Suala La Kumi Ua la Emirdagh

[Jibu la kutosheleza na kukinaisha juu ya upingaji kuhusu kukariri ndani ya Qur’an]

Ndugu zangu wapendwa wa dhati!

Nilikuwa ninasumbuliwa na hali mbaya ya mgongano wakati nikiandika maudhui hii, kwa hiyo imechukuliwa na kiasi fulani cha kufumbika maana kwa sababu ya kubaki kwake kama ilivyo kuja kwa msukumo wa mawazo. Lakini nimetambua kwamba hizo ibara zenye kuchanganya zinabeba muujiza wa  kuvutia. Basi ee majuto yangu mimi! Kwa kushindwa kwangu kutimiza haki ya muujiza huu katika ufundi wa kuelezea vema. Basi ibara za risala vyovyote zitakavyo kuwa zenye nuru fifi isipokuwa zinahesabika – kwa upande wa kuambatana kwake na Qur’an tukufu – ni (ibada ya kifikira) na (chombo) lenye kukusanya lulu za nafsi za juu, basi matarajio ni kuwa msiangalie gamba lake  mtazame kwa makini lulu zake zenye kung’ara zilizomo ndani yake. Mkiziona zenye kufaa hasa basi zifanyeni (Suala la kumi) la Risala ya matunda, na kama si hivyo basi ifanyeni kuwa ni barua tu ya majibu kuhusu pongezi zenu. Ilikuwa dharura kwangu kuiandika kwa ufupi sana kutokana na hali niliyokuwa ninasumbuka nayo ya mlo mbaya na maumivu ya maradhi, hadi kwamba nimeingiza katika kifungu kimoja cha maneno ya Risala hiyo hakika na hoja nyingi, na niliikamilisha – kwa fadhila ya Allah (s.w) – katika siku mbili za masiku ya mwezi wa Ramadhani yenye baraka basi nataraji msamaha ikiwa kuna kasoro zitakazojitokeza kwangu.

Suala hili ni kiua angavu cha mwezi huu mtukufu na kwa mji wa (Emerdagh) limeunganishwa na Tunda la jela ya Denizli ya kwamba ni (Suala la kumi). Nalo kwa idhini ya Allah linaondosha sumu za dhana za uozo wanazozieneza watu wa upotevu kuhusu tukio la kukariri ndani ya Qur’an. na hii kwa kubainisha kwake hekima miongoni mwa hekima zake nyingi. (Mtunzi)

Ndugu zangu wa dhati wa kweli

Nilipokuwa ninasoma Qur’an – yenye ufasaha wa muujiza – katika mwezi wenye baraka (Ramadhani), nilizingatia maana ya aya thelathini na tatu – ambayo ishara yake ipo katika Risale-i Nur katika (Mwale wa kwanza) – nikaona kwamba kila aya kati yake – bali aya katika ukurasa huo kwenye msahafu na maudhui yake – kana kwamba zinachungulia kwenye Risale-i Nur na wanafunzi wake kwa upande wa kupata sehemu ya mwanga wake na kiasi cha maana yake na hasa aya ya nuru katika Surat An-Nur inaashiria Risale-i Nur kwa vidole kumi, kama vilevile aya ambazo zinazoifuatia – nayo ni aya ya giza –  inaangalia wapingaji wa Risale-i Nur na maadui wake bali inawapa fungu kubwa, kwani haifichiki kwamba makamo ya aya hizo na malengo na shabaha zake haziishii katika wakati na mahali maalum, bali inajumuisha zama na mahali pote, yaani inatoka katika hali ya sehemu ya mahali na zama kwenda katika hali ya ujumla, kwa hiyo nimehisi kwamba Risale-i Nur na wanafunzi wake katika zama zetu hizi wanawakilisha – haki ya kuwakilisha – mtu mmoja katika watu wa jumla hiyo yenye kuenea.

Hakika ya kauli ya Qur’an tukufu imevuna sifa ya ujumla, ukunjufu kabisa, hali ya juu na kuzungukia kwa ujumla, kwa sababu ya kuwa inatoka moja kwa moja kutoka katika makamo makunjufu kabisa ya ulezi wa kiungu wa jumla wa Mzungumzaji wa azali (s.w), na inaivuna kutoka katika makamo makunjufu makubwa kwa yule ambaye kitabu hiki kimeteremshwa juu yake, ni huyo mtume mtukufu (s.a.w) mwakilishi wa sampuli ya wanadamu na msemeshwa kwa jina la wanadamu wote, bali kwa viumbe wote, na inaipata pia kutokana na waliosemeshwa katika makamo kunjufu pana kabisa la tabaka la wanadamu wote na kwa zama zote, inapata pia kutoka katika makamo makubwa yenye kuzunguka yenye kuchimbuka kutoka kwenye ufasaha wenye kutosheleza wa kanuni za Allah (s.w) zinazoambatana na dunia na Akhera, kwa Ardhi na Mbingu, kwa azali na Milele, kanuni ambazo zinahusu ulezi wake wa kiungu na unajumuisha mambo ya viumbe wote.

Basi kauli hii tukufu ambayo imevuna ukunjufu, kuinuka kuzunguka, kuenea kiasi cha kuvuna, inadhihirisha muujiza wa kuvutia na kuzunguka kwenye kuenea kwa kiasi kwamba: Ngazi zake za nje na za kimaumbile ambazo zinapendeza fahamu za watu wa kawaida – nao ndio walio wengi wa wanaosemeshwa –  wakati huo huo inatunuku sehemu kubwa kwa ngazi za juu sana za kifikra na tabaka za juu za kiakili, haiwapi wasemeshwa wake kitu kutoka katika maelekezo yake tu, wala haiwatengi wao peke yao kwa mazingatio kutoka katika masimulizi ya kihistoria tu, bali pamoja na hivyo inasemesha kila tabaka kila zama – kwa kuwa kwake ni mmoja katika watu wa kanuni ya jumla – maelezo ya ulingano maridadi mapya kana kwamba ni hivi sasa yanashuka.

Na hasa hasa wingi wa ukariri wake:

(الْظَّالِمِينَ) …(الْظَّالِمِينَ)

na makemeo yake makali kwao na maonyo yake ya kutisha kutokana na kuteremka masaibu ya mbinguni na Ardhini kwa sababu ya dhambi zao na dhulma zao, huzindua macho – kwa kukariri huku – katika kutazama dhuluma zisizokuwa na kifani katika zama hizi, kwa kuonesha aina ya adhabu na masaibu yaliyoshuka kwa kaumu ya Adi, Thamuda na Firauni. Na wakati huo huo inapeleka maliwazo na utulivu katika nyoyo za waumini wenye kudhulumiwa, kwa kueleza kwake kuokoka kwa Mitume watukufu mfano wa Ibrahimu na Musa (a.s).

