Kutoka Katika: Mng’ao Wa Kumi Na Tatu

Nukta ya tatu:

Hakika kinachoharibu maisha ya kijamii ya mwanadamu ni hila ya kishetani ifuatayo:

Hakika shetani anafunika kwa muumini kwa ovu moja mazuri yake yote. Basi wale wanaotegea sikio vitimbi hivi vya kishetani katika wasiokuwa na insafu wanamfanyia uadui muumini. Wakati Allah (s.w) anapopima amali za wenye kukalifishwa kwa mizani kubwa na kwa uadilifu wake wa hali zote siku ya ufufuo, hakika anahukumu kwa upande wa uzito wa mema au maovu. Na anaweza kafuta kwa jema moja na kuondosha madhambi mengi. Ambapo hakika kutenda maovu na dhambi ni rahisi na wepesi na njia zake ni nyingi. Kwa hiyo inatakikana kutenda katika hii dunia na kupima kwa mithili ya mizani ya uadilifu wa kiungu. Ikiwa mema ya mtu ni mengi kuliko maovu yake kwa kiasi au kwa aina, basi hakika anastahiki mapenzi na heshima. Na huenda yakatazamwa maovu yake mengi kwa jicho la msamaha, maghfira na kuachilia kwa jema moja lenye aina mahususi.

Isipokuwa mwanadamu hakika anasahau kwa mafunzo kutoka kwa shetani na kile kilichopo katika maumbile yake miongoni mwa dhulma, mamia katika mema ya ndugu yake muumini kwa ajili ya ovu moja lililodhihiri kutoka kwake basi anaanza kumfanyia uadui, na kuingia katika dhambi. Kama ilivyo kuweka ubawa wa mbu mbele ya jicho moja kwa moja kunazuia kuona mlima mkubwa, na chuki vilevile inafanya ovu – ambalo lina ukubwa wa ubawa wa mbu – kuzuia kuona mazuri kama mlima mkubwa, wakati huo basi mwanadamu anasahau kutaja hayo mazuri na anaanza kumfanyia uadui ndugu yake muumini, na anakuwa ni kiungo kibovu na zana ya kubomoa katika maisha ya waumini ya kijamii.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.