Suala La Kumi Na Moja

Hakika ya mti mtakatifu wa nguzo za imani za kijumla una matunda manono mojawapo ni pepo, na lingine ni furaha ya milele, na la tatu ni kumwona Allah (s.w).

Na kwa kuwa Risale-i Nur imeweka wazi mamia ya matunda hayo – ya jumla yake na baadhi yake – pamoja na hoja zake zenye nguvu katika (Siraji an-Nur) tunaelekeza huko na hapa tunaashiria vielelezo vichache tu vya matunda ya kisehemu bali sehemu ya sehemu na iliyo mahususi katika matunda hayo mazuri.

Mojawapo:

Siku moja nilikuwa ninaomba dua lenye ujumbe huu: “Ewe mola nakuomba kwa kutawasali kwako kwa utukufu wa Jibril, Mikail, Israfil na izrail na kwa shufaa yao unihifadhi kutokana na shari za majini na watu” na mara nilipolitaja jina la Izrail – ambao utajo wake unawajaza watu hofu na kutetemeka – nilihisi hali yenye ladha katika upeo wa utamu na maliwazo, nikamshukuru Allah (s.w) kwa kusema: (Alhamdulillah), na nikaanza kumpenda Izrail mapenzi ya dhati kwa kuwa yeye ni mmoja kati ya malaika ambao inazingatiwa kuamini uwepo wao nguzo katika nguzo za imani. Tutaashiria kwa muhtasari sana tunda dogo kutoka katika matunda mengi ya kumwamini malaika huyu.

Katika hizo:

Hakika ya thamani ya aliyokuwa nayo mwanadamu na kikubwa sana anachokipupia na kukitetea na anajitahidi kukihifadhi, bila shaka ni roho yake. Hakika nilihisi kwa yakini furaha ya kina kwa mwanadamu kusalimisha kitu kitukufu mno alichonacho – nacho ni roho yake – mkononi mwa (Mwenye nguvu mwaminifu) ili aihifadhi isichezewe, isipotee na kutoweka.

Kisha nikakumbuka malaika waliowakilishwa kusajili amali za mwanadamu nikakuta kuwa wana matunda matamu mno kama haya:

 Kati ya hayo:

Kila mwanadamu ili amali zake nzuri zipate kukaa milele na maneno yake mazuri yabakie hujitahidi kuyahifadhi na kuyalinda yasipotee sawa iwe kwa njia ya kuandika au ushairi au hata kwa mkanda wa sinema, na hasa ikiwa amali hizo zina matunda yake ya kubaki peponi, hupata shauku sana kuyahifadhi.

Na waandishi watukufu wamesimama karibu ya mabega ya mwanadamu ili wamdhihirishe katika shuhuda za milele, na ili wapige picha amali zake katika mandhari ya kudumu milele, ili wenye amali hizo walipwe na wapate zawadi za kudumu na za thamani. Nimepata ladha ya matunda haya kwa utamu nisioweza kuuelezea. Na waliponiepusha watu wa upotevu na sababu za maisha ya kijamii na kuniweka mbali na vitabu vyangu, wapendwa wangu na wahudumu wangu na kila kilichokuwa kikinipa maliwazo, na wakanitupa katika makazi ya ugeni na upweke, na nilikuwa katika dhiki na kukereka kutokana na hali yangu kwa kiwango cha kuwa nikihisi kuwa dunia iliyo tupu itavunjikia kichwani kwangu. Wakati nikiwa katika hali hiyo tahamaki tunda moja katika matunda ya kuamini malaika ikaja kunipa msaada na ikaangazia pande za dunia yangu yote na kunawirisha ulimwengu unaonizunguka na kuuimarisha na malaika na kujaza wakazi wa roho nzuri hadi ikaingia furaha kila mahali.

Imeinama mbingu na ni haki yake kuinama, hakuna mahali pa vidole vinne isipokuwa juu yake kuna malaika mwenye kuweka paji lake akimsujudia Allah (s.w). ( Tazama: Ahmad Bin Hanbali, Al-Musnad 5/173. At-Tirmidhy, Az-Zuhd 9. Ibn Maajah, Alzuhd 19).

Na pia ikanionesha vipi dunia ya watu wa upotevu ilivyojaa kelele za upweke na majuto ya mchezo na giza.

