FURAHA YA KWELI

Katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari ya Juu mkabala na gereza, wasichana wakubwa walikuwa wakicheza na kucheka, lakini walionekana kama Mahurulaini wa jahanamu katika pepo hiyo ya kidunia. Ghafla wakaonekana kwangu kama watakavyokuwa katika kipindi cha miaka hamsini, na kicheko chao kikageuka kuwa kilio cha kusikitisha. Kutokana na hayo, ukweli ufuatao ukadhihirika. Maana yake, niliwaona kama watakavyokuwa katika miaka hamsini katika kioo cha sinema ya kufikirika. Niliwaona wasichana hamsini kati ya hao sitini wakiadhibiwa kaburini na wamegeuka mchanga. Ilhali kumi kati yao walikuwa wazee wabaya katika umri wa miaka sabini wakiwa katika mwonekano mbaya tu. Mimi pia niliwalilia.

Hali halisi ya fitna katika zama za mwisho ilinitokea. Ilionekana kwangu kuwa kipengele chake cha kutisha na cha kupotosha kitaibuka kutoka katika nyuso za wanawake wasio na haya. Kwa kukana hiari, itawatupia watu katika moto wa upotovu, kama nondo, na kuwafanya wachague dakika moja ya maisha ya dunia badala ya miaka kumi ya maisha ya milele.

Siku nyingine wakati nikiangalia mtaani, nikaona mfano wenye nguvu katika hayo. Niliwasikitikia sana vijana niliowaona. Wakati nikifikiria: “Wenye hasara hawa hawawezi kujiokoa dhidi ya moto wa tamaa hizi potovu zinazovuta kama sumaku,” namna ya kufanyika mwili kwa nguvu zote zinazohimiza uasi wa imani, zinazopepea moto wa vishawishi hivyo na mfarakano huo, na kuelekeza huko, zilijitokeza mbele yangu. Nikayaambia hayo na waasi wanaofuata mafundisho yake na kupotoka kutoka katika Uislamu:

Enyi viumbe mnaotaabika wanaoitoa kafara dini yao kwa ajili ya kujumuika na Mahurulaini wa Jahanamu, na kupenda kufanya kosa kwa kukengeusha katika njia ya upotovu, wanaokubali upingaji dini na kutoka katika njia ya furaha na tamaa za roho, na kuabudu uhai, wanatishwa na kifo, hawataki kukumbuka kaburi, na wamegeuzia nyuso zao kwenye ukanaji dini! Mnapaswa mjue kwa hakika kuwa, kwa sababu ya kutokushika dini, dunia hii yenu kubwa, saa iliyopita na dakika ijayo, ulimwengu wenu huu wote na muda wenu uliopita na ujao, aina na mbari za wakati uliopita na viumbe na vizazi vya wakati ujao, na ulimwengu wote na mataifa yaliyopita na watu wote na jamii zitakazokuja, yote hayo hayapo kabisa na yamekufa. Kwa hiyo, kwa sababu ya namna ya upotovu wenu, dunia hizi zote zinazosafiri mlioungana nazo kwa sababu ya ubinaadamu wenu na akili, zinaendelea kumwagika kichwani mwenu taabu nyingi za vifo vingi vya kutisha. Kama una ufahamu, hilo jambo litakuwa linaunguza moyo wako. Kama ungekuwa na roho, litakuwa linauunguza. Kama sababu zako hazijazimwa, litakuwa linazama katika huzuni. Kama saa moja pungufu ya ubadhirifu wako na furaha chafu inaweza kuwa sawa na huzuni hii isio na mipaka, masikitiko na maumivu, basi, baki humo. Lakini kama si hivyo, tumia akili! Ili kuokolewa kutokana na jahanamu hiyo, ingia katika pepo ambamo imani inahakikisha duniani pia, na kuonja furaha ya maisha, zingatia mafunzo ya Qur’an, badilisha furaha ndogo katika dakika ya mpito kwa furaha ya ujazo wa ulimwengu mzima, isiyokoma, na ya milele

