WANAADAMU WATAISHIKA QUR’AN

Nitadokeza kwa kifupi ukweli mpana sana na mrefu uliotokea moyoni mwangu katika Usiku wa Cheo.

Kwa sababu ya uasi mkubwa na udhalimu wa Vita vya Dunia vya mwisho na uharibifu wake usio na huruma, na mamia ya wasio na hatia kutawanyika na kuhiliki kwa sababu ya jeshi moja, na ukataji tamaa mkubwa kwa walioshindwa, na mshituko wa kutisha wa washindi na maumivu yao makali yanayotokana na ukuu wasioweza kuudumisha na uharibifu wasiyoweza kuukarabati, na hali ya mpito na muda mfupi wa maisha ya dunia na hali ya hadaa, na ulevi wa ndoto za ustaarabu kudhihirika kwa wote, na uwezo wa juu katika hali halisi ya binaadamu na dhati yake kujeruhiwa katika hali ya kuenea kote na ya kutisha, na mapenzi ya ndani ya mwanaadamu ya kutaka kuendeleza kuishi na kutokujali na upotovu na kutosikia, hali ya asili isiyokuwa na uhai kupondwapondwa na panga la almasi la Qur’an, na uso mbaya zaidi wa siasa ya dunia kuwa dhahiri, ambao ni kifuniko chenye kusonga koo na kuhadaa kwa kutokujali na upotovu, kwa hakika zaidi na bila kivuli chochote cha shaka, kwa kuwa maisha ya dunia – ambayo hupendwa na wanaadamu – ni mabaya na ya mpito hasa, hali halisi ya mwanaadamu itatafuta uzima wa milele kwa nguvu zake zote, anaoupenda na kuutamani kikweli, kama kulivyo na alama za kutokea huku kwa Kaskazini, Magharibi, na Marekani.

Na lililo hakika zaidi pasi na shaka ni kwa kuwa Qur’an yenye Ufafanuzi wa Kimiujiza, ambayo kila karne kwa miaka elfu moja mia tatu na sitini imekuwa na wanafunzi milioni mia tatu hamsini, na kuweka muhuri juu ya kila tangazo lake na kudai kwa uthibitisho wa mamilioni ya wanazuoni wakubwa, wanyoofu, na kila dakika imekuwepo kwa utukufu wake nyoyoni mwa mamilioni ya mahafidhi na imetoa maelekezo kwa wanaadamu kwa ndimi zao, na ambayo katika namna ya kutolingana na kitabu kingine chochote kinafikisha bishara ya uzima wa milele na furaha ya milele kwa mwanaadamu na kuponya vidonda vyao, – kwa kuwa Qur’an imeeleza habari hizi njema za uhakika kuhusu uzima wa milele na furaha kwa maelfu ya msisitizo wake, aya zenye nguvu na zenye kujirudia, na kwa shuhuda imara na hoja zisizo na idadi za wazi, inatoa habari waziwazi na kwa kudokezea mara maelfu ya idadi, kwa kuwa mwanaadamu hapotezi akili yake yote na kiama cha kimwili na kiroho hakilipukii kichwani mwake, makundi makubwa na mataifa makubwa duniani yataitafuta Qur’an yenye Ufafanuzi wa Kimiujiza, na baada ya kupata ukweli wake, wataipokea kwa uhai wao wote na roho, kama kulivyo [kwa sasa] kuna wahubiri katika Sweden, Norway, Finland na Uingereza wakifanya kazi ya kufanya Qur’an ipokelewe, na jamii muhimu ya Marekani inatafuta dini ya kweli. Kwa sababu katika mtizamo wa ukweli huu, Qur’an kwa hali yoyote haina wala haitakuwa na chenye kulingana nayo. Na bila ya shaka hakuna kinachoweza kuchukua nafasi ya muujiza huu mkubwa.

Pili:

Kwa kuwa Risale-i Nur imetoa huduma kama upanga wa almasi mkononi mwa muujiza huu mkubwa zaidi na kuwashurutisha maadui zake wakaidi kutii, na inafanya kazi kama mpiga mbiu kwenye hazina za Qur’an katika mtindo unaoangaza na kuponya moyo na roho kikamilifu, na hisia, na haina chanzo wala mamlaka mengine ghairi ya Qur’an na ndiyo muujiza wake, inafanya kazi hiyo kikamilifu.

Zaidi ya hivyo imewang’oa kikamilifu wakana mungu wakaidi na propaganda zao za kutisha dhidi yake, na kupondaponda kwa risala ya (Asili, Sababu au Athari), ambayo ni ngome isiyoshindika ya upotovu, na kwa mada ya Sita ya (Matunda ya Imani) pamoja na Shuhuda za Kwanza, Pili, Tatu na Nane ambazo zote zimo katika kitabu (Fimbo ya Musa), zimeondoa hali ya kutokujali katika mtindo mzuri zaidi katika uwanja wake mnene, wenye kukaba koo na mpana chini ya vizuizi vikubwa vya sayansi na kuonesha nuru ya umoja wa kiungu.

Kwa hakika, kwa kuwa maelekezo ya kidini kwa sasa yameruhusiwa rasmi na ruhusa imetolewa kufungua sehemu binafsi za masomo, ni lazima kwetu na lazima kwa umma kuwa, kadiri iwezekanavyo, Wanafunzi wa Risale-i Nur wanapaswa wafungue Kituo kidogo cha Kusoma Risale-i Nur kila mahali. Ingawa kila mmoja atanufaika na yaliyomo humo, si kila mmoja anaweza kufahamu kila jambo kikamilifu. Lakini kwa kuwa masuala haya ni maelezo ya mambo ya ukweli wa imani, yote ni kujifunza, na kumjua Allah, na huelekezea kwenye kuwepo kwa Allah, na pia ni ibada.

Inshallah, Madrasa hizi za Risale-i Nur zitahifadhi katika majuma matano mpaka kumi, matokeo yaleyale ambayo Madrasa zilizotangulia zimeleta katika miaka mitano mpaka kumi – na kwa hivyo, zimekuwa zikifanya kwa miaka ishirini.

Pia ni muhimu kwa serikali kutokuingilia Miale hii ya Qur’an, Risale-i Nur, ambayo ni mpiga mbiu wa Qur’an na ni pia ni yenye kufaa kwa njia nyingi katika maisha ya kidunia na kisiasa kwa umma na nchi hii, na kwa ajili ya maisha yake katika Akhera. Badala yake, ifanye kazi ya kuieneza kikamilifu na kukubalika, ili ifute madhambi yake mabaya ya muda uliopita, na kuweka kizuizi kwenye majaribu mengi na vurugu za mustakabali.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.