MADA YA PILI KUTOKA KITUO CHA TATU KATIKA (NENO LA THALATHINI NA MBILI) SIRI YA UOVU WA MPOTEVU NA WEMA WA MUUMINI

Mwakilishi wa watu wa upotevu na mlinganiaji wake, kama hakupata cha kujengea upotevu wake, na anapokosa ushahidi, na kushindwa hoja, husema: Mimi naona kwamba furaha ya dunia, na kustarehe na ladha ya maisha, na maendeleo na ustaarabu, na maendeleo ya kiviwanda, ipo katika kutokukumbuka Akhera, na katika  kutokumuamini Allah (s.w), na katika kupenda dunia na katika kujikomboa kutokana na pingu na katika kuijali nafsi na kupendezwa nayo, kwa ajili hiyo nimewachunga wengi ya watu na sijaacha kuwa ninawachunga – kwa hima ya shetani – kuelekea njia hii.

Jawabu:

Nasi kwa upande wetu tunasema -kwa jina la Qur’an tukufu- ewe Mwanaadamu mwenye hali mbaya! Rejea kwenye busara yako, usimsikilize mlinganiaji wa watu wa upotevu. Kama utamtegea sikio itakuwa hasara yako, hasara ambayo roho akili na moyo hutetemeka kutokana na kutisha kuifikiria kwake, hivyo mbele yako kuna njia mbili:

Ya Kwanza:

Ni njia ya uovu ambayo anakuonesha mlinganiaji wa upotevu.

Ya Pili:

Ni njia ya mafanikio ambayo inakubainishia Qur’an tukufu.

Na kwa hakika umeona nyingi katika mizania kati ya njia hizo mbili katika sehemu nyingi za (Maneno) na hasa katika (Maneno madogo) na sasa kwenda sawa na mada zingatia katika moja wapo kati ya maelfu ya malinganisho na vipimo na uyazingatie, nayo:

Hakika njia ya shirki, upotevu, ujinga, na uasi humporomosha mwanaadamu katika ukomo wa anguko na katika chini ya walio chini, na kuweka juu ya mgongo wake dhaifu wenye kushindwa katika giza la maumivu yasiyo na mipaka mzigo mzito hauna mwisho wa uzito wake, na hii ni kwa kuwa Mwanaadamu kama hakumjua Allah (s.w), na kama hakumtegmea, anakuwa kama mnyama mwenye kutoweka anapata maumivu daima na kuhuzunika kwa kuendelea, na kupinduka pinduka katika kushindwa na udhaifu visiokuwa na mwisho, na kufululiza katika haja na ufakiri visivyo na kikomo, na kukutana na masaibu yasio na mpaka, na kuonja maumivu ya utengano kutoka kwa yule aliyempenda na kufuma kati yake na yeye nyuzi za mahusiano, anaumia – na haachi kuumia – mpaka awaache waliyobakia katika wapendwa wake mwisho wa mzunguko na kufarikiana nao akihuzunika mpweke mgeni kuelekea katika aina kwa aina za giza la kaburi.

Na ataikuta nafsi yake muda wote wa uhai wake mbele ya maumivu na matumaini yasiokuwa na mwisho, naye hamiliki isipokuwa matakwa ya sehemu tu, (irada juz’iyyah) uwezo mdogo, uhai mfupi, umri wenye kutoweka na fikira yenye kufifia, basi juhudi zake katika kuituliza zinapotea bure, na kwenda patupu nyuma ya matakwa yake yasiokuwa na mipaka. Na namna hii uhai wake unapita pasi na kuvuna matunda. Na zama unapomuona kuwa ni mwenye kushindwa, kubeba mizigo ya nafsi yake, utaona anaubebesha mgongo na hima yake masikini mizigo mikubwa ya dunia, hapo anateseka mateso ya kuunguza na kuumiza kabla ya kufika katika adhabu ya jahiim.

