Nyongeza Ya Pili

(Inahusu Miiraji ya Mtume)

بِسْمِهِ سُبْحَانَهُ

وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ يُسَبِّحُ بِحَمْدَهِ Qur’an, 17:44.

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَى* عِندَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَى * عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَى * إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَى*  مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَى* لَقَدْ رَأَى مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَى Qur’an, 53:13-18.

Tutabainisha nukta tano kuhusu sehemu ya Miiraji kutoka katika Qaswida ya Mawlid an-Nabawy.

Nukta ya kwanza

Hakika (As-Sayyid Sulayman Efendy) ambaye ameandika kasida Kuhusu Maulid ya Mtume Mtukufu (s.a.w), anabainisha humo matukio ya ashiki ya kuhuzunisha kuhusu Buraq ambaye aliletwa kutoka peponi. Na kwa vile yeye ni katika mawalii wema na kasida yake inaegemea mapokezi kutoka katika Sira, hapana shaka kwamba anazingatia kwa sura hiyo juu ya hakika maalum. Na hakika yenyewe na hii ifuatayo:

Viumbe wa ulimwengu wa kubaki wana uhusiano wenye nguvu na nuru ya Mtume wa Allah (s.a.w), kwa sababu kwa nuru ambayo aliyokuja nayo itawaweka majini na watu peponi na katika makazi ya akhera, na bila ya yeye kusinge kuwepo na furaha hiyo ya milele, majini na watu wasingelikaa peponi wala wasingeneemeka kwa aina zote za viumbe wa peponi, yaani bila ya yeye pepo ingebaki ya bure na tupu bila wakazi wake.

Na hakika tulieleza katika (Tawi la nne  katika neno la ishirini na Nne): Imeteuliwa kutoka katika kila sampuli Chiriku, Mhutubu, anayeelezea kundi lake, na mwanzoni mwa hao wahutubu, chiriku mwenye kuashiki Ua, ambaye anatangaza haja za kundi la wanyama waliyo katika upeo wa kiwango cha ashiki, kwa msafara wa mimea unayokuja kutoka kwenye hazina ya rehema ya kiungu na yenye kubeba riziki za wanyama. Hawa chiriku wanaitangaza kwa naghama zake laini katika vilele vya mimea mizuri zaidi kuelezea mapokezi mema yaliyoshehenishwa kwa tasbihi na tahalili.

Basi mtume mtukufu Muhammad mwaminifu (s.a.w) ambaye yeye ni sababu ya kuumbwa kwa sayari, na njia ya furaha ya makazi mawili, na kipenzi wa Bwana Mlezi wa walimwengu, kama alivyokuwa Bwana wetu Jibril (a.s) ni mwakilishi wa aina ya malaika, katika kumtii na kumtumikia katika ukamilifu wa mahaba akibainisha siri ya kumsujudia malaika na kumfuata Bwana wetu Adam (a.s), basi wakazi wa peponi hivyo hivyo, bali hata wanyama wake wana uhusiano na mtume huyo mtukufu (s.a.w).

As-Sayyid Suleyman Efendy ameelezea hakika hii kwa hisia za mapenzi na ashiki ambayo aliyoyaelezea Buraq aliyempanda Mtume (s.a.w).

Nukta ya pili

Hakika moja ya matukio ya (Kasida ya Miiraji ya mtume s.a.w) ni kuwa (As-Sayyid Efendy) ameelezea kuhusu mahaba yaliyotakata ya Allah (s.w) kwa Mtume (s.a.w) kwa fungu la maneno: (Nimekuashiki).

