Suala La Tisa

… آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ Qur’an, 3:285.

Hakika sababu ambayo imepelekea kufafanua aya hii yenye kujumuisha ya hadhi ya juu tukufu na kuhitajia kuibainisha, ni hali mahususi maalum iliyotokana na suala la kimaanawy lenye kuchokoza, na kufunuka kwa neema ya kiungu kubwa, kama ifuatavyo:

Limepita katika roho swali hili: Kwa nini anazingatiwa kuwa ni kafiri yule anayekanusha sehemu ya hakika ya kiimani, na wala hahesabiwi kuwa ni Mwislamu asiyeikubali pamoja na kuwa nuru ya Imani ya kumwamini Allah na siku ya mwisho ni kama jua inatokomeza kila giza?

Kisha kwa nini anakuwa mwenye kuritadi anayekanusha hakika moja au nguzo moja ya Imani na kumtupa katika ukafiri halisi, na asiyeikubali anatoka katika duara la Uislamu. Wakati ambapo inatakikana imani yake ya nguzo nyingine imwokoe – ikiwa imepatikana – kutoka katika ukafiri huo halisi?

Jibu:

Imani ni hakika moja inayotokana na nguzo sita zilizoungana na kuwa kitu kimoja hazikubali kutenganishwa, nayo ni kitu kizima hakikubali kugawanyika katika sehemu, nayo ni yote nguzo zake hazikubali kugawanyika, na hiyo ni kwa sababu kila nguzo katika nguzo hizo za imani – pamoja na hoja zake ambazo zinaithibitisha – inathibitisha nguzo nyingine zilizobaki. Hapo inakuwa kila nguzo basi ni hoja ya kukinaisha kubwa ya kila nguzo katika nguzo nyingine. Kwa hiyo basi ambaye hawezi kujeruhi nguzo zote pamoja na dalili zake zote anashindwa jumla – kwa upande wa hakika – kukanusha nguzo moja katika hizo,  na kuivunja hakika moja katika hakika zake, isipokuwa mkanushaji afumbe macho yake na ang’ang’anie kutokukubali au kukataa, wakati huo basi atauingia ukafiri wa kupinga, na kwa kupita kwa muda hilo litampeleka katika ukafiri halisi, basi ubinadamu wake unakosekana na kuelekea katika moto wa kimaada, achilia mbali ambao yeye yumo ndani yake miongoni mwa moto wa kimaanawy.

Kama tulivyobainisha kwa ufupi katika masuala ya (Tunda), kujulisha kwa nguzo za imani juu ya ufufuo vivyohivyo hapa tutabainisha kwa ishara za muhtasari mno na majumuisho wa maana ya kina kubwa ya aya hii tukitegemea uangalizi wake (s.w). Na hiyo ni katika nukta sita:

Nukta ya kwanza

Hakika imani ya (Kumwamini Allah) kwa hoja zake za kukinaisha inathibitisha imani ya Akhera pamoja na kuthibitisha kwake baki ya nguzo nyingine za imani. Kama ilivyowekwa wazi katika (Suala la saba).

Naam, hakika ufalme wa kiungu na uweza wake wa azali na nguvu yake yenye kubaki na utajiri wake wa hali zote na utawala wa kiungu wa milele wa kudumu ambao unaendesha ulimwengu huu usio na mpaka – pamoja na mahitaji yake yote ya lazima na yaliyo muhimu – kama kuendesha kasri au mji. Na ambayo inasarifu mambo yake yote ndani ya mpangilio na mizani na kuigeuza kulingana na hekima nyingi.  Na ambayo inaendesha atomu na sayari na kumwandaa nzi na nyota kwa pamoja kama askari watiifu wa jeshi lililonadhimiwa, na ambayo inaendesha vyote  – ndani ya matakwa yake na amri yake – katika maonesho makubwa ya jumla ya uja ulio takata, kupitia mazoezi matukufu, majaribio na mazoezi ya majukumu na kuyafundisha, kwa utendaji na uchangamfu wa kudumu na kutembea na kuzunguka kwa kuendelea. Je, inayumkinika, au je inaingia akilini, hapana bali je, kuna uwezekano wowote katu ya kuwa kusiwepo makao ya kubakia, na mamlaka ya kudumu, na kudhihiri kwa kudumu milele na udhihirisho wa milele katika makazi ya milele kwa mfano wa ufalme huu wa milele na kwa mfano wa utawala huu wa kubakia daima? Hasha na sivyo hivyo! Na mara elfu sivyo hivyo.

