MWALE WA SABA Ishara Kuu

Tanbihi muhimu na ufafanuzi:

Pamoja na umuhimu wa risala hii na ukubwa wa hali yake, sio kila mtu anafahamu, kila suala katika masuala yake, lakini habaki bila ya kupata sehemu kati ya hilo. Ambaye anaingia katika bustani kubwa na mkono wake haufikii katika matunda yake yote, basi inamtosha kile alichopata katika bustani hiyo; kwani hiyo bustani haikufanywa kwa ajili yake pekee, bali wenye mikono mirefu nao wana hisa na fungu lao pia.

Na kuna sababu tano zinazokwaza kuifahamu risala hii:

Ya kwanza:

Ni kwamba mimi niliandika niliyoyaona kama yalivyoonekana kwangu kwa mujibu wa ufahamu wangu, niliyaandika kwa ajili yangu mwenyewe, kwa hiyo haikuandikwa kama zilivyo risala nyingine kwa kiwango cha ufahamu wa wengine.

Ya pili:

Hakika tawhidi ya kiukweli imeandikwa katika sura yake kuu kwa baraka ya kudhihiri kwa (Jina kuu la Allah (s.w)), masuala yake yakawa kunjufu sana, na ya kina sana, na marefu sana, kwa hiyo sio kila mtu ataweza kuyafahamu moja kwa moja na kwa mara ya kwanza.

Ya tatu:

Kila suala katika masuala yake lenyewe ni hakika kubwa ndefu, – na kwa kuhifadhi umoja wa hakika na kutoigawa – yaweza kuwa ukurasa mmoja ni sentensi moja iliyorefushwa, kuna vitangulizi vingi huletwa kwa nafasi ya dalili moja tu.

Ya Nne:

Kila suala – katika mengi ya masuala ambayo risala hii inayaelezea – yana dalili zake nyingi, na hoja zake chungu nzima, wakati wa kukusanya dalili kumi au mara nyingine ishirini kwa kuelezea hoja moja suala huwa refu, wenye uelewa mfupi hawataweza kuelewa.

Ya tano:

Nimekutana na nuru za risala hii kwa neema za mwezi wa Ramadhani mtukufu na baraka zake, isipokuwa imeandikwa kwa haraka, na nimetosheka na mswada wa kwanza kutokana na maradhi yaliyokuwa yakinisumbua na tabu za dhiki kutoka pande mbalimbali, na nilikuwa nikihisi wakati nikiiandika kuwa inapita moyoni bila ya hiari yangu, wala kutaka kwangu. Sikuona kuwa inafaa kuigusa kwa chochote katika mpangilio au marekebisho kulingana na kufikiri kwangu; kwa ajili hiyo risala hii imechukua umbo hili, ambalo linakuwa ni ngumu kuifahamu, ukiachilia mbali kile kilichoongezwa katika vifungu vya kituo cha kwanza kilichoandikwa katika lugha ya Kiarabu.

Lakini, pamoja na sababu hizi tano ambazo ndio palipo na upungufu na ugumu, risala ni yenye umuhimu mkubwa.

Basi risala hii ni hakika katika hakika za (Ishara kuu) na ni tafsiri yake, ni mwale wa saba na hoja ya kiimani ya kwanza katika (Mkusanyiko wa fimbo ya Musa).

Mwale huu unaundika kutokana na vituo viwili, pamoja na utangulizi unaofafanua masuala manne muhimu:

Kituo cha kwanza:

Kinabainisha kwa lugha ya Kiarabu, tafsiri ya Al-Ayatul kubra.

Na kituo cha pili:

Kinabainisha hoja za kituo cha kwanza na kuzifafanua kwa uwazi na kuzithibitisha.

Hakika urefu wa utangulizi ufuatao, na ufafanuzi wake unaokunjuka, ulikuwa bila ya hiari yangu, hivyo kuna haja ya mimi kupewa imla kama hivyo, na baadhi huenda wakaona kuwa urefu wake ndio ufupi. 

Saidi Nursi

Tumeweka vifungu vilivyokuja kwa lugha ya Kiarabu katika maelezo vikiwa vimefungiwa kati ya mabano .

UTANGULIZI

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ Qur’an, 51:56.

