KIJANA BORA

Kutoka Barua ya Ishirini na Tatu Je ifuatayo ni Hadithi, na inamaanisha nini? “Vijana bora ni wale wanaojifananisha na wazee, ilhali wazee wabaya ni wale wanaojifananisha na vijana.”

Al-Tabarani, al-mujam al-kabir 22/83, al-mujam al-awsat 6/94.

Jibu:

Nimesikia kuwa ni Hadithi. Maana yake ni haya: Kijana bora ni ambaye, hufikiria kifo na kuifanyia kazi Akhera kama mzee, huepuka kujumuika na wale ambao ni wafungwa wa utashi wa ujana na waliotumbukia katika kutokujali.        

Na mzee mbaya zaidi miongoni mwenu ni anayetaka kufanana na kijana katika kutokujali na hisia, na anafuata utashi wa nafsi kama mtoto.

Namna sahihi ya sehemu ya pili uliyoona ubaoni kwako ni haya yafuatayo, nimeyatundika juu ya kichwa changu kutokana na hekima yanayofundisha. Huwa ninayaangalia kila asubuhi na jioni, na kupata maelekezo kutokana nayo:

“Kama unataka rafiki, Allah anatosha.” Ndiyo, kama yeye ni rafiki, kila kitu ni rafiki.

“Kama unataka mwenza, Qur’an inatosha.” Kwani  kifikra mtu anaweza kukutana na mitume na malaika ndani yake, kuona mambo waliyohusika nayo na kuyazoea.

Kama unataka mali, kuridhika kunatosha. Ndiyo, mtu aliyeridhika ni mwekevu, na mtu mwekevu hupata baraka kwa wingi.

Kama unataka adui, nafsi inatosha. Ndiyo, mtu anayejipenda sana hupatwa na majanga na kukumbwa na matatizo, ilhali asiyejipenda sana, hupata furaha na hupata rehema.

Kama unataka nasaha, mauti yanatosha. Ndiyo mtu anayetafakari mauti huokolewa dhidi ya kuipenda dunia, na hufanya bidii kwa ajili ya akhera.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.