Hakika watu wa upotevu hawahisi maumivu haya machungu na adhabu ya kiroho ya kutisha, kwani nafsi zao wanazitupa vifuani mwa mghafala ili wabatilishe hisia zao na kuzitia ganzi hisi zao kwa muda kwa ulevi wake.Lakini muda mfupi tu mmoja wao anapokaribia ukingoni mwa kaburi tahamaki hisi zake zinashika kasi na hisia zake huongezwa kwa maumivu haya mkupuo mmoja, hii ni kwa sababu kama hakua mja mwenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Atadhani kwamba yeye ni mmiliki wa nafsi yake, pamoja na kuwa yeye ni mwenye kushindwa kwa utashi wake wa kisehemu, (irada juz’iyyah) na uwezo wake mdogo, hata katika kujiendesha yeye mwenyewe peke yake mbele ya hali za dunia hii zenye kupiga, kwani anaona ulimwengu wa maadui unamzunguka kuanzia kwenye vijidudu vidogo vya kueneza maradhi na kuishia katika matetemeko yenye kuteteketeza wakiwa katika maandalizi timamu ya kumshambulia na kumaliza uhai wake hapo viungo vyake vinatetemeka na moyo wake unatetemeka kwa woga na kufazaika kila anapofikiria kaburi na kulianagalia.

Na wakati ambapo Mwanaadamu huyu anaumia kutokana na hali yake wakati huo huo hali mbali mbali za dunia humtopeza daima, na wakati huo hali za wanadamu anaoungana nao zinamchosha daima, na hii  kwa dhana yake kwamba matukio haya yanatokana na mchezo wa na laabu ya maumbile na sadifa, na sio kutokana na utendaji wa Mmoja wa pekee Mwingi wa hekima Mjuuzi, na wala sio kwa makadirio ya  Muweza Mwingi wa rehama mwenye kurehemu Mkarimu sana, hivyo huugulia pamoja na maumivu yake maumivu ya watu wengine vilevile, matetemeko, tauni, tufani, ukame, ughali, kutoweka, kuondoka na mfano wa hayo huwa masaibu yenye kutokea na mabalaa yenye kuhangaisha na kutesa.

Basi Mwanaadamu huyu ambaye amejichagulia mwenyewe hali hii ya kutisha, hasababishi huruma ya kusikitikiwa, mfano wake katika hili kama mfano uliotajwa katika malinganisho kati ya ndugu wawili (katika neno la nane) kwamba mtu ambaye hakukinai na ladha halali na furaha safi na maliwazo mazuri na matembezi matukufu ya halali, kati ya wapendwa wazuri katika bustani yenye hewa nzuri kati ya ugeni mtukufu, akawa antumia pombe ya najisi apate ladha isiyo ya halali, akalewa hata akaanza kuoneshwa katika mawazo yake kwamba yuko mahali pachafu na kati ya wanyama washambuliaji, anapatwa na kutetemeka kama yupo kwenye majira ya baridi kali, akaanza kupiga kelele ya kuita msaada na hakuna aliyemuhurumia, kwa sababu yeye ameleta taswira wale marafiki wema kuwa ni wanyama wakali akawadharau na kuwadhalilisha. Na vyakula vitamu na vyombo visafi ambavyo vipo katika ukumbi wa ugeni akafikiria kuwa ni mawe yaliyochafuliwa na kuanza kuvivunjavunja. Na vitabu vya thamani na risala adimu zilizopo kwenye baraza alidhani ni nakshi za kawaida na mapambo yasiyo na maana, akaanza kuvichana na kuvitupa chini miguuni. Na kama hivi.

Basi kama mtu huyu na wengine kama yeye wasivyokuwa wenye kustahiki kuhurumiwa wala kustahiki kusikitikiwa kwa upole bali anawajibika kutiwa adabu na kupatilizwa na ndivyo hali ilivyo kwa mtu ambaye anadhani kwa sababu ya ulevi wa ukafiri na wazimu wa upotevu vinavyotokana na uchaguzi wake mbaya, dunia ambayo ni nyumba ya wageni ya mtengenezaji Mwingi wa hekima, yeye ameifanya kuwa ni mchezo wa sadifa pofu, na mchezo wa maumbile butu na anafanya taswira kupatisha upya vililivyoundwa kwa udhirisho wa majina mazuri, na kuvuka kwake kwenda kwenye ulimwengu usioonekana pamoja na mkondo wa muda baada ya kumaliza majukumu yake na kwisha malengo yake, kana kwamba vinamiminwa kwenye bahari ya kutokuwepo, na bonde la kukosekana na kupotea katika fukwe za kutoweka. Na anafikiri sauti za tasbihi na tahmiid ambazo zinazojaa ulimwenguni kuwa ni manung’uniko na kelele wanazozitoa wakuondoka na kutoweka katika utengano wao wa milele na anadhani kurasa za vilivyomo ambazo ni barua za kiungu mkusudiwa kwa kila haja zenye kupendeza, ni mchanganyiko usiokuwa na maana yoyote wala faida na anafikiri mlango wa kaburi ambao unafungua njia kwenda kwenye ulimwengu wa rehema uliompana kuwa ni handaki linalopelekea kwenye aina ya giza la hali ya kutokuwepo. Na anadhani ajali ambayo ni wito wa kuungana na kukutana kwa wapenzi wa kweli ni muda wa kutengana kwa wapenzi wote.

