Suala La Saba

Tunda lililoiva siku ya Ijumaa katika siku za jela ya Denizli

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

ومَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلاَّ كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ Qur’an, 16:77.

مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Qur’an, 31:28.

فَانظُرْ إِلَى آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذَلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَى وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ Qur’an, 30:50.

Siku moja nilikuwa nimetoa somo (Kastamonu) kwa lugha ya elimu za shule kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondari ambao walikuja kuniuliza: “Tutambulishe Muumba  wetu” kama ilivyokuja katika suala la sita lililoelezwa huko nyuma, walilipata baadhi ya walioweza kuwasiliana nami katika wafungwa huko (Denizli), wakapata utulivu wa imani na ukinaifu kamili uliowafanya wapate shauku kubwa kuhusiana na Akhera, wakaharakisha kusema: “Tujulishe Akhera yetu vilevile kwa ukamilifu, kiasi baada ya hapo tusipotezwe na nafsi zetu na mashetani wa enzi hizi vikatutupia kwenye jela kama hizi”. Na kuitikia ombi lao na kusaidia haja ya wanafunzi wa Risale-i Nur katika jela ya (Denizli) na kwa matakwa makubwa kutoka kwa wale waliopitia (Suala la sita) nikaona ni jambo la lazima juu yangu nibainishe muhtasari mdogo kuhusu nguzo ya imani muhimu: (Akhera).

Basi ninasema kwa muhtasari kutoka kwenye Risale-i Nur: Kama tulivyouliza katika (Suala la sita) ardhi na mbingu kuhusu Muumba  wetu (s.w), zikatujibu kwa ulimi wa elimu za sasa na kutujulisha kuhusu Muumba  wetu ujuzi wa wazi uwazi sawa na jua, kadhalika tutamuuliza kwanza Mola wetu mlezi tuliyemjua kwa yakini kuhusu Akhera yetu kisha tutamuuliza mtume wetu mtukufu (s.a.w), kisha Qur’an yetu tukufu,  kisha baki ya manabii (a.s) na vitabu vitakatifu, kisha malaika  kisha viumbe. Haya sasa ndio tupo katika ngazi ya mwanzo tunamuuliza Allah (s.w) kuhusu (Akhera) anatueleza (s.w) kwa amri zake zote na kwa mitume yake yote  na kwa majina yake mazuri yote na sifa zake tukufu zote kwa kusema: Akhera haina shaka na mtapelekwa huko. Na kwa kuwa (Neno la kumi) limethibitisha Akhera kwa hakika kumi na mbili za kukinaisha safi kwa dalili za sehemu za majina mazuri; kwa hiyo tunaashiria hapa – ishara fupi – kwenye dalili hizo kwa kutosheka na ufafanuzi huo.

Naam, ni kwamba hakuna mfalme mkuu bila ya kuwa na zawadi kwa watiifu na adhabu kwa waasi. Hivyo hapana budi kwamba mfalme wa milele – naye yuko juu katika hali ya juu ya Rububiyya ya moja kwa moja – ana zawadi kwa wenye kujinasibisha kwake kwa imani na wenye kusalimu amri zake kwa utiifu. Na ana adhabu kwa wale waliokanusha ukuu wake na enzi yake kwa ukafiri na uasi. Hapana budi kwamba zawadi hiyo itakuwa yenye kulingana na rehema yake na uzuri wake, na hiyo adhabu itakuwa inawiana na enzi yake na utukufu wake.

Na kwa hivi linatujibu jina la (As-Sultan Ad-dayyan) na (Rabbul alamiin) swali letu kuhusu Akhera.

 Kisha tunaona kwa macho yetu – kwa uwazi sawa na jua – kwamba rehema enevu na huruma yenye kuzunguka na ukarimu wenye kuenea kwenye uso wote wa ardhi; majira ya machipuo yenye kupambika hayaingii hadi unaona rehema inapamba miti, mimea na matunda na kuivika mavazi ya kijani kana kwamba hao ni mahuri wa peponi, na kusalimisha mikononi mwake aina mbalimbali za matunda tofauti, na kutuletea kwa kusema: (Hivyo hapo kuleni na stareheni…) na unaiona ikitulisha asali safi yenye kuponya yenye ladha kupitia mdudu mwenye sumu! na kutuvika hariri laini inayofumwa na mdudu asiye na mkono! na kuhifadhi katika gao la mbegu ndogondogo na punje, maelfu ya tani za chakula na kuzibadili kuwa ni hazina ya akiba kwetu. Basi ambaye ana rehema hii kunjufu na huruma hii enevu na ukarimu wenye kuenea hapana shaka kwamba yeye hata wafanya waja wake waumini wapendwa kwake kutoweka na kutokuwepo kabisa, wale ambao amewalea na kuwaneemesha na kuwakirimu kwa kiwango hiki cha upole ulaini na uangalizi. Bali ataweka ukomo wa jukumu lao katika uhai wa dunia ili kuwaandaa kwa rehema kunjufu na kubwa zaidi.

Na kwa hivi jina la Allah (Ar-Rahaman) na (Al-Kariim) katika majina mazuri yanajibu swali letu kuhusu Akhera yakitwambia: (Pepo ni haki).

Kisha tunaona majukumu ya viumbe yakifumwa kwa mtindo wa hekima na kupimwa kwa mizani ya uadilifu. Navyo ni katika umakini na unyeti kiasi mwanadamu hajengi taswira bora kuliko viwili hivyo. Basi tunaona hekima ya kiazali imemtunuku mwanadamu uwezo wa kuhifadhi – kama punje ya haridali kwa ukubwa – na imeandika humo maelezo ya uhai wake na matukio yanayomhusu yasiyohesabika, kana kwamba hiyo ni maktaba ndogo sana yenye hati za kumbukumbu, na imeyaweka kwenye pembe moja ya ubongo wake, ili daima imkumbushe siku ya hesabu, siku yatakapo kunjuliwa yaliyomo katika nyaraka za amali.

