Msingi Wa Nne

Nini matunda ya Miiraji na faida zake?

Jibu:

Miiraji hii kuu ambayo ni mti wa Tuba wa kimaanawy ina faida kubwa nyingi, na matunda manono yapo hadi chini kiasi zaidi ya matunda na faida mia tano. Isipokuwa tutataja hapa matano tu kati ya hayo kwa njia ya mfano:

Tunda la kwanza

Ni kuona hakika za nguzo za Imani, kuona kwa jicho hasa, yaani kuona malaika, pepo na Akhera, bali hata kuiona dhati tukufu, kuona huku na kushuhudia kwa hakika kumeipa viumbe wote na wanadamu kwa sifa maalum hazina kubwa isiyokwisha, na nuru ya kiazali haififii, na zawadi ya milele ya thamani, kwani nuru hiyo imevitoa viumbe vyote katika inayodhaniwa kwamba vinaporomoka katika hali za kutoweka, kuondoka vya migongano na ya machungu, na kuvidhihirisha katika hakika yake kwamba ni maandishi ya kiungu Mtegemewa na kila kitu, na barua za kiungu Mola mlezi zilizo takatifu, na vioo vizuri vinaakisi uzuri wa upekee, jambo lililoingiza furaha katika nyoyo za wenye utambuzi wote bali limewafurahisha viumbe wote.

Na kama hiyo nuru ilivyowatoa viumbe kutoka kwenye hali za maumivu za kudhaniwa, imemtoa mwanadamu asiyejiweza mbele ya maadui wasio na mpaka, fukara wa mahitajio mengi kutokana na hali za kutoweka za kupotea anababaika nazo. Ikaweka wazi sura yake ya hakika kwamba ni muujiza katika miujiza ya uweza wa Allah (s.w), na kiumbe wake ambaye yuko katika umbo bora kabisa, na nakala jumuishi ya barua zake za kiungu, na msemeshwa mtambuzi wa Mfalme wa azali na milele na mja wake mahususi, na mwenye kuhisi makamilifu yake na mwandani wake mpendwa, na mwenye kupendezwa kwa uzuri wake mtakatifu na mpendwa, na mgeni mwenye kukirimiwa mbele yake na mwenye kupitishwa kuingia pepo yake ya kubaki milele.

Ee, furaha kubwa iliyoje isiyo na ukomo! Na shauku kubwa isiyo na mwisho nuru hii humpa kila mwenye kujizingatia kuwa yeye ni mtu.

Tunda la pili

Nalo ni kwamba ameleta misingi ya Kiislamu ikitanguliwa na (Swala). Misingi ambayo inawakilisha mambo yanayomridhisha mola mlezi wa walimwengu, Mtawala wa azali na milele. Hakika amezileta zikiwa ni zawadi na tunu nzuri kwa majini na watu wote.

Hakika kuyajua hayo yanayomridhisha Mola Mlezi peke yake huamsha kwa mwanadamu mapenzi na shauku na kutazamia kutaka kuyajua kwa kiasi kisicho yumkinika kukielezea, ukiachilia mbali furaha na ukunjufu inayoleta, kwani hakuna shaka kwamba kila mwanadamu anataka kwa bidii kujua, japo kutokea mbali, yale ambayo Mfalme wake anayataka ambaye amemneemesha, na ana shauku kwa pupa ajue nini anataka kwake ambaye amempa neema zake na kumtendea wema? Na hata anapojua yanayomridhia humjaa furaha kubwa na kumuenea ridhaa na utulivu, bali hata anatamani kutoka moyoni mwake wote kwa kusema: “Ee laiti kungekuwapo na mkaa kati baina yangu na  mola wangu ili nijue anachokitaka kutoka kwangu, na nini anataka niwe kwake”?.

