Suala La Nne

Ndugu zangu wanaonihudumia siku moja waliniuliza wakisema: Vita vya ulimwengu vimechukua umuhimu kwa watu, na kushughulisha tufe la ardhi na kuliweka katika migongano na shaka na vina uhusiano na majaaliwa ya ulimwengu wa Kiislamu, isipokuwa sisi tunakuona huviulizii pamoja na kuwa zimepita siku hamsini tangu kuanza kwake – bali miaka saba –

Sentensi hii ya kuingilia kati inarejea Mnamo mwaka 1946 Ad.

wakati ambao tunawaona watu wa dini na wanazuoni wanaacha msikiti na jamaa wakiharakisha kwenda kusikiliza redio Je, kuna kadhia kubwa zaidi kuliko hiyo inayoshughulisha akili yako? Au katika kujishughulisha navyo kuna hasara na madhara?

Nikawajibu: Kwamba rasilimali ya umri ni chache na msafara wa umri hapa ni mfupi, wakati ambapo wajibu wa dharura na majukumu ambayo tuliyokalifishwa kuyatekeleza ni mengi na mambo hayo ya wajibu ni kama maduara yenye kuingiliana yenye kituo kimoja kwa mwanadamu:

Kuanzia kwenye duara la moyo tumbo mwili nyumba mahali mji nchi na tufe la Ardhi na wanadamu, na kukomelea katika duara la walio hai wote na ulimwengu kwa jumla yote, hayo ni maduara yenye kuingiliana baadhi kwa baadhi nyingine. Kila mwanadamu ana aina ya kazi katika kila duara katika maduara hayo lakini wajibu mkubwa na muhimu zaidi bali wa kudumu kwa mujibu wake ni ule uliopo katika duara dogo zaidi na lililo karibu naye zaidi kati ya maduara hayo, wakati ambapo wajibu madogo sana na wenye hadhi chache na kudumu ni katika maduara hayo makubwa zaidi na yaliyo mbali zaidi na yeye. Basi kwa kupimia juu ya hili: Kazi na wajibu yamkini vikanasibiana kwa kinyume pamoja na upana wa duara, yaani kila duara linapokuwa dogo na karibu Jukumu huwa kubwa na kila linapokuwa duara ni kubwa na kuwa mbali umuhimu wa kazi hupungua. Lakini kwa kuwa duara kubwa ni lenye kushawishi na kuvutia linamshughulisha mwanadamu na mambo yasiyo ya lazima kwake na kugeuza fikira yake katika mambo yasiyomhusu chochote hata kumfanya apuuze wajibu wake wa kidharura katika duara dogo lililo karibu na yeye, wakati huo anaharibu rasilimali ya umri wake na kupoteza uhai wake bure bileshi. Ongeza juu ya hapo kuwa moyo wake unaweza kuelemea na kupendelea upande mmoja kati ya pande mbili zenye kuhasimiana kwa kufuatilia kwake kwa hima habari za vita vinavyotimba kati yao. Hapati nafsini mwake kukanusha dhuluma za upande huo, bali anaridhika nazo na anakuwa mshirika katika udhalimu wake.

Ama jawabu la nukta ya kwanza ni kwamba mbele ya kila mwanadamu – na hasa Mwislamu – kuna suala muhimu na tukio la hatari ni kuu kuliko ugomvi unaotokea kati ya mataifa makubwa kwa ajili ya kutawala tufe la Ardhi. Suala hilo lina umuhimu na hatari kiasi ambacho laiti mwanadamu mwenye akili angekuwa anamiliki nguvu ya Wajerumani na Waingereza kwa pamoja asingesita kuzitumia zote kwa ajili ya kushinda kadhia hiyo inayotakiwa.

Kadhia hiyo ni ile ambayo wameitangaza mia moja elfu kati ya wateule bora na kunyanyua bendera yake kiasi kisicho na mpaka katika nyota wa wanadamu na waelekezi wao wenye kuegemea maelfu ya ahadi za mola mlezi wa walimwengu bali wameshuhudia baadhi yao kwa dhahiri kwamba kadhia hii ni kadhia ya hatima ya mwanadamu nayo:

Mwanadamu achume kwa imani au apate hasara kwa kutokuwa na imani, ufalme mkubwa wa kudumu milele na makazi mazuri katika pepo ya kudumu upana wake ni sawa na mbingu na ardhi. Basi asiyefaulu tikiti ya imani na wala hakuichunga haki ya kuichunga ni lazima atapoteza kadhia hiyo na kupata hasara na hiyo ndiyo hasara dhahiri.