Na tunaona uadilifu wa moja kwa moja unaweka kila kiungo katika kiumbe hai mahali pake panapofaa kwake, na kuratibu kwa mizani madhubuti nyeti – kuanzia kijidudu kidogo hadi mnyama mkubwa kabisa, na kutoka katika nyuki dhaifu hadi kipanga wa kutisha, na kutokana na ua maridadi hadi majira ya machipuo yenye kupambika kwa mamilioni ya maua, na tunaona unakipa kila kiungo mpangilio usiokuwa na mchezo ndani yake, na mizani sawa isiyo na upungufu, na mpangilio huoni ndani yake isipokuwa ufundi wa ajabu, yote hayo ndani ya uzuri wenye kurembeka na urembo wenye kudhihirika hata viumbe vinakua ni vielelezo vilivyochukua umbo kwa ajili ya ufundi utengenezaji vema na uzuri, ukiachilia mbali kuwa unatunuku kila mwenye uhai haki ya kuishi; humrahisishia njia za maisha, na kumwekea vipimo vya uadilifu vya hali ya juu; basi malipo ya wema ni wema mfano wake na malipo ya ovu ni ovu mfano wake,  na wakati huohuo unafahamisha nguvu na umilele wake, kwa unayoyateremsha katika adhabu yenye kudamirisha juu ya wachupao mipaka na madhalimu tangu enzi za Adamu (a.s). Kama isivyokuwepo jua bila mchana, basi hekima hiyo ya kiazali na uadilifu huo wa milele haviwezi kuthibiti kuwepo kwake kikamilifu isipokuwa kwa maisha ya Akhera ya kudumu milele, na kwa hiyo haviridhii wala kusamehe kwa hali yoyote juu ya mwisho usio na uadilifu wala hekima wala kuhakikisha haki, huo ndio umauti ambao hauna ufufuo baada yake, na ambapo huwa sawa madhalimu wakaidi pamoja na wenye kudhulumiwa na kudhuriwa! kwa hiyo hapana budi nyuma yake kuwepo uhai mwingine wa kudumu milele ili hekima na uadilifu vikamilishe uhakika wake.

Na kwa hivi linatujibu – jibu la kukinaisha – jina la Allah (s.w) (Al-Hakiim) na (Al-Hakamu) na (Al-Adlu) (Al-Adilu) katika majina mazuri kuhusu swali letu juu ya Akhera.

Kisha tunamwona kila kiumbe hai hupewa mahitaji yake ambayo hayako katika uwezo wake kuyapata, na yanajibiwa maombi yake yote anayoyaomba – kwa aina ya dua – sawa kwa ulimi wa haja zake za kidharura, au kwa lugha ya maandalizi yake ya kimaumbile, na hukabidhiwa katika wakati munasibu sana na ulio bora kutokea kwenye mkono mrehemevu mkunjufu wa rehema, msikivu wa kila hali na mpole ambaye upole wake ni wenye kuenea, na pia aghalabu ya dua za mwanadamu za kihiari zinajibiwa na hasa dua za wateule kati ya watu, na hasa zaidi dua za manabii (a.s), – ambazo aghalabu yake hujibiwa kwa namna ya kufurutu ada – kujibiwa huko kunatufahamisha kwa yakini kwamba nyuma ya pazia kuna mwenye kusikia kila kitu mwenye kujibu anasikia miguno ya kila mwenye msiba na kuugua kwa kila mwenye ugonjwa na anasikiliza dua ya kila muhitaji na anaona haja duni kabisa ya kiumbe mdogo kabisa na anasikia kuugua kulikojificha sana kwa kiumbe mnyonge sana anamjumuisha kwa upole wake na kumpa msaada hasa na kumridhisha. Maadamu mambo yako hivi dua ya furaha ya kiakhera, kubakia, na kukaa milele – ambayo ni dua bora na enevu zaidi na inagusa viumbe vyote na inafungamana na majina yote mazuri na majina yote matukufu – dua hii anaiomba kiumbe bora zaidi – ambaye ni mwanadamu – na mja mtukufu mno na kipenzi mno mbele ya Allah (s.w) anaijumuisha katika dua zake, huyo ni mtume mtukufu (s.a.w), naye ni imamu wa manabii (a.s) ambao ni majua ya wanadamu na viongozi wao na kila muumini katika uma wake anaitikia amina kwa dua yake hii, bali kila muumini husema amin kwa kumsalia kila siku mara kadhaa kwa uchache, bali wanashirikiana viumbe wote katika dua yake kwa kusema: (Jibu ewe mola wetu mlezi jibu dua yake hakika sisi tunaomba na kunyenyekea kwako kama yeye). Basi dua kama hili lenye kujumuisha kudumu na furaha ya milele kutoka kwa mtume kama huyu kipenzi (s.a.w) na ndani ya masharti haya ambayo hayakataliwi, hapana shaka hilo peke yake ni lenye hoja na sababu tosha ya kupatisha kwa pepo ya kudumu milele na kuzusha Akhera kati ya sababu zisizohesabika wala kudhibitika za kuipatisha. Ukiachilia mbali kwamba kuipatisha ni jambo jepesi kwa uweza wake (s.w) na rahisi kwake kama kuumba majira ya machipuo.

Na kama hivi jina la Allah (s.w) (Al-Mujiib), (As-Samii) na (Al-Rahiim) katika majina mazuri yanatujibu juu ya swali letu kuhusu Akhera.

Kisha yaliyo katika kubadilika kwa majira mbalimbali miongoni mwa matukio ya umauti na ufufuo juu ya Ardhi yote yanajulisha kwa uwazi – kama kujulisha kwa mchana juu ya jua – kwamba nyuma ya pazia kuna Bwana mlezi anayeendesha Ardhi kubwa kwa upeo wa mpangilio na ukomo wa wepesi – sawa na kuendesha bustani ndogo bali kama kuendesha mti mmoja kwa mpangilio – na anaendesha majira ya machipuo makubwa sawa na wepesi wa kuendesha ua moja na kwa mapambo yake yaliyokuwa kwenye vipimo, na anaandikia kwenye ukurasa wa ardhi aina mia tatu elfu za makundi ya mimea na wanyama ambayo ni mfano wa aina mia tatu elfu za vitabu vinavyoonesha vielelezo na mifano ya ufufuo.