Hakika hii Qur’an tukufu inaongoza kila tabaka la kila zama maongozi ya wazi kwa muujiza wa kupendeza ikibainisha kuwa: (Zama zilizopita) na enzi zilizoondoka ambazo katika mtazamo wa wenye kughafilika wapotevu ni bonde la kukosekana la kitambo sana lenye kutisha na makaburi yaliyoteketea yenye uchungu na huzuni, inayaonesha hali ya kuwa ni ukurasa ulio hai hutoa mazingatio na masomo, na ulimwengu wa ajabu unatweta uhai na kububujika uhai kutoka mawanda ya mbali hadi mbali yake zaidi, na ufalme wa kiungu inafungamana nasi kwa mahusiano inaibainisha kwa – muujiza wake wa kuvutia – ukiwa wazi kana kwamba inashuhudiwa imehudhurishwa mbele yetu kwenye kioo cha sinema, basi wakati mwingine huja na enzi hizo zikiwa hadhiri mbele yetu na wakati mwingine inatuchukua katika zama hizo.

Na kwa muujiza wenyewe huo huo inabainisha (Ulimwengu) ambao wenye kughafilika wanauona kuwa ni anga lenye kuogofya bila ya ukomo, na vitu visivyo na uhai vyenye kugongana bila roho yoyote vinabimbirika katika balaa la utengano na maumivu, inaainisha Qur’an ukiwa ni kitabu fasaha, amekiandika Mpweke Mtegemewa kwa haja zote, na mji ulioratibika ameuimarisha Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, na maonesho mazuri ameyaweka Bwana mlezi Mkarimu ili kutangaza kazi zake. Kwa ufafanuzi huu anatia uhai katika vitu hivyo visivyo na uhai na kujaalia baadhi yake hujitahidi kuvipa msaada vingine, na kila sehemu inaisaidia nyingine kana kwamba inafanya mazungumzo nayo kwa mapenzi ya dhati kabisa, kila kitu kimetiishwa na kila kitu kimekabidhiwa jukumu na wajibu, na kama hivi Qur’an inatoa masomo ya hekima ya hakika na elimu yenye kunawirisha kwa wanadamu, majini na malaika wote. Basi hapana shaka kwamba Qur’an hii tukufu – ambayo ina muujiza huu katika kubainisha – ni yenye kustahiki kuwa na sifa maalum za hali ya juu na sifa pambanuzi takatifu za kuheshimika sana mfano:

Katika kila herufi yake moja kuna mema kumi bali wakati mwingine mema elfu moja, bali maelfu ya mema katika nyakati nyingine, na majini na watu wameshindwa kuleta mfano wake japo wangali kusanyika kwa hilo, na kuzungumza kwake na wanadamu wote bali viumbe wote mazungumzo ya ufasaha na yenye hekima. Na pupa ya mamilioni ya watu katika kila zama katika kukihifadhi kwa moyo kwa shauku na kufurahia, na kutochoka kutokana na kukisoma mara nyingi licha ya kukariri kwake, na kutulia kwake tuli kwenye fahamu za watoto wadogo nyororo nyepesi pamoja na kuwemo na vifungu na maeneo yenye kuwachanganya, na kupata ladha wagonjwa na wenye kukata roho kwa kuisikiliza – ambao husumbuka kusikiliza japo maneno madogo sana – na kupita kwa hiyo Qur’an kwenye masikio yao ikiwa tamu nzuri. Na nyingi nyinginezo katika sifa tukufu ilizonazo Qur’an tukufu, hivyo inawapa wasomaji na wanafunzi wake aina kwa aina za furaha za makazi mawili.

Na inadhihirisha muujiza wake mzuri pia katika (Mtindo wa maelekezo yake ya fasaha) ambapo imechunga vema hali ya mfikishaji wake ya kuwa ni Ummiyyu (Sio msomaji wa maandishi) kwa kuhifadhi kikamilifu urari wake wa kimaumbile, ni tukufu zaidi kukaribiwa na taklifa, kujifanyisha au ria – vyovyote iwavyo aina yake – basi mtindo wake ni wenye kuchukulika kwa watu wa kawaida ambao wao ndio wenye kusemeshwa walio wengi ikielekeza upole kwenye wepesi wa fahamu zao kwa kushuka kwa maneno yalio karibu na fahamu zao, hali ya kukunjua mbele yao kurasa zilizo wazi kabisa kama kudhihiri kwa mbingu na ardhi, Ikielekeza macho kwenye miujiza ya kiuweza wa kiungu na mistari ya hekima yake ya upeo, vyenye kudhamiriwa chini ya vitu na mambo ya kawaida.

Kisha Qur’an tukufu inadhihirisha aina moja wapo katika aina za muujiza wake wa ajabu pia katika (Kukariri kwake kwa ajabu) kwa fungu moja la maneno, au kisa kimoja, na hii wakati wa kuashiria tabaka mbali mbali za wenye kusemeshwa katika maana chungu nzima na mazingatio mengi kwenye aya au kisa hicho, ikahitajika kukariri kwa kuwa hicho ni kitabu cha dua, daawah kama kilivyo pia ni kitabu cha dhikiri na tawhiid, na kila moja kati ya haya yanahitajia kukariri, kila kilichokaririwa katika Qur’an tukufu kwa hiyo katika aya au kisa hakika kinabeba maana mpya na mazingatio mapya.

Na inadhihirisha muujiza wake pia wakati wa kuongelea (Matukio ya kisehemu) yaliyotokea  wakati wa masahaba wema wakati wa kuteremka kwake na kusimika jengo la Uislamu na misingi ya sharia, hivyo basi unaiona inayachukulia matukio hayo kwa mtazamo wa kutilia muhimu sana, kwa kubainisha kupitia matukio hayo kwamba  mambo nyeti zaidi ya matukio madogo mno ya kisehemu, hakika hayo katika mtazamo wa rehema yake (s.w), na yapo ndani ya duara la uendeshaji wake na utashi wake, ukiachilia mbali ya kwamba kwa matukio hayo inadhihirisha sunna za kiungu zinazopita kwenye ulimwengu na kanuni za jumla zenye kuenea. Ongezea juu ya hayo kwamba matukio hayo – ambayo ni sawa na mbegu wakati wa kuasisi Uislamu na sharia – zitatoa matunda katika nyakati zijazo matunda manono ya hukumu na faida mbali mbali.

