Msingi Wa Kwanza

Kwa mfano husemwa:

Hakika ya Allah (s.w) naye ametakasika na mwili mahali na yuko karibu zaidi ya kila kitu kuliko kila kitu kama aya tukufu inavyoeleza:

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ Qur’an, 50:16.

Hata kila walii katika mawalii wema wa Allah anaweza kukutana na mola wake mlezi na kuongea naye moyoni mwake. Kwa nini kila walii anawafikishwa kuongea na Allah (s.w) ndani ya moyo wake, wakati ambapo uwalii wa Muhammad unawafikishwa kuongea naye baada ya mwendo mrefu na matembezi marefu kwa Miiraji?.

Jibu:

Tunaisogeza siri hii iliyojifumba katika ufahamu kwa kutaja mifano miwili, isikilize, na mifano hiyo imetajwa katika (Neno la kumi na mbili) katika kutaja siri ya muujiza wa Qur’an na hekima ya Miiraji.

Mfano wa kwanza:

Hakika ya mfalme ana aina mbili za mazungumzo na kukutana, na sampuli mbili za kuongea, takrima na kuonesha umuhimu.

Kwanza:

Mazungumzo maalum kupitia simu maalum, na mmoja wa raia wake katika watu wa kawaida, katika jambo dogo linalohusu haja mahususi kwake.

Na nyingine:

Mazungumzo kwa niaba ya ufalme mkuu na kwa anuani ya Ukhalifa mkuu, na kwa sifa ya utawala ya jumla, kwa jambo la hadhi ya juu tukufu anadhihirisha adhama yake na kubainisha heshima yake, inakusudiwa kwa mazungumzo hayo kueneza amri zake za kifalme katika pande mbali mbali. Ni mazungumzo yanapita pamoja na mmoja wa wajumbe wake katika ambao amri hizo zinawahusu, au pamoja na mmoja wa wakubwa wa maafisa wake katika ambao amri hizo zinawahusu.

Na kama hivi, kwa mfano kama huu – na Mwenyezi Mungu ana mfano wa juu – hakika Muumba wa ulimwengu wote na mmiliki wa ufalme na falme zote, na mtawala wa kiazali kwa hali zote, ana sampuli mbili za mazungumzo na kuonesha umuhimu na takirima:

Ya kwanza:

Ni ya sehemu ndogo na mahususi:

Na nyingine:

Ni ya sehemu nzima na ya jumla.

Basi Miiraji ya mtume (s.a.w), ni mwonekano wa heshima wa hali ya juu ya uwalii wa Muhammad uliodhihiri kwa hali ya ukamilifu wote unaopita uwalii wote na kwa cheo na kuwa juu ya uwalii wote, kwani yeye (s.a.w) amepata heshima ya kuongea na Allah (s.w), na kuzungumza naye kwa karibu kwa jina la mola wa walimwengu na kwa anuani ya muumba wa vilivyomo.

Mfano wa pili

Mtu anashika kioo kuelekea jua, kwa hiyo kioo kinachota  kulingana na uwezo wake, mwanga unaobeba rangi saba kutoka kwenye jua. Hapo mtu anakuwa na uhusiano na jua kulingana na kile kioo, na anaweza kufaidika kutokana nalo ikiwa atakielekeza kwenye chumba chake chenye giza au katika bustani yake maalum ndogo iliyowekewa paa, licha ya kuwa kufaidika kwake na mwanga kunaishia tu kwa kadiri ya upokeaji wa kioo kwa mwanga unaoakisi kutoka kwenye jua na sio kwa kadiri ya ukubwa wa jua.

Wakati ambapo mtu mwingine anaacha kioo, na kulielekea jua moja kwa moja, na anashuhudia haiba yake na kutambua adhama yake, kisha anapanda juu ya mlima mrefu sana na anaangalia katika mmuliko wa utukufu wake mkubwa sana, na kulielekea kwa dhati bila ya pazia, kisha anarejea na kufungua madirisha mapana upande wa jua hali ya kuwa liko juu sana mbinguni kutoka katika nyumba yake ndogo au katika bustani yake yenye paa, na kufanya mazungumzo na mwanga wa kudumu wa jua la kihakika.

Na kama hivi mtu huyu anaweza kufanya mkabala huu na mazungumzo haya yenye kuliwaza yaliyovikwa taji la shukurani na kukiri neema, na kuzungumza na jua kwa kusema: “Ewe jua! Ewe uliyetandawaa katika kiti cha enzi cha uzuri wa ulimwengu! Ewe kipole cha mbingu na mwanga wake! Ewe uliyeweka juu ya Ardhi furaha na nuru na kutunuku tabasamu na furaha kwa maua! hakika umeipa nyumba yangu na bustani yangu ndogo joto na mwanga kwa pamoja, kama ulivyoipa dunia nuru na Ardhi joto. Wakati ambao mwenye kioo wa awali hawezi kuzungumza na jua kwa mfano wa mazungumzo haya, kwa sababu athari za mwanga wa jua zina ukomo wa mipaka ya kioo na masharti yake. Na unaishia tu kulingana na uwezo wa kioo kupokea mwanga.