Naam. Hakika mtu ambaye anayeishi katika hali hii ya taswira hizi na dhana anajiingiza katika mateso ya dunia yaumizayo, basi ukiachilia mbali kuwa yeye kutokuwa mstahiki wa kuhurumiwa na kusikitikiwa, bali anastahiki adhabu kali, kwa kule kudharau kwake viumbe, kwa kuvituhumu kuwa vipo kwa mchezo, na kwa kupotosha kwake majina mazuri, kwa kukana kudhihiri kwake, na kukukana kwake barua za kiungu kwa kukata ushahidi wake juu ya upweke.

Basi enyi wapotevu wapumbavu, na enyi wahasirika waovu! Mnaona kwamba je, elimu zenu zinafaa kitu, na juu ya majengo makubwa ya ustaarabu wenu, na vyeo vya juu sana vya umahiri wenu na umaridadi wa mipango ya werevu wenu – vinafaaa kitu chochote mbele ya huku kudondoka kunakotisha kwa Mwanaadamu? na je,anaweza kusimama imara mbele ya huku kukata tamaa kunakoteketeza roho ya wanadamu yenye kupenda sana kupata maliwazo? na je yanaweza mnayoyaita  (maumbile) kwenu, na mnazoziegemezea athari za kiungu katika (sababu) kwenu, na mnazozinasibishia mema ya kiungu katika (mshirika) kwenu, na mnayojifaharisha nayo kati (vumbuzi zenu) na mnaojivunia nao miongoni mwa (watu wenu) na mnvyoviabudu katika (muabudiwa wenu) batili, je, wote hao wanaweza kuwaokoeni kutokana na giza aina kwa aina la kifo ambacho ni kunyongwa kwa milele kwenu? na je wote hao wanaweza kuwapitisheni katika mipaka ya kaburi kwa usalama na katika hadidu za kizuizi kwa amani? na katika medani ya ufufuo kwa utulivu? na kuweza kuwasaidieni kuvuka daraja la sirata sawa sawa, na kuwafanya wenye kustahiki furaha ya milele na maisha ya milele?

Hamna namna mtapita katika njia hii, kwani sio uwezo wenu kuufunga mlango wa kaburi kwa mtu yeyote. Hivyo nyinyi ni wasafiri wa njia hii hakuna kimbilio. na mtu apitaye kwenye njia hii hulazimika ajiegemeze na kufanya tawakkul kwa mwenye ujuzi wakuzungukia kila jambo unaenea kwa kila njia zake na matawi yake na mipaka yake mipana. Bali duru zote hizo kubwa ziwe chini ya utendaji wake na ndani ya amri yake na hukumu yake.

Basi enyi wapotevu wenye kughafilika! Hakika kilichowekwa katika maumbile yenu, katika utayari wa mahaba na ujuzi, na katika sababu za shukurani na njia za ibada ambazo zinabidi zifanywe kuelekezwa kwa dhati ya Allah (s.w), na yapasa zielekee kwenye sifa zake tukufu na majina yake mazuri, nyinyi mmezipa – upaji usio wa halali- kwa ajili yenu na kwa ajili ya dunia, basi mnapata adhabu yake kwa kustahiki, na hii ni kwa siri ya kanuni: (Hakika matokeo ya mapenzi yasiyo ya halali ni kuumizwa na adhabu pasipo na huruma). Kwa sababu nyinyi mmezipa nafsi zenu mahaba ambayo yanamhusu Allah (s.w), hivyo mnapata taabu za mabalaa ya mnaowapenda pasipo idadi, pale ambapo hamkuzipa raha zake za kweli, na hivyo hivyo hamsalimu amari yake kwa kumtegemea mahbubu wa haki naye ni Allah (s.w) Muweza wa kila jambo bila mipaka, hivyo mnapata maumivu daima. Na kama hivyo mmeipa dunia mapenzi ambayo yanarejea kwenye majina ya Allah (s.w), na sifa zake tukufu takatifu. Na mkagawa athari za ufundi wake na kuweka mafungu baina ya sababu za kimaada, basi mnaonja shida ya amali yenu, kwa sababu sehemu ya wapendwa wenu wengi wanakuacheni wakirejea pasipo kuaga, na kati yao wale wasiokujueni kamwe, na hata wakikujueni hawakupendeni, na hata wakikupendeni hawakufaeni kitu, basi mnabaki ndani ya adhabu ya kudumu miongoni mwa adhabu za utengano usio na mpaka na katika maumivu ya kutoweka kwa kukata tamaa ya kurejea.