Inafahamika kutokana na siri za aya hii tukufu: Hakika hekima ya kuja kwa mwanadamu katika dunia hii na lengo lake ni kumjua Muumba wa ulimwengu (s.w), na kumwamini na kumwabudu. Kama ilivyo kazi ya maumbile yake na faradhi ya dhima yake ni kumjua Allah (s.w), na kumwamini na kusadiki uwepo wake na upweke wake kwa kunyenyekea na kwa yakini.

Naam, hakika ya mwanadamu aliye dhaifu ambaye anatamani, – kimaumbile – uhai wa kudumu milele na maisha ya milele yenye furaha na ambaye ana matumaini pasi na mipaka na maumivu pasi na ukomo, hapana budi kuwa vitu vyote na kamilifu zote ni zenye kudondoka duni kulingana na yeye, bali nyingi zake hazina thamani yoyote ya kutajwa, isipokuwa imani ya kumwamini Allah (s.w) na kumjua, na isipokuwa njia na nyenzo ambazo zina mshika mkono kwenda katika imani hiyo ambayo ni msingi wa msingi wa huo uhai wa milele na ni ufunguo wake.

Na ilipokuwa Risale-i Nur imethibitisha hakika hii kwa ufasaha sana na hoja za kukata shauri tunarejesha huko, tukibainisha hapa shida mbili ambazo huteteresha ile yakini ya kiimani katika enzi hizi, na kupelekea katika kutahayari na kutaradadi, na hiyo ni ndani ya masuala manne:

Shida ya kwanza na njia ya kuokoka nayo ni masuala mawili:

Suala la kwanza:

Kama ilivyothibitishwa katika (Mng’ao wa kumi na tatu) kutoka katika (Andiko la thelathini na moja) kwa upambanuzi ni kwamba: (Hakuna umuhimu wa kukanusha katika masuala ya jumla mbele ya kuthibitisha, kwani hukumu yake ni dhaifu sana).

Mfano wa hilo:

Ikiwa mashahidi wawili wamethibitisha kati ya watu wa kawaida kuuona mwezi mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani na maelfu ya watu wakakanusha kuuona kati ya watu wenye hadhi kubwa na wanazuoni kwa kusema: (Hakika sisi hatujauona mwezi), huku kukanusha kwao kunabaki kuwa hakuna thamani au umuhimu; hii ni kwa sababu kwa (Kuthibitisha) mtu humuimarisha mwingine na kumtia nguvu, na kuna kuegemeana na kukusanyika, wakati ambapo (Kukanusha) hakuna tofauti iwe kunatoka kwa mtu mmoja au kwa watu elfu moja; kwa kuwa mkanushaji yupo peke yake kwa kuzingatia kuwa yeye peke yake ndiye ambaye anakanusha. Hii ni kwa sababu mthibitishaji anaangalia jambo lenyewe kisha hutoa hukumu yake kama ilivyo hali katika mfano wetu, mmoja wao akisema: Ule pale mwezi mbinguni, mwingine humsadiki na kumuunga mkono kwa kuonesha mahali palepale, hivyo hushirikiana kuangalia sehemu ileile husaidiana na hukumu yao hupata nguvu na kujikita. Ama katika kukanusha na kukataa mkanushaji hatazami jambo lenyewe lile na hawezi kufanya hivyo, kwa hiyo kanuni imekuwa: (Haiwezekani kuthibitisha kukanusha kusiko maalumu na kusiko ainishwa mahali pake) kanuni mashuhuri.

Mfano wa hilo:

Nikikuthibitishia kuwepo kwa kitu maalumu duniani na wewe ukakanusha kuwepo kwake duniani, hapo itakupasa ufanye utafiti na kuhakikisha pande zote za dunia ili uthibitishe kutokuwepo kwa hicho kitu, ambacho ninaweza kwa nafsi yangu kuthibitisha kwa ukomo wa wepesi na kwa ishara rahisi tu kukielekea. Bali ni juu yako kuzama mbizi vilevile katika vina vya nyakati zilizo pita kale, hata uweze kusema: (Hakipo kwa hakika, halikutokea tukio kama hili!).

