Dirisha La Thelathini Na Moja

Hapa tupo mbele ya dirisha la Mwanadamu, tunachungulia kupitia nafsi ya mwanadamu kwenye nuru ya Tawhiid, Nasi wakati tunaelekeza maelezo ya hilo kuelekea katika vitabu vya kawaida na vikubwa vilivyoandikwa na maelfu ya mawalii wema ambao wamechunguza kwa wasaa nafsi ya mwanadamu, tunapenda kuashiria ishara chache zilizofahamika kwa Ilhamu kutoka katika mwanga wa nuru ya Qur’an tukufu, nazo ni kama ifuatavyo:

Hakika Mwanadamu ni nakala inayokusanya sifa za kipekee zilizopo kwenye Ulimwengu, hadi mola wa haki anampa utambuzi wa majina yake mazuri yote yenye kudhihirika kwa sifa pambanuzi za kipekee zilizokuwa jumuishi ambazo ameziweka katika nafsi ya Mwanadamu.

Tunatosheka katika kubainisha hili kwa yale tuliyoyaeleza katika (Neno la kumi na moja) na katika Risala nyingine, isipokuwa hapa tutabainisha nukta tatu tu.

Nukta ya kwanza:

Hakika (Mwanadamu) ni kioo chenye kuakisi midhihirisho ya majina ya kiungu yaliyo mazuri, naye ni kioo cha majina hayo kwa pande tatu:

Sura ya kwanza:

Kama lilivyo giza ni sababu ya kuona nuru, yaani giza la usiku na kuzidi kugubika kwake kunabainisha mwanga na kuudhihirisha kwa namna ya wazi zaidi, basi mwanadamu vilevile kwa udhaifu wake, kushindwa kwake, ufukara wake, mahitaji yake, kasoro zake na upungufu wake, anatambulisha uweza wa mweza mwenye utukufu, nguvu yake kubwa, ukwasi wake wa hali zote na rehema zake kunjufu.

Mwanadamu kwa hiyo anakuwa kwa hili kana kwamba ni kioo chenye kuakisi nyingi ya midhihirisho ya sifa za kiungu zilizo tukufu. Bali hata anachobeba katika udhaifu mkubwa na aliyo nao katika maadui wasio na mpaka, kunamfanya daima kutafuta kwa bidii ngome ya kushikilia na mahala pa kuegemea, moyo wake wenye shauku mno haupati isipokuwa Allah (s.w).

Na yeye vilevile ni mwenye kulazimika kutafuta kwa bidii nukta ya kupata msaada anaomba haja zake kutoka katika nukta hiyo haja ambazo hazina ukomo na kwa nukta hiyo anakidhi ufukara wake usio kuwa na ukomo na kushibisha matumaini yake yasiyokuwa na ukomo, hakuti katika giza la kutafuta kwake ila kuegemea kutokea upande huu, kuelekea mlango wa Mkwasi Mwenye kurehemu na kunyenyekea kwake kwa dua na tawasali.   

Yaani katika kila moyo wa ndani kabisa kuna madirisha mawili madogo kwa upande wa nukta ya kuegemea na kuomba msaada, kupitia madirisha hayo mawili mwanadamu daima anachungulia  mahali pa utawala wa rehema ya Mweza Mwingi wa rehema.

Ama sura ya pili:

Ni kwamba mwanadamu ni kioo cha kudhihiri kwa majina mazuri, kwani vielelezo alivyotunukiwa vya kisehemu vya (Ujuzi, Uwezo, Uoni, Usikivu, Kutamalaki na Utawala) na mfano wa hizo katika sifa za kisehemu, anakuwa ni kioo chenye kuakisi kutokana na kioo hicho hutambulika sifa za hali zote za Allah (s.w), na kutambua ujuzi wake, uweza wake, uoni wake, usikivu wake, utawala wake na ulezi wake, kwa hiyo hufahamika sifa hizo za hali zote za ubwana mlezi wa Allah (s.w) kwa kulingana na hali ya mipaka yake kwake. Na hapana shaka baada ya hapo atazungumza na nafsi yake na kusema kwa mfano:

Kama mimi nilivyojenga nyumba hii na kujua migawanyo yake yote, na ninaona pande zake zote na sehemu zake na ninaiendesha mwenyewe, basi mimi ni mmiliki wake, kadhalika hapana budi kuwa huu ulimwengu mkubwa una Mtengenezaji na Mmiliki anayejua sehemu zake ujuzi kamili, na anona kila kidogo na kikubwa ndani yake  na anaiendesha.

Sura ya tatu:

Kwa kuwa mwanadamu ni kioo chenye kuakisi majina mazuri, basi yeye vilevile ni kioo chenye kuyaakisi kwa upande wa nakshi zake zinazodhihiri kwake. Hili limefafanuliwa kwa kiasi cha upambanuzi mwanzoni mwa (Kisimamo cha tatu) katika (Neno la thelathini na mbili) kuwa (Ainisho) lenye kukusanya la Mwanadamu ndani yake kuna zaidi ya nakshi sabini zilizo dhahiri katika nakshi za majina ya kiungu yaliyo mazuri.

