Katika siri za بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ Kituo hiki kinajumuisha siri sita kati ya maelfu ya siri za بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

Utanabahisho:

Imejitokeza kwa mbali katika akili yangu fifi, nuru yenye kuchomoza iliyochomoza kutoka juu ya rehema za Allah katika bismillah. Nikataka kuisajili katika sura ya maangalizo na kumbukumbu zangu mahususi, nikafanya jaribio la kuinasa nuru hiyo angavu kwa kuzunguka kwake na wigo wa siri zake zinazofikia kiasi cha siri thelathini ili iwe rahisi kuzidhibiti na kuwa wepesi kuziandika, isipokuwa mimi kwa masikitiko sikuwafikishwa kikamilifu hivi sasa katika dhamira yangu, hivyo siri zikapungua hadi kuwa sita tu.

Na maelezo katika kituo hiki yameelekezwa kwenye nafsi yangu kiudhati, pale nisemapo: “Ewe mwanaadamu!” naikusudia nafsi yangu.

Basi somo hili pamoja na kuwa linanihusu mimi, isipokuwa mimi ninalihudhurisha kwa mitazamo yenye kusibu kwa ndugu zangu wenye kupekuwa kwa makini ili iwe (Kituo cha pili cha muale wa kumi na nne). Na nataraji litakuwa ni mahali pa faida kwa atakae fungamana nami kwa mahusiano ya kiroho na ambaye nafsi yake iko macho zaidi kuliko mimi na imezindukana zaidi. Somo hili linaelekea moyoni zaidi kuliko kwenye akili na linachungulia kionjo cha kiroho zaidi kuliko dalili ya kimantiki.

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

قَالَتْ يَا أَيُّهَا المَلَأُ إِنِّي أُلْقِيَ إِلَيَّ كِتَابٌ كَرِيمٌ إِنَّهُ مِن سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ Qur’an, 27: 29-30

Katika kituo hiki tutataja kiasi cha siri.

Siri Ya Kwanza

Katika kuchunguza kwangu Bismillah nikaona nuru kati ya nuru za

             بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

katika sura ifuatayo:

Kuna alama tatu zenye nuru angavu ya kiungu juu ya vijialama vya viumbe, na migawanyiko ya sura ya ardhi, na katika mionekano ya uso wa mwanaadamu. Alama hizi zenye kupendeza na aya zenye kuchomoza ni zenye kuingiliana baadhi yake ndani ya nyingine, hata hakika kila mojawapo inabainisha kielelezo cha mwingine na mfano wake.

Alama ya kwanza

Ni alama ya kiungu, ile ishara kuu ichomozayo kutokana na kusaidiana na kutegemeana na kukumbatiana na kuitikiana kulikoenea katika sehemu za ulimwengu mzima, kiasi

بِسْمِ اللهِ

inaelekea huko na kujulisha juu yake.

Alama ya pili

Ni alama ya Al-rahmania, ile ishara kuu yenye kung’aa kutokana na kuendana kunasibiana, kujipanga vema na kuwiana na upole na rehema viendavyo katika malezi ya mimea na wanyama, kiasi

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

inaelekea huko na inajulisha juu yake.

Alama ya tatu

Nayo ni alama ya alrahimiya, ile alama ya juu, yenye kudhihiri kutokana na mazuri ya upole wa kiungu na madhubuti ya huruma yake na mionzi ya rehema yake iliyoundika katika alama za hakika jumuishi ya mwanaadamu, kiasi jina Al-rahiim ambalo limo katika

 بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

linaelekea huko na kujulisha juu yake.

Yaani hakika

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

ni anuani takatifu ya aya tatu katika aya za ahadiyya (Upekee), hata kwamba inaunda mstari wa nuru katika kitabu cha uwepo, na kupiga mstari unaoangaza katika ukurasa wa ulimwengu na inawakilisha kamba ngumu kati ya Muumba na kiumbe.

Yaani hakika

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

hali ya kuteremka kutoka katika arshi tukufu inafungamana ncha yake na ukomo wake na mwanaadamu ambaye ni tunda la viumbe na nakala ya ulimwengu mdogo, basi inaunga tandiko na arshi tukufu na kuwa ni njia nzuri ya kukwea mwanaadamu kwenda katika arshi ya makamilifu yake.