Na ilivyokuwa wakanushaji na wakataaji hawatazami jambo lenyewe kwa dhati yake, bali wanatoa hukumu zao kulingana na nafsi zao na akili zao na mitazamo yao, kwa hiyo haiwezekani kuegemeana na kuwa ni wasaidizi wao kwa wao, hii ni kwa kuwa pazia za kuona ni nyingi kwao na sababu zinazozuia kujua ni nyingi kwao, ambapo anaweza kila mtu kusema: (Mimi sikioni kitu fulani) na (Kwangu mimi kitu hicho hakipo) (Kwa itikadi yangu kitu hicho hakipo) lakini hawezi kusema: (Hakika kitu hicho kwa hakika hakipo) na atakapo sema kwa kukanusha huku – na hasa katika masuala ya kiimani ambayo yanakusanya ulimwengu wote – basi maneno yake yatakuwa ni uzushi mkubwa na uongo mkubwa sawa na ukubwa wa dunia, na kamwe hautokuwa ukweli na haiwezekani kuwekwa katika kusibu au kunyooka kamwe.

Ufupi wa hayo yaliyotangulia:

Hakika matokeo katika kuthibitisha ni mamoja, na kwamba kuna kuegemeana, na katika kukanusha matokeo siyo mamoja bali ni mengi, kwani masharti: (Kwangu), (Kwa mtazamo wangu), (Kwa itikadi yangu) na mifano ya hizo katika jumla ya sababu ambazo zinazuia kuona kwa usahihi huwa nyingi na hutofautiana kwa kutofautiana kwa watu, kwa hiyo matokeo yanakuja kuwa mengi vilevile na tofauti, basi kuegemeana hakutokei kamwe.

Na kama hivi kwa mintarafu ya hakika hii: Hakuna thamani au umuhimu, katika wingi unaoonekana wa makafiri, na wakanushaji ambao wanazuilia imani, lakini, katika wakati ambao haitakikani kuathirika yakini ya muumini na isichafuliwe imani yake kwa sampuli yoyote katika sampuli za shaka na kutaradadi, tunaona wanayoyachokoza wanafalsafa wa kimagharibi katika utata na upingaji katika enzi hizi yameleta tahayari kwa baadhi ya wenye majanga waliofitiniwa nao, yakaondoa yakini yao na kuteketeza furaha yao ya milele, na kuwaingiza katika mateso na kuharibikiwa, hiyo ni kwa sababu kukanusha kwao huku kumebadilisha maana ya (Umauti) ambao unawasibu kwa kila siku watu thelathini elfu kutokana na maana yake ya hakika, ambayo ni kuhitimisha jukumu la mwanadamu ardhini, na kuufanya kuwa ni kunyongwa kwa milele, kutoweka na kumalizika moja kwa moja na mwisho wenye kutisha na kuogofya, na kaburi – ambalo mlango wake haufungiki – limekuwa linatia sumu ladha ya uhai wa yule mkanushaji na kumtibulia maisha yake kwa machungu makali yenye kumpa ishara ya kutokuwepo kunakotisha daima na kunyongwa kwake milele, kutokana na hili basi fahamu:

Ukubwa ulioje wa imani na ukubwa ulioje wa neema yake! Na fahamu vipi kwamba hiyo ni (Uhai) kwa ajili ya uhai!

Suala la pili:

Hayachukuliwi maneno ya watu ambao wako nje ya uwanja wa elimu au tasnia fulani katika suala mojawapo kati ya masuala yake, ambayo kumepita mjadala kuhusu jambo hilo, hata kama wangekuwa ni wakubwa na wanazuoni na wanatasnia mahiri katika nyanja zao maalumu za elimu, wala maamuzi yao hayachukuliwi kuwa ni hoja katika suala hilo, wala hawaingii katika jumla ya makubaliano ya pamoja ya wanazuoni wa aina hiyo ya elimu.

Basi kwa mfano:

Haifanani hukumu ya mhandisi mkubwa kuwa kama hukumu ya mmoja kati ya matabibu katika kuchunguza maradhi fulani au kuyatibu. Kwa ajili hiyo haziwekwi katika mazingatio kauli zinazokanusha zitokazo kwa mwanafalsafa mkubwa katika mambo yanayohusu elimu ya mambo ya kimaanawy, wala hazitapewa uzito wowote. Na hasa hasa yule ambaye kati yao amebobea katika elimu ya mambo ya kimaada ikafuta uoni wake na kujifanya kipofu mbele ya nuru, akili yake ikakosa maarifa ya mambo ya kimaanawy na akili yake ikaporomoka na kwenda katika macho yake na kuanguka hata akawa haoni isipokuwa maada na hafahamu kitu kingine isipokuwa hicho.

