Bediuzzaman Said Nursi alikuwa nani na Risale-i Nur ni nini?

Bediuzzaman Said Nursi alizaliwa mashariki mwa Uturuki mwaka 1873 na kufariki dunia mwaka 1960 akiwa na umri wa miaka 87 baada ya maisha ya kupigiwa mfano ya mapambano na kujitoa mhanga katika Uislamu. Alikuwa mwanazuoni wa nafasi ya juu ambaye hakusoma sayansi zote za kimapokeo ya kidini tu bali pia sayansi ya sasa na kupewa jina la Bediuzzaman, Muujiza wa Zama, katika ujana wake kutokana na uwezo na elimu yake.

Wakati wa uhai wa Bediuzzaman kulikuwa na miongo ya mwisho ya ukhalifa na Dola ya Uthman, kuanguka na kugawanyika baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, na baada ya kusimama kwa Jamhuri ya chama kimoja cha miaka ishirini na mitano ikifuatiwa na utawala wa Kidemokrasia wa miaka kumi, hali ilipotulia kidogo kwa ajili ya Bediuzzaman.

Mpaka miaka iliyofuatia Vita vya Kwanza vya Dunia, mapambano yake kwa ajili ya Uislamu yalikuwa hai katika umiliki wa umma. Hakuwafundisha tu wanafunzi wengi na kuingia katika mijadala na wanazuoni wakubwa katika ulimwengu wote wa Kiislamu, bali pia aliongoza yeye binafsi kwa kujitolea dhidi ya uvamizi wa Warusi mashariki mwa Uturuki katika mwaka 1914 kwa takribani miaka miwili mpaka alipofungwa jela. Kwa kuongezea, mpaka wakati huo alitaka kupeleka mbele maslahi ya Uislamu kwa kujishughulisha vilivyo katika maisha ya umma. Hata hivyo, miaka ambamo kulifanyika mpito kutoka dola kwenda kwenye jamhuri pia kulifanyika mpito kutoka “Said wa Zamani” kuwa “Said Mpya” ambamo kulikuwa na sifa ya kujitoa kutoka maisha ya umma  na kuzama katika masomo, swala na tafakuri kwa sababu kilichohitajika kwa sasa ni mapambano ya namna tofauti.

Baada ya miaka miwili, katika mwaka 1925, Bediuzzaman alipelekwa uhamishoni huko magharibi mwa Anatolia ingawa hakutenda uhalifu wowote au dosari yoyote. Katika miaka ishirini na mitano iliyofuatia, na kwa kiasi kidogo, katika miaka kumi ya mwisho ya uhai wake, alikabiliwa na uhamisho, kifungo na kutengwa, lakini katika miaka hii iliandikwa Risale-i Nur, Muhutasari wa Nuru na kuenezwa kwake katika Uturuki nzima. Kwa kumnukuu Bediuzzaman mwenyewe, “Sasa ninaona waziwazi kuwa sehemu kubwa ya uhai wangu imeelekezwa katika namna iliyo nje ya utashi wangu, uwezo, ufahamu na uoni, ambao ungeweza kuleta mihutasari hii ili kufuata njia ya Qur’an. Ni kana kwamba maisha yangu kama mwanazuoni yametumika katika maandalizi kwa ajili ya maandiko hayo, ambayo yanaonesha muujiza wa Qur’an.

Bediuzzaman alifahamu njia muhimu ya kuanguka kwa ulimwengu wa Kiislamu mpaka katika kudhoofika kwa misingi yenyewe ya imani, kudhoofika huku pamoja na mashambulizi ya aina yake kwenye misingi hiyo katika karne za 19 na 20 yaliyofanywa na wayakinifu, wakana mungu na wengine chini ya jina la sayansi na maendeleo, kulimfanya atambue kuwa haja ya dharura ilitakiwa ili kutumia kuimarisha na hata kuokoa, imani. Kilichohitajika kilikuwa ni kutumia juhudi zote katika kujenga upya jumba la Uislamu kutokea katika misingi yake, imani, na kujibu katika hatua hiyo, mashambulizi haya kwa ‘jihadi ya amani’ au ‘jihadi ya neno.’

Hivyo, akiwa uhamishoni, Bediuzzaman alifanya kazi ya kuandika, Risale-i Nur, ambayo ingeeleza na kudhihirisha itikadi za msingi za imani, ukweli wa Qur’an, kwa mtu wa sasa. Mpango wake ulikuwa kuchanganua imani na ukafiri na kueleza kwa hoja za waziwazi kuwa si kwamba tu inawezekana, kwa kuifuata Qur’an, kuthibitisha kimantiki ukweli wote wa imani, kama vile uwepo wa Mungu, na umoja, utume na ufufuo wa kimwili, bali pia ukweli huo ndiyo maelezo pekee ya kimantiki ya kuwepo kwa mwanaadamu na ulimwengu.