Hakika kukariri kwa uhitaji kunalazimu kukariri, hii ni kanuni iliyothibiti, kwa hiyo Qur’an tukufu imejibu maswali mengi yaliojirudia rudia ndani ya miaka ishirini, ikaelekeza tabaka tofauti za wanaosemeshwa kwa kujibu kwake kwa namna ya kurudiarudia, inakariri mafungu ya maneno ambayo yenye maelfu ya natija, na inakariri maelekezo ambayo ni matokeo ya dalili zisizo na mpaka. na hii wakati wa kutilia mkazo katika fahamu na kuthibitisha kwenye nyoyo juu ya mapinduzi makubwa na mabadiliko ya kutisha kwenye ulimwengu yatakayotokea na kudamirika kutakaousibu ulimwengu na kuvunjika vunjika sehemu, (Zinazounda vitu mbali mbali) na hali itakayofuatia ya ujenzi wa Akhera ya kudumu milele ya kupendeza  badala ya ulimwengu huu wenye kutoweka.

Kisha inakariri mafungu hayo ya maneno na aya vilevile wakati wa kuthibitisha kwamba sehemu zote (zinazo unda vitu vizima) na jumla (Vitu vizima) kuanzia atomu hadi nyota hakika vipo katika shiko la mmoja wa pekee (s.w) na ndani ya usarifu wake (s.w).

Na inakariri pia katika ufafanuzi wake ghadhabu ya kiungu na kuchukia kwa Mola mlezi dhidi ya mwanadamu mwenye kutenda dhuluma nyingi wakati wa kukiuika kwake lengo la kuumbwa, dhuluma ambazo zinachokoza hisia za viumbe na Ardhi na mbingu na chembe za vitu na kukoleza ghadhabu yake dhidi ya watendaji wa dhuluma hizo.

Kwa hiyo kukariri kwa sentensi hizo na aya katika kubainisha mambo kama haya makubwa ya kutisha sio tu haihesabiwi kuwa ni upungufu katika ufasaha bali ni katika muujiza katika ubora na ufundi mkubwa na ufasaha wa hali ya juu sana na uwazi – bali  ufasaha – wenye kuendana na muktadha wa hali kikamilifu. Kwa mfano:

Hakika fungu la maneno

(بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ)

ni aya moja imekariri mara mia moja na kumi nne ndani ya Qur’an Tukufu ni kwa sababu aya hiyo ni hakika kubwa inajaza ulimwengu nuru na mwanga, na kushikamanisha tandiko na arshi kwa fungamano madhubuti – kama tulivyobainisha katika mng’ao wa kumi na nne – hakuna yeyote ila anayo haja kubwa ya hakika hii katika kila wakati – ikiwa hakika hii kuu itakariri mamilioni ya mara uhitaji bado upo unaendelea kuwepo haitazima kiu, kwani sio haja ya kila siku kama mkate bali pia kama hewa na mwanga ambavyo huhitajika sana na kufanyiwa shauku kila dakika.

Na hakika ya aya tukufu:

(وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

inakariri mara nane katika Surat Al- Shuaraa, kukariri kwa aya hii tukufu ambayo inabeba maelfu ya hakika katika sura inayoelezea kuokoka kwa manabii (a.s) na adhabu ya kaumu zao, hakika sio kwa sababu yoyote ila ni kwa ajili ya kubainisha: Kwamba dhuluma ya kaumu zao zinagusa lengo la kuumbwa, na kuingilia katika adhama ya ulezi usiyo na mpaka, enzi ya kiungu inahitajia kuwaadhibu kaumu hizo dhalimu kama rehema ya kiungu inavyohitajia kuokoka kwa manabii (a.s). Ikiwa aya hii itakariri maelfu ya mara bado haja na shauku isingemalizika, kukariri hapa ni ufasaha wa hali ya juu wenye muujiza na muhtasari.

Vilevile aya tukufu:

(فَبِأَيِّ آلَاء رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ)

iliyokariri katika Surat (Al- Rahman) na aya tukufu

(وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ)

iliyokariri katika Surat (Al-Mursalat) zote hizo zinapiga kelele usoni mwa zama zote na kutangaza wazi wazi katika maeneo ya mbingu na Ardhi kwamba ukafiri wa majini na watu na kukanusha kwao neema, na dhuluma zao mbaya kunaamsha ghadhabu za viumbe na kujaalia mbingu na ardhi katika kero na hasira juu yao. Na kuhalifu hekima na makusudio ya kuumbwa kwa ulimwengu. Na kukiuka haki za viumbe wote na kudharau adhama ya kiungu na kuikanusha pia, kwa hiyo aya hizi mbili zinafungamana na maelfu ya mfano wa hakika hizi, na zina umuhimu na nguvu ya maelfu ya masuala, ikiwa zitakariri maelfu ya mara katika kauli ya jumla iliyoelekezwa kwa majini na watu bado dharura ingeendelea kuwepo na haja ingebakia kuwepo. Kwa hiyo kukariri hapa ni balagha ya muhtasari tukufu na muujiza mzuri.

liyokariri katika Surat (Al-Mursalat) zote hizo zinapiga kelele usoni mwa zama zote na kutangaza wazi wazi katika maeneo ya mbingu na Ardhi kwamba ukafiri wa majini na watu na kukanusha kwao neema, na dhuluma zao mbaya kunaamsha ghadhabu za viumbe na kujaalia mbingu na ardhi katika kero na hasira juu yao. Na kuhalifu hekima na makusudio ya kuumbwa kwa ulimwengu. Na kukiuka haki za viumbe wote na kudharau adhama ya kiungu na kuikanusha pia, kwa hiyo aya hizi mbili zinafungamana na maelfu ya mfano wa hakika hizi, na zina umuhimu na nguvu ya maelfu ya masuala, ikiwa zitakariri maelfu ya mara katika kauli ya jumla iliyoelekezwa kwa majini na watu bado dharura ingeendelea kuwepo na haja ingebakia kuwepo. Kwa hiyo kukariri hapa ni balagha ya muhtasari tukufu na muujiza mzuri.

Na tunaelezea mfano mwingine kuhusu hekima ya ukariri katika hadithi ya Nabii (s.a.w), Munaajaat wa mtume unaoitwa (Al-Jaushan al-kabiir)ni Munaajaat mzuri wenye kuendana na hakika ya Qur’an tukufu na ni kielelezo kilichopatikana kutokea huko. Tunaona ndani yake fungu la maneno:

(سُبْحَانَكَ يَا لاَإِلَهَ إِلَّا أَنْتَ الأَمَانُ الأَمَانُ خَلِّصْنَا مِنَ النَّارِ.. أَجِرْنَا مِنَ النَّارِ.. نَجِّنَا مِنَ النَّارِ)

vifungu hivi vinajirudia mara mia moja, vingejirudia maelfu ya mara visingeleta uchovu kwa sababu vinabeba hakika tukufu katika ulimwengu, nayo ni Tawhid na jukumu tukufu sana la viumbe kumwelekea Mola wao mlezi mtukufu nayo ni Tasbihi, Tahamiid na Takdisi na kadhia kuu kabisa ya kihatima ya wanadamu nayo ni kuokoka kutokana na moto na kukomboka kutokana na mateso ya milele, na lengo la lazima sana la uja na la kushindwa kwa mwanadamu nayo ni dua.