Naam, hakika mwanadamu ambaye ni muhitaji sana kwa mola wake (s.w) kila wakati, na katika kila hali zake na mambo yake, na amepata fadhila zake tukufu, na neema zake enevu kiasi kisichohesabika, na yeye ana yakini kwamba vilivyopo vyote vipo katika mkono wa usarifu wake (s.w), na yanayoshamiri katika nuru ya uzuri na ukamilifu juu vilivyokuwepo, si kingine isipokuwa ni kivuli dhaifu ukilinganisha na uzuri wake na ukamilifu wake (s.w), nasema: Je, ni kiasi gani mwanadamu huyu anakuwa na shauku na pupa ya kutambua yanayomridhisha bwana Mlezi, na kutambua anachotaka kutoka kwake! huenda unathamini hili!. Basi huyo hapo Mtume Mtukufu (s.a.w) amekuja na mambo yanayomridhisha Mola Mlezi wa walimwengu na hakika ameyasikia kwa moja kwa moja kwa haki ya yakini nyuma ya pazia sabini elfu, ameyaleta hayo ikiwa ni tunda katika matunda ya Miiraji na kuyaleta yakiwa ni zawadi nzuri kwa watu wote.

Al-Bukhary, Manaqibul answary 42. Muslim, Al-Iman 279; Al-Musafirina 253; Attirmidhy, Tafsir ya Suratu Al-Najm 1; Al-Nasaiy, Al-Swala 1; Al-Iftitah 25; Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad 1/387,422.

Naam, Hakika ya mwanadamu ambaye anataka kujua nini kinatokea mwezini? Na akienda mmoja wao huko na kurudi na kueleza yalioko huko pengine atajitolea kwa wingi kwa ajili ya habari hiyo, itamchukua tahayuri na kupendezwa kila anapotambua habari za yaliyo huko!!.

Ninasema ikiwa hali ya mwanadamu ni kama hivi na habari za aliyekwenda mwezini, basi vipi itakuwa pupa yake na shauku yake kupokea habari za anaye kuja kutoka kwa Mmiliki wa ufalme mwenye utukufu ambaye mwezi katika ufalme wake sio chochote isipokuwa kama nzi anaye ruka kuzunguka kipepeo, huyo kipepeo anaruka kuzunguka taa miongoni mwa maelfu ya mataa ambazo zinaangazia mahali pake pa wageni.

Naam, hakika Mtume (s.a.w) aliona mambo ya huyu mfalme mtukufu (s.w) na kashuhudia maajabu ya utengenezaji wake na hazina za rehema zake katika ulimwengu wa kubakia. Na amerejea baada ya kuona hayo na kuwasimulia watu aliyoyaona na kuyashuhudia.

Kama watu hawakumsikiliza Mtume huyu mtukufu (s.a.w) kusikiliza kwa shauku na utashi na kwa utukuzo wote na kupendezwa, basi fahamu kiasi cha kujitenga kwao na akili na kuepuka kwao hekima.

Tunda la tatu

Hakika ameshuhudia kanzi za furaha ya milele na neema madhubuti za kudumu, na kupokea ufunguo wake, na kuuleta ikiwa ni zawadi kwa wanadamu na majini.