Huu ndio ukweli wa wanayodai watu wa upotevu, na kiini cha wanacholingania katika (furaha ya maisha) na (ukamilifu wa Mwanaadamu) na (mazuri ya usataarabu) na (ladha ya kujiweka huru) !!

Ehe! Uzito ulioje wa pazia la upumbavu na ulevi unaotia ganzi fahamu na hisi!

Ehe! Sema: Maangamio kwa akili ya hao wapotevu!

Ama njia iliyonyooka au njia yenye nuru ya Qur’an, inatibu majeraha yote ambayo watu wa upotevu wanateseka nayo na kuyaagua kwa hakika za kiimani, na kuteketeza viza vyote vilivyotangulia kwenye njia hiyo na kufunga njia zote za upotevu, na maangamio kwa kutumia yafuatayo:

Hakika inatibu udhaifu wa Mwanaadamu, kutojiweza kwake, ufakiri wake, na mahitajio yake kwa kumtegemea Muweza wa kila kitu Mwingi wa rehema, hali ya kusalimisha mazito ya maisha na majukumu ya kuwepo kwa uweza wake (s.w), na kwa rehema zake kunjufu, bila ya kuyabebesha mgongoni mwa Mwanaadamu. Bali anamfanya mwenye kumiliki hatamu ya nafsi yake na uhai wake mwenye kupata kwa hivyo makamo ya kustarehesha na kumtambulisha kuwa sio mnyama mwenye kufikiri, bali yeye ni Mwanaadamu kwa hakika na mgeni mwenye heshima na kutukuzwa mbele ya Mfalme Mwingi wa rehema.

Inatibu pia yale majeraha ya kibinaadamu yatokanayo na kutoweka kwa dunia na kuondoka kwa vitu, na kutokana na kupenda vyenye kumalizika inayatibu kwa upole na huruma kwa kumuonesha kuwa dunia ni nyumba ya ugeni ya Mwingi wa rehema na kubainisha kwamba vilivyomo kati ya viumbe ni vioo vya majina mazuri, na hali ya kuweka wazi kwamba vitengenezwa vyake ni barua za kiungu zinzokuwa upya kila zama kwa idhini ya mola wake, na hivyo kumuokoa Mwanaadamu kutokana na kubanwa na magiza ya dhana.

Na inatibu pia yale majeraha ambayo yanaachwa na umauti ambayo  watu wa upotevu wanayapata kuwa ni utengano wa milele na  wapendwa wote, kwa kubainisha kuwa umauti ni utangulizi wa kuungana na kukutana pamoja na wapenzi ambao walisafiri kwenda kwenye ulimwengu wa kizuizi, na ambao wao hivi sasa wako katika ulimwengu wa kubakia, na inathibitisha kuwa huko kutengana ni hasa kukutana.

Na pia inaondosha hofu kubwa ya Mwanaadamu kwa kuthibitisha kwamba kaburi ni mlango uliofunguliwa kuelekea katika ulimwengu wa rehema kunjufu, na katika mji wa furaha ya kudumu milele , na katika bustani za pepo na katika miji ya nuru ya Al-rahamani Al-rahiim, kwa kubainisha kuwa matembezi ya kizuizi ambayo yana maumimivu makali mno na matembezi yenye tabu zaidi kwa watu wa upotevu ni matembezi ya starehe zaidi na yenye kuliwaza na kufurahisha zaidi kwani kaburi sio mdomo wa nyoka wa kutisha bali ni malango kuelekea katika bustani miongoni mwa bustani za Janna.

