NUKTA YA KITAWHIID KATIKA LAFUDHI (HUWA)

Kwa Jina Lake, (s.w)

Na hakuna kitu, bali humtukuza Yeye na kumsifu.

Ndugu zangu wapendwa!

Ndugu zangu, nimeangalia kwa matazamo wenye kupambanua kuhusu Umoja wa Allah, ambao ghafla ukawa dhahiri wakati nilipokuwa nikisoma ukurasa wa hewa katika safari ya kufikirika na kiakili, yaani, katika neno YEYE (HU) lililo katika maneno

لآ إلَهَ إِلَّا هُو

na

قُلْ هُوَاللهُ أَحَد

(na hiyo ilikuwa tu katika upande wa kimaada) kuwa njia ya imani ni rahisi kabisa, rahisi kiasi cha kuwa lazima, na kuwa njia ya upotovu na kumshirikisha Allah ni ngumu mno, ngumu mno kiasi cha kushindikana. Nitaieleza nukta hiyo ndefu na pana kwa ishara fupi sana.

Ndiyo, kama udongo, kiasi cha kujaa kwenye mikono unaweza kuwa kama chungu cha maua cha mamia ya mimea inayowekwa mmoja baada ya mwingine, umeegemezwa kwa asili au sababu, inakuwa lazima ama kuwepo kwenye udongo huo mamia ya mashine za kimaana, bila ya shaka, mashine na viwanda kwa idadi ya mimea, au kwa kila punje ya kiasi hicho kidogo cha udongo kujua namna ya kufanya mimea yote hiyo mbalimbali pamoja na sifa zake tofauti na viungo hai; kwa ufupi, kila moja itapaswa iwe na elimu isiyo na kikomo na uwezo usio na mpaka kama Allah.

Kadhalika ni kweli kwa hewa, ambayo ni mahali pa udhihirisho wa juu wa Utashi na amri ya Kiungu; ama kutapaswa kuwepo katika kipimo kidogo katika kila moja ya sehemu zake ndogo, katika kila mpeperuko wa upepo, kila pumzi, na katika kiasi kidogo cha hewa inayotoka kwa kutamka neno Hu (Yeye), mabadilishano yasiyohesabika, vituo, vipokezi na visambazaji vya simu zote na redio duniani ili kila moja ya sehemu zake iweze kufanya kazi hizo nyingi katika wakati huo huo. Au kama si hivyo kila chembe ya kila sehemu ndogo ya hewa inayotoka kwa kutamka neno Hu, na kwa hakika ya kipengele hewa, itapaswa kuwa na uwezo na nafsi kwa idadi ya watumiaji wote wa simu za sauti, za maandishi, na wanaozungumza redioni, na kujua lugha zao mbalimbali, na kuzitangaza kwenye chembe zingine kwa wakati huo huo. Kwa hali hiyo kwa hakika iko dhahiri, na kila nukta ya hewa ina uwezo huo. Hivyo, katika njia za makafiri, wanaasili, na Wayakinifu, si muhali mmoja tu, bali mihali mingi iko dhahiri kwa idadi ya chembe ndogo za hewa.

Kama itarejeshwa sifa hiyo kwa Muumbaji (s.w), hata hivyo, hewa pamoja na chembe zake zote zinakuwa askari chini ya amri Yake. Kwa idhini ya Muumba wake na kwa uwezo Wake, na kwa kuunganika na Muumbaji Wake na kumtegemea Yeye, na kwa udhihirisho wa Uwezo wa Muumbaji wake, papo kwa papo kwa kasi ya radi, na kwa wepesi wa kutamka neno Hu na mtikisiko wa hewa katika mawimbi, majukumu yake mengi ya kuenea kote hufanywa kiurahisi kwa mpangilio kama shughuli moja ya chembe moja. Yaani, hewa inakuwa ukurasa wa maandishi yasiyo na ukomo, ya ajabu, na yaliyopangika ya kalamu ya Uwezo. Na chembe zake zinakuwa ncha za kalamu, na shughuli zao ni nukta zilizoandikwa nayo. Hewa inafanya kazi kwa urahisi kama mtikisiko wa chembe moja.