 Basi mola huyu mweza ambaye anaandika vielelezo hivi vyenye kuingiliana bila ya kubabaika wala kuchanganya na bila ya kusahau wala kukosea na kwa namna nzuri, mpangilio na maana fasaha pamoja na kuwa kwake kama nyavu na kushabihiana, inadhihirisha ndani ya utukufu mkubwa uweza wenye nguvu wenye kurehemu wenye wingi wa hekima, basi yeye (s.w) anaeneza uwepo wote kwa rehema yake na hekima yake hii anampa mwanadamu makamo ya juu na kumdhalilishia ulimwengu mkubwa na anamfanyia kuwa ni makazi na matulio kwake, kisha anamtawaza kuwa khalifa kwenye ardhi na anambebesha amana kubwa ambayo mbingu na ardhi na milima imeikataa kuibeba na anamfadhilisha kuliko viumbe wote, Na kumtukuza kwa maneno yake ya kiungu – mazungumzo yake ya ki Subuhana na kuwa msaidizi wake, ukiachilia mbali kuwa amekata ahadi juu ya nafsi yake na kumwahidi mwanadamu huyu ahadi fulani – katika vitabu vyake vyote vilivyoteremshwa – kwamba atamweka milele kwa furaha ya kudumu na kubakia kiakhera. Hapana shaka kwamba yeye atamfungulia milango ya furaha ya kudumu, na kuleta ufufuo na kiama kwa lazima na hilo ni jepesi kwake kuliko majira yenyewe ya machipuo.

Na kwa hivi majina ya Allah (s.w) (Al-Muhyi), (Al-Mumiit), (Al-Hayyu), (Al-Qayyum), (Al-Qadiir) na (Al-Aliim) yanatujibu swali letu kuhusu Akhera. Kwa kweli hakika uweza wa kiungu ambao unahuisha mashina ya miti na majani kwa ujumla katika kila majira ya machipuo na kupatisha vielelezo vya aina mia tatu elfu ya ufufuo katika wanyama na mimea yote, bali unadhihirisha mifano elfu moja ya ufufuo na dalili elfu moja katika majira elfu mbili ya machipuo

Hakika kila majira ya machipuo yanayokuja ni sawa na Ufufuo wa majira ya machipuo yaliyotangulia ambayo kiama chake kimesimama na uhai wake umekoma. (Mtunzi).

inapotazamwa kimawazo miaka elfu moja kati ya miaka ambayo waliyoishi watu wote kati ya nabii Muhammad na Musa (a.s) na kulinganishwa pamoja! basi vipi ikanushwe kukufuliwa viwiliwili kwa uweza huu wa hali zote? Kukanusha hilo haiwi upofu usiozidiwa na upofu wowote?

Kisha mia moja na ishirini na nne elfu katika binadamu bora nao ni manabii (a.s), wametangaza furaha ya milele na kudumu milele Akhera hali wakiwa wameafikiana na wenye kuegemea katika maelfu ya makamio na ahadi ambazo amezikata Allah (s.w) juu ya nafsi yake. Na wakathibitisha ukweli wao kwa miujiza iliyo kuwa wazi. Na kwamba idadi kubwa mno ya mawalii na waja wema wanathibitisha hakika hiyohiyo kwa ufunuo na maonjo.

Hapana budi kuwa hakika hiyo ni dhahiri udhahiri sawa na wa jua katikati ya mchana mwenye kutilia shaka hilo amenyimwa akili: Kwa sababu maamuzi ya bingwa mmoja au wawili katika elimu au kazi kwenye suala lililomo ndani ya ujuzi wake, yanaangusha kuzingatiwa kwa uzito wa maoni na fikira ya wapingaji elfu moja wasiobobea katika elimu au kazi hiyo hata kama ni wabobezi katika elimu nyingine. Na kwamba hukumu ya mashahidi wawili wa kuthibitisha katika suala fulani hupewa uzito dhidi ya maelfu ya wakanushaji au wanaokataa suala hilo.

Kama ilivyo katika kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Ramadhani katika Yawmu ash-Shakk au kudai kuwepo kwa mashamba ya minazi yanayofanana na makopo ya maziwa ardhini; hii ni kwa sababu mwenye kuthibitisha anashinda kadhia kwa kiasi tu cha kuiashiria au kudhihirisha nazi au kubainisha ilipo. Ama mkanushaji anayekataa uwepo wake hawezi kuthibitisha madai yake isipokuwa atakapo tafuta na kutembea katika pande zote za ulimwengu na kuthibitisha madai yake kwa umakini katika mahali pote. Na kama hivi ambaye anaelezea kuhusu pepo na nyumba ya furaha na kuishi milele hakika anathibitisha hilo na kushinda kadhia kwa kiasi tu cha kudhihirisha kwake athari mojawapo katika athari za pepo, au alama moja katika alama zake, au kivuli katika vivuli vyake kwa kufunua; wakati ambapo anayekanusha uwepo wake hawezi kupata uwanja wa kukanusha kwake – vyovyote atakavyojitahidi – isipokuwa atakaposhuhudia na kuwashuhudisha wengine limwengu zote na zama zote kuanzia azali hadi milele, na akadhihirisha kutokuwepo kwake na akathibitisha hilo!! Basi kwa ajili ya hekima hii wanazuoni wahakiki wameridhia kanuni ya msingi ambayo ni: (Haiwezekani kuthibitisha ukanusho usio ainishwa mahala pake maalum – kama hakika za kiimani za jumla kwa ulimwengu wote – kama jambo lenyewe sio muhali).