Ibara hizi pamoja na maana yake ya kimazowea hayaendani na utakatifu na utukufu wake (s.w), lakini kwa kuwa (As-Sayyid efendy) ni katika watu wa uwalii na watu wa hakika, ambapo kasida yake hii imepata kukubalika na kuridhiwa na jumla ya Waislamu, hapana shaka kwamba maana aliyoyaonesha ni sahihi, nayo ni haya:

Hakika Allah (s.w) ana uzuri na ukamilifu wa hali zote, na kwamba aina zote za uzuri na ukamilifu uliogawika kwa viumbe, hizo ni alama za uzuri wake na ukamilifu wake na ishara zake. Na kwa kuwa kila Mwenye Uzuri na ukamilifu, anapenda uzuri wake na ukamilifu wake bila hoja, Basi Allah (s.w) anapenda uzuri wake

Muslim, Al-Iman 147. Ibnu Maajah, Ad-dua, 10. Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad 4/133, 134, 151.

kwa mapenzi yanayolingana na dhati yake tukufu. Na kwamba anapenda vilevile majina yake ambayo ni miale ya uzuri wake (s.w).

Na kwa kuwa yeye anapenda majina yake, kwa hiyo yeye anapenda ufundi wake ambao unadhihirisha uzuri wa majina yake.

Na anapenda kwa hiyo alivyovitengeneza ambavyo ni vioo vya uzuri wake na ukamilifu wake.

Na kwa vile anapenda kinachobainisha uzuri wake na ukamilifu wake anapenda, basi anapenda mazuri ya viumbe wake ambayo yanaashiria kwenye uzuri wa majina yake na ukamilifu wake.

Na Qur’an yenye hekima zote inaashiria katika aya zake katika hizi aina tano za mahaba.

Na kama hivi mtume (s.a.w) ambaye ni mtu mkamilifu zaidi katika vilivyotengenezwa na Allah (s.w), na haiba ya dhahiri zaidi katika viumbe vyake. Na yeye ndiye ambaye anakadiria na kutangaza kuhusu ufundi wa kiungu kwa dhikiri yenye mvuto na tasbihi na tahalili. Na yeye ndiye ambaye amefungua kwa ulimi wa Qur’an hazina za uzuri wa majina mazuri na ukamilifu wake. Na yeye ndiye ambaye anabainisha kwa ufasaha – kwa ulimi wa Qur’an aya za kimaumbile zenye kujulisha juu ya ukamilifu wa Mtengenezaji wake. Na yeye ndiye ambaye ametekeleza kazi ya kioo cha uungu Bwana mlezi na Mola Muabudiwa kwa uja wake wa kiujumla, hadi akapata utimilifu wa midhihirisho ya majina mazuri yote, kwa ujumuishi wa hakika yake.

Kwa ajili ya yaliyotangulia inasihi kusemwa:

Hakika ya mzuri mwenye utukufu kwa kupenda kwake uzuri wake anampenda Muhammad (s.a.w) ambaye ni kioo kikamilifu zaidi cha wenye utambuzi kwa uzuri huo.

Na kwamba yeye (s.w) kwa kuyapenda kwake majina yake anampenda Muhammad (s.a.w) ambaye ni koo kilichodhihiri zaidi kinachoakisi majina hayo mazuri. Na anawapenda vilevile wanaojishabihisha na Muhammad (s.a.w), kila mmoja kwa mujibu wa daraja yake.

Na kwamba yeye (s.w) kwa kupenda kwake ufundi wake anampenda Muhammad (s.a.w) ambaye ametangaza huo ufundi katika pande za ulimwengu wote hata akamjaalia kuwa katika furaha na shauku kwayo masikio ya mbingu yanagonga na kuamsha hisia za bara na baharini kumwekea shauku. Na anawapenda vilevile wanaomfuata.

Na kwamba yeye (s.w) kwa kupenda kwake alivyovitengeneza anampenda Muhammad (s.a.w), kwani yeye ni mbora wa watu wote ambao wao ni wakamilifu zaidi katika wenye utambuzi, ambao ni wakamilifu zaidi ya wenye uhai, ambao wao ni wakamilifu zaidi kati ya alivyovitengeneza.

Na kwamba yeye (s.w) kwa kupenda kwake tabia za viumbe wake anampenda Muhammad (s.a.w), kwa kuwa yeye yuko kileleni mwa tabia njema, kama walivyoafikiana juu ya hilo wapenzi na maadui, na vile vile anawapenda wanaojishabihisha na yeye katika tabia, kila mmoja kulingana na daraja yake.