Kwa hakika, imani inaweza kuleta furaha za peponi humu humu duniani pia. Fikiria faida ifuatayo kati ya mamia ya nuru za furaha. Mathalani, katika dakika ileile unapomwona mpendwa wako akiwa katika hatari kubwa na kufariki, daktari ambaye ni kama Luqman mwenye hikima na Khidr anawasili. Ghafla rafiki yako anarudia kuwa hai. Utajisikia furaha iliyoje. Halikadhalika, imani huwapa furaha wafu wengi mnaowapenda na mliounganika nao. Kwani kwa kupitia katika nuru imani, mamilioni ya watu  mliowapenda katika eneo la kaburi ya waliotangulia wanatolewa ghafla katika kifo na kufufuliwa mbele yenu. Wanafufuka huku wakisema, “Hatukufa, na hatutakufa.” Katika nafasi ya maumivu yasiyopimika kutokana na upweke mwingi, kwa njia ya imani, furaha zisizopimika zinazotokana na muunganiko na kufufuka kunaweza kupatikana duniani pia. Hivyo, hii inaonesha kuwa “Imani ni mbegu inayowaletea waumini vitawi vya Pepo pamoja na furaha zote na mali humu duniani, na ndivyo pia itakavyowaletea matunda huko akhera.” (mwandishi)

ya imani.

Pia msiseme: “Nitapitisha maisha yangu kama mnyama”, kwa sababu kwa mnyama wakati uliotangulia na ujao umefichikana, kama vile haupo. Kwa kutowasababishia watambue hilo, Mwingi wa hekima na Mwingi wa rehema amewaokoa dhidi ya idadi kubwa ya maumivu. Kuku aliyeekwa chini ili achinjwe, hata hasikii maumivu au huzuni yoyote. Hutaka kuhisi pale kisu kinapokata, lakini hisia hizo hupita na kunusuriwa mbali na maumivu hayo, pia. Maana yake, rehema na upole kamili wa Allah (s.w), havifanyi ghaibu ijulikane kwao. Hayo ni kamilifu zaidi kwa wanyama wasio na makosa. Na kwa hivyo, katika furaha za kifisadi hautafikia kiwango cha wanyama; unadondoka chini mno mara elfu moja. Kwa kuwa akili zenu huona mambo waliyofichwa wanyama, na hayo huwaletea maumivu. Nyinyi nyote mmenyimwa wepesi kamilifu unaopatikana katika pazia ya ghaibu.

Pia, kwa kuwa sifa zenu nzuri, kama undugu, heshima, na bidii, ambazo ni sababu ya fahari kwenu, zimezuiliwa katika muda mfupi sana na nafasi ya kidole kimoja katika jangwa kubwa, na ni mahususi katika saa ya wakati huu katika wakati usio na mpaka, zinageuka kuwa za kubuni, za muda mfupi, za kuvumbuliwa, zisizo za msingi, zisizo muhimu, na utu wenu na mafanikio yanafifia kiurari, na kupungua hadi kuwa si chochote si lolote. Ilhali, kwa kuwa undugu, heshima, mapenzi, na bidii za waumini zinaenea wakati uliopita na ujao, ambao upo kwa sababu ya imani yao, hunyanyua utu wao na mafanikio kiurari.

Pia, kama muuza dhahabu kichaa wa Kiyahudi anayetoa thamani ya almasi kwa ajili ya vipande vya kioo, kwa ajili ya mafanikio yenu ya kidunia, mmelipa thamani ya maisha marefu, ya kudumu na mapana, kwa ajili ya maisha mafupi, ya muda mfupi, kwa hivyo hakika mtakuwa washindi katika mipaka hiyo. Kwa kuwa mnajieleza kwa dakika moja yenye thamani ya mwaka wa hisia kama ulafi mkubwa, mapenzi na kisasi, mtakuwa kwa muda mfupi juu ya watu wa dini.

Pia, kwa kuwa akili zenu, roho, moyo na hisia vimeacha kazi zake tukufu, na kushirikiana na kusaidia katika matendo maovu ya roho zenu mbaya na tamaa chafu, mtakuwa washindi juu ya waumini duniani. Na kwa hali ya juu sana mtakuwa wenye kupendwa zaidi. Kwa kuwa akili zenu, moyo, na roho zimeporomoka, zimeharibika, na kuangukia kiwango cha chini kabisa, na zimebadilika, zimechukua muundo mwingine, na kuwa  tamaa chafu na roho ya kudharaulika. Kwa hakika, katika hali hii mtakuwa washindi kwa muda mfupi, utakaokupelekeni Jahanamu, na Pepo kwa waumini waliodhulumiwa.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.