Wakati mawazo yangu yakiwa yanafurahia kupata ladha ya tunda hili tahamaki inapokea tunda katika matunda mengi – yalio mfano wa haya – ya kuamini mitume (a.s), ikaonja hasa na moja kwa moja nikahisi kuwa Imani yangu imepanuka na kukunjuka hadi ikawa kitu kizima jumuishi, ambapo zama hizo zilizopita zote ziliangaza kwangu na kuangaza kwa nuru ya kusadiki na kuwaamini, hata nikahisi kana kwamba ninaishi pamoja nao, akawa kila nabii katika manabii anasadikisha kwa maelfu ya usadikishaji juu ya nguzo za imani ambazo amekuja nazo na kuzilingania nabii wa mwisho Muhammad (s.a.w), jambo ambalo lilimnyamazisha Shetani.

Kisha swali lenye jibu la kutosheleza lililopo katika mng’ao (Hekima ya kujikinga) likaja haraka moyoni nalo ni: Kwamba watu wa imani ambao wana mfano wa matunda haya ya imani na mfano wa faida hizi na natija tamu bila ukomo na wana natija nzuri za mema na manufaa yake mengi, na wana uangalizi wa kudumu kutoka kwa (Arhamu Ar-Rahimina) na tawfiki yake na rehema yake, vyote hivyo vinawapa nguvu na egemeo, basi ni kwa nini watu wa upotevu aghalabu wanawashinda, bali ishirini katika watu wa upotevu wanaweza kuwashinda mia moja kati yao na kuwateketeza?! na katikati ya tafakuri hii ilipita moyoni mwangu: Ni kwa nini Qur’an tukufu inakusanya mkusanyo huu mkubwa kwa watu wa Imani kwa kutaja msaada wa Allah (s.w) kwao kwa kuwaleta malaika na hali ya kuwa wanakabiliana na madhila duni dhaifu ya kishetani?

Kwa kuwa Risale-i Nur imefafanua hekima ya hilo kwa hoja zenye kukinaisha hapa tutaashiria jibu la swali hilo kwa ufupi mno:

Naam, wakati mwingine watu mia moja wanalinda kasri, wakati mmoja wa watu wa shari au mtu yeyote mharibifu anapojaribu kurusha moto katika kasri hiyo kwa siri ili kuliteketeza, au huenda akaombwa mfalme au taifa kuhifadhi kasri hiyo, hii ni kwa kuwa kubakia jengo la kasri kunahitajia masharti yote na nguzo na sababu zenye kupelekea kuhitajia kubaki. Ama kuliharibu na kulivunja huwa kwa kukosekana sharti moja tu.

Na katika mfano kama huu tunafahamu namna mashetani wa majini na watu wanavyofanya uharibifu wa ajabu na uchomaji moto mkubwa kwa matendo machache mno, kama ambavyo mshari anavyoteketeza jengo kubwa kwa kutupia kijiti cha kibiriti.

Naam, msingi na hamira ya shari na maovu na makosa yote ni kukosekana na kuvunja, na kinachoonekana katika uwepo wake wa dhahiri kinaficha chini yake ufisadi, kuharibu na kukosekana.

Na kwa kuegemea nukta hii, hakika mashetani wa majini na watu na wenye shari wanaweza kwa nguvu ndogo dhaifu mno kuzuia nguvu isiyo na mpaka ya watu wa haki na hakika na kuwafikisha mlangoni kwa Allah (s.w) na kujitahidi kumwendea daima. Na kwa sababu hii Qur’an tukufu inaweka maandalizi hayo makubwa ili kuwalinda, na kukabidhi mikononi mwao majina mazuri tisini na tisa, na kutoa amri kali wapate uthabiti mbele ya maadui hao.

Na kutokana na jawabu hili ghafla umedhihiri msingi wa suala la kushangaza na mwanzo wa hakika kuu nayo:

Kama ilivyo pepo inahazini mavuno ya limwengu zote za uwepo na matokeo yake, na kuizalisha kokwa iliyopandwa ardhini duniani na kuifanya inatoa chakula chake kila wakati. Hakika jahanamu inakusanya mavuno ya kutokuwepo kwa ajili ya kudhihirisha matokeo yenye kuumiza sana ya limwengu za kukosekana na kutoweka kusiko na mipaka, basi kiwanda cha jahanamu ya kutisha – licha ya majukumu yake mengi – kinatakasa yaliyopo katika ulimwengu wa uwepo kutokana na takataka za ulimwengu wa kukosekana. Tutafafanua baadaye Inshallah suala hili kuu kwa sababu hatutaki kufungua mlango wake hapa. Vivyo hivyo, sehemu ya matunda ya imani ya malaika ni ile inayorejea kwa Munkar na Nakir,