Basi ufalme wa Uungu wa Allah (s.w) na adhama yake kwa hiyo, na aghalabu ya majina ya Allah Mazuri – kama ilivyokuja katika (Suala la saba) – na dalili zote na hoja za kupasa kuwepo kwake (s.w), zote zinashuhudia juu ya Akhera na kuihitajia.

Basi ni ngome kuu ilioje nguzo hii adhimu ya imani na ni nukta madhubuti ilioje kuiegemea! ehe basi tambua hilo na ulisadiki kana kwamba unaliona.

Kisha hakika imani ya (Kuamini Allah (s.w)) kama isivyowezekana kuwa bila ya (Imani ya Akhera), vivyo hivyo haiyumkiniki wala haingii akilini kuwepo (Imani ya Allah (s.w)) bila ya (Imani ya mitume) – kama ilivyoelezwa kwa ufupi katika (Risala ya ufufuo) -.

Na hiyo: Hakika Allah (s.w) ambaye ameumba ulimwengu huu kwa kudhihirisha kuwa yeye ni Mungu na Mwabudiwa kwa namna ya kitabu cha Mtegemewa na waja chenye kupewa mwili kiasi kila ukurasa katika kurasa zake unaelezea maana ya kitabu, na kila mstari katika mistari yake unadhihirisha maana ya ukurasa, na ameiumba kwa umbo la Qur’an ya subuhana yenye kupewa mwili kwa kiasi kwamba kila aya katika aya zake za kimaumbile, na kila neno katika maneno yake, bali hata herufi kati yake na kila nukta ni katika nafasi ya muujiza inamtukuza na kumtakasa, na ameiumba katika sura ya msikiti wa Mwingi wa rehema mkubwa na ameupamba kwa kiasi kisichokuwa na mpaka katika aya na nakshi zenye hekima, kiasi kwamba kila pembe katika pembe zake kuna kundi lililozama katika aina ya ibada ya kimaumbile kwa Muumba wao Mwingi wa rehema.

Je, inayumkinika kwamba huyu Muumbaji Mwaabudiwa wa haki asitume Maustadhi ili wasomeshe maana ya yaliyomo kwenye kitabu kikubwa na kuelimisha yaliyomo ndani yake? Au Je, inayumkinika asitume wafasiri ili wafasiri aya za Qur’an hiyo iliyopewa mwili ya Mtegemewa na kila mja?. Na je, inayumkinika kwamba asiteue maimamu wa msikiti huo mkuu ili kuwaongoza wale wanaoabudu kwa mitindo na namna mbali mbali za ibada?. Au je, inayumkinika Maustadhi wafasiri na maimamu hao asiwape amri za kifalme? Hasha na hapana na mara elfu hapana!

Kisha hakika Muumba Mwenye kurehemu Mwenye ukarimu ambaye ameumba ulimwengu huu ili kudhihirisha uzuri wa rehema yake kwa wenye utambuzi na wema wa upole wake kwao na ukamilifu wa ulezi wake kwao, na ili awahimize kushukuru na kuhimidi ameuumba kwa namna ya nyumba kubwa ya ugeni na maonesho ya kupendeza mapana na mahali pa matembezi pazuri pa kupendeza. Na ameandaa ndani yake kiasi kisicho na mpaka katika neema zenye ladha anuai na amepangilia humo kiasi kisichokuwa na mpaka katika maajabu ya ufundi yenye kupendeza.

Je, inayumkinika kwamba huyu Muumba Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu asizungumze kupitia Wajumbe wake na wenye utambuzi katika viumbe vyake katika nyumba ya ugeni yake hii ya kifahari. Au je, inaingia akilini kwamba asiwajulishe majukumu ya shukurani yao na namna ya kukiri kwao mkabala na neema hizo kubwa, na majukumu ya uja wao upande wa rehema zake enevu na upendo wake wa dhahiri?! Hapana, kisha mara elfu elfu hapana!

Kisha hakika Muumba ambaye anapenda uumbaji na ufundi wake na anataka kuleta kumstaajabia na kumthamini bali anataka watu watambue uzuri wake na kumtukuza kwa dalili ya kuweka kwake hisia kwa maelfu ya aina za vionjo kwenye vinywa basi Allah (s.w) hujitambulisha kwa kila kiumbe katika viumbe vyake na kwa hiyo anadhihirisha aina fulani katika uzuri wake na kuufanya mahali pa upendo wa viumbe wake, akaupamba ulimwengu huu kwa uzuri wa ufundi wake na viumbe wake.