Kwa msingi wa hakika hii ya kukinaisha kukanusha kwa maelfu ya wanafalsafa na kupinga kwao hakuwezi kuleta utata wowote wala wasiwasi mbele ya mpasha habari wa kweli katika maswala kama haya ya kiimani. Uzuzu uliyoje kwa ambaye anajichafua kwa utata – vyovyote iwavyo – katika nguzo za imani kwa kiasi tu cha kukanusha wachache kati ya wanafalsafa wa kiyakinifu ambao akili zao zimeteremka katika macho yao hawaoni isipokuwa maada bali nyoyo zao zimekufa hawahisi vitu vya kimaanawy, wakati ambapo wameafikiana juu ya nguzo hizo mia moja na ishirini elfu katika wenye kuthibitisha wenye ubobezi miongoni mwa manabii wa kweli (a.s), na katika wasiohesabika katika wenye kuthibitisha na wenye kubobea katika watu wa hakika mawalii na wanazuoni watu wa tahakiki.

Na kadhalika sisi tunashuhudia, sawa sawa katika nafsi zetu au katika vinavyotuzunguka rehema enevu na hekima jumuishi na uangalizi wa kudumu wenye kutawanya nuru yake kama mchana, na tunaona vilevile athari kubwa za kiungu na nuru za uadilifu zenye busara, na midhihirisho ya taratibu tukufu azizi, bali tunaona (Hekima) inaupa mti hekima kwa idadi ya maua yake na matunda yake, na tunaona (Rehema) inasimamisha kwa kila mwanadamu hisani na vipawa kwa idadi ya milango yake ya fahamu na nguvu zake na viungo vyake. Na tunauona (Uadilifu) wenye enzi kwa adhabu yake kali unaangamiza waasi mithili ya kaumu za Musa, Nuhu, Hud, Saleh na kaumu ya Adi, Thamudi na Firauni, nao ni wenye uangalizi vilevile unahifadhi haki za kiumbe mdogo na dhaifu mno. Aya tukufu ifuatayo inabainisha kwa ufupi wa kimuujiza ukuu wa ulezi huo wa kiungu mtukufu na haiba yake ya hali zote:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاء وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ Qur’an, 30:25.

Ambapo inabainisha kwamba mbingu na Ardhi vinatekeleza amri za kiungu kama wanajeshi waliopiga kambi na waliolala katika kambi mbili. Kama wanavyoharakisha katika kuchukua nafasi zao na kuchukua silaha zao kwa wito kutoka kwa kiongozi na kwa mpulizo wa tarumbeta, kadhalika mbingu na Ardhi ni kama kambi mbili kwa vile maiti huitwa katika kambi mbili hizo kwa baragumu la Israfil (a.s), tahamaki wanatoka makaburini kwa haraka wakiwa wamevaa mavazi ya mwili. Bali tunaona taadhima hii na utiifu katika kila majira ya machipuo, ambapo wanakusanywa askari waliopo katika kambi ya Ardhi na kutawanywa kwa mpulizo wa tarumbeta la malaika wa radi. Kwa msingi wa hakika zilizopita, hapana budi kuwa hizo rehema, hekima, uangalizi, uadilifu na ufalme wa milele malengo na shabaha zake zitathibiti katika maisha ya Akhera, Yaani yahitajia ufufuo kwa dharura, kama (Neno la kumi) lilivyothibitisha hilo; kwani hapana shaka katika ujio wa Akhera, bali kutokuja kwake ni muhali kwani kukosekana kwake kuna maana ya kuwa: Kubadilika kwa (Rehema) ambayo imo katika ukomo wa uzuri kuwa ni ukatili katika ukomo wa ubaya na ina maana akuwa: Kugeuka kwa ukamilifu wa (Hekima) kuwa ni kasoro ya mchezo wenye hali ya upungufu na upeo wa israfu, na ina maana ya mapinduzi ya (Uangalizi) ambao uko katika ukomo wa uzuri na upole kuwa dharau katika ukomo wa ubaya na uchungu na ina maana: Kughairisha (Uadilifu) ambao uko katika ukomo wa insafu na haki kwenda katika giza katika ukatili mkubwa na ubatili, ongezea kwamba kutokuja kwa Akhera kuna maana vilevile ya kuanguka kwa haiba ya ufalme wa milele wenye enzi na kubomoka utukufu na nguvu yake, na ina maana ya kutuhumu ukamilifu wa ulezi wa kiungu kwa kushindwa na upungufu. Na vyote hivi ni batili na muhali akili ya mwanadamu hailikubali hili vyovyote iwavyo, nalo ni jambo lisilokuwa na liko nje ya eneo la uwezekano; kwa kuwa kila mwenye utambuzi anafahamu kwamba Allah (s.w) amemuumba mwanadamu huyu katika umbo bora kabisa na kumlea malezi mazuri sana na kampatia zana na viungo – kama akili na moyo –  hali anayotazamia kwayo furaha ya milele na kumpeleka upande huo, na inatambulika pia kiasi cha udhalimu na ukatili ikiwa hatima ya mwanadamu huyu aliyetukuzwa kuwa katika kukosekana kwa milele! Na inafahamika pia kiasi cha kukosekana hekima katika kutofufuliwa ambako kunafanya zana na nguvu zote za kimaumbile – ambazo zina maelfu ya masilahi na faida – bila mafanikio na bila ya thamani – wakati ambapo Allah (s.w) ameweka mamia ya hekima na faida katika ubongo wake tu! Na inafahamika vilevile kiasi cha kushindwa kwa dhahiri na ujinga timamu wenye kukinzana kwa jumla na adhama ya ufalme huo na ukamilifu wa malezi ya kiungu katika kutotimiza maelfu ya makamio na ahadi? Ametakasika Allah (s.w) na hayo kutakasika kukubwa. Pima kwa hili vyote (Uangalizi) na (Uadilifu).

