VIPI TUNAWEZA KUYAOKOA MAISHA YETU?

[Mazungumzo na baadhi ya vijana ambao japo wamezingirwa na vishawishi, hawajapoteza uwezo wao wa kimantiki.]

          Huku likiwa limevamiwa na anasa za kilaghai na potovu za zama hizi, kundi la vijana lilikuwa likiuliza: “Tutawezaje kuokoa maisha yetu katika Akhera?” na wakatafuta msaada katika Risale-i Nur. Kwa hivyo nikawaambia yafuatayo kwa jina la Risale-i Nur:

          Kaburi lipo na hakuna wa kulikana. Watake wasitake, kila mmoja lazima ataingia. Licha ya ‘Njia tatu’ zifuatazo, hakuna njia nyingine ya kuliendea:

Njia ya Kwanza:

Kwa waumini, kaburi ni mlango wa kuingia katika ulimwengu bora zaidi kuliko dunia.

Njia ya Pili:

Kwa wenye kuamini Akhera, lakini wanaiendea kwa njia ya ubadhirifu na upotovu, ni mlango wa kuingia jela ya kifungo cha upweke, gereza la milele, ambapo watatenganishwa na wapenzi wao wote.

Njia ya Tatu:

Kwa makafiri na wapotevu wasioamini Akhera, ni mlango wa kuelekea kifo cha milele. Maana yake, ni vitanzi vya kuwanyongea wao na wote wanaowapenda. Kwa kuwa wanadhania hivyo, hivyo ndivyo hasa watakavyokuwa: kama adhabu.

Njia hizi mbili za mwisho ziko dhahiri, hazihitaji ushahidi, ni wazi kwa wenye kuona. Kwa kuwa saa iliyoteuliwa ni siri, na kifo kinaweza kuja wakati wowote na kukikata kabisa kichwa cha mmojawapo, na hakibagui kati ya kijana na mzee, na kudumu katika hali ya hofu hiyo na jambo zito mbele yake, mtu asiye na furaha kwa hakika atatafuta njia za kujitoa kutoka katika kifo cha milele, kifungo hicho cha upweke kisichokwisha; njia za kubadili mlango wa kaburi kuwa mlango unaoelekea ulimwengu wa milele, furaha ya milele, na dunia ya nuru. Litakuwa swali kubwa kwake kama dunia.           Ukweli wa kifo, basi, unaweza tu kufikiwa kwa njia hizi tatu, na mitume na manabii wanyoofu mia moja na ishirini na nne elfu, waliokuwa na miujiza kama dalili za uthibitisho – wametangaza kuwa njia hizo tatu ni kama zilivyoelezwa hapo juu. Kwa kuegemea katika nuru na maono yao, mawalii milioni mia moja ishirini na nne wamethibitisha na kuweka alama zao katika bishara za kinabii. Na Wanazuoni wengi wamethibitisha kimantiki kwa shuhuda zao dhahiri katika kiwango cha ‘uhakika katika kiwango cha elimu.

Mojawapo ni: Risale-i Nur na ipo kwa ajili ya wote kuona.

Wote kwa kauli moja wametangaza kuwa ni uhakika kabisa, kwa kusema: “Njia pekee ya kunusurika na kifo na kifungo cha milele, na kupelekwa kwenye furaha ya milele, ni kwa kumwamini Allah na kumtii.”

Kama mtu anazingatia lakini hafuati neno la mjumbe mmoja la kutokufuata njia ya hatari yenye asilimia moja ya hatari ya kuangamia, na akaifuata, wasiwasi alionao wa kuangamia unaweza kumwondolea hata hamu yake ya kula. Hivyo, mamia ya maelfu ya mitume wa kweli na waliothibitishwa wametangaza kuwa kuna uwezekano wa asilimia mia moja kuwa upotovu na uovu unapelekea katika vitanzi vya kaburi, mbele kabisa ya macho, na kifungo cha milele cha upweke, na kuwa kuna uwezekano wa asilimia mia moja kuwa imani na ibada huondoa vitanzi hivyo, hulifunga gereza la upweke, na kubadili kaburi la dhahiri daima na kuwa mlango unaoelekea katika hazina ya milele na kasri la furaha; na wameonesha dalili na alama za hayo. Kama alivyokabiliwa, basi, kwa jambo hili geni, la kutisha, ikiwa mwenye huzuni na – hususani kama yeye ni mwislamu – haamini na kuabudu, Je, ataweza kweli kuondoa maumivu ya huzuni yenye kuletwa na wasiwasi alionao kwa kuwa muda wote anangojea zamu yake ya kuitwa kwenye vitanzi hivyo, mbele kabisa ya macho yake, hata kama amepewa utawala juu ya dunia yote pamoja na furaha zake zote? Ninakuulizeni.          