Siri Ya Pili

Hakika Qur’an tukufu daima inabainisha udhihirisho wa (upekee) ndani ya udhihirisho wa (kiumoja) ili kuzuia dhidi ya kuzama kwa akili na kutawanyika ndani ya (kiumoja) uliodhihiri katika viumbe wengi hawadhibitiwi na idadi.

Haya tufafanue hilo kwa mfano:

Jua linazunguka kwa mwanga wake vitu visivyo na mipaka. Basi kwa ajili ya kutazama dhati ya jua katika mkusanyiko wa mwanga wake inalazimu iwe kuna taswira pana sana na mtazamo unaokusanya. Kwa ajili hiyo jua linaonesha dhati yake kwa kupitia kuakisi kwa mwanga wake katika kila kitu penyezi, yaani kila chenye kung’ara kulingana na ukubalifu wake kinadhihirisha udhihirisho wa kidhati wa jua pamoja na sifa zake maalumu kama mwanga na joto, na hiyo ili dhati ya jua isije kusahaulika,  na kama kinavyodhihirisha kila chenye kung’ara jua kwa sifa zake zote kulingana na ukubalifu wake, kila sifa katika sifa za jua kama joto na mwanga na rangi zake saba inazungukia pia kila kitu kinachokabiliana nalo.

Hakuna makosa katika kupiga mifano

وللهِ المثَلُ الأعْلَي

Basi kama Allah (s.w), wa pekee, mkusudiwa kwa haja zote ana udhihirisho katika kila kitu kwa majina yake mazuri yote, na hasa katika waliohai, na hasa katika kioo cha dhati ya mtu, vilevile kila jina katika majina yake mazuri yanayoambatana na vilivyomo linazungukia vilivyomo vyote kwa namna ya umoja na upekee, basi (s.w) anaweka muhuri wa upekee katika Umoja mbele ya jicho la mwanaadamu na mbele ya uoni wake, ili akili zisizame na kupotea katika upana wa umoja na ili nyoyo zisisahau na kuhemewa na dhati takatifu ya kiungu.

Basi

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

inatoa dalili juu ya mafundo matatu muhimu ya muhuri huo pambanuzi na kuubainisha.

Siri Ya Tatu

Ni dhahiri bali inashuhudiwa kwamba rehema ya kiungu ndio ambayo imewafurahisha viumbe wasiokuwa na mipaka.

Na kwamba rehema yenyewe ndio iliyotoa nuru kwa hivi viumbe vilivyomo vilivyofunikwa na kiza. Na kwamba rehema vilevile ndio ambayo katika malezi yake imelea viumbe hivi vyenye kugeuka katika haja zisizo na mipaka. Na pia rehema hiyo ndio ambayo imeelekeza viumbe kutoka kila upande na eneo na kuwaongoza kwa mwanaadamu na kuwatiisha kwake. Bali imewafanya kuwa wanatazamia kusaidiana naye na kujitahidi kumsaidia kama sehemu za mti zinavyoelekea katika tunda lake. Na tena rehema hiyo ndio ambayo imeimarisha anga hili pana na kuupamba huu ulimwengu mtupu. Na kwamba rehema hiyo hiyo ndio ambayo imemfanya mwanaadamu huyu mwenye kutoweka ameteuliwa kwa ajili ya kudumu na kubaki milele na kumfanya kuwa mstahiki wa kupokea maongezi ya mola mlezi wa walimwengu wote, na kumpa fadhila ya utawala wake (s.w).

Basi ewe mwanaadamu! kwa kuwa rehema ni yenye kupendwa, na ina nguvu na mvuto na msaada kwa kiasi hiki, basi shikamana na ukweli huo kwa kusema kwako:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

na ujiokoe kutokana na balaa la upweke wa moja kwa moja na uikomboe nafsi yako kutokana na maumivu ya haja zisizo na ukomo, na jikurubishe kwa mwenye kiti cha enzi mtukufu, na uwe msemezwa mwaminifu na mwandani mkweli kwake kwa nuru za rehema hiyo na upole wake.

Naam, hakika kukusanya viumbe kumzunguka mwanaadamu ni ndani ya hekima iliyokadiriwa, na kufanya kila mmoja kati yao anyooshe mkono wa msaada kwake ili kukidhi haja zake zenye kuongezeka pasi na shaka inatokana na moja ya hali mbili:

Ima kila sampuli kati ya sampuli za viumbe kinamjua mwanaadamu na hivyo kumtii na kujitahidi kumhudumia yaani mwanaadamu huyu aliyezama katika udhaifu wa bila kikomo anamiliki uwezo wa mamlaka yasiyo na ukomo na hili ni mbali kabisa na mantiki ya akili achilia mbali kwa muhali zilizomo.