Na kama hivi yanatujibu majina: ya (Ar-Rahman)  (Al-Hakim) (Al-Adlu) (Al-Kariim) na (Al-Hakim) katika majina mazuri kwa hakika hiyo iliyoelezwa kuhusu swali letu tulilouliza juu ya Akhera na yanatuthibitishia uthibitisho usio na utata bali ni wazi bayana kama uwazi wa jua. Kisha tunaona (uhifadhi) mkubwa wenye kuzunguka dhahiri wenye kuonekana unahukumu juu ya kila kitu kilichokuwa hai, na kutawalia kila kitu, unahifadhi sura zake nyingi, unasajili kazi za majukumu yake ya kimaumbile, unasajili tasbihati zake – kwa ulimi wa hali – mbele ya majina mazuri, unazisajili katika mbao za kimfano, katika mbegu zake na kokwa zake ndogo, na katika nguvu yake ya kuhifadhi nazo ni vielelezo vilivyopewa maumbo madogo ya Lauhul Mahfudh – na hasa katika kumbukumbu ya mwanadamu ambayo ni maktaba kubwa iliyopewa umbo dogo mno iliyowekwa kwenye ubongo wake, unavisajili kwenye vioo vingine na viakisi vya kimaada na kimaanawy. Na hayaji majira ya machipuo – ua hilo lililopewa umbo la kudura ya kiungu – hadi uhifadhi unatudhihirishia maandishi hayo ya kimaanawy yakiwa dhihiri yenye kushuhudiwa yakiwa yamechukua umbo. Na unahudhurisha katika ua hilo kubwa hakika ya ufufuo ambayo iliyomo ndani ya aya tukufu:

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ Qur’an, 81:10.

na kuitangaza kwa ndimi za mamilioni ya mamilioni ya mifano na dalili, na kutusisitizia kwa yakini kwamba vitu vyote – na hasa walio hai – havikuumbwa ili viishie katika kutoweka, wala kuporomoka katika kutokuwepo, wala kufutwa kuwa sio chochote – na hasa mwanadamu – bali vimeumbwa ili kuendelea kupanda kwao katika kubakia – na ili kuingia kwa kutakasa nafsi zao katika ulimwengu wa uhai wa kudumu milele, na kwa ajili ya kuingia kwa maandalizi ya kimaumbile katika jukumu la milele linalowangojea katika makazi ya milele. Naam, hakika kila mti na shina na kila punje na kokwa katika mimea isiyo na mipaka ambayo ilikufa katika kiama cha mapukutiko, haingii ufufuo wa machipuo ila inasoma aya tukufu:

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ

kwa ulimi wake mahususi na kutafsiri maana katika maana zake, na hii kwa kutenda kila sehemu kati ya sehemu zake mfano wa nyadhifa za kimaumbile ambazo imezitenda katika miaka iliyopita na kubainisha wakati huohuo – adhama ya uhifadhi katika umbali wake mkunjufu zaidi kama ilivyo katika aya tukufu:

هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ Qur’an, 57:3.

na inatuelekeza katika hakika nne za wazi katika kila kitu na kusimamisha hoja yenye nguvu juu ya ulazima wa ufufuo kama ulazima wa kuja kwa majira ya machipuo na wepesi wake.

Naam, hakika nuru za majina haya mazuri manne inaelekea na kufanya kazi kuanzia sehemu ndogo zaidi hadi kwenye sehemu kubwa zaidi hebu tufafanue hili kwa mifano:

Mbegu ambayo ndio asili ya mti inabainisha adhama ya uhifadhi kwa kupokea kwake nuru ya jina la Allah (Al-Awwal) na hiyo ni kwa ajili ya mpango madhubuti ulio kamilika wa mti uliomo ndani ya hiyo mbegu Na zana za kiufundi inazozikusanya za kuufanaye uwepo na kukuwa kwake ukiwa kamili bila upungufu na yaliyomo katika masharti ya kuundika kwa mti pamoja na kuwa hiyo mbegu ni pakiti ndogo sana.

Na tunda vilevile linashuhudia ushahidi wa kweli juu ya uhifadhi huokwa kupokea kwake nuru za jina la (Al-Akhir) na hiyo ni kwa yale inayobeba katika faharisi za kazi zote za kimaumbile za mti huo na n nyaraka za matendo yake inazozikusanya  na kanuni zilizomo za maisha yake ya pili hali ya kujua kwamba hilo ni sanduku dogo sana.

Ama dhahiri ya mti iliyopewa umbo inadhihirisha adhama ya uweza na ukamilifu wa hekima na uzuri wa rehema ndani ya uhifadhi wa hali zote na unaidhihirisha kwa ajili ya kuonekana waziwazi ikishuhudiwa kwa kupokea kwake nuru za jina la Allah (Adh-dhahir) na hii kwa mapambo yake yenye kujitokeza yakirembeshwa kwa nakshi za kupendeza aina kwa aina na nishani zilizopangika kana kwamba ni nguo za Mahuri al-aini zenye kutiwa rangi namna sabini. Ama zana za ndani za mti huo ambao umekuwa kama kioo chenye kuakisi nuru zaa jina la Allah (s.w) (Al-Batin) nazo pia zinathibitisha – uthibitisho wenye kung’ara kama jua – ukamilifu wa uweza na uadilifu na uzuri wa Rehema na Hekima kwa kuwa huo mti ni kiwanda kamili chenye mpangilio wenye kufurutu ada bali ni maabara kubwa ya kikemia bali ni ghala la chakula na riziki haliachi tawi wala tunda wala jani isipokua huipa chakula inachokihitajia kama vyote mbegu na tunda  na nje ya mti na ndani yake vinavyodhihirisha midhihirisho ya majina ya Allah (s.w) yaliyo mazuri (Al-Awwal, Al-Akhir, Adh-Dhaahir na Al-Baatin) basi tufe la Ardhi pia linayadhihirisha na kuyabainisha wazi kwamba Al-Hafiidh (Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu) mwenye utukufu na ukarimu hakika anafanya kwa uweza na uadilifu na hekima na rehema kwa hali zote kwani hilo tufe la Ardhi kama mti kwa upande wa kubadilika kwa majira ya mwaka  basi kokwa zote na punje ambazo zimehifadhiwa kwenye majira ya mapukutiko – kwa kudhihiri kwa jina lake Allah (s.w) (Al-Awwal) hali ya kuwa ni amana kwa Uhifadhi inatuma kiasi kisichohesabika katika mashina na miundi ya miti na matawi na kuipeleka kaika pande mbali mbali na inafungua kiasi kisichohesabika cha maua yenye kupendeza na matunda mazuri, huivisha ardhi mtandio wa kufurahisha wa majira machipuo. Kwa sababu kila moja kati yake ina madaftari madogo ambayo ndani yake kumeandikwa amri za kiungu mola mlezi Na inasitiri kurasa ndogo ndogo yameandikwa humo matendo yaliyotendwa katika mwaka uliopita bali mbegu na kokwa hizo mambo yote yanayorejea katika muundo wa mti mkubwa wa Ardhi.