Na kama hivi tunaona mifano ya misingi hii katika yaliyomo katika aina za ukariri ndani ya Qur’an tukufu. Hata tunaona kwamba inaelezea zaidi ya mara ishirini kuhusu hakika ya tawhiid – kwa uwazi au kwa madhumuni – ndani ya ukurasa mmoja wa Msahafu na hiyo ni kulingana na muktadha na haja ya lazima katika kufahamisha, na balagha ya ufasaha, huamsha shauku kwa kukariri kisomo na kwa hivyo kuipa nguvu balagha na heshima bila ya kusababisha uchovu au unyong’onyo.

Sehemu za Risale-i Nur zimefafanua hekima ya kukariri katika Qur’an tukufu na kubainisha hoja zake na kuthibitisha kiasi cha uwiano wa kukariri na kuchukuana kwake na balagha na kiasi cha uzuri wake na kupendeza kwake mno.

Ama tofauti ya hekima za sura za Makka na za Madina kwa upande wa balagha na kwa upande wa muujiza na katika upambanuzi na kujumuisha ni kama ifuatavyo:

Hakika ya safu ya kwanza ya watu waliosemeshwa na wapingaji huko ndani ya Makka walikuwa Washirikina wa kikuraishi na ni wajinga hawakuwa na kitabu, balagha ikahitajia mtindo wa hali ya juu wenye nguvu na ujumuishi wa kimuujiza wenye kukinaisha, na ukariri unaolazimu kuthibitisha maana katika fahamu, na kwa hiyo aghalabu ya sura za Makka zimeelezea nguzo za imani na ngazi za Tawhiid kwa mtindo uliyo katika upeo wa nguvu na kiwango cha juu, na kwa muhtasari wa kimuujiza mno na kukariri sana imani ya kuamini Allah (s.w) na mwanzo na Akhera, bali imeeleza nguzo hizo za kiimani katika kila ukurasa au aya au katika fungu moja la maneno au katika neno moja, pengine huelezea katika herufi moja, katika kutanguliza na kuchelewesha, au katika maana mahususi au maana ya jumla, katika kuacha kutaja au kutaja. Ikathibitisha nguzo za imani katika mifano ya hali hizo na miundo ya kibalagha kuthibitisha kulikowafanya wanazuoni wa balagha na viongozi wao wasimame kwa kutahayari wakishangazwa mbele ya mtindo huu wa kimuujiza. Risale-i Nur imefafanua na hasa (Neno la ishirini na tano (Miujiza ya Qur’an)) – na nyongeza zake – muujiza wa Qur’an kwa namna arobaini katika namna zake, na kadhalika tafsiri ya (Ishaarat al-I’jazi fy madhan al-Ijaz) kwa lugha ya Kiarabu ambayo inabainisha vizuri muujiza wa Qur’an kwa upande wa namna ya utungo baina ya aya za Qur’an. Risala zote mbili zimethibitisha hasa kuwa juu kwa mtindo wa kibalagha wa kipekee na kuwa juu kwa muhtasari wa kimuujiza.

Ama aya za Madina na sura zake katika safu ya kwanza ya wasemeshwa wake na wapingaji wake walikuwa katika Mayahudi na Manasara nao ni watu wa kitabu wenye kumuamini Allah (s.w), kanuni za balagha na mitindo ya kuelekeza na misingi ya tablighi ilihitajia maelezo yenye kuelekezwa kwa watu wa kitabu yawe yanaambatana na hali yao halisi, ikaja na mtindo mwepesi wa wazi laini pamoja na ubainifu na ufafanuzi katika sehemu ndogo ndogo – bila ya mashina na nguzo za imani – kwa sababu sehemu hizo ndogo ndio chimbuko la hukumu za kimatawi na kanuni za kijumla, na eneo la hitilafu katika sharia na hukumu. Kwa ajili hiyo aghalabu tunaziona aya za Madina zikiwa wazi nyepesi kwa mtindo wa ubainifu wa kimuujiza maalum kwa Qur’an tukufu. Lakini kutaja kwa Qur’an mjengo wa nguvu au natija iliyofupishwa au hitimisho lililopangika au hoja yenye nguvu baada ya tukio la sehemu ndogo la kitawi, hufanya tukio hilo la sehemu ndogo kuwa ni kanuni ya jumla enevu, na baada ya hapo hudhamini utekelezaji wake kwa kuimarisha imani ya kuamini Allah (s.w) ambayo huhakikishwa na kutaja vipambanuzi hivyo vya mwisho vilivyofupishwa vya tawhidi, imani na Akhera. Utaona kwamba makamo hayo ya wazi, mepesi yanapata nuru na kuinuka juu kwa vipambanuzi hivyo vya mwisho. – Hakika Risale-i Nur imebainisha na kuthibitisha hata kwa wakaidi kiasi cha balagha ya hali ya juu na sifa pambanuzi za juu na aina za usheheni wa thamani madhubuti za hali ya juu katika mijengo hiyo na vipambanuzi nayo katika sifa kumi na nukta kumi katika nuru ya pili katika mwako wa pili katika neno la ishirini tano linalohusu muujiza wa Qur’an – ukitaka tazama:

 (إنَّ اللّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ )

(وَهُوَ الْعَزِيزُ الْرَّحِيمُ)

(وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ)

(أنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ)

na mifano yake katika aya ambazo zinafidisha tawhidi na kukumbusha Akhera, na ambazo huishia aghalabu ya aya tukufu, utaona kwamba Qur’an tukufu katika kubainisha hukumu za kisharia za kimatawi na kanuni za kijamii huinua mtazamo wa msemeshwa katika mawanda ya juu ya jumla matukufu, na kubadilisha – kwa vipambanuzi hivi vya kuhitimishia – Mtindo huo mwepesi ulio wazi, mtindo wa ngazi ya juu, Kana kwamba inamhamisha msomaji kutoka katika darsa la kisheria na kwenda katika darsa la tawhiid. Hivyo basi kuthibitisha kuwa Qur’an ni kitabu cha shari, hukumu na hekima, kama kilivyo ni kitabu cha itikadi na imani, nacho pia ni kitabu cha dhikiri na tafakuri, kama pia ni kitabu cha dua na daawah.