Au kusaidiana huku na kusaidia, bali hutendeka kwa elimu yenye kuzungukia kila kitu ya Muweza asiye na mipaka iliyojificha nyuma ya viumbe, yaani hakika aina za viumbe hazimjui mwanaadamu huyu hadi zimnyooshee mkono wa msaada,bali hizo ni dalili za yule anayemjua mwanaadamu huyu na kumhurumia na kumjua hali yake naye ni Muumba Mwenye kurehemu.

Basi ewe mwanaadamu rejea katika akili yako! Je, inayumkinika mola huyu Mwingi wa rehema asikujue wala kukuona na hali yeye ndie ambaye aliyeshinikiza viumbe kukusaidia hali ya kuitikia mahitaji yako yote.?

Basi kwa kuwa (s.w) anakujua na kukujulisha kujua kwake huku kwa kueneza neema zake juu yako, sio juu yako ila kufanya jitihada kumtambua na kujitahidi kuonesha kuwa unamjua kwa kuheshimu amri zake. Na ujue kwa yakini kuwa hakika si lingine bali ni ukweli wa rehema ya kiungu -ambao unaenea hekima, uangalizi, ujuzi, na uweza- umetiisha kwa ajili yako viumbe hivi na umevijaalia kufuata matakwa yako na hali ya kuwa wewe ni kiumbe dhaifu, mdogo, mshindwa, fakiri na mwenye kutoweka.

Basi rehema kubwa kwa kiasi hiki, pana kwa kadiri hii, hapana shaka, hiyo inataka shukrani ya jumla safi kwako na taadhima isiyochanganyika na chochote.

Tambua kuwa, haitafsiriwi shukrani hiyo ya jumla na taadhima safi isipokuwa na

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

basi iseme na uichukue kuwa ni kifikisho kufikia kwako katika hiyo rehema pana, na uifanye kuwa ni muombezi wako mbele Al-rahman Al-rahim.

Ni kweli, kuwepo kwa rehema na kudhihiri kwake ni dhahiri mno kuliko jua katika tumbo la mbingu, kwa sababu kama upatikanavyo mfumo wa nakishi nzuri katikati kwa kupangika ujazo wake na vizuizi vyake na kupangika kwa miweko ya nyuzi inayonyooka kila upande kuelekea katikati, hakika nyuzi za mionzi ya nuru inayochomoza kutokana na kudhihiri kwa majina elfu moja na moja katika majina mazuri, na iliyonyooka kuelekea ulimwengu huu mpana sana inafuma juu ya alama zake ndogo ndogo mfumo wa ukomo wa kupendeza na uzuri ndani ya mzunguko wa rehema nyingi, hadi inadhihirisha kwa akili -wazi zaidi kuliko jua kwa macho- muhuri uliyo wazi wa sifa ya urehemevu na nakshi ya kupendeza ya huruma na upole, na alama ya ajabu ya uangalizi.

Naam, hakika ambaye anapangilia jua, mwezi, chembe chembe, madini, mimea na wanyama, na kuviratibu vyote kwa mionzi ya majina elfu moja na moja, kana kwamba ujazo wa nakshi ya ajabu na vizuizi vyake, na nyuzi zake za kinuru, na kuvitiisha vyote katika kuhudumia maisha. Na ambaye anadhihirisha upole wake na huruma yake kwa viumbe wote kwa vile alivyoweka amana kwa wazazi -kuanzia mimea na wanyama- huruma ile tamu yenye ladha kuelekea vitoto vyao. Na ambaye amedhihirisha madhihirisho ya rehema yake yenye kung’ara zaidi na nakshi ya Rububiya yake nzuri mno (s.w) kwa kule kuvidhalilisha viumbe hai kwa maslahi ya maisha ya mwanaadamu akibainisha kwa hilo daraja ya mwanaadamu kwake na umuhimu wake kwake. Yeye ndiye Mwingi wa rehema mwenye uzuri ambaye amejaalia rehema yake hii pana muombezi, mwenye kukubaliwa, na mwenye kuzoeleka mbele ya utajiri wake usio na mipaka, hutaka maombezi kwayo wenye uhai na mwanaadamu mwenye ufukara muhitaji kabisa wa rehema hiyo.