Ama mwisho wa kila mwaka wa mti wa Ardhi ni yale yanayo yaweka katika pakiti ndogondogo mno katika kazi zote ambazo mti umezitenda ndani majira ya mapukutiko na tasbihati zote na Dhikiri zote za kimaumbile ambazo imezitimiza kwa upande wa majina mazuri na yote yanayoyumkinika kuyaeneza katika ufufuo wa majira ya machipuo yajayo miongoni mwa kurasa za matendo na zote hizi hukabidhiwa katika mkono wa Hekima wa muhifadhi wa kila kitu vema mtukufu kwa hivi ikiwa inasoma jina la Allah (s.w) (Al-Akhir) kwa ndimi zisizo na ukomo juu ya masikio ya viumbe na  mifano yake.

Ama nje ya mti huu ni: Maua hayo ya jumla aina mbali mbali ambayo yanabainisha juu ya aina mia tatu elfu ya mifano ya ufufuo na lama zake nazo ni ni meza zile zilizotandikwa za mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu na Mtoa riziki aliye Karimu nayo nizile dhifa zilizofunuliwa kwa ajili ya wote wenye uhai basi kila kilichomo nje ya nti huo kinataja na kusoma jina la Allah (s.w) (Al-Dhaahir) kwa ndimi za matunda yake na maua yake na ladha zake zikidhihirisha hakika ya

وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ

iking’ra kama jua katikati ya mchana).

Ama ndani ya mti huu ni maabara na kiwanda kinachakata kiasi kisichohesabika wala kudhibitika katika mashine yaliyopangika na maabara madhubuti hata kwamba inaandaa tani moja ya vyakula na kuivisha kutoka na dirhamu moja ya maada na kuwafikishia wenye njaa. Na inatekeleza kazi katika ukomo wa umakini kiasi kisichotoa nafasi ya sadfa kucheza katika hilo basi uso wandani wa Ardhi unataja jina la Allah (s.w) (Al-Matin) bali inalithibitisha na ulitangaza kwa aina mia moja elfu ya mitindo na picha kama sehemu ya malaika ambao wanafanya tasbihati kwa ndimi  mia moja elfu wanavyolitangaza jina hilo.

Kama ilivyo Ardhi kwa upande wa uhai wake wa kila mwaka kama mti imebainisha (Uhifadhi) uliopo katika majina hayo mazuri manne kwa ufasaha na kuyafanya kuwa ni ufunguo wa mlango wa ufufuo hiyo nayo kama mti uliopangika sana kwa upande wa maisha ya enzi na dahari kwani hutuma matunda yake – kwa kitambo cha enzi na dahari – kwenda kwenye soko la Akhera.

Kama hivyo Ardhi yote inakuwa ni kioo kipana sana kwa ajili ya midhihirisho ya majina hayo manne na inafungua njia apana sana kwenda Akhera kiasi akili zetu zitabaki na lugha zetu ni  pungufu na zenye kushindwa kuzungukia hilo kwa kulifahamu kwa hiyo tunatosheka na yafuatayo wala hatuzidishi: Kurabu za saa ambazo zinahesabu sekunde na dakika na saa na siku zinashabihiana baina yake moja inajulisha nyingine na kuikumbusha basi anayefuatilia mwendo wa kurabu ya sekunde analazimika kusadiki mwendo wa meno mengine. Hali kadhalika dunia ni kama saa kubwa ya Muumba mbingu na Ardhi ambapo siku zinahesabu sekunde za saa hii kubwa zinafanana na miaka ambayo inahesabu dakika zake na enzi ambazo zinadhihirisha saa zake na karne nyingi ambazo zinajulisha masiku yake basi pamoja nakufanana kwake nyakati hizi kila mmoja inajulisha  juu ya mwingine na kuuthibitisha

Na kwa pembe hii Ardhi tunaiona inaelezea kwa lama zisizo na mpaka juu ya ujio wa majira ya machipuo ya kudumu milele na asubuhi ya milele baada ya majira ya baridi ya dunia yenye kutoweka yenye giza. Inaelezea hilo kwa ulazima wa kuja kwa asubuhi kwa usiku huu na kwa kukata shauri la ujio wa majira ya machipuo kwa majira haya ya baridi. Na kwa hakika hii jina (Al-Hafiidh) linatujibu pamoja na majina manne mazuri (Al-Awwal, Al-Akhir, Adh-Dhaahir na Al-Baatin) juu ya swali letu ambalo tumeuliza kuhusu ufufuo midhali tunaona kwa macho yetu na kufahamu kwa akili zetu kwamba mwanadamu:

Ni hitimisho la matunda ya mti wa ulimwengu na ndiye jumuisho la kila kitu katika sifa zote zilizomo katika ulimwengu.

Na yeye ndiye mbegu yake ya asili kwa upande wa hakika ya Muhammad (s.a.w). Na yeye ni aya  kubwa ya ulimwengu ya Qur’an ya ulimwengu. Bali ni aya yenye kubeba madhihirisho ya jina Kuu katika hilo Qur’an ya kiulimwengu kama Ayat Al-kursy ndani ya Qur’an tukufu.

Na yeye ni mgeni mtukufu mno katika kasiri ya ulimwengu. Naye ni mfanya kazi hodari zaidi aliyepewa idhini kusarifu katika wakazi wa kasiri hiyo. Na yeye ndiye aliyepewa mari aliye kalifishwa kulima shamba la Ardhi na mwangalizi masuuli juu ya bidhaa zake na matumizi yake kwa vipawa alivyotunukiwa katika mamia ya elimu na maelfu ya sifa. Na yeye ni khalifa wa Ardhi na mkaguzi mtafiti katika Milki ya Ardhi na aliyetumwa kutoka kwa Mfalme wa azali na milele na mtendaji chini ya uangalizi wake.

