SULUHU KUPITIA RISALE-I NUR

Kwa Jina Lake, (s.w).

Hakuna chochote isipokuwa kinamtukuza Yeye kwa sifa.

Rafiki zangu gerezani na ndugu zangu katika dini!

Ilinitokea kukuelezeni ukweli utakaokuokoeni dhidi ya adhabu ya duniani na Akhera. Ni kama ifuatavyo:

Mathalani:

Mtu akimuua ndugu wa mtu mwingine au jamaa yake mmojawapo. Mauaji yenye kuleta furaha ya dakika moja ya ulipizaji kisasi yanasababisha mamilioni ya dakika za huzuni moyoni na maumivu makali ya jela. Na hofu ya kisasi kutoka kwa ndugu na jamaa za aliyeuawa, na wasiwasi wa kukabiliana uso kwa uso na adui yake huondoa furaha na starehe zote maishani. Anapata adhabu ya kuwa na hofu na hasira. Kuna utatuzi mmoja tu katika hili, na hilo ni mapatano, ambayo Qur’an inaamuru, na ukweli, usahihi, manufaa, utu, na matakwa ya Uislamu na ujasiri.          

Kwa hakika, kinachohitajika kweli ni amani, kwa sababu saa imeshapangwa, haibadiliki. Kwa kuwa saa yake iliyopangwa imefika, mtu aliyeuawa asingekaa zaidi katika hali yoyote. Na ama kwa muuaji, ilikuwa njia ya kudura ya Allah kufanyika. Kwa kuwa hakuna mapatano, pande zote mbili zinapata adhabu za hofu na kisasi. Ni kwa sababu ya hili ndipo Uislamu unaamuru kuwa “muumini mmoja asikasirikiane na muumini mwingine kwa zaidi ya siku tatu”.

Al-Bukhari, Al-Adab 57,62.

Kama mauaji hayakuwa matokeo ya mfundo au uadui uliothibitika, na mfanya vurugu ndumila kuwili ameanzisha mfarakano, ni muhimu kufanya amani kwa haraka. Vinginevyo, tatizo hilo dogo linakuwa kubwa, na kuendelea. Kama wanafanya amani, na muuaji anatubu na anamwombea mtu aliyemuua bila ya kukoma, basi pande zote mbili zitapata zaidi na kuwa kama ndugu. Katika nafasi ya ndugu aliyeondoka, atapata ndugu wengi wa kidini. Atakuwa ameondolewa kwa Kudura ya kiungu na kumsamehe adui wake. Na hususani kwa kuwa wanazingatia mafunzo ya Risale-i Nur, amani na ustawi wa mtu mmoja mmoja, na umma, na undugu uliopo katika wigo wa Risale-i Nur unahitaji kuwa waweke pembeni hisia zote ngumu zilipo baina yao.

Ilikuwa hivyo katika Gereza la Denizli; wafungwa wote waliokuwa maadui wakawa ndugu kwa mafunzo ya Risale-i Nur. Ilikuwa sababu mojawapo ya kuachiliwa kwetu, na ilisababisha hata ukosefu wa dini na kutomjua mungu kusema kuhusu wafungwa hao: “Mashallah! Barakallah!” na ilikuwa faraja kabisa kwa wafungwa hao. Mimi mwenyewe nimewaona hapa watu mia moja wakipata taabu kwa sababu ya mtu mmoja na kutokutoka kwenda kushughulika kwa pamoja. Ni dhuluma kwao. Muumini wa kiume mwenye ufahamu hatamdhuru kila mmoja katika mamia ya waumini wengine kwa sababu ya kosa dogo au manufaa machache. Kama atafanya kosa na kusababisha madhara, anapaswa atubu upesi.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.