Tazama: At-Tirmidhy, Al-Janaiz 70. Ibn Maajah, Al-Janaiz 65. Ahmad Bin Hanbal, Al-Musnad 3/126, 4/288.

nayo ni kama ifuatavyo:

Siku moja nilisema: (Hakika mimi sina budi – kama mtu yeyote awaye – ni mwenye kuingia kaburini hapana namna). Nikaingia humo kimawazo na nilipokuwa ninahisi upweke hali ya kukata tamaa na jela ya pekee ya kaburi na kuachana na kila kitu kabisa, bila ya msaidizi mahali hapo pembamba penye giza na baridi, ghafla wanatokea marafiki wawili wema katika kundi la (Munkar na Nakiir) na kuja kwangu na kuanza mjadala na mimi, walikunjua vyote moyo wangu na kaburi langu, wakaleta mwanga na joto na kufunguliwa madirisha yanayokabiliana na ulimwengu wa roho. Nilifurahishwa kutokea kina cha roho yangu na nikamshukuru sana Allah (s.w) kutokana na hali nilizoziona ambazo lazima zitatimia katika mustakabali japokuwa kwa sasa naziona kimawazo. Kama ilivyokuwa wakati alipofishwa mwanafunzi wakati wa kujifunza Sarufi na Nahau, Munkar na Nakiir walimuuliza kaburini: “man Rabbuka” (Mola wako ni nani?) akajibu: (man ni kiima na Rabbuka ni kielezi cha kiima. Niulizeni swali lingine gumu hili ni rahisi!!) – anadhani kuwa bado yuko madrasa akipokea somo – kama pia jibu hili lilivyo wachekesha malaika na roho zilizokuwepo na yule walii mwema ambaye kaburi lilimfunukia akashuhudia tukio hili, bali limefanya rehema ya Allah (s.w) itabasamu ikamuokoa kutokana na adhabu. Vivyo hivyo, shahidi hodari katika wanafunzi wa Risale-i Nur naye ni (Al-hafiz Ally) alifishwa jela hali akiwa anaendelea kusoma na kuandika (Risala ya Matunda) kwa ukamilifu wa shauku, alijibu maswali ya malaika wawili wa kaburini – kama alivyojibu mahakamani – kwa kutumia hakika za (Risala ya Matunda). Nami vilevile na wanafunzi wengine wa Risale-i Nur tutajibu inshallah maswali hayo ambayo ni hakika huko mustakabali, na ni majazi katika wakati uliopo. Tutayajibu kwa hoja za Risale-i Nur zenye kumulika na dalili zake zenye nguvu na kuwaelekeza kwa hoja hizo katika kusadikisha kusifu, uzuri na kuthamini.

Na vivyo hivyo hakika kielelezo cha sehemu ya kuamini malaika ikiwa ni mhimili wa furaha ya dunia ni kuwa:

Wakati ambapo mtoto asiye na hatia akipokea masomo yake katika misingi ya fiqhi, ghafla mtoto mwingine anamjia akiwa analia akihuzunika kwa kifo cha ndugu yake asiye na hatia basi anamtuliza na kumliwaza kwa kusema: (Usilie ewe ndugu yangu, bali mshukuru Allah (s.w) kwa sababu ndugu yako amekwenda pamoja na malaika na kwenda peponi atazunguka na kutembea huko kwa uhuru kamili kama malaika na atapata furaha na starehe bora kabisa na ataruka kama malaika na kushuhudia kila mahali). Akabadilisha kilio, kelele na masikitiko yake kuwa ni tabasamu na furaha.

Na mimi vilevile kama mtoto huyu mwenye kulia katika hali ya machungu, pamoja na hali niliyokuwamo na katika majira haya ya baridi ya kuhuzunisha nilipokea habari ya vifo vya wawili na kuwahuzunikia kwa masikitiko na machungu makubwa mno.