Naye ndiye mwenye kusarifu katika mambo ya Ardhi pamoja na kusajiliwa kikamilifu kazi zake madogo na makubwa yake. Naye ni mja mjumuishi mwenye kukalifishwa kwa ibada pana yenye kukusanya na mchukuzi wa amana kubwa ambayo mbingu na Ardhi na milima vilikataa kuibeba mbele yake zikapachana njia mbili: Mojawapo ni ya wabaya na nyingine ni ya wema.

Na yeye ndiye ambaye anakisi kama kioo midhihirisho yote ya majina mazuri na kwake linadhihiri jina Kuu la Allah (s.w).

Na yeye ndiye msemeshwa aliyekusudiwa kwa mazungumzo ya kisubuhana na mwenye kufahamu sana maneno ya mola mlezi.

Naye ndiye mhitaji na mshindwe zaidi fakiri bila mipaka pamoja na kuwa ana maadui na vya kumpa udhia bila idadi na makusudio na maumivu bila mpaka naye ni tajiri mno wa kuandaliwa kati ya wenye uhai. Naye ni mwenye utambuzi mkubwa na hisia kali ya maumivu – ndani ya ladha ya uhai – ambapo ladha zake zinachanganyika na maumivu yenye kutibua.

Na yeye ndiye mwenye shauku kubwa ya kubakia na mwenye haja sana ya kuishi milele bali ndiye mwenye kustahiki zaidi kwa hilo.

Na yeye ndiye anayeomba kwa unyenyekevu ili abakie milele kwa dua zisizo na mipaka angepewa starehe zote zilizomo duniani zisingekonga kiu chake cha kudumu milele.

Na huyu ndiye ambaye anampenda aliyemneemesha kwa kiwango cha kumwabudu na kumpendezesha kwa wengine naye ni mwenye kupendwa vilevile.

Na yeye ni muujiza mkuu katika miujiza yauweza wa Allah (s.w) mwenye kutegemewa kwa haja zote bali yeye ni ajabu ya uumbaji kwa vile ulimwengu mkubwa ulivyoingia ndani yake na kwa kuwa viungo vyake vyote vinashuhudia kwamba yeye ni kiumbe aliyeimbwa ili kuendelea mbele katika kudumu milele.

Mwanadamu huyu ambaye anafungamana na mfano wa hakika hizi ishirini za kiujumla kwa jina la Allah (s.w), (Allah) mwenye mafungamano madhubuti na jina la Allah (s.w) (Al-Hafiidh) ambaye hakimpiti kitu mbinguni na Ardhini anaona haja duni kabisa ya mdogo sana aliye hai na anasikia mnada wa haja yake anamsaidia waandishi wake watukufu wanasajili matendo yote ya huyu mwanadamu yenye kuambatana na viumbe Mwanadamu huyu – kwa hukumu za hakika hizi ishirini – hapana budi kuwepo kwa kukusanywa na kutawanywa – na hapana budi kwamba atalipwa – kwa jina la (Al-Haqq) – kwa huduma na matendo aliyotanguliza na atapata jaza ya kasoro aliyofanya hakuna utata kwamba atapelekwa katika mahesabu na kuulizwa kuhusu matendo aliyosajili – kwa jina la (Al-Hafiidh) madogo na makubwa na hakuna shaka kwamba utafunguliwa mbele yake mlango wa furaha ya milele na dhifa ya kudumu milele au milango ya magereza ya kutisha na mateso ya kudumu na kwamba haiyumkiniki kwamba asihesabiwe na kujificha asionekane na mdhibiti amewaongoza wengi wa viumbe wa ulimwengu huu na kuingilia katika mambo yao na haiyumkiniki kuwa asizindushwe kutoka katika usingizi wake!

Kwa sababu haingii akilini katu kusikilizwa dua hafifu kuliko king’ong’o cha mbu na kukusaidiwa kiuhakika kwa kupewa mahitaji ya muhimu katika maisha kisha zisisikike dua zenye nguvu ya kutetemesha Arshi na tandiko na ambazo zinatamka kutoka katika hakika zile ishirini na kuomba kubakia na kudumu milele. Wala haingii akilini katu – bali ni nje ya yamkini – kwa haki hizo nyingi kupotezwa kabisa bali haiyumkiniki kwa hekima isiyo na mchezo katu japo kwa kiasi cha ubawa wa nzi kwa ushahidi wa kupangiliwa kwake na kuwekwa vema – kufanya mchezo kabisa na maandalizi ya mwanadamu yenye kufungamana na hakika hizo na kuchezea matarajio yake yote na matakwa yake yenye kuendelea hadi katika kudumu milele na kuchezea mafungamano yote hayo na hakika za viumbe mbalimbali ambao wanakuza maandalizi na matakwa hayo kwa sababu dhana hii ni dhuluma mbaya sana viumbe wote waliopo wanaikataa kwa kusema: Hakika hilo ni muhali ndani ya muhali kwa pande mia moja na ni jambo lisilowezekana kabisa kwa namna elfu nyingi. Bali vitu vyote vilivyopo vyenye kushuhudia majina mazuri: Al-Haqq, Al-Hafiidh, Al-Hakiim, Al-Jamiil na Ar-Rahiim vinaikataa.

Namna hii majina ya mazuri yanatujibu: Al-Haqq, Al-Hafiidh, Al-Jamiil na Ar-Rahiim” swali letu kuhusu Akhera majina hayo yazungumza na sisi kwa kusema: Hakika ya ufufuo ni haki hauna shaka nayo ni hakika yenye nguvu haina mabishano mithili ya kuwa sisi ni haki na mithili itushuhudiavyo hakika ya kuthibiti kwa vilivyopo).

