KUHUSU TAQWA

Barua hii ni muhimu sana

TAQWA NA MATENDO MEMA

باسمه سبحانه

Wapendwa ndugu zangu wa dhati!

Nimekuwa hivi karibuni nikifikiri juu ya misingi ya taqwa, na matendo mema,ambayo baada ya imani mara nyingi huchukuliwa kama msingi kwa mtazamo wa Qur’an. Taqwani kuepuka dhambi na makatazo, wakati kutekeleza mambo mazuri ni kufanya ndani ya eneo la yaliyoamrishwa na kwa njia ya kutafuta radhi za Allah (s.w).

Ingawa kukataa uovu hutangulia kuliko kuvutia manufaa, katika nyakati hizi za ufisadi, kuchupa mipaka, ushawishi, na anasa, kujizuia na utendaji maovu, na kuacha madhambi makubwa ambayo inaunda taqwalimekuwa ni jambo la msingi na kuchukua nafasi ya kipaumbele.Uharibifu na mawimbi ya hasi yamefikia kiwango cha kutisha wakati huu, kwa hivyo, taqwainaunda msingi wenye nguvu kabisa usoni mwa movu hayo. Mtu ambaye anatekeleza majukumu ya lazima ya kidini na hatendi dhambi kubwa ataokolewa. Matendo mema ambayo yametekelezwa kwa ikhlas katikati ya madhambi makubwa kama hayo ni mafanikio kwa kiwango kidogo sana. Pia katika hali ngumu kama hizi, kitendo kidogo sana cha wema huwa ni kikubwa.

Zaidi ya hapo Taqwa inaingiza pia aina ya mambo mema, kwa sababu ni lazima kuachana na mambo ya haramu. Kutenda mambo ya wajibu kunavuna malipo sawa na matendo mengi ambayo ni ya sunna. Katika zama mfano kama hizi za sasa kwa kutekeleza tendo dogo na kuachana na madhambi makubwa, kuepuka tendo moja tu la haramu wakati wa  kukabiliwa na mashambulizi ya maelfu ya madhambi ni sawa na  kutimiza mamia ya mambo ya wajibu. Kwa nia ya kuepuka madhambi kwa jina la taqwa, nukta hii muhimu inabeba matendo muhimu mazuri sana kutokea katika ibada (hasi).

Jukumu muhimu kabisa kwa wanafunzi wa Risale-i Nur wakati huu, inapasa liwe kuichukuwa taqwa kama msingi wa tabia zao. Kwani katika maisha ya kijamii leo hii, kila dakika mtu anakabiliwa na mamia ya dhambi, kwa hakika, hata hivyo, kupitia Taqwa na nia ya kuyaepuka madhambi, anakuwa kana kwamba anatekeleza mamia ya matendo mema.

Inajulikana vizuri kwamba watu ishirini hawawezi kujenga kasri kwa siku ishirini ambalo mtu mmoja anaweza kulivunja kwa siku moja, ambapo watu ishirini wanalazimika kufanya kazi mbele ya uharibifu wa mtu mmoja, wakikabiliwa na maelfu ya mawakala wa uharibifu katika muda uliopo upinzani mkubwa kabisa na taathira ya mtengenezaji kama Risale-i Nur ni ya hali zaidi ya kwaida. Kama hizi nguvu mbili kinzani zikiwa kwenye ngazi moja, mafanikio na ushindi wa matengenezo ya Risale-i Nur itakayofikia yatakuwa yakimiujiza.

Kwa ufupi:

Heshima na huruma, ni misingi muhimu kabisa katika kuendesha maisha ya kijamii, imetikiswa vibaya kabisa. Katika maeneo mengine, matokeo yamekuwa makubwa na ya kutisha – kuhusiana na wazazi wenye umri mkubwa. Shukrani ziwe kwa Allah (s.w) ambaye kila ambapo Risale-i Nur inapokabiliana na uhribifu wa kutisha, inatoa upinzani na kutengeneza palipoharibika.

Kama Yaajuja Na Maajuja walivyosababisha ufisadi na vurugu ulimwenguni kwa kupitia kuharibu kizuizi cha Dhal qarnayn, vilevile kwa kutikisika kwa kizuizi cha Qur’an kilichoundwa na sharia ya Muhammad (s.a.w), giza la kukosekana utawala na ukatili wa kutokuwa na dini katika maadili na maisha kunatisha zaidi kuliko Yaajuaja na Maajuja vimeanza kuharibu na kuibuka.

Kama katika zama za masahaba wa mtume (s.a.w), wakati ambapo matendo madogo yalikuwa ni sababu ya malipo makubwa inshaAllah, mapamabano ya kimaadili na kiroho ya wanafunzi wa Risale-i Nur katika mazingira kama haya yatakuwa ni sababu ya kazi nzuri na malipo makubwa.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.