Na wengi wamepoteza kadhia yao hii katika zama zetu hizi – katika waliotahiniwa kwa tauni ya u-maada – hadi amefunuliwa mmoja wao naye ni katika watu wa elimu na kufunuliwa na ameshuhudia kwamba watu wachache tu katika kila watu arobaini – mahali fulani – ndio ambao waliyo okoka kwa imani katika machungu ya umauti na uhai wao kuhitimishwa kwa wema, ama waliobaki wameangamia! Unaonaje kama mmoja wao angepewa utawala na ufalme wa dunia na mapambo yake badala ya kadhia hiyo kuu, je, badala hii itakuwa ni yenye kufanana na alichokikosa? Au kuchukua nafasi yake kwa hali yoyote? Hapana!

Na kwa ajili hii sisi changamani wa wanafunzi wa Nur tunajua kwa yakini kwamba kuacha huduma kubwa ambazo zinatufanya tufaulu kadhia hiyo, na kupuuza majukumu ya wakili wake ambaye anayatunza kwa tisini katika mia na kushughulika na yasiyo na maana miongoni mwa mambo ya nje na kutilia muhimu kusiko na maana kana kwamba dunia ni yenye kudumu milele, sio chochote ila ni uzuzu wa akili na wendawazimu.

Hakika sisi tuna yakini na utulivu kamili wa hili kwa hiyo mmoja wetu lau kama angekuwa na akili na utambuzi wa mambo maradufu na maradufu ya aliyonayo hivi sasa angeitoa yote kwa ajili ya kadhia hiyo.

  Basi enyi ndugu zangu wenye muda wa hivi karibuni katika msiba wa jela! Nyinyi bado hamjafanya mtalaa wa Risale-i Nur bado kama walivyofanya ndugu zangu waliotangulia ambao waliingia jela pamoja nasi, mimi nawasikilizisheni kauli na kukushuhudilieni ndugu hao wote maelfu ya mifano yao na nimesema hilo mara nyingi na nimelithibitisha mara kwa mara:

Hakika Risale-i Nur imewapa ushindi wa kadhia hiyo kuu kwa asilimia tisini katika mia kati yao, nayo ndiyo iliyokabidhi hati na tikiti ya kufuzu – nayo ni imani ya hakika – kwa watu ishirini elfu ndani ya miaka ishirini iliyopita. Basi sio ajabu hilo imechimbuka kutoka katika muujiza wa Qur’an tukufu na kuwa mbele ya mawakili wa kadhia kuu na wenye kuitetea katika zama hizi, basi licha ya kumalizika miaka kumi na nane na maadui na wazandiki na wana maada wanasuka aina za njama na hila mbaya na hawajaacha kuwa wanahamasisha baadhi ya maafisa dhidi yetu wakiwatumia kwa lengo la kutuangamiza na hata kutusukumiza kwenye giza la jela mfano wa mara hii. Isipokuwa hawakufanya jambo la kutajika, na – kwa idhini ya Allah (s.w) – hawatofanya, hii ni kwa sababu wao hawakuweza kuidhuru ngome ya chuma cha pua ya Risale-i Nur na wala kugusa zana zake zenye kufikia mia moja na thelathini (Risala) isipokuwa risala mbili au tatu tu kati ya hizo.

Basi anayetaka kuweka wakili kutetea kadhia yake yatosha kushikamana na ngome hiyo na kuchota katika nuru yake.

Enyi ndugu! Msihofu, Risale-i Nur haitazuiliwa kwenye macho wala haitafunikwa isionekane. Wala haitaondoshwa kati ya watu – kwa idhini ya Allah (s.w) – kwani sehemu zake muhimu zinasomwa – ila risala mbili au tatu – na wawakilishi wa bunge na nguzo za taifa kwa uhuru kamili.

Na itafika hiyo siku ambayo maafisa na wakurugenzi wenye hadhi watagawa Risale-i Nur – Inshaallah – kwa wafungwa kama wanavyowagawia mkate na dawa na watayageuza magereza kuwa madrasa za maelekezo, malezi na kutengeneza maadili.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.