Basi ewe mwanaadamu! ukiwa mwanaadamu kweli basi sema:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

upate muombezi huyo.

Hakika ni wazi bali inashuhudiwa kuwa rehema ndio inayolea makundi ya mimea na wanyama ambayo yanavuka makundi mia nne elfu licha ya kutofautiana kwake na kuwa aina mbalimbali na ndio inayoendesha mambo yao yote pasina kuchanganya wala kusahau na katika wakati ufaao hasa na mpangilio kamili zaidi na hekima timamu na utunzaji muwafaka mno mpaka kwa uendeshaji huu na ulezi umeweka muhuri wa upekee na kuugonga juu ya vijialama vya ardhi.

Naam, hakika kuwepo kwa rehema hiyo ni thabiti na ya mkato kama uwepo wa vilivyomo vilivyotawanywa ardhini, kama zilivyo dalili za kutokea kwake ni kwa idadi ya hivyo vilivyomo.

Na kama tunavyoshuhudia katika uso wa ardhi ishara ya upekee na alama yake na muhuri wa rehema, hakika katika vialama vya uhakika wa kimaanawi wa kibinaadamu kuna muhuri wa rehema pia, muhuri huu sio mchache kwa uwazi kuliko ule ambao uko juu ya uso wa ardhi wala kuliko ule ambao uko juu ya uso wa vilivyomo bali hakika ya sifa pekee ya rehema hii ina ujmla na ukusanyaji kana kwamba ni kipenyo chenye kujumuisha nuru za udhihirisho wa majina mazuri.

Basi ewe mwanaadamu! hakika yule ambaye amekupa alama hizi za kimaanawi na kuziwekea rehema na kuzipiga muhuri wa umoja, Je, ni katika yanayowezekana kuwa akuache bure bure, wala asikujali wala kukupa umuhimu wala asifuatilie matendo yako na harakati zako? Je, ni katika yumkini ajaalie michakato ya vyote vilivyomo kukuelekea wewe kimchezo tu hakuna sababu nyuma yake? Au ajaalie mti wa uumbaji mkuu kuwa ni mti usio na maana yeyote, na tunda lake ni tunda linaloharibika? au Je, yawezekana aweke rehema yake iliyodhahiri sawa na kudhihiri kwa jua -na ambalo haliruhusu kuwepo shaka yoyote- na kuweka hekima yake iliyo wazi uwazi wa mwanga muweko wa kukana na kupinga? Kamwe ametukuka Allah na hayo utukufu mkubwa.

Basi ewe mwanaadamu!

Tambua hakika kufikia arshi ya rehema hiyo kuna ngazi, ngazi hiyo ni:

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

Ukitaka kujua kiasi cha umuhimu wa ngazi hizi, na kiasi cha ukubwa wake na nafasi yake basi tazama mianzoni mwa sura za Qur’an tukufu zinazofikia sura mia moja na kumi na nne, na tazama vianzio vya kila kitabu cha thamani, na tazama kuanza kwa kila jambo lenye umuhimu. Hadi ihesabiwe ni hoja ya kukata shauri juu ya utukufu wa Bismillahi na heshima yake kuwa juu aliyosema Imamu Shafii (r.a) na mifano yake katika mujitaidina wakuu: “Hakika Bismillah japokuwa ni aya moja hakika imeshuka katika Qur’an mara mia moja na kumi na nne”.

Al-Shafii, Al-Umm 1/208. Al-Ghazzaly, Al-Mustasfaa 1/82.

Siri Ya Nne

Kudhihiri kwa umoja katika viumbe visivyo na mpaka hauzungukii kila anayesema

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

kwani inatawanyika akili na kupotea katika wingi huo kwa sababu inalazimu ili kuitazama dhati ya Allah (s.w) ya pekee kupitia mkusanyiko wa viumbe wakati wa kutamka:

 إيَّاكَ نَعْبُدُ وإيَّاكَ نَسْتَعِيْنُ

inalazimu kuwepo kwa moyo mpana kutoshea ardhi yote.

