Msingi Wa Pili

Ni nini hakika ya Miiraji?

Jibu:

Miiraji ni kwenda kwa dhati ya Muhammad na kupita kwake katika ngazi za ukamilifu.

Na hii ina maana kwamba ishara za kiungu na athari zake ambazo amezidhihirisha (s.w) katika kupangilia viumbe, kwa majina na anuani tofauti, na amedhihirisha adhama ya Uungu wake kwa kupatisha na kuendesha katika mbingu ya kila duru katika duru alizozitengeneza vyema, kila mbingu kuna eneo kubwa la arshi ya ulezi wa kiungu na kituo kitukufu katika kusarifu kwa uungu. Ishara hizi kuu na athari tukufu, Allah (s.w) alizionesha moja moja kumwonesha mja huyo aliyefanywa kuwa mahususi mteule, buraq alikwenda naye juu na kukata ngazi kama umeme kutoka duru moja kwenda duru nyingine na kutoka kituo hadi kituo, kama vituo vya mwezi, ili amwoneshe Rububiyya ya Uluhiyya yake mbinguni, na kumkutanisha na ndugu zake mitume mmoja mmoja, kila mmoja katika makamo yake katika mbingu hizo, hadi akampandisha katika makamo ya (Ukaribu wa pinde mbili) akamtukuza kwa upweke, kuongea naye na kwa kumuona, ili kumjaalia mja huyo kuwa ni mja mwenye hali jumuishi za makamilifu yote ya kibinaadamu, akiwa mwenye kupata midhihirisho yote ya kiungu, akiwa ni mwenye kushuhudia juu ya matabaka yote ya viumbe, mlinganiaji katika mamlaka ya kiungu, mfikishaji wa vyenye kuridhiwa na Allah (s.w), mwenye kufumbua talasimu (fumbo) la viumbe. Inawezekana kuiona hakika hii ya thamani kupitia mifano miwili:

Mfano wa kwanza

Tumeufafanua katika (Neno la ishirini na nne), kwamba mfalme ana anuani tofauti katika ofisi za Serikali yake, na sifa mbalimbali kulingana na matabaka ya raia wake, na majina na alama mbali mbali katika ngazi za ufalme wake, kwa mfano: Ana jina la mtawala mwadilifu katika ofisi za haki na anuani ya mfalme katika ofisi za kiraia, wakati ambao ana jina la kamanda mkuu katika ofisi za kiaskari na anuani ya khalifa katika ofisi za kisharia, na kama hivi ana majina mengine na anuani, ana katika kila ofisi miongoni mwa ofisi za dola yake makamo na kiti kwa hali iliyo kama kiti cha enzi chake cha kimaanawy, na kwa hivi inayumkinika kwa mfalme huyu mmoja kuwa ni mmiliki wa majina elfu moja na moja katika ofisi za ufalme huo na katika ngazi za tabaka za serikali, yaani anaweza kuwa na viti vya enzi elfu moja na kimoja vyenye kuingiliana, na hata kana kwamba mtawala huyu yupo katika kila ofisi miongoni mwa ofisi za dola yake, na anajua yanayotokea humo kwa haiba yake ya kimaanawy, (mfumo unaotenda kama mtu mmoja) na ujumbe wake maalum. Na anashuhudiwa na kushuhudia katika kila tabaka, kwa kanuni yake na mfumo wake na wawakilishi wake, na anaangalia na kuongoza kutokea nyuma ya pazia kila ngazi kati ya ngazi hizo kwa hekima yake, ujuzi wake na kwa nguvu yake, na kila ofisi ina kituo kinachoihusu na mahali maalum, hukumu zake ni tofauti, tabaka zake ni tofauti.

Mfano wa mfalme huyu humwendesha amtakaye na amteuaye katika msafara mpana kwenye msafara huo anatembelea ofisi zote za ufalme huo, hali ya kumwonesha haiba ya dola yake na adhama ya ufalme wake, akimwonesha amri zake zenye hekima ambazo zinahusu kila ofisi, akimtembeza kutoka ofisi kwenda ofisi kutoka tabaka moja kwenda tabaka lingine, mpaka anamfikisha kwenye makamo ya kuhudhuria kwake, na baada ya hapo anamtuma kuwa ni mjumbe kwa watu, akimkabidhi baadhi ya amri zake za jumla enevu zenye kuhusiana na ofisi zote hizo.

Na kama hivi tunatazama kwa darubini ya mfano huu na tunasema: Hakika Bwana mlezi wa walimwengu na yeye ni mfalme wa azali na milele, ndani ya ngazi za ulezi wake wa kiungu ana mambo na anuani mbali mbali. Lakini yanarandana baadhi yake na baadhi nyingine, na ndani ya ofisi zake za kiungu (Mola Muabudiwa) kuna alama na majina tofauti, lakini baadhi yake hushuhudiwa ndani ya nyingine, na katika shughuli zake kuu ana midhihirisho na maonesho yenye kutofautiana, lakini yanarandana, na ndani ya usarifu wa Uweza wake kuna anuani tofauti, lakini hutambuana baadhi yake na baadhi nyingine, na ndani ya midhihirisho ya sifa zake kuna mandhari takatifu mbalimbali, lakini baadhi yake huyadhihirisha baadhi nyingine. Na ndani ya midhihirisho ya vitendo vyake kuna usarifu tofauti, lakini mmoja huukamilisha mwingine. Na ana ulezi mkubwa wenye kubadilika ndani ya ufundi wake na alivyovitengeneza, lakini kimoja wapo kinakiona kingine.