Na kwa hivyo, nikiwa katika safari yangu ya tafakuri iliyochochewa na fungu la maneno,

لآ إلَهَ إلَّا هُو

na

قُلْ هُوَاللهُ أَحَد

na nikiangalia dunia ya hewa na kusoma ukurasa wa kipengele hicho, ninashuhudia ukweli huu mfupi kwa uhakika kabisa, na kwa kina. Na ninafahamu kwa ‘Elimu ya yakini’ kuwa ilikuwa kwa sababu katika neno Hu, katika hewa ya utamkaji wake, kuna ushahidi huo mzuri na muale wa Umoja wa Kiungu, na pia katika maana yake na kudokezea dhihirisho angavu la Umoja wa Kiungu na ushahidi imara wa Upekee wa Kiungu, na katika ushahidi huo kuna ishara kuwa kwa kuwa neno Hu halijafungamana na kitu na halimlengi mtu, linapelekea kwenye swali, “Linamwakilisha nani?” Kuwa Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza na wale wenye kuendelea kusoma Majina ya Kiungu mara nyingi huwa wanakariri neno hili tukufu katika kituo cha Umoja.

Kwa hakika, kama, kwa mfano, kuna nukta moja katika karatasi nyeupe na nukta nyingine mbili au tatu zimechanganywa karibu yake halafu mtu mwingine ambaye tayari ana kazi nyingi anajaribu kuzitafautisha, atavurugikiwa; na kama mizigo mingi imepakiwa juu ya kiumbe mdogo, ataelemewa; na kama maneno mengi yanatoka katika ulimi mmoja na kuingia kwenye sikio moja kwa pamoja kwa wakati mmoja, mpangilio wao unaweza kuvurugika na yatakuwa vurugu.

Licha ya hali kuwa hivyo, niliona kwa hakika kabisa kwa ufunguo na dira ya Hu, ingawa maelfu ya nukta mbalimbali, herufi na maneno yamewekwa katika kila sehemu ndogo ya hewa na hata katika kila chembe ya kilicho katika hewa, ambapo kupitia humo nilisafiri kiakili, hazikuchanganyikana wala hazikuvuruga mpangilio wao; na ingawa zilifanya kazi kubwa nyingi tofauti tofauti, zilifanyika bila ya kuchanganyikana kwa namna yoyote; na ingawa mizigo mizito sana iliwekwa juu ya kila molekuli na chembe, zilibeba kwa pangilio bila ya kukawia wala kuonesha udhaifu wowote. Na niliona kuwa maelfu ya maneno ya namna tofauti yanaingia na kutoka kwa mpangilio kamilifu kutoka katika masikio madogo na midomo katika wakati huo bila ya kuchanganyikana kuharibika kwa hali yoyote, yanaingia katika masikio hayo madogo na kutoka katika ndimi hizo ndogo mno, na kwa kufanya kazi hizo za kimaajabu, kila chembe na kila molekuli inatangaza kwa ulimi mzuri sana wa hali na uhuru wake kamili, na kwa ushahidi na ulimi wa ukweli wa hapo juu:

لآ إلَهَ إِلَّا هُو

na

قُلْ هُوَاللهُ أَحَد

na kusafiri baina ya mawimbi ya kwenye hewa kama mvua na radi bila ya kuharibu mpangilio wao kwa namna yoyote au kuvuruga shughuli yao. Na kazi mojawapo si kizuizi cha kazi nyingine. Niliyaona haya na nikawa na hakika kabisa.

Hivyo ni kusema, ama kila chembe na kipande cha hewa kinapaswa kiwe na hekima isiyo na kikomo, elimu, utashi, na uwezo, na sifa za kuwa na kutawala bila ya shaka juu ya chembe zote zingine ili iweze kuwa njia ya kazi zote hizo kuweza kufanyika, jambo ambalo ni upuuzi na lisilowezekana kwa idadi ya chembe, na hakuna shetani ambaye hata anaweza kufikiri hilo, au mwingine, na inajitosheleza kihoja kwa kiwango cha elimu ya yakini, dhati ya yakini, na yakini kamili kuwa ukurasa wa hewa unafanya kazi katika elimu isiyo na mipaka wala ukomo na hekima ya Mmoja (s.w), na ni ukurasa unaobadilika wa kalamu ya Uwezo na Kudura ya Kiungu, na kama ubao wa kuandika na kufuta, unaojulikana kama Ubao wa Kutokeza na Kupotea, ambao una kazi ya ubao uliohifadhiwa katika dunia ya mageuzi na mabadiliko.