Kujengea siri hii madhubuti hakika Allah (s.w) anabainisha kwa uwazi chapa ya upekee katika kila sehemu kama anavyo idhihirisha katika kila sampuli na hii ili mitazamo ikazwe kuelekea dhati ya Allah (s.w) ya pekee na kila mtu aweze -vyovyote itakavyofikia daraja yake- katika kuelekea moja kwa moja katika tamko lake:

إيَّاكَ نَعْبُدُ وإيَّاكَ نَسْتَعِيْنُ

kuelekea dhati ya Allah (s.w) takasifu kuliko zote bila ya kujikalifu au ugumu.

Kubainisha siri hii kuu Qur’an tukufu inapochambua aya za Allah katika anga za juu na katika duara pana zaidi tahamaki inataja duara dogo mno katika maduara ya viumbe na sehemu ndogo mno katika sehemu zake kudhihirisha chapa ya upekee kwa uwazi katika kila kitu.

Mfano wa hilo:

Pale Qur’an tukufu inapobainisha aya za kumba mbingu na ardhi inamaliza na aya za kuumbwa mwanaadamu na kubainisha neema ndogo ndogo katika sauti yake na maajabu ya hekima katika muonekano wake ili fikira isitawanyike katika anga pana wala moyo usizame katika wingi usio na kikomo na ili roho imfikie muabudiwa wake wa haki pasina kiunganishi. Basi aya tukufu ifuatayo inabainisha hakika iliyotangulia bayana ya kimuujiza.

وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ Qur’an, 30: 22

Na kama hivi hakika aya za umoja na hitimisho zake pamoja na kuwa zimewekwa katika viumbe kwa wingi usio na kikomo kuanzia vihitimisho vipana zaidi na vingi zaidi kiujumla kwenda vidogo zaidi kisehemu, katika maduara yenye kuingiliana na katika ngazi anuwai na sapuli mbali mbali, ila kuwa wazi kwa vihitimisho hivi vya kiumoja -vyovyote itakavyofikia katika kudhihiri- huo ni uwazi ndani ya wingi wa viumbe hautoshelezi haki ya kutosheleza kiuhakika tamko katika

 إِيَّاكَ نَعْبُدُ

Hivyo inalazimu kuwepo chapa ya upekee katikati ya kuhitimisha umoja ili ufungue njia mbele ya moyo ili kuifikia dhati ya Allah (s.w) takatifu bila ya kukumbushia wingi.

Kisha kwa ajili ya kugeuza mitezamo katika chapa ya umoja na kuzileta nyoyo upande wake imewekwa juu ya alama hiyo ya upekee nakshi ya ajabu katika ukomo wa mvuto, na nuru angavu katika ukomo wa kuangaza, na utamu wenye ladha katika ukomo wa maonjo, na uzuri wa kupendwa katika ukomo wa kupendeza, na hakika imara katika ukomo wa nguvu, hiyo ndio alama ya rehema na muhuri wa urehemevu.

Naam, hakika nguvu ya rehema hiyo ndio ambayo inaleta mitazamo ya wenye hisia kwake na kuifikisha katika chapa ya umoja na kuifanya itazame dhati ya wa pekee tukufu mno hadi inamfanya mwanaadamu anapata kusemeshwa kwa hakika katika

إيَّاكَ نَعْبُدُ وإيَّاكَ نَسْتَعِيْنُ

Na hivyo hivyo katika

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

kwa kuwa ni faharisi ya Al-fatiha ufunguo wa kitabu kilicho wazi na muhtasari wake imekuwa ni anuani ya siri hii kubwa na mfasiri wake basi awezaye kupata anuani hii anaweza kutembea katika tabaka za rehema na ambaye anamtaka mfasiri huyu atamke anatambua siri za rehema na kujifunza hizo na kushuhudia nuru za urehemevu na upole.

Siri Ya Tano

Na hakika imepatikana katika hadithi tukufu “Hakika Allah amemuumba Adamu kwa sura ya Mwingi wa rehema”

Al-Darakutny, Al-Sifaat 36, imepokewa kutoka kwa Ibn Umar kwa tamko: “Msiusifu vibaya uso, kwa hakika Allah (s.w) amemuumba Adam kwa sura ya Al-rahmani (s.w).

au kama rehema na amani ziwe juu yake alivyosema.

Baadhi ya watu wa tarika za kisufi wamefasiri hadithi hii tukufu tafsiri ya ajabu haiafikiani na itikadi za kiimani wala haikubaliani. Bali baadhi ya watu wa ashki wamefikia kutazama alama ya maanawi ya mwanaadamu kutazama sawa na wanavyotazama sura ya Mwingi wa rehema.