Suala hili lau lisingekuwa wazi kuliko jua ningeongeza kubainisha lakini nimefupisha kwa kutosheka na mifano iliyotajwa na kwa kupimia yaliyomo kwenye vifungu vilivyotangulia hakika kila jina katika majina mazuri mia moja bali elfu yenye kuelekea katika ulimwengu yanathibitisha linathibitisha mwenye majina hayo (s.w) kwa dhahiri kwa midhihirisho yake na kwa vioo vyake ambavyo ni viumbe vilivyomo kama yanavyodhihirisha ufufuo na maisha ya Akhera na kuithibitisha kwa namna ya kukinaisha.

Kama anavyotujibu mola wetu (s.w) jibu takatifu na kukinaisha kwa amri zake zote katika vitabu vyake vyote alivyoviteremsha na kwa majina yake yote aliyoiita nafsi yake swali letu ambalo tumemuuliza kuhusu Akhera, kadhalika Allah (s.w) anatujibu kwa ndimi za malaika wake na kutujulisha Akhera kwa mtindo mwingine ambapo malaika wanasema: (Kuna alama na dalili zisizo na mpaka juu ya kuwepo kwetu na ulimwengu wa kiruhani na imepita mijadala na mazungumzo na kutambuana baina yenu na sisi na baina ya maruhani tangu zama za Adam (a.s) nayo ni matukio ya yakini yenye kupokelewa kwa tawaturi hayakubali shaka  na hakika tulieleza na daima tunaeleza tunayoyaona wakati wa matembezi yetu katika nyumba za Akhera na kumbi zake kwenda kwa manabii wenu nyakati za kukutana na kwetu pamoja nao: Hakika tunakubashirieni bishara isiyo na shaka kwamba hizi kumbi za kudumu nyuma yake kuna kasri za kudumu milele na nyumba zenye kuandaliwa kwa yakini zimeandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya wageni watukufu wenye kutukuzwa na kutayarishwa kwa ujio wao. Kwa hivi malaika wanajibu swali letu kuhusu Akhera

Kisha hakika Muumba wetu mkarimu ametuteulia mwalimu mkuu na Ustadhi mkamilifu mno ruwaza ya kweli sana na kiongozi mnyofu sana. Naye ni Mwarabu wa tumbo la Bani Hashim (a.s) na hakika amemtuma kuwa Mwisho wa mitume watukufu (a.s) – kwa hiyo basi ni juu yetu – na kabla ya kila kitu – tumuulize ustadhi wetu yale tuliyomuuliza Muumba wetu Mwenye ushindi na utukufu kuhusu Akhera huenda tukakamilika katika maarifa yetu na kupanda kutoka katika ngazi ya Elimu ya yakini hadi Dhati ya yakini na haki ya yakini  kwa sababu Nabii huyu kipenzi Mkweli mwenye kusadikishwa kutoka kwa Muumba mjuzi wa kila kitu kwa maelfu ya miujiza kama ambavyo ni muujiza wa Qur’an tukufu akathibitisha kwa ulimwengu wote kwamba hicho ni kitabu cha walimwengu batili haikifikii kutoke mbele yake wala nyuma yake Qur’an tukufu pia imekuwa ni muujiza katika miujiza yake (s.a.w) na dalili juu yakuwa yeye ni mkweli mwenye kusadikishwa na kwamba yeye ni mjumbe wa Mlezi wa walimwengu.

Basi miujiza yote hiyo miwili – mmojawapo ni ulimi wa ulimwengu wa kushuhudia pamoja nao sadikisho la Manabii wote (a.s) na mawalii na mwingine ni ulimi wa ulimwengu wa ghaibu wenye kujumuisha vitabu vyote vya mbinguni na hakika zote za ulimwengu – imesimamisha hoja juu ya kukusanywa na kutawanywa (ufufuo) ikiwa na nguvu wazi kama jua na mchana. Kwa uhai wote wa muujiza wa kwanza na maelfu ya aya za muujiza wa pili.

Kweli (Suala la ufufuo na Akhera) ni katika maswala ambayo ni juu ya uwezo na mipaka ya akili ya mwanadamu wala hayafahamiki ila kwa mafunzo ya hawa Maustadhi wawili wenye muujiza (Qur’an karimu na mtume mahabubu (s.a.w)) na miongozo yao.

Ama kwa nini manabii waliotangulia hawakuweka wazi kwa nyumati zao suala la ufufuo kama ilivyo wazi katika Qur’an karimu? Ni kwa kuwa enzi zao zilikuwa enzi za uchanga wa kibinadamu na ujima wa utu na ufafanuzi unakuwa mfupi katika masomo ya msingi kama ijulikanavyo.

Na teuzi ya kauli: Maadamu mengi ya majina mazuri yanahitajia na yanajulisha juu ya hilo, basi hapana budi kuwa hoja na dalili zenye kujulisha majina mazuri kwa nafasi yake yenyewe ni dalili za kuthibitisha Akhera na kusimama kwake.

Na madhali malaika wanapasha habari yale wanayoyashuhudia katika nyumba za Akhera na ulimwengu wa kudumu milele, hapana budi kuwa dalili zenye kushuhudia juu ya kuwepo kwa malaika na ulimwengu wa kiruhani na ibada zao ni dalili za kuthibitisha juu ya Ulimwengu mwingine.

Maadamu muhimu zaidi aliyotangaza Muhammad (s.a.w) wakati wa uhai wake twahara wenye baraka na msingi wa aliyolingania – baada  ya Tawhiid – nayo ni Akhera, basi hapana budi kwamba hoja na miujiza yote inayojulisha juu ya utume wake na ukweli wake (s.a.w) zenyewe kwa nafasi zao ni shahidi juu ya hakika ya ujio wa Akhera.

Na maadamu robo ya Qur’an inachambua juu ya Ufufuo na Akhera na kusimamisha dalili juu yake kwa maelfu ya aya zake na inapasha habari kuhusu hilo, hapana budi kwamba shahidi, hoja, dalili na vithibitisho vyenye kujulisha vyote juu ya kuwa Qur’an ni , kwa nafasi zake ni shahidi juu ya kuthibiti kwa Akhera.

 Na kama hivi zingatieni katika nguzo hii kuu ya imani ili mutathmini kiasi cha kukinaisha (Kuamini Akhera) na kiasi cha uthabiti na uimara wake.You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.