SHUHUDA ZA KUFUFULIWA WAFU

Mshale wa Tisana sehemu ya kwanza ya nyongeza muhimu kwenye Neno la Kumi

Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ ۞ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ۞ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذَلِكَ تُخْرَجُونَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاء مَاء فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ۞ وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاء وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ و۞َ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ۞ وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَى فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

Qur’an, 30:17-27

Katika Mshale huu wa tisa kutaelezwa kinagaubaga nukta tukufu ya aya hizi tukufu, zinazoonesha mojawapo katika ‘nguzo za imani; shuhuda hizi tukufu zenye nguvu za kufufuliwa wafu zitaelezwa. Ni msimamo pambanuzi wa rehema ya kimamlaka kuwa miaka thelathini iliyopita mwishoni mwa kazi yake iliyoitwa Muhâkamat (Utoaji hoja), ambayo iliandikwa ili kuweka kanuni za ufafanuzi wa Qur’an, Said wa zamani ameandika: “Kusudio la Pili: Aya Mbili za Qur’an zenye kudokezea ufufuo wa wafu zitafafanuliwa kinagaubaga. Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.” Akaishia hapo na hakuandika zaidi. Sasa, sifa na shukurani zimwendee Muumbaji Mwingi wa Rehema kwa idadi ya dalili na ishara za ufufuo, kuwa miaka thelathini baadaye Alinipa mafanikio ya kukamilisha hilo. Ndiyo, miaka tisa au kumi iliyopita, Ameneemesha neno la kumi na la Ishirini na Tisa, shuhuda mbili ng’aavu na zenye nguvu zinazodhihirisha hukumu ya Kiungu ya:

فَانظُرْ إِلَى آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذَلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَى وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ Qur’an, 30:50

ambayo ilikuwa aya ya kwanza kati ya mbili. Zikawanyamazisha wenye kukanusha ufufuo. Sasa, miaka tisa au kumi baada ya ngome mbili zisizopenyeka za kuamini ufufuo wa wafu, Ameneemesha kwa maandiko ya sasa ya sherehe ya aya mbili hizo tukufu hapo juu. Mshale huu wa Tisa, unajumuisha ‘Vituo’ tisa vya juu vilivyoashiriwa na aya zilizotajwa hapo juu, na Utangulizi muhimu.

UTANGULIZI

[Nukta mbili zenye kujumuisha maelezo ya muhutasari ya moja ya matokeo jumuishi ya manufaa mbali mbali ya kiroho ya kuamini ufufuo na matokeo yake muhimu; kuonesha umuhimu wake katika maisha ya mwanaadamu na hususani kwa uzima wa jamii; muhutasari wa ushahidi mmoja wenye kuenea kutoka miongoni mwa shuhuda nyingi za itikadi ya kuamini ufufuo wa wafu; na kauli ya jinsi isivyo na shaka na yenye kujionesha wazi itikadi hiyo ya imani.]

NUKTA YA KWANZA

Tutaonesha, kama kipimo, nne tu kati ya mamia ya shuhuda kuwa kuamini akhera ni msingi kwa maisha ya jamii na ya mtu binafsi, na pia ni msingi wa furaha yake, ustawi, na mafanikio.

Mosi:

Ni kwa fikra ya Pepo ambapo watoto, wanaounda takribani nusu ya wanaadamu, wangehimili vifo vyote baina yao, vinavyoonekana kwao kuwa huzuni na vyenye kutisha, na kuimarisha nguvu yao dhaifu na nyonge ya kimaumbile. Kwa fikra ya Pepo wanapata matumaini kwenye roho zao zenye kudhurika, zenye kukaribia kulia, na wanaweza kuishi kwa furaha. Mathalani, huku akiitafakari Pepo, mtoto anaweza kusema: “Mdogo au rafiki yangu amefariki na kuwa ndege wa Peponi. Yeye anarukaruka Peponi na kuishi kwa furaha zaidi kuliko sisi.” Vifo vya mara kwa mara mbele ya macho yao yasiyo na furaha vya watoto wenzao au vya wakubwa, vinginevyo vingevunja ukinzani wao wote na hamasa yao yote, na kufanya akili zao pambanuzi, kama vile roho zao, nyoyo, na akili, zilie pamoja na macho yao; ama wataporomoka kihisia kabisa au kuwa wanyama wenye wazimu, na wanyonge.