Na ilivyokuwa ndani ya wengi mno ya watu wa ashiki hali ya kuzama, ya kuhamisha akili na kuchanganya mambo, pengine wasamehewe katika mapokeo yao yanayohalifu uhakika. Isipokuwa watu wa mwamko na ufahamu na muongozo wanakataa kabisa kabisa maana haya yanayokataana na misingi ya itikadi ya Imani wala hawazikubali kamwe. Na lau mmoja wapo ataziridhia atakuwa ameanguka katika kosa na kuwa kando na haki.

Naam, hakika ambaye anaendesha mambo ya ulimwengu na anayetawalia mambo yake kwa wepesi kama kuendesha kasri au nyumba yoyote, na ambaye anazitikisa nyota na maumbo makubwa ya mbinguni kama punje ndogo za vumbi kwa ukomo wa hekima na wepesi, na ambaye zinamfuata chembe hizo ndogo na kushika amri yake na kunyenyekea kwa hekima yake, hakika anayefanya haya yote ni Allah mtukufu (s.w) basi kama yeye alivyoepukana na sifa zote pungufu na mtakatifu yu mbali na shirki basi hana mshirika wala ruwaza wala dhidi wala mwenza, basi kabisa hana mfano wala mrandano wala sura pia na hii kwa tamko la aya tukufu:

 لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ Qur’an, 42: 11

Isipokuwa mambo yake ya hekima na sifa zake tukufu na majina yake mazuri hutazamwa kwa miwani ya kumithilisha na methali kulingana na madhumuni ya aya

وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَى فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ Qur’an, 30: 27

Yaani methali na kumithilisha kupo katika kutazama mambo yake makubwa (s.w).

Na hadithi hii tukufu ina makusudio matukufu mengi kati ya hayo: kwamba mwanaadamu ni kiumbe kilichoumbwa kwa sura inayodhihirisha jina la Allah (Al-rahman) udhihirisho timamu. Tumekwishabainisha katika siri zilizotangulia kwamba kama mfano linavyodhihiri jina la (Al-rahman) kutokana na miale ya madhihirisho ya majina elfu moja na moja katika majina mazuri juu ya uso wa ulimwengu, na kama linavyooneshwa jina la Ar-rahman kwa madhihirisho yasiyo na mpaka kwa Rububiyya isiyo na mipaka juu ya alama za ardhi, hivyo hivyo anadhihirisha (s.w) udhihirisho uliyo kamili wa jina hilo (Al-rahman) katika sura inayokusanya ya mwanaadamu, analidhihirisha kwa kipimo kidogo mithili ya anavyodhihirisha katika alama za ardhi na ulimwengu kwa kipimo kipana na kikubwa zaidi.

Na katika hadithi tukufu kuna ishara vilevile kwamba kwa wanadamu na vyenye uhai kuna madhihirisho yenye kujulisha juu ya Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu ambayo ni mfano wa vioo vyenye kuakisi madhihirisho yake (s.w) basi mwanaadamu kujulisha kwake (s.w) ni jambo dhahiri lenye kukata shauri linafanana katika kuwa kwake wazi ujulishaji wa kioo chenye kung’ara picha ya jua na kuliakisi kwake jua lenyewe. Basi kama inavyowezekana kusemwa kwa kioo hicho: ni jua kuashiria kiasi cha kung’aa kwake na uwazi wa kulijuulisha kwake, hivyo hivyo inasihi kusemwa -na imekwishasemwa katika hadithi- kwamba katika mwanaadamu kuna sura ya Mwingi wa rehema kuashiria uwazi wa kujulisha kwake jina la (Al-rahman) na ukamilifu wa kunasibiana naye na umadhubuti wa uhusiano wake naye hivi hakika ya wale wenye kuwa kati na kati katika watu wa umoja wa uwepo wamesema: “Hakuna kilichopo isipokuwa yeye” kwa kujenga siri hii ya uwazi wa kujulisha na anuani ya ukamilifu wa kunasibiana.

