Suala La Tano

Kama ilivyoelezwa katika Risala ya (Mwongozo kwa vijana):

Hakika ya ujana ni wenye kwenda zake na utaondoka hakuna namna, kwani ni kama majira ya joto yanafuatiwa na mapukutiko na majira ya baridi na mchana hufuatiwa na jioni na usiku na ujana pia utageuka kuwa uzee na umauti. Kwa mfano wa hakika hii isiyo na budi.

Kijana atakapotumia nguvu aliyonayo ya muda mfupi katika kheri na wema ndani ya duara la usafi, kujizuia na msimamo, kwa hakika amri zote za mbinguni zinambashiria kwamba atavuna kwa ujana huo ujana wenye kubakia usiotoweka, kama ilivyo ghadhabu ya dakika moja inaweza kumsukuma mwanadamu katika kuingia hatia ya kuua akahukumiwa kuteseka mamilioni ya dakika ya mateso na adhabu ya jela, vilevile mihemko ya ujana na usafihi wake na vionjo vyake vya mpito – katika asiyoyahalalisha Allah (s.w) – humsababishia maumivu mengi na yakuendelea ndani ya ladha hiyohiyo, ukiachilia mbali adhabu ya kutisha Akhera na adhabu chungu kaburini, na taabu ya majuto ya kuendelea yatokanayo na kuondoka kwa ladha, na adhabu duniani kutokana na dhambi na maovu. Kila kijana mtambuzi kwa uzoefu alioupata anashuhudia kwa ukweli uwepo wa maumivu haya ndani ya ladha yenyewe.

Kwa mfano:

Mapenzi yaliyoharamishwa au ashiki kwa namna isiyo ya haki, ina maumivu kiasi cha kuharibu ladha ndogo iliyomo; kati ya hayo ni kuhisi wivu na husuda, na kati ya hayo ni maumivu ya kufarikiana na mpenzi, na kati ya hayo ni kutopata mahaba ya sawa sawa na mengineyo mengi katika yenye kuharibu ambayo hufanya ladha hiyo ndogo kuwa ni sawa na asali iliyowekwa sumu. Ikwa unataka kufahamu kwamba matumizi mabaya ya ujana na israfu yao katika mambo yao huwasababishia magonjwa yanayowapeleka mahospitalini na makaburini. Na ukitaka kufahamu kwamba kudanganyika kwa vijana na kutangatanga kwao huwapeleka magerezani. Na ukiwa unataka kufahamu kuwa yanayowasibu katika maumivu ya kimaanawy na majonzi ya kinafsi – ni kutokana na njaa ya kiroho, njaa ya moyo na kuwa na muda wa bure – vinawapeleka katika milango ya baa na nyumba za starehe. Ndiyo, ukitaka kuhakikisha hili uliza hospitali, magereza, vilabu vya pombe, na makaburi kwa vyovyote utasikia masikitiko na miguno na vilio vikali na malalamiko ya majuto na sauti za kuumia na kujutia huzitoa – aghalabu – vijana waovu ambao wamepata mapigo ya kuumiza kwa kutoka kwao nje ya aliyoyahalalishia Allah (s.w) katika vitu vizuri kwa msukumo wa hisia na israfu zao na uovu wa matendo yao na kutenda kwao mambo yaliyoharamishwa na kufuatilia kwao matamu yenye uovu.

Wakati ambao kijana akitumia ujana wake kwa alivyomwamrisha Allah (s.w) na kushika njia ya sawa na akwa na msimamo basi  ataifanya kuwa ni neema tamu mno ya kiungu na hiba nzuri mno ya mwingi wa rehema, na kuifanya kuwa ni njia iliyonyooka iliyo nyepesi kuelekea katika matendo mema, na kumpatia ujana wenye kung’ara pia wa kudumu milele huko Akhera badala ya ujana huu unaokwisha na kutoweka. Hilo ndilo ambalo vitabu vya mbinguni na suhufi zilizoteremshwa vyote vinatubashiria vikiongozwa na Qur’an tukufu kwa aya zake tukufu zenye hekima.

Maadamu ukweli ndio huu, na maadamu medani ya halali inatosha kwa ajili ya maliwazo, starehe na burudiko, na maadamu ladha moja – ndani ya yaliyo haramishwa – humuonjesha mtendaji maumivu yanayodumu mwaka mmoja ya adhabu ya jela na mara nyingine ni miaka kumi, kwa hiyo ni lazima kutumia kipindi cha ujana kwa kujitunza, usafi na msimamo katika njia ya sawa sawa kwa kutekeleza shukurani ya neema hiyo tamu iliyotunukiwa, bali hili ndio la lazima zaidi.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.