Na kama hivi inaonekana kudhihiri kwa dhati ya Allah wa pekee mwenye kukusudiwa kwa haja zote (s.w). Na yeye ni nuru ya Mbingu na Ardhi na Mfalme wa azali na milele juu ya hakika ya kibinadamu kwa sura mbili, ambazo zinabeba viwango visivyo na mpaka.

Sura ya kwanza:

Kudhihiri katika kioo cha moyo kwa mafungamano ya kiungu mola mlezi na kunasibika kwake, kiasi kwamba hakika kila mwanadamu ana fungu na nuru hiyo ya kiazali, na ana mazungumzo nayo ni sawa tu iwe katika hali ya sehemu, au hali ya kiujumla, kulingana na u- tayari wake na kulingana na kudhihiri kwa majina na sifa, na hiyo ni katika mwendo wake ndani ya ngazi hizo. Basi ngazi za walio wengi katika uwalii unaoenda chini ya vivuli vya majina mazuri na sifa tukufu na ngazi zake zinatokana na sehemu hii.

Sura ya pili:

Kudhihiri kwa Allah (s.w) kwa mtu mtukufu mno katika sampuli ya wanadamu na mbora wao wote kwa jumla, kudhihiri kwa dhati yake (s.w), na kwa ngazi kuu kabisa katika ngazi za majina yake mazuri, kwa kuwa mwanadamu ni mwenye kuweza kudhihirisha midhihirisho ya majina ya Allah (s.w) mazuri yenye kudhihiri katika Uwepo wote kwa mkupuo mmoja katika kioo cha roho yake, kwa kuwa yeye ndiye tunda lenye nuru zaidi la mti wa viumbe na mwenye kujumuisha zaidi kwa upande wa sifa na maandalizi.

Hakika kudhihiri huku ndio siri ya Miiraji ya Mtume (s.a.w), kiasi kwamba uwalii wake ni mwanzo wa ujumbe wake. Uwalii ambao unatembea ndani ya kivuli, kama mtu wa kwanza katika mfano wa pili, wakati ambapo hakuna kivuli katika utume, bali unaelekea kwenye dhati tukufu moja kwa moja, kama mtu wa pili katika mfano wa pili. Ama Miiraji kwa kuwa ni karama kubwa ya uwalii wa Muhammad na ngazi zake za juu, imepanda na kugeuka katika ngazi ya utume.

Basi ndani ya Miiraji kuna uwalii, kwani amepandishwa kutoka kwa viumbe kwenda kwa Mola wa haki (s.w), na dhahiri ya Miiraji ni ujumbe; kwa vile unatoka kwa Mola wa haki (s.w), kwenda kwa viumbe wote, basi uwalii ni kupita katika ngazi za ukaribu kuelekea kwa Allah (s.w), nao unahitaji muda na kupita ngazi nyingi. Ama utume ambao ni nuru kuu kabisa, unaelekea katika kufunuka siri ya kuwa karibu zaidi kwa kiungu; ambayo inatosha punde kidogo sana na muda unaokwenda haraka. Na kwa sababu hii ndio maana imepokewa katika hadithi tukufu kinachofidisha kwamba yeye alirejea haraka papo hapo.

Na sasa tunaelekeza maneno yetu kwa yule kafiri ambaye amekaa mkao wa kusikiliza, basi tunasema: Kwa kuwa ulimwengu huu unafanana na nchi ya kifalme iliyo katika mpangilio mkubwa, na mji ambao uko katika upeo wa kuratibiwa, na kasri yenye upeo wa mapambo na uzuri, hapana budi kuwa una mtawala, mmiliki, na mtengenezaji. Na kwa kuwa mmiliki huyo mtukufu na Mtawala mkamilifu na fundi mzuri yupo, na kuna mtu mwenye mtazamo wa kiujumla na mwenye mahusiano enevu kwa milango yake ya fahamu na hisia zake pamoja na ulimwengu huo, na nchi hiyo ya kifalme na kasri hiyo, hapana budi kwamba fundi huyo mtukufu atakuwa na uhusiano mtukufu wenye nguvu, pamoja na mwanadamu huyu mwenye kumiliki mtazamo wa kiujumla na hisia enevu, na hapana shaka atakuwa na mazungumzo matakatifu na mwelekeo wa hadhi ya juu.

Na kwa kuwa Muhammad (s.a.w), Nabii asiyejua kusoma (maandishi) amedhihirisha uhusiano huo wa hadhi ya juu kati ya wale ambao waliopata heshima hiyo tangu zama za Bwana wetu Adamu (a.s), kwa sura kuu na tukufu zaidi, kwa ushahidi wa athari zake, yaani kwa utawala wake kwa nusu ya Ardhi na sehemu ya tano ya wanadamu, na kubadilisha mwonekano wa kimaanawy wa viumbe na kuviangazia nuru, kwa hiyo yeye ni mwenye kustahiki zaidi kupata utukufu wa Miiraji ambayo ni ngazi kuu kabisa katika ngazi za uhusiano huo.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.