اللَّهُمّ يَا رَحْمَن يَا رَحِيْم بِحَقّ

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

ارْحَمْنَا كَمَا يَلِيْق بِرَحِيْمِيّتِك، وَفَهّمْنَا أَسْرَارَ

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

كَمَا يَلِيْقُ بِرَحْمَانِيَّتِكَ آمِيْن

Siri Ya Sita

Ewe mwanaadamu unayegeuka geuka katika udhaifu usio na ukomo na ufukara usio na mpaka ukitaka kufahamu kwamba vipi rehema ni kisaidizi kikubwa na muombezi mtarajiwa zaidi elewa:

Rehema ni msaidizi mkubwa kwenda kwa mfalme mkuu mwenye utukufu ambaye nyota na chembe vumbi vinamtii utiifu timilifu katika mpangilio timamu wote kwa pamoja mfalme huyo mwenye utukufu na ukarimu, mola mlezi wa walimwengu wote, mkwasi asiyehitajia viumbe wote, mkubwa mwenye hadhi ya juu kuvuka vyote vilivyomo, hana haja asilani kwa vilivyomo bali kila kitu kimenyenyekea utukufu wake na kusalimu amri kwa uweza wake na kuwa dhalili kwa ushindi wake usiyoshindwa na kunyenyekea haiba ya utukufu wake. Rehema basi ewe mwanaadamu inakunyanyua hadi kwenye viunga vya hadhara ya huyo mkwasi wa moja kwa moja na kukufanya mwandani wa mfalme huyo wa milele mkuu, bali inakupandisha katika makamo ya mazungumzo yake matukufu na kukufanya kuwa mja mwenye kukirimiwa mpendwa kwake. Lakini kama ilivyo hufiki kwenye jua kwa sababu ya kuwa kwako mbali nalo, bali huwezi kulikaribia kwa hali yoyote, hakika mwanga wake unakupa udhihirisho wake na sura yake kupitia kioo

ولله المثَلُ الأَعْلَي

Basi sisi pamoja na umbali wetu kabisa na Allah (s.w) hakika nuru ya rehema yake inamkaribisha kwetu.

Basi ewe mwanaadamu! Hakika anayebahatika kupata rehema hii amepata hazina kubwa isiyokwisha, hazina ujazo wake ni nuru. Ama njia ya kufikia kwenye hazina hiyo kuu elewa: kuwa mfano ung’aao zaidi wa rehema na mbora wa anayeiwakilisha, na ulimi fasaha mno unaoitamka, na mlinganiaji wake mtukufu zaidi, ni yule ambaye ameitwa katika Qur’an

 رَحْمَةً لِلْعَالمَين

naye ni mjumbe wetu mpendwa (s.a.w). Basi njia ifaayo zaidi kufikia hazina hiyo ya milele ni kufuata sunna yake iliyotakaswa. Lakini vipi namna ya kumfikia mtume kipenzi (s.a.w) na kipi kifikishaji kwake?

Basi elewa cha kukufikisha ni kumswalia. Ndio, kumswalia kuna maanisha rehema, kumswalia ni kuomba dua ya rehema kwa ajili ya rehema hiyo iliyo katika sura ya mwili hai na ndio njia ya kufikia kwa ambaye ni rehema kwa walimwengu.

Basi ewe mwanaadamu! jaalia kumswalia ni njia ya kumfikia, kisha shikamana naye akufikishe kwenye rehema ya Al-rahmanirrahiim, hakika umati wote kwa dua yake na swala zake kwa mtume (s.a.w) inathibiti kwa uwazi kiasi cha kima cha rehema hii na kiasi cha umuhimu wa zawadi hii ya kiungu na kiasi cha upana wake na utukufu wake.

Muhtasari:

Hakika mlinzi wa hazina ya rehema ya kiungu na mlinganiaji wake Mkarimu mno ni mtume mtukufu (s.a.w) kama ilivyo kuwa funguo kuu zaidi ya hazina hiyo ni

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

Na kifunguacho kwa ulaini hiyo rehema ni swala juu ya mtume mpendwa (s.a.w).

اَللّهُمَّ بِحَقِّ أَسْرَارِ بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

صَلِّ عَلَي مَن أَرْسَلْتَه رَحْمَةً لِلْعَالَمِيْنَ كَمَا يَلِيْقُ بِرَحْمَتِك وَبِحُرْمَتِهِ وَعَلَي آلِهِ وَأَصْحَابِهِ أَجْمَعِيْنَ، وَارْحَمْنَا رَحْمَةً تُغْنِيْنَا بِهَا عَنْ رَحْمَةٍ مَنْ سِوَاكَ مِنْ خَلْقِكَ آمِيْنَ.

سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَناَ إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنْتَ العَلِيْمُ الحَكِيْمُ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.