Kwa msingi wa siri hii kuu, Allah (s.w) ameufuma ulimwengu kulingana na mpangilio wa ajabu unao amsha tahayuri na kustaajabia, kwani kutokea kwenye atomu ambazo zinahesabiwa ni viumbe vidogo kabisa hadi kwenye mbingu, na kutokea kwenye tabaka lake la kwanza na hadi kwenye kiti kikuu cha enzi, mbingu zilizojengwa baadhi ya nyingine, kila mbingu ni kwa mazingatio ya dari ya ulimwengu mwingine, na kwa nafasi ya arshi ya Uungu wake (hali ya Ubwana mlezi wa kila kitu) na kituo cha Usarifu wa mambo ya kiungu (Mola Muabudiwa wa haki).

Na pamoja na kuwa yawezekana kudhihiri kwa majina yote kwa anuani zote katika ofisi hizo na katika tabaka kwa kuzingatia upekee, isipokuwa kama inavyokuwa anuani ya Mtawala mwadilifu ni mwenye kutawalia na ni shina katika ofisi ya mambo ya uadilifu, na anuani nyingine zenye kumhusu zenye kungojea amri yake, vilevile – na Allah (s.w), ana mfano wa juu – kuna jina la kiungu na anuani ya kiungu yenye kutawala na kutamalaki katika kila tabaka katika tabaka za viumbe na katika kila mbingu, na baki ya anuani zimo ndani yake.

Kwa mfano:

Katika mbingu ambayo Bwana wetu Issa (a.s), aliyepata utukufu kwa jina la (Al-Qadiir), amekutana na Bwana wetu Mtume (s.a.w), basi Allah (s.w) ni mwenye kujidhihirisha katika duru ya mbingu hiyo kwa dhati kwa anuani ya (Al-Qadiir).

Kwa mfano:

Hakika ya anuani ya Mwongeaji ambayo Bwana wetu Musa (a.s) amepata utukufu wake ni yenye kutawalia katika duru ya Mbingu ambayo ni kituo cha Bwana wetu Musa (a.s).

Na kama hivi, Mtume mtukufu (s.a.w), kwa kuwa amebahatika jina kuu, na kwa kuwa unabii wake ni enevu wenye kukusanya, na amepata midhihirisho yote ya majina mazuri, kwa hiyo ana uhusiano na duru zote za kiungu, hapana budi kwamba hakika ya Miiraji yake inahitajia yeye kukutana na manabii na wao ni wenye makamo katika duru hizo, na kupita katika tabaka zote.

Mfano wa pili

Hakika ya anuani ya (Amiri jeshi mkuu) ambayo ni katika anuani za mfalme, ina udhihiriko katika kila cheo katika vyeo vya kiaskari kuanzia kwenye cheo cha (Kamanda mkuu) na (mkuu wa vikosi – cheo kikunjufu cha kiujumla – hadi kwenye cheo cha koplo nacho ni cheo cha kisehemu maalumu.

Kwa mfano:

Hakika mwanajeshi mmoja anaona kielelezo cha uongozi mkuu na mfano wake katika haiba ya Koplo, anamwelekea na kupokea amri kutoka kwake. Na hali ambapo Koplo anakuta anuani ya uongozi huo katika cheo cha mkuu wake, mkuu wa makoplo na kumwelekea. Na anapokuwa mkuu wa makoplo anaona kielelezo cha jumla na udhihiri wake katika cheo cha Luteni. Na ana kiti maalum katika kituo hicho. Na kama hivi inaonekana anuani ya uongozi huo mkuu katika kila cheo katika vyeo vya Kapteni Meja Jenerali na Fidmashali kulingana na upana wa cheo au ufinyu wake.

Na sasa huyo kiongozi mkuu akitaka kukabidhi jukumu linalohusu vyeo vyote vya kiaskari kwa mwanajeshi mmoja, na akataka kumpandisha cheo cha juu, kinachoshuhudiwa upande wa vyeo hivyo na wote wanakishuhudia, kana kwamba ni mwangalizi wake, hakika yeye (Kamanda mkuu) bila shaka atampitisha mwanajeshi huyo mmoja katika vyeo hivyo kuanzia cheo cha koplo na kuishia katika duru yake kuu, duru hadi katika cheo chake kikuu, ili apate kushuhudia na kushuhudiwa kutokea hapo, kisha anamkubali katika makamo ya hadhara yake na kumpa utukufu kwa kuongea naye na kumkirimu kwa amri zake na nishani zake, kisha anamtuma kule alikotoka wakati mmoja na katika punde hiyo hiyo.

