NJIA YA KUHIFADHI UZURI

Inafahamika kutokana na masimulizi ya Hadithi ya hakika kuwa jambo baya katika mfarakano wakati wa zama za mwisho litakuwa wanawake na fitina zao. Ndiyo, kama ilivyosimuliwa katika historia kuwa hapo zamani, kundi la wanajeshi lililokuwa na wanawake mashujaa walioitwa Waamazoni walikuwa mahiri vitani, hivyo kwa namna hiyo hiyo kwa wakati huu, kundi linaloogopesha zaidi katika vita vya upotovu wa ukanaji Mungu dhidi ya Uislamu, ambapo ukuu wake amepewa Shetani kupitia amri mbaya za nafsi iamrishayo maovu, ni wanawake walio nusu uchi, ambao kwa miguu yao mitupu –visu hivyo vya kuua– wanawashambulia waumini. Kwa kujitahidi kufunga njia ya kuelekea kwenye ndoa na kupanua njia za kuelekea kwenye nyumba za ufisadi, wanazikamata mateka roho za watu wengi na kujeruhi nyoyo na roho zao kwa dhambi kubwa. Kwa hakika, huua baadhi ya nyoyo hizo.

Kama adhabu stahiki kwa kuwaonesha maono yenye kutamanisha ya wale ambao kisheria ni wageni, miguu ile iliyo kama kisu inakuwa magogo ya kuwashia kuni za Jahanamu na watakuwa wa mwanzo kuchomwa. Na kwakuwa wanawake hao wamepoteza madai yao ya kutumainiwa na kuaminiwa humu duniani hawawezi tena kupata waume bora, ambao kwa hali zao halisi wanawataka na wanawahitaji sana. Hata kama watawapata, itawaletea taabu tu. Inafahamika kutoka katika Hadithi kuwa kutokana na hali hii, katika zama za mwisho kwa sababu ndoa haitakuwa ikichungwa wala kutunzwa katika baadhi ya maeneo, wanawake watapoteza hadhi yao kwa kiasi kwamba mtu mmoja atakuwa akiwahifadhi wanawake arubaini.

Imepokewa kutoka kwa Anas r.a amesema: Hakika nitakusimulieni hadithi hatakusimulieni yeyote baada yangu, nimemsikia mjumbe wa Allah (s.a.w) anasema: “Miongoni mwa alama za kiama kupungua elimu, kudhihiri zinaa, kukithiri wanawake, na kuwa wachache wanaume hata iwe hamsini ni kwa msimamizi mmoja” Al-Bukhary kitab al- Ilm. Mlango wa Raf’u al-Ilm wa dhuhuuru al-Jahl.

Kwakuwa ukweli wa jambo hilo ni huu: na kwa kuwa kila mzuri anapenda uzuri wake na anataka kuuhifadhi kadiri awezavyo na hataki uharibiwe, na kwa kuwa uzuri ni neema na kwa kuwa neema ikishukuriwa inaongezeka, ilhali kama haitashukuriwa inabadilika na kuwa mbaya, kwa hakika kama mtu wa namna hiyo ni mwenye akili, atakimbia kwa nguvu zake zote kutoka katika kutenda madhambi, na kuufanya uzuri na kupendeza kwake kutenda dhambi, na kuufanya uwe mbaya na wenye sumu, na kwa kukosa shukrani kuugeuza uzuri huo kuelekea katika jambo linalopelekea kwenye adhabu. Na kwa ajili ya kuudumisha ukimbiaji wake kwa uzuri wa miaka mitano au kumi, ataushukuru uzuri kwa kuutumia katika halali. Vinginevyo katika kipindi kirefu cha uzee wake, atasukumwa mbali na atalia katika hali ya kukata tamaa.

Kama uzuri wake utafanywa mzuri kwa kupambwa na tabia na maadili ya Qur’an katika nyanja za mafunzo ya Kiislamu, uzuri wake wa mpito utageuka kuwa wa milele na peponi atapewa uzuri zaidi na wenye kung’aa kuliko wa Mahurulaini, kama ilivyoelezwa kwa hakika katika Hadithi kadhaa.

Kwenye mlango huu kuna hadithi nyingi kati ya hizo: Kutoka kwa Ummu Salamat mke wa mtume (s.a.w) amesema: (Katika hadithi ndefu) nimesema: Ewe mjumbe wa Allah je, wanawake wa duniani ni bora au mahurulaini? Akasema: Wanawake wa duniani ni bora kuliko mahurulaini kama ubora wa nguo ya nje kwa ya ndani. Nikasema: Ewe mjumbe wa Allah na kwanini wawe hivyo? Akasema: Kwa swala zao na swaumu zao na kumuabudu kwao Allah (s.w). Allah (s.w) amezivika nyuso zao nuru na viwiliwili vyao hariri, wana rangi nyeupe, nguo za kijani, mapambo ya manjano… n.k. Al-Tabarany, Al-Muujam al- Kabir.

Kama mzuri wa namna hiyo ana akili hata chembe, hataruhusu uzuri huu, ung’aaji na matokeo ya milele yaponyoke kutoka mkononi mwake. 

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.