Ushahidi wa pili:

Ni kupitia maisha ya akhera tu ambapo wazee, wenye kuunda nusu ya wanaadamu, wanaweza kuhimili ujirani na kaburi, na kufarijika kwa fikra kuwa maisha yao, waliyoshikamana nayo sana, yatazimika hivi karibuni na dunia zao nzuri zitafikia ukomo. Ni kwa kutumainia uzima wa milele tu ndipo wanaweza kukabili ukataji tamaa mkubwa walio nao katika roho zenye hisia kama watoto katika kufikiria mauti. Baba na mama wenye kustahiki na wenye shauku, wenye kustahiki huruma na wana haja ya utulivu na amani ya akili, badala yake watahisi msukosuko wa kiroho na kukata tamaa nyoyoni mwao, na dunia hii itakuwa gereza lenye kiza kwao, na uhai pia, mateso ya kuhuzunisha.

Ushahidi wa tatu:

Ni fikra ya moto wa jahanamu inayodhibiti hisia zilizovurugika za vijana, kikundi chenye nguvu zaidi katia uzima wa jamii, na kuvuka kwao mpaka katika fujo, kuwazuia dhidi ya ushari, dhuluma, na uharibifu, na kuhakikisha kuwa maisha ya jamii yanaendelea kwa utulivu. Kama si kuhofia Jahanamu, kwa mujibu wa ‘Mwenye nguvu yuko sahihi,’ katika kufukuzia matamanio yao, vijana hao walevi wangezibadili dunia za watu dhaifu wasiojiweza na wasio na nguvu ziwe Jahanamu, na kuufanya utu uwe unyama.

Ushahidi wa Nne:

Kituo kipana zaidi cha maisha ya kidunia, na kiini chake, na pepo, hifadhi, na ngome ya furaha ya kidunia, ni uzima wa familia. Makazi ya kila mmoja ni dunia yake ndogo. Uzima na furaha ya makazi yake na familia vinawezekana kwa heshima halisi, shauku, na uaminifu na huruma, wepesi, na kujitolea. Heshima hii ya kweli na wema halisi vinaweza kupatikana kutokana na fikra kuwa wanafamilia wanapokuwa na usuhuba wa kudumu na urafiki na upamoja, na mwendelezo wa mahusiano ya kiuzazi, kutoto, kindugu, na kirafiki kwa kudumu katika maisha yasiyo na kikomo, na imani yao katika hili. Mtu anasema, kwa mfano: “Mke wangu atakuwa mwenzangu wa mara zote katika dunia ya milele na uzima wa milele. Haijalishi kama yeye kwa sasa ni mzee na mbaya, kwa kuwa atakuwa na uzuri wa milele.” Atajiambia kuwa atakuwa mwema na kujitolea kadri atakavyoweza kwa ajili ya usuhuba wa milele, na kumfanyia mapenzi na wema mkewe mpendwa na mzee kana kwamba ni hurulaini. Usuhuba uliokuwa uishe katika utengano wa milele baada ya saa moja au mbili ya urafiki mfupi wa juu juu ungekuwa badala yake, wa juu juu tu na wa muda mfupi, wa kubuni, wenye fikra kama za mnyama, na huruma ya uongo na heshima ya kutengeneza. Ama wanyama, kujiona na hisia nyingine zenye kushinda zingeweza kuzidi heshima na huruma, na kuibadili pepo hiyo ya kidunia kuwa Jahanamu.

Hivyo, mojawapo kati ya mamia ya matokeo ya kuamini ufufuo yameunganishwa na uzima wa jamii. Kama utafanywa mlinganisho baina ya shuhuda nne za hapo juu kutoka katika mamia ya vipengele na manufaa ya tukio hili moja na mengine, itafahamika kuwa kuutambua ukweli wa ufufuo na kutokea kwake, hizo ni hakika kama ukweli wa juu wa utu na haja yake iliyoenea. Ni dhahiri hata kuliko ushahidi kwa kuwepo chakula kilichotolewa kwa kuwepo wa haja tumboni mwa mwanaadamu, na kueleza kuwepo kwake kwa uwazi zaidi. Pia inathibitisha kuwa kama matokeo ya ukweli wa ufufuo yangelitolewa kutoka katika utu, ambao hali yake halisi ni ya wazi sana, ya juu zaidi, na hai, utu ungeshuka mpaka kuwa mwili ulioharibika na kuliwa na wadudu.