Moja wapo:

Ni mtoto wa ndugu yangu marehemu (Fuad) ambaye alifanikiwa kupata daraja ya kwanza katika shule ya juu naye ndiye mwenezi wa hakika za Risale-i Nur.

Pili:

Ni yule aliye hiji na kutufu nyumba ya Allah na akiwa katika machungu ya kukata roho na alisalimisha roho yake akiwa kwenye tawafu, naye ni marehemu dada yangu mwanazuoni: (Khanim).

Wakati vifo viliponiliza vya hawa ndugu wawili kama kumlilia kwangu (Abdul Rahmani) – iliyotajwa katika (Risala ya wazee) – niliona kwa nuru ya Imani – kwa moyo na maana – urafiki wa malaika na usuhuba na mahuru al-aini kwa kijana yule mzuri: (Fuad) na kwa yule bibi mwema, badala ya urafiki wa watu, na nimeona kuokoka kwao kutokana na maangamizo ya dunia na kukombolewa kutokana na makosa yake. Nikaanza kumshukuru Allah (s.w) –  na yeye ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu – shukurani elfu moja na moja, jambo ambalo limegeuza huzuni hiyo kali kuwa hisia ya furaha, na nikaanza kuwapongeza na kumpongeza ndugu (Abdul Majid) (Baba Fuad) na ninaipongeza nafsi yangu vilevile. Hili limeandikwa na kusajiliwa hapa ili marehemu hawa wawili wapate baraka ya dua.

Hakika yote yaliyomo kwenye Risale-i Nur katika vipimo na milinganisho hakika ni kwa ajili ya kubainisha matunda ya furaha ya imani na matokeo yake yanayorejea katika maisha ya dunia na Akhera, hayo matunda ya jumla makubwa huonyesha furaha ya maisha duniani na kuonjesha ladha zake ndani ya umri, kama inavyoelezea kwamba imani ya kila muumini itampa furaha ya milele huko Akhera, bali itazaa matunda na kufunuka na kukunjuka kwa sura hiyo hiyo huko Akhera. Basi katika mifano ya matunda hayo mengi ya jumla nimeandika matunda matano kati ya hayo kwamba hayo ni ya (Miiraji) mwishoni mwa (Neno la thelathini na moja) na matunda matano katika (Tawi la tano katika neno la ishirini na nne).

Kama tulivyotaja karibuni kwamba kila nguzo miongoni mwa nguzo za imani ina matunda mengi sana bila mipaka, basi jumla ya nguzo za imani kwa pamoja zina matunda yasiyo na mpaka pia:

Moja wapo:

Pepo kuu.

Nyengine:

Furaha ya milele.

Ya Tatu:

Ni yenye ladha zaidi ambayo ni kumwona Allah (s.w) huko.

Imefafanuliwa kwa uwazi katika mlinganisho uliyofanywa mwishoni mwa (Neno la thelathini na mbili) baadhi ya matunda ya imani ambayo ni muhimili wa makazi mawili.

Hivyo, na dalili kwamba (Kuamini Kadari) ina matunda yake ya thamani pia hapa duniani ni jambo linalozunguka katika ndimi za wote, hadi imekuwa ni ya kupigiwa mithali: (Mwenye kuamini kadari amesalimika na huzuni), na mwishoni mwa (Risala ya Kadari), nimebainisha moja ya matunda yake ya jumla kwa mfano nao: Kuingia kwa watu wawili katika kasri ya kifalme. Hata nimeshuhudia katika uhai wangu kwa maelfu ya uzoefu wangu na nikatambua kuwa hakuna furaha katika maisha ya dunia bila ya kuamini Kadari, bila ya imani hii basi furaha hiyo ingefutwa na kutoweka. Bali nilikuwa kila nilipotazama masaibu ya kuumiza katika pembe ya kuamini Kadari, masaibu hayo yalikuwa na tahafifu na shida yake inapungua kwangu, Nikawa ninauliza kwa tahayuri: Vipi mtu asiyeamini Kadari anaweza kuishi?