Na inamwambia muumini: Kama utashi na hiyari yako ni ya kisehemu (juz ‘iyyah) basi salimisha mambo kwa utashi wa mola wako wenye sifa ya kuenea kila kitu. Na kama uweza wako ni dhaifu basi tegemea juu ya uweza wa Muweza bila kikomo. Na ikiwa uhai wako ni wa kutoweka na mfupi basi fikiria uhai wa kubakia wa milele, na ikiwa umri wako ni mfupi basi usihuzunike kwani unao umri mrefu, na kama fikira yako ni fifi basi ingia chini ya nuru ya jua la Qur’an tukufu na tazama kwa kutumia nuru ya imani ili kila aya katika aya za Qur’ani tukufu ikupe nuru kama nyota zinazomeremeta, zenye kuangaza badala ya fikira zako zenye kushindwa. Na ukiwa na maumivu na matarajio yasiokuwa na ukomo hakika thawabu isiokuwa na ukomo na rehema zisizo na ukomo zinakusubiri na kama una malengo na makusudio yasiokuwa na mipaka usitaabike kufikiria kwani hapa duniani havidhibitiki, bali mahali pake ni katika mji mwingine, na mpaji wake ni mwema Mkarimu mno, mkunjufu wa kutoa.

Inamsemesha Mwanaadamu tena na inasema: Ewe Mwanaadamu! Wewe sio mmiliki wa nafsi yako, bali wewe umemilikiwa na Muweza mwenye uwezo usiokuwa na ukomo, na Mwingi wa rehema isiokuwa na ukomo. Usiitaabishe nafsi yako kwa kuibebesha mashaka ya uhai wako, hakika aliyetoa uhai ndiye anayeuendesha.

Kisha dunia sio hame lisilo na mwenyewe, hata uwe na wasiwasi nayo, na kujikalifisha nafsi yako kubeba mizigo yake na kuichosha fikra yako katika hali za hiyo dunia. Hii ni kwakuwa mmiliki wake ni Mwingi wa hekima na mola wake ni mjuzi wa kila kitu, na wewe sio ila ni mgeni  katika hiyo dunia basi usiingilie kwa kuvuka mipaka katika mambo, na wala usiyachanganye bila fahamu.

Halafu Mwanaadamu na mnyama sio viumbe waliopuuzwa, bali ni wenye kupewa wadhifa na kuamuriwa chini ya utawala wa Mwingi wa hekima, Mwingi wa rehema, na chini ya uangalizi wake. Roho yako usiitatize kwa maumivu kwa kufikiria katika mashaka ya hao na maumivu yao wala usitangulize huruma yako juu yao mbele ya huruma ya Muumba wao Mwingi wa rehema.

Kisha hakika hatamu ya hao ambao wamechukua hatua ya uadui na wewe, kuanzia vijidudu hadi tauni, tufani, na ukame, na matetemeko bali hatamu ya kila kitu iko mkononi mwa huyo Mwingi wa rehema, Mkarimu (s.w). Yeye ni Mwingi wa hekima kwake hakutokei mchezo, naye ni Mwingi wa rehema mkunjufu wa rehema kila anachokifanya kuna athari ya upole na huruma yake.

Na inasema vilevile: Hakika ya huu ulimwengu japokuwa ni wa kutoweka, unaanda mahitaji ya ulimwengu wa milele, pamoja na kuwa ni wa kutoweka na wa muda mfupi isipokuwa unaleta matunda ya kudumu, na unaonesha madhihirisho mazuri katika madhihirisho ya majina mazuri ya kudumu milele, pamoja na kuwa ladha zake ni chache na maumivu yake ni mengi, isipokuwa mazuri ya Mwingi wa rehema mwenye kurehemu na ukarimu wake na ufadhili wake zenyewe ni ladha za kikweli kweli hazitoweki, ama maumivu nayo pia huzalisha ladha za kimaanawi kwa upande wa thawabu za kiakhera. Madamu duara la halali linatosha kwa kuchukua vyote roho, moyo, na nafsi ladha zake na furaha zake kwa pamoja. Kwa hiyo hapana haja kuingia katika duara la haramu kwa sababu ladha moja katika duara hili, inaweza kuwa na maumivu elfu moja na moja , ukiachilia mbali kuwa hiyo ni sababu ya kuzuiliwa kwa ladha ya takrima ya Mwingi wa rehema, Mkarimu ile ladha safi iliyotakata ya kudumu milele na milele.