Inapasa tugeuze mtazamo katika nukta moja kwenye mfano huu nayo: Ikiwa mfalme sio mwenye kushindwa, ana uwezo wa kiroho wa kimaanawy na kama alivyo na nguvu dhahiri, hakika hatawawakilisha watu mfano wa generali na fidmashali na Luteni, bali atahudhuria mwenyewe kila mahali, na kutoa amri yeye mwenyewe moja kwa moja akiwa amejificha kwa baadhi ya pazia, na nyuma ya watu wenye hadhi, kama inavyosimuliwa kwamba wafalme walikuwa mawalii wakamilifu walitekeleza amri zao katika duru nyingi katika sura ya baadhi ya watu.

Ama hakika ambayo tunaitazama kwa miwani ya mfano huu, nayo ni kuwa amri na utawala inakuja moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu kwenda kila duru katika duru, na kutekelezwa huko kwa amri yake na matakwa yake na nguvu yake kwa hali ambayo hakuna kushindwa ndani yake.

Vivyo hivyo kwa mfano sawa na huu: Katika kila tabaka miongoni mwa tabaka za viumbe na makundi yaliyokuwepo, kutoka katika atomu hadi kwenye sayari na kutoka kwenye vidudu hadi mbinguni, vinavyopita humo na kutekelezwa kwa utiifu kamili, na kutekeleza amri ya mfalme wa azali na wa milele na mambo ya mtawala wa Ardhi na mbingu, Mwamrishaji wa hali yote Mmiliki wa amri:

كُنْ فَيَكُوْنُ

hushuhudiwa, katika kila moja miongoni mwao, duru ya Uungu Bwana mlezi uliyo mtukufu na tabaka la kiutawala lenye kutamalaki, kwa matabaka ya aina tofauti tofauti na makundi mbalimbali, madogo na makubwa, ya kisehemu au kiujumla, kila moja ikiielekea nyingine.

Kwa ajili ya kufahamu makusudio yote ya kiungu (Mola Muabudiwa wa haki) ya juu na matokeo makuu yaliopo kwenye ulimwengu, kupitia kushuhudia majukumu ya kiuja ya aina mbali mbali kwa tabaka zote, na ili kutambua yanayomridhisha Allah Mwenye utukufu na ukubwa, kwa uoni wa ufalme wake wa kiungu mtukufu na haiba ya utawala wake wenye ushindi usioshindwa, na ili awe Mlinganiaji kwa Allah (s.w), hapana budi kuwepo na matembezi katika tabaka hizo na kupita katika duru hizo hadi aingie katika arshi tukufu ambayo ni anuani ya duru yake kubwa na kuingia katika

(قَابَ قَوْسَيْنِ)

yaani aingie katika makamo kati ya (imkani na wajibu) kulikoashiriwa kwa

(قَابَ قَوْسَيْنِ)

na kukutana na dhati tukufu iliyo nzuri.

Mwendo huu na kupita huku na kukutana ndio hakika ya Miiraji.

Na kama inavyopatikana kwa kila mwanadamu mwendo kwa akili yake kwa kasi ya kufikirika, na kila walii ana matembezi kwa moyo wake kwa kasi ya umeme, na kila malaika ana mzunguko kwa mwili wake wa kinuru kwa kasi ya roho, kutoka kwenye kiti cha enzi hadi kwenye tandiko na kutoka kwenye tandiko hadi kwenye kiti cha enzi, na watu wa peponi wana kupanda Miiraji kwa kasi ya Buraki, kutoka katika medani ya ufufuo hadi peponi na katika umbali unaozidi miaka mia tano elfu, hakika mwili wa Muhammad (s.a.w), ambao ni ghala la viungo vyake vitukufu na eneo la majukumu yasiyo kuwa na mpaka ya roho yake ya hadhi ya juu, itafuatana na roho hiyo ya Muhammad ambayo ni nuru, na katika upokeaji wa nuru, na mpole kuliko nyoyo za mawalii, na laini kuliko roho za maiti, na angavu kuliko viwiliwili vya malaika, na vyenye kupendeza zaidi kuliko kiwiliwili cha nyota na mwili wa kimfano, atafuatana nayo kwa vyovyote na kupanda nayo hadi kwenye kiti cha enzi tukufu.

Na sasa tumtazame kafiri ambaye yuko katika nafasi ya kusikiliza:

Inapita mawazoni kwamba huyu kafiri anasema moyoni mwake: Mimi siamini Allah (s.w), na wala simjui mtume (s.a.w), basi vipi nitasadiki Miiraji?

