KUAMKA KWA UDANGANYIFU

Elewa ewe rafiki yangu! Mimi ni katika wale ambao wanarejewa na shairi ambalo linakwenda kama hivi:

“Macho yangu yalilala kwenye usiku wa ujana; nikaja kuamka tu asubuhi ya uzee.”

Kwani nilidhani kuwa nilifika kilele cha juu mno cha kuwa macho ujanani, lakini sasa ninafahamu kwamba huko hakukuwa kuamka, huko kulijumisha tu usingizi mwingi. Kwa hiyo, waangavu na wenye kuzinduka katika ada ya wastaarabu kwa mwenye kujidai na kujivuna yaweza kuwa ndivyo nilivyokuwa kwenye ujana wangu.

Watu wa namna hiyo wanafanana na mwenye kulala ambaye anaota kuwa yuko macho, na anawaambia watu kuhusu njozi zake. Lakini kuwa macho kwake kwenye njozi kuna ashiria kwamba, amepita katika pazia ndogo ya usingizi na kuingia kwenye pazia nzito. Mlalaji wa namna hiyo ni kama vile amekufa. Anawezaje kuwaamsha watu ambao nusu wamelala?

Ewe ambaye unajidhania kuwa unamiliki utambuzi wako kikamilifu, wakati mumelala! Usiyumbe kuelekea ‘utamaduni’ au kuwa mvumilivu kwao katika mambo ya dini, au kujaribu kurandana nao, kwa kuwa ghuba ilopo kati yetu ni kubwa. Hutaweza kuijaza na kujenga njia ya mawasiliano. Ama utaungana nao au kuanguka katika upotevu na kuzama.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.