Kama hivi kutokana na yaliyotangulia imebainika: Kwamba njia ya upotevu humtupa mwanaadamu kwenda chini ya walio chini, kwa kiwango ambacho ustaarabu wowote unashindwa na falsafa yeyote iweyo kuweza kuleta ufumbuzi wake, bali maendeleo ya kibinaadamu na kiasi alichofikia cha ngazi za kielimu kuweza kumuondoa kutoka katika giza hilo nene katika upotevu.

Wakati ambapo Qur’an tukufu inamshika mkono Mwanaadamu, kwa imani na amali njema, na kumnyanyua kutoka chini ya walio chini na kumpandisha juu ya walio juu, na kumbainishia dalili zenye kukata hoja  na kukunjua dalili zenye nguvu juu ya hayo mbele yake, na kufukia hayo mahandaki ya kina kwa ngazi za maendeleo ya kimaanawi na kwa vifaa vya muungano wa kiroho, na kama hivi inamrahisishia kwa wepesi bila kikomo safari yake ndefu ya kuchosha yenye kupiga, inayokwenda kwa kasi kuelekea umilele, na kumrahisishia, na hiyo kwa kudhihirisha nyenzo na vitendea kazi ambavyo anaweza kuvitumia kukata masafa ya miaka elfu, bali miaka hamsini elfu, ndani ya siku moja.

Na namna hii humfunika Mwanaadamu joho la utumwa na kumpatia  hatua ya mja muamuriwa, na mgeni mfanya kazi mbele ya dhati tukufu,  na hii kwa kumjulisha kwamba Allah (s.w), ndie mmiliki wa azali na  milele, na kumdhaminia raha kamili katika utalii wake duniani katika hali ya ugeni au katika nyumba za kwenye vizuizi na miji ya Akhera. Na kama alivyo mfanya kazi muaminifu kwa mfalme anatembea kwa  wepesi kamili, katika duara la mamlaka ya ufalme na anatembea katika mipaka ya utawala wake kwa vyombo vya usafiri wa haraka kama ndege, meli, na treni, hivyo hivyo Mwanaadamu ambaye anajinasibisha na imani kwa mmiliki wa kiazali anapita na amali njema kutoka katika nyumba za dunia za ugeni na katika miji ya ulimwengu ya kizuizini na ufufuo na kutoka katika mipaka yake, mikunjufu yenyen kuenea kwa wepesi wa umeme na buraki hata apate furaha ya milele. Qur’an tukufu inathibitisha hakika hizi uthibitisho wa kukata hoja na kuyaonesha waziwazi kwa wateule na mawalii.

Halafu hakika yake inaendelea kwa kusema: Ewe Mwanaadamu usipoteze unachomiliki katika ukubalifu usio na mipaka kwa ajili ya kupenda nafsi yako ambayo ni yenye kuamuru sana maovu, nayo ni mbaya, pungufu yenye shari na yenye kudhuru, wala usimfanye mpendwa wako wala usiabudu matamanio yake, bali mfanye mpenzi wako ambaye anastahiki mapenzi yasokuwa na ukomo, huyo ni Muweza wa kukufanyia hisani, hisani ambayo isiokuwa na ukomo, na Muweza wa kukufanya ufurahi furaha ambayo haina kikomo bali atakufurahisha tena kwa hisani zake anazotoa kwa wote ambao unafungamana nao kwa mahusiano, yeye ndiye ambaye mwenye ukamilifu usiokuwa na ukomo na uzuri mtakatifu na alioepukana na upungufu na kasoro na kuondoka na kumalizika. Uzuri wake hauna mipaka na majina yake yote ni mazuri.

Naam, hakika katika kila jina miongoni mwa majina yake kuna nuru za kupendeza na uzuri zisizokuwa na ukomo, kwa hiyo pepo na mazuri yake yote, urembo wake, na neema zake, hakika hiyo si jambo lingine isipkuwa ni udhihirisho kwa ajili ya kudhihirisha uzuri wa rehema yake na rehema ya uzuri wake, na urembo na uzuri wote, mazuri na makailfu yenye kupendwa na yenye kupendezeshwa katika ulimwengu wote, hiyo sio bali ni ishara ya uzuri wake na dalili ya ukamilifu wake (s.w).

