“USILIE KWA SABABU YA KUKOSA BAHATI!”

Kutoka Kituo cha Pili cha Neno la Kumi na Saba

Vipande katika Kituo hichi cha pili vinashabihiana na ushairi, lakini si ushairi. Havikuwekwa kuwa hivyo kwa makusudi, bali vinaonekana hivyo vilivyo kwa kiwango kutokana na mpangilio kamilifu wa ukweli vinavyoueleza.

Usilie kwa kukosa bahati, Ewe mnyonge, njoo, mtumaini Allah!

Tambua kuwa kulia huleta mkosi na pia ni kosa kubwa.

Mtafute Mwenye kuleta bahati mbaya, na ujue ni zawadi ndani ya zawadi na furaha.

Hivyo acha kulia na ushukuru; Kama ndege, tabasamu kupitia machozi yako!

Kama utamkosa Yeye, tambua kuwa dunia yote ni maumivu ndani ya maumivu, mpito na hasara.

Hivyo kwanini ulalamikie mkosi mdogo ilhali juu yako kuna majuto makubwa?

Njoo umtumaini Allah!

Mtumaini Allah! Cheka mbele ya mkosi; nao pia utacheka.

Mkosi ukicheka, utapungua; utabadilika.

Tambua, Ewe mjeuri, furaha duniani ipo katika kuiacha.

Kumjua Allah kunatosha. Iache dunia; mambo yote yatakuwa kwa ajili yako.

Kuwa mjeuri ni hasara kabisa; chochote unachofanya, mambo yote yatakuwa dhidi yako.

Hivyo hali zote zinahitaji kuiacha dunia hapa.

Kuiacha dunia ni kuichukulia kama mali ya Allah, kwa idhini Yake, kwa Jina Lake;

Kama unataka kufanya biashara, ni katika kuyafanya maisha haya kuwa ni ya milele.

Kama unaitafuta nafsi yako, ni uozo na hakuna msingi.

Kama unaitafuta dunia nje, muhuri wa kuondoka haraka umeshagongwa juu yake.

Hiyo inamaanisha hakuna thamani katika kuichukua; bidhaa zote katika soko hili zimeoza.

Kwa hivyo, songa mbele, bidhaa nzuri zimepangwa baada ya hapo.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.