JUU YA MAOVU YA NAFSI

Kutoka katika Muale wa Ishirini na Nane.

Haya yanahusu nukta moja iliyo kwenye aya:

 إِنَّ النَّفْسَ لأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ Qur’an: 12:53

na Hadithi, yenye maana ifuatayo:

(Adui wako mbaya zaidi ni nafsi yako.)

Al-Baihaki, al-zuhd 2/156.

Mtu anayejipenda mwenyewe – kama nafsi yake yenye kuamuru uovu haikutakaswa – hatampenda mwingine. Hata kama atafanya hivyo waziwazi, hatafanya kwa unyoofu, atafanya hivyo kwa ajili ya kujifurahisha au kwa ajili ya kunufaika. Kila mara huwa anajaribu apendwe. Pia, kamwe hajinasibishi na dosari. Huwa anajilinda na kujiweka huru kama mwanasheria. Anajisifu huku akijikweza na hata kudanganya, kwa kujionesha kutokuwa na makosa na anajitukuza, na kwa mujibu wa kiwango chake, anapata pigo kutoka katika aya,

 مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ Qur’an, 25:43

Nafsi yake inayojisifu na inafanya juhudi ya kumfanya apendwe hupata matokeo tofauti kwa kufanyiwa dharau na kutendewa vibaya. Pia anakosa ikhlasi kwenye vitendo vyake vya kuelekea akhera na vinachanganyika na unafiki. Anazidiwa na hisia na utashi wa nafsi ambavyo havioni matokeo yake, havitafakari athari na vimejawa na anasa za sasa; anatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa sababu ya furaha ya saa moja iliyohitajiwa na hisia zake zilizopotoka. Anataabika kwa adhabu ya miaka kumi kwa sababu ya fahari au ulipizaji kisasi wa dakika moja. Sawa sawa, na mtoto mpumbavu anayeuza juzu ya Qur’an kwa pipi moja, ili afurahishe matamanio yake, kutimiza hisia zake na kutosheleza hamu zake, anabadili amali zake njema kama almasi katika njia ya furaha na majisifu yasiyo muhimu kwa vipande vya chupa, na kupata hasara kubwa ambapo alipaswa apate faida kubwa.

اللَّهُمَّ احفَظْنَا مِن شَرَ النَّفْسِ وَالشَيْطَان ومِن شَرِّ الجِنّ وَالإِنْسِ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.