Wataalamu wa sayansi ya jamii, wanasiasa, na wahubiri wanaomwongoza mwanaadamu na wanaohusika na masuala yao ya kijamii na kimaadili watambue hili! Wana mapendekezo gani ya kuziba mwanya huu? Majeraha haya makubwa watayatibu kwa dawa ipi?

NUKTA YA PILI

Hii inaeleza kwa muhutasari ushahidi mmoja – kati ya nyingi – juu ya ukweli kuhusu ufufuo kutokea nguzo nyingine za imani. Ni kama ifuatavyo:

Miujiza yote inayoonesha utume wa Muhammad (Rehema na Amani zimwendee) na shuhuda za utume wake, na shuhuda zote juu ukweli wake, pamoja vinashuhudia kuwepo ufufuo na kuukubali. Kwa kuwa baada ya umoja wa kiungu, kila kitu alichosema maishani mwake kote kimefungamana na ufufuo wa wafu. Pia, miujiza yake na shuhuda zenye kuthibitisha, na kuthibitika, mitume wote waliotangulia walithibitisha ukweli huo huo. Pia, ushahidi wa fungu la maneno, “na katika Maandiko Yake,” yanayoshuhudia kikamilifu maneno, “na kwa Mitume wake,” yanathibitisha ukweli huo huo. Kama hivi:

Miujiza yote, ukweli, na shuhuda zinazothibitisha kwanza kabisa ukweli wa Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza, vinashuhudia na kuthibitisha ukweli na kutokea ufufuo. Takribani theluthi ya Qur’an ni kuhusu ufufuo, na mwanzoni mwa sura nyingi fupi fupi kuna aya zenye nguvu kuhusu hilo. Inaeleza ukweli huo huo waziwazi na kwa kuashiria kwa maelfu ya aya zake, na kuthibitisha na kuionesha. Kwa mfano:

 إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ Qur’an, 81:1

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ Qur’an, 22:1

 إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا Qur’an, 99:1

إِذَا السَّمَاء انفَطَرَتْ Qur’an, 82:1

إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ Qur’an, 84:1

عَمَّ يَتَسَاءلُونَ Qur’an, 78:1

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ Qur’an, 88:1

Licha ya kuonesha kwa uhakika kabisa mwanzoni mwa sura thelathini au arubaini kuwa ufufuo ni ukweli muhimu zaidi na wa lazima ulimwenguni, inaleta shuhuda zenye kushawishi kuhusu ukweli huo katika aya zake nyingine.

Je, kuna uwezekano wowote kuwa imani ya akhera ni uongo, inayoibuka kama jua kutoka katika maelfu ya matamko na kauli za Kitabu, ishara ya aya mojawapo kati yake imeleta mbele yetu matunda ya ukweli mwingi uliojulikana na wa kiulimwengu mzima katika sayansi ya Kiislamu? Je, kuna uwezekano wowote wa kulikana jua, au kuwepo kwa ulimwengu? Je, hilo halitokuwa muhali na upuuzi? Je, inawezekana kuwa ingawa jeshi linaweza wakati mwingine kuingia vitani ili tu alama ya mfalme isiongope, kuonesha uongo wa maelfu ya maneno, ahadi, na vitisho vya utawala ulio makini zaidi na wa kifahari? Je, inawezekana kuwa hayo yakawa uongo?          

Ingawa alama moja ya utawala huo mtukufu wa kiroho ambao kwa karne kumi na tatu mfululizo umetawala roho zisizohesabika, akili, nyoyo, na roho ndani ya mipaka ya ukweli na usahihi, na kuwafundisha na kuwaelekeza, ungetosha kuthibitisha ukweli wa ufufuo, umeonesha hilo kwa maelfu ya kauli za dhahiri. Je, adhabu ya moto wa Jahanamu si ya lazima kwa mpumbavu asiyetambua ukweli huu? Je huo si uadilifu halisi?

