Kutoka Katika (Hutuba Ya Sham)

Katika niliyojifunza kutokana na maisha ya kijamii ya kibinaadamu katika uhai wangu wote na yale ambayo nimeelekezwa na ufuatiliaji na utafutaji wa hakika ni:

Hakika kitu bora zaidi kwa mapenzi ni mapenzi yenyewe. Na sifa bora zaidi ya uhasama ni uhasama wenyewe. Yaani sifa ya mapenzi ambayo ni dhamana ya uhai wa kijamii ya kiutu, na ambayo inapelekea kupatikana uhakika wa furaha ni yenye kufaa zaidi kwa mapenzi, na kwamba sifa ya uadui na chuki ambayo ni sababu ya uharibifu wa maisha ya kijamii na kuyabomoa ni sifa mbaya mno na yenye madhara mno na yenye kustahiki mno kuepukwa na kukimbiwa. Na tulipokuwa tumekwisha fafanua hakika hii katika andiko la ishirini na mbili (Barua ya undugu) hapa tunaiashiria kwa namna ya ufupilizo.

Zama za uadui na uhasama zimekwishapita. Hakika vita viwili vikuu vya ulimwengu vimekwisha onesha kiasi cha yaliyomo kwenye roho ya uadui ikiwemo dhulma mbaya na uvunjifu wa kutisha. Na imekuwa wazi kwamba hakuna faida katika hayo kabisa. Na kwa hiyo, haitakikani maovu ya maadui zetu kuleta– kwa sharti la kutoyavuka – uadui wetu, basi inawatosha adhabu ya kiungu na moto wa Jahannam.

Hakika ghururi ya mwanaadamu na kuipenda nafsi yake wakati mwingine vinaweza kumuongoza katika kuwafanyia uadui ndugu zake waumini hali ya kuwadhulumu na bila ya kuhisi, basi mtu akadhani nafsi yake ina haki. Pamoja na kuwa mfano wa uadui huu unahesabiwa kuwa ni dharau ya mafungamano na sababu ambazo zinawafungamanisha waumini wao kwa wao – kama Imani, Uislamu na utu – na kuangusha hadhi yake. Na hilo linafanana mno ilivyo na upumbavu wa mtu anatia uzito sababu za kipuuzi za kufanyiana uadui kama changarawe juu ya sababu zenye ukubwa wa milima mikubwa za mapenzi.

Kwa kuwa mapenzi ni kinyume cha uadui na yenye kupingana nayo basi havikutaniki katu kama isivyokusanyika kiza na nuru. Basi kinachozidia sababu zake kuliko kingine ndicho kinapata nafasi yake moyoni kwa uhakika wake, ama dhidi yake haiwi kwa hakika yake.

Kwa mfano: Kama mahaba yatapatikana kwa hakika yake moyoni wakati huo uadui unageuka kuwa huruma na upole, na hii ndiyo hali ilivyo kwa upande wa watu wa Imani. Ama uadui ukipatikana kwa hakika yake moyoni, mapenzi wakati huo yatageuka kuwa ni kuzungukana na kuachiliana mambo yapite na urafiki wa kinje. Hili hakika huwa pamoja na watu wa upotevu wasioachilia mbali mambo.

Ndiyo, sababu za mapenzi ni Imani, Uislamu na utu, na mfano wa hizo, katika nyororo za kinuru zenye nguvu na ngome za kimaanawi madhubuti. Ama sababu za uadui na chuki kwa muumini hizo ni mambo maalumu ya kipuuzi sawa na upuuzi wa vichangarawe. Kwa hiyo kudhamiria uadui kwa muislamu kudhamiria kwa hakika, hakika ni kosa kubwa, kwa sababu ni dharau ya sababu za mahaba ambazo zinafanana mno na milima.

Yatokanayo:

Kwamba mapenzi na udugu ni katika tabia za uislamu na mafungamano yake. Na ambaye anabeba uadui moyoni mwake, anafanana mno na mtoto mbaya wa tabia, anakusudia kulia kwa sababu duni kabisa ya kulia, na yaweza kuwa ni ndogo zaidi kuliko ubawa wa nzi yatosha kumsukuma yeye kulia, au ni sawa kabisa na alivyo mtu mwenye kukata tamaa, hadhanii chochote kwa dhana njema, madam dhana mbaya inawezekana, anafunika mema kumi ya mtu kwa ovu moja tu. Na katika yanayojulikana, hakika ya hili ni lenye kupingana kabisa na tabia ya kiislamu ambayo inahukumu insafu na dhana njema.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.