UDUGU GEREZANI

Kwa Jina Lake, (s.w)

Ndugu zangu waaminifu na wafungwa wa zamani! Nimefanya suluhisho imara ambalo, kwa heshima ya upendeleo wa kiungu, nyinyi ni sababu muhimu ya sisi kuingia kwetu hapa. Maana yake, kwa faraja yake na ukweli wa imani, Risale-i Nur ni yenye kukuokoeni dhidi ya huzuni ya balaa la gereza na kutoka katika madhara mengi ya kidunia, na maisha yenu yasipite bila ya manufaa na kukosa kitu kwa masikitiko na huzuni na kupotezwa katika upepo wa udhanifu, na Akhera yenu dhidi ya kulia kama dunia yenu inavyolia sasa; inakupeni kitulizo cha kweli.

Kwa kuwa ukweli wa jambo hilo ni huu, kwa kweli lazima muwe ndugu nyinyi kwa nyinyi, kama wafungwa wa Denizli na Wanafunzi wa Risale-i Nur. Mnaweza kuona kuwa wanachunguza mali zenu zote, chakula, mkate, na mchuzi unaokuja kutoka nje ili kisu kisikufikieni miongoni mwenu na msishambuliane. Maaskari magereza wanaokuhudumieni kwa uaminifu hupata taabu sana. Pia, hamtoki nje kwenda kufanya mazoezi kwa pamoja, kama vile mtashambuliana kama wanyama wa mwituni. Na kwa hivyo, marafiki wapya, ambao kwa asili ni wakakamavu na jasiri, kwa ujasiri mkubwa wa kimaadili mnapaswa mliambie kundi hilo kwa wakati huu:

“Kama si visu, bali bastola zingegawiwa kwetu, na amri ya kupiga pia, tusingewadhuru marafiki zetu wenye mkosi na waliopata janga hili kama sisi. Kwa mwongozo na kwa amri ya Qur’an, na imani, na undugu wa Kiislamu, na utashi wetu, tumeamua kuwasamehe na kujaribu kutowakashifu, hata kama hapo mwanzo kulikuwa na sababu mia moja za uadui na uhasama wetu.” Hivyo basi, ndivyo mnavyobadili gereza hili liwe nafasi kubwa ya mafunzo.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.