Kwa kuongezea, kuukubali kwao wazi wazi ukweli wa ufufuo, ambao Qur’an – inayotawala mustakabali na nyakati zote, inakariri kuthibitisha kwa upana na kufafanua, maandiko yote na vitabu vitukufu, kila kimoja kilitawala kipindi mahususi, kilithibitisha kwa mujibu wa nyakati na karne zao, lakini bila ya kufafanuliwa, bali imefichwa na kufupishwa, vikithibitisha maelfu ya alama za mafundisho ya Qur’an.

Kilichojumuishwa hapa kwa kuwa kinahusiana na mjadala huu ni ushahidi mwishoni mwa Mshale wa Tatu wa nguzo nyingine za imani na hususani “Manabii” na “Maandiko Matakatifu,” mpaka “kuamini Siku ya Mwisho.” Inaunda ushahidi unaokinaisha kuhusu ufufuo, pia ipo katika umbo la dua yenye nguvu ambayo ni yenye maneno mafupi yanayoondoa mashaka yote. Yanasema katika dua:

“Ewe Mwenye kuniruzuku Mwenye Huruma!”

Nimefahamu kutokana na maelekezo ya Mjumbe Wako Mtukufu (s.a.w) na mafundisho ya Qur’an, kuwa awali ya yote, Qur’an na Mjumbe, na maandiko yote matukufu na manabii, wamethibitisha kwa kauli moja na kuashiria kuwa udhihirisho wa Majina yenye kuhusiana na uzuri na utukufu Wako, mifano yake ni yenye kuonekana duniani, yataendelea kwa nuru zaidi katika muda wote milele, na kuwa neema zako, ambapo sampuli zake ni zenye kuonekana katika dunia hii ya mpito, zitadumu katika makazi ya upeo wa furaha katika hali ya kung’aa zaidi, na kuwa wanaozitaka humu duniani watakuwa pamoja nazo milele.

“Pia, kwa kuegemea mamia ya miujiza dhahiri, alama za wazi, na kwanza kabisa Mtume Wako Mtukufu (Rehema na amani zimwendee) na Qur’an yenye Hekima zote, na manabii kwa roho zao zenye nuru, na mawalii, ambao ni nguzo za kiroho kwa nyoyo zao zilizojaa nuru, na wanazuoni waliotwaharika kwa akili zao zenye elimu ya juu, kwa kuegemea vitisho Vyako vyenye kukaririwa na ahadi katika maandiko yote matukufu, na kutumainia sifa Zako tukufu kama vile uwezo, rehema, kufadhili, hekima, utukufu, na uzuri, na juu ya sifa Zako, na heshima ya utukufu Wako, na mamlaka ya utawala Wako, na kwa sababu ya nuru zao na maono na imani kwa kiwango cha ‘elimu ya yakini,’ hutoa bishara kwa watu na majini kuhusu furaha ya milele na kuwajulisha kuhusu Jahanamu kwa waliopotea; wanakuwa na imani yenye nguvu na kukiri.”

“Ewe Mweza wa Yote na Mwenye Hekima Zote! Ewe Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu! Ewe Mkarimu Unayetimiza Ahadi! Ewe Jabari Mwenye Utukufu, Mshindi Mtukufu!”