Hivyo, kama ambavyo kipengele cha hewa kinavyoonesha maajabu yaliyotajwa hapo juu na udhihirisho wa Umoja wa Kiungu katika jukumu la kusafirisha sauti tu na kuonesha mihali ya upotovu, hivyo pia inaweza kufanya kazi nyingine kwa mpangilio bila ya kuchanganya kama kupitisha nguvu kubwa, kama umeme, mwangaza, na nguvu za mvutano na ukinzani. Na wakati huo huo ikiyafikisha hayo, kwa mpangilio kamili, inafanya shughuli muhimu kwa ajili ya maisha ya mimea yote na wanyama, kama vile kupumua. Inathibitisha kwa mtindo mkataa kwamba ni mahali pa udhihirisho wa juu kabisa wa Utashi na Amri ya Kiungu. Nikafikia katika hitimisho imara kuwa inathibitisha kuwa kwa namna yoyote ile, hakuna fursa yoyote ya kubahatisha, nguvu yenye upofu, asili kiziwi, sababu zisizo na lengo, na jambo lisilo na uwezo, lisilo uhai, lisilojua linaloingilia katika kuandikwa na shughuli za ukurasa wa hewa. Na nimefahamu kuwa kila chembe na sehemu yake inasema kwa ulimi wa hili yake:

 لآ إلَهَ إلَّا هُو

na

قُلْ هُواللهُ أحَد

Na kama ambavyo kwa ufunguo wa Hu niliyaona maajabu haya katika upande wa kitu wa hewa, hivyo pia, kama ilivyo Hu, ndivyo kipengele hewa kinakuwa ufunguo wa dunia ya Mifanano na dunia ya Maana. Niliona kuwa dunia ya Mifanano kila mara inapiga picha zisizohesabika bila ya kuzivuruga, na kuwa kila picha ina matukio yasiyohesabika ya yanayotokea duniani. Nilifahamu kuwa ilikuwa kamera kubwa, na sinema pana ya akhera ambayo ni kubwa sana kuliko dunia kwa ajili ya kuonesha matunda ya hali za mpito na zisizo za kudumu na maisha ya viumbe wa mpito katika kumbi za milele, kwa ajili ya kuwaonesha wale wanaofurahia upeo wa furaha ya milele katika taswira za Peponi kutoka katika kumbukumbu zao za zamani na maisha yenye matukio ya duniani.

Wakati, mahali na hali haviruhusu hili kuthibitishwa kwa shuhuda na hoja imara kama ukweli dhahiri. Hivyo, tutaishia hapo.

 Wakati viungo katika kichwa cha mwanaadamu vya kumbukumbu na kufikiria, ambavyo ni shuhuda mbili, mifano miwili midogo, na nukta mbili za Ubao Uliohifadhiwa na ulimwengu wa Mfano, ni ndogo kama chembe ya haradali, ndani mwake kumeandikwa katika mpangilio kamilifu na bila ya kuchanganya kama habari nyingi zilizo katika maktaba kubwa. Hili linathibitisha kuwa mifano mikubwa ya vitivo hivyo ni ulimwengu wa Mfano na Ubao Uliohifadhiwa.

Ni hakika kabisa na hakuna shaka kwa elimu ya yakini kuwa vipengele vya hewa na maji, na hewa na maji hususani kama maji yenye kuchupa, ni bora sana kuliko kipengele cha ardhi, na vimeandikwa kwa hekima zaidi na utashi, na kwa kalamu ya Kudura ya Kiungu na Uwezo, na kuwa muhali kabisa kubahatisha, nguvu isiyoona, chanzo kiziwi, na sababu zisizo na malengo kuziingilia, na kuwa hizo ni ukurasa wa kalamu ya Uwezo na hekima za Mmoja  Mwingi wa Hekima (s.w).

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.