VISA VIWILI KUTOKA KWENYE MFANO WA UJANA WA BEDIUZZAMAN

Nilipokuwa na umri wa miaka ishirini au kama hivyo, nilikaa miaka miwili nyumbani kwa liwali wa Bitlis, Ömer Pasha, kwa msisitizo wake na kwa heshima yake kupita kiasi kwa elimu. Alikuwa na wasichana sita, watatu kati yao walikuwa wadogo na watatu walikuwa wakubwa. Japo nilikaa kwenye nyumba hiyo hiyo kama wao kwa miaka miwili, sikuweza kuwatambua wale watatu kwa kuwabainisha na niliwazingatia kiasi kidogo sana, ningewezaje? Mwanazuoni mwingine alikuja na kukaa pamoja na mimi kama mgeni na ndani ya siku mbili, aliwajua na aliweza kuwatofautisha mmoja baada ya mwingine. Wote walipigwa na bumbuazi kutokana na tabia yangu na wakaniuliza: “kwanini huwatazami?” nilijibu: “Heshima ya elimu, ambayo nalazimika kuilinda, hainiruhusu kuwatazama.”

Kadhalika, miaka arobaini ililyopita katika Istambul wakati wa sikukuu ya Kağıthane, nilipanada boti pamoja na wajumbe wa zamani wa Bunge Molla Seyyid, Taha, na Haji İlyas. Tukiwa njiani kutokea darajani kuelekea Kağıthane maelfu ya wasichana wasiojifunika wa kigiriki na wa Armenia. na wanawake wa Istambul na wasichana wao, walifurika kwenye fukwe mbili za Golden Horn. Sikua najuwa kabisa lakini Molla, Seyyid Taha, na Haji İlyas waliamua kunipa mtihani, mwishoni mwa safari ya saa moja walikiri kwamba waliniangalia kwa zamu kwa karibu, walisema: “Tulikuwa tumeshangazwa na wewe, hukuwaangalia kabisa hata mara moja!” Nilijibu: “Furaha zisizokuwa na muelekeo za kupita haraka za madhambi zinaleta maumivu na majuto tu; sitaki yoyote kati ya furaha kama hizo!”

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.