“Umetakasika kabisa na umetukuka juu ya kuwaongopea marafiki wengi, na ahadi nyingi, na sifa, na kukanusha amri za hakika za utawala wako na swala na dua za waja wako wa kukubaliwa, Unaowapenda na wanaokupenda kwa kuridhika Nawe na kukutii; na Wewe umetakasika dhidi ya ukanusho wa ufufuo kutoka kwa wapotovu na makafiri, ambao kwa ukafiri, uasi wao na kukana ahadi Zako, wanaukosea ukubwa wa utukufu wako na kukashifu heshima Yako na Uungu wako, na kuondoa huruma ya Mamlaka Yako. Tunatangaza kuwa uadilifu Wako, uzuri, na rehema kutakasika dhidi ya uasi huo usiokoma, ubaya huo. Tunaamini kwa nguvu kuwa ushahidi wa manabii, wanazuoni waliotwaharika, na mawalii, ambao ni wajumbe Wako wa kweli, wapiga mbiu wa mamlaka Yako, katika viwango vya ‘uhakika kabisa,’ ‘elimu ya uhakika,’ na ‘maono ya uhakika,’ katika hazina za rehema Zako huko akhera na maghala ya Neema Zako katika ulimwengu wa milele, na uzuri wa kimiujiza wa udhihirisho wa Majina Yako Mazuri, yatakayodhihirishwa kikamilifu katika makazi ya upeo wa furaha, bila ya shaka ni kweli, na walichoelekeza kinaendana na usahihi bila ya shaka, na kuwa bishara walizotoa ni kweli na zitatokea. Kwa kuamini kuwa mshale mkuu wa Jina la Ukweli, ambalo ni chanzo, jua, na hifadhi ya ukweli wote, ni ukweli huu wa ufufuo na Mkusanyiko Mkubwa, wanaowafundisha waja Wako.”

Ewe Allah! Kwa ajili gani wanafundisha na kwa utukufu wa hilo, tupe sisi na wanafunzi wote wa Risale-i Nur imani kamilifu na mauti ya furaha. Utujaalie tupate uombezi wao. Amin!

Kwa kuongezea, kama zilivyo shuhuda zote zenye kuonesha utukufu wa maandiko yaliyoteremshwa, na miujiza yote na shuhuda zenye kushuhudia utume wa Kipenzi cha Allah (s.a.w), na wa manabii wote, katika hali isiyo ya moja kwa moja, zinathibitisha ukweli wa akhera, ambacho ndicho wanachofundisha juu ya kila kitu kingine; hivyo ushahidi mwingi wa uwepo na umoja wa Mwenye uwepo wa wajibu unathibitisha kuwepo na kufunguka ulimwengu wa milele wa furaha ya milele, utakaokuwa dalili kuu ya mamlaka na uungu. Kama itakavyoelezwa na kuthibitishwa katika vifungu vifuatavyo, yote mawili, kuwepo kwa mwenye uwepo wa wajibu, na Sifa Zake nyingi, na Majina, kama vile mamlaka, Uungu, rehema, upole, hekima, na uadilifu, hulazimisha uwepo wa akhera kwa uhakika mkubwa sana, na kuhitajia ulimwengu wa milele na ufufuo wa wafu na Hukumu ya Mwisho kwa ajili ya kutoa malipo na adhabu.

Kwa kuwa yupo Allah wa tangu na wa Milele, kwa hakika kabisa akhera ipo, uwanja wa milele wa mamlaka ya Uungu Wake.

Na kwa kuwa ulimwenguni na hasa kwa viumbe hai kuna utawala kamili wenye rehema na mtukufu mno na wa hekima nyingi, na huo uko dhahiri; kuna uhakika wa kuwepo ulimwengu wa milele wa furaha utakaotukuza utukufu wa utawala huo dhidi ya kuukosea heshima, busara yake kutoka katika kusikokuwa na lengo, na rehema yake dhidi ya ukatili; na ulimwengu huo unapaswa kuwepo.

Na kwa kuwa neema zisizokuwa na idadi, fadhila na matukio mengi ya rehema yanayoonekana wazi, yanazionesha akili ambazo hazijazimika na nyoyo ambazo hazijafa kuwa nyuma ya pazia ya Ghaibu kuna Mmoja Mwingi wa Rehema; kwa hakika kuna uhai wa milele utakaohifadhi neema hizo dhidi ya dhihaka, neema dhidi ya ulaghai, upendo dhidi ya uadui, rehema dhidi ya ukatili, huruma na zawadi dhidi ya udanganyifu, na utafanya neema ziwe neema na ukarimu uwe ukarimu.

