UJANA UTAONDOKA

[Onyo, Fundisho na Ukumbusho Waliopewa Vijana Wengi Wasiokuwa na Furaha]

Siku moja vijana kadhaa wenye akili walikuja kwangu, wakihitaji jambo jingine lenye athari ili wajihifadhi dhidi ya hatari za katika maisha, ujana, na tamaa za roho. Kama nilivyowaambia wale ambao hapo awali walitaka msaada kutoka katika Risale-i Nur, pia niliwaambia vijana hawa:

Ujana wenu kwa hakika utakutokeni, na kama hambakii katika wigo wa halali, mtapotea, na badala ya furaha hizi, utakuleteeni majanga na maumivu duniani, kaburini, na Akhera. lakini kama, kwa mafunzo ya Kiislamu, mtatumia neema ya ujana wenu kama shukurani kwa heshima, katika unyoofu na utii, matokeo yake utasalia ukiendelea na utakuwa sababu ya kupata ujana wa milele.

Ama kuhusu uhai, kama ni bila ya imani, au kwa sababu ya uasi, imani  haiathiri, italeta maumivu, huzuni na masikitiko ya juu, kuliko furaha za mpito na faraja inayoleta. Kwa kuwa, tofauti na Wanyama, mwanaadamu ana akili na fikra, ameunganika na wakati huu uliopo, uliopita na ujao. Anaweza kupata maumivu na furaha katika nyakati hizo. Ilhali, kwa kuwa Wanyama hawafikirii, huzuni inayokuja kutokana na wakati uliopita na hofu na wasiwasi kwa ajili ya mustakabali hauharibu furaha zao za sasa. Na hususani kama furaha ni haramu; basi ni kama asali yenye sumu kwa pamoja.

Maana yake, kutokana na mtizamo wa furaha ya maisha, mwanaadamu anaangukia katika kiwango cha kuwa chini kuliko Wanyama. Kwa hakika, maisha ya watu wapotovu na wasio wazingatiaji, na kwa hakika kuwepo kwao, hata dunia yao, ni siku ambamo wao hujikuta humo. Kutokana na mtizamo wa upotovu wao, wakati wote na ulimwengu wa wakati uliopita haupo, umekufa. Hivyo akili zao, zinazowaunganisha wao kwenye wakati uliopita na ijao, huwaletea kiza na weusi. Na kutokana na kukosa kwao imani, mustakabali pia haupo. Zaidi ya hivyo, kwa sababu wana fikra, utenganisho wa milele unaotokana na kutokuwepo huku kunaendelea kuwazalishia giza katika maisha yao.

Ilhali, kama imani inayapa uhai maisha, kupitia katika nuru ya imani, huangaza wakati uliopita na ujao na kuwezesha kuwepo. Kama wakati wa sasa, inaleta furaha tukufu za juu na nuru za kuwepo kwa ajili ya roho na moyo -kwa mujibu wa imani. Kuna maelezo juu ya ukweli huu katika ‘Matumaini ya Saba’ katika Ujumbe kwa wazee. Unaweza kurejea huko.

Na kwa hivyo, maisha ndivyo yalivyo. Kama unataka furaha ya uhai, uhuishe uhai wako kwa imani, na uupambe kwa matendo ya kidini. Na uuhifadhi kwa kujiepusha na madhambi.

Kuhusu ukweli wa kutisha wa kifo, unaooneshwa na vifo kila siku, kila mahali, kwa nyakati zote, nitakuelezeni kwa mifano hai, halikadhalika hayo niliwaambia vijana wengine.

Mathalani, vitanzi vimesimamishwa hapa mbele ya macho yenu. Licha ya kuwa ofisi ya bahati nasibu, lakini inagawa tiketi kwa zawadi kubwa za kweli. Sisi tuliopo hapa tuko watu kumi, iwe tunapenda au hapana, tutaitwa hapo; hakuna mbadala. Watatuita, na kwa kuwa wakati huo ni siri, dakika yoyote wanaweza kusema ama: “Njoo uchukue tiketi ya kunyongwa kwako! Panda kwenye kitanzi!” Au: “Tiketi ya kujishindia zawadi za mamilioni ya dola zenye thamani ya dhahabu zimekufikia. Njoo uchukue!” Katika hali ya kuwasubiri waseme hayo, watu wawili ghafla wanatokea mlangoni. Mmoja ni mwanamke aliyevaa mavazi ya kubana, mzuri na mwenye kuhadaa. Mkononi mwake ameshika vitu ambavyo kwa juujuu ni vitamu sana, lakini kwa hakika ni haluwa yenye sumu, ametuletea ili tule. Mwingine ni mtu makini asiyedanganya wala kudanganywa. Anaingia baada ya mwanamke huyo na kusema:

“Nimekuleteeni zindiko, fundisho. Mkilisoma, na msipokula haluwa hiyo, mtanusurika mbali na vitanzi. Kwa zindiko hili, mtapata tiketi kwa ajili ya zawadi zisizo na kifani. Angalia, mnaona kwa macho yenu kuwa wanaokula asali wanapanda kwenye vitanzi, na mpaka wakati huo wanapata maumivu makali ya tumbo kutokana na sumu ya haluwa. Na nani atakayepokea tiketi kwa ajili ya zawadi kubwa hajulikani; inaonekana kuwa wao pia watapanda kwenye vitanzi. Lakini kuna mamilioni ya mashahidi wanaoshuhudia kuwa wanaweza kuingia kwenye uwanja wa zawadi kirahisi. Kwa hivyo, angalieni dirishani! Maofisa wa juu kabisa na watu wenye hadhi za juu jambo hili kwa sauti za juu: ‘Kama mnavyoona kwa uhakika kabisa kwa macho yenu hao wanaopanda kwenye vitanzi, kwa hivyo pia muwe na hakika kama mwangaza wa mchana, bila ya shaka au wasiwasi, wanaokuwa na zindiko wanapata tiketi kwa ajili ya zawadi.’”

Kwa hivyo, kama mshabaha ulivyo, kwa kuwa furaha potovu za ujana katika uwanja wa haramu, ambazo ni kama asali yenye sumu, hupoteza imani, ambayo ni tiketi kwa ajili ya hazina ya milele na viza ya kuelekea kwenye furaha ya milele, mtu anayejiingiza humo anaishia kwenye mauti, ambayo ni kama vitanzi, na taabu za kaburi ambazo ni kama mlango wa kwenda kwenye kiza cha milele. Na kwa kuwa saa iliyopangwa haijulikani, myongaji wake, hatofautishi kati ya kijana na mzee, wakati wowote anaweza kukata kichwa chako. Kama utaacha matamanio haramu, ambayo ni kama asali yenye sumu, na kupata imani na kutekeleza wajibu wa kidini, ambao ni zindiko la Qur’an, manabii mia moja ishirini na nne elfu (rehema na amani ziwafikie) pamoja na mawalii wasio na idadi na watu wa kweli wamesema kwa kauli moja kuwa mtapata tiketi kwa ajili ya hazina ya furaha ya milele inayokuja kutoka katika bahati nasibu ya ajabu ya majaaliwa ya kibinaadamu. Na wameonesha alama zake.

Kifupi:

Ujana utaondoka. Na kama utaendelea kubadhiriwa, utaleta majanga mengi sana na maumivu duniani na Akhera. Na kama mnataka kufahamu namna vijana wengi wa aina hiyo wanavyoishia mahospitalini wakiwa na magonjwa yanayotokana na ujana uliotumika vibaya na ubadhirifu, na katika jela au hosteli kwa ajili ya mafukara katika ziada zao, na katika sehemu za starehe kutokana na huzuni zitokanazo na maumivu yao, basi nenda ukaulize mahospitalini, magerezani na makaburini. Kwa hakika, kama utakavyosikia kutoka katika hospitali nyingi minong’ono na kugumia ya wanaougua kutokana na ubadhirifu na ufisadi unaotokana na misukumo ya ujana, ndivyo pia utakavyosikia magerezani miguno ya majuto ya vijana wasio na furaha walioadhibiwa kwa matendo ya haramu hususani yanayotokana na matumizi mabaya ya ujana. Na mtafahamu kuwa adhabu nyingi za kaburi -ambalo ni Ulimwengu wa Kati na Kati ambao ni milango ambayo inaenendelea kufunguliwa na kufungwa kwa wenye kuingia- ni matokeo ya ujana uliotumiwa vibaya, kama inavyoshuhudiwa na watu wa ufunuo wa maisha ya kaburi, na yamethibitishwa na watu wa kweli.          

Pia, waulize wazee na wagonjwa, ambao ndiyo wengi katika idadi ya watu. Kwa hakika, wengi katika wao watasema kwa huzuni na majuto: “Tambueni! Tumepoteza ujana wetu katika matamanio na njozi; kwa hakika, kwa maumivu. Muwe na tahadhari, msifanye kama tulivyofanya!” Kwa sababu, matokeo ya furaha za haramu za vijana watano kati ya kumi, mtu anapata maumivu kwa miaka mingi ya masikitiko na majuto duniani, adhabu na madhara katika Ulimwengu wa Kati na Kati, na majanga ya jahanamu katika Akhera. Na ingawa mtu wa aina hiyo yupo katika hali ya kusikitisha, yeye kwa vyovyote anastahiki kusikitikiwa. (Kwa wanaoridhika kujiingiza katika matendo haramu anaweza kuwa asisikitikiwe).

Imamu Al-Rabbani, Al-Maktubat Jim 2, andiko la 49: “Anayeridhia dhara hastahiki kutazamwa”.

Hawastahiki.

حَفَظَنَا اللهُ وَإِيَّاكُم مِن فِتْنَةِ هَذَا الزَّمَان المُغْرِيَة وَنَجَّانَا مِنْ شُرُورِهَا..آمِيْن

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.