Je, kwa kufikiria, ni thamani gani ya maneno ya wanafalsafa ambao wamehemewa mbele ya migawanyiko ya sehemu ndogondogo na kupotea mbele ya nyingi zake kwa mitawanyiko na kuzama ndani yake, na maneno yao yana thamani gani pamoja kauli zao katika masuala ya tawhidi na imani na mambo ya kimaanawy ya hali ya juu ambayo wamewafikana juu yake mamia ya maelfu miongoni mwa watu wenye elimu na hakika mfano wa sheikh Al-Kaylani (Qaddasa Allah sirrahu) mwenye maarifa matakatifu na busara yenye kufurutu ada ambaye alikuwa anaiona Arshi tukufu na hali ya kuwa bado yuko ardhini, na ambaye ameendelea kupanda ngazi za kimaanawy takribani miaka tisini hata akafunuliwa hakika za kiimani kwa elimu ya yakini, dhati ya yakini, bali hata kwa haki ya yakini. Je, haiwi kukana na kupinga kwao ni dhaifu duni kunafanana na sauti ya mbu mbele ya ngurumo za mbingu na vishindo vya radi zake? 

Hakika kiini cha ukafiri ambao unadhihirisha uadui kwa hakika za Kiislamu, na kutambiana nao hakika si vingine bali ni kukanusha, ujinga, na kukana. Na hata lau itadhihiri – kwa nje – kuthibitisha na hali ya uwepo, ila maana yake ni kukosekana na kukanusha; ama imani: Ni elimu na hali ya uwepo na kuthibitisha na kuhukumu. Na hata masuala yake yenye hali hasi ni pazia ya hakika ya hali chanya na anuani yake.

Lau watu wa kufuru ambao wanazuilia watu kufuata imani wangejitahidi kuthibitisha – kwa matatizo magumu – itikadi zao zenye kukanusha za kihasi na kuzifanya kuwa zikubaliwe kwa sura ya (Kukubali kukosekana) na (Kusadiki kukosekana),  hakika ukafiri huo yawezekana kuhesabiwa – kwa upande mmoja – elimu ya makosa na hukumu isiyosibu. Na kama siyo hivyo hakika kosa rahisi kulitenda kuliko hata (Kutokukubali) na (Kukanusha) na (Kutokusadiki) si vingine isipokuwa ni ujinga usio na ukomo na (Kukosa hukumu).

Muhtasari:

Itikadi ya ukafiri ni sehemu mbili:

Ya kwanza:

Ambayo haina uhusiano na hakika za Kiislamu. Ni kusadiki kwa makosa, itikadi iliyo batili, kukubali kwa makosa na hukumu yenye kudhulumu maalum kwake. Sehemu hii ya ukafiri iko nje ya eneo la uchambuzi wetu, hatuhusiki nalo wala halihusiki na sisi.

Ya pili:

Ambayo inashindana na hakika za kiimani na kuzipinga na hii nayo ina sehemu mbili:

Kwanza:

Ni kukataa na kutokukubali, hii ni kule tu kutosadiki kuthibitisha. Ukafiri huu si lolote ila ni ujinga, na kama sivyo ni kukosa kuhukumu, na huo ni rahisi kuutenda nao ni nje ya eneo la uchambuzi wetu vilevile.

Pili:

Ni kukubali kukosekana, na kusadiki kimoyo kwa kukosekana, sehemu hii ya ukafiri ni hukumu, na hii ni itikadi inayompelekea mwenye nayo kushikamana. Analazimika kuthibitisha kukanusha na kukataa kwake.

Na vilevile kukanusha kuna sehemu mbili:

Ya kwanza:

Kusema mkanushaji: Kwamba hakuna katika mahali maalum na katika sehemu maalum kitu fulani. Na sehemu hii ya kukanusha kilicho maalum yawezekana kuthibitisha kwake na hii pia ipo nje ya uchambuzi wetu.

Sehemu ya pili:

Kukana masuala ya kiimani na utakatifu na jumla na yenye kuzunguka kila sehemu ambako kunaelekea katika dunia, na inajumuisha ulimwengu na kutazamia akhera na kukusanya enzi na enzi. Na kukanusha huku – kama tulivyothibitisha katika suala la kwanza – haiyumkiniki kuthibitisha kabisa, kwa sababu inalazimu kuwepo na uoni unaozunguka ulimwengu wote na mtazamo jumuishi wa akhera na ushuhuda unaopenya katika zama zisizowekewa mipaka katika pande zake zote, ili kuthibitisha mfano wa kukanusha huku.