Na kwa kuwa katika majira ya kuchipua katika ukurasa finyu wa ardhi, kalamu ya uwezo huandika maelfu ya malaki ya vitabu bila ya dosari pasi na kuchoka mbele ya macho yetu; na kwa kuwa mwenye kumiliki kalamu ameahidi mara nyingi mno: “Nitaandika kitabu kizuri cha milele katika ulimwengu mpana, kilicho rahisi zaidi ya kitabu hiki cha majira ya kuchipua kilichoandikwa kwenye ulimwengu huu mfinyu, uliovurugika na kuchanganyikana, na nitakuachilia ukisome;” kwa kuwa anataja kitabu kwenye amri zake zote; kwa hakika, sehemu kubwa ya kitabu imeshaandikwa, na kwa ufufuo na Hukumu ya Mwisho kitaongezewa tanbihi chini ya kurasa, na madaftari yote ya amali za watu yataandikwa humo.

Na kwa kuwa, kutokana na wingi wa viumbe, ardhi ni makazi, chanzo, kiwanda, udhihirisho, na mahali pa mkusanyiko wa mamia ya maelfu ya viumbe hai vyenye kuendelea kubadilika na viumbe wenye roho, na ni moyo, kituo, muhtasari, na matokeo ya ulimwengu, na sababu ya kuumbwa kwake; umuhimu wake mkubwa, na kuwekwa sawa na mbingu zenye nguvu licha ya udogo wake; katika hukumu za kiungu, mara zote husemwa:

ربُّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ

Na kwa kuwa mwanaadamu, anayetawala ardhi, ambayo kwa hivyo, ana haki ya kuwatumia viumbe wengi, na kuwatiisha viumbe hai kwa kuwakusanya karibu yake; na kwa kuwa anatoa amri, anaonesha, na kukusanya pamoja kila namna nzuri mahali pamoja kama orodha, kwa kuwapamba, kiasi kwamba huvutia, si hisia na mastaajabu ya watu na majini, bali wakazi wa mbingu na ulimwengu, na mtizamo wa kushukuru wa Mwenye kumiliki ulimwengu, hivyo kupata umuhimu mkubwa na kuaminiwa sana; na kwa kuwa anaonesha kwa sayansi na sanaa yake kuwa yeye ni lengo la kuumbwa ulimwengu, na matokeo yake muhimu zaidi, na tunda la thamani zaidi, na khalifa wa Kiungu ardhini; na kwa kuwa kwa sababu kuhusu dunia hii, ameamuru na kuonesha vyema kabisa sanaa ya ajabu ya Muumba dunia, mwanaadamu huachwa duniani licha ya uasi na ukafiri wake, na adhabu imeahirishwa, na kwa sababu ya kazi hii, muda wake umerefushwa ili afanye kazi yake kwa mafanikio.

Na kwa kuwa yupo Muumbaji mwenye nguvu, mwenye hekima na mwenye rehema, Anayeumba tufe lenye nguvu na kuwa hazina ya namna zote za metali na madini anayohitaji mwanaadamu kwa namna iliyo nje ya nguvu na utashi wake, ambaye licha ya kuwa dhaifu, mwenye kuhitajia kiasili na kimaumbile, ana haja nyingi na ni pia ni mwenye kupata masumbuko mengi – na kwa kuwa Anaijaalia iwe ghala la kila namna ya chakula, na duka lililosheheni bidhaa za kila namna zenye kumridhisha mwanaadamu, na kumwangalia mtu kwa namna hii, na kumlea, na kumpa anachohitaji.

Na kwa kuwa yupo Mwenye kuruzuku Ambaye ni kwa hiyo, Anayempenda mwanaadamu na kumsababisha ampende Yeye, na Ambaye ni mwenye kubaki na ana dunia za milele, na Anayefanya kila jambo kwa haki na hekima; na kwa kuwa fahari ya utawala huo Wenye Enzi wa Tangu na mamlaka Yake ya Milele hauwezi kuwemo tu kwenye maisha haya mafupi ya kidunia, na katika umri wa mpito wa mwanaadamu, na katika ardhi ya muda mfupi na mpito; na kwa kuwa kukithiri kwa uovu na maasi yanayotokea baina ya watu, ambayo yako tofauti na ustawi, haki, urari na uzuri wa ulimwengu, na kukana kwao, udanganyifu, na ukafiri kwa Mpaji wao, Anayewalea kwa wema, kwakuwa hawaadhibiwi humu duniani, na dhalimu katili anaishi kwa raha ilhali wanaodhulumiwa wasio na furaha wanaishi kwa taabu; na kwa kuwa haki kamili ambayo alama zake ni zenye kuonekana ulimwenguni kote ziko tofauti kabisa na mwasi mkatili na wadhulumiwa waliokata tamaa kulingana katika wakati wa mauti, haiwezi kukubali kwa namna yoyote ile.