Na kama hivyo utaona kuwa kuna namna wa ufupisho wa muujiza wenye kung’ara katika aya za Madina ambao sio ile balagha ya aya za Makka kulingana na tofauti ya muktadha na aina za makusudio ya uongozi na ufikishaji.

Unaweza kuona namna hii katika maneno mawili tu:

( رَبُّكَ)

na

(رَبِّ الْعَالَمِينَ)

kwani inajulisha upweke kwa ibara ya

(رَبُّكَ)

na inaelewesha umoja kwa,

(رَبِّ الْعَالَمِينَ)

kwa kujua kwamba umoja unajumuisha pia upekee.

Bali unaweza kuona mtindo huo wa balagha ndani ya fungu moja la maneno unakuonesha kwa mfano katika aya moja utendaji wa ujuzi wake mahali pa atomu katika kipenyo cha jicho na mahali lilipo jua katikati ya anga, na kuzunguka kwa uweza wake ambao kwa zana moja unaweka kila kimoja katika mahali pake, ukijaalia jua kana kwamba ni jicho la mbingu unafuatilishia:

(وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُور)

baada ya aya

يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ Qur’an, 57:6.

yaani unafuatilishia utendaji wa ujuzi wake (s.w) katika vilivyojificha vifuani baada ya kutaja kwake adhama ya mbingu na ardhi na kuikunjua mbele ya macho, unafanya ithibiti katika fahamu kwamba yeye anajua yanayopita kwenye nyoyo na mambo yake yaliyojificha ndani ya utukufu wa uumbaji wake wa Mbingu na Ardhi na uendeshaji wa mambo yake. Kimalizio hiki:

(وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُور)

ni aina karibu katika fahamu za watu wa kawaida – unaugeuza kuwa ni mwongozo wa ngazi ya juu na tablighi enevu ya kuvutia.

Swali:

Hakika mtazamo wa juu juu wa mpito hauwezi kuona yanayoletwa na Qur’an tukufu miongoni mwa hakika zenye umuhimu wala haujui aina ya munasaba na uhusiano kati ya vipande vinavyoelezea Tawhiid ya ngazi ya juu au kufidisha kanuni ya kiujumla, na kati ya tukio la sehemu ndogo lenye kuzoeleka kwa ajili hii baadhi wanadhani kuwa kuna chochote cha kasoro kwenye balagha, kwa mfano haudhihiri munasaba wa kibalagha katika kutaja kanuni kuu:

(وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ)

kufuatia tukio la sehemu ndogo nalo ni Yusuf (a.s) kumpa makao ndugu yake kwa mpango wa busara. Inaombwa kubainisha siri  katika hilo na kufunua pazia la hekima yake?

Jibu:

Kwamba aghalabu ya sura ndefu na za kati kati – ambazo kila moja kati ya hizo ni kana kwamba ni Qur’an pekee – haitosheki na makusudi mawili au matatu katika makusudio ya Qur’an tukufu   manne (Nayo ni: Tawiid, Unabii, Ufufuo, Uadilifu pamoja na Uja) bali kila moja kati ya hizo inabeba kiini cha Qur’an yote na makusudio manne kwa pamoja, yaani kila moja ni kitabu cha dhikri, imani na fikira, kama kitabu cha sharia, hekima na mwongozo. Kila sura katika sura hizo inakusanya vitabu vingi, na inaelekeza masomo mbali mbali, Utaona kwamba kila kituo – bali hata ukurasa mmoja – unafungua milango ya imani mbele ya mwanadamu inahakikishia kuthibiti makusudio mengine, ambapo Qur’an inaeleza yaliyoandikwa kwenye kitabu kikubwa cha ulimwengu na kukibainisha kwa ufasaha, inatia nguvu fahamu za kina za muumini kuzungukia ulezi wake wa kiungu (s.w) kwa kila kitu, na kumwonesha midhihirisho yake ya kutisha katika anga na katika nafsi. Hakika kinachoonekana kuwa uwiano dhaifu, hujengewa makusudio ya jumla, hapo hukutana uwiano madhubuti na mahusiano ya nguvu kwa uwiano huo dhaifu kwa nje, kwa hiyo mtindo unawiana kabisa na muktadha huo, kwa hiyo ngazi yake ya kibalagha inapanda na kuwa ya juu.

Swali lingine: Ni nini hekima ya Qur’an kuelezea maelfu ya dalili kwa ajili ya kuthibitisha mambo ya Akhera na kufundisha Tawhiid na kuwapa thawabu wanadamu? Na kuna siri gani katika kuzindua watu watazame mambo hayo kwa uwazi na kwa madhumuni na kwa ishara  katuika kila sura bali katika kila ukurasa kwenye Msahafu na katika kila kituo?

Jibu: Kwa kuwa Qur’an tukufu inamtanabahisha mwanadamu kuhusu mapinduzi makubwa mno yatakayotokea ndani ya viumbe na katika eneo la yamkini katika historia ya Ulimwengu, nayo ni Akhera. Na inamwongoza kwenye suala kubwa linalomhusu naye akiwa ndiye mbebaji wa amana kubwa na Ukhalifa wa ardhi, hilo ni suala la Tawhiid ambalo furaha na mateso yake ya milele yanazunguka katika eneo hilo. Na wakati huo huo Qur’an inaondoa mfereji wa utata mwingi uliopo bila kukatika, na kuvunja aina ngumu zaidi ya upingaji na ukanushaji wenye chuki.

Kwa ajili hiyo lau kama Qur’an itaelekeza mitazamo kwenye kuamini hayo mageuzi ya ajabu na kuwafanya wengine kusadikisha suala hilo kuu kidharura kwa Wanadamu, Naam, ingefanya hivyo maelfu ya mara na kukariri masuala hayo mamilioni ya mara, kwake haihesabiwi kuwa ni Israfu katika Balagha katu, kama kufanya hivyo kusivyoleta uchovu wala unyong’onyo kabisa, bali haja ya kukariri usomaji wa Qur’an haikatiki kwani hakuna suala muhimu wala kubwa zaidi katika uwepo kuliko tawhiid na Akhera.

Mathalani: Hakika ya aya tukufu:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ Qur’an, 85:11.

ni bishara ya furaha ya kudumu milele inaieleza aya hii tukufu kwa mwanadamu masikini ambaye anakutana na hakika ya umauti kila wakati, bishara hii kwa hiyo inamwokoa kutokana na kuleta taswira ya umauti kuwa ni kunyongwa kwa milele na kumwokoa – na ulimwengu wake na wapendwa wake wote – kutokana na shiko la kutoweka bali inamtunuku ufalme wa milele na kumpa mavuno ya furaha ya kudumu. Ikiwa aya hii tukufu itakariri mabilioni ya mara katu kukariri kwake hakuhesabiwi kuwa ni Israfu katu wala hakigusi kitu chochote balagha yake.