Na inasema tena: Ewe Mwanaadamu! hakika chemchemu za mahaba zenye kupasuka kwenye kina cha ndani yako na zenye kuelekea kwa Allah (s.w), na zenye kuamabatana na majina yake mazuri, na zenye kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake tukufu, usizifanye zitumike katika kushikamana na viumbe vyenye kutoweka na wala usizipoteze bure bila faida, kwa viumbe vyenye kuondoka, hiyo ni kwa sababu athari na viumbe ni vyenye kuondoka, wakati majina mazuri yenye kuonesha udhihirisho wake na uzuri wake kwa athari hizo na hivyo vilivyoundwa, ni yenye kubaki daima. Katika kila jina miongoni mwa majina mazuri ya Allah (s.w), na katika kila sifa miongoni mwa sifa takatifu kuna maelfu ya ngazi za hisani na uzuri na maelfu ya tabaka za ukamilifu.

Tazama jina (Al-rahman) tu, upate kuona kwamba pepo ni moja ya madhihirisho yake na furaha ya milele ni moja ya miale yake, na riziki zote na neema zilizotawanywa kote pande za dunia ni moja ya matone yake.

Tazama kwa makini sana na uchunguze aya tukufu ambazo zinaashiria vipimo hivi kati ya hakika ya watu wa upotofu na watu wa Imani kwa upande wa uhai na upande wa jukumu:

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ۞ ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ۞ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ Qur’an, 95:4-6

Na aya nyingine ni:

فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاء وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ Qur’an, 44:29

Aya hizi zinaashiria mwisho wa kila mmoja kati ya makundi mawili hayo. Zichunguze utaona kiasi cha ukuu wake na miujiza yake katika kubainisha tuliyoyataja katiaka vipimo na malinganisho.

Ama aya za mwanzo tunarejesha kubainisha hakika ya maana yake iliyomo ya miujiza kwa ufupi kwenda katika (Neno la kumi na moja) ambayo inafafanua kwa uwazi kabisa. Ama aya ya pili tutaashiria -ishara moja tu- kiasi cha kutoa kwake maana ya ukweli mkuu nayo ni kama ifuatavyo.

Zinasema kuwa: Hakika mbingu na ardhi havilii kwa kifo cha watu wa upotevu. Na kwa maana ya kinyume chake ni kuwa mbingu na ardhi vinalia kwa kuondoka duniani kwa watu wa imani. Yaani kwa kuwa watu wa upotevu wanakanusha majukumu ya mbingu na ardhi na kuvituhumu kwa mchezo na hawatambui maana ya majukumu yonayotekelezwa na mbingu na ardhi. Kwa hiyo wanadhulumu haki za mbingu na ardhi. Bali hawamjui Muumba wake wala dalili za juu ya Muumba wake (wa mbingu na ardhi) wanazidharau na wanazishikia msimamo wa uadui kuzidunisha na kubeza, hapana budi kwa mbingu na ardhi kutotosheka na kutokuwalilia tu, bali pia kuwaombea dua mbaya na kustarehe kwa kuanagamia kwao. Na inasema vilevile kwa maana tofauti: Hakika mbingu na ardhi zinalia kwa ajili ya kufa kwa watu wa Imani, kwa sababu wao wanajua majukumu ya hizo mbingu na ardhi na kuzithamini ukweli wa kuzithamini, na wanakubali kweli zake za hakika na wanafahamu kupitia imani umuhimu na maana yake yanayopatikana, kwani kila wanapozingatia na kuzichunguza husema kwa mshangao: “uzuri ulioje wa kuumbwa kwake!” Na “uzuri ulioje wa majukumu yanayotekelezwa na mbingu na ardhi!” Hivyo huzipa thamani na heshima zinazostahiki na kueneza mapenzi kwa hizo mbingu na ardhi kwa kumpenda Mwenyezi Mungu, yaani kwa ajili ya Allah kwa kuzizingatia kuwa ni vioo vya kudhihirishia majina mazuri ya Allah. Kwa ajili hii mbingu hutetemeka na ardhi kuhuzunika, kwa ajili ya umauti wa watu wa imani kana kwamba zinalia kwa ajili ya kutoweka kwao.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.