Basi je, inaingia akilini kwamba huyu Muumba Fundi wa ajabu asizungumze na mwanadamu ambaye ni Bwana wa viumbe?. Na je inayumkinika kwamba asitume Wajumbe kutokana na watukufu hawa, ziwe hizo kazi nzuri bila kuthaminiwa na uzuri wa majina hayo mazuri yenye kufurutu ada bila kutambuliwa uzuri wake wala kustaajabiwa, na utambulisho wake na kupendezesha kwake kusiwe na mkabala wowote?! hasha na hapana kisha mara elfu hapana!

Kisha hakika mzungumzaji mjuzi ambaye anaitikia – katika wakati munasibu – maombi ya wenye uhai wote, akiitikia mahitaji yao ya kimaumbile na kutoa msaada kwa unyenyekevu wao na matakwa yao yanayoelekezwa kwake kwa ulimi wa hali, basi anaongea kwa uwazi na kimatendo na kwa hali kwa hisani zake kwao zisizokuwa na ukomo na neema zake kwao zisizokuwa na mpaka hali akiwa anadhihirisha makusudi, hiari na matakwa. Basi je, inayumkinika na je, inaingia akilini mzungumzaji huyu mjuzi azungumze na kiumbe mdogo mno aliye hai kwa kimatendo na kwa hali na kusaidia ugonjwa wake na kumsaidia kwa hisani yake na kukidhi haja zake, kisha asiweke wakuu wa kimaanawy kwa mwanadamu ambaye ni bwana wa viumbe wengi wa ardhini, na yeye ni khalifa wa Allah (s.w) katika ardhi yake, na yeye ni natija iliyoteuliwa kutoka katika viumbe?. Na je inaingia akilini asiseme nao kwa kauli na maneno kama anavyoongea na kila mwenye uhai kimatendo na kwa hali?. Na je, inawezekana asitume pamoja naye amri zake, nyaraka na vitabu vyake vitakatifu? Hashalillah, kisha mara elfu hapana!

Na kama hivi (Imani ya kuamini Akhera) pamoja na hoja zake thabiti za kukinaisha inathibitisha (Kuamini vitabu vyake) vitakatifu (Mitume wake) watukufu (a.s).

Kisha ambaye ameufanya ulimwengu ungurume kwa hakika ya Qur’an na kuremba sauti kwa hakika hiyo, na ambaye amemjua na kumjulisha Muumba wa ajabu kwa namna kamili zaidi akampenda na kuwafanya wengine wampende, na akatimiza shukurani yake kwake na kuwajulisha wengine kumshukuru, bali ameifanya ardhi inakariri (Subuhanallah, Alhamdulillah na Allahu Akbar) hata ikazisikilizisha mbingu za juu, ambaye amekutanisha ulezi wa kiungu uliyo dhahiri wa Muumba kwa uja mkunjufu wa jumla, akaongoza robo ya wanadamu kwa idadi na nusu yao kwa aina ndani ya miaka elfu moja na mia tatu uongozi ambao kutumia uongozi huo ameamsha hisia za bara na bahari na kuzijaza shauku na mapenzi, na ambaye ameinong’oneza Qur’an katika sikio la ulimwengu na kwa kitambo cha zama zote kuhusu makusudio ya kiungu, akatoa somo kubwa na akalingania malinganio matukufu, akidhihirisha majukumu ya mwanadamu na thamani yake, na kwa kubainisha cheo chake, huyo ni Muhammad (s.a.w) mwaminifu mkweli mwenye kusadikishwa kwa miujiza elfu moja na mmoja.

Je, inayumkinika mja huyu mtukufu mteule asiwe mtume mtukufu zaidi wa mwaabudiwa wa haki?. Na je, inayumkinika asiwe mtume wake mtukufu?. Hasha na hapana, mara elfu elfu hapana.

Basi hakika ya

(أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا الله)

pamoja na hoja zake kwa hiyo inathibitisha hakika ya

(أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُوْلُ الله)

Kisha hakika Muumba ambaye amejaalia viumbe wake wanabadilishana maneno kwa maelfu ya lugha na yeye ndiye ambaye anasikia maneno ya wote na kuyaelewa, je, inayumkinika kwamba yeye asiongee? Hapana kisha hapana! Na je, inaingia akilini kwamba asijulishe makusudio yake ya kiungu kwa kitabu kikubwa kama Qur’an tukufu ambayo inajibu maswali matatu ambayo akili zina tahayari mbele yake: Wapi vinatokea viumbe hivi? Na hatima ni wapi? Na kwa nini vinakuja baada ya vingine kisha havikai bila kupotea? Hapana.

