Neno La Mwisho Kuhusu Kusengenya

بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ

Mfano uliotajwa baina ya mifano ya makamu ya kukemea kwenye nukta ya tano ya Mwale wa kwanza ya neno la ishirini na tano, umeonesha katika utajo wa aya moja tukufu ubaya mzito wa kusengenya, katika mtazamo wa Qur’an, aya imedhihirisha kwa utukufu vipi inamkataza mwanaadamu na kusengenya katika sura sita, na hakika Qur’an ni yenye kutosheleza katika kubainisha na hakuna chengine zaidi yake.

Kauli yake Allah (s.w):

أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَنْ يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيْهِ مَيْتًا فَكَرِهْـتُمُوهُ Qur’an, 49:12

inakataza na kukemea kusengenya kwa daraja sita kama ifuatavyo:

Aya inakataza kusengenya kwa daraja sita na inakemea kwa nguvu zote, na inaelekeza mazungumzo kwa wasengenyaji hivyo maana inadhihiri kama ifuatavyo:

Herufi “Hamza” iliopo mwanzo wa neno ni ya kuuliza na kukanusha kwa pamoja na hukumu inakuwa ni yenye kutiririka kama maji na kuenea katika maneno yote ya aya, kila neno miongoni mwa maneno yake lina hukumu.

Katika neno la mwanzo aya imeanza kuzungumza kwa herufi “hamza”: Je, nyie hamna akili – napo ndipo mahala pa swali na jawabu – kuonyesha kwamba suala hili ni baya mno?

Katika neno la pili:

يُحِبُّ

Aya imeanza kwa herufi “hamza”, Je, nyoyo zenu zimekufa? – Napo ni mahala pa mapenzi na kuchukia – mpaka kufikia mmoja wenu kupenda vinavyochukiza kabisa kabisa?

Katika neno la tatu:

أَحَدُكُمْ

aya imeanza kwa herufi “hamza”, Kitu gani kimetokea kwenye maisha yenu ya kijamii, – ambayo yanapata uhai wake katika uhai wa jamii (kundi) – ustaarabu wenu na utamaduni wenu umesibiwa na kitu gani mpaka kufikia kuridhia yale yanayotafuna na kuutia dosari na kutia sumu safu zenu?

Katika neno la nne:

أَنْ يَأْكُلَ لَحْمَ

aya imeanza kwa herufi ya “hamza”, Ni kitu gani kimeusibu utu wenu? Mpaka mkawa ni wenye kumwinda ndugu yenu kipenzi?

Katika neno la tano:

أَخِيْهِ

imeanza kwa herufi “hamza”, je hakuna nyoyoni mwenu mapenzi kwa wanadamu wenzenu, hakuna mahusiano ya kizazi, yenye kuwafungamanisha, mpaka mkawa ni wenye kufanya mashambulizi kwa ndugu yenu kutoka kila pembe, na mkawa ni wenye kumrarua kisawasawa, je ni mwenye akili yule anayenyofoa  kipande toka kwenye mwili wa ndugu yake? Je, huyo sio mwendawazimu?

Katika neno la sita

مَيْتًا

imeanza kwa “hamza”, ziko wapi hisia na roho zenu, kiasi gani fitra zenu zimeharibika, mpaka kufikia kufanya mambo maovu kabisa na mabaya, nayo ni kula nyama ya ndugu yenu, wakati ambao ni mwenye kustahiki aina zote za heshima. Inafahamika katika aya tukufu na kwa haya tuliyoyataja katika maana tofauti za maneno ya aya, kuwa kusengenya ni tendo ovu kiakili, kimoyo, kibinadamu, kifitra na kimila.

Zingatia aya hii tukufu, na tazama ni vipi inakataza kosa hilo la kusengenya kwa ubora na kwa ufupisho kabisa kupitia daraja sita.

Kusengenya ni silaha dhaifu wanayoitumia wenye uhasama na mahasidi na wakaidi, kwani mtu mwenye nafsi tukufu, hakika nafsi yake inamkataza kutumia silaha chafu kama hii, amesema mshairi:

                     “Naitukuza nafsi yangu dhidi ya malipo ya kusengenya                        hakika kusengenya ni juhudi kwa asiyetaka kujitahidi’’

Diwan al-Mutanabbiy, uk 198 chapa Dar sadir.

Kusengenya ni kumsema ndugu yako kwa yale yanayomchukiza, ama ikiwa yamo unayoyasema utakuwa umemsengenya, na ikiwa hamna utakuwa umemsingizia, na kwa maana hii utakuwa umefanya makosa mara mbili.

Muslim, Al-Bir 70; Tirmidhi, Al-Bir 23; Abu Daud, Al-Adab 35.

Kusengenya japokuwa ni haramu ila tu kunaruhusika katika hali maalumu.

Nawawi, Al-Adhkaar, uk 360-362, 366.

Katika kutoa ushauri: Atakapokutaka ushauri mtu mwenye kutaka kufanya jambo na mwenzake, nawe ukataka kumpa ushauri na nasaha za kweli kwa ajili ya Allah (s.w), pasina kuingiza malengo ya kibinafsi unaweza kumwambia “Mtu fulani usishirikiane nae, utapata hasara na matatizo.”

Ibn Majah, Al-Adab 37; Ahmad  bin Hambal, Al-Musnad 3/418-419, 4/259; Al-twayyalasiy, Al-Musnad 185.

Kumfahamisha mtu pasina kukusudia kumdhalilisha: Kama vile kusema, mtu yule kiguru au yule muovu. Ikiwa ni fasiki mwenye kujitangazia ufuska wake, hajifichi machafu yake, pengine ni mwenye kujivunia maovu yake na anajisikia raha kwa kuwadhulumu wengine.

Al-Bayhaki, Al-sunan al-Kubra 10/210.

Katika hali kama hizi maalumu inajuzu kusengenya, kwa ajli ya maslahi, pasina kuwa na kitu maalumu moyoni, bali itajuzu kwa nia ya kufikia kwenye haki pekee. Vyenginevyo kusengenya ni kwenye kuangusha amali njema na kuzitafuna kama vile moto unavyokula kuni.

Mwanaadamu anapofanya kosa la kusengenya, au kusikiliza kwa hamu, basi na aombe hivi:

اللّهُمَّ اغفِرْلَنَا وَلِمَنْ اغْتَبْنَاه Assuyuti, al-fathul-kabir 1/84.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.