TUNDA LA FOROSADI NYEUSI

Said wa zamani aliyasema haya kwa ulimi wa Said Mpya

chini ya mforosadi uliobarikiwa.

Ninayemwambia si Ziya Pasha, ni wale wenye kuvutiwa na Ulaya.

Anayezungumza si nafsi yangu, ni moyo wangu kwa jina la wanafunzi wa Qur’an.

Maneno yote yaliyotangulia ni ukweli; tahadhari, usipotee njia, usikiuke mipaka yao!

Usisikilize fikra za Ulaya na uepuke, vinginevyo watakufanya ujutie hilo!

Unawaona walio elimika zaidi katika wao, waking’aa kwa walio katika hali ya wastani,

Patwa na mshangao: Kuhusu nani, na kwa nani nitalalamika?

Qur’an inasema, nami ninasema pia sitageuka nyuma:

Nitampa Yeye mashitaka yangu. Sijachanganyikiwa, kama nyinyi.

Ninamlilia Mungu wa kweli; Siondoki, kama nyinyi.

Nitapigia kelele njia yangu kutoka chini mpaka angani; Sikimbii, kama nyinyi.

Kwa kuwa njia yote ya Qur’an ni nuru juu ya nuru; sivunji ahadi, kama nyinyi.

Katika Qur’an kuna ukweli na hekima; Nitathibitisha hilo. Sizingatii chochote katika falsafa adui.

Katika Kigezo kuna ukweli wa dhahabu; ninachukua mimi mwenyewe, si kuuza, kama nyinyi.

Mimi nasafiri kutoka kwa viumbe mpaka kwa Muumbaji; Sipotei njia, kama nyinyi.

Mimi hupita katika njia zenye miba, sitembei juu ya miba, kama nyinyi.

Kutoka ardhini mpaka kwenye Kiti cha Enzi, ninatoa shukurani; sipuuzii, kama nyinyi.

Ninayaangalia mauti na saa teule kama rafiki; siogopi, kama nyinyi.

Nitaingia kaburini huku nikitabasamu, si kwa kutetemeka, kama nyinyi.

Silioni kama kinywa cha dubwana, malalo ya mnyama wa mwitu, enye kushuka kwenye kutokuwepo, kama nyinyi.

Linaniunganisha na marafiki zangu; sichukizwi na kaburi, kama nyinyi.

Ni mlango wa Rehema, lango la Nuru, lango la Ukweli; Mimi sijachukizwa nalo; Sitakimbia. Kwa kusema: Kwa Jina la Allah, nitabisha hodi.

Sitasema “Basi”, na kukimbia.

Sitageuka nyuma yangu wala kutishika.

Huku nikisema: Kila sifa njema ni kwa Allah!, Nitalala chini na kupata urahisi. Sitapata taabu wala kubakia upweke.

Kwa kusema, Allah ni Mkubwa Zaidi! Nitasikia Wito wa ufufuo na kuinuka,

Nitasikia wito wa Israfil katika mapambazuko ya Ufufuo na kutangaza, “Allah ni Mkubwa zaidi,” nitainuka. Sitachelewa kwenda kwenye Mkusanyiko Mkubwa na Mkutano wa Swala.

Sitarudi nyuma kutoka kwenye Mkusanyiko Mkuu, au Msikiti Mkubwa.

Sitahuzunika, shukurani kwa fadhila ya Kiungu, nuru ya Qur’an, na mwangaza wa Imani;

Bila ya kusimama, nitaharakisha, kupaa, kwenda kwenye kivuli cha Kiti cha Enzi cha Mwingi wa Rehema.

Allah akipenda, sitapotea, kama nyinyi.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.