Qur’an tukufu ambayo imetia nuru karne kumi na tatu na kuzipa mwanga, na ambayo wanapokezana kila saa ndimi mia moja milioni kwa heshima na utukuzo wote, na iliyoandikwa vifuani mwa mamilioni ya mahafidhi kwa kila heshima na utukufu, na ambayo imeongoza kwa kanuni zake sehemu kubwa ya wanaadamu, na imelea nafsi zao na kutakasa roho zao na kusafisha nyoyo zao na kuziongoza akili zao, na ambayo ni muujiza wa milele kama tulivyobainisha muujiza wake kwa namna arobaini katika Risale-i Nur, ikabainisha kwamba ina muujiza kwa watu kila tabaka miongoni mwa tabaka arobaini (kama ilivyokuja katika (Andiko la kumi na tisa) lenye karama ya ajabu). Qur’an hii tukufu kwa haki kabisa imestahiki kuitwa: (Maneno ya Allah (s.w)) Muhammad (s.a.w) akawa pamoja na maelfu ya miujiza yake ni muujiza wake wa dhahiri.

Je, inayumkinika Qur’an hii tukufu isiwe maneno ya yule mzungumzaji wa azali (s.w)? Na je, inayumkinika zisiwe amri za Muumba huyo wa milele (s.w)? Hashalillah na hapana na hapana mara elfu elfu hapana!

Basi (Imani ya Allah) pamoja na hoja zake kwa hiyo inathibitisha kuwa Qur’an ni maneno ya Allah (s.w).

Kisha hakika Mfalme mtukufu ambaye anajaza uso wa dunia kwa wenye uhai kisha anaupakua, hali ya kuimarisha dunia yetu kwa wenye utambuzi ili wamtambue (s.w), kumwabudu na kumsabihi.

Je, inayumkinika kwa mfalme huyu mwenye utukufu aziache mbingu na nyota zikiwa tupu, wala asiziimarishe kasri hizo za mbinguni kwa wenyeji na wakazi wanaolingana nazo?

Je inayumkinika kuacha (Mfalme huyu mtukufu) ufalme wa ulezi wake wa kiungu katika mamlaka zake kunjufu zaidi bila ya haiba na utukufu na bila wafanya kazi wenye kuamriwa na bila ya mabalozi Mitume na bila ya watazamaji waangalizi na bila watazamaji wenye kupendezwa, na bila waja wakirimiwa na bila ya raia watiifu? Hashalillah (s.w) na hapana kwa idadi ya malaika.

Hakika Mtawala Mwingi wa hekima Mjuzi wa kila kitu Mwenye kurehemu ambaye ameandika huu ulimwengu kwa muundo wa kitabu, hata amesajili historia ya maisha ya kila mti katika kila mbegu miongoni mwa mbegu zake, na kusajili majukumu ya maisha ya kila jani na majukumu ya kila ua katika kokwa zake zote. Na akaandika matukio yote ya uhai ya kila mwenye utambuzi katika nguvu zake za kuhifadhi ndogo kama punje ya haridali. Na kuhifadhi kila amali katika ufalme wake wote na kwa kila tukio katika ofisi za ufalme wake kwa kuchukua picha zake mbali mbali, na ambaye ameumba pepo, moto Sirata na mizani kubwa kwa ajili ya midhihirisho na kuthibiti kwa uadilifu, hekima, na rehema ambayo ni msingi muhimu kabisa wa ulezi wa kiungu.

Je inayumkinika kwa mtawala huyu Mwingi wa hekima na huyu Mjuzi Mwenye kurehemu asisajili matendo ya mwanadamu ambayo yanaambatana na viumbe?.

Na je inayumkinika kwamba asiandike matendo yake kwa ajili ya thawabu na adhabu na asiandike maovu yake na mema yake katika mbao za Kadari?! Hashalillah na hapana kwa idadi ya herufi za yaliyoandikwa katika Lauhul Mahafudhi kwa ajili ya Kadari.

Yaani hakika ya (Kumwamini Allah) pamoja na hoja zake inathibitisha hakika ya Imani ya (Kuamini malaika) kama inavyothibitisha pia hakika ya (Kuamini Kadari) uthibitisho wa kukinaisha kama jua ambalo linadhihirisha mchana na mchana ambao unajulisha jua.