Kwa hivyo, Bediuzzaman alifafanua katika namna ya simulizi zenye kufahamika kirahisi, milinganisho, shuhuda za kimantiki ambazo, badala ya ukweli wa dini kutokuendana na tafiti za sayansi ya leo, tafsiri ya wayakinifu ya tafiti hizi haziingii akilini na upuuzi. Kwa hakika, alithibitisha katika Risale-i Nur kuwa ugunduzi wa ajabu wa kisayansi wa utendaji wa ulimwengu unathibitisha na kuimarisha ukweli wa dini.

Umuhimu wa Risale-i Nur hauwezi kukuzwa thamani, kwani kupitia huo Said Nursi ilifanya kazi kubwa katika kuhifadhi na kujaza nguvu upya imani ya Kiislamu katika Uturuki katika kipindi cha mabadiliko ya haraka sana ya kijamii, na kwa hakika, kazi yake imeendelea kuzidisha umuhimu mpaka leo. Lakini zaidi ya hayo, Risale-i Nur imetosha kwa namna ya kipeke katika kuwaeleza, si kwa Waislamu tu, bali kwa watu wote kwa sababu nyingi. Kwanza imeandikwa kwa mujibu wa akili ya mwanaadamu wa leo, akili ambayo ima ni mwislamu au hapana amekuwa akijazwa moyoni masuala ya falsafa ya uyakinifu, hususani inajibu maswali yote, mashaka na mkanganyiko unaotokea. Pia inajibu ‘kwanini’ zote zinazopatikana katika uulizaji akilini mwa mwanaadamu wa leo.

Kadhalika, inaeleza masuala ya ndani kabisa ya imani, ambayo hapo mwanzoni wanazuoni wakubwa tu walisoma kwa upana, katika namna ambayo kila mmoja, hata wale ambao somo ni jipya, anaweza kufahamu na kupata kitu bila ya kusababisha matatizo au kosa.

Sababu nyingine zaidi ni kuwa, katika kuelezea hali halisi na lengo la mwanaadamu na ulimwengu, Risale-i Nur inaonesha kuwa furaha ya kweli inaweza tu kupatikana katika imani na kumjua Mungu, duniani na akhera. Pia inaonesha huzuni na majonzi ambayo ukafiri unasababisha katika roho na akili ya mwanaadamu, ambayo kwa ujumla, ni jaribio lisilo na mwongozo la kuzuia kwa njia ya uzembe na ukwepaji, hivyo yeyote mwenye akili atajihifadhi katika imani.

Hitimisho

Qur’an Tukufu inaeleza kwa kumlenga mwenye akili, halikadhalika na sehemu nyingine za ndani mwa mwanaadamu. Inamwelekeza mtu atafakari ulimwengu na utendaji kazi wake ili kujifunza hali halisi na malengo ya uumbaji na hivyo kujua sifa za Muumbaji Wake Mmoja na majukumu yake mwenyewe kama kiumbe. Hili, basi ni njia aliyotumia Bediuzzaman katika Risale-i Nur. Ameeleza hali halisi ya ulimwengu kama dalili za Muumba na anafafanua kwa hoja za wazi ambapo kama utasomwa namna hiyo, misingi yote ya imani inaweza kuthibitishwa kiakili.

Njia hii inapofuatwa, mtu anapata imani ya kweli ambayo itakuwa nzuri na imara kiasi cha kutosha kukabili mashaka yoyote yanayoweza kuibuka mbele ya mashambulizi magumu ya uyakinifu, itikadi ya nguvu za asili, na ukanaji Mungu, au mtizamo wa kiyakinifu katika maendeleo ya kisayansi. Maendeleo yote ya kisayansi na ya kitekinolojia, ni kuvumbua tu utendaji kazi wa ulimwengu. Ulimwengu unapoonekana mpana na mchangamano, usio na ukomo na kitabu chenye maana kubwa na kilichounganika kikieleza sifa za Mwandishi wake Pekee, badala ya kusababisha mashaka na utatanishi, uvumbuzi wote huo na maendeleo yanaimarisha imani, yanaifanya iingie ndani zaidi na kuitanua.

Haja ya msingi zaidi ya mwanaadamu ni haja ya kuwa na dini, haja ya kumtambua na kumwabudu Mwenyezi Mungu pamoja na Majina Yake yote Mazuri zaidi na sifa, na kutii sheria Zake, zilizodhihirika ulimwenguni na zilizofunuliwa kwa manabii Wake. Katika kueleza ujumbe wa Qur’an, Kitabu cha mwisho alichoteremsha Mwenyezi Mungu, kilichoelezwa kinagaubaga na Nabii Wake wa Mwisho (rehema na amani zimfikie), na Uislamu, dini kamili na sahihi kwa mwanaadamu. Bediuzzamana Said Nursi alieleza katika Risale-i Nur kuwa hakuna utata au mgawo wa sehemu mbili baina ya sayansi na dini, bali, maendeleo ya kweli na furaha kwa mwanaadamu inaweza, na itaweza kupatikana kwa njia hii tu, njia ya Qur’an.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.