Naam, ameshuhudia kwa jicho lake kwa Miiraji pepo ya kudumu milele, na ameona midhihirisho ya milele ya rehema ya mwingi wa rehema Mwenye kurehemu (s.w), na ametambua utambuzi kwa haki ya yakini furaha ya milele, akaleta habari njema ya kuwepo kwa furaha ya milele kwa majini na wanadamu, habari hiyo kubwa ambayo wanaadamu wanashindwa kuielezea. Wakati ambapo hali ya kudhania inamzunguka jini na mwanadamu, ambapo vyote vilivyomo vinapigwa kofi kwa makofi ya kutoweka na utengano katika dunia isiyo na utulivu, na kutiririka kwa muda na harakati za Atomu huzoazoa kwenda kwenye bahari ya kukosekana na utengano wa milele, naam, katika hali hizi za kuumiza ambazo zinatoa roho za majini na wanadamu zinawazunguka kwa kila upande, tahamaki habari hiyo ya kufurahisha inawajia, pima katika mwanga wa hili, ni kiasi gani kinacholetwa na habari hizo njema cha furaha kwa majini na wanadamu ambao wanadhani kwamba wamehukumiwa dhidi yao kunyongwa kwa milele, na kwamba hao wawili ni wenye kutoweka kabisa! kisha fahamu baada ya hapo thamani ya habari hiyo njema! Mwenye kuhukumiwa kunyongwa angeambiwa wakati akipiga hatua zake kuelekea kwenye kitanzi: (Hakika Mfalme amefanya ukarimu kwa kukusamehe, isitoshe amekupa nyumba kwake). Una nafasi ya kupata picha ya kiasi maneno haya yanavyofungua mawanda ya furaha kwa huyo aliyehukumiwa kunyongwa. Na ili uweze kupata picha ya thamani ya tunda hili na habari hii njema sana, kusanya furaha zote hizo kwa idadi ya majini na watu ili ukadirie umuhimu wa habari hiyo njema!.

Tunda la nne

Ni kuona uzuri wa Allah (s.w), kama alivyotunukiwa hilo mtume (s.a.w) imekuja (habari) kwamba inayumkinika kwa kila muumini kupata hilo tunda lililobaki vilevile. Kwa hili ametoa zawadi kubwa kwa majini na watu. Na huenda unaweza kukadiria kiasi cha ladha iliyomo katika tunda hilo lililotolewa zawadi na kiasi cha utamu wake na uzuri wake na ughali wake kupitia mfano huu:

Hakika kila anayebeba moyo ulio hai, bila shaka anampenda mwenye kuwa na uzuri na ukamilifu na hisani, na mapenzi haya yanazidi kulingana na daraja za huo uzuri ukamilifu na hisani, hata inafikia daraja ya ashiki na kuabudu, basi mwenye nayo hayo anajitolea anachomiliki kwa ajili ya kuona uzuri huo, bali anaweza kujitolea dunia yake yote kwa ajili ya kuuona mara moja. Na tukijua kwamba uwiano wa katika vilivyokuwepo katika uzuri ukamilifu na hisani, kuwianisha na uzuri ukamilifu na hisani yake (s.w) haufikii kuwa ving’ao hafifu kuwiana na jua lenye kuangaza. Kwa hiyo unaweza kutambua – ukiwa kweli ni Mtu – kiasi kinacholeta katika furaha ya kudumu na kiasi kinacholeta katika furaha, ladha na neema, kuwafikishwa kumuona ambaye mwenye kustahiki mapenzi bila ukomo na kumuona bila ukomo katika furaha bila ukomo.

Tunda la tano

Nalo ni kwamba mwanadamu – kama ilivyofahamika kutoka kwenye Miiraji – ni tunda la thamani katika matunda ya viumbe, mwenye cheo kitukufu, na kiumbe aliyekirimiwa mpendwa mbele ya Mtengenezaji Mtukufu. Tunda hili zuri mtume (s.a.w) amekuja nalo kwa Miiraji, ikiwa ni zawadi kwa majini na watu, Tunda hilo likamnyanyua mwanadamu kutoka katika kuwa kwake ni kiumbe mdogo na mnyama dhaifu na mwenye utambuzi asiyejiweza hadi makamo ya juu na ngazi ya juu, bali kwenda katika makamo ya juu mno yenye utukufu na kukirimiwa kuliko viumbe wote. Tunda hili hivyo basi limempa mwanadamu furaha ya dhati kiasi cha kushindwa kuielezea.