Na kama hivi nguzo za kiimani zinathibitishana.

Nukta ya pili

Hakika yote ambayo vitabu na nyaraka za mbinguni zimelingania na mbele yake ni Qur’an tukufu na Daawah zote ambazo wamezitekeleza manabii (a.s) na mbele yao ni Muhammad (s.a.w), zinazunguka katika misingi thabiti na nguzo maalum. Na wote wamejitahidi kuthibitisha misingi na kuifundisha kwa wengine. Kwa hiyo hoja zote na dalili zote zinazoshuhudia unabii wao na ukweli wao zote kwa pamoja zinaelekea katika misingi hiyo na nguzo hizo jambo ambalo linaongeza nguvu na ustahiki. Na misingi hiyo si mingine isipokuwa ni kuamini Allah (s.w), siku ya mwisho, malaika wake, vitabu vyake, mitume wake na kadari kheri yake na shari yake ni kutoka kwa Allah (s.w).

Kwa hiyo haiyumkiniki kutenganisha kati ya nguzo sita za imani kabisa, kwani kila nguzo katika nguzo zinathibitisha nguzo zote kwa ujumla, bali inahitajia na kuilazimisha, kwa hiyo nguzo sita zote hazikubali kugawika kamwe, na jumla isiyokubali kugawanyika abadani. Kama ilivyo kila tawi miongoni mwa matawi ya mti uliobarikiwa (Mti wa Tuba) ambao shina lake linaloendelea mbinguni, na kila tunda katika matunda yake na kila jani katika majani yake linaegemea juu ya uhai wa milele wa mti huo, haiyumkiniki kwa yeyote kukanusha uhai wa jani moja linaloungana na mti huo maadamu hawezi kukanusha uhai wa mti huo uliyo dhahiri udhahiri wa wazi kama jua.

Na ikiwa ataukanusha mti huo utamkadhibisha kwa idadi ya matawi yake, matunda yake, na majani yake na kumnyamazisha, kadhalika imani na nguzo zake sita ipo katika sura hiyo hiyo.

Nia ilikuwa imefungwa juu ya kubainisha nguzo sita za imani  katika nukta sita na katika kila nukta moja kuna nukta tano zenye maana. Na makusudio yalikuwa kujibu swali lenye kuamsha mawazo lililopatikana kwenye utangulizi kwa ufafanuzi zaidi na ulio wazi, isipokuwa vizuizi na vipingamizi vimezuia hilo. Licha ya kuwa ninafikiri kwamba (Nukta ya kwanza) haikuacha njia yoyote ya kufafanua zaidi kwa wenye ufahamu kwa sababu hiyo ni kipimo tosha cha maudhui.

Na kama hivi imefafanuliwa kikamilifu kwamba, ikiwa Mwislamu atakanusha hakika yoyote ya imani, hakika ataporomoka katika ukafiri halisi, kwani nguzo za imani ni mnyororo iliyoungana pamoja, Uislamu umepambanua na kubainisha yale yaliyofupishwa katika dini nyingine.  Basi Mwislamu ambaye hamtambui Muhammad (s.a.w) na hamsadiki hatomjua Allah (s.w) (kwa sifa zake) na hataitambua Akhera vilevile. Imani ya Mwislamu ni yenye nguvu na imara kwa kiwango ambacho haitetereki kamwe na wala haiachi nafasi ya kukanusha kamwe, kwa sababu ya kuegemea kwake hoja nyingi sana hata kana kwamba akili inalazimika kukubali imani hii.

Nukta ya tatu:

Mara moja nilisema: “Alhamdulillah” kisha nikatafuta neema kubwa sana iliyo sawa na maana yake kunjufu mno ikapita kwenye moyo fungu la maneno lifuatalo:

[Alhamdulillah kwa kumwamini Allah, na juu ya upekee wake, na juu ya kupasa kuwepo kwake na sifa zake, na majina yake, shukurani kwa idadi ya midhihirisho ya majina  yake kutokea azali hadi milele]. Nikaichunguza na kuiona inaendana kabisa na maana, nayo ni kama ifuatavyo.

Maelezo yamekoma hapa ni kana kwamba pazia imefunikwa mbele ya Ustadh hivyo hakuendelea kuandika, au huenda mazingira aliyokuwamo yalizuilia hilo. Akatosheka na vifungu vilivyotangulia.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.