Na kama hivi unaona Qur’an tukufu ambayo inashughulikia mifano ya masuala haya muhimu na kujitahidi kuwakinaisha walengwa wa masuala hayo kwa kusimika hoja zenye nguvu, inayaweka kwa kina kwenye akili na nyoyo mageuzi hayo makubwa na mabadiliko makubwa kwenye ulimwengu, na kufanya kuwa mepesi na wazi mbele yao kama kubadilika nyumba na kugeuka kwa umbo lake. Hapana budi kwamba kuzindua mitazamo kuelekea masuala kama haya – kwa uwazi na kwa madhumuni na kwa ishara – kwa maelfu ya mara ni jambo la kidharura sana bali hilo ni kama dharura ya mwanadamu kuhitajia mkate, hewa na mwanga ambavyo uhitaji wa mwanadamu kwa vitu hivyo hukariri daima.

Na mathalani: Hekima ya kukariri kwa Qur’an tukufu

وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ Qur’an, 35:36.

إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ Qur’an, 14:22.

na mfano wa hizo katika aya za kuonya na vitisho. Na kuelezea kwake kwa miundo iliyo katika upeo wa ukali – ni kama vile tulivyothibitisha katika Risale-i Nur kwa namna ya kukinaisha – hakika ukafiri wa mwanadamu hakika ni kukiuka – kukiuka kwa hali ya juu – haki za viumbe na mno ya viumbe, jambo ambalo linaamsha ghadhabu ya mbingu na Ardhi na kujaza kero na chuki katika nyoyo za aina mbali mbali juu ya makafiri, hadi aina hizo zinapiga kofi makafiri hao kwa tufani na mengineyo. Bali hata moto wa jahimu unawaghadhibikia ghadhabu ambayo inakaribia kulipuka kutokana na ukali wake kama ilivyo wazi katika aya:

إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُور

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظ Qur’an, 67:7-8.

Lau kama angekariri mfalme wa ulimwengu katika amri zake jinai hilo kubwa (kufuru) na adhabu yake kwa mtindo wa upeo wa kukemea na ukali maelfu ya mara, bali mamilioni ya mara, bali mabilioni ya mara isingehesabiwa hiyo ni israfu kabisa wala upungufu katika balagha,  kwa kuangalia ukubwa wa jina hiyo ya jumla na kukiuka haki zisizokuwa na mpaka, na kwa msingi wa kudhihirisha hekima ya haki za raia wake (s.w) na kudhihirisha ubaya usiokoma katika ukafiri wa wakanushaji na udhalimu wao mbaya. Kwani hakariri hilo kwa sababu ya udogo wa mwanadamu na uduni wake bali kwa ukubwa wa ukiukaji wa kafiri na ukubwa wa dhuluma yake.

Kisha hakika tunaona kwamba mamia ya mamilioni katika watu tangu elfu na mamia ya miaka wanaisoma Qur’an kwa pupa na shauku na kwa kuihitajia sana bila unyong’nyo wala uchovu.

Naam, hakika kila wakati na kila siku hakika ni ulimwengu unaopita na ni mlango unaofungulia ulimwengu mwingine, na kwa hiyo kukariri kwa:

(لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ)

kwa shauku ya kuihitajia maelfu ya mara kwa ajili ya kuangazia limwengu hizo zenye kutembea zote na kuzinawirisha kwa nuru ya Imani, inafanya fungu hilo la kitawhiid kana kwamba ni taa yenye nuru katika mbingu za limwengu hizo na masiku. Basi kama jambo hili lilivyo hivi katika:

(لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ)

kadhalika kusoma Qur’an tukufu hutokomeza giza lililogubika juu ya uwingi huo chungu tele katika shahidi zenye kutembea, na kwa limwengu hizo zenye kutembea zenye kurudia upya, na kuondosha kuharibu sura zake zenye kuakisi katika kioo cha uhai, na kufanya hali hizo zinazokuja kuwa ni mashahidi wake siku ya kiama na sio mashahidi dhidi yake. Na kupanda katika ngazi ya maarifa ya ukubwa wa malipo ya jinai, na kumfanya atambue thamani ya maonyo yaliojificha ya mfalme wa azali na milele ambazo zinatawanya ukaidi wa madhalimu matwaghuti,na kumpa shauku akomboke na uchupaji wa nafsi yenye kuamrisha maovu, basi kwa ajili ya hekima hizi zote Qur’an tukufu inakariri inayokariri katika upeo wa hekima kwa kudhihirisha kwamba maonyo mengi ya Qur’an tukufu ni kwa kiasi hiki, na kwa nguvu na ukali na ukariri huu ni hakika kubwa, Shetani anashindwa kwa kuidhania kuwa ni batili na anakimbia kuifikiria kuwa ni mchezo.

Naam hakika adhabu ya jahanamu ndio uadilifu wenyewe kwa ajili ya hao makafiri ambao hawasikilizi kabisa maonyo.

Na katika vinavyokaririwa vya Qur’an (Visa vya manabii (a.s)), basi hekima katika kukariri kwa kisa cha Musa (a.s) – mathalani – ambacho kina hekima na faida ambayo imo katika fimbo ya Musa (a.s), na kadhalika hekima katika ukariri wa visa vya manabii hakika ni kwa ajili ya kuthibitisha utume wa Muhammad (s.a.w), na hii ni kwa kudhihirisha unabii wa manabii wote ni hoja ya  u-haki wa utume wa nabii Muhammad (s.a.w) na ukweli wake, kiasi kwamba hawezi kukanusha isipokuwa anayekanusha unabii wao wote, basi kuutaja basi ni dalili ya utume.

Kisha hakika wengi wa watu hawawezi kila wakati na wala  hawawafikishwi katika kusoma Qur’an tukufu yote, bali wanatosheka na kilichokuwa chepesi kwao katika Qur’an. Na kutokea hapa hekima inaonekana kuwa wazi katika kufanya kila sura ndefu na ya kati na kati kwa mfano wa Qur’an ndogo, na hivyo kukariri kwa visa ndani ya sura hizo ni kwa mfano wa kukariri kwa nguzo za Imani za lazima. Yaani kwamba kukariri kwa visa ni hitajio la kibalagha na katika kufanya hivyo katu  hakuna israfu. Ongezea juu ya hilo ndani yake kuna ujulisho kwamba tukio la kudhihiri kwa Muhammad (s.a.w) ni tukio kubwa sana kwa Wanadamu na suala muhimu mno katika masuala ya ulimwengu.