Kwa sababu mwanajeshi mmoja akiambiwa: Umekuwa afisa wa cheo cha juu katika jeshi, kiasi gani atahisi kuwa amefanyiwa wema na shukurani yake na furaha yake na ridhaa yake itakuwaje? Haikadiriwi kwa vyovyote, wakati ambapo kiumbe dhaifu na mnyama mwenye kufikiri, na asiyejiweza mwenye kutoweka, aliye dhalili mbele ya dhoruba za kuondoka na kutengana, angeambiwa: Hakika wewe utaingia pepo ya milele na kupata neema za Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu kunjufu ya kubaki, utembee katika ufalme na falme zake ambao una upana wa Mbingu na Ardhi, na ustarehe nao kwa mapendeleo yote ya moyo katika kasi ya kufikirika na kwa upana wa roho na kutembea kwa akili, na juu ya yote haya utapata kuuona uzuri wake katika furaha ya milele. Kila mwanadamu, ambaye utu wake haujaporomoka anaweza kutambua kiasi cha furaha zinazomjaa yule ambaye anayeambiwa mfano wa maneno haya.

Na sasa tunaelekea kwa yule aliyekaa katika nafasi ya usikilizaji, tunamwambia: Chana kanzu ya ukafiri, na uitupe mbali, na usikilizie kwa sikio la muumini, na uweke macho ya Mwislamu, nitakubainishia thamani ya matunda machache kupitia mifano midogo miwili:

Mfano wa kwanza:

Kwa mfano tuko pamoja nawe katika ufalme mpana. Kila unapoelekeza macho yako kuangalia huoni isipokuwa uadui, kila kitu ni adui yetu, na kila kitu kinadhamiria uadui kwetu, kila kilichomo humo ni kigeni kwetu hatukitambui, Na kila pembe yake imejaa majeneza yanayoamsha woga na mshangao. Na zinapaa sauti huku na huko ni sauti za maombolezo na kuomba msaada kwa mayatima na wadhulumiwa. wakati tukiwa katika majonzi na maumivu haya, ghafla mmoja anakwenda kwa mfalme wa ufalme na anakuja kutoke huko na habari njema ya kufurahisha kwa wote.

Basi hapo ikiwa habari hiyo ya furaha itabadilisha vilivyokuwa vigeni kwetu na kuwa wapenzi, ikibadilisha umbo la tuliyekuwa tunamwona ni adui na kuwa katika sura ya ndugu mpenzi. Na ikidhihirisha kwetu majeneza mfu yenye kuhofisha katika sura ya waja wenye kumdhukuru Allah (s.w) wenye kumsabihi kwa kumsifu, na ikageuza kelele hizo na maombolezo hayo kuwa katika mfano wa himidi, kusifia na kushukuru. ikiwa itabadili wale maiti na upokonyaji kuwa ni ruhusa na kusamehewa kutokana na mizigo ya majukumu. Na tukiwa tunashirikiana na wengine katika furaha yao ukiachilia mbali furaha yetu. Hapo utaweza kukadiria kiasi gani cha furaha ambayo inatuenea kwa sababu ya habari hiyo njema.

Na kama hivi, moja ya matunda ya Miiraji ni nuru ya Imani, dunia isingekuwa na tunda hili, yaani ikiwa viumbe vitaangaliwa kwa mtazamo wa upotevu, vilivyokuwepo hutuviona isipokuwa vigeni vya kuogofya, vyenye kukera, na vyenye kudhuru, na miili mikubwa – kama milima – kuwa ni majeneza yanayoamsha mshangao na hofu. Na muda uliopangwa ni mnyongaji anakata shingo za vilivyokuwapo na kuvitupa katika kisima cha kutokuwepo. Na sauti zote na miangwi yote si chochote isipokuwa ni kelele na maombolezo hutokana na kutengana na kutoweka.

Wakati ambapo upotevu unakupa sura kama hivi ya vilivyokuwepo, tahamaki tunda la Miiraji ambalo ni hakika za Imani linanawiri vilivyokuwepo vyote na linabainisha kwamba hivyo ni wapenzi wenye kuishi kidugu, katika tasbihi na kumdhukuru Mola wao Mlezi, na umauti na kuondoka ni ruhusa kuachiliwa huru kutokana na majukumu na kupumzishwa nayo. Na hizo sauti ni tasbihati na tahmidati, na kama hivi, ukitaka kuona hakika hii kwa sura yake iliyokuwa wazi zaidi rejea (Neno la pili) kutoka katika  (Maneno mafupi).

