SWALI LENYE KUSUMBUA SANA LEO

Swali tulilomuuliza ‘Ustadhi’, Mkuu wetu, lilikuwa hili: “Kwa miaka miwili katika nyakati ngumu zaidi za Vita vya dunia,

Vita vya pili vya dunia.

ambavyo vimeunganika kwa ukaribu na majaaliwa ya Ulimwengu wa Kiislamu, -na sasa ni takribani miaka kumi haujamuuliza yeyote katika sisi, wala Amin, ambaye kila siku anaangalia haja zako, haujauliza chochote katika hilo, haujalipa umuhimu hata kidogo. Je, kuna ukweli mwingine mkubwa kuliko tukio hili, linalotawala na kulizidi? Au je, kuna madhara yoyote kujihusisha nayo?” Akajibu kama ifuatavyo:

Naam, kuna ukweli mkubwa, tukio lenye athari kubwa kuliko Vita vya Dunia, na kwa kuwa linatawala Vita, basi Vita vinakuwa si muhimu kabisa ukililinganisha navyo. Sababu ni hii: Vita vya dunia vinahusika na serikali mbili zikigombania utukufu wa kidunia; na wakati ambapo dini mbili kubwa zimefungua haja ya amani na mapatano, mkono wa kutisha wa ukosefu wa dini umeingia katika mapambano ya nguvu kwa dini zilizoteremka, mashitaka yenye kuzidi sana umuhimu yamefunguliwa katika mahakama kuu ya ‘tabaka la wafanyakazi na la mabwanyenye’ la wanaadamu. Jambo hilo kubwa limekuwa kubwa kiasi kwamba thamani ya mashitaka haya inayomhusu hata mtu mmoja ni kubwa kuliko Vita vya Dunia. Mashitaka ni kama ifuatavyo:          

Kwa Kila muumini, kwa hakika kwa kila mmoja katika wakati huu, mashitaka haya yamefunguliwa, kama kila mmoja angelikuwa na utajiri na nguvu kubwa kama Waingereza na Wajerumani kwa pamoja, na akili kadhalika, angetumia vyote ili ashinde katika mashitaka haya. Kwa hakika, yeyote anayeambatanisha umuhimu kwenye mambo mengine kabla ya kushinda mashitaka ni mwendawazimu. Na hatari ni kubwa sana ambapo kwa mujibu wa uchunguzi wa mtabiri wa ukweli wa viumbe, kati ya watu arubaini katika mahali walipopokea karatasi zao za ruhusa ya kuondoka kutoka mkononi mwa saa iliyopangwa, ni mmoja tu aliyeshinda mashitaka. Watu thelathini na tisa walishindwa.

Na kwa hivyo, kama mwanasheria ni wa kutafutwa ambaye ameshinda mashitaka hayo makubwa na muhimu kwa watu wanane kati ya kumi kwa miaka ishirini, na atashinda hata hii, yeyote mwenye akili yoyote atalazimika kufungamanisha umuhimu mkubwa kwa chochote anachoweza kufanya kitakachomshawishi mwanasheria huyo afanye kazi yake na kushinda mashitaka kwa ajili yake.

Mwanasheria mmojawapo wa namna hiyo, wa kwanza kwa hakika, ni Risale-i Nur, ambayo utendaji wake, inatoa na imechukuliwa kutoka katika Qur’an ya ufafanuzi wa Kimiujiza, kama wanavyoweza kuthibitisha maelfu ya walioshinda mashitaka kupitia hiyo.

Kwa hakika, imekuwa haipingiki kuwa kila mwanaadamu aliyetumwa kama afisa duniani ni mgeni hapo, na kuwa hali yake halisi imeelekezwa katika maisha ya milele. Lakini katika wakati huu ngome ambayo ni mahali pake pa msaada na itamletea maisha ya milele imetikisika, na inaonekana ataiacha dunia milele na marafiki zake wote waliomo humo. Katika wakati huo mashitaka yamefunguliwa ambayo ama yatamnufaisha au kumpa hasara ya mali ya milele ambayo ni kamilifu mno mara elfu kuliko dunia. Kama hana waraka wa imani, na kama imani yake, inayounda kibali chake na makaratasi, si imara, atapoteza madai. Basi kuna chochote kinachoweza kuchukua nafasi ya alichopoteza?          

Hivyo, kutokana na ukweli huu, hata kama akili na fikra za kila mmoja wetu, yaani, mimi na ndugu zangu, zitapanuliwa zaidi ya mara mia moja, zitakuwa tu zenye kutosha kwa ajili ya kazi hii kubwa na tukufu. Kufikiria mambo mengine ni kupita kiasi na hakuna maana. Kwa hakika, tungeweza kufikiria mambo mengine wakati wanafunzi fulani wa Risale-i Nur walipojihusisha na mashitaka mengine; katika nyakati ambapo bila ya sababu, tumepatwa na chuki isiyo ya lazima na kushambuliwa na wasio na akili, na basi ilikuwa dhidi ya utashi wetu na kwa umuhimu mdogo sana.

Haya yanahusiana na maneno ya kujihami katika mahakama.

Zaidi ya hivyo, kuna madhara kuhusisha akili na moyo kwenye mashitaka na migongano nje ya kesi hii kubwa na ya haki. Kwa mtu anayezingatia na kujishughulisha na nyanja kubwa na za ushawishi za kisiasa ama ataacha majukumu aliyo nayo katika uwanja mdogo, au hamasa yake itafifia. Pia, mtu wakati mwingine hujikuta amechukuliwa kabisa kwa kuzingatia uwanja mpana wenye kulaghai wa siasa na mgogoro. Kisha, kwa vile hatekelezi wajibu wake, hata kama hapotezi ubora wa moyo wake, usafi wa nia, uadilifu wa fikra na ikhlasi katika majukumu yake, anaweza kwa hali yoyote kushutumiwa hivyo. Kwa hakika, walipokuwa wakinishambulia mahakamani kuhusu nukta hii, niliwanyamazisha kwa maneno yafuatayo:

Kama ulivyo ukweli wa dhahiri kama jua wa imani na Qur’an haviwezi kuwa chombo au kufuata mvuto wa nuru za mpito ardhini, kwa hivyo pia anayejua vyema ukweli huo hawezi kuvitumia kama chombo kwenye ulimwengu wote, wachilia mbali matukio ya ardhini.”

Jibu la Mkuu wetu liliishia hapo. Na tukalikubali kwa nguvu zetu zote.

Wanafunzi wa Risale-i Nur

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.