Na kwa kuwa kama ambavyo Mmiliki wa ulimwengu alivyoichagua ardhi kutoka katika ulimwengu, na mwanaadamu kutoka katika ardhi na kumneemesha kwa hadhi ya juu na umuhimu; hivyo kati ya wanaadamu ameteua manabii, mawalii, na watakatifu, wanaadamu wa kweli wenye kuendana na malengo ya mamlaka yake na kupitia imani yao na kujisalimisha kunamfanya Awapende; amewafanya kama marafiki na wasemeshwa wake, na kujaalia miujiza na kufaulu juu yao na kuwaadhibu maadui wao kwa mapigo ya kiungu. Na katika marafiki hawa wapendwa Amemteua kiongozi wao na chanzo cha utukufu, Muhammad (Rehema na amani zimwendee), na kwa karne nyingi ameangazia Nuru yake kwenye nusu ya dunia na sehemu moja kati ya tano za wanaadamu; kana kwamba ulimwengu uliumbwa kwa ajili yake, malengo yake yote yanakuwa dhahiri kupitia kwake, na dini yake na Qur’an. Na ingawa anastahili kuishi wakati mrefu usio na mpaka katika kufidia huduma yake ya thamani kubwa sana, kwa mamilioni ya miaka, aliishi kwa muda mfupi tu wa miaka sitini na mitatu ya taabu kubwa. Basi je, kuna uwezekano wowote kuwa asifufuliwe pamoja na wenzi na marafiki zake? Kwamba kwa sasa asipaswe kuishi kiroho? Kwamba angeangamizwa milele? Allah aepushe hilo! Ndiyo, ulimwengu wote na ukweli wa dunia unahitaji afufuliwe na wanamwomba Mmiliki wa ulimwengu kuwa awe hai.

Na kwa kuwa katika Mshale wa Saba, (Ishara kuu), kila moja kwa uimara wa mlima, miafaka thelathini na tatu yenye nguvu imethibitisha kuwa ulimwengu umetoka kwa mmoja na hiyo ni mali ya mmoja; na imedhihirisha Umoja Wake na upweke, ni njia ya makamilifu ya Kiungu; na kupitia umoja na upweke, viumbe wote wanakuwa kama askari chini ya amri na maafisa watiifu; na kwa kuja kwa akhera, makamilifu huokolewa dhidi ya kuporomoka, haki kamili dhidi ya ukatili, hekima yenye kuenea dhidi ya upumbavu, rehema yenye kuenea dhidi ya adhabu, na heshima ya uwezo dhidi ya udhaifu wa kudhalilika, na kuachiliwa huru dhidi ya haya.

Kwa hakika na bila ya shaka yoyote, kama ilivyolazimishwa na ukweli katika ‘kwa kuwa’ hizi sita – sita kati ya mamia ya nukta za kumwamini Allah – mwisho wa dunia utafika na ufufuo wa wafu utatokea. Milango ya mlipo na adhabu itafunguliwa ili umuhimu wa ardhi uliotajwa hapo juu, na umuhimu wake, na  umuhimu wa mwanaadamu na thamani yake vitambulike, na ili ibaki haki, uadilifu uliotajwa hapo juu, hekima, rehema, na  mamlaka ya Mpangaji Mwingi wa Hekima, Ambaye ni Muumbaji wa ardhi na mwanaadamu, na Mwenye kuwaruzuku; na marafiki wa kweli wa Mwenye kuruzuku milele watanusuriwa dhidi ya kuangamia milele; na mkuu zaidi na kustahiki katika marafiki hao atapata malipo ya huduma zake tukufu, zilizofanya viumbe wote wawe radhi na kuwa na deni; na makamilifu ya Enzi ya Milele yatakaswe na kumwepusha mbali na dosari yoyote na upungufu wowote, na uwezo Wake dhidi ya udhaifu, na hekima Yake dhidi ya upumbavu, na haki dhidi ya dhuluma.