Naam, hakika kuipa dhati ya mtume (s.a.w) makamo makuu na ya juu zaidi katika Qur’an tukufu, na kujaalia (Muhammad Rasulullah) – ambayo inajumuisha nguzo nne katika nguzo za imani – ikiunganishwa na

(لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ)

ni dalili – na dalili iliyoje – kwamba utume wa Muhammad (s.a.w) ni hakika kubwa ulimwenguni na kwamba Muhammad (s.a.w) ni mbora mno wa viumbe wote na kwamba hakika ya Muhammad (s.a.w) ambayo inawakilisha alShakhsiyyat al maanawiyyat (Haiba ya pamoja) ya ujumla ya Muhammad (s.a.w) ni taa yenye kuangaza kwa limwengu zote mbili, na kwamba (s.a.w) ni mwenye stahiki ya makamo haya yenye kufurutu ada kama ilivyo thibitishwa hivyo katika sehemu za Risale-i Nur kwa hoja na dalili nyingi kwa namna ya kukinaisha. Hapa tunaileta mojawapo kati ya elfu moja kama ifutavyo:

Hakika yote waliyofanya umati Muhammad wote (s.a.w) katika mema katika zama zote huandikwa mfano wake katika daftari la mema yake mtume (s.a.w), na hii kulingana na kanuni: (Sababu kama mfanyaji) na hakika kutia kwake nuru kwa hakika zote za viumbe kwa nuru aliyokuja nayo haifanyi majini, wanadamu na malaika na wenye uhai katika kushukuru na kuridhia wao peke yao, bali inajaalia ulimwengu wote na mbingu na ardhi vyote kuwa vyenye kumridhia na kuzungumza fadhila zake, na hakika mamilioni ya dua ambazo wema wa umma huu wanazozielekeza kila siku na pamoja na wema katika mabilioni ya dua za kimaumbile zenye kujibiwa ambazo hazirejeshwi – kwa dalili za kukubaliwa kimatendo kunakoshuhudiwa kwa dua za mimea kwa ulimi wa kimaandalizi, na dua za wanyama kwa ulimi wa haja ya kimaumbile – na kutokana na dua za rehema kwa kumswalia na kumsalimu yeye na wanayoyatuma katika waliyoyavuna miongoni mwa mavuno ya kimaanawy na mema kama zawadi, hakika hupelekwa kwake kwanza. Ukiachilia mbali yale yanayoingia katika daftari la mema yake (s.a.w) miongoni mwa nuru zisizo na mipaka kwa wanachosoma umma wake – kwa kusoma tu – Qur’an tukufu ambayo kwa kila herufi miongoni mwa herufi zake – ambazo zinazidi mia tatu elfu – mema kumi na matunda kumi ya kiakhera bali mia bali elfu ya mema.

Naam, hakika ya mjuzi wa mambo ya ghaibu (s.w) imetangulia elimu yake na kushuhudia kwamba hakika ya Muhammad ambayo ni haiba ya kimaanawy ya pamoja ya dhati hiyo yenye baraka, itakuwa kama mfano wa mti wa Tuba huko peponi, kwa hiyo akaipa umuhimu mkubwa katika Qur’an yake umuhimu huo mkubwa ambapo yeye ndiye mwenye kustahiki makamo hayo ya juu. Na akabainisha katika amri zake kwamba kupata shufaa yake hakika huwa tu kwa kumfuata yeye na kufuata sunna yake tukufu nalo ni suala kubwa mno katika masuala ya mwanadamu. Bali amechukua kwa jicho la mazingatio – mara kwa mara – hali zake za kibinadamu ambazo ni sawa na mbegu ya mti wa Tuba katika pepo.

Na kama hivi hakika za Qur’an zilizokariri zina thamani hii ya juu na ndani yake kuna hekima kiasi kilichomo ndani yake katika hekima, maumbile salama yanaona kwamba katika kukariri kwake kuna muujiza wa kimaanawy wenye nguvu na mpana, isipokuwa ambaye moyo wake na hisia zake za ndani zimeugua kwa tauni ya mrengo wa kimaada, basi anaingia katika kanuni mashuhuri:

Huenda mtu akakanusha Mwanga wa jua kwa sababu ya maradhi ya macho

Na kinywa hukanusha ladha ya chakula kutokana na ugonjwa

Ubeti ni wa Mshairi Sharaf ad-Diin Al-Buswiry ndani ya Kasida ya Al-Burdah:

Jicho linaweza kukana mwanga wa jua kwa sababu ya ugonjwa wake.

Na kinywa hukana ladha ya maji kutokana na maradhi mwilini.

Hitimisho la kumi ndani ya sehemu mbili za maelezo

Sehemu ya kwanza:

Masikio yangu yaligongwa na habari kabla ya miaka kumi na mbili kwamba mzandiki mkaidi nia yake mbaya imefedheheka na uhabithi wa makusudio yake kwa kutaka kuitafsiri Qur’an, akasuka mpango wa kutisha ili kuidhalilisha heshima yake kwa kujaribu kuitafsiri. Na akasema wazi: Ifasiriwe Qur’an ili idhihiri thamani yake? Yaani ili watu wapate kuona kukariri kwake kusiko kwa lazima! Na tafsiri yake isomwe badala yake! Hadi mwisho wake katika fikira zenye sumu. Isipokuwa Risale-i Nur – kwa fadhili ya Allah (s.w) – imevunja fikira hiyo na kuporomosha mpango huo kabla haujazaliwa kwa hoja zake zenye nguvu na kwa kuenea kwake kupana kila mahali, Ikathibitisha kwa uthibitisho wa kukinaisha kwamba haiwezekani kamwe kuitafsiri Qur’an tafsiri ya hakika na kwamba lugha yoyote isiyokuwa lugha ya Kiarabu fasaha haina uwezo wa kuhifadhi sifa bainifu za Qur’an tukufu na nukta zake nyororo za kibalagha, na kwamba tafsiri za kawaida za kibaadhi ambazo wanadamu wanazifanya hazikai – kwa hali yoyote ile – mahali pa maelezo yenye kujumuisha yaliyo muujiza ya maneno ya Qur’an ambayo katika kila herufi moja miongoni mwa herufi zake kuna mema yanayopanda kutokea kumi hadi elfu, na kwa hiyo haiwezekani kamwe kusoma tafsiri ikiwa badala yake.

Licha ya kwamba wanafiki ambao waliojifunza kwa yule mzandiki wamejitahidi kwa majaribio ya hasira katika njia ya shetani ili kuzima nuru ya Qur’an tukufu kwa vinywa vyao. Lakini nilivyokuwa sikutani na yeyote sina ninalojua kuhusu hakika ya hali zinayoendelea, lakini dhana yangu mno niliyoyaeleza huko nyuma ndiyo sababu iliyopelekea kuandika (Suala hili la kumi) juu yangu licha ya dhiki inayonizingira.