Na sisi tunamwambia: Kwa kuwa viumbe hivi vipo kwa hakika, na kunashuhudiwa ndani yake matendo na upatishaji, na kwamba tendo lililopangika haliwi bila ya mtendaji, na kitabu chenye fasaha hakiwi bila ya Mwandishi, nakshi ya kupendeza haiwi bila mtia nakshi. Hakuna budi kuwepo kwa mtendaji wa matendo haya yenye hekima yaliyojaa kwenye viumbe, na hapana budi kuwepo mtia nakshi na mwandishi kwa nakshi hizi za kupendeza na barua za fasaha ambazo zinajaa uso wa Ardhi na kuja upya kila majira na majira, na kwa kuwa kuwepo kwa watawala wawili katika jambo fulani kunaharibu nidhamu ya kitu hicho, na kwamba kuna mpangilio kamili na uratibu uliotimia, kuanzia kwenye ubawa wa mbu hadi kwenye kandili za mbinguni, kwa hiyo basi Mtawala huyo ni Mmoja wa pekee, kwa kuwa utengenezaji na hekima katika kila kitu ni katika ufundi wa ajabu na kufanya vizuri kiasi kwamba inalazimu kuwa mtengenezaji wa kitu hicho ni Mweza wa hali zote, mweza juu ya kila kitu na mjuzi wa kila kitu, kwani kama asingekuwa mmoja ingelazimu kuwepo miungu kwa idadi ya vilivyopo, na kila Mungu angekuwa dhidi ya mwingine na mfano wake! Na wakati huo inakuwa kubakia kwa nidhamu hii bila ya kuharibika ni muhali katika Muhali elfu moja! (Kitu ikisicho wezekana).

Kisha hakika ya tabaka za vilivyomo visingekuwa vyenye mpangilio sana, na vyenye kutii sana amri kwa mara elfu kuliko jeshi liliopangiliwa, kama inavyoshuhudiwa kwa dhahiri, kwani kila mpangilio katika mipangilio ya harakati za nyota, jua na mwezi hadi mpangilio wa maua ya lozi unadhihirisha mpangilio wa ajabu na kamili katika aliyotunuku Mweza wa azali katika nishani na kuvivika mavazi yenye kupambika, na kuyatengea harakati na matendo, yanazidi yale yanayooneshwa na jeshi, katika nidhamu na utiifu mara elfu, kwa hiyo viumbe hivi vina Mwenye hekima wa hali zote amefichikana nyuma ya ghaibu, vilivyopo vinangojea amri yake ili kuzitekeleza.

Na kwa kuwa huyo mwenye hekima kwa hali zote ni mfalme mwenye utukufu, kwa ushahidi wa kazi zake zenye hekima, na kwa athari tukufu zinazoonekana dhahiri, na mola Mwingi wa rehema Mkunjufu wa Rehema, kwa neema anazozidhihirisha, na fundi wa ajabu anayependa sana ufundi wake, kwa kazi zake za ufundi wa ajabu alizozionesha, na Muumbaji, Mwingi wa hekima, anataka kuamsha kupendezwa na wenye utambuzi na kuleta usifiaji wao mzuri, kwa mapambo mazuri na kazi za kupendeza alizozieneza, na inafahamika katika uzuri wa aliyotengeneza, unaochukua akili katika kuumba ulimwengu, ya kwamba yeye anataka kuwajulisha wenye utambuzi kutokana na viumbe wake: Nini makusudio ya upambaji huu? Na wapi viumbe vinatokea? Na hatima yake ni wapi? Hapana shaka hakika Mtawala huyu Mwingi wa hekima na fundi Mjuzi wa kila kitu atadhihirisha Uungu wake (Bwana Mlezi wa kila kitu) Mtukufu.

Na kwa kuwa yeye anataka kuitambulisha nafsi yake na kuipendezesha kwa wenye utambuzi, kwa athari za upole na huruma alizozidhihirisha, na kwa maajabu ya ufundi aliyoyaeneza, hapana shaka kwamba atapasha habari kwa kupitia mfikishaji mwaminifu, anayoyataka kutoka kwa wenye utambuzi, na kwa kile atakachowaridhia nacho? na kwa hiyo kwa vyovyote atatangaza Uungu wake (wa hali ya kuwa Bwana Mlezi) kwa kupitia kwa mwenye kumteua mahususi katika wenye utambuzi na kumpa utukufu mlinganiaji miongoni mwa wenye utambuzi kwa ukaribu wa kuhudhuria kwake, akimjaalia kuwa ni wasita (mkaa kati) wa kutangaza kuhusu kazi za ufundi wake zenye kupendwa kwake, na atamteua mwalimu anayedhihirisha makamilifu yake kwa kufundisha makusudio yake ya juu kwa wengine wenye utambuzi, na atamteua kiongozi anayejulisha maana ya vilivyokuwepo ili katika vilivyoingizwa katika ulimwengu huu isibaki talasimu yoyote (Fumbo) bila ufumbuzi na yaliyofichwa katika hivi vilivyokuwepo katika mambo ya kiungu (Hali ya kuwa Bwana Mlezi) bila maana yoyote, na atamteua kiongozi anayefundisha makusudio yake ili yasibaki kuwa ni mchezo bila ya manufaa yale aliyo yadhihirisha katika mazuri ya utengenezaji (wake) au kuyaeneza mbele ya macho, na atamnyanyua mmoja wao na kumpandisha katika makamo ya juu katika wenye utambuzi wote na amfundishe yanayomridhisha na kumtuma kwao.