Kwa kifupi:

Kwa kuwa Allah yupo, ndivyo pia akhera, kwa hakika ipo.

Kwa kuongezea, kama ambavyo ushahidi wote unathibitisha hayo, nguzo tatu za hapo juu za imani zinathibitisha na zinaashiria ufufuo; ndivyo pia nguzo mbili “na kuamini malaika, na Kudura ya Kiungu, kuwa heri na shari ni kutoka kwa Allah (s.w)” pia inalazimisha ufufuo na kuthibitisha kwa mtindo wenye nguvu kwenye ulimwengu wa milele. Ni kama hivi:

Shuhuda zote zinazothibitisha kuwepo kwa malaika na majukumu yao ya ibada, na tafiti zisizohesabika kuwahusu na mazungumzo nao, zinathibitisha moja kwa moja kuwepo kwa Dunia ya Kiroho, na dunia ya ghaibu, na ulimwengu wa milele na dunia ya akhera, na kuwepo kwa makazi ya furaha na Pepo na Jahanamu, ambavyo katika mustakabali vitajaa watu na majini. Kwa idhini ya Kiungu, malaika wanaweza kuziona dunia hizo na kuingia. Na Malaika wengi wa daraja za juu wanaokutana na wanaadamu, kama vile Jibrili, wameeleza kwa kauli moja juu ya kuwepo dunia hizo na wao kusafiri baina ya hizo. Kama tulivyo na uhakika, kutokana na habari ya wanaokuja kutoka Marekani, kuwa bara la Marekani lipo, ingawa hatukupata kuliona, hivyo kutokana na habari kuhusu malaika, ambazo zina miafaka mingi madhubuti, tunapaswa kuamini kwa uhakika huo huo juu ya kuwepo kwa dunia ya milele, ulimwengu wa akhera, na Pepo na Jahanamu. Na hivyo tunaamini.

Kwa kuongezea, ushahidi wote unaothibitisha nguzo ya “kuamini Kudura ya Kiungu,” iliyo katika Risala ya  Kudura ya Kiungu, (Neno la Ishirini na Sita), unathibitisha moja kwa moja juu ya kufufuliwa wafu, kupimwa amali kwenye mizani kuu, na kusambazwa kurasa za amali. Kuandikwa kwa habari za maisha ya viumbe hai vyote katika kumbukumbu zao, na kuandikwa kwa madaftari ya amali za viumbe wote wenye roho, na hususani wanadamu, katika Ubao Uliohifadhiwa, kudura hiyo pana na utengaji wa hekima na uandishi makini na kuhifadhiwa maandishi kunaweza tu kwa hakika kuwa matokeo ya hukumu  kuu katika muundo mtukufu wa kimahakama kushughulikia malipo na adhabu ya milele. Uandishi huo sahihi na hifadhi ungekuwa vinginevyo hauna maana kabisa na hauna lengo, na kinyume na hekima na uhalisia.

Pia, kama kusingekuwa na ufufuo, maana zote za hakika za kitabu cha ulimwengu, ikiwa kimeandikwa kwa kalamu ya Kudura ya Kiungu, ingebatilika, jambo ambalo haliwezekani kabisa. Ni kama isivyowezekana kukana kuwepo kwa ulimwengu, kwa hakika, ni kuweweseka.

Kwa kifupi:

Kwa ushahidi wake wote, nguzo tano za imani zinahitajia kuwepo kwa ufufuo na Hukumu ya Mwisho, na kuwepo kwao, na kuwepo na kufunguka ulimwengu wa akhera, na zinathibitisha hayo na kuyalazimisha.

Hivyo, ni kwa sababu kuna hoja na shuhuda kubwa zisizotetereka kuhusu ufufuo, katika kuendana kikamilifu na ukubwa wake, kiasi kuwa takribani theluthi ya Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza imeundwa na ufufuo na akhera, na inaufanya ukweli huo jiwe la msingi la ukweli wake wote, na kukijengea kila kitu juu yake.

(Mwisho wa Utangulizi)

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.