JAMBO LA AJABU KWA MWANAADAMU

Kutoka kwenye Muale wa kumi na saba

Ewe Mwanaadamu! Hali ya ajabu ambayo Muumba Mwingi wa hekima, ameijumuisha katika maumbile yako ni kushindwa kumaliza haja katika ulimwengu huu; kama mtu aliyezibwa pumzi kwenye gereza, unaangalia mahali pengine papana zaidi kuliko ulimwengu huu, na bado unaingia katika mambo madogo sana, kumbukumbu, punde, na kutua ndani yake. Moyo wako na akili ambavyo haviwezi kutuama katika ulimwengu mkubwa vinatulia kwenye kitu hicho kidogo. Utashangaa pamoja na mihemko yako iliyosheheni katika muda huo mfupi, kumbukumbu hiyo ndogo sana.

Na amefungasha katika maumbile yako nguvu ambazo sio za kimaada na vipawa madhubutii, ambazo kama baadhi yake zingemeza ulimwengu, zisingetosheka. Na baadhi ya hizo haziwezi kuhimili hata kidogo sana ndani yake wenyewe. Kama jicho haliwezi kuhimili unywele japo kichwa kinaweza kubeba mawe mazito, vipawa hivyo haviwezi kuhimili uzito hata wa unywele, ambapo, baadhi ya hali zisizokuwa kubwa, hutokea kutokana na kughafilika na upotevu. Baadhi ya wakati huzimwa na hata kufa.

Kwa kuwa ni hivyo, kuwa muangalifu, kanyaga kwa tahadhari, kuwa na hofu ya kuzama! Usizame katika ujazo wa kinywa, neno, mbegu, mwanga, ishara, busu! Usivitumbukize vipawa vyako vipana ambavyo vinaweza kumeza ulimwengu katika vitu kama hivi. Kwa sababu kuna vitu ambavyo ni vidogo sana ambavyo kwa namna moja vinaweza kumeza vitu ambavyo ni vikubwa sana. Mbingu pamoja na nyota zake vinaweza kuingia kwenye kipande kidogo sana cha kioo na kuzamishwa. Na aghlabu ya kurasa za amali zako na majani ya maisha yako huingia katika kipawa cha kumbukumbu yako, kidogo sana kama mbegu ya hardali. Kwa hiyo kuna vitu vidogo sana pia vinavyomeza vitu vya ukubwa wa namna huo na kuvihifadhi ndani yake.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.