Kwa mfano: Mwanadamu kwa kuwa kwake ni kiumbe anabinisha jina la fundi (Al-Khaliq) na kutokana na kuumbwa kwake vyema, anadhihirisha jina la (Ar-Rahman Ar-Rahiim), na anajulisha kutokana na namna ya malezi na uchungaji wake kwa jina la (Al-Kariim) na jina (Al-Latif). Na kama hivi Mwanadamu anadhihirisha nakshi anuai na tofauti za majina mazuri anuai kwa viungo vyake vyote na kwa vipole vyake vyote na hali zake zote za kimaanawy, na kwa milango yake ya fahamu yote na hisia zake zote. Yaani kama ilivyokuwa katika majina mazuri kuna jina kuu la Allah (s.w), basi ipo nakshi kuu katika nakshi za majina hayo na hiyo ni mwanadamu. Basi ewe unayejihesabu nafsi yako kuwa ni Mwanadamu wa kweli, isome nafsi yako kwa nafsi yako,  kama hukufanya basi huenda ukaporomoka kutoka ngazi ya utu kwenda katika ngazi ya wanyama.

Nukta ya pili:

Hii inaashiria siri muhimu sana katika siri za upekee, na ufafanuzi wake kama ifuatavyo: Kama ilivyo roho ya mwanadamu, inafungamana na mahusiano pamoja na pande zote za mwili wa mwanadamu, hadi inafanya viungo vyake vyote na sehemu zake zote kuwa katika kusaidiana kikamilifu kati yao. Yaani roho ambayo ni kipole cha kiungu na kanuni ya kiamri imevikwa uwepo wa nje kwa amri za kimaumbile ambazo ni udhihirisho wa utashi wa kiungu, hakizuilii kitu chochote katika kuendesha mambo ya kila sehemu katika sehemu za mwili, wala hakiishughulishi kitu chochote katika kupekua kwake na kutosheleza mahitaji ya mwili kwa kila sehemu katika sehemu zake, basi aliye mbali na karibu kwake ni sawa, wala kitu hakizuilii kitu kingine katu,  ambapo inaweza kukinyooshea kiungo kimoja misaada kutoka viungo vingine na inaweza kuvipeleka viungo vingine kwenda kukihudumia kiungo hicho, bali inaweza kujua haja zote kwa kila sehemu katika sehemu za mwili, na kuhisi kupitia sehemu hii kwa hisia zote, na kuendesha kutokea katika sehemu hii moja mwili mzima, bali roho inaweza kuona na kusikia kwa kila sehemu katika sehemu za mwili ikiwa imechuma hali ya kinuru zaidi.

Madhali roho ambayo ni kanuni ya kiamri katika kanuni za Allah (s.w), ina uwezo huu wa kudhihirisha mfano wa matendo haya katika ulimwengu mdogo ambao ni mwanadamu, basi vipi iwe ngumu juu ya utashi wa hali zote – na Allah (s.w) ana mfano wa juu – na juu ya uwezo wake wa hali zote kutenda matendo yasiyo na mpaka katika ulimwengu mkubwa, nao ni Ulimwengu na kusikia sauti zisizo kuwa na mpaka humo, na kujibu dua zisizokuwa na ukomo zinazotoka kwa viumbe wake? Basi yeye (s.w) hufanya analotaka katika ndani ya muda mmoja, hakimtopei kitu na wala hakijifuniki kwake chochote, wala hakizuiliki naye chochote, wala hakimshughulishi kitu dhidi ya chochote kingine. Vyote anaviona katika muda mmoja, na anasikia vyote katika muda mmoja. Kilicho karibu na kilicho mbali kwake ni sawa, akitaka kitu hukipelekea kila kitu. Anatazama kila kitu kutoka katika kitu chochote kiwacho, anasikia sauti za kila kitu, na anajua kila kitu kwa kila kitu kwani yeye ndiye Bwana Mlezi wa kila kitu.

Nukta ya tatu:

Uhai una ainisho kubwa muhimu na jukumu lenye umuhimu mkubwa, na kwa kuwa mada hii imepambanuliwa katika (Dirisha la Uhai) kutoka katika (Dirisha la ishirini na tatu) na katika Andiko la Ishirini, neno la nane la mada hiyo, tunaelekeza mada huko na hapa tunatanabahisha yafuatayo:

Hakika ya nakshi zilizochanganyika katika uhai na ambazo zinadhihiri katika sura ya milango ya fahamu na hisia, nakshi hizi zina ashiria majina ya Allah (s.w) yaliyo mazuri mengi na katika mambo ya kidhati ya Allah (s.w). Uhai kwa upande huu unakuwa ni kioo chenye kuakisi kiangavu kwa midhihirisho ya mambo ya kidhati ya Mola (Al-Hayyu Al-Qayyum).

Na kwa kuwa wakati wetu hautoshi kuweka wazi siri hii kwa wale ambao hawakumridhia Allah (s.w) kuwa Bwana Mlezi, na wale ambao hawajafika bado ngazi ya Imani ya yakini, kwa hiyo mlango huu tutaufunga.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.