Sehemu ya pili ya maelezo:

Siku moja nilikuwa nimekaa katika ghorofa ya juu ya Hoteli ya (Şehir) baada ya kuruhusiwa kwetu kutoka jela ya (Denizle), nikichunguza miti iliyonizunguka ya (matete) iliyo mingi katika viunga venye sauti za kupendeza na bustani nzuri, niliiona ikiwa na furaha na kwa harakati zake ya kucheza na kuvutia, ikiyumbayumba kwa mashina na matawi yake, na majani yake kutetemeka kwa mguso mdogo sana wa upepo mbele yangu ikadhihiri kwa sura ya wazi na ya kupendeza mno kana kwamba inamsabihi Allah katika duara za dhikiri a tahalili.

Mchakatiko huu nyororo umegusa mishipa ya moyo wangu wenye huzuni kutokana na kutengana na ndugu zangu, nami nikiwa na majonzi kutokana na kubakia kwangu peke yangu, ikapita akilini – ghafla – majira mawili ya mapukutiko na ya baridi, mghafala ukanichukua wakati majani yatakapopukutika maji yakaondoka na uzuri pia. Nikawa ninayasikitikia yale mabua mazuri na kuwasikitikia wengine walio hai ambao hudhihiri kwao furaha hiyo ya hali ya juu masikitiko makubwa mpaka macho yangu yalilengalenga machozi na huzuni zikajikusanya juu ya kichwa changu zilizofoka kwa kasi kutokana na kutoweka na utengano unaojaza hii pazia iliyopambwa yenye kufurahisha kwa viumbe!

Wakati ambapo nikiwa katika hali hii ya kuhuzunisha tahamaki nuru ambayo hakika ya Muhammad imeileta ikanipa msaada – kama inavyompa msaada kila muumini – ikabadilisha huzuni hizo na majonzi makubwa na kuwa furaha isiyo na mipaka. Nikawa katika neema ya milele na kuridhika kwa daima kutokana na hakika ya Muhammad ambayo imeniokoa neema moja katika neema za nuru zake zisizokuwa na mpaka neema hiyo ikaeneza maliwazo katika pande za nafsi zangu na katika kina cha moyo wangu na hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:

Mtazamo huo wenye kughafilika umeonesha majani hayo laini na miti yenye matawi yenye kubaki bure bila jukumu lolote na bila manufaa yoyote na kwamba hayatikisiki mtikisiko mpole kutokana na ukali wa shauku  na furaha bali yanatetemeka kutokana na kishindo cha kukosekana na pia kutengana. Ole wake kwa mtazamo wa mghafala umesibu nukta ya maumbile yaliyowekwa kwangu – na kama kwa mwenzangu – ya kutamani kubakia na kupenda kuishi na kufitinika na mazuri na huruma kwa wana wa kundi moja – ikabadili dunia kuwa ni jahanamu ya kimaanawy na akili kuwa ni kiungo cha mateso na adhabu. Nilipokuwa nina machungu ya  hali hii ya kuumiza, tahamaki kwa nuru ambayo Muhammadi ameitumia kunawirisha wanadamu wote inaondosha funiko na kuondosha kizuizi na inaonesha hekima na maana na kazi na majukumu mengi mno yanayofikia idadi ya majani ya miwilo. Risale-i Nur imethibitisha kwamba nyadhifa na hekima hizo zinagawika katika sehemu tatu:

Sehemu ya kwanza:

Nayo inayaelekea majina mazuri ya Fundi mtukufu. Kama ilivyo fundi mahiri anapotengeneza mashine ya ajabu, wote humsifia na kuipa thamani kazi yake na kubariki ufundi wake, hakika ya mashine hiyo nayo kwa nafasi yake vilevile inambariki fundi wake na kumsifia kwa ulimi wa hali yake, hufanya hivyo kwa kumwonesha kikamilifu natija zilizokusudiwa kwake.

Sehemu ya pili:

Ni yenye kuangalia katika mitazamo ya wenye uhai na utambuzi katika viumbe yaani inakuwa ni mahali pa mtalaa na mazingatio matamu, hivyo kinakuwa kila kitu kana kwamba ni kitabu cha maarifa na elimu, na hauachi ulimwengu huu – ulimwengu wa kushuhudiwa –  ila baada ya kuweka maana yake katika fahamu za wenye utambuzi na kuchapa picha zake katika kumbukumbu zao, na kuingia chapa ya picha yake katika mbao za mifano ya mafaili ya elimu ya Ghaibu yaani haiondoki kutoka katika ulimwengu wa kushuhudiwa kwenda katika ulimwengu wa ghaibu ila baada ya kuingia kwake katika jumla ya maduara ya uwepo mengi na kuchuma aina za uwepo wa kimaanawy, kighaibu na wa kielimu.

Naam, madhali Allah yupo, na ujuzi wake unazungukia kila kitu, hapana budi kusiwepo katika ulimwengu wa muumini kukosekana, kutoweshwa, kutokuwepo, mchezo, kufutwa na kutoweka katika pembe ya hakika, wakati ambapo dunia ya makafiri imejaa kukosekana kutengana na kutokuwepo na imejaa mchezo na kutoweka. Na katika yanayofafanua hakika hii yale yanayozunguka katika ndimi ya kauli mashuhuri ambayo: (Mwenye kuwa na Allah (s.w) anacho kila kitu na asiyekuwa na Allah hana chochote).

Muhtasari:

Hakika imani kama inavyomwokoa mwanadamu kutoka katika kunyongwa kwa milele wakati wa umauti, unaokoa dunia ya kila mtu vilevile kutoka katika giza la kutokuwepo. kukosekana na mchezo. Wakati ambapo ukafiri – na hasa ukafiri halisi – hakika kwa umauti unamfanya huyo mwanadamu asiwepo na kuifanya dunia yake inayomhusu isiwepo na kumtupa katika magiza ya jahanamu ya kimaanawy hali ya kugeuza tamu za maisha yake kuwa ni machungu na maumivu.

Na yasikie masikio ya wale ambao wanapendelea zaidi maisha ya dunia kuliko Akhera, na waje na ufumbuzi wa jambo hili ikiwa wao ni wa kweli au waingie ngome ya Imani na wazikomboe nafsi zao kutokana na hasara hii kubwa.

سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنْتَ الْعَلِيْمُ الْحَكِيْمُ

Ndugu yenu anayetarajia dua zenu na mwenye shauku nanyi

Said Nursi

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.