Imeashiriwa katika moja ya matunda ya kiujumla ya nguzo ya imani: (Kuamini malaika) (Katika Kituo cha pili cha neno la ishirini na mbili) kama ifuatavyo:

Hakika Izrail (a.s) alisema akiongea na mola wake: Hakika waja wako watanilalamikia na kunichukia wakati wa kutekeleza kwangu jukumu la kutoa roho. Akajibiwa: Nitajaalia maradhi na masaibu kuwa ni pazia za jukumu lako ili malalamiko yao yapate kuelekea huko na sio kwako. Na jukumu la Izrail lenyewe vilevile ni pazia katika pazia hizo ili malalamiko batili yasielekee kwa Mola wa haki (s.w), kwa sababu hekima, rehema, uzuri na masilahi yaliopo katika umauti huenda asiyaone kila mmoja, kwani anaangalia nje ya mambo na anaanza kupinga na kulalamika. Kwa ajili ya hekima hii – yaani malalamiko ya batili yasielekee kwa Mwingi wa rehema wa hali zote – Izrail (a.s) amekuwa ni pazia.

Na mfano wa hili kabisa wanayotenda malaika na sababu zote za dhahiri katika majukumu, hakika hizo ni pazia za Izza ya Ulezi wa kiungu, ili Izza ya uweza wa kiungu na utakatifu wake na rehema ya Allah (s.w) yenye kuzungukia kila kitu na enevu zibakie zimehifadhika katika mambo na vitu ambavyo pande za uzuri uliomo hauonekani, na wala haijulikani hakika za hekima ndani yake, pasipo kuwa ni shabaha ya upingaji batili. Wakati huo basi haionekani kwa mtazamo wa dhahiri utendaji wa mkono wa kudura katika mambo ya kibaadhi na yenye kupingana na rehema na vitu duni. Hivyo, na hakika Risale-i Nur imethibitisha kwa dalili zake nyingi, kwamba sababu yoyote ile katika sababu mbalimbali haina taathira ya hakika na wala haina nguvu ya kupatisha kitu asilani. Hakika mihuri ya Tawhiid isiyo na mpaka imeweka katika kila kitu na kwamba uumbaji na upatishaji unamhusu yeye (s.w), sababu sio chochote isipokuwa ni pazia, na malaika – nao ni wenye utambuzi – hawana isipokuwa ni sehemu katika hiari ya kisehemu (Eneo dogo analo miliki hiari) ambayo yeye ana nafasi ya kuchuma na sio kupatisha, nayo ni aina ya huduma ya kimaumbile na aina ya uja wa kimatendo na sio vinginevyo.

Naam, hakika ya enzi na adhama vinahitajia kuweka sababu za dhahiri ni pazia mbele ya macho ya akili, isipokuwa Tawhidi na utukufu hunyanyua mikono ya sababu na kuizuia kuhusu taathira ya kihakika.

Na kama hivi kama malaika na sababu za dhahiri zinazotumika katika mambo ya kheri na uwepo, ni nyenzo za utukuzo wa kiungu na utakaso katika yasiyoonekana wala kujulikana uzuri wake katika vitu, na hiyo ni kwa kuutakasa uweza wa kiungu na kuuhifadhi dhidi ya kasoro na dhuluma, vilevile kuwatumia mashetani wa kijini na wanadamu na vitu vyenye kudhuru katika mambo ya shari na kukosekana nayo ni aina nyingine ya kuhudumia tasbihi za kiungu na ni nyenzo ya kutukuza, kutakasa na kuweka mbali na kila kinachodhaniwa kuwa ni upungufu na kasoro katika viumbe na hiyo ni kwa sababu ya kulinda uweza wa kiungu, isije kuwa ni shabaha inayohusishwa na dhulma na kuelekezwa upinzani wa batli kwake, kwa sababu kasoro zote hutokea kwenye kukosekana, kushindwa, uvunjaji na kuzembea wajibu – ambayo yote  ni  kukosekana – na kutoka katika visivyokuwa na uwepo katika matendo ya kutokuwepo. Basi pazia hizi za kishetani zenye shari zimekuwa ni nyenzo za kumtakasa Mola wa haki (s.w) kwa yale mambo zilizoyabeba – kwa kustahiki – upingaji huo na malalamiko hayo kwa kuwa ndio marejeo na chanzo cha kasoro hizo. Wakati amali za shari na za kukosekana na kiharibifu hazihitajii – asilani – nguvu na uweza, basi matendo machache au nguvu ya kisehemu bali kuzembea wajibu fulani wakati mwingine, hupelekea katika aina za kukosekana na ufisadi. Kwa hiyo inadhaniwa mwenye kutenda matendo hayo ya shari kuwa mwenye uweza, wakati ambapo mambo yalivyo kwa hakika ni kwamba hana taathira isipokuwa kutokuwepo na hana nguvu isipokuwa kuchuma kwa kisehemu (Sehemu ndogo ya hiari). Na ilipokuwa shari hizo zinatokana na kutokuwepo basi watu hao wa shari wanahesabiwa kuwa ndio watendaji wa hakika wa mambo hayo, ikiwa ni katika wenye utambuzi wanastahiki kuonja matokeo mabaya ya jambo lao. Na hii inamaanisha kuwa hao wa shari mafisadi ni watendaji wa maovu. Ama katika mema na kheri na matendo mema kwa kuwa ni vya hali ya uwepo, walio wema sio watendaji wa hakika wa matendo hayo, bali wao wanastahiki ili matendo mazuri kupita kwenye mikono yao na basi wanapokea ukarimu wa kungu. Na kuwalipa hao kwa amali zao sio lolote isipokuwa ni ukarimu na neema tupu ya kiungu. Na Qur’an tukufu inafafanua hili kwa amri yake:

مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللّهِ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ Qur’an, 4:79.

Muhtasari:

Hakika limwengu za uwepo na limwengu za kukosekana kusiko na mpaka zinapogongana kwa pamoja na zinapozaa matunda ya pepo na moto, na wakati limwengu zote za uwepo zinaposema: (Alhamdulillah,  Alhamdulillah) na limwengu zote za kukosekana zinarudia kusema: (Subhanallah, Subhanallah) na hata malaika na mashetani wanapopambana, na kheri na shari, bali hata unapotokea mjadala katika moyo kati ya ilhamu na wasiwasi, wakati yanatokea yote haya kwa kanuni ya mkabala yenye kuzunguka hudhihiri tunda katika matunda ya (Kuamini malaika), kadhia inamalizwa na kutatuliwa tatizo ikinawirisha viumbe vyenye giza ikitudhihirishia nuru katika nuru nyingi za:

اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ Qur’an, 24:35.

Hivyo inatuonjesha utamu wake utamu uliyoje wa nuru hiyo!! Na ladha yake iliyoje!!

Hivyo, hakika vyote katika neno la (Ishirini na nne) na (Neno la ishirini na tisa) yameashiria katika tunda la jumla lingine na yamethibitisha uthibitisho wa uwazi uwepo wa malaika na kazi zao.

Naam, hakika ulezi wa kiungu wenye rehema mkunjufu ambao umejitambulisha na kupendezesha katika uliyoyaeneza katika pande za ulimwengu sawa yawe ya kiujumla au kisehemu, utukufu huo na rehema hiyo utambulisho huo na kupendezesha huko kunapasa kukabiliwe na uja mkunjufu wenye kuzungukia kila hali enevu wenye shukurani ndani ya utukuzo, shukurani na kusifu.

Hakika ya visivyo na uhai na nguzo kuu za ulimwengu ambazo hazina utambuzi huwezi kutimiza uja (utumishi) huu mkubwa, hivyo hawatimizi kwa niaba yao isipokuwa kiasi kisichohesabika cha malaika, hawa ndio wanaoweza kuwakilisha – kwa hekima zote na utukufu – shughuli za ufalme wa ulezi wa kiungu katika kila nguzo katika nguzo za ulimwengu, na katika kila sehemu miongoni mwa sehemu zake kutokea kwenye mchanga hadi kwenye Thurea (aina ya nyota) kutokea katika vina vya ardhi hadi kwenye anga.

Kwa mfano:

Hakika taswira inayowekwa na kanuni mfu za falsafa za kuumbwa kwa ardhi na kazi yake ya kimaumbile kwa namna ya kutisha yenye giza, tunda hili la imani inaigeuza taswira hiyo na kuwa ni taswira yenye kuliwaza yenye kuangaza ambapo malaika wawili wanaoitwa Ng’ombe na Samaki, wanabeba juu ya mabega yao – yaani chini ya uangalizi wao – dunia, ambapo mada hiyo ya kiakhera imeletwa kutoka peponi, na hakika hiyo ya kiakhera inayoitwa (Jiwe) lipate kuwa jiwe la msingi lenye kubakia la hili tufe la Ardhi lenye kutoweka, ikiashiria kwamba sehemu fulani ya ardhi itapakuliwa na kugeuzwa kuelekea kwenye pepo ya kubaki, Jiwe limekuwa ni nukta ya kuegemea malaika wawili: (Ng’ombe na Samaki), kama hivi riwaya hii imesimuliwa kutoka baadhi ya manabii Waizraili wa mwanzo nayo imesimuliwa pia kutoka kwa Ibn Abbas (r.a)  lakini cha kusikitisha mno tashibiha hii ya upole na maana hii ya juu kugeuka kwa kupita kwa muda kuwa ni hakika ya kimaada yenye kupewa mwili kwa watu wa kawaida, kiasi imekuwa nje ya eneo la akili, kwa kuwa malaika wanaweza kupita na kuzunguka katika udongo na katika mawe na katikati ya ardhi kama kutembea kwao hewani, kwa hiyo hawana haja kabisa – wala tufe la ardhi halina haja – ya jiwe la kimaada katika hali ya kimwili wala ng’ombe na samaki wa kimaada katika hali ya kimwili! Kwa maana riwaya hiyo sio vingine isipokuwa ni kwa Tashbiha.

Mathalani:

Kwa kuwa tufe la ardhi linamsabihi Allah kwa idadi ya vichwa vya aina zilizopo ndani yake, ikiwemo wanyama, mimea na visivyo na uhai na kwa idadi ya ndimi za kila moja ya aina hizo, na kwa kiasi cha viungo vya kila moja, na kwa idadi ya majani yake na matunda yake, hakika kutanguliza uja huu wa kimaumbile usio wa kiutambuzi mkubwa sana, na kuwepo kwake na kuonesha kwa ujuzi na utambuzi mbele ya hadhara ya kiungu tukufu, Inahitajia kwa lazima malaika mwenye kuwakilishwa ambaye ana vichwa arobaini elfu, na katika kila kichwa kuna ndimi arobaini elfu, kwa kila ulimi anasabihi kwa tasbihi arobaini elfu, kama mpashaji habari wa kweli alivyoelezea hakika hii hii.

Tazama: At-Tabary, Jaamiu Al-bayan,15/156. Abu Al-shaikh , Al-Adhamat 2/ 547, 740, 742, 747,3/868. Ibn Kathiir, Tafsirul Qur’an 3/62.

Naam, ni katika yanayolazimu utukufu wa ulezi wa kiungu, adhama na ufalme wake kwamba Jibril awe katika haiba ya ajabu na yeye ndiye mwenye sifa ya kufikisha mahusiano ya kiungu kwa mwanadamu ambaye ndiye matokeo muhimu ya kuumbwa kwa ulimwengu, na wawe Izrail na Israfil (a.s) katika haiba ya ajabu vilevile, nao wanawakilisha – ni kuwakilisha tu – shughuli maalum za kiungu za Muumba (s.w) na kusimamia kwa uja (Utumishi) wa dhati juu ya kitu adhimu sana katika ulimwengu wa wenye uhai, nacho ni ufufuo na umauti. Na Mikail (a.s) awe katika haiba ya ajabu, ambapo anawakilisha kwa utambuzi kamili aina za shukurani zisizo za kiutambuzi juu ya hisani za mwingi wa rehema katika riziki ambayo ni duara jumuishi zaidi katika duara za maisha na kunjufu zaidi na lenye hali nyingi za kuonja, licha ya uangalizi wake juu ya jambo hili.

Naam, ni mambo ya lazima ya utukufu wa ulezi wa kiungu na heshima yake kubakia kwa roho na kuwepo kwa mifano ya malaika kama hawa kwa haiba ya ajabu mno, kwa kuwa uwepo wa hawa na kuwepo kwa kila kundi maalum kati yao ni wenye kuthibiti kimkataa na hakuna shaka katika hilo kwa hali zote, nalo ni lenye kuthibiti kwa kiwango kinacholingana na uthabiti wa kuwepo kwa utukufu na ufalme wa dhahiri katika ulimwengu kama jua. Na mada nyengine zinazohusu malaika zipimiwe hili.