Kwa kuwa uzee, maradhi, majanga, na katika pande zote kifo hufungulia maumivu ya kutisha na pia ni ukumbusho, hata kama watu wa upotovu na uovu wanafurahia anasa na furaha mia moja elfu, kwa hakika kabisa wanapata namna ya jahanamu nyoyoni mwao, lakini mzubao mkubwa wa kutokuwa na usikivu huwafanya kwa muda mfupi wasiihisi.

Kwa kuwa wanaoamini na kuabudu kaburi, ambalo mara zote liko machoni mwao, ni mlango wa kuelekea kwenye hazina ya milele na furaha ya milele, na kwa kuwa, kwa sababu ya ‘kuponi ya imani’, tiketi kutoka katika bahati nasibu ya milele ya kudura ya Kiungu kwa mamilioni ya mamilioni ya dhahabu na almasi za thamani kubwa zimekuja kwa kila mmoja wao, muda wote wanasubiri neno, “Njooni mchukue tiketi zenu” kwa furaha kubwa ya kweli na ya kiroho. Furaha hii ipo kwa kiasi kwamba, kama inakuwa kitu na mbegu inakuwa mti, itakuwa kama pepo binafsi. Hata hivyo, anayeacha furaha na anasa kubwa kutokana na misukumo ya ujana, na kuchagua namna ya ufisadi na ufasiki, furaha zilizoharamishwa, zinazofanana na asali yenye sumu iliyochafuliwa na maumivu yale mengi, anaangukia katika kiwango kidogo mno kuliko hata mnyama.

Zaidi ya hivyo, mtu wa namna hiyo hatakuwa kama Wamagharibi wasioamini, kwani kama watamkanusha Nabii Muhammad (s.a.w), wanaweza kuwatambua manabii wengine. Kama hawamjui Allah, wanaweza kuwa na sifa nzuri ambazo ni njia za makamilifu ya hakika. Lakini mwislamu anajua manabii, na Mwenye kumruzuku, na ukamilifu wote kupitia kwa Muhammad (s.a.w). Kama mmoja wao ataacha maelekezo ya Nabii atakuwa anajitoa nje ya mlolongo wake, hatamtambua nabii yeyote mwingine, wala hatamtambua Allah. Wala hatajua msingi wowote rohoni mwake utakaohifadhi makamilifu yake. Kwa kuwa Muhammad (s.a.w) ni nabii wa mwisho na mtukufu, na dini yake na ulinganiaji ni kwa watu wote, na kwa kuwa yeye ni mbora kuliko wote kwa miujiza yake na dini, na yeye ni mwanaadamu kwa watu wote katika mambo yote kuhusu uhakika, na ameyathibitisha haya katika namna nzuri sana kwa karne kumi na nne, na ni sababu ya fahari ya wanaadamu, mwislamu anayekataa mafundisho muhimu ya Muhammad (s.a.w) na misingi ya dini yake kwa hakika hataweza kupata nuru, wala kupata ukamilifu wowote. Ataanguka kabisa.

Na kwa hivyo, enyi wenye hasara waliotawaliwa na anasa za maisha ya dunia, na kuwa na wasiwasi wa mustakabali, pambaneni ili kuuhifadhi na maisha yenu! Kama mnataka anasa, raha, furaha, na wepesi duniani, fanyeni mambo ya halali. Hayo yanatosha kukupeni furaha. Kwa hakika mtakuwa mnafahamu kutoka sehemu nyingine za Risale-i Nur kuwa katika kila furaha iliyo nje ya hilo, na ni haramu, kuna maumivu mengi sana. Kama matukio ya hapo baadaye – mathalani, ya miaka hamsini tangu sasa yangeoneshwa katika sinema kama wanavyoonesha kwa wakati huu matukio yaliyopita, wanaojiingiza katika uovu watalia huku wakiwa wamejaa hofu na maudhi katika mambo ambayo kwa sasa yanawafurahisha.

Wale wanaotaka wawe na furaha ya kudumu na ya milele duniani na Akhera wafuate maelekezo ya Muhammad (s.a.w) katika wigo wa imani.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.