Kwa maana ya kuwa mahaba ya Allah (s.w) yamezungukia ulimwengu kama ilivyouzungukia rehema yake, na kwa ajili hiyo makamo ya juu kabisa katika pande tano zilizotajwa ndani ya wenye kupendwa ambao hawana idadi ni makamo yaliyo mahususi kwa ajili ya Muhammad (s.a.w), na kwa ajili hiyo ametunukiwa jina la (Habibullah).

Na ameelezea (Suleyman Efendy) kuhusu makamo haya ya juu, makamo ya kuwa mahabubu, kwa kauli yake: “Nimekuashiki” pamoja na kujua kwamba maelezo haya, yanachochea kutafakari na sio vinginevyo, na kwa kuashiria hakika hii kwa bali. Na pamoja na hivyo hakika ya maelezo haya kwa kuwa kwake yanatia dhana katika mawazo maana yasiolingana na dhati ya Uungu Mtukufu, basi ni bora zaidi kusema: “Nimekuridhia”.

Nukta ya tatu

Mijadala inayoendelea katika (Kasida ya Miiraji) inashindwa kuelezea hakika hizo takatifu kwa maana yanayojulikana kwetu,  bali mazungumzo hayo ni anuani za mazingatio na angalizo, na vituo vya kutafakari na sio vinginevyo, na ishara ya hakika za hadhi ya juu za kina, na tanbihi za sehemu ya hakika za Imani, na mafumbo ya baadhi ya maana ambayo haiwezekani kuyaelezea.

Na kama sio hivyo, mijadala hiyo na matukio hayo sio kama mijadala inayopita kwenye visa ili iwe kwa maana yanayojulikana kwetu. Kwani sisi hatuwezi kuvuta ilhamu kwa mawazo yetu hakika hizo, kutoka katika mijadala hiyo, bali tunaweza kuvuta ilhamu kutokana na hiyo mijadala kwa nyoyo zetu, vionjo vya kiimani vyenye kuamsha hisia, na furaha ya kiruhani ya nuru, kwa sababu Allah (s.w) kama asivyokuwa na mwenza wala mshabaha wala mithili katika dhati yake na sifa zake, vivyo hivyo hana mithili katika mambo yake ya kiungu (Kuwa yeye ni Bwana Mlezi wa walimwengu), na kama sifa zake zisizoshabihiana na sifa za viumbe wake, vilevile mahaba yake hayashabihiani na mahaba ya viumbe wake.

Basi maelezo haya yaliyopatikana katika (Kasida ya Miiraji) yanahesabiwa ni katika maelezo yenye kushabihiana. Na kwa ajili hii tunasema:

Hakika Allah (s.w) ana mambo – kama mahaba yake (s.w) – yanayowiana na wajibu wa kuwepo kwake na utakatifu wake, na kulingana na ukwasi wake wa kidhati na ukamilifu wake wa kila hali. Yaani kasida iliyotajwa inatanabahisha mambo hayo kwa matukio ya Miiraji.

(Neno la thelathini na moja) linalohusu Miiraji ya Mtume (s.a.w), limebainisha hakika za Miiraji ndani ya Misingi ya Imani. Kwa hiyo hapa tunafupisha tukitosheka na maelezo hayo.

Nukta ya nne

Swali:

Maelezo: (Kwamba yeye (s.a.w) hakika alimwona Mola wake Mlezi nyuma ya pazia sabini elfu.)

Abuu Ya’laa, Al-Musnad 13/520. At-Tabarany, Al-Muujam Al-Ausat 6/278, 8/382. Ar-Ruuyany, al-Musnad 2/212. Jaamiu Al-bayan 16/95. Al-Haythamy, Maj-maa Al-zawaid, 79/1.

yanaelezea kuhusu umbali wa mahali, na hali ya kuwa Allah (s.w) ametakasika na mahali, kwani yeye yuko karibu na kila kitu kuliko kitu chochote kile kiwacho. Kwa hiyo nini makusudio ya maelezo hayo?!.

