Suala La Kwanza

Suala hili linaweza kufupishwa ambalo ufafanuzi wake umefanyika katika (Neno la nne) kama ifuatavyo:

Hakika rasilimali za uhai wetu ni hizi saa Ishirini na nne ambazo siku inazileta kwetu zikiwa ni neema safi miongoni mwa neema za Muumba  wetu mkarimu (s.w), ili kwa kila saa tupate kuchuma tunachohitajia na kilicho lazima katika uhai wetu wote wa sehemu mbili wa kidunia na kiakhera.

Na ikiwa hatujatumia saa moja – nayo inatosha kutekeleza swala zilizofaradhishwa – kwa uhai wetu wa kiakhera wa kudumu milele wakati ambapo tunatumia saa ishirini na tatu kwa ajili ya maisha haya mafupi ya dunia, tunakuwa tumefanya kosa kubwa akili iliyo sawa hailioni sahihi kamwe. Basi hapana shaka kuwa sisi tunasumbuliwa na ugumu wa moyo kutokana na kosa hili baya sana na kufungika na giza la roho kwa ujumla wake hupelekea katika kutibua usafi wa tabia na kuchafua umaridadi wa roho. Na juu ya haya uhai wetu unapita ukiwa ni mpangilio wa kuchosha wenye kukatisha tamaa na usio na maana. Hapo kero hutusibu, hatufaidi kutokana na Madrasa hii ya Yusuf na kutokana na shida ya mtihani na majaribio yanayotulea na kutupandisha, kwa hili tunapata hasara dhahiri.

Ama ikiwa tutatumia saa moja katika kutekeleza swala tano, basi kila saa katika saa za balaa na nyakati za mateso inageuka kuwa ni siku kamili ya ibada kana kwamba saa zenye kutoweka zimevuna – kwa baraka ya saa hii – sifa za kuishi milele na kuwa ni katika sifa za saa za kudumu milele, hutanduka moyoni mawingu ya kukata tamaa na kutokomea giza la kukata tamaa katika roho. Saa hii inakuwa katika ibada ambayo ni kafara ya makosa na dhambi zilizofanywa na pengine yalikuwa ndiyo sababu ya kuingia jela. Na kwa hivyo tunagundua hekima ya kupewa kwetu mtihani kwa kufungwa jela na jela inakuwa ni madrasa ambamo tunapokea masomo yenye manufaa na humo pamoja na ndugu zetu kwenye msiba na mateso kitulizo na maliwazo.

Imeelezwa katika (Neno la nne) vilevile mfano unaobainisha ukubwa wa hasara ambayo anaipata anayehemea kutafuta fungu lake duniani na kujitenga na Akhera nayo ni:

Kuna ambao wanalipa lira tano au kumi kati ya lira ishirini na nne alizonazo katika kununua tikiti ya bahati nasibu – huenda inakuwa uwezekano wa kufanikiwa ni sehemu moja kati ya elfu kwa sababu ya kushiriki pamoja naye watu elfu – wakati ambapo hatumii moja katika saa ishirini na nne aliyonayo katika kununua tikiti inayompa faida ya hazina ya kudumu milele ya kiakhera. Hali ya kujua kwamba uwezekano wa kufanikiwa – kwa waumini ambao amali zao zilihitimishwa kwa wema – yeye ana yakini ya sehemu mia tisa na tisini na tisa katika elfu. Kama walivyo sisitiza hivyo manabii na mitume wote wema (a.s) na kuwasadikisha – kwa kufunuliwa na kwa kuhakikisha – mawalii na wateule ambao hawadhibitiki kwa idadi.

Basi darasa hili fasaha kutoka katika Risale-i Nur inapasa wakuu wa jela wasiwe na shaka nalo na kila ambaye yanamhusu mambo ya nchi, kwa kuwa imethibiti kwa uzoefu: Kuongoza watu elfu katika wenye hofu na adhabu ya jela ya jahanamu na wenye kumuomba Allah (s.w) awalinde na adhabu hiyo ni rahisi sana kuliko kuwaongoza watu kumi katika wenye kuacha swala na wenye itikadi na tabia mbovu ambao hawaonyeki ila kwa adhabu na jela ya dunia na wala hawapambanui kati ya halali na haramu.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.