KATIKA KUMTAMBUA MMILIKI WA DUNIA

Kutoka katika barua ya kumi na sita

Kwa kuwa dunia ni ya mpito na maisha haya ni mafupi; na kwa kuwa kazi muhimu za kufanya ni nyingi na maisha ya milele hupatikana hapa; na kwa kuwa nyumba hii ya wageni ya dunia haiwezi kuwa bila ya mmiliki, bila ya shaka ina Meneja Mwenye hekima sana na Mkarimu; na kwa kuwa hakuna jema wala baya litakalosalia bila ya kulipwa; na kwa kuwa kwa mujibu wa aya:

لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا Qur’an, 2:286

hakuna jukumu lisilowezekana, na njia salama inatangulizwa juu ya yenye madhara na kwa kuwa marafiki na hadhi hubakia mpaka kwenye mlango wa kaburi tu, kwa hakika, mtu mwenye bahati zaidi ni asiyeisahau Akhera kwa ajili ya dunia, wala kuiacha Akhera kwa ajili ya dunia, wala kuharibu maisha yake ya milele kwa ajili ya maisha yake ya hapa, wala kupoteza uhai wake juu ya kisicho na maana, bali anajichukulia kuwa ni mgeni na kutenda kulingana na amri ya mmiliki wa nyumba ya wageni, kisha hufungua mlango wa kaburi kwa kujiamini, na kuingia kwenye upeo wa furaha ya milele.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.