Naam, hakika ambaye anaumba katika tufe la ardhi mia nne elfu aina za walio hai, bali anaumba wenye roho kwa wingi mkubwa kutokana na maada rahisi mno na kutokana na uozo, na anaimarisha pande za ardhi kwa kuwaweka wao na kuwajaalia kuwa wanatamka kwa ulimi wao kwa kupendezwa: (Mashaallah, Baarakallah, Subhanallah), mbele ya miujiza ya ufundi wake (s.w), na ambaye amefanya hata wanyama wadogo mno wanatamka: (Alhamdulillah wa Ash-shukru lillah wallahu akbar) mbele ya hisani za rehema kunjufu na neema zake. Hakika ya huyu Mweza mwenye utukufu na uzuri, hakika ameumba bila shaka wala utata wakazi wa kiruhani wenye kuwiana na mbingu zenye mawanda makubwa sana katika ambao hawaasi amri yake na wanamwabudu yeye daima, kwa kuwatumia wao anaimarisha mbingu bila ya kuiacha tupu kame. Akapatisha aina nyingi mno katika malaika ambao ni wengi mno kuliko aina za walio hai na makundi yao, sehemu kati yao ni ndogo sana wanapanda matone ya mvua na chenga za barafu na wanabariki ufundi wa kiungu wakifanya tahalili kwa rehema zake kunjufu kwa ulimi wao maalum, na sehemu kati yao wanapanda migongo ya sayari zenye kutembea hivyo huelea katika anga la ulimwengu hali ya kuwa wanatangazia ulimwengu wote uja wao kwa takbira na tahalili mbele ya adhama ya ulezi wa kungu na enzi yake na utukufu wake

Amepokea Abu Daud kwa sanad sahihi kwamba Mtume (s.a.w) amesema: Nilipewa idhini niongee kuhusu malaika katika wabebaji wa Arshi miguu yake iko kwenye Ardhi ya chini na juu ya pembe yake kuna Arshi, na katika ndewe ya sikio lake na shingo yake ni masafa ya kuruka kwa ndege kwa miaka mia saba, malaika huyo anasema: Utakatifu ni wako popote nilipo.

Naam, hakika kuafikiana vitabu vyote vya mbinguni na dini zote tangu zama za Bwana wetu Adam (a.s), juu ya kuwepo kwa malaika na uja wao, na yaliyopokewa katika riwaya zenye tawaturi ya kuongea na malaika ndani ya zama zote, imethibitisha kwa kukinaisha kuwepo kwa malaika na uhusiano wao na sisi kwa kiwango cha kuthibiti kwa kuwepo kwa watu marekani ambao hatujawaona.

Na sasa tazama kwa nuru ya imani katika tunda hili la jumla la pili na ulionje uone vipi kwamba limetia furaha viumbe mwanzoni mpaka mwishoni mwao na kuwaimarisha na kuwapamba na kuwafanya kuwa ni msikiti mkubwa na mahali pakubwa pa kufanyia Ibada.

Basi ulimwengu wenye giza baridi ambao hauna uhai ndani yake – kama mrengo wa kimaada wa kisayansi na falsafa unavyoleta taswira – kwa imani unakuwa ni ulimwengu wenye uhai na utambuzi na wenye nuru na maliwazo na wenye ladha, tunda hili basi linawaonjesha wenye imani mwale katika ladha ya maisha ya kubakia milele na hali ya kuwa bado wakiwa wangali kwenye dunia kila mmoja kulingana na daraja yake.

Ukamilisho:

Kama ilivyo kwamba kwa siri ya umoja na upekee hupatikana uwezo uleule na jina lilelile na hekima ileile na ufundi uleule, katika kila upande kwenye pande miongoni mwa pande za ulimwengu, kila kilichotengenezwa kinatangaza – kiujumla au kisehemu – kwa ulimi wake wa hali: Umoja wa Muumba (s.w), usarifu wake, upatishaji wake, ulezi wake wa kiungu, hali ya uumbaji wake na hali ya utakatifu wake, kadhalika yeye (s.w) anaumba malaika katika pande zote za ulimwengu ili watimize – kwa ndimi zao zenye kudhukuru zenye kuhimidi – kwa tasbihi kila kiumbe anazitimiza kwa ulimi wa hali yake bila hisia. Malaika hawamwasi Allah kwa anayowaamrisha, na hawana isipokuwa ni uja wa dhati na hawana upatishaji wowote uwao, na hawana kuingilia bila idhini, na haiwi kwao shufaa bila idhini kutoka kwake (s.w), na kwa ajili hii wamepata utukufu wa:

 بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ Qur’an, 21:26.

وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ Qur’an, 66:6.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.