Na kwa kuwa hakika na hekima vinahitajia hili, mwenye kustahiki zaidi wa kutimiza haki ya majukumu hayo ni Muhammad (s.a.w), ametekeleza majukumu hayo hasa kwa sura yake kamilifu zaidi, na shahidi Mwadilifu Mkweli juu ya hilo ni alichoasisi katika ulimwengu wa Kiislamu na aliyoyadhihirisha katika nuru ya Uislamu iliyo dhahiri. Kwa hiyo kwa ajili ya yaliyotangulia inalazimu kumpandisha na kumuinua nabii huyu mtukufu uinuaji wa moja kwa moja kuelekea katika makamo ya juu yaliyo juu ya viumbe wote na kuvuka vyote vilivyokuwepo, ili abahatike kutokea mbele ya Bwana Mlezi wa walimwengu.

Miiraji ina maanisha hakika hii.

Muhtasari

Hakika ya mwingi wa hekima wa hali zote amevipamba viumbe hivi vikuu na kuvipangilia kwa kudhihirisha mifano ya makusudio haya makuu na shabaha tukufu, na kwamba katika hivi vilivyomo imo sampuli ya mwanadamu ambaye anaweza kushuhudia Uungu huu (Hali ya Bwana mola Mlezi) ya ujumla na sehemu zake zote ndogo mno, na Uungu huu mtukufu (hali ya kuwa Mola Muabudiwa wa haki) kwa hakika zake zote, hapana shaka kwamba huyo Mwingi wa hekima wa hali zote ataongea na mwanadamu na kumjulisha makusudio yake.

Na kwa kuwa kila Mwanadamu hawezi kupanda katika makamo ya juu sana ya kiujumla akiwa mwenye kuepukana na hali ya kisehemu na kihali ya chini, hakuna shaka kwamba baadhi ya watu mahususi kati ya hao watu atakalifishwa jukumu hilo, ili awe na uhusiano pamoja na pande mbili kwa pamoja, yaani awe mwanadamu anayewafundisha watu, na katika wakati huo huo awe mwenye roho iliyo katika upeo wa hadhi ya juu ili apate utukufu wa maongezi ya kiungu moja kwa moja. Na baada ya hayo, kwa kuwa aliyefikisha makusudio ya Bwana Mlezi wa walimwengu kati ya wanadamu, na kufumbua talasimu (fumbo) lake na kutatua kitandawili cha kuumbwa na mkamilifu zaidi aliyelingania adhama ya mazuri ya Uungu (Bwana mlezi) ni Muhammad (s.a.w), hapana shaka kuwa atakuwa na mwenendo wa kimaanawy wa hadhi ya juu baina ya wanadamu, kiasi atakuwa na Miiraji kwa sura ya mwendo na utalii katika ulimwengu wa kimwili, na atakata ngazi hadi zilizokuwa nyuma ya tabaka za vilivyokuwepo na kizuizi cha majina na kudhihiri kwa sifa na matendo yanayoyaelezea kwa pazia sabini elfu.

Abuu Ya’la, Almusnad 13/520; Attabarany, Almu’jam Al-awsat 6/278.

Basi hii ndio Miiraji.

Na inapita mawazoni vilevile, hakika wewe msikilizaji unasema katika vina vya moyo wako: Hakika Bwana mlezi yuko karibu mno na sisi kuliko kila kitu, nini inamaanisha kuwepo mbele yake baada ya kukata masafa ya maelfu ya miaka na kupita katika pazia sabini elfu? Vipi nitaitakidi hili?  Na sisi tunasema: Hakika Allah (s.w) yuko karibu na kila kitu kuliko kila kitu, isipokuwa kila kitu kiko mbali na yeye umbali wa hali zote, tukikadiria kwamba jua lina utambuzi kamili, linaweza kuongea na wewe kwa kioo ambacho kiko mkononi mwako, na linasarifu kwako namna lipendavyo, wakati ambapo liko karibu kwako kuliko mboni ya jicho lako lenye kufanana na kioo, wewe uko mbali nalo takriban kwa miaka elfu nne. Na haiyumkiniki kwako kulikaribia kwa hali yoyote iwayo, hata kama ungepanda hadi katika makamo ya mwezi, na kuinuka juu hadi katika nukta ya kukabiliana nalo moja kwa moja, hautakuwa isipokuwa ila kama kioo chenye kuliakisi jua.

Na kama hivyo (s.w), naye ni jua la azali na milele – na Allah ana mfano wa juu – yuko karibu na kila kitu kuliko kila kitu, pamoja na kuwa kila kitu kiko mbali naye kwa hali zote, isipokuwa yule anaye kata vyote vilivyopo, na kukomboka na hali ya u-sehemu na kupanda katika ngazi za ujumla akipenda kutoka ngazi hadi ngazi na anapita kupitia maelfu ya pazia na analikaribia jina lenye kuzungukia vilivyokuwepo vyote, na kukata ngazi nyingi mbele yake, kisha baada ya hapo anapata utukufu wa aina fulani ya ukaribu.

Na mfano mwingine:

Hakika mwanajeshi mmoja yuko mbali kabisa na haiba ya kimaanawy ya kiongozi mkuu, yeye anamtizama kiongozi wake kutoka masafa ya upeo wa umbali na kupitia pazia nyingi za kimaanawy, anamwona katika kielelezo kidogo katika cheo cha Koplo. Ama kutaka ukaribu wa hakika wa haiba ya kimaanawy ya kiongozi mkuu, hiyo inamlazimu kupita katika ngazi nyingi za kiujumla kama ngazi ya Luteni na kapteni na Meja na kadhalika. Wakati ambao kiongozi mkuu yupo kwake na anamuona kwa amri yake na kanuni yake, na uangalizi wake, hekima yake na ujuzi wake, naye akiwa yupo kwa dhati yake mkabala wake ikiwa ni kiongozi katika maana – na roho – kama ilivyo katika sura na dhahiri.

Na ilivyokuwa hakika hii imethibitishwa kwa ithibati ya kukinaisha katika (Neno la kumi na sita) hapa tunatosheka kwa kiasi hiki cha muhutasari.

Na inapita kwenye mawazo vilevile, kwamba wewe unasema kwa moyo wako wote: Mimi ninakana kuwepo kwa mbingu na wala siamini malaika, vipi basi nitasadiki kwenda kwa mwanadamu na kutembea kwake mbinguni na kukutana kwake na malaika?

Naam, hapana shaka kwamba kuonesha kitu na kufahamisha jambo kwa mtu kama wewe, na kifuniko kimefunikwa kwenye uoni wake na akili yake imeshuka hadi kwenye jicho lake haoni tena isipokuwa maada, ni jambo gumu mno, lakini kwa sababu ya haki kuwa wazi sana, hata vipofu wanaiona.

Kwa hiyo tunasema: Ni kwamba watu wanaafikiana kwamba, anga la juu limejaa (Ether). Mwanga, umeme na joto na mfano wa hayo ni katika vyenye kumiminika vipole, ni dalili ya kuwepo kwa maada yenye kujaa mbinguni.

Kama matunda yanavyojulisha miti yake, na maua juu ya bustani yake, na mashuke juu ya shamba lake, na samaki kwa bahari yake kwa uwazi, hizi nyota pia zinasongamana kwenye macho ya akili zinajulisha kwa vyovyote juu ya uwepo wa bustani na chanzo na shamba na bahari yake.

Kwa kuwa ulimwengu wa juu umejengwa kwa namna mbali mbali, kila moja kati yake inabainisha hukumu tofauti katika mazingira mbali mbali, chanzo cha maamuzi hayo, yaani mbingu, zinazotofautiana pia, kama ilivyo kwa mwanadamu kuna aina za uwepo wa kimaanawy, isipokuwa mwili wa kimaada, kama akili, moyo na roho, na mawazo ya kufikirika na kumbukumbu na kadhalika, na katika ulimwengu vilevile ambao ni katika sura ya mwanadamu mkubwa, na katika viumbe ambavyo ni mti wa tunda la mwanadamu, limwengu nyingine zisizokuwa ulimwengu wa kimwili, ukiachilia mbali kwamba kila ulimwengu katika limwengu mbali mbali una mbingu yake kuanzia kutoka katika ulimwengu wa Ardhi hadi ulimwengu wa pepo.

Kwa mnasaba na Malaika tunasema: Ardhi nayo ni katika sayari za ukubwa wa kati na kati na ndogo na nyingi kulingana na nyota, ikiwa ni zenye kujaa kwa kiasi kisichohesabika katika mitindo ya maisha na utambuzi, na hivyo ni kitu cha thamani zaidi katika vilivyopo na vyenye nuru zaidi. Basi vipi mbingu ambazo ni bahari pana nyota huogelea humo kana kwamba ni majengo makubwa yenye kuratibika na kasri ndefu kulingana na Ardhi ambayo ni nyumba ndogo yenye giza?

 Kwa hiyo mbingu basi ni makazi ya wenye utambuzi na uhai, na jinsi anuai na kwa idadi isiyohesabika wala kudhibitika, nao ni Malaika na Maruhani, na kwa kuwa tumeshathibitisha kwa namna ya kukinaisha, kuwepo kwa mbingu na wingi wake katika tafsiri yetu iitwayo: (Ishaaratul iijaz fy madhannil iyjaz) nayo ni tafsiri ya kauli yake:

ثُمَّ اسْتَوَى إِلَى السَّمَاء فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ Qur’an, 2:26.

na kadhalika tumethibitisha kuwepo kwa malaika uthibitisho ambao shaka haiukaribii katika (Neno la ishirini na tisa), hapa tunafupisha mada hii na tunaielekeza katika risala hizo mbili.

Muhtasari:

Hakika kuwepo kwa mbingu ambazo zimesawazishwa kutokana na Ether na kuwa mwendo wa mwanga na joto na nguvu ya uvutano na mifano ya hivyo katika vimiminiko nyororo, na kuwa ni vyenye kuwiana na harakati za nyota na sayari kama hadithi tukufu ilivyoashiria (Mbingu ni wimbi lililozuiliwa)

Ahmad bin Hanbal, Almusnad 2/370; Attirmidhy, Tafsiri ya Surat Al-Hadid aya 1.

imechukua hali tofauti na maumbo mbalimbali, kutoka katika njia kuu ya sayari, (Inayoitwa njia za mbingu) hadi sayari ya karibu mno na sisi, katika tabaka saba, kila moja inachukuliwa kuwa ni dari ya ulimwengu mwingine, kutoka katika ulimwengu wa Ardhi hadi ulimwengu wa kizuizi hadi katika ulimwengu wa mfano, hadi katika ulimwengu wa Akhera, kama hivi hekima na mantiki ya akili vinahitajia hayo.

Na inapita mawazoni vilevile: Ewe kafiri! Wewe unasema: Sisi hatupandi kwa ndege kwenda maeneo ya juu ila kwa mashaka ya nafsi na tunafika kwa ugumu mno hadi masafa ya kilo mita chache, basi vipi inayumkinika kwa mwanadamu kukata kwa mwili wake masafa ya maelfu ya miaka kisha arudi alipotoka ndani ya dakika chache?!

Nasi tunasema: Mwili mzito kama ardhi hukata kwenye dakika moja masafa ya takriban saa mia moja na themanini na nane kwa mwendo wake wa mwaka, kulingana na mliyoyafikia katika elimu. Yaani Ardhi inakata masafa ya miaka ishirini na tano elfu ndani ya mwaka mmoja! Je, hawezi huyo Mweza wa kila kitu mwenye utukufu ambaye anaye endesha Ardhi hii kwa nyendo hizi zilizopangika madhubuti, kumleta mwanadamu kwenye kiti cha enzi? na kwamba isiweze hekima hiyo ambayo inaendesha ardhi nzito – kama Muriid mevlevi – kwa kanuni ya kiungu (Bwana mlezi) inayoitwa nguvu ya uvutano wa jua, kupandisha mwili wa mwanadamu kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mwingi wa Rehema kama umeme, kwa nguvu ya mvuto wa rehema ya Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu, na kwa kuvutika kwa mahaba ya nuru ya mbingu na Ardhi?

Na inapita kwenye akili kwamba wewe unasema: Na iwe kwamba anaweza kupanda na kwenda Miiraji mbinguni lakini kwa nini alipandishwa? na kuna dharura ipi ya kwenda Miiraji? Je, haikuwa inamtosha kupanda Miiraji kwa moyo wake na roho yake kama wanavyofanya hivyo Mawalii wema?

Na sisi tunasema: Madhali fundi mtukufu ametaka kudhihirisha ishara zake kubwa kwake (s.a.w) katika ufalme wake na falme zake, na kataka kumwonesha katika vyanzo na viwanda vya huu ulimwengu, na kataka kumwonesha matokeo ya kiakhera ya amali za wanadamu, basi hapana shaka kwenda pamoja naye hadi kwenye kiti cha enzi, macho yake ambayo yanazingatiwa kuwa ni ufunguo wa ulimwengu wa vyenye kuonekana kwa macho, na sikio lake ambalo anasikilizia ishara za ulimwengu wa vyenye kusikilizwa. Kama katika yanayolazimu akili na hekima kwenda pamoja naye kwenye kiti cha enzi, mwili wake wenye kubarikiwa vilevile ambao unazingatiwa kuwa ni mashine za zana na vifaa ambavyo hutendeka juu yake majukumu ya roho yake yasiyo na mpaka. Kama hekima ya kiungu inavyojaalia mwili ni rafiki wa roho peponi, kwa sababu mwili ni mahali pa majukumu mengi ya kiuja na kisicho na mpaka cha ladha na machungu, hapana budi kwamba huo mwili wenye kubarikiwa utakuwa pamoja na roho. Na kwa kuwa mwili utaingia peponi na roho, ni katika hekima tupu pia kuufanya mwili wake wenye kubarikiwa mshirika wa dhati ya Muhammad (s.a.w), ambao alipandishwa nao hadi Mkunazi wa Ukomo ambao ni mwili wa pepo ya Maawa.

Na inapita kwenye akili kwamba wewe unasema: Ya kwamba ni muhali kiakili kukata masafa ya maelfu ya miaka, ndani ya dakika chache?

Na sisi tunasema: Hakika ya michakato katika alivyovitengeneza mtengenezaji Mtukufu vinatofautiana sana, basi kwa mfano: Hakika kiasi cha kutofautiana kwa kasi ya sauti, mwanga, umeme, roho na mawazo kinajulikana kwetu. Basi vilevile kasi ya sayari – kama inavyojulikana kisayansi – kuna tofauti za kuzifanya akili zitahayari. Basi vipi uonekane mwendo wa mwili wake nyororo (s.a.w), ambao umepata kasi kwa kupanda Miiraji, na ikafuata roho yake ya hadhi ya juu, kasi hiyo ya haraka sana kasi ya roho ni kinyume na akili?

Wewe kwa nafsi yako ukilala dakika kumi, unapitia hali ambazo huzipitii katika hali ya kuwa macho kwa mwaka. Hata anachokiona mtu kwenye ndoto kwenye dakika moja na maneno anayosikia humo na maneno anayotamka humo kama yatajumuishwa na kukusanywa pamoja, inalazimu muda wa siku moja au zaidi katika ulimwengu wa kuwa macho. Basi wakati mmoja kwa hiyo kulingana na watu wawili inaweza kuwa sawa na siku moja kwa mmoja wao na mwaka mmoja kwa mwingine.

Basi angalia maana hii kwa mtazamo wa mfano huu: Tukadirie kuwepo kwa saa ya kupima kasi ya nyendo ya mwanadamu na risasi, sauti, mwanga, umeme, roho na mawazo. Na katika saa hii kuna kurabu, kurabu moja inahesabu saa, na nyingine inahesabu dakika, katika mzunguko mpana zaidi kuliko wa awali mara sitini, na kurabu nyingine inahesabu sekunde, katika duara pana zaidi kuliko hili kwa mara sitini, hivyo hivyo kurabu za robo, humusi, sudusi na sehemu ya saba na sehemu ya tisa na sehemu ya kumi. Yaani saa inakuwa na kurabu za ajabu kila moja inazunguka katika duara pana zaidi kuliko la kabla yake kwa mara sitini mara dufu. Ikiwa kurabu inayohesabu saa kwa kiwango cha saa zetu ndogo za mkononi, italazimu duara la kurabu linalohesabu sehemu ya kumi kwa kiwango cha mzunguko wa mwaka wa Ardhi au mkubwa zaidi kuliko huo.

Na sasa ebu tukadirie kwamba kuna watu wawili: Mmoja wao: Kana kwamba amepanda kurabu ya saa anatazama na kuangalia yanayomzunguka, na mwingine amepanda kurabu ya sehemu ya kumi na kushuhudia yanayomzunguka. Tofauti kati ya vitu wanavyoshuhudia hawa watu wawili katika wakati mmoja, ni uwiano wa tofauti kulingana na saa zetu za mkono na mzunguko wa ardhi wa mwaka, yaani tofauti ni kubwa mno. Na vivyo hivyo, kwa kuwa muda ni aina katika aina za mwendo na pambo lake au mkanda wake, basi uamuzi unaopita katika nyendo huamuliwa pia katika wakati, wakati tunashuhudia katika saa moja kiasi cha anachoshuhudia mpandaji mwenye utambuzi juu ya kurabu ya saa, na hakika ya umri wake ni kwa kiasi hicho hicho, hakika Mtume mtukufu (s.a.w), katika wakati huo huo – kama aliyepanda juu ya kurabu ya sehemu ya kumi – katika hiyo saa maalum anapanda buraq wa taufiki ya kiungu na anakata duru zote za yamkini kama umeme na anaona ishara za ufalme na falme na anapanda katika duru ya wajibu, na kupata utukufu kwa kukutana na kuongea, na anafaulu kupata kuona uzuri wa kiungu na kutekeleza ahadi na amri ya kiungu ili kutekeleza jukumu kisha anarudi. Na amerudi hasa. Naye ni kama hivyo.

Na inapita kwenye akili vilevile: Kwamba nyinyi mnasema: Naam, inajuzu, na pengine inayumkinika kutokea! lakini sio kila kinachotazamiwa na yamkini kutokea hutokea kweli, je, vipi itasihi kuhukumiwa juu ya kitu kisicho na mfano, kwa sababu tu ya kuwepo uwezekano wa kutokea kwake?

Nasi tunasema: Hakika mifano ya Miiraji ni mingi kupita kiasi, basi kila mwenye uoni kwa mfano anapanda na uoni wake kutoka ardhini hadi katika sayari ya (Neptune), ndani ya dakika moja, na kila mwenye ujuzi anakwenda kwa akili yake akiwa amepanda kanuni za falaki hadi maeneo ya nyuma ya nyota na sayari ndani ya dakika moja, na kila mwenye imani hupandishwa fikira yake kwenye matendo ya swala na nguzo zake hali akiviaga viumbe nyuma ya mgongo wake anakwenda kwenye hadhira ya kiungu kwa hali inayoshabihiana na Miiraji, na kila mwenye moyo na walii mkamilifu anaweza kwenda kwa mwendo na kupita kutokea katika kiti cha enzi na kutoka katika duru ya majina na sifa ndani ya siku arobaini, hata kwamba Sheikh al-Kailany na Imamu al-Rabbany na wengine katika watu wa kipekee imepatikana kwao kupanda Miiraji ya kiroho kwenda kwenye Arshi ndani ya dakika moja, kama wanavyoelezea kwa masimulizi ya kweli. Na kwamba malaika ambao ni viwiliwili vya kinuru inapatikana kwao kwenda na kurudi kutoka katika kiti cha enzi hadi kwenye tandiko na kutoka kwenye tandiko hadi kwenye kiti cha enzi, katika muda mfupi mno. Na watu wa peponi watapanda kutoka katika mahali pa kukusanywa (Siku ya kiama) hadi katika bustani za pepo katika muda mfupi.

Kiasi hiki cha mifano mingi kinabainisha kwa kukinaisha kwamba mfalme wa mawalii na mitume na kiongozi wa waumini wote na bwana wa watu wote wa peponi na mpokewa na malaika wote, ambaye ni mtume mtukufu, bila shaka itapatikana kwake Miiraji iwe ni eneo la mwendo na kupita kwake kuelekea kwa Allah (s.w), kwa namna inayowiana na makamo yake ya hadhi ya juu.

Hii ndiyo hekima yenyewe hasa, na inakubalika vilivyo kiakili. Na imetokea kiuhalisia pasi na shaka japo kidogo.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.