Miiraji Ya Mtume (s.a.w)

Tanbihi

Hakika masuala ya Miiraji ni matokeo yanayokuja juu ya misingi ya imani na nguzo zake. Ni nuru inayochukua mwanga wake kutoka katika nuru za nguzo za kiimani. Hazisimamishwi hoja juu ya kuthibitisha Miiraji yenyewe hasa kwa makafiri wapingaji wa nguzo za Imani, bali haitajwi asilani kwa asiye amini Allah (s.w), wala hamsadiki mtume (s.a.w) au anakanusha malaika na mbingu, ila baada ya kutangulia kuwathibitishia nguzo hizo. Kwa hivyo muumini ambaye zinamtembelea shaka na dhana na kuiweka mbali Miiraji (kuona haiwezekani), tutamfanya kuwa shabaha ya mazungumzo yetu, tutambainishia yanayomfidisha na kumtosheleza Biidhinillah. Lakini tunamuona nyakati nyingine huyo kafiri ambaye anavizia katika nafasi ya usikilizaji hivyo tutamwelezea pia maneno yanayomfaidisha.

Hakika imetajwa ming’ao ya hakika ya Miiraji katika risala nyingine, tukaomba msaada kutoka kwa Allah (s.w) – pamoja na kushikilia kwa ndugu zangu wapendwa – kukusanya ming’ao hiyo iliyotawanyika, na kuifungamanisha na asili ya hakika yenyewe ili kuifanya ni kioo kinachoakisi mkupuo mmoja makamilifu ya uzuri wa mtume (s.a.w).

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ Qur’an, 17:1.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى۞ عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَى ۞ ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَى ۞ وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَى ۞ ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّى ۞ فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَى ۞ فَأَوْحَى إِلَى عَبْدِهِ مَا أَوْحَى ۞ مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى ۞ أَفَتُمَارُونَهُ عَلَى مَا يَرَى ۞ وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَى ۞ عِندَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى ۞ عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَى ۞ إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى ۞ مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَى ۞ لَقَدْ رَأَى مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَى Qur’an, 53:4-14.

Tunataja alama mbili tu, kutoka katika hazina kubwa kutoka katika aya tukufu iliyotangulia, nazo ni alama mbili zinazoegemea katika kanuni ya kibalagha kwenye dhamiri (Hakika yeye) na hii ni kwa uhusiano wake na suala letu hili, kama tulivyobainisha katika Risala ya (Al-Muujizat al-Qur’aniyyah).

Hakika Qur’an tukufu inahitimisha aya iliyotajwa hapo juu kwa:

إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ

hiyo ni baada ya kutaja kwa Israa ya Mtume Mpendwa (s.a.w), kutokea mwanzo wa Miiraji, yaani kutoka msikiti Mtukufu wa Makka hadi msikiti wa Aqsaa, na ukomo wake ambao surat An-Najm inauashiria. Basi dhamiri katika (Hakika yeye) ima irejee kwa Allah (s.w), au kwa Mtume mtukufu (s.a.w).

Ikiwa inarejea kwa Mtume (s.a.w), hakika kanuni za balagha na uwiano wa urari wa maneno vinafaidisha kuwa hakika ya matembezi haya ya kisehemu (kiasi kidogo) ndani yake kuna mwendo wa kiujumla na kupanda kiujumla kwa namna ambayo mtume (s.a.w) amesikia na kushuhudia kila alichokutana nacho kwa macho yake na masikio yake katika Ishara za kiungu, na maajabu ya ufundi wa kiungu wakati wa kupanda kwake katika ngazi za kiujumla za majina ya kiungu yaliyo mazuri zifikazo hadi kwenye Mkunazi wa ukomo. Hadi alikuwa ukaribu wa pinde mbili au karibu zaidi, katika yanayojulisha kwamba matembezi haya ya kisehemu yamo katika hukumu ya Ufunguo wa matembezi ya kiujumla yenye kukusanya maajabu ya ufundi wa kiungu.

Na ikiwa dhamiri inarejea kwa Allah (s.w), wakati huo maana inakuwa: Hakika yeye (s.w), alimwita mja wake kuhudhuria na kuwepo mbele zake ili amkabidhi jukumu na kumkalifisha kazi, kwa hivyo akampeleka kutoka msikiti mtukufu wa Makka hadi msikiti wa Aqsaa, ambao ni makutano ya manabii. Na baada ya kukutana nao na kumdhihirisha kwamba yeye ndiye mrithi kwa hali zote wa misingi ya Dini za manabii wote. Alimpeleka katika matembezi ndani ya ufalme wake na utalii ndani ya maeneo mengi ya ufalme wake, hadi kumfikisha katika Mkunazi wa ukomo akawa ukaribu wa pinde mbili au karibu zaidi.

Na kama hivyo, utalii au mwendo huo, ingawa ni Miiraji ya kisehemu, na kwamba aliyepelekwa Miiraji ni mja, isipokuwa mja huyu anabeba amana kubwa inayoambatana na viumbe wote, na ana nuru pamoja ya dhahiri inaangaza viumbe, na anabadilisha maana ya mandhari yake na kupamba kwa pambo lake, ukiachilia mbali kwamba anao ufunguo anaweza kufungulia mlango wa furaha ya milele na neema za kudumu.

Kwa ajili ya yote haya, Allah (s.w) anasifu nafsi yake:

إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ

ili aonyeshe kwamba katika amana hiyo na katika nuru hiyo na katika ufunguo huo, kuna hekima tukufu zinazojumuisha viumbe wote na kuzunguka ulimwengu wote.

Na siri hii ina misingi minne:

Kwanza:

Nini siri ya ulazima wa Miiraji?

Pili:

Nini hakika ya Miiraji?

Tatu:

Nini hekima ya Miiraji?

Nne:

Nini matunda na faida za Miiraji?

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.