Shida ya pili na namna ya kuokoka kutokana nayo:

Nayo ni masuala mawili vilevile:

Kwanza:

Hakika ya akili ambazo zimefinyika mbele ya (Ukuu), (Kiburi) na (Huria isiyo kuwa na kikomo) na ni pungufu katika kutambua kwake ikiwa ni matokeo ya kughafilika au maasi au kuzama katika mambo ya kimaada na kufuata nyuma yake – akili hizi – zimeanza kuteleza kwenye kukanusha na zinakanusha – kwa kudanganyika kielimu –  masuala makubwa kwa sababu ya kushindwa kwake kuyazungukia mambo hayo kwa ujuzi.

Naam, hakika wale ambao wameshindwa kuyafahamu masuala ya kiimani yenye kuzunguka kote na mapana sana na ya kina mno katika akili zao ngumu finyu kimaana, na kuyakiri katika nyoyo zao fisadi mfu – upande wa mambo ya kimaanawy – wanajitupa wenyewe katika hifadhi ya ukafiri na upotevu, hatimaye wanazama. Lakini laiti wangeweza hawa kutazama kwa makini katika kiini cha kufuru yao na katika hakika ya upotevu wao, wangeona kuwa kinacho kubalika kiakili katika imani upande wa ukuu na chenye kuendana nao na ni cha lazima, inakabiliana na muhali kufuatia muhali na lisilowezekana na lenye kukataa ndani ya ukafiri huo.

Risale-i Nur imethibitisha hakika hii kwa mamia ya mizani na kwa kukata kabisa kama mkato wa jibu la mbili mara mbili kuwa ni nne.

Mathalan:

Ambaye anashindwa kukubali imani ya kupasa kuwepo kwake (s.w), uazali wake na sifa zake zinazozunguka utukufu wake (s.w), kwa ukubwa wake na kwa ukubwa wa sifa zake tukufu, atahaulisha kupasa kwa uwepo, uazali wake na sifa za kiungu kwenda kwa vyote vilivyomo visivyo na mpaka, bali katika chembe ndogo sana zisizo kuwa na ukomo, ili aweze kuitakidi ukafiri wake au ni juu yake ajivue na akili kama Wanasafsata mazuzu kwa kukanusha uwepo wa nafsi yake na kukana uwepo wa ulimwengu.

Na kama hivi hakika za kiimani na Kiislamu zinatulia zote kwa kujiegemeza kwake kwa (Ukuu) – ambao ni katika hali ya hakika hizo na katika yanayolazimu – na zinathibiti katika nyoyo safi na akili salama, kwa ukamilifu wa kutii, kusalimu amri ambako ni tulivu, zikiwaokoa kutokana na ukafiri unaokabiliana nazo na muhali zake za kushangaza na fikra potofu zenye kustaajabisha na ujinga wake wenye kiza.

Naam, hakika Ukuu na Kiburi ni pazia mbili hazina budi kuwepo; na linabainika hilo kutokana na kutangaza ukuu huo na kiburi hicho kila wakati: Katika adhana, kwenye swala, na katika aghalabu ya alama za Kiislamu kwa kukariri.

الله أكبر.. الله أكبر.. الله أكبر.. الله أكبر          

Na inakuwa wazi hilo pia katika hadithi Qudusi: (Ukuu ni shuka yangu na kiburi ni kishari changu).

Angalia: Abu Daud, Al-Libas, 25. Ibn Majah, Az-Zuhd 16. Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad 2/376.

Na inadhihiri pia katika fundo la themanini na sita kutoka katika Al-Munaajat Al-Ahmadiyya yenye ufasaha katika )Al-Jawshan Al-Kabiir).

Ewe ambaye hakuna ufalme ila ufalme wake

Ewe ambaye waja hawadhibiti wasifu wake

Ewe ambaye viumbe hawasifu utukufu wake

Ewe ambaye dhana hazipatii hasa alivyo

Ewe ambaye macho hayadiriki ukamilifu wake

Ewe ambaye fahamu hazifikii sifa zake

Ewe ambaye fikira hazifikii kiburi chake

Ewe ambaye mwanadamu hafanyi vizuri kumsifu kwake

Ewe ambaye waja hawarudishi hukumu yake

Ewe ambaye katika kila kitu zimedhihiri ishara zake

Utakatifu ni wako ewe ambaye hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila wewe, amani, amani tuokoe na moto.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.