hiifupi katika hazina hiyo tajiri kubwa kwa kuangalia hali yangu isiyowiana.

Kama hivi swahiba wetu mtalii anasema: Alhamdulillah ambaye ameniwafikisha nisikilize hakika thelathini na tatu ambazo zinashuhudia uwepo wa Muumba wangu na mmiliki wangu na juu ya umoja wake na ambaye nimekuwa nikimtafuta kila mahali na ninamuuliza kila kitu hakika zile ambazo kila moja kati ya hizo ni mazingatio ya jua lenye kuchomoza linaloteketeza giza lote na kila moja kati ya hizo ina nguvu ya mlima uliosimama madhubuti na kila moja kati ya hizo kwa thibitisho zake inashuhudia kwa upeo wa uwazi juu ya uwepo wake (s.w) zinajulisha kwa kufunika kwake katika upeo wa uwazi juu ya upweke wake, na kuthibitisha kupitia hakika hizo nguzo nyingine za imani kwa uthibitisho wa nguvu hakika makubaliano a pamoja na kuafikiana kwa hakika zote yamebadilisha imani zetu kutoka katika kuiga na kuwa katika kuhakikisha na kutoka katika kuhakikisha na kwenda katika elimu ya yakinia na kutoka katika elimu ya yakini na kuwa katika kuona kwa yakini na kutoka katika kuona kwa yakini kwenda katika haki ya yakini basi Al-hamdulillah hii ni katika fadhila za Mola wangu Mlezi.

وَقَالُواْ الْحَمْدُ لِلّهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلا أَنْ هَدَانَا اللّهُ لَقَدْ جَاءتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ Qur’an, 7: 43.

Hivi, na imekuja katika mlango wa pili katika kituo cha awali ishara fupi kabisa ya Nuru za kiimani ambazo amezipata huyu mtalii mtafiti mwenye shauku na katika shuhuda zake katika nyumba ya tatu ya hakika nne tukufu.

[Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w) mmoja wa pekee ambaye juu ya upweke wake katika kupasa uwepo wake kumejulisha kushuhudia kwa utukufu wenye kufunika wa hakika ya hali ya ufunguzi kwa kufungua sura kwa mia nne elfu ya aina za wenye uhai zilizokamilishwa bila mapungufu kwa ushahidi wa sanaa ya mimea na wanyama na kadhalika kushuhudia kwa utukufu wa kufunika kwa hakika ya Ar-Rahmaaniyya pana yenye kupangika bila kupungua  kwa kushuhudia na kuona kwa macho na kadhalika kushuhudia kwa utukufu wa uendeshaji wenye kufunika kwa wenye uhai wote na wenye kupangika bila ya kosa wala upungufu. Na kadhalika kushuhudia utukufu wa kufunika kwa hakika ya Ar-Rahiimiyya na utoaji maisha wenye kuenea kwa kila wenye kuruzukiwa wenye kuwekewa kanuni kwa kila wakati wa uhitaji bila kupitiwa wala kusahau ametukuka sana mruzuku wake Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu mpole mneemeshaji na imeenea kupatikana kwake na hisani yake imejumuisha na hapana mola wa haki ila yeye].

سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَناَ إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنْتَ العَلِيْمُ الحَكِيْمُ

يَا رَبِّ بحَقِّ بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْم

يَا الله يَا رَحْمنُ يَارَحِيْمُ

صَلِّ وَسَلَّم عَلَي سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ وَعَلَي آلِهِ وَأَصْحَابِه أَجْمَعِيْن بِعَدَدِ جَمِيْعِ حُرُوْفِ رَسَائِلِ النُّوْرِ المضْرُوْبَةِ تِلْكَ الحُرُوْف فِي عَاشِرَاتِ دَقَائِقِ جَمِيْعِ عُمْرِنَافِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ مَعَ ضَرْبِ مَجْمُوْعِهَا فِي ذَرَّاتِ وَجُوْدِيّ فِي مُدَّةِ حَيَاتِي وَاغْفِرْ لِي وَلِمَنْ يُعِيْنُنِي فِي نَشْرِ رَسَائِلِ النُّوْرِ وَكِتَابَتِهَا بِصَدَاقَةِ، بِكُلِّ صَلَاةٍ مِنْهَا وَلِآبَائِنَا وَلِسَادَاتِنَا وَشُيُوْخِنَا وَلِأَخَوَاتِنَا وَإِخْوَانِنَا وَلِطَلَبَةِ رَسَائِلِ النُّوْرِ الصَّادِقِيْنَ وَبِالَخاصَةِ لِمَنْ يَكْتُبُ وَيَسْتَنْسِخُ هذِهِ الرِّسَالَةَ

بِرَحْمَتِكَ يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِيْنَ.. آمِيْن.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.