Mfano wa pili:

Kwa mfano kwamba tupo na wewe katika jangwa kubwa. Pepo za michanga kutoka kila upande zinatuzunguka, na giza la usiku linatuzuia kona kila kitu hata tunakaribia kutoona mikono yetu. Na njaa inatushambulia na kiu kina unguza nyoyo zetu, na hatuna msaidizi wala hatuna makimbilio. Chukua picha ya hali hii ambayo tunasukwasukwa ndani yake, tahamaki mtu mkarimu ana chana pazia ya giza kisha anakuja kwetu, akiwa na kipando cha kifahari akituletea zawadi kwetu, na kutuchukua hadi kwenye mahali panapofanana sana na ilivyo pepo. Kila kitu ndani yake kiko katika hali nzuri, na kila kitu kimetayarishwa na kukusudiwa sisi, anatutawalia yule ambaye yupo katika ukomo wa rehema, huruma na upole, na hakika ametuandalia sisi kila tunachohitaji miongoni mwa nyenzo za kula na kunywa na ninakudhania sasa unathamini kiasi gani tuwe ni wenye kushukuru fadhila ya huyo mtu mwema, ambaye ametuchukua kutoka mahali pa kukata tamaa na kuvunjika moyo kwenda mahali ambapo pote ni matumaini na furaha.

Basi jangwa hilo kubwa ni hii dunia, na hivyo vimbunga vya mchanga ni harakati za Atomu na mitiririko ya wakati ambazo husukwasukwa vilivyokuwamo kwa vimbunga hivyo na huyu mwanadamu masikini. Kila mwanadamu ana hofu mwenye kuhofia yale yanayofichwa na siku zake za usoni zenye giza zenye kutisha, kama hivi upotevu unamwonesha na wala hajui atake msaada kwa nani? Na hali ya kuwa anapata picha ya njaa na kiu.

Na kama hivi, kujua mambo yanayomridhisha Allah (s.w), nalo ni tunda katika matunda ya Miiraji, kunafanya hii dunia kuwa ni mahali pa wageni pa mwenyeji mwema mkarimu, na kufanya watu kuwa ni wageni waliokirimiwa, na wenye kuamrishwa na yeye katika wakati huo huo, na amewadhaminia mustakabali wenye kung’ara kama pepo ya starehe na yenye ladha kama rehema, na yenye kung’ara kama furaha ya milele.

Ukiwa na picha hii na ile, wakati huo unaweza kupimia kiasi cha ladha ya tunda hilo, uzuri wake na utamu wake!.

Hakika aliyekuwa katika nafasi ya usikilizaji anasema: Himidi kwa Allah (s.w) na shukurani kwa Allah shukurani elfu kwa fadhila zake nimeokoka na ukafiri, nikapita njia ya imani na tawhiidi. Na nimevuna imani Alhamdulillah.

Na sisi tunamwambia: Ewe ndugu! Tunakupongeza kwa imani, na tunamwomba Allah (s.w) atujaalie tuwe katika watakaopata shufaa ya Mtume (s.a.w).

اللَّهُمَّ صَلِّ عَـلَى مَنِ انْشَقَّ بِإِشَارَتِهِ الْقَمَرُ، وَنَبَعَ مِنْ أَصَـابِعِهِ الْمَـاءُ كَالْكَوْثَرِصَاحِبِ الْمِعْرَاجِ وَمَازَاغَ الْبَصَــر،ُ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ أَجْمَعِيْنَ. مِنْ أَوَّلِ الدُّنْيَا إِلَى آخِرِ الْمَحْشَرِ.

 (سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ)

 (رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ)

 (رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِيْنَا أَوْ أَخْطَأْنَا)

 (رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا)

 (رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)

 (وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ)

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.