Jibu:

Nimeweka wazi hakika hiyo katika (Neno la thelathini na moja) na nilibainisha kwa namna ya kutosheleza kwa upambanuzi uliotiwa nguvu na hoja. Isipokuwa hapa tunasema:

Hakika ya Allah (s.w) yuko karibu na sisi upeo wa ukaribu, na sisi tuka mbali na yeye upeo wa umbali.

Mfano:

Hakika jua liko karibu na sisi kwa kupitia kioo kilichomo mikononi mwetu. Bali kila kilicho angavu kinakuwa ni aina moja ya kuonesha jua na kituo chake. Jua lingekuwa na utambuzi, lingekuwa linatusemesha kwa kioo tulicho nacho. Lakini tuko mbali nalo kwa miaka elfu nne.

Na kama hivi, jua la azali – (bila ya kufananisha),

 وَلِلّهِ الْمَثَلُ الأَعْلَىَ

yuko karibu na kila kitu kuliko chochote kiwacho, kwa sababu yeye ni wajibu kuwepo, na mwenye kutakasika na mahali, na wala hakimzuilii chochote, wakati ambapo kila kitu kiko mbali naye umbali wa hali zote.

Na kutokana na hili tunafahamu: Siri ya masafa marefu mno katika Miiraji pamoja na kutokuwepo kwa masafa ambayo yanaelezwa na aya tukufu:

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ Qur’an, 50:16.

Na vilevile kutokana na siri hii: Kwenda kwa mtume Mtukufu (s.a.w) na kupunguza kwake masafa marefu mno na kurejea kwake katika wakati mmoja mahali pake.

Miiraji ya Mtume (s.a.w) ni kutembea na kupita kwake, na ndio anuani ya uwalii wake, kwani kama mawalii wanavyopanda katika daraja la haki ya yakini katika daraja za Imani kupanda kimaanawy kwa mwendo na kupita kiruhani kuanzia siku arobaini hadi miaka arobaini, kadhalika Mtume (s.a.w) ni mfalme wa mawalii na Mkuu wao alipandishwa kwa mwili wake na hisia zake na sifa zake laini zote na sio kwa moyo wake na roho yake peke yake akifungua njia iliyonyooka sawa sawa na barabara kubwa hadi akafika ngazi za hakika ya imani na ya juu yake kwa hadhi kwa Miiraji ambayo ni karama ya uwalii wake mkubwa katika dakika arobaini badala ya miaka arobaini, na kupanda katika kiti cha enzi kwa ngazi ya Miiraji na ameshuhudia kwa jicho lake kwa dhati ya yakini – katika makamo ya ukaribu wa upinde na mshale au zaidi – hakika kuu mno ya imani, nayo ni kumwamini Allah (s.w), na kuamini siku ya mwisho, na aliingia peponi na alishuhudia furaha ya milele na amefungua mlango wa barabara kubwa na kuuacha ukiwa wazi ili wapite mawalii wote wa umma wake kwa kwenda na kwa kupita kiruhani yaani kwa mwendo wa kiruhani na kimoyo katika kivuli cha Miiraji hiyo. kila mmoja kulingana na daraja yake.

Nukta ya tano

Kusoma maulidi ya Mtume (s.a.w) na (Kasida ya Miiraji) ni kawaida ya Kiislamu yenye kupendeza, na ya manufaa sana, bali iko katika nafasi ya kukaa pamoja na kuliwazana kwa upole katika maisha ya kijamii ya Kiislamu. Nalo ni somo katika upeo wa ladha na uzuri la kukumbushia hakika za Kiimani. Nayo ni nyenzo yenye nguvu sana ya kuamsha hisia na kusisimua ya kudhihirisha nuru za imani, na kutikisa mahaba ya Allah (s.w), na ashiki ya Mtume (s.a.w).

Tunamwomba Allah (s.w) adumishe kawaida hii hadi milele, na amrehemu mwandishi wake (Bwana Suleyman Efendy) na mfano wake katika waandishi, na ajaalie mafikio yao pepo ya Firdaus. Amiin.

Hitimisho

Kwa kuwa Muumba wa ulimwengu huu, anaumba kutokana na kila sampuli (kiumbe) mmoja wa kipekee mkamilifu na jumuishi, na kumfanya ni sehemu ya fahari na ukamilifu wa sampuli hiyo, hapana shaka kwamba anaumba mmoja wa kipekee mkamilifu –  kulingana na viumbe wote – na hiyo kwa kudhihiri kwa jina tukufu katika majina yake mazuri. Atakuwa katika alivyotengeneza mmoja mkamilifu kama jina tukufu katika majina yake. Anakusanya makamilifu yake yaliyozagaa katika viumbe ndani ya huyo mmoja mkamilifu zaidi, na kumjaalia kuwa wa kutazamwa kwa hali zote.

Na hapana shaka kwamba huyo mmoja atakuwa ni kutokana na wenye uhai, kwa kuwa mkamilifu zaidi wa sampuli ya viumbe ni wale wenye uhai, na anakuwa kutokana na wenye utambuzi, kwa kuwa wakamilifu wa sampuli ya viumbe wenye uhai ni wenye utambuzi, na mtu huyo wa kipekee atakuwa ni katika wanadamu, kwa kuwa mwanadamu ndiye aliyepewa sifa stahiki kwa kupanda kusiko na mpaka. Na huyo mtu kwa vyovyote atakuwa ni Muhammad mwaminifu (s.a.w), kwa sababu hakutokea mtu katika historia yote mithili yake tangu zama za Adamu (a.s) na hadi sasa hatodhihiri. Kwa sababu huyo nabii mtukufu (s.a.w) amekusanya nusu ya tufe la Ardhi na moja ya tano ya wanadamu kuwa ndani ya ufalme wake wa kimaanawy na utawala wake ambao umedumu kwa miaka elfu moja na mia tatu na hamsini kwa ukamilifu wa haiba yake na utukufu wake. Na amekuwa ni ustadhi wa watu wote wa ukamilifu katika aina zote za hakika, na amepata ngazi za juu sana katika tabia njema kwa maafikiano ya marafiki na maadui, na ameupa changamoto ulimwengu wote yeye pekee – mwanzoni mwa jambo lake – na ameidhihirisha Qur’an tukufu ambayo wanaisoma zaidi ya watu milioni mia moja ndani ya kila dakika moja.

Hapana budi kwamba nabii mkarimu kama huyu nabii (s.a.w) ndiyo yule mtu mmoja wapekee hapana mwingine asiyekuwa yeye abadani. Yeye ni mbegu ya ulimwengu huu na tunda lake. Juu yake na juu ya Ali zake na sahaba zake iwashukie ziada za rehema na salama kwa idadi ya sampuli za viumbe na vilivyokuwamo.

Na jua kwamba kusikiliza Maulid ya mtume (s.a.w) na Miiraji yake (s.a.w) yaani kusikiliza mwanzo wa kupanda kwake na mwisho wake. Yaani kujua historia ya maisha yake ya kimaanawy, kuna ladha, na ni nuru, na kunaleta fahari kwa umma wake na utukufu kwao, na maliwazo ya kijuu yenye hadhi ya juu kwa waumini ambao wamemchukua yeye kuwa ni Mkuu, Bwana, Imamu na Mwombezi wao.

يَارَبِ بِحُرْمَةِ الْحَبِيْبِ الْأَكْرَم عَلَيْهِ الصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ، وَبِحَقِّ الإِسْم الْأَعْظَم، اجْعَلْ قُلُوْبَ نَاشِرِي هَذِهِ الرِّسَالَة وَرُفَقَاءَهُمْ مَظْهَرًا لِأَنْوَارِ الْإِيْمَانِ. وَاجْعَلْ أَقْلَامَهُمْ نَاشِرَةً  لِأَسْرَارِ الْقُرآنِ وَاهْدِهِـمْ إِلَى